Msemaji wa
Chama cha Mapinduzi CCM Christopher Ole Sendeka akizungumza na
waandishi wa habari leo katika Makao Makuu Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba
kushoto ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba
Bakari Hamis.
……………………………………………………………………………………………………..
Jana tarehe 27/7/2016 Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walitoa kauli kwa Waandishi wa Habari
kupitia Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Ndugu Freeman Mbowe (Mb). Tamko
hilo kama ilivyo kawaida ya CHADEMA lilijaa uongo mwingi na ghiliba
nyingi za kibabaishaji na kuthibitisha ukweli kuwa kwa hakika kutokana
na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dr. John Pombe Magufuli
wapinzani nchi hii wamekosa ajenda na hivyo njia peke yake wanayoona
inafaa ili waendelee kufanya utapeli ni kutunga uongo, kujiaminisha
katika uongo huo na kuusambaza uongo huo ili kujaribu kupata wafuasi.
Katika uongo na uzushi huo
walioutangaza jana, CHADEMA wanasema wameamua kufanya mikutano na
maandamano nchi nzima kwa tarehe waliyoitaja na maandamano hayo
yatafanyika chini ya operesheni waliyoiita UKUTA. Kimsingi hoja
walizozitumia kufikia uamuzi wao bila kuzirudia zimejaa upotoshaji na
uongo uliokithiri. Kwa mfano wanadai Serikali imezuia mikutano yote ya
vyama vya siasa, huku wakijua kuwa ni uongo kwani Serikali haijazuia
mikutano kwenye majimbo yao, Wabunge wako huru kufanya shughuli zao
kwenye majimbo yao, na tumeona Wabunge wakifanya shughuli zao majimboni
bila shida wakiwemo hao wa vyama vya upinzani.
Lakini vyama vya siasa kufanya
shughuli kwa mujibu wa katiba ya vyama vyao sio jambo lililozuiliwa pia,
ndiyo maana tumeshuhudia vyama vikifanya mikutano yao ya kikatiba bila
tabu.
Lakini mfano mwingine wa hoja za
uongo na uzushi, ni hoja eti ya Serikali hii ya Awamu ya Tano kuwa ya
kidikteta. Udikteta hasa unaosemwa na Chadema ni upi? Ni huu wa
kushughulikia watumishi hewa? Ni huu wa kuwabana wakwepa kodi? Ni huu wa
kupunguza na kudhibiti safari za nje? Ni huu wa kubana matumizi ya
Serikali? Ni huu wa kufukuza wabadhirifu na wazembe kazini? Hivi
udikteta huo ni huu wa kushughulikia mafisadi mpaka kuanzisha mahakama
yao? CCM inaamini Watanzania walio wengi wanaunga mkono hatua
zinazochukuliwa na Rais Magufuli na Serikali yake, sasa kama kwa Chadema
hatua hizi ndiyo tafsiri yake ni udikteta basi bila shaka wao ni sehemu
ya mfumo mbovu ndiyo maana wako tayari kuleta vurugu ili wautetee.
Kwa kuwa CHADEMA wamezoea kujenga
Chama chao kwa harakati zinazohusisha kumwaga damu za Watanzania
wasiokuwa na hatia, ukweli huu wa maelekezo ya Serikali hawausemi,
isipokuwa wanafanya juhudi kubwa kuhakikisha wanafanya mambo ambayo
mwisho wa siku yatasababisha vurugu, uvunjifu wa amani na umwagaji damu.
Lakini pengine ni muhimu
Watanzania na wapenda amani nchini na duniani wakajiuliza ni kweli kuwa
lengo la hizi vurugu na maandamano haya ni la kujenga na si kubomoa? Kwa
nini kila operesheni ikifanywa na CHADEMA huwa inaambatana na
umwagikaji wa damu za Watanzania wasiokuwa na hatia? Wakati wa
Maandamano hayo inapotokea madhara ni kwa nini waathirika huwa sio
viongozi waanzilishi wa maandamano hayo wala wake au waume zao au watoto
wao au hata ndugu zao wa karibu bali huwa ni watu wengine nje ya hao
ndugu zao wa karibu? Mpaka lini damu za Watanzania wasio na hatia
zitaendelea kutumika kutafuta umaarufu wa CHADEMA na viongozi wake?
Hii ni kwa faida ya nani hasa?
Kwa nini pamoja na kuelekezwa namna bora ya kufanya siasa wao huwa
hawataki kufuata utaratibu? Hivi ni kweli kuwa hawajui bila kufuata
utaratibu jambo lolote huwa ni vurugu?
