wenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Centre uliopo mjini Dodoma ambapo ndipo mkutano mkuu maalum wa kuthibitisha jina la Rais Dk John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho baada ya kukabidhiwa na Mtangulizi wake Mh. Dk Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akimsikiliza Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akikagua matayarisho ya
mkutano huo, kushoto ni Ndugu Rajab Luhwavi Naibu Katibu Mkuu Bara.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula akizungumza na mjumbe wa kamati kuu Ndugu Mohamed Seif Khatib.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akizungumza jambo wakati
akikagua kumbi mbalimbali za Wageni Maalum, wanaomsikiliza kulia ni
Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM na kusoho ni Nape Nnauye
Katibu Mwenezi wa CCM Taifa na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Rajab
Luhwavi.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akijaribu kipaza sauti
huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia.
Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya
Kikwete akionyesha mandhali ya ukumbi na Nape Nnauye Katibu Mwenezi
Taifa wa CCM wakati alipokuwa akikagua ukumbi huo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu
Mwenezi Taifa CCM
WARSHA YA WADAU YA KUPITIA RASIMU YA SERA YA TAIFA YA MAZINGIRA YAFANYIKA DAR ES SALAAM
Sehemu
ya wadau kutoka Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakifuatilia
Hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais
(hayupo pichani) katika Warsha ya kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya
Mazingira.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbaraka AbdulWakil akiteta jambo na
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Richard Muyungi (kushoto) mara baada
ya kufungua Warsha ya kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira.
Warsha hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Bw. Deogratius Paul.
Wana
warsha wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi mara baada ya
ufunguzi wa Warsha katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es
Salaam.
Picha na Mpiga Picha Wetu
MWENYEKITI WA CCM, DKT. JAKAYA KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MJINI DODOMA
Mwenyekiti
wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Kamati
Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma
Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John
Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt.
Ali Mohamed Shein, kuliani ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip
Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM na
Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete kwa ajili ya kufungua Mkutano wa
Kamati Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini
Dodoma Julai 21, 2016 pamoja na wajumbe wa mkutano huo. Kushoto ni
Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais Dkt John Magufuli, Wapili kushoto ni
Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kuliani ni
Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa
ajili ya kupendekeza jina la Dkt John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti na
baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili
ya kupeleka kwenye mkutano unaotarajiwa kufanyika Julai 23,2016.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuanza kwa kikao chao kwenye
ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuanza kwa kikao
chao kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokea Mwenyekiti Mtarajiwa wa
CCM,Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokuwa wakiwasili kwenye ukumbi wa
Sekretarieti, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini
Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la
Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye
Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.
Mwenyekiti
Mtarajiwa Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanachama na
wafuasi wa chama cha CCM nje ya ukumbi wa ukumbi wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Mkoani Kagera,
Joseph Mwaiswelo akitoa mada juu ya athari zakutoa ama kupokea Rushwa, vyanzo vya rushwa katika serikali za mitaa, Hatua zinazochukuliwa na taasisi kukabiliana na tatizo la rushwa na Mambo ya kuzingatiwa na Madiwani katika kupambana na rushwa.
MAKAMU WA RAIS AZINDUA RIPOTI YA LISHE YA DUNIA LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Ripoti ya Lishe ya Dunia kwenye mkutano
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
akizungumza kwenye mkutano wa kuzindua ripoti ya lishe ya Dunia ambao
mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia
Suluhu Hassan.
Baadhi ya Wadau wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa uzinduzi ya ripoti ya Lishe ya Dunia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akikata utepe kuashiria kuzindua ripoti ya Lishe ya Dunia,
katkati ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa PANITA ,Dkt. Tumaini Mikindo
……………………………………………………………………………………
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema
serikali ya awamu ya TANO itatoa msukumo mkubwa katika kukabiliana na
tatizo la utapiamlo nchini kwa kuweka mipango na mikakati imara ikiwemo
kuongeza bajeti ya lishe, kuongeza virutubisho kwenye vyakula na kutumia
vyema wataalamu wa lishe katika kupambana na tatizo hilo hapa nchini.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam Trh
20-Jul-16 katika hotuba yake ya uzinduzi wa Ripoti ya Dunia ya
Utapiamlo
ambayo imetilia mkazo masuala ya lishe kama msingi wa Maendeleo hapa nchini na Duniani kwa ujumla.
ambayo imetilia mkazo masuala ya lishe kama msingi wa Maendeleo hapa nchini na Duniani kwa ujumla.
