JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail:
press@ikulu.go.tz
Tovuti :
www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 07 Julai, 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri
za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania
Bara.
Uteuzi
huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya
wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wameteuliwa kutoka orodha ya
wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.
Orodha
ya wakurugenzi walioteuliwa kulingana na mikoa yao ni kama ifuatavyo;
ARUSHA
- Arusha Jiji - Athumani Juma Kihamia
- Arusha DC - Dkt. Wilson Mahera Charles
- Karatu DC - Banda Kamwande Sonoko
- Longido DC - Jumaa Mohamed Mhiwapijei
- Meru DC - Kazeri Christopher Japhet
- Monduli DC - Stephen Anderson Ulaya
- Ngorongoro DC - Raphael John Siumbu
DAR
ES SALAAM
- Dar es salaam Jiji - Siporah Jonathan Liana
- Kinondoni Manispaa - Aron Titus Kagurumjuli
- Temeke Manispaa - Nassibu Bakari Mmbaga
- Ilala Manispaa - Msongela Nitu Palela
- Kigamboni Manispaa - Stephen Edward Katemba
- Ubungo Manispaa - Kayombo Lipesi John
DODOMA
- Dodoma Manispaa - Dkt. Leonard M. Masale
- Kondoa DC - Kibasa Falesy Mohamed
- Kondoa Mji - Khalifa Kondo Mponda
- Mpwapwa DC - Mohamed Ahamed Maje
- Kongwa DC - Mhandisi Ngusa Laurent Izengo
- Chemba DC - Semistatus Hussein Mashimba
- Chamwino DC - Athuman Hamis Masasi
- Bahi DC - Rachel Marcel Chuwa
GEITA
- Bukombe DC - Dionis Maternus Nyinga
- Chato DC - Mhandisi Joel Bahahari
- Geita DC - Ally Abdallah Kidwaka
- Geita Mji - Modest J. Apolinaly
- Mbogwe DC - Mahwago Elias Kayandabila
- Nyang'wale DC - Carlos K. Gwamagobe
IRINGA
- Iringa Manispaa - William Donald Mafwele
- Mafinga Mji - Saada S. Mwaruka
- Mufindi DC - Riziki Salas Shemdoe
- Iringa DC - Robert Mgendi Magunya
- Kilolo DC - Aloyce Kwezi
KAGERA
- Biharamulo DC - Wende Israel Ng'ahala
- Bukoba DC - Abdulaaziz Jaad Hussein
- Bukoba Manispaa - Makonda Kelvin Stephen
- Karagwe DC - Godwin Moses Kitonka
- Kyerwa DC - Shedrack M. Mhagama
- Missenyi DC - Limbe Berbad Maurice
- Muleba DC - Emmanuel Shelembi Luponya
- Ngara DC - Aidan John Bahama
KATAVI
- Mlele DC - Alex Revocatus Kagunze
- Mpimbwe DC - Erasto Nehemia Kiwale
- Mpanda DC - Ngalinda Hawamu Ahmada
- Mpanda Manispaa - Michael Francis Nzyungu
- Nsimbo DC - Joachim Jimmy Nchunda
KIGOMA
- Buhigwe DC - Anosta Lazaro Nyamoga
- Kakonko DC - Lusubilo Joel Mwakabibi
- Kasulu DC - Godfrey Msongwe Masekenya
- Kasulu Mji - Fatina Hussein Laay
- Kigoma Ujiji - Manispaa - Judethadeus Joseph Mboya
- Kigoma DC - Hanji Yusuf Godigodi
- Kibondo DC - Shelembi Felician Manolo
- Uvinza DC - Weja Lutobola Ng'olo
KILIMANJARO
- Manispaa ya Moshi - Michael Nelson Mwandezi
- Hai DC - Yohana Elia Sintoo
- Siha DC - Valerian Mwargwe Juwal
- Same DC - Shija Anaclaire
- Mwanga DC - Golden A. Mgonzo
- Rombo DC - Magreth Longino John
- Moshi DC - Emalieza Sekwao Chilemeji
LINDI
- Kilwa DC - Bugingo I. N. Zabron
- Lindi DC - Samwel Warioba Gunzar
- Lindi Manispaa - Jomaary Mrisho Satura
