Thursday, June 2, 2016

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, PROF. JUMANNE MAGHEMBE NA MBOBEZI WA PICHA BW. ROBERT ROSS

mag1 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akikabidhiwa kitabu cha picha za wanyamapori waliopo katika Pori la Akiba la Selous na Mtaalamu wa picha wa  Kimataifa, Bw. Robert Ross wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini  Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo  katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Mhe. Waziri ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu , Injinia Angelina Madete, katika Hoteli ya Slip way. Kitabu hicho kinatarajiwa kutumika  kama nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania katika Nyanja za Kimataifa.
mag3 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akiangalia baadhi ya picha katika kitabu cha picha za wanyamapori  waliopo katika Pori la Akiba la Selous na mara baada ya kukabidhiwa kitabu hicho na  Mtaalamu Kimataifa, Bw. Robert Ross (kushoto)  wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini  Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo  katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo jioni katika Hoteli ambapo Kitabu hicho kitakuwa ni nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania  katika Nyanja za Kimataifa.
mag4 
Huu ni mwonekano wa nje wa kitabu cha Picha  zilizochukuliwa katika Pori la Akiba Selous na Mtaalamu wa picha wa  Kimataifa, Bw. Robert Ross, Kitabu hicho kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Waziri, Prof. Maghembe ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Injinia Angelina Madete  katika hoteli ya Slipway.

Prof Ntalikwa azindua Bodi ya STAMICO Aitaka kuhakikisha STAMICO inaendeshwa kwa faida

sta1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa (mbele) akiongoza kikao cha uzinduzi wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
sta2 
Kaimu Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Ally Samaje akizungumza katika kikao cha uzinduzi wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) uliofanyika jijini Dar es Salaam
sta3 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Prof James Mdoe, akielezea historia ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
sta4 
Baadhi ya wajumbe wa Bodi Mpya ya Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO)  wakifuatilia kwa makini hotuba ya  uzinduzi  wa bodi  hiyo iliyokuwa inatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa.(hayupo pichani).
sta5 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa (mbele kulia) akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)   Balozi Alexander Muganda, (mbele kushoto) mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo  uliofanyika jijini Dar es Salaam.
sta6 
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa (mbele kulia) akimkabidhi vitendea kazi mmoja wa wajumbe wa  Bodi ya  Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO)   Dk. Lightness Mzava, (mbele kushoto) mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo  uliofanyika jijini Dar es Salaam
sta7 
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa ( wa tatu kutoka kushoto waliokaa mbele) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini  Prof James Mdoe ( wa pili kutoka kushoto waliokaa mbele)  wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya  Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO) mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi  huo.
……………………………………………………………………………
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa amezindua bodi  ya wakurugenzi ya  Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO) na kuitaka  bodi hiyo kuhakikisha kuwa shirika hilo linaendeshwa kibiashara na kuchangia katika ukuaji wa sekta ya madini.
Bodi hiyo iliyoteuliwa hivi karibuni na  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo  inaundwa na wajumbe watano ambao ni pamoja na Abdalah  Musa, Dkt. Coretha Komba, Felix  Maagi, Dkt. Lightness Mnzava, John  Seka chini ya Mwenyekiti wake  Balozi  Alexander Muganda.

Uzinduzi wa umezadi dawa za vikope monduli

index 
Na.Catherine Sungura, WAMJW-Monduli
Wilaya ya Monduli inatarajia kutoa kingatiba ya ugonjwa wa trakoma(vikope) wa watu wapatao 140,962 kwa ngazi ya jamii  kaya kwa kaya hadi ifikapo mwezi julai mwaka Huu
Haya yamesemwa leo Na mkuu wa wilaya ya Monduli Fransic Miti wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji dawa katika kijijo cha Losingirani wilayani hapa
Miti alisema kila mtu yupo katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi  kipaumbele”napenda kusisitiza kila mwanajamii ahakikishe kila mtu katika familia anatumia dawa hizi ili tuweze kupunguza kasi ya maambukizi ambayo ni tayari  katika jamii yetu
Aidha aliahidi kulisimamia zoezi hili ipasavyo katika ngazi zote kwani vifaa vyote vya utekelezaji wa zoezi hili vimeshawafikia katika wilaya Nzima
Mkuu wa Wilaya alisema kwa mwaka uliopita wilaya yake imetekeleza zoezi la ugawaji wa  dawa za kudhibiti magonjwa ya kichocho  na minyoo ya tumbo kwa watoto wenye umri wa kwenda shule kwa ufanisi mkubwa ambapo kati ya watoto 29,427,watoto 28,205 walipatiwa kingatiba ambayo ni sawa na asilimia 95.8
Hata hivyo alisema kwa zoezi la mwezi wa tano mwaka huu la umezaji dawa za minyoo zilitolewa kwa watoto 31,150 sawa na asilimia 97.3 kati ya watoto 32,000.
Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa
 Hayapewi kipaumbele toka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Upendo Mwingira alisema maambukizi ya ugonjwa wa vikope(trakoma) upo kwa kiwango cha juu kwenye maeneo ya wafugaji ambapo asilimia 57 ya watu waliofanyiwa utafiti mwaka 2004 hadi 2006 ilionesha wana tatizo la vikope hasa wilaya ya Monduli,Longido pamoja na Ngorongoro.
inakadiliwa hadi kufikia mwaka 2020 dunia nzima iwe imetokomeza ugonjwa huu kwa kugawa dawa ambazo ni tiba na kinga

YALIYOJIRI NDANI NA NJE YA UKUMBI WA BUNGE LEO MJINI DODOMA JUNI 3, 2016.

 Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto), Mhe.
Margaret Sitta Mbunge wa Urambo (katikati) na Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakielekea ndani ya Ukumbi
wa Bunge, Dodoma leo.
 Baadhi
ya Waheshimiwa wabunge wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Baadhi
ya Waheshimiwa wabunge wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson akiendesha
kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
 Mchezaji
wa kulipwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kutoka Tanzania Hasheem
Thabeet (kulia) akiwa na
  baadhi ya
wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge leo.
 Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akichangia jambo
  wakati wa kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania leo.
 Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni akijibu maswali ya
wabunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Dodoma.
 Baadhi
ya Wabunge na Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge
wakati wa kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
 Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia)
akisalimiana na Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa
Bunge leo mjini Dodoma.Katikati ni Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia)
akizungumza jambo na Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga (kushoto) na Mbunge
wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Mchezaji
wa kulipwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kutoka Tanzania Hasheem
Thabeet (kushoto) akifurahia jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju (wa pili kutoka kushoto) na baadhi ya Wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
 Mwenyekiti
wa Kamati ya Haki , Maadili na Madaraka ya Bunge na Mbunge wa Newala Mhe.
George Mkuchika (katikati) akizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe.
Peter Msigwa nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
 Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsisitiza jambo Meneja wa VETA mkoa wa Iringa  Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.
 Kiongozi
wa Kambi ya Upinzania Bungeni Mhe. Freeman Mbowe akifurahia jambo na Mbunge wa
Mtera Mhe. Livingstone Lusinde nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.
 Wabunge
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Venance Mwamoto (wa pili kutoka kulia), ,
Mhe. Livingstone Lusinde (wa tatu kutoka kulia) na Mhe. Joseph Kasheku Msukuma
( pili kutoka kushoto)wakifurahia jambo

na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe nje ya
Ukumbi wa Bunge leo.
 Mbunge
wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (wa pili kutoka kulia), Mbunge wa Mtera Mhe.
Livingstone Lusinde (wa tatu kutoka kulia) na Mbunge wa Geita vijijini Mhe.
Joseph Kasheku Msukuma ( pili kutoka kushoto)wakimweleza jambo Kiongozi wa
Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Kulia) akizungumza jambo na Kiongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni leo mjini Dodoma.
Picha
na Aron Msigwa na Fatma Salum–MAELEZO, DODOMA.