Chama Cha Mapinduzi kinapenda
kuwakumbusha Watanzania kuwa ni vizuri kutafakari na kujiuliza maswali
ya msingi kabla ya kuamua kushiriki au kuruhusu watoto wetu kwenda kuwa
kafara ya walafi wachache wa madaraka. Ni vizuri tukayakumbuka matukio
kwenye operesheni kama hizi yaliyopoteza maisha ya vijana wetu na
matokeo ya kila operesheni.
Pamoja na ukweli kuwa hakuna
operesheni yeyote kati ya zote zilizowahi kufanywa na Chadema ambayo
imewahi kuwasaidia Watanzania wa kawaida zaidi ya kujenga umaarufu wa
viongozi wachache wa Chadema na kuneemesha matumbo yao na ya familia
zao, operesheni zote zimepoteza maisha ya Watanzania kadhaa wasiokuwa na
hatia wala wasiofaidika kwa lolote na operesheni hizo.
Kama nia ni njema kwa nini
hawataki kufuata Sheria na taratibu tulizojiwekea? Demokrasia gani
isiyokuwa na mipaka? Demokrasia bila mipaka ni fujo. Tunaomba vyombo
vinavyohusika visisite kuchukua hatua zinazostahili bila kumuonea mtu
lakini bila kufumbia macho vitendo vyenye lengo la kuwahujumu Watanzania
waliowengi walioamua kuchapa kazi kuitikia wito wa Rais na Serikali ya
Awamu ya Tano ya kufanya kazi.
Lakini pia tunawashauri
Watanzania, wapenda amani, utulivu na maendeleo kupuuza wito wa vurugu
na uvunjifu wa amani badala yake wajikite kwenye kuchapa kazi na
kujitafutia maendeleo yao kwa kufanya kazi kwa bidii.
Maendeleo hayaji kwa maandamano,
maendeleo huja kwa kuchapa kazi kwa bidii. Maendeleo hayaji kwa vurugu
na fujo nchini, bali amani na utulivu ni vichocheo muhimu vya maendeleo
ya kweli.
Imetolewa na:-
Christopher Ole Sendeka (MNEC),
MSEMAJI WA CHAMA
28/07/2016
WAZIRI MKUU ATOA SIKU MOJA KWA HALMASHAURI YA WILAYA TEMEKE KUMALIZA TATIZO LA AJIRA ZA MIKATABA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia walimu na wanafunzi wa Shule ya
Msingi ya Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kuwasili shuleni hapo
kukbidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya Shule za
Dar es salaam Julai 28, 2016.Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, Theresia Mmbando, Mkuu wa mkoa wa Dar
es salaam, Paul Makonda na Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaviva.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa Temeke baada ya
kuwasili kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi kukabidhiwa madawati na fedha
shilingi milioni 100 kwa ajili ya Shule za Dar es salam Julai 28,
2016. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. (Picha na
Oisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi
ya wanafunzi na mmoja wa wananchi waliohudhuria hafla ya kukabidhi
madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa Waziri Mkuu kwenye shule ya
Msingi yaChamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mlkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi, Augustine Mahiga (katikati)
na Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya Mabohora Nchini katika hafla ya
kakabidhi madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa shule za Dar es
salaam iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es
salam Julai 28, 2016.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wanafunzi wa Shule ya Msingi ya
Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kupokea madawati na fedha
shilingi milioni 100 kwa ajili ya mkoa wa Dar es salaam Julai 28,
2016.Madawati ayo yalitolewa na Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika ya Mashariki ikishirikiana na Ubalozi wa Kuwait nchini pamoja na
Jumuiya ya Mabohora nchini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru , Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya
Mabohora nchini baada ya kukabidhiwa madawati 105 kwenye Shule ya Msingi
ya Chamazi jijini Dar es salam Julai 28, 2016. Kushoto ni Balozi wa
Kuwait nchini, Jaseem Al Najem na Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Temeke kuondoa wafanyakazi wa mkataba
kwa anjia ya kuwapa ajira ya kudumu kwa wenye sifa na kuwaondoa
wasiokuwa na sifa ifikapo Julai 30 mwaka huu.
Amesema kitendo cha kutowaajiri
na kuwatumikisha kwa mikataba kwa muda mrefu kinasababisha wakose
stahiki zao jambo ambalo si halikubaliki.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo
(Alhamisi, Julai 28, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa
halmashauri hiyo na kusisitiza kwamba ni lazima sula hilo lishughulikiwe
haraka kwa sababu hayo ndio matundu watumishi hewa.
“Mnawatumikisha watu kama vibarua
kwa muda mrefu, hapa kuna wengine wanafanya kazi kwa mikataba kwa miaka
mitano hadi sita hii haikubaliki kwani mnawakosesha stahili zao pale
mnapowaachisha kazi,” amesema.