- Liwale DC - Justine Joseph Monko
- Nachingwea DC - Bakari Mohamed Bakari
- Ruangwa DC - Andrea Godfrey Chezue
MANYARA
- Babati Mji - Fortunatus Hilario Fwema
- Hanang DC - Bryceson Paul Kibasa
- Mbulu DC - Festi Fungameza Fwema
- Mbulu Mji - Anna Philip Mbogo
- Simanjiro DC - Yefred Edson Myezi
- Kiteto DC - Tamim Kambona
- Babati DC - Hamis Iddi Malinga
MARA
- Manispaa ya Musoma - Fidelica Gabriel Myovela
- Bunda DC - Amos Jeremiah Kusaja
- Bunda Mji - Janeth Peter Mayanja
- Butiama DC - Solomon Kamlule Ngiliule
- Musoma DC - Flora Rajab Yongolo
- Serengeti DC - Juma Hamsini Seph
- Rorya DC - Charles Kitanuru Chacha
- Tarime DC - Apoo Castro Tindwa
- Tarime Mji - Hidaya Adam Usanga
MBEYA
- Busokelo DC - Eston Paul Ngilangwa
- Chunya DC - Sofia Kumbuli
- Kyela DC - Mussa Joseph Mgata
- Mbarali DC - Kivuma Hamis Msangi
- Mbeya DC - Ameichiory Biyengo Josephat
- Mbeya Jiji - Zacharia Nachoa Ntandu
- Rungwe DC - Loema Isaya Peter
SONGWE
- Momba DC - Adrian Jovin Jungu
- Tunduma Mji - Valery Alberth Kwemba
- Mbozi DC - Edna Amulike Mwaigomole
- Ileje DC - Haji Mussa Mnasi
- Songwe DC - Elias Philemon Nawela
MOROGORO
- Gairo DC - Agnes Martin Mkandya
- Kilombero DC - Dennis Lazaro Londo
- Ifakara Mji - Francis Kumba Ndulane
- Kilosa DC - Kessy Juma Mkambala
- Morogoro DC - Sudi Mussa Mpili
- Morogoro Manispaa - John Kulwa Magalula
- Mvomero DC - Florent Laurent Kyombo
- Ulanga DC - Audax Christian Rukonge
- Malinyi DC - Marcelin Rafael Ndimbwa
MTWARA
- Mtwara DC - Omari Juma Kipanga
- Mtwara Mikindani Manispaa - Beatrice Dominic Kwai
- Masasi Mji - Gimbana Emmanuel Ntayo
- Masasi DC - Mkwazu M. Changwa
- Nanyumbu DC - Hamis Hassan Dambaya
- Newala DC - Mussa Mohamed Chimae
- Newala Mji - Andrew Frank Mgaya
- Tandahimba DC - Said Ally Msomoka
- Nanyamba Mji - Oscar Anatory Ng'itu
MWANZA
- Mwanza Jiji - Kiomoni Kibamba Kiburwa
- Ilemela Manispaa - John Paul Wanga
- Kwimba DC - Pendo Anangisye Malabeja
- Magu DC - Lutengano George Mwalwiba
- Misungwi DC - Eliud Leonard Mwaiteleke
- Ukerewe DC - Tumaini Sekwa Shija
- Buchosa DC - Crispian Methew Luanda
- Sengerema DC - Magesa M. Boniphace
NJOMBE
- Njombe Mji - Iluminata Leonald Mwenda
- Makambako Mji - Paul Sostenes Malala
- Makete DC - Francis Emmanuel Namaumbo
- Njombe DC - Monica Peter Kwiluhya
- Ludewa DC - Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija
- Wanging'ombe DC - Amina Mohamed Kiwanuka
PWANI
- Bagamoyo DC - Azimina A. Mbilinyi
- Chalinze DC - Edes Philip Lukoa
- Kibaha DC - Tatu Seleman Kikwete
- Kibaha Mji - Jenifer Christian Omolo
- Kisarawe DC - Mussa L. Gama
- Mafia DC - Erick Mapunda
- Mkuranga DC - Mshamu Ally Munde
- Kibiti DC - Alvera Kigongo Ndabagoye
- Rufiji DC - Salum Rashid Salum
RUKWA
- Kalambo DC - Simon Ngagani Lyamubo
- Sumbawanga DC - Nyangi John Msemakweli
- Sumbawanga Manispaa - Hamid Ahmed Njovu
- Nkasi DC - Julius M. Kaondo
RUVUMA
- Mbinga DC - Gumbo Samanditu Gumbo
- Mbinga Mji - Robert Kadaso Mageni
- Namtumbo DC - Christopher Michael Kilungu