Makamu
wa Rais amesema viongozi wa serikali katika ngazi zote za wilaya na
mikoa wanatakiwa kuunga mkono jitihada za kuondoa utapimlo nchini kwa
kuweka msukuko wa kipekee katika ngazi zote za maamuzi.
Ameeleza
kuwa jitihada zinazofanywa na serikali kwa ushirikiano na wadau wa
Maendeleo wa Ndani na Nje ya Nchi zimesaidia kwa kiasi kikubwa kushusha
kiwango cha udumavu nchini kutoka asilimia 42 mwaka 2010 hadi kufikia
asilimia 34 mwaka 2015.
Amefafanua
kuwa kutokana na mafanikio hayo, serikali imetoa mwongozo wa bajeti ya
mwaka 2016/17 kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya
masuala ya lishe kwa kila mtoto wa umri chini ya miaka MITANO hapa
nchini Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na fedha hiyo
kuwa kidogo lakini serikali itaendelea kuongeza kiasi cha fedha kwenye
bajeti zijazo hadi kufikia kiasi cha dola 8.5 sawa na shilingi elfu
18000 kwa kila mtoto hapa nchini kama
ilivyoshauriwa na jopo la wataalamu wa Benki ya Dunia na wa masuala ya afya na uchumi duniani.
ilivyoshauriwa na jopo la wataalamu wa Benki ya Dunia na wa masuala ya afya na uchumi duniani.
Makamu wa Rais pia ameziagiza Halmashauri zote
Nchini kupitia TAMISEMI zihakikishe zinatumia fedha hizo vizuri na kwa malengo
yaliyokusudiwa na sio vinginevyo.
Nchini kupitia TAMISEMI zihakikishe zinatumia fedha hizo vizuri na kwa malengo
yaliyokusudiwa na sio vinginevyo.
MADIWANI WA BIHARAMULO NA KYERWA WAFUNDWA KUHUSU MAADILI, RUSHWA NA UENDESHAJI MIKUTANO
MKUFUNZI
katika Mafunzo elekezi kwa Madiwani, Lazaro Kasumbe Busiga kutoka Mradi
wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika
la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) akitoa mada ya Kanuni na
Taratibu za Uendeshaji wa Mikutano katika Serikali za Mitaa na panoja na
mada ya Kanuni
kuhusu Maadili ya Madiwani kwa madiwani wa Halmashauri za Biharamulo na Kyerwa mkoani Kagera leo.
kuhusu Maadili ya Madiwani kwa madiwani wa Halmashauri za Biharamulo na Kyerwa mkoani Kagera leo.
Kasumbe
ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo mkoani
Dodoma, alisema lengo la mada hiyo ni kuwawezesha madiwani hao ambao
Halamashauri zao zinaanza utekelezaji wa mradi wa PS3 Mkoani Kagera
kujua taratibu muhimu zinazotumika katika kuendesha mikutano na shughuli
nyingine muhimu za serikali
za mitaa. Source: Father Kidevu Blog, Bukoba.
za mitaa. Source: Father Kidevu Blog, Bukoba.
Mwezeshaji
wa Mradi wa PS3, kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Manumbu
Daudi akiwasilisha mada kuhusu Usimamizi wa Watumishi katika Mamlaka za
Serikali za Mitaa.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Mkoani Kagera,
Joseph Mwaiswelo akitoa mada juu ya athari zakutoa ama kupokea Rushwa, vyanzo vya rushwa katika serikali za mitaa, Hatua zinazochukuliwa na taasisi kukabiliana na tatizo la rushwa na Mambo ya kuzingatiwa na Madiwani katika kupambana na rushwa.
Madiwani
wengi waliilalamikia taasisi hiyo kutoakana na kuchelewa kutolea
maamuzi baadhi ya malalamiko ya Rushwa pamoja na kukosekana kwa ofisi za
TAKUKURU katika maeneo yao na kuwataka kufungua ofisi katika ngazi ya
Kata.
Mwaiswelo
alisema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo katika kesi nyingi za
Rushwa ni kukosekana kwa ushahidi hasa pale Mtoa taarifa anaposhindwa
kufika kutoa ushahidi.