Awali Kaimu Ofisa Utumishi wa
Manispaa hiyo Zaitun Hassan alisema wamekuwa wakitoa ajira za mikataba
kwa sababu wamekosa watu wenye sifa za kuweza kuajiriwa husan madereva.
“Kwa mara ya mwisho umetangaza
lini nafasi za ajira? Katika mkoa wa Dar es Salaam kweli wanaweza
kukosekana madereva wenye sifa za kuajiriwa? Alihoji Waziri Mkuu.
Zaitun alisema kuwa madereva
wengi wanaojitokeza pindi wanapotangaza ajira wanashindwa kufikia vigezo
ikiwemo kuwa na cheti cha VETA na badala yake wanakuwa na cheti cha
kidato cha nne tu.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema
kuwa kuna wafanyakazi wengine katika Idara ya Uhasibu na Ujenzi ambao
nao wameajiriwa kwa mkataba hivyo amemtaka Ofisa Utumishi kuomba kibali
cha kuajiri kwa Katibu Mkuu Utumishi.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kufanya tathmini
ya maeneo yote ya shule kwenye mkoa wake na watakaobainika kuingia
katika maeneo hayo waondolewe haraka.
Amesema baada ya kukamilisha
utengenezaji wa madawati kinachofuatia sasa ni ujenzi wa vyumba vya
madarasa, ambapo amezitaka halmashauri kuweka mipango ya kujenga
majengo ya madarasa ya ghorofa ili waweze kuwa na madarasa mengi katika
eneo dogo.
Awali Waziri Mkuu alipokea msaada
wa madawati 705 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya
msingi Chamazi wilayani Temeke ambapo kati yake Ubalozi wa Kuwait nchini
Tanzania umetoa madawati 600 na Jumuia ya Mabohora imetoa madawati 105.
Pia Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Agustino Mahiga alimkabidhi
Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 85 fedha zilizochangwa na watumishi wa
wizara hiyo kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati.
Dk. Mahija alisema watumishi hao
walichanga sh. milioni 100 kwa ajili ya utengenezaji wa madawati ambapo
sh. milioni 15 wamekabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe
ambaye alikuwa mtumishi wa wizara hiyo ili naye akatengeneze madawati
kwa shule za wilayani kwake.
Kwa upande wake Balozi wa Kuwait
nchini Jaseem Al Najem amesema Serikali ya Kuwait itaendelea
kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika shughuli zote za maendeleo
hususan katika sekta za elimu na afya.
WAREMBO WANAOWANIA SHINDANO YA MISS TANGA 2016 USIPIME SASA KUFANYIKA IJUMAA MJINI TANGA
Warembo wanaowania Taji la Mrembo wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016) wakiwa kwenye pozi katika hotel ya Tanga
Beach Resort kutakapofanyika shindano hilo Ijumaa Kesho.
Beach Resort kutakapofanyika shindano hilo Ijumaa Kesho.
Warembo hao wakiwa kwenye picha ya pozi |
Mratibu wa Shindano ya Miss Tanga 2016,Mboni Muya akizungumza na waandishi wa Habari leo kuhusiana na maandalizi ya kuelekea shindano hilo |
Warembo hao wakimsikiliza Mratibu waShindano ya Miss Sinza 2016 ambaye aliitembelea kambi hiyo leo |
Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa
nchini,Benny Kisaka akitoa nasaha kwa warembo wanaotarajiwa kushiriki
kinyang’anyiro cha kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga
2016 )itakayofanyika Ijumaa kesho kwenye Ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach
Resort.
nchini,Benny Kisaka akitoa nasaha kwa warembo wanaotarajiwa kushiriki
kinyang’anyiro cha kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga
2016 )itakayofanyika Ijumaa kesho kwenye Ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach
Resort.
Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa
nchini,Benny Kisaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na warembo
wanaotarajiwa kushiriki shindano la kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa
Tanga Ijumaa
nchini,Benny Kisaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na warembo
wanaotarajiwa kushiriki shindano la kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa
Tanga Ijumaa
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
Manispaa ya Dodoma yakusanya asilimia 80.28 ya mapato katika vyanzo vyake
NA RAMADHANI JUMA
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma
imefanikiwa kukusanya asilimia 80.28 ya mapato kutoka katika vyanzo
vyake mbalimbali vya ndani katika mwaka wa fedha 2015/2016 uliomalizika
Juni 30 mwaka huu.
Katika mwaka huo wa fedha
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ilipanga kukusanya shilingi
4,566,075,181 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani (own sources) ambapo
mpaka mwisho wa mwaka huo makusanyo halisi ni 3,665,699,279 sawa na
asilimia 80.28 ya makisio.