Walioficha sukari ardhi iwakatae

index 
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Askofu wa Kanisa la Good News for All Ministry Dkt. Charles Gadi amewapa siku tatu walioficha sukari kuitoa na ikiwa watakaidi agizo hilo basi ardhi iwakatae.
Askofu Gadi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uhaba wa sukari nchini na  maandalizi ya mkutano wa kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika jiji la Arusha.
“Tanzania haina tatizo la sukari bali sukari ziko kwenye maghala, wafanyabiashara wamezificha ili waje kuuza kwa bei ya juu. Tunamuomba Mungu ili watu hao ardhi iwakatae ikiwa hawatatoa sukari ndani ya siku ya tatu,”alisema Askofu huyo.
Pia, Askofu Gadi ametoa wito kwa wafanyabiashara kuacha tabia ya kuficha sukari na wakumbuke kuwa waislam wapo katika maandalizi ya kutimiza nguzo muhimu ya imani ya dini yao ambapo wataanza  mwezi wa Ramadhani na watahitaji sukari kwa ajili ya kuandaa futari.
Vile vile Askofu huyo ameiomba Serikali kuagiza sukari kwa wingi ili waumini wa dini ya Kiislam waweze kutimiza kwa urahisi nguzo ya mwezi wa Ramadhani.
Aidha, akizungumzia juu ya mkutano wa maombi utakaofanyika jiji la Arusha, Askofu Gadi amesema kuwa mkutano huo ni maalum kwa ajili ya kumuombe Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kufanikiwa katika nia yake ya kujenga upya uchumi, uadilifu na ustawi wa Tanzania.
Mkutano huo unategemewa kufanyika siku ya Jumatano Juni 08, 2016 kuanzia 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni viwanja vya relini, ambao umeandaliwa na Kanisa la Good News for All Ministry kwa kushirikiana na Umoja wa Makanisa ya Arusha.

eGA yataka Taasisi Mbalimbali kutekeleza Miradi ya TEHAMA.

suz01 
Meneja habari, elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao(eGA) Bibi. Suzan Mshakangoto akiongea na waandishi wa habari na wafanyakazi wa taasisi hiyo hawapo pichani  kuhusu ushiriki wa Taasisi za kiserikali katika kupanga na kutekeleza miradi ya TEHAMA Serikalini uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
suz1 
Meneja habari, elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao(eGA) Bibi. Suzan Mshakangoto katikati akiongea na waandishi wa habari na wafanyakazi wa taasisi hiyo kuhusu ushiriki wa Taasisi za kiserikali katika kupanga na kutekeleza miradi ya TEHAMA Serikalini uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Picha zote na Ally Daud-Maelezo
………………………………………………………………………………………….
Na: Frank Shija, MAELEZO
Ofisi naTaasisi za umma zashauriwa kushirikiana naWakala wa Serikali Mtandao (eGA) katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya Tehama.
Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao  (eGA) Bibi. Suzan Mshakangoto wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Bi. Mshakangoto amebainisha kuwa kumekuwapo na changamoto ya Taasisi za umma kuanzisha miradi ya TEHAMA inayofanana huku zikiwa na taarifa zinazokinzana na kuisababishia gharama zisizo za lazima Serikali.
Aidha alisema kuwa ili kujiridhisha na miradi ya TEHAMA Wakala hiyo imeweka vigezo katika Orodha hakiki ya miradi ya TEHAMA Serikalini, inayopatikana katika tovuti ya Wakala ili uweze kuhakikiwa na kuthibitishwa.
“Kutokana na utaratibu huo kuleta changamoto mbalimbali,taasisi yeyote ya umma inatakiwa kuwasilisha mradi wake kwaWakalaya Serikali Mtandao ukiwa unaendana na vigezo vilivyowekwa katika orodha ya miradi ya TEHAMA Serikalini inayopatikana katika tovuti ya wakala ambayo ni www.ega.go.tz” AlisemaBi. Suzan.
Changamoto zinazojitokeza kutokana na utaratibu huo ni pamoja na kutofautiana kwa taarifa ya aina moja kutoka taasisi tofauti akitolea mfano wa Rita wanaweza kuwa na Jina la Juma Hassan na mtu yulelyule ukienda Bima ya Afya anaitwa Juma Kassim Hassan.
Kutokana na mkanganyiko huo na Wakala inashauri na kuzitaka taasisi zote za Serikali kuwasilisha andiko la miradi yao ya Tehama kwa Wakala ya Serikali Mtandao ili kuhakikiwa kama zinakidhi vigezo, malengo na dira ya maendeleo ya Serikali ya mwaka 2025 na kama mradi huo niendelevu.
Aidha wito umetolewa kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na miradi au utengenezaji wa mifumo ya Tehama Serikalini kujiridhisha kama miradi waliyokusudi kuitekeleza inakidhi vigezo vya kuanzisha miradi ya TEHAMA kama vilivyoainishwa katika orodha ya miradi ya Tehama Serikalini.
Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) ni taasisi ya Serikali kwa mamlaka iliyonayo kisheria inawajibika kusimamia na kuratibu masuala yote yanayohusu Serikali Mtandao hivyo ni wajibu wake inapoona mambo yanaenda kinyume na taratibu na miongozo ya usimamizi wa miradi ya Tehama Serikalini.
Na: Frank Shija, MAELEZO
02/06/2016
Ofisi naTaasisi za umma zashauriwa kushirikiana naWakala wa Serikali Mtandao (eGA) katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya Tehama.
Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao  (eGA) Bibi. Suzan Mshakangoto wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Bi. Mshakangoto amebainisha kuwa kumekuwapo na changamoto ya Taasisi za umma kuanzisha miradi ya TEHAMA inayofanana huku zikiwa na taarifa zinazokinzana na kuisababishia gharama zisizo za lazima Serikali.
Aidha alisema kuwa ili kujiridhisha na miradi ya TEHAMA Wakala hiyo imeweka vigezo katika Orodha hakiki ya miradi ya TEHAMA Serikalini, inayopatikana katika tovuti ya Wakala ili uweze kuhakikiwa na kuthibitishwa.
“Kutokana na utaratibu huo kuleta changamoto mbalimbali,taasisi yeyote ya umma inatakiwa kuwasilisha mradi wake kwaWakalaya Serikali Mtandao ukiwa unaendana na vigezo vilivyowekwa katika orodha ya miradi ya TEHAMA Serikalini inayopatikana katika tovuti ya wakala ambayo ni www.ega.go.tz” AlisemaBi. Suzan.
Changamoto zinazojitokeza kutokana na utaratibu huo ni pamoja na kutofautiana kwa taarifa ya aina moja kutoka taasisi tofauti akitolea mfano wa Rita wanaweza kuwa na Jina la Juma Hassan na mtu yulelyule ukienda Bima ya Afya anaitwa Juma Kassim Hassan.
Kutokana na mkanganyiko huo na Wakala inashauri na kuzitaka taasisi zote za Serikali kuwasilisha andiko la miradi yao ya Tehama kwa Wakala ya Serikali Mtandao ili kuhakikiwa kama zinakidhi vigezo, malengo na dira ya maendeleo ya Serikali ya mwaka 2025 na kama mradi huo niendelevu.
Aidha wito umetolewa kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na miradi au utengenezaji wa mifumo ya Tehama Serikalini kujiridhisha kama miradi waliyokusudi kuitekeleza inakidhi vigezo vya kuanzisha miradi ya TEHAMA kama vilivyoainishwa katika orodha ya miradi ya Tehama Serikalini.
Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) ni taasisi ya Serikali kwa mamlaka iliyonayo kisheria inawajibika kusimamia na kuratibu masuala yote yanayohusu Serikali Mtandao hivyo ni wajibu wake inapoona mambo yanaenda kinyume na taratibu na miongozo ya usimamizi wa miradi ya Tehama Serikalini.