- Nyasa DC - Oscar Albano Mbuzi
- Songea DC - Simon Michael Bulenganija
- Madaba DC - Shafi Kassim Mpenda
- Tunduru DC - Abdallah Hussein Mussa
- Songea Manispaa - Tina Emelye Sekambo
SHINYANGA
- Kishapu DC - Stephen Murimi Magoiga
- Msalala DC - Berege Sales Simon
- Shinyanga DC - Mark Emmanuel Malembeka
- Kahama Mji - Anderson David Msumba
- Shinyanga Manispaa - Lewis Kweyemba Kalinjuna
- Ushetu DC - Michael Augustino Matomola
SIMIYU
- Bariadi DC - Abdallah Mohamed Malela
- Bariadi Mji - Melkizedek Oscar Humbe
- Itilima DC - Mariano Manyingu
- Maswa DC - Fredrick Damas Sagamiko
- Busega DC - Anderson Njiginya
- Meatu DC - Said F. Manoza
SINGIDA
- Ikungi DC - Rustika William Turuka
- Iramba DC - Linno Pius Mwageni
- Mkalama DC - Martin Msuha Mtanda
- Manyoni DC - Charles Edward Fussi
- Itigi DC - Luhende Pius Gerald
- Singida DC - Rashid Mohamed Mandoa
- Singida Manispaa - Kizito L. Brava
TABORA
- Igunga DC - Revocatus Lubigili Kuuli
- Kaliua DC - John Marco Pima
- Nzega DC - Jacob James Mtalitinya
- Nzega Mji - Phillimon Mwita Magesa
- Sikonge DC - Simon Saulo Ngatunga
- Tabora Manispaa - Bosco Addo Ndunguru
- Urambo DC - Magreth Nakainga
- Tabora -Uyui - Hadija Maulid Makuani
TANGA
- Tanga Jiji - Daudi R. Mayeji
- Korogwe DC - George John Nyaronga
- Korogwe Mji - Jumanne Kiangoshauri
- Muheza DC - Luiza Osmin Mlelwa
- Handeni Mji - Keneth K. Haule
- Handeni DC - William Methew Mafukwe
- Pangani DC - Sabas Damian Chambasi
- Mkinga DC - Mkumbo Emmanuel Barnabas
- Bumbuli DC - Peter Isaiah Nyalali
- Kilindi DC - Clemence Andagile Mwakasenda
- Lushoto DC - Kazimbaya Makwega Adeladius
Wakurugenzi
wote walioteuliwa wanatakiwa kufika Ikulu Jijini Dar es salaam siku
ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 saa tatu asubuhi kwa ajili ya kula
kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es salaam
07
Julai, 2016
RAIS DK. MAGUFULI ATEUWA MKUU WA WILAYA YA KONGWA
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail:
press@ikulu.go.tz
Tovuti :
www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi
anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi
katika Mkoa wa Songwe.
Uhamisho
wa Bw. John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya
Mhe. Rais Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya
aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake
utenguliwe kutokana na sababu binafsi.
Bw.
Deogratius John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa
viongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini
Dar es salaam.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es salaam
07
Julai, 2016
MASHABIKI WADAI CHUCHU ZA SERENA WILLIAMS ZINAWAPOTEZA KUFUATILIA MCHEZO
Akiwa ameshinda mataji ya Grand Slam
21, huku pia akiwa ni mchezaji wa kike wa tenesi anayelipwa bei mbaya
duniani, Serena Williams amegonga tena vichwa vya habari.
Safari hii ni baada ya mashabiki wa tenesi
kudai kuwa chuchu zake zimekuwa zikiwachanganya na kuwafanya washinde
kufuatilia vyema mchezo anapovaa nguo nyeupe za kampuni ya Nike.