Akizungumza katika kikao cha
mwaka cha Baraza la Halmashauri ya Manispaa hiyo, Meya wa Manispaa hiyo
Mstahiki Jaffar Mwanyemba aliwaambia wajumbe wa Baraza hilo kuwa,
mafanikio hayo yametokana na uchapaji kazi wa watendaji na madiwani wa
Manispaa hiyo.
Katika kikao hicho kilichofanyika
katika ukumbi wa Manispaa, Mstahiki Mwanyemba aliwapongeza wote
waliohusika kwa namna yeyote katika kufikia hatua hiyo huku akitoa wito
kwa Ofisi ya Mkurugenzi na Madiwani wa kuimarishwa kwa juhudi zaidi
katika ukusanyaji katika mwaka wa fedha 2016/2017.
“Mwaka mpya wa fedha umeshaanza
hivyo Mkurugenzi na watendaji wako anzeni kukusanya kodi mapema…na
waheshimiwa madiwani tuongeze nguvu katika kusimamia vyanzo vya mapato
katika maeneo yetu” alisema.
Aidha, katika mkutano huo ambao
kwa mujibu wa kanuni unakuwa na ajenda mbili tu ambazo ni kujadili
taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa Halmashauri kwa mwaka uliopita na
kupitia na kupitisha ratiba ya vikao vya Halamshauri kwa mwaka
unaofuata, wajumbe walipitisha ratiba ya vikao vya Halmashauri hiyo kwa
mwaka wa fedha 2016/2017 .
HOMA YA INI B NA C KUTOKOMEZWA IFIKAPO MWAKA 2030
Baadhi
ya vijana waliokuwa wakitumia dawa za kulevya wakiwa na mabango yenye
ujumbe mbalimbali wa kutokomeza homa ya ini wakielekea kwenye
maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe
Yanga Dar es Salaam leo mchana.
Bango likihimiza kuungana kutokomeza homa ya ini.
Maandamano
yakiendelea kuelekea viwanja vya Mwembe Yanga. Katikati ni Mratibu wa
Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan.
Vijana waliopo kwenye mtandao wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mratibu wa Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan, akizungumza kwenye maadhimisho hayo. |
Mwenyekiti wa TanPud Tanzania, Godfrey Ten, akizungumza katika maadhimisho hayo.
Ofisa
Maendeleo ya Jamii, Mratibu wa Asasi za Kiraia kutoka Tume ya Kuratibu
Udhibiti wa Dawa za Kulevya Tanzania, Salome Mbonile, akizungumza kwenye
maadhimisho hayo.
Mwakilishi wa Taasisi ya Pasada, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mratibu
wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya Temeke, Mwajuma Mwihumbo
akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo.
Maadhimisho yakiendelea.
Vijana waathirika na dawa za kulevya wakicheza kwenye maadhimisho hayo.
Meneja wa Afya Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya Medicins Du Monde akizungumza kuhusu ugonjwa huo.
Wageni waalikwa katika picha ya pamoja.
Dotto Mwaibale
UGONJWA
wa homa ini umepangwa kutokomezwa ifika mwaka 2030 imefahamika ambapo
watu wapatao milioni 1.4 upoteza maisha ulimwenguni kutokana na
maambuki ya ugonjwa huo ulimwenguni hasa kwa wale wanaotumia mihadarati
kwa njia ya kujidunga.
Hayo
yalibainishwa na Mratibu wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya
Temeke, Mwajuma Mwihumbo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya homa ya ini
yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam jana.
Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza ufahamu kuhusu na kuungana na juhudi za ulimwengu za kutokomeza homa ya ini.
Alisema mada ya kampeni ya kimataifa ya homa ya ini ya mwaka huu ni utokomezaji ambao ni mwaka muhimu kwa homa ya ini.
Alisema
lengo la maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na asasi za kiraia,
wafanyakazi wa huduma za afya, taasisi na vikundi vya utetezi na
ushawishi ni kuongeza ufahamu wa homa ya ini B na C hasa kwa makundi
hatarishi kama watumiaji wa mihadarati wanaojidunga.
Meneja
wa Afya Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya
Medicins Du Monde alisema katika mkutano mkuu wa 69 wa Shirika la Afya
Duniani (WHO) ni serikali zote ziliazimia kwa pamoja kuidhinisha mkakati
wa ulimwengu wa utokomezaji wa homa ya ini.
Alisema
hadi Februari 2016 nchi 36 zilikuwa zina mipango ya kitaifa ya
utokomezaji wa homa ya ini na nchi 33 zipo katika mikakati ya kuandaa
mipango hiyo.