Pia
alisema lengo linguine ni kumpa Diwani ufahamu muhimu juu ya kanuni za
Maadili ya Madiwani ili kumwezesha kuwa na mwenendo unaotazamiwa na
jamii anayoitumikia katika maisha ya utekelezaji wa majukumu yake.
Mafunzo
hayo yanamuwezesha Diwani kuainisha mahitaji muhimu ya uendeshaji wa
vikao, kueleza maana na dhana ya akidi ya mikutano na vikao, kuainisha
mambo muhimu wakati wa maandalizi ya mikutano pamoja na kumuwezesha
diwani kuanisha taratibu za uundaji wa Kamati za kudumu.
Aidha
kwa upande wa mafunzo juu ya Kanuni kuhusu maadili ya Madiwani
yatamuwezesha diwani kuainisha kanuni za maadili ya madiwani ,
kuzingatia maadili hayo wakati wa utekelezaji wa majukumu yake na
yatamfanya diwani kutambua mahusiano ya kiutendaji kati yake na
watumishi wa halmashauri.
Washiriki wakiuliza maswali mbalimbali kutokana na mada zilizo wasilishwa na wawezeshaji.
Washiriki wakifuatilia kwa makini mada hizo.
Wakuu
wa Wilaya za Kyerwa, Kanali (Mstaafu) Shaaban Lissu akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde (katikati) na Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo, Wende Ng’ahala wakifuatilia mada hizo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Maswali yaliendelea kwa pande zote.
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akutana na uongozi wa Radio Maarifa iliyopo Jijini Tanga.
DC KAKONKO APOKEA MSAADA WA MADAWATI 100 KUTOKA BENKI YA CRDB KIGOMA
Mkuu
wa Wilaya ya Kankonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagaa (kulia)
akipokea moja ya madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya CRDB Kigoma na
kukabidhiwa kwake na meneja wa CRDB Tawi a Kasuu, Paul Chacha kushoto.
Wanao shuhudia ni Mkurugenzi wa Hamashauri ya Wilaya ya Kakonko,
Lusubilo Mwakibibi katikati na ofisa wa CRDB.
Mkuu
wa Wialaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala (waioketi kulia) akiwa na
Meneja wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (katikati) na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi na walio simama kushoto ni
Katibu Tawala wa Kakonko, Zainab Mbunda na watumishi wengine wakipokea
madawati hayo 100 kutoka Benki ya CRDB.
Mkuu
wa Wialaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala (kulia) akimshukuru Meneja
wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (katikati) baada ya makabidhiano ya
madawati hayo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo
Mwakibibi.
Mkuu
wa Wialaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala (wapili kushoto) akiwa na
Meneja wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (wapili kulia), Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi (kushoto) na Katibu Tawala
wa Kakonko, Zainab Mbund. Benki ya CRDB Mkoani Kigoma ilikabidhi msaada
wa madawati 100 leo ikiwa niungaji mkono jitihada za serikali katika
kukabiliana na tatizo la madawati na kuboresha maeneo ya kufundisha na
kufundishia katika shue za Msingi na Sekondari Mkoani Kigoma hususani
Wilayani Kakonko. Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala ameishukuru Benki ya CRDB kwa msaada huo ambao umeendelea kupunguza hitaji
a madawati Wilayani humo ambapo hadi sasa imekamilisha asiliamia 73 ya
mahitaji na bado wakiendelea kusubiri utekelezaji wa ahadi za madawati 3,000 kutoka kwa wadau mbalimbali walioko ndani na nje ya Wilaya hiyo.
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA BENKI YA EXIM YA CHINA IKULU NDOGO YA CHAMWINO MKOANI DODOMA.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu
ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang wa kwanza kulia katika
Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma. Wakwanza kushoto ni Balozi wa
China hapa nchini Lu Youqing.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza
kikao cha pamoja na ujumbe wa Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang
katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang
(watatu) kutoka kulia mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu ndogo
ya Chamwino mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Balozi wa China hapa
nchini Lu Youqing wakwanza kushoto, Waziri wa Fedha na Mipango Filipo
Mpango, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Suzan Kolimba.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang
watatu kutoka kulia mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu ndogo ya
Chamwino mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
kwa msisitizo mara baada ya kikao chake na ujumbe wa Rais wa Benki ya
Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika
Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Prof. Ndalichako akiomba chuo Kikuu Ardhi kubuni majengo ya shule.