UNESCO YATAJA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI MAENEO YENYE URITHI AFRIKA

LIW5 
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni limetaja baadhi ya changamoto zinazoyakabili maeneo yenye Urithi wa dunia barani Afrika hivi sasa
Akizungumza  katika Mkutano wa Siku nne  unaofanyika Arusha, Tanzania Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa  cha Urithi wa dunia kutoka Makao Makuu ya UNESCO Dkt  Mechtild Rossier amesema maeneo hayo mengi barani afrika  yanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na shughuli mbalimbali zikiwemo za binadamu
Dkt Rossier amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa  ni mabadiliko ya tabia nchi ambapo 16 kati ya 48 yenye  urithi wa dunia  yaliyopo barani afrika  hususani kusini mwa jangwa na sahara  yapo hatarini kutoweka .
Changamoto nyingine ni kuwepo na migogoro ya vita katika baadhi ya nchi katika bara la afrika, vitendo vya ugaidi, uwindaji haramu, kupanuka kwa  ujenzi wa makazi na kusikosimamiwa vizuri
Pia kutokuwepo na kukosekana kwa mipango mizuri na ujenzi holela wa makazi pamoja na uchimbaji w amadini na  mafuta katika maeneo yenye urithi wa dunia.
Amyataka mataifa ya bara la afrika kuhakikisha  kwamba yanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi wake  juu ya umuhimu wa maeneo hayo kwa faida ya vizazi vijaavyo na dunia
Maeneo hayo ni pamoja na  hifadhi ya Taifa ya Serengeti,,Bonde  la hifadhi ya Ngorongoro,Pori la akiba  la Selous,Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro,,Mji Mkongwe wa Zanzibar,,Magofu ya Kilwa kisiwani,na Songo Mnara pamoja na  Michoro ya  Miambani  iliyopo Kondoa Mkoani Dodoma 

Maeneo ya urithi wa dunia yakabiliwa na changamoto

???????????????????????????????????? 
Mahmoud Ahmad Arusha 
 MKOA wa Arusha, utaadhimisha siku ya mazingira duniani June 5 kwa kupanda miti aina mbalimbali ya matunda ,vivuli na ya asili kwenye shule za msingi na vyanzo vya maji ili kutunza na kuhifadhi mazingira.
Katibu tawala mkoa wa Arusha,Richard Kwitega, amesema kwenye maadhimisho hayo ambayo kilele chake kitakuwa ni Juni 5 mwaka huu mkoa utapanda miti kwenye maeneo yote ya mkoa huo lengo ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Amesema shirika la umoja wa mataifa la mazingira UNEP, limepanga juni 5 kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya mazingira duniani,ili watu wajue umuhimu wa kutunza na kusimamia mazingira yao.
Kwitega,alisema mwaka huu 2016 maadhimisho ya mazingira kimataifa yanaadhimishwa nchini Angola,yakiwa na kauli mbiu isemayo uvumilivu  ufike mwisho juu ya biashara haramu ya wanyama pori ambayo hupelekea wanyama pori kutoweka kwenye IKolojia.
Alisema kwa kuanza mkoa utapanda miti ya matunda kwenye shule tano za msingi za jijini Arusha, ambazo ni Makumbushi, Arusha school, Naura, Meru na Levolosi,na kwenye chanzo cha maji cha Kiranyi, kutapandwa miti ya asili  ambayo ni rafiki wa mazingira ili kutunza chanzo hicho.
Alisema maadhimisho hay mwaka huu hayataadhimishwa kitaifa bali kila mkoa kila mkoa umepewa jukumu la kuadimisha maadhimisho hayo ambayo kli mbiu yake  ya taifa inasema tuhifadhi vyanzo  vya maji  kwa uhai wa taifa  letu .
Kwitega, alisema  katika maadhimisho hayo wananchi na wadau watafanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo soko la Kilombero, na kwenye makazi kuanzia ngazi ya kaya ,kitongoji,kijiji,mtaa na kata ,na akatoa wito kwa kila mwananch na taasisi mbalimbali kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao.
Alisema siku ya kilele ya maadhimisho hayo ya mazingira duniani,mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,(KIJIKO)ataongoza wananchi kupanda mti wa kumbukumbu kwenye bustani ya Peace Park, iliyopo mzunguko wa Impala hotel jijini hapa .
Jun 1 at 2:32 PM

MAKAMO MWENYEKITI WA CCM AZUNGUMZA NA VIONGOZI WILAYA YA DIMANI MKOA WA MJINI MAGHARIBI UNGUJA

SHE1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa CCM Mkoa Amani leo katika mkutano wa Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya ya Dimani CCM kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 2/06/2016.
SHE2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Dimani leo wakati alipowasilli katika viwanja vya CCM Mkoa Amani wakati alipohudhuria katika mkutano wa Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya ya Dimani CCM uliofanyika leo  kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 2/06/2016.
SHE3Wanachama Viongozi wa Wilaya ya Dimani CCM wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza katika mkutano wa  Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya ya Dimani CCM uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,  kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 2/06/2016.
SHE4Wanachama Viongozi wa Wilaya ya Dimani CCM wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza katika mkutano wa  Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya ya Dimani CCM uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani, kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 2/06/2016.
SHE5Wanachama Viongozi wa Wilaya ya Dimani CCM wakinyoosha mikono juu kuunga mkono hotuba ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza katika mkutano wa  Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya hiyo uliofanyika leo  katika ukumbi CCM Mkoa Amani,kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 2/06/2016.
SHE6 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi wa CCM wakiwemo Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya ya Dimani CCM uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani, kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,[Picha na Ikulu.] 2/06/2016.
SHE7 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi wa CCM wakiwemo Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu na Maskani za CCM wa Wilaya ya Dimani CCM uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani, kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza  kwa ushindi uliopatikana katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi machi mwaka huu,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,[Picha na Ikulu.] 2/06/2016.

KWILAYA YA ILALA YAJIPANGA KUSAMBAZA MAENEO YOTE MAKASHA YA KUHIFADHIA TAKA

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya mazingira duniani ambapo manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd na nyingine kwa kufanya usafi katika fukwe za bahari ya Salender jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea-View Upanga, Victor Muneni na kulia ni Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda.
 