“Mkakati
unalenga kutokomeza homa ya ini B na C ifikapo mwaka 2030 ambapo
unahusisha malengo ya tiba ambayo iwapo yatafikiwa yatapunguza vifo
vinavyosababishwa na homa ya ini kwa asilimia 65 na kuongeza huduma ya
tiba kwa asilimia 80 hivyo kuokoa maisha ya watu milioni 7.1 ifikapo
mwaka 2030” alisema Dk. Aikaeli
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MAJALIWA ATAKA MABARAZA YA MADIWANI KUFANYA MAPITIO YA UPUNGUFU VYA VYUMBA VYA MADARASA KATIKA HALMASHAURI NCHINI
Na Beatrice Lyimo
MAELEZO- Dar es Salaam
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
Majaliwa ametoa maagizo kwa Mabaraza ya Madiwani nchini kufanya mapitio
katika shule zote za Halmashauri ili kujua upungufu wa madarasa na
kuanza mkakati wa utekelezaji wa ujenzi wake.
Aliyasema hayo leo wakati
akipokea mchango wa madawati kwa shule ya msingi Chamazi kutoka Wizara
Ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikiwa ni utekelezaji wa agizo
la Rais la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari
nchini.
Mhe. Majaliwa alisema suala la
upatikanaji wa madawati linakwenda sambamba na ujenzi wa madarasa hivyo
ni wajibu wa kila halmashauri kuweka mkakati wa ujenzi wa vyumba vya
madarasa kwani elimu bora ni pamoja na kuwa na mazingira rafiki ya
kusomea.
‘Mbali na utekelezaji wa agizo
la Rais juu ya mkakati wa upatikanaji wa madawati, suala hili linakwenda
sambamba na ujenzi wa madarasa hivyo Serikali imeanza utekelezaji wa
ujenzi huo kwa maeneo machache hivyo ni jukumu la halmashauri
kuhakikisha mnaandaa mikakati ya kuongeza vyumba vya madarasa’ alisema
Majaliwa.
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa
alisema kuwa Serikali imeanza mkakati wa utekelezaji wa mpango wa
kutumia mfumo mpya wa upandishaji madaraja walimu kwa kuwa mfumo wa
uliuotumika awali haukuwa na tija kwa maslahi ya walimu nchini.
Akipokea madawati hayo Waziri
mkuu alisema kuwa anajua shida iliyopo ya upungufu wa madawati katika
wilaya ya Temeke hivyo na kugawa madawati hayo katika shule tatu
zilizopo katika Wilaya hiyo ikiwemo shule ya msingi Chamazi, shule ya
msingi Mbande pamoja na shule ya msingi Majimatitu .
Kwa upande wake Waziri wa
Wizara Ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine
Mahiga alisema wizara yake ina jukumu la kuhakikisha inaitangaza nchi
ili kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi, na kuongeza kuwa elimu
bora ni msingi imara katika kufanikisha hilo.
Waziri Mahiga alisema Ubalozi
wa Kuwait nchini pamoja na Jumuiya ya Mabohora wameikabidhi Serikali
jumla 405 ili kuunga mkono jitihada za Rais ikiwemo
“Serikali ya Kuwait kupitia
Ubalozi wake hapa nchini wametoa madawati 300 na kuahidi kutoa mengine
300 na Jumuiya ya Mabohora nao wamechangia madawati 105” alisema Balozi
Mahiga.
Kwa mujibu wa Waziri Mahiga
alisema watumishi wa Wizara yake walichanga kiasi cha Tsh. Milioni 100
ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha umma ili kuhamasisha umma kuhusu zoezi la
upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na Sekondari nchini.
WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI HUNDI YA TSH. 85 MILIONI KWA JESHI LA MAGEREZA ZITAKAZOTUMIKA KUTENGENEZEA MADAWATI, JIJINI DAR
Waziri
Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi mfano wa hundi Afisa
Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, SACP. John Masunga(kushoto) leo Julai
28, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chamazi. Waziri Mkuu
amelekeza Fedha hizo zitumike kutengeneza madawati ya shule za msingi
Majimatitu na Mbande zilizopo Wilayani Temeke.
Waziri
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa ameketi kwenye madawati
yaliyotolewa kwa Msaada wa Ubalozi wa Kuwait Nchini Tanzania kama
inavyoonekana katika picha(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
…………………………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………………………
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) amekabidhi hundi ya Tsh.
85 Milioni kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza ili litengeneze jumla ya
madawati 1,703 yatakayotumika katika Shule za Msingi za Majimatitu na
Mbande zilizopo Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es Salaam.