Waziri
wa Elimu , Sayansi , teknolojia na mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce
Ndalichako wa kwanza kulia akitoa maelekezo kwa Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia alipotembelea banda la
chuo hiko wakati wa ufunguzi wa wa maonesho ya 11 ya elimu ya juu ,
sayansi na teknolojia leo jijini Dar es salaam wa (tatu kulia) ni Katibu
Mtendaji (TCU) Prof. Eleuther Mwageni.
Afisa
uhusiano Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu Ardhi Bi. Hadija Maulid wa
kwanza kulia akitoa maelekezo kwa baadhi ya wateja waliofika kwenye
banda lao wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 11 ya elimu ya juu ,
sayansi na teknolojia yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud-Maelezo
Chuo Kikuu Ardhi kimetakiwa
kubuni majengo ya shule kwa kiwango kikubwa na teknolojia ya sasa ili
kuweza kupata majengo imara na usanifu mkubwa nchini kwa ajili ya
maendeleo ya elimu kwa wasomi wa ndani.
Akizungumza hayo Waziri wa Elimu ,
Sayansi , teknolojia na mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako
wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 11 ya elimu ya juu , sayansi na
teknolojia na kutembelea banda la chuo hiko amesema kuwa wana uwezo wa
kubuni majengo hivyo wajitahidi na kuwakilisha kwake.
“Kwa kuwa mmeweza kunionyesha
baadhi ya ubunifu wa majengo katika banda lenu basi nawaomba muendelee
na kubuni majengo ya shule kwa usanifu mkubwa ili yatusaidie kukuza
elimu nchini” aliongeza Prof. Ndalichako.
Katika maonyesho hayo yalioanza
leo na kufikia tamati Julai 22 mwaka huu banda la Chuo kikuu Ardhi kina
baadhi ya michoro ya majengo yaliyobuniwa na wanafunzi wa chuo hiko na
ramani mbalimbali za majengo.
DKT. REGINALD MENGI AMTUMIA UJUMBE MZITO WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA
Mwenyekiti
wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akizungumza
katika Kongamano la Mashauriano ya Ushiriki wa Watanzania katika
Uwekezaji kwa niaba ya TPSF ambapo alitumia fursa hiyo kuishauri
serikali mambo ambayo anaamini serikali ikiyafanyia kazi uchumi wa
Tanzania utakua kwa kasi tofauti na sasa.
Waziri
wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye
Ulemavu Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba katika kongamano hilo pamoja
na kujibu baadhi ya hoja alizotoa Dkt. Mengi.
WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NA CONGO JIJINI DAR ES SALAAM
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akizungumza na
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem (kulia) masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika
katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Wapili
kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, kushoto
ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu,
Balozi Simba Yahya. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Balozi wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Jean-Pierre Mutamba (kushoto)
masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kongo na Tanzania. Mazungumzo
hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam
leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza na
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem (kulia) wakati alipokuwa
akizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na
Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu,
jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara
hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, kushoto ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali
Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
RASILIMALI KUBWA NI BINAADAMU, ASEMA MKUU WA WILAYA YA IRINGA AKIFUNGUA KONGAMANO
Mkuu
wa wilaya Iringa, Richard Kasesela akipokea kitabu toka kwa Bwana
Daniel El Noshokaty ambaye alikabidhi vitabu kwa kila mwanafunzi kwa
ajili ya kujisomea.
MKUU
wa wilaya ya Iringa,Richard Kasesela leo amefungua kongamano la
wanafunzi wa shule za sekondari kujadili maendeleo na matumizi ya
rasilimali.
Kongamano
hilo liliandaliwa na umoja wa walimu wa masomo ya Uraia CETA
wakishirikiana na KAS -taasisi ya kujerumani. Katika hotuba yake, mkuu
wa wilaya alisistiza kuwa rasilimali kubwa inayotakiwa kufanyiwa kazi ni
Binadamu.
Alisema
" binadamu akijengewa uwezo anaweza kubadilisha rasilimali hizi ziwe na
faida kwa maisha yake na wengine". Mkuu wilaya alisistiza suala la
nidhamu kama msingi wa maisha, upendo na udailifu vinaleta mabadiliko
katika maisha ya mwanadamu.