BONDIA IDD MKWELA KUTOKA KWA 'SUPER D COACH' AJIFUA KUMKABILI HUSSEIN GOBOS JULAI 16 MAGOMENI
| Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Idd Mkwela wakati wa mazoezi yanayoendelea kwa 'Super D Coach Uhuru GYG' Kariakoo Mkwela anajiandaa na mpambano wake wa Julai 16 katika ukumbi wa Traveltain Hotel Magomeni kuzipiga na Hussein Goboss mpambano wa raundi sita KG 63 Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia
Vicent Mbilinyi kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Idd
Mkwela wakati wa mazoezi yanayoendelea kwa 'Super D Coach Uhuru GYG'
Kariakoo Mkwela anajiandaa na mpambano wake wa Julai 16 katika ukumbi wa
Traveltain Hotel Magomeni kuzipiga na Hussein Goboss mpambano wa
raundi sita KG 63 Picha na SUPER D BOXING NEWS
WATOTO 13,266 MKOANI TANGA WANUFAIKA NA HUDUMA ZA AFYA ZITOLEWAZO NA UHIC
Lee
Kwiwoon akuzungumza na washiriki wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo
vijana(Keepers) katika vijana waliofundishwa kuhudumia watoto katika
masuala ya Afya na Lishe
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika mafunzo hayo JUMLA ya watoto 13,266 wenye umri chini ya miaka 10 wamenufaika mkoani hapa na huduma za afya zitolewazo na taasisi ya Kikorea ijulikanayo kama UHIC (United Help for International Children) .
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo kanda ya Tanzania, Lee Kwiwoon alitoa taarifa hiyo hapa mwishoni mwa juma lililopita katika mkutano uliojumuisha madaktari, manesi na wahudumu wa afya kutoka wilaya tatu za mkoa huu, ambazo zimelengwa katika mradi wa taasisi hiyo.
Mkurugenzi huyo alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutoa huduma kwa watoto wenye matatizo mbalimbali ya kiafya yanayowapata wenye umri chini ya miaka 10.
Aliwaeleza wanasemina hao kwamba watoto wengi walio katika umri chini ya miaka 10 hukumbwa na magonjwa mengi, hasa malaria, upungufu wa damu na utapiamlo. Magonjwa mengine ni pamoja na kifua, kuzaliwa njiti na kuharisha.
Lee aliwaambia maofisa na manesi pamoja na wahudumu wa afya kwamba jukumu kubwa la taasisi yake ni kuzuia magonjwa yanayowanyemelea zaidi watoto wadogo pamoja na kuhakikisha watoto hao wanakua katika afya bora.
Alifahamisha kwamba taasisi hiyo ya UHIC imeanzisha mradi ujulikanao Keepers' ambao unawafundisha na kuwapatia mafunzo vijana wanaotoa huduma ya kuokoa maisha ya watoto kutoka janga la njaa, maradhi na kuwasaidia waishi katika mazingira mazuri ya kiafya.
"Afya na uzuiaji wa magonjwa yawapatayo watoto wengi mkoani Tanga ni suala linalozungumzika na hivyo kuwafanya wadau kuamua kujitolea kuanzisha taasisi zitakazosaidia kuondoa adha hiyo kwa watoto wetu", alisema Lee.
DK. SHEIN MGENI RASMI BARAZA LA EID
Baadhi ya
Viongozi akina Mama waliohudhuria katika Baraza la Eid el Fitri
lilofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi
Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni katika kusherehekea Sikukuu hiyo ya EID El
Fitri inayofanyika kila mwaka baada ya mfungo Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan,katika baraza hilo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na
Ikulu.] 06/07/2016.
Baadhi ya Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi na Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Eid el Fitri wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kusherehekea Sikukuu hiyo ya EID El Firi iliyofanyika leo,[Picha na Ikulu.] 06/07/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake kwa Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi na Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Eid el Fitrilililofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja, [Picha na Ikulu.] 06/07/2016.
Mawaziri wa Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi wakiangalia vitabu vya hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiitoa leo katika Baraza la Eid el Fitri lililofanyika katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Mnazi mmoja Mjini Unguja,ambapo hufanyika kila mwaka baada ya kumaliza Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 06/07/2016.
Kikosi cha Jeshi la Polisi cha FFU wakitoa heshma katika gwaride maalum la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipohudhuria katika Baraza la Eid el Fitri lililofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 06/07/2016.

AKINAMAMA DAKAWA WAFUGA NYUKI KUPAMBANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA
Ofisa
Nyuki wa Wilaya ya Mvomero, Oscar Kunambi (aliyechuchumaa kushoto)
akisaidiana na mwanakikundi cha Dakawa Green Voices, Neema Obeid, kuweka
vizuri mzinga.