Hafla ya makabidhiano hayo
yamefanyika leo tarehe 28 Julai, 2016 katika Viwanja vya Shule ya
Msingi Chamazi iliyopo Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es salaam ambapo
Waziri Mkuu Majaliwa amekabidhi madawati katika Shule ya Msingi Chamazi
yaliyotolewa na Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania na Jumuiya ya
Mabohora Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Waziri Mkuu Majaliwa amewashukuru na kuwapongeza Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kutoa mchango huo na pia
amewapongeza wadau wengine ambao wameitikia wito wa Rais Magufuli wa
kuchangia madawati kwa lengo la kuondoa tatizo la wanafunzi kukaa chini.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema
baada ya kuanza kutekeleza ahadi ya kuondoa ada kwa shule za msingi na
sekondari, idadi ya wanafunzi waliojiandikisha kuanza darasa la kwanza
katika shule mbali mbali imeongezeka hali iliyosababisha upungufu wa
madawati lakini tatizo hilo limetatuliwa kwa kiasi kikubwa hapa nchini.
Aidha, amelitaka na Jeshi la
Magereza kutengeneza madawati hayo mapema iwezekanavyo ili yakamilike
haraka na kuanza kutumika katika Shule za Msingi Majimatitu na Mbande
kwani shule hizo zinakabiliwa na idadi kubwa ya Wanafunzi hapa Jijini
Dar es Salaam.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine
Mahiga, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mhe. Ramadhani Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Mhe. Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam,
Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam, Wabunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa wa Dar es Salaam, Wananchi pamoja na wanafunzi wa Shule ya msingi
Chamazi.
Lucas Mboje, Mrakibu Msaidizi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
28 Julai, 2016.
TUNAZISUBIRI NEC NA ZEC KUIPIGIA KURA YA MAONI KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Mwenyekiti
wa Kikosi cha Kupambana na Haki za Mirathi (KIKUHAMI ) chini ya
WiLDAF Bibi Thabita Siwale akizungumza kumshukuru Waziri wa Mambo ya
Katiba na sheria Dkt Harrison Mwakyembe walipokutana nae Ofisini kwake
jijini Dar es salaam
Uongozi
wa Kikosi cha Kupambana na Haki za Mirathi (KIKUHAMI ) chini ya
WiLDAF katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Katiba na sheria
Dkt Harrison Mwakyembe na katibi Mkuu Prof Sifuni Mchome walipokutana
nao Wizarani jijini Dar es salam
waziri
wa Mambo ya Katiba na sheria Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza
na Kikosi cha Kupambana na Haki za Mirathi (KIKUHAMI ) chini ya
WiLDAF uliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam
……………………………………………………………………………………………………………
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt
Harrison Mwakyembe amesema Serikali inazisubiri Tume ya Uchaguzi nchini
(NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanziba (ZEC) zimalize majadiliano yao ili
mchakato wa kuipigia kura ya maoni Katiba Inayopendekezwa ufanyike.
Mhe. Mwakyembe ametoa kauli hiyo
jijini Dar es Salaam alipokutana na uongozi wa Kikosi cha Kupambana na
Haki za Mirathi (KIKUHAMI ) kilichoko chini ya Chama cha Wanawake
katika Sheria na Maendeleo Afrika – WiLDAF.
Amesema zoezi hilo lingekuwa
limeshakamilika ila Tume za Uchaguzi ziliona ni bora liahirishwe kwanza
ili kupisha zoezi la Kikatiba lililokuwa likiikabili nchi la Uchaguzi
Mkuu wa mwaka jana likamilike na kwamba kukamilika kwa zoezi hilo
kunatoa fursa kwa Serikali kuendelea na mpango wake wa kuendesha kura ya
maoni juu ya Katiba Inayopendekezwa ili kupata Katiba Mpya ya Tanzania.
Aliongeza kuwa Katiba
Inayopendekezwa ina vitu vingi sana ambavyo vitasaidia upatikanaji wa
haki za wanawake na kuondoa uonevu dhidi yao na hivyo kufanikisha
harakati ambazo wadau mbalimbali wa wanawake nchini wamekuwa
wakizipigania na hivyo kukamilika wakati Katiba mpya itakapokuwa
imepatikana.
Aidha Mhe. Waziri ameutaka
uongozi huo wa KIKUHAMI kupitia WiLDAF kuwasilisha Wizarani mapendekezo
yao juu ya mabadiliko ya sheria mbalimbali za Mirathi nchini wanazoziona
zinawakandamiza wanawake ili ziweze kufanyiwa marekebisho na ziendane
na wakati uliopo.
“si mnataka sheria mbalimbali za
mirathi zibadilishwe?, leteni mapendekezo yenu , hili ni jukumu letu
sote, sisi tupo na hapa wizarani tunao wataalamu watazipitia na kuona
namna ya kuzifanyia kazi, ili ziendane na wakati uliopo sasa, alisema na
kuongeza kuwa ndio maana amesema Katiba Inayopendekezwa ina vipengele
vingi ambavyo vitasaidia kuondoa uonevu kwa wanawake nchini
itakapopitishwa na wananchi kupitia kura ya maoni.”