Naye
Mwakilishi wa KAS, Bwana Daniel El Noshokaty akimkaribisha Mkuu wa
wilaya alisema, Taasisi ya KAS imeanza toka mwaka 1964 ikiwa na kazi ya
kuelimisha wananchi juu ya elimu ya uraia hapa Tanzania, na imetoa
vitabu vingi kuhakikisha Watanzania wanapata uelewa wa elimu hiyo.
Kwa
Iringa wataendelea kuelimisha wanafunzi watambue fursa zilizopo katika
rasilimali nyingi. Kongamano la siku moja lilikuwa na na mada zenye
kutambua uwezo wa nchi katika kuleta thamani kwa rasilimali zilizopo
Tanzania hasusan Iringa.
Shule za Lugalo, St Joseph, Kleruu, Kwelu, Highland na Mkwawa zililishirki katika kongamno hilo.
MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA UPANUZI NA UKARABATI UWANJA WA NDEGE DODOMA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza king’ola kuashiria uwekaji jiwe la
msingi la Mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma
Julai 302016. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan
Lugimbana. Kushoto ni Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafari Mwanyembwa na
wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa.
Waziri Mkuu,Kassim Majliwa akikagua upanizi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi mjini Dodoma Julai 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuweka jiwe la misngi la upanuzi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Dodoma mjini Dodoma Julai 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la upanuzi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Dodoma Julai 20, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Lugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majliwa akikagua upanizi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi mjini Dodoma Julai 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuweka jiwe la misngi la upanuzi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Dodoma mjini Dodoma Julai 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la upanuzi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Dodoma Julai 20, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Lugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
UDOM WASHIRIKI MAONESHO YA VYUO VIKUU KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE
Mhadhiri
Msaidizi kutoka chuo kikuu cha Dodoma, Lucian Ngeze akitoa ufafanuzi
kuhusu kutenga matumizi ya LUKU ya nyumba moja kadili ya matumizi ya
kila mtu.
Mhadhiri kutoka collage ya Education chuo kikuu cha Dodoma, Dk. Pambasi Tandika akimsikiliza mwanafunzi baada ya kumweleza jinsi ya kujiunga chuoni hapo wakati wa maonesho ya vyuo vikuu yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali hapa nchini.
CHUO kikuu cha Dodoma chashiriki Maonesho ya Vyuo vikuu hapa nchini yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambayo yatafanyika kwa kwa takribani siku tatu kuanzia leo Julai 20 hadi Julai 22 mwaka huu.
Mhadhiri kutoka collage ya Education chuo kikuu cha Dodoma, Dk. Pambasi Tandika akimsikiliza mwanafunzi baada ya kumweleza jinsi ya kujiunga chuoni hapo wakati wa maonesho ya vyuo vikuu yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali hapa nchini.
CHUO kikuu cha Dodoma chashiriki Maonesho ya Vyuo vikuu hapa nchini yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambayo yatafanyika kwa kwa takribani siku tatu kuanzia leo Julai 20 hadi Julai 22 mwaka huu.
Katika
maenesho hayo Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa
Joyce Ndalichako ametembelea mabanda mbalimbali katika maonesho hayo ya
Vyuo Vikuu(TCU)
Mhadhiri Msaidizi kutoka collage ya CIVE chuo kikuu cha Dodoma, Ms Tulibako Tulibonywa akitoa ufafanuzi mbele ya vijana waliotembelea kwenye banda la chuo hicho
Mhadhiri Msaidizi kutoka collage ya CIVE chuo kikuu cha Dodoma, Ms Tulibako Tulibonywa akitoa ufafanuzi mbele ya vijana waliotembelea kwenye banda la chuo hicho
UTUMIKISHWAJI WA WATOTO BADO NI TATIZO NCHINI
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya
utangulizi kuhusu Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka
2014 katika uzinduzi wa matokeo hayo uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Mwakilishi
wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Azfar Khan akizungumza leo
jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa
Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014.Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Dkt. Abdallah Possi akionyesha Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014. Uzinduzi huu umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA)
Na: Veronica Kazimoto
UTUMIKISHWAJI wa Watoto bado ni tatizo kubwa nchini ambapo kati ya watoto watatu wenye umri wa miaka 5 – 17, mtoto mmoja anafanya kazi ambazo ni hatarishi katika maisha yake kiafya, kimwili na kisaikolojia.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Dkt. Abdallah Possi wakati wa uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014 uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
Matokeo ya Utafiti huo yameonyesha kuwa, kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5 – 17, watoto milioni 4.2 sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali za kiuchumi.