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea-View Upanga, Victor Muneni akizungumza jambo na wadau wa mazingira waliokusanyika kwenye viwanja vya Salender Club kabla ya kuanza zoezi la usafi wa mazingira.
Baadhi ya wadau wa mazingira kutoka ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, makapuni ya usafi yaliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala ikiwemo Green Waste Pro Ltd, Vijana kutoka Roots and Shoot waliokusanyika kwenye uzinduzi wa wiki ya mazingira duniani iliyozinduliwa jana duniani kote.
Kiongozi wa dhehebu la Dawoodi Bohra nchini, Bw. Zainuddin Adamjee (wa pili kushoto) akimtambulisha Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin (wa tatu kushoto) kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia) mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (kushoto) akitoa salamu za serikali kwa Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Bohora duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin aliyewasili jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akielezea mipango ya manispaa ya Ilala katika kuweka jiji safi wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa ‘Dustbin’ 53 zilizotolewa na Burhani Foundation Tanzania iliyofanyika katika mskiti wa dhehebu la Mabohra nchini.
Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin moja ya Dustbin kati ya 53 zilizotolewa na Burhan Foundation kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Kiongozi huyo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akimshukuru Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin kwa zawadi ya kikoi.
Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda akipokea zawadi ya kikoi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin.

.NSSF yashauriwa kusaidia wasanii.

index 
Meneja  wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso.
……………………………………………………………………………………………………………
Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii( NSSF) Mkoa wa Ruvuma  limeshauriwa kuinua maisha ya wasanii kwa kuwaunganisha na mfuko huo ili kuhakikisha maisha ya wasanii yanaboreshwa.
Akizungumza katika kikao kati ya wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara, Katibu Mkuu wa Wizara Wizara hiyo Prof  Elisante Ole Gabriel  amesema kuwa mfuko huo uangalie  namna ya kukusanya wasanii na kuwaweka pamoja ili waweze kujiunga.
“kwa upande wa wasanii wao ni jeshi kubwa tutafute namana ya kuwasajili kama wanachama rasmi wa NSSF ili waweza kutambulika katika ajira rasmi” alisema Prof Gabriel.
Prof Gabriel alisema kuwa  wasanii wanachangamoto nyingi zinazo wakabili ambazo zinarudisha nyuma kada yao moja wapo ikiwa ni hiyo ya kutokuwa wanachama wa mifuko ya Jamii.
Kwa upande wake Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso amesema lengo la mfuko huo ni kudumisha maisha ya watanzania walio katika sekta zote hivyo basi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa wanaangalia namna ya kuwainua  wasanii hao kupitia mikopo itolewayo na mfuko huo.
Ameongeza kuwa shirika lake limejipanga kikamilifu kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya tano hivyo basi elimu ya kujiunga na mfuko huo itaendelea kutolewa kwa wananchi .
“Wasanii wanaweza kuitangaza nchi yetu vizuri sana  kama tu jamii itaamua kuwatambua na sanaa ikawa ni ajira kamili kama ajira nyingine.”Alisema Bw. Wisso
Aidha aliwasisitiza viongozi wa wasanii pamoja na Maafisa Utamaduni kuwahamasisha wadau wao kuingia katika mfuko huo wa jamii kwani ni dhamana ya maisha yao.

MAJALIWA ATETA NA KAMISHINA WA TRA

KID1 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KID2

MUHIMBILI YAPOKEA VIFAA VYA KUTOA HUDUMA KWA WATOTO WADOGO

zaw1 
Kushoto ni Mkuu wa Uuguzi na Mazingira ya Ndani, Zuhura Mawona wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akipokea LEO vifaa vya kutoa huduma kwa watoto wadogo kutoka  kwa Mratibu wa Global Health Alliance, Sally Dawit.
zaw2 
Vifaa vya kutoa huduma kwa watoto wadogo vikiwa kwenye toroli maalumu la kuhifadhia katika hospitali hiyo.
zaw3 
Kushoto ni Mkuu wa Uuguzi na Mazingira ya Ndani, Zuhura Mawona wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akipokea LEO vifaa vya kutoa huduma kwa watoto wadogo kutoka  kwa Mratibu wa Global Health Alliance, Sally Dawit.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Tutangaze vivutio vya kiutamaduni: Prof. Elisante Ole Gabriel

eli1 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma  Bw  Hassan Bendeyeko  akifungua kikao  kati ya wadau wa Sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara husika kilichofanyika Mjini Songea Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na  kulia ni Afisa Elimu MkoaBw.Gharama Kinderu
eli2 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo akisikiliza maelezo ya baadhi ya vifaa vilivyotumika katika vita ya Majimaji kutoka kwa Afisa Elimu Makumbusho ya Taifa  Bi. Blantina Raphael wakati alipotembelea makumbusho hayo mjini Songea, katikati ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma  Bw.Gharama Kinderu. picha na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
………………………………………………………………………………..
Na Zawadi Msalla- Ruvuma
Serikali imetoa wito kwa viongozi na wadau wa sekta ya Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma kutangaza Utamaduni na Utalii unaopatikana katika mkoa huo.
Wito huo umetolewa jana mjini Songea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
“Mkoa wenu una vivutio vingi vya asili vinavyoonesha tamaduni za wanaruvuma  ambavyo vikitumika vizuri ni fursa nzuri ya mapato” alisema Prof Gabriel.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma una vivutio vingi vya Utamaduni  vya kuvutia watalii ambavyo ni fursa nzuri ya kutangaza Utamaduni wa Mkoa na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Bendeyeko alikiri kuwepo kwa changamoto ya kuvitangaza vivutio hivyo kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo .
Hata hivyo  alisema kuwa ujenzi wa miundombinu utasaidia vivutio hivyo kufikika kwa urahisi na wanategemea Mkoa huo kuinuka kiuchumi hasa baada ya changamoto hiyo kutatuliwa.
Bw.Bendeyeko alisema kuwa baadhi ya vivutio vya kiutamaduni vinavyo hitaji kutangazwa ili vifahamike ndani na nje ya nchi ni pamoja na Makumbusho ya Majimaji, eneo waliponyongwa wapiganaji wa vita vya majimaji, Ziwa Nyasa pamoja na mbuga mbali mbali.
Aidha alieleza kuwa wanatarajia kuajiri Maafisa Utamaduni wakutosha  katika kila Halmashauri ambapo  kwa kushirikiana na Maafisa Habari na waandishi wa habari kutangaza vivutio hivyo.Na Zawadi Msalla- Ruvuma
Serikali imetoa wito kwa viongozi na wadau wa sekta ya Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma kutangaza Utamaduni na Utalii unaopatikana katika mkoa huo.
Wito huo umetolewa jana mjini Songea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
“Mkoa wenu una vivutio vingi vya asili vinavyoonesha tamaduni za wanaruvuma  ambavyo vikitumika vizuri ni fursa nzuri ya mapato” alisema Prof Gabriel.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma una vivutio vingi vya Utamaduni  vya kuvutia watalii ambavyo ni fursa nzuri ya kutangaza Utamaduni wa Mkoa na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Bendeyeko alikiri kuwepo kwa changamoto ya kuvitangaza vivutio hivyo kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo .
Hata hivyo  alisema kuwa ujenzi wa miundombinu utasaidia vivutio hivyo kufikika kwa urahisi na wanategemea Mkoa huo kuinuka kiuchumi hasa baada ya changamoto hiyo kutatuliwa.
Bw.Bendeyeko alisema kuwa baadhi ya vivutio vya kiutamaduni vinavyo hitaji kutangazwa ili vifahamike ndani na nje ya nchi ni pamoja na Makumbusho ya Majimaji, eneo waliponyongwa wapiganaji wa vita vya majimaji, Ziwa Nyasa pamoja na mbuga mbali mbali.
Aidha alieleza kuwa wanatarajia kuajiri Maafisa Utamaduni wakutosha  katika kila Halmashauri ambapo  kwa kushirikiana na Maafisa Habari na waandishi wa habari kutangaza vivutio hivyo.