KIKUHAMI chini ya Uongozi wa Bibi
Thabita Siwale ulimuomba Waziiri wa Katiba na Sheria Dkt Mwakyembe
kuangalia uwezekano wa kuondoa sheria zinazowakandamiza wanawake hasa
zile za mirathi kwani zinawafanya wanawake hasa wajane kunyanyasika
katika nchi yao
RAIS WA SIMBA SPORTS CLUB EVANS AVEVA AZINDUA WIKI YA SIMBA NA SIMBA DAY 2016.
Rais
wa Simba Sport Club Evans Aveva akizungumza na Vyombo vya Habari leo
wakati wa Uzinduzi wa Simba Week Akiwa Sambamba Katibu Mkuu wa Simba
Patrik Kahemela (Kulia) na Afisa Masoko na Mawasiliano Kutoka Eaggroup
Richard Ryaganda( kushoto) .
Simba
inasherehekea wiki maalum iliyo Batizwa Jina la Simba Week
ambayoImezinduliwa Leo na Rais wa Simba Sport Club Ndugu Evans Aveva na
hufikia kilele chake Tarehe 8 Mwezi Agosti. Mwaka huu siku hii ya Simba
week itakuwa na uzito wa kipekee kwani Klabu ya Simba itakuwa inaanza
Sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya klabu Hiyo. Sherehe
za Wiki ya Simba zinaenda sambamba na dhima yetu ya kuendeleza
Mabadiliko chanya ndani ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika
kipindi cha mwaka mzima.
Katika
Kipindi Hiki Simba Sport Club imekuwa na utaratibu wa kuwa na siku
maalum kwaajili ya kufurahi, kuwatambulisha Rasmi wachezaji,Jezi za timu
na kujiandaa kwa Msimu Mpya, siku hii imekuwa Maarufu kama Simba Day.
Tangu Ianzishwe imekua ikiboreka Siku hadi siku, mwaka huu Imeona ni
Muhimu kuiboresha zaidi na hususani kuangalia Mchango wa timu Hiyo kwa
Jamii inayoizunguka.
Simba
iliamua kuanzisha Simba Week ambayo lengo lake kuu ni kuwa wiki ya
Simba Sports Club kufanya kazi za Jamii, kukuza vipaji vya soka vya
vijana, kutembelea Wadau wa Maendeleo na pia Shughuli Nyingine Zenye
Tija kwa Timu..Siku
ya Simba Day, Simba Sports Club itacheza Mechi naInter Clube ya Angola
kwenye Mechi hii Wachezaji Wapya wataonekana Rasmi baada ya Maandalizi.
Nyauhenga ateuliwa kuwa Kaimu Meneja
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Prof. Makame Mbarawa amemteua Bw. Eliud Nyauhenga kuwa Kaimu Meneja wa
Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB).
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri huyo
iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam inaeleza
kuwa, uteuzi huo umefanyika baada ya Meneja wa Bodi hiyo Bw. Joseph
Haule kumaliza mkataba wake.
“Kwa mamlaka niliyonayo chini ya Sheria ya
Bodi ya Mfuko wa Barabara Sura 220 ya mwaka 2006, nimemteua Bw. Eliud
Nyauhenga kuwa Kaimu Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara tangu Julai 27
mwaka huu”, alisema Mbarawa.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa, kabla ya uteuzi huo Bw. Eliud Nyauhenga alikuwa Meneja Msaidizi wa Bodi hiyo.
Aidha, katika taarifa hiyo, Waziri huyo
amempongeza Bw. Joseph Haule kwa kuuongoza Mfuko huo kwa weledi,
uadilifu na mafanikio makubwa tangu ulivyoanzishwa mwaka 2000.
Bodi ya Mfuko wa Barabara ilianzishwa kwa
Sheria Na. 11 ya mwaka 1998 chini ya Sheria ya Ushuru wa
Barabara Na.2 ikiwa na jukumu la kusimamia makusanyo, matumizi na
ufuatiliaji wa Bodi hiyo,
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AKEMEA TAMKO LA CHADEMA
Nimepokea
kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari,
kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini. Tamko hilo limejaa
lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa
amani. Ili kuepuka kurejea tamko lote, nimeona ni vyema nitoe mfano wa
maneno yafuatayo yaliyosemwa, ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya
Siasa:-
“CHADEMA tunasema tunaitangaza
siku ya tarehe 1 Septemba, 2016 kama siku ambayo itakuwa ni siku ya
mikutano nchi nzima ikiwamo maandamano ambapo ngazi zetu mbalimbali za
chama kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa tutafanya mikutano in defiance
ya order ya Rais, ya Jeshi la Polisi kwamba haturuhusiwi kufanya
mikutano ya kisheria”
Kimsingi, Sheria ya Vyama vya
Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2)(c) inakataza chama cha siasa
kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia
malengo yake ya kisiasa.