Matokeo haya yameonesha kuwa hali ya utumikishwaji wa watoto umepungua kutoka asilimia 31.1 kwa mwaka 2006 hadi asilimia 28.8 kwa mwaka 2014.
“Kutokana na matokeo ya utafiti huu, ni dhahiri kwamba, utumikishwaji wa watoto bado ni tatizo kubwa nchini na duniani kwa ujumla. Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kazi Duniani (ILO), asilimia 11 ya watoto wote duniani sawa na watoto milioni 264 wenye umri wa miaka 5 – 17 wanatumikishwa kwenye ajira za aina mbalimbali,” amesema Dkt. Possi.
WAZIRI MKUU ATAKA CDA ITENGE ENEO LA BANDARI KAVU
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Dodoma pamoja na
Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kutenga eneo la bandari kavu
ili mkoa huo uweze kupokea na kuhifadhi mizigo na kurahisisha biashara
kwa mikoa jirani.
Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatano, Julai 20, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa awamu ya kwanza ya ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma.
"Ninazo taarifa kiwa Benki ya Dunia kupitia shirika la Local Investment Climate (LIC) tayari wametenga fedha kiasi cha shilingi milioni 100kwa ajili ya kujenga bandari kavu na tayari fedha hizo zimeshapokelewa na Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kazi hiyo.”
“Uzuri wa mkoa wa Dodoma kuna reli. Kwa hiyo makontena yanayoenda Burundi na mahali kwingine yatashushwa hapa na kukaa kwenye bandari kavu; hivyo, wafanyabiashara watachukua mizigo yao hapa badala ya kupata shida ya kuyafuata Dar es Salaam kama ilivyo sasa,” amesema.
Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano itoe wataalam ili washirikiane na CDA kufanikisha kazi hiyo. Amesema hatua hiyo itasaidia kurahisisha wananchi na wafanyabiashara kupata huduma hiyo kwa urahisi na umbali mfupi tofauti na hali ilivyo sasa.
Ameuagiza pia uongozi wa CDA utenge eneo maalum la kituo cha biashara (commercial hub)) ili Kanda zote zinazozunguka mkoa wa Dodoma na nchi jirani wapate bidhaa mbalimbali kutokea Dodoma. “Kutokana na upanuzi huu na fursa zinazojitokeza, hii iende sambamba na kuwatengea maeneo maalum wajasiriamali badala ya kuwaacha kuzagaa kila mahali,” amesisitiza Waziri Mkuu.
Akizungumzia kuhusu upanuzi wa uwanja huo, Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi huo kutaziwezesha ndege zenye uwezo wa kubeba abiria 90 zianze kutua kwenye kiwanja hicho na kukuza fursa za kibiashara zinazohitaji usafiri wa haraka na salama.
“Katika Ilani ya CCM, suala la ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya viwanja vya ndege limepewa umuhimu mkubwa sana na ndiyo maana leo tunashuhudia utekelezaji wa ahadi za Mheshimiwa Rais ambaye amewezesha upatikanaji wa fedha za ukarabati na fidia kwa wananchi wa kata za Makole na Uwanja wa Ndege ambao maeneo yao yametwaliwa na Serikali ili kufanikisha upanuzi huu,” amesema.
Amesema uzinduzi huo ni mwanzo tu wa utekelezaji wa miradi mingine ya kuboresha na kupanua viwanja vya ndege nchini ambapo Serikali kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato ya ndani na ya nje, itaendelea kuboresha zaidi miundombinu na huduma nyingine za viwanja vya ndege kama vile Mtwara na Mwanza ambavyo amesema vitapanuliwa kufikia hadhi ya kimataifa.
MADUKA MAKUBWA YA BIDHAA YA TESCO YAANZA KUUZA PILIPILI KALI KULIKO ZOTE DUNIANI
Pilipili
kali kuliko zote duniani sasa imeanza kuuzwa kwenye maduka makubwa ya
bidhaa ya Tesco, pilipili ambayo inaogopwa mno kwa ukali wake kuliko
hata sprei ya kutoa machozi ya pilipili.
Pilipili
hiyo iitwayo Carolina Reaper sasa inaweza kununuliwa kwa mara ya
kwanza Uingereza, na imewekewa tahadhari kwa wateja kutoishika kwa
mikono yao bila kuvaa glovu.
No comments :
Post a Comment