HALMASHAURI ZA BUTIAMA NA RORYA KUTEKELEZA MRADI WA PS3 AWAMU YA KWANZA MKOANI WA MARA

 
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Felix Lyniva wakifuatilia mada katika mafunzoa ambapo Halmashauri za Wilaya zao za Butiama na Rorya mkoani Mara ndio zimechaguliwa kuwa za kwanza kuanza utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za umma(PS3) katika sekta za afya, elimu na kilimo.
***************
HALAMSAHAURI Za Wilaya ya Rorya na Butiama
mkoani Mara zimechaguliwa kuwa za kuanza utekelezaji wa mradi Uimarishaji
Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maemdeleo la
Kimataifa la Marekani (USAID).
Tayari watendaji kutoka halamshauri
husika wanapatiwa mafunzo ya siku moja leo na wiki ijayo madiwani wao nao
watapatiwa mafunzo maalum ya namna ya kushiriki utekelezaji wa mradi huo. Mafunzo
hayo ya wiki moja yatafanyika mjini Bunda. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Benki ya Barclays yatoa msaada wa madawati Handeni

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kushoto) akipokea sehemu ya madawati 70  kutoka kwa  Meneja Masoko  wa Benki ya B arclays Tanzania  (BBT) Nasikiwa Berya  yaliyotolewa ba benki hiyo kusaidia  Shule ya Sekondari Handeni kupitia timu yake ya soka iliyopewa jina la ‘Blue Eagle’ ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika wilayani Handeni mkoani Tanga hivi karibuni.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kushoto), akikabidhi madawati hay kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Handeni wilayani humo hivi karibuni. 
 Meneja Masoko  wa Benki ya B arclays Tanzania  (BBT) Nasikiwa Berya (watatu kushoto), akikabidhi sehemu ya  msaada wa madawati 70 kwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari handeni, Amani Mmbaga, yaliyotolewa na benki kupitia timu yake ya soka iliyopewa jina la ‘Blue Eagle’ ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika wilayani Handeni mkoani Tanga .  
 Mmoja wa maofisa wa Benki ya Barclays Tanzania, Raymond Bunyinyiga (kushoto), akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo.  
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Barclays wakibeba madawati tayari kuyakabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Tanga kusaidia shule za sekondari wilayani Handeni.
Mchezaji wa timu ya soka ya Benki ya Barclays iitwayo ‘Blue Eagle’ Edwin Makata, akichuana na Issa Silaji (kulia) wa timu ya soka ya Shule ya Sekondari Handeni, katika mchezo wa kirafiki mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati 70 yaliyotolewa na timu hiyo.

Mama Janeth Magufuli alipowasili mikoa ya Lindi na Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.

LIN1 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akimkaribisha Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani huko kwa ajili ya Ziara ya kikazi katika mikoa ya kusini.
LIN2 
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi na Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
LIN4 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na kinamama waliojitokea kumpokea alipowasili Mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.
LIN5 
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akimshukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kwa kuamua kufanya ziara ya kikazi mkoani humo.
LIN6 
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiongea kwa niaba ya kina mama waliojitokeza kumpokea Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli ambapo alimuahidi kuendelea kumuunga mkono kwenye shughuli zake na kumtaka kwenda mkoni humo mara kwa mara kwa ajili ya ziara za kikazi.Katikati mwenye pochi ya bluu ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
LIN8 
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Ungo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi. Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
LIN9 
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Kitenge Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.
LIN10 
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Kitenge Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa.
LIN11 
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiwakabidhi zawadi ya mbuzi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kushoto) na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa (katikati).
LIN12 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwashukuru kinamama na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea alipofika mkoani Lindi.
LIN13 
Mtoto Lulu Charles akimpa shada la maua Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipowasili Mkoani Mtwara.
LIN14 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali waliofika kumpokea alipowasili Masasi Mkoani Mtwara.
LIN15 
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akimueleza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli utekelezaji wa mambo mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wake.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

NAIBU WAZIRI JAFO AZINDUA MADARASA SHULE YA MSINGI NZUGUNI B. DODOMA

jaf2 
Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu wa Waziri Vijana na AJIRA Anthony Mavunde akitoa neno la shukrani wakati wa uzinduzi huo
jaf3 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jasmine Tiisekwa akitoa taarifa ya mradi huo wakati wa uzinduzi wa madarasa.
jaf4 
Picha ya Pamoja na walimu wa shule ya msingi Nzuguni B pamoja watendaji wengine
jaf5 
Jengo la madarasa yaliyozinduliwa linavyoonekamana mara baada ya uzinduzi huo.
PICHA ZOTE NA RAMADHANI JUMA

Copa America,Je nani ataendeleza ubabe? Usikose hii ni ndani ya STARRIMES PEKEE!!

index

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MWANZA

index
KWAMBA TAREHE 01.06.2016 MAJIRA YA SAA 12:30HRS KATIKA MAENEO YA KABANGAJA – MNARANI KATA YA BUGOGWA WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA ASKARI WALIOKUWA DORIA PAMOJA NA MISAKO YA WAHALIFU NA UHALIFU WALIMKAMATA LETICIA ELIAS MIAKA 52 MKAZI WA IGOMBE AKIWA NA MISOKOTO 12 YA BHANGI PAMOJA NA MWENZAKE AITWAYE THOMAS LIPOVITIA MIAKA 49 MKAZI WA KIBAGAJA AKIWA NA KILO 02 ZA BHANGI KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA BAADA YA ASKARI KUWAKAMATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU WALIENDELEA NA MSAKO WA KUSAKA WAHALIFU WENGINE NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MAJANI MANYEGO MIAKA 38 AKIWA NA POMBE AINA YA GONGO LITA 10 KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI. WATUHUMIWA WOTE WATATU WAMEKAMATWA WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA AMBAYO YANAHARIBU NGUVU KAZI YA TAIFA LETU, HIVYO JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LITAWASAKA KILA SEHEMU WAHALIFU WA AINA KAMA HIYO NA KUHAKIKISHA WANAKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMESAINIWA NA
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