Aidha, kifungu cha 9(2)(f)
kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia
lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au
ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani. Vile vile kanuni za Maadili ya
Vyama vya Siasa, Tangazo la Serikali namba 215 la mwaka 2017, zinakataza
chama cha siasa kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.
Kanuni ya 5(1)(d) inakitaka kila
chama cha siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo.
Kuhusu mtu yoyote au chama cha siasa chochote.
Kanuni ya 5(1)(f) inasema kuwa, kila chama cha siasa kina wajibu wa kulaani na kupinga yafuatayo:-
(i) Matumizi ya lugha ya matusi;
(ii) Vitendo vya kibabe na vurugu; na
(iii) Matumizi ya nguvu ili kujipatia umaarufu wa chama au sababu yoyote ile.
Hivyo, tamko la CHADEMA ni
ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa. Aidha, hii siyo mara ya kwanza
kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).
Natumia fursa hii kukemea tamko
hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6(2) ya Kanuni za Maadili ya
Vyama vya Siasa. Pia nawaasa CHADEMA wasiendeleze tabia hii.
Mwisho, napenda kusisitiza kuwa,
kwa dhamana niliyopewa kama Msimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa,
napenda kutumia fursa hii kuviasa vyama vyote vya siasa vitimize wajibu
wao kwa weledi kama taasisi za kisiasa.
Ni vema Viongozi wa Vyama vya
Siasa wakaonyesha taswira stahiki ya wanasiasa wakomavu, au Vyama vya
Siasa vya kutolea mfano ndani na nje ya mipaka yetu, kwa kuzingatia
Sheria za Nchi katika kuendesha shughuli za kisiasa.
Vyama vya Siasa viepuke vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha Umma na Serikali yao.
Madhali zipo Sheria na njia
stahiki za kidemokrasia za mawasiliano na Taasisi za Umma, basi navisihi
Vyama vyote vya Siasa kuzingatia utaratibu huo wa mawasiliano kwa
mujibu wa Sheria zilizopo. Aidha, uvumilivu wa kisiasa katika azma za
kudumisha ukuaji wa kidemokrasia nchini haukwepeki.
Tudumishe amani ya nchi yetu.
“MUNGU IBARIKI TANZANIA”
Jaji Francis S.K. Mutungi
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
28 Julai, 2016
MPANGO WA OFISI YA WAZIRI MKUU KUHAMIA DODOMA WIKI IJAYO WAKAMILIKA
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Uratibu, na Watu Wenye Ulemavu) Jenista
Mhagama (Mb)amepokea Mpango Mkakati wa Kuhamia Dodoma wiki ijayo wa
Ofisi ya Waziri Mkuu leo Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Julai,2016
katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo.
Mhagama amekutana na wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi katika kukamilisha Mpango Mkakati huo ili kukamilisha utekelezaji huo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala na Rasilimali akiwasilisha Issa Nchasi akiwaitisha
wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Mpango
wa Ofisi hiyo kuhamia Dodoma wiki ijayo.
Wakuu
wa Idara, Vitengo na Taasisi wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa
Mpango Mkakati wa Kuhamia Dodoma leo Jijini Dar es Salaam tarehe 28
Julai, 2016.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama
na Naibu Waziri anayeshughulikia ( Watu Wenye Ulemavu )Abdallah Possi
pamoja na wakuu wa Idara wakifuatilia uwasilishwaji wa Mpango Mkakati wa
Kuhamia Dodoma wa Ofisi hiyo, leo Jijini Dar es Salaam tarehe 28
Julai, 2016.
Maafisa
wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Mpango
Mkakati wa kuhamia Dodoma katika JIjini Dar es Salaam tarehe 28
Julai,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo.
NAIBU WAZIRI HAMAD MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI NCHINI
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza katika kikao cha Baraza hilo cha kujadili Mkakati wa
Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni
Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto
meza kuu) akimsikiliza Mjumbe wa Kikao hicho, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo
cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dk. Zakaria Mganilwa (kulia)
alipokuwa anachangia mawazo katika Kikao cha kujadili Mkakati wa
Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni
Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza katika kikao cha Baraza hilo cha kujadili Mkakati wa
Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na
wajumbe mbalimbali wa Baraza hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto
meza kuu) akimsikiliza Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga
(kulia meza kuu) alipokuwa akizungumza katika Kikao cha kujadili Mkakati
wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments :
Post a Comment