Mwanahabari Judica Losai (wa pili kushoto) akimuuliza maswali Ofisa Nyuki wa Wilaya ya Mvomero, Oscar Kunambi, wakati wakiwa kwenye eneo la ufugaji wa nyuki.
Baadhi ya mizinga ya akinamama wa Dakawa Green Voices ikionekana kuning’inia kwenye miti. Mizinga hii tayari ina nyuki.
Akinamama wa Dakawa Green Voices wakisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa ufugaji nyuki, Oscar Kunambi, ambaye hayupo pichani. Ofisa nyuki wa Wilaya ya Mvomero,, Oscar Kunambi, akiwaelekeza akinamama wa Dakawa Green Voices namna ya ufugaji bora wa nyuki.

TAKRIBAN kilometa 10 kutoka Kijiji cha Dakawa kuna kitongoji cha Magogo kilichoko msituni kabisa ambako pia kuna mashamba ya mpunga.
Msitu huu ambao bado ungali na miti mingi ya asili ambayo imenusurika kucharangwa na wachoma mkaa na wanaotafuta ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo, ndiko akinamama wapatao 30 wameamua kutundika mizinga kwa ajili ya ufugaji wa nyuki katika shamba lenye ukubwa wa ekari nne.
Licha ya kujikwatua vilivyo, lakini wanapoingia katika msitu huu akinamama hawa hawana mchezo kabisa, baadhi yao wanavaa mavazi maalum ya kujikinga na nyuki na kuanza kukagua mizinga yao kama tayari nyuki wamekwishaingia.
“Kujipamba ni jambo la kawaida, lakini tunapokuja huku tuko kikazi zaidi,” anasema Neema Obeid huku akipenya kwenye vichaka kuiendea mizinga ambayo iko juu ya miti mikubwa.
Akina mama hao wa kikundi cha Dakawa Green Voices Women Group wameamua kuingia kwenye ujasiriamali wa ufugaji wa nyuki kwa malengo makubwa mawili – kupata fedha kutokana na mazao ya nyuki pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabinchi.
“Misitu inateketea, watu wanaendelea kuchoma mkaa na wengine wanafyeka miti ili wapate mashamba, lakini kwa kuanzisha ufugaji huu wa nyuki, kamwe hatutakubali kuona yeyote akikata hata fimbo, achilia mbali miti mikubwa,” anasema Bi. Mariam Bigambo, mshiriki kiongozi wa mradi huo.
Mariam Bigambo ni miongoni mwa akinamama 10 waliopatiwa mafunzo nchini Hispania mapema mwaka huu na wanatekeleza kwa vitendo mradi wa Green Voices, ambao unafadhiliwa na taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Women for Africa Foundation inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega. Hapa nchini, mradi huo unasimamiwa na asasi ya Environment Media Agenda (EMA) chini ya uratibu wa Bi. Secelela Balisidya

RONALDO AIZAMISHA WALES NA KUONYESHA UBORA WAKE DHIDI YA BALE
Timu
ya Wales imejikuta ikishindwa kuweka historia ya kutinga fainali za
michuano ya Euro baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-0 kutoka Ureno
katika mchezo uliopigwa huko Lyon.
Katika
mchezo huo washambuliaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na
Gareth Bale wote walishindwa kutikisa nyavu katika kipindi cha kwanza
kilichoishia bila kufungwa goli.
Hata
hivyo katika kipindi cha pili Ronaldo aliandika goli la kwanza la
mchezo huo kwa mpira wa kichwa katika dakika ya 50, na kuifanya Ureno
iongoze.
Wakati
Wales na Bale wao wakiwa bado wanatafakari goli hilo, Ronaldo tena
aliachia shuti ambalo Luis Nani aliugonga mpira huo na kuandika goli
la pili katika dakika ya 53.
Cristiano Ronaldo akiwa juu angani baada ya kuupiga mpira kwa kichwa ambao unaelekea wavuni
Mpira wa kichwa uliopigwa na Ronaldo ukijaa wavuni na kumshinda kipa wa Wales
Luis Nani akiugonga mpira uliopigwa na Ronaldo na kuubadilisha muelekeo na kuandika goli la pili

No comments :
Post a Comment