MASAUNI AONGOZA VIONGOZI WA SERIKALI KUHANI MSIBA WALIOCHINJWA KITONGOJI CHA KIBATINI MKOANI TANGA


kib1 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimpa pole Hussein Mkola ambaye ni mtoto wa marehemu Mkola Hussein ambaye alichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia nane zilizofiwa katika kitongoji hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
kib3 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo wakati alipokuwa anawasili msibani katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga, ambapo watu wanane walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia hizo zilizofiwa katika kitongoji hicho. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
kib4 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwapa pole wanafamilia ya marehemu Mkola Hussein ambaye alichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia nane zilizofiwa katika kitongoji hicho. Nyuma ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
kib5 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo akiwaonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wapili kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu (watatu kushoto), nyumba ya kwanza katika Kitongoji cha Kibatini walioivamia watu wanaohofiwa kuwa majambazi na kufanya mauaji. Naibu Waziri na Viongozi hao walienda kutoa pole katika familia zilizofiwa katika Kitongoji hicho kilichopo katika Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
kib6 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa salamu za pole kwa ndugu wa marehemu Mkola Hussein pamoja na wananchi wa Kitongoji cha Kibatini kulipotokea mauaji kwa watu wanane ambao walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji hicho kilichopo Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Katika hotuba yake Masauni alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo na itahakikisha inawakamata wauaji wote waliofanya ukatili huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
kib7 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange kabla ya kwenda kutoa pole kwa familia ya wafiwa katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga ambapo watu wanane walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MGODI WA BUZWAGI WAKABIDHI HUNDI YA MILIONI 588 KWA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA

 
Mkuu wa Wilaya Kahama, Vita Kawawa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kahama wakikabidhi mfano wa Hundi ya Sh Milioni 5888,842,728  kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba,fedha zilizotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kama ushuru wa Hudma (Service Levy)  kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya kisasa .wengine pichani ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo (kushoto) akishuhudia tukio hilo.
 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa akiwahutubia baadhi ya wananchi
(hawapo picha) na viongozi wakati wa hafla hiyo ya kupokea hundi
kutoka kwa Mgodi wa Buzwagi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya
mji wa Kahama Anderson Msumba
akitoa neo la shukrani mara baada ya kukabidhiwa hundi.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Vita Kawawa akiteta jambo na Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Mhandisi
Asa Mwaipopo
wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi hiyo.
 

Kahama: Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi umeikabidhi halmashauri ya mji wa Kahama
hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni miatano themanini na nane ikiwa
ni sehemu ya kodi ya huduma (service levy) katika kipindi cha kuanzia
Julai – desemba 2015.
Akikabidhi hundi hiyo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama, katika hafla fupi iliyofanyika
katika uwanja wa taifa Kahama, Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi
Mhandisi Asa Mwaipopo amesema Kampuni yake imekuwa ikizingatia sheria
kwa kulipa kodi mbalimbali ambazo zimewekwa kwa mujibu wa sheria.
“Toka kuanza kwa shughuli zetu za uchimbaji mwaka 2009 mpaka 2015 mgodi wa
Buzwagi pekee umelipa kodi mbalimbali ambazo zinafikia kiasi cha
shilingi za kitanzania bilioni 197 kiasi hiki kinahusisha kodi na tozo
mbalimbali kama vile kodi ya huduma (service levy), Pay as you earn
(PAYE), kodi ya zuio (withholding tax), na kodi ya mrabaha”.alisema Mwaipopo.
  “Katika kodi hizi, kodi ya huduma (service levy) imekuwa ikilipwa
moja kwa moja kwa halmashauri ya mji wa Kahama ambapo mpaka mwisho wa
mwaka jana zaidi ya shilingi bilioni 3.4 sawa na asilimia mbili ya kodi
zote zimelipwa kwa halmashauri ya Kahama pekee.”aliongeza Mwaipopo.
Mwaipopo amesema licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali bado
imekuwa ikijishughulisha katika kuhakikisha inakuwa mdau muhimu wa
maendeleomkwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo
yanayozunguka Mgodi.
“Mheshimiwa mkuu wa wilaya katika kipindi cha mwaka 2015 pekee takribani shilingi
bilioni moja nukta saba 1.7 zimetumika katika kutekeleza miradi
ya elimu, afya na maji na miradi yote hii ilelenga katika kuinua uchumi
wa wilaya pamoja na kuboresha ustawi wa maisha ya wenyeji.”alisema Mwaipopo.
“Acacia kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa mdau muhimu wa maendeleo
kwa halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na
tunafarijika sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata.”
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa aliyepokea hundi
hiyo kutoka kwa uongozi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti
wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa
jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana
na jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali, huku akiwataka viongozi wa
halmashauri ya mji wa Kahama kuhakikisha pesa
hizo zinatumika kutekeleza miradi itakayokuwa na manufaa ya moja kwa
moja kwa Jamii.
“Ombi langu kwa wataalamu wa halmashauri na madiwani ambao ndio wasimamizi wa
pesa hizi kuhakikisha kuwa zinatumika kama zilivyokusudiwa na kwa
sababu safari hii tumeamua zijenge hospitali basi hakikisheni tunapata majengo
ya kisasa pamoja na vifaa tiba kwa manufaa ya watu wa Kahama”alisema Kawawa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija
amesema wao kama madiwani watahakikisha kwamba pesa hizo zinatumika
katika utekelezaji
wa miradi iliyokusudiwa.
“Ndugu zetu hawa wa Mgodi wamekuwa wakilipa kodi hizi lakini wananchi wamekuwa
hawaoni kinachofanyika hali ambayo imepelekea minung’uniko miongoni
mwa wananchi, Kwa kuamua kuzitumia fedha katika ujenzi wa Hospitali ya
wilaya kila mtu ataona kinachofanyika na itasaidia kuondoa
minunung’uniko ambayo imekuwa ikijitokeza kutoka kwa wananchi”
Hafla hiyo pia ilisindikizwa na burudani ya mpambano mkali wa mpira wa miguu
baina ya timu za Mgodi wa Buzwagi na timu ya hospitali ya
wilaya mchezo ambao uliisha kwa timu ya hospitali ya wilaya kuibuka
mshindi kwa kuifunga timu ya Buzwagi 2-1.
 

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JUMUIYA YA WATANZANIA HOUSTON (THC)

Afisa Bismas Asenga mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania hapa Marekani akiongea mbele ya watu waliojitokeza ndani ya kanisa kwa ajili ya Ibada ya misa na kuaga mwili wa Andrew Nicky Sanga. Afisa Bismas ndiye aliyemwakiliza Balozi Wilson Masilingi.
……………………………………………………………………………….
Uongozi wa Tanzania Houston Community (THC) unapenda kukanusha taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa mitandaoni ya kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Mh. Balozi Wilson Masilingi haukufanya lolote wakati Jumuiya yetu ilipopatwa na misiba miwili ya Bw.Henry Kiherile na Bw.Andrew Nicky Sanga iliyotokea kwa nyakati tofauti mapema mwezi April mwaka huu.
Uongozi wa THC unapenda umma utambue kwamba tulipata na tunathamini sana ushirikiano ulioonyeshwa na kutolewa na Ubalozi pamoja na Balozi mwenyewe Mh. Masilingi wakati wa misiba hiyo miwili na hata baada ya shughuli hizo za misiba kumalizika.
Baadhi ya mambo yaliyofanywa na Balozi ni kuwatafuta viongozi wa JumuiyaTHC na kuzungumza nao mapema baada ya misiba hiyo kutokea (Balozi alitutafuta viongozi na si vinginevyo) ambapo alizungumza na Rais wa Jumuiya Bw.Daudi Mayocha kwa simu na Katibu Mkuu wa Jumuiya Bw.Michael Ndejembi na kuwapa pole kwa niaba ya familia na Jumuiya nzima.
Uongozi unafahamu kwamba sababu za balozi kushindwa kufika Houston wakati wa misiba hiyo ni yeye kumuwakilisha Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli kwenye kongamano la DICOTA lililokuwa likifanyika jijini Dallas, Texas. Tunatambua pia kwamba nia ya Balozi kuja Houston bado iko pale pale.
Aidha Balozi Masilingi alimtuma afisa Ubalozi Bismas Asenga kumuwakilisha katika shughuli za Misa na Kuaga mwili wa marehemu Andrew Nicky Sanga, ambapo afisa huyo pamoja na mambo mengine alitoa salamu za rambirambi toka kwa Balozi na alikabidhi rambirambi ya $500 kwa kila familia pamoja na kuzungumza na wafiwa hao kwa nyakati tofauti.
Kwa taratibu za kiupelelezi Uongozi wa THC hauwezi kutoa taarifa zaidi ya namna suala hili linavyoshughulikiwa kati ya vyombo vya usalama nikimaanisha HPD Homicide Department na Ubalozi wa Tanzania lakini tunatambua kwamba Ubalozi unafuatilia kesi zote mbili kwa ukaribu sana.
Uongozi wa THC unasisitiza kuwa hauhusiki kwa aina yoyote na Waraka (Petition)unaosambazwa kwenye mitandao.
kumchafua Balozi Masilingi na Ubalozi wetu wa Washington D.C kwa ujumla.
Daudi Mayocha,
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Houston (THC)

Wajumbe wapya wa bodi ya NHIF wateuliwa

index 
KufuatiakuteuliwakwaBi. Anne S. MakindakuwaMwenyekitiwaBodiyaMfukowaTaifawaBimayaAfya (NHIF),Waziri waAfya, MaendeleoyaJamii, Jinsia, WazeenaWatotoMhe. Ummy A. Mwalimu (Mb), pia ameteuawafuataokuwaWajumbewaBodiyaMfukowaTaifawaBimayaAfya (NHIF).
1. 2.
3.
4.
5.
6.
7.
Dkt. DorothGwajima Ndugu Lydia Choma
NduguYahayaMsulwa
Dkt. Kaushik Ramaiya
NduguJaffer Machano
NduguTryphon D. Rutazamba
Dkt. Bughayo Abdallah Saqware
Uteuzihuunikuanziatarehe 01/6/2016 haditarehe 31/5/2019.
Imetolewana:
Dkt. UlisubisyaMpoki
KATIBU MKUU
01 Juni, 2016

Mkoa wa Arusha kuazimisha siku ya mazingira kwa upandaji miti june 5

images 
MKOA wa Arusha, utaadhimisha siku ya mazingira duniani June 5 kwa kupanda miti aina mbalimbali ya matunda ,vivuli na ya asili kwenye shule za msingi na vyanzo vya maji ili kutunza na kuhifadhi mazingira.
Katibu tawala mkoa wa Arusha,Richard Kwitega, amesema kwenye maadhimisho hayo ambayo kilele chake kitakuwa ni Juni 5 mwaka huu mkoa utapanda miti kwenye maeneo yote ya mkoa huo lengo ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutekeleza jukumu la  shirika la mazingira duniani, UNEP.
Amesema shirika la umoja wa mataifa la mazingira UNEP, limepanga juni 5 kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya mazingira duniani,ili watu wajue umuhimu wa kutunza na kusimamia mazingira yao.
Alisema kila nchi mwanachama ikiwemo Tanzania, inayo sauti katika kikao cha baraza la mazingira duniani  juu ya mazingira endelevu .
Kwitega,alisema mwaka huu 2016 maadhimisho ya mazingira kimataifa yanaadhimishwa nchini Angola,yakiwa na kauli mbiu isemayo uvumilivu  ufike mwisho juu ya biashara haramu ya wanyama pori ambayo hupelekea wanyama pori kutoweka kwenye IKolojia.
Alisema kaulimbiu hiyo inatutaka kuacha kuwauwa wanyamapori  kwa lengo la kuuza viungo vyao  na kuharibu mazingira .
Kwitega,amesema katika kutekeleza jukumu hilo mkoa huo, unashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwemo halmashauri na asasi binafsi kuadhimisha siku hiyo ya mzngira duniani kwa kupanda miti maeneo mbalimbali.
Alisema kwa kuanza mkoa utapanda miti ya matunda kwenye shule tano za msingi za jijini Arusha, ambazo ni Makumbushi, Arusha school, Naura, Meru na Levolosi,na kwenye chanzo cha maji cha Kiranyi, kutapandwa miti ya asili  ambayo ni rafiki wa mazingira ili kutunza chanzo hicho.
Alisema maadhimisho hay mwaka huu hayataadhimishwa kitaifa bali kila mkoa kila mkoa umepewa jukumu la kuadimisha maadhimisho hayo kwa kushirikiana na halmashauri zake na wadau wake wa maendeleo.
Alisema kauli mbiu ya taifa mwaka huu inasema tuhifadhi vyanzo  vya maji  kwa uhai wa taifa  letu  na mkoa utaendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa jamii kuanzia juni 2 hadi siku ya kilele juni 5
Kwitega, alisema  katika maadhimisho hayo wananchi na wadau watafanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo soko la Kilombero, na kwenye makazi kuanzia ngazi ya kaya ,kitongoji,kijiji,mtaa na kata ,na akatoa wito kwa kila mwananch na taasisi mbalimbali kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao.
Alisema kuwa siku ya kilele ya maadhimisho hayo ya mazingira duniani,mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,(KIJIKO)ataongoza wananchi kupanda mti wa kumbukumbu kwenye bustani ya Peace Park, iliyopo mzunguko wa Impala hotel jijini hapa .

ULIMWENGU ATUA, KILIMANJARO KUTEMBELEA STARS

Mbwana Samatta akitarajiwa kuwasili usiku wa Juni 1, 2016 kutoka Genk Ubelgiji, tayari Thomas Ulimwengu kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amejiunga na kambi ya timu ya soka ya Tanzania- Taifa Stars.
Na katika hatua nyingine, Uongozi wa Bia ya Kilimanjaro inayozalishwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), unatarajia kutembelea timu ya Taifa Stars kesho Alhamisi Juni 2, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo kabla ya kuivaa Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Maataifa ya Afrika (AFCON).
Mchezo huo utasimamiwa na Waamuzi wanne kutoka Gabon, ambao ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric. Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) na Misri imetua alfajiri ya leo Juni 1, 2016 na imeweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.
Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei 30,2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1. 

UCHAGUZI YANGA UNASIMAMIWA NA TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwafahgamisha wanachama wa Young Africans na familia ya mpira kwa ujumla kuwa mchakato wa uchaguzi wa Klabu ya Young Africans unaendelea vizuri na unasimaiwa na Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho kwa mujibu wa utaratibu ulioutoa awali.
Fomu za uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa katika ofisi za Makao Makuu ya TFF-Karume. Vilevile fomu zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya TFF amayo ni www.tff.or.tz.
TFF inafuatilia kwa karibu mwenendo mzima wa mchakato na taarifa zote zitatolewa na TFF kupitia wasemaji wake na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ambaye ni Wakili Msomi, Alloyce Komba.
Tayari Kamati ya Uchaguzi ya TFF, iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Klabu ya Young Africans imeridhishwa na mwenendo wa wanachama kwa namna wanavyochukua na kurejesha fomu.
Na kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu mpaka Jumatatu Juni 6, 2016 saa 10:00 jioni.
Hadi sasa wanachama tisa (9) wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.
Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.
Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz
Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.    

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KUSIMAMIA UKUAJI WA UCHUMI KWA MAENDELEO YA

NGO1 
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameliambia Bunge Mjini Dodoma, Leo, Juni Mosi, 2016 kwamba serikali imejipanga kuchukua hatua madhubuti zinazolenga kujenga Taifa linalojitegemea kwa kukuza uchumi na kupunguza umasikini. 
Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na  kusimamia na kufuatilia kwa ukamilifu utekekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. Mpango huu unajikita katika kujenga msingi wa uchumi wa viwanda na maendeleo ya watu.
Amesema kuwa ili mpango huu uweze kutekelezwa kwa ufanisi na kupata matokeo tarajiwa, ni dhahiri kuwa zinahitajika rasilimali za kutosha, hususan rasilimali fedha. 
“Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na wadau wengine inalo jukumu la kuimarisha ukusanyaji wa mapato ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa rasilimali fedha” alisisitiza
Dkt. Mpango amesema kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 imeweka bayana majukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango ya kuimarisha usimamizi na ukusanyaji wa mapato, kupanua wigo wa vyanzo vipya vya mapato na kusimamia kwa ufanisi matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali.
Amenukuu kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, alipokuwa anawasilisha hotuba yake katika Bunge, Aprili 25 mwaka 2016, aliposema kuwa  mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano yenye falsafa ya HAPA KAZI TU, imelenga kufikia kipato cha kati na kufanyika mapinduzi makubwa ya viwanda yanayotegemea sana utulivu wa uchumi.
“Tutasimamia kikamilifu matumizi ya vifaa na mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ili kuongeza ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato” Aliongeza Dkt. Mpango
Amesema kuwa serikali itarasimisha sekta isiyo rasmi kuingia katika mfumo wa kodi na hivyo kupanua wigo wa kodi na Kuimarisha ufuatiliaji wa mapato yanayokusanywa na taasisi na mamlaka mbalimbali za Serikali ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Dkt. Mpango amebainisha kuwa watasimamia na kuimarisha ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi na kuboresha usimamizi wake chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kutokana na uzoefu na mifumo ya ukusanyaji iliyopo nchi nzima
“Tutaendelea kuchukua hatua za kudhibiti na kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija na Kuendelea kuimarisha usimamizi na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara bandarini na maeneo ya mipakani ili kuhakikisha kwamba kodi stahiki zinakusanywa” aliongeza Dkt. Mpango.
Ametaja mikakati hiyo kuwa ni moja ya njia ya kupunguza utegemezi wa misaada kutoka nje ambayo imezidi kupungua kila mwaka.
Ametoa mfano wa mwaka wa fedha unaoishia Juni mwaka huu ambapo hadi Machi, wadau wa maendeleo wametoa shilingi bilioni 1,064.89 sawa na asilimia 46 ya fedha zote zilizoahidiwa kutolewa na wadau hao hali iliyoathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyokusudiwa
Ametaja sababu za hali hiyo kuwa ni kupungua kwa misaada toka nje kunatokana na kujiondoa kwa baadhi ya Washirika wa Maendeleo wanaochangia kupitia Misaada na mikopo ya kibajeti na baadhi ya Washirika wa Maendeleo kupunguza ahadi zao.
“Wafadhili wanaochangia kupitia misaada ya kibajeti walipunguza michango yao kutoka shilingi bilioni 660 mpaka shilingi bilioni 399 katikati ya mwaka wa fedha 2015/16 na wengine kuhusisha utoaji wa fedha na masharti ambayo hayakuwemo katika makubaliano ya awali” Aliongeza Dkt. Mpango
Alisema kuwa katika kushughulikia changamoto hizo, Serikali inaendelea na mazungumzo na Washirika wa Maendeleo ili kuhakikisha kwamba fedha zilizoahidiwa zinatolewa kwa wakati.
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameliomba Bunge, liidhinishie Wizara yake kupitia mafungu yote tisa ya kibajeti, jumla ya Shilingi Trilioni 8.7 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na shilingi Bilioni 791.99 kwaajili ya miradi ya maendeleo.
Amesema kuwa  Kati ya fedha hizo,shilingi bilioni 45.45 ni kwa ajili ya Mishahara na shilingi bilioni 8,671.04 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM (BARA) AKUTANA NA WAJUMBE WA TIMU YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI WA UMOJA WA ULAYA (EU)

 
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Philip Mangula akizungumza na Timu ya Wajumbe  Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya waliomtembelea leo ofisini kwake Lumumba jijini Dar es salaam.
Waangalizi wa Uuchaguzi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) wakimsikiliza kwa makini Makamu Mwenyekiti wa CCM Mhe. Philip Mangula ofisini kwake Lumumba jijini Dar es salaam.
 Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) wakizungumza na  Makamu
Mwenyekiti wa CCM Mhe. Philip Mangula ofisini kwake Lumumba jijini Dar
es salaam .Kikao hicho pia kilihuzuliwa na Kaimu Mkuu wa Idara Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dkt. Pindi Chana.

Timu hiyo ya Waangalizi wa Umoja wa Nchini za Ulaya ilikuwa na ujumbe wa watu watano ambao ni Mhe. Judith Sargetini, Mbunge na Kiongozi Mkuu wa Waangalizi, Ms Tania Marques Naibu Kiongozi wa Waangalizi, Balozi Roeland Van De Geer (Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya), Ms Luana Reale, (Kansela) na Ms Anna Constatini (Mwambata wa Masuala ya Uchaguzi)  

SERIKALI YATOA UFAFANUZI UBORESHAJI WA MASLAHI YA POLISI NA NAFASI ZA MAFUNZO YA JKT.

TU1 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha 34 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
TU2 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ndani ya Ukumbi wa Bunge kabla ya kuanza kwa kikao cha 34 cha Mkutano wa 3 wa Bunge mjini Dodoma.
TU3 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar es salaam wakifuatilia shughuli za kikao cha 34 cha Bunge mjini Dodoma. Wanafunzi 90 wa shule hiyo wamelitembelea Bunge hilio kujifunza namna linavyoendeshwa.
TU4 
Baadhi ya Mawaziri na Wabunge wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 34 mjini Dodoma.
TU5 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Muhagama akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa Serikali ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
TU6 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kulia) akimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
TU7 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.
TU8 
Baadhi ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatilia shughuli za kikao cha 34.
TU9 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kulia) kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma. Picha/Aron Msigwa –MAELEZO
………………………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa- DODOMA.
Serikali imesema kuwa itaendelea kuboresha maslahi ya askari wa Jeshi la Polisi na kuwajengea nyumba za kisasa za kuishi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu mkakati wa Serikali wa kuboresha maslahi ya Askari wa Jeshi hilo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bungeni mjini Dodoma leo
Amesema kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 itatekeleza Mpango kabambe wa ujenzi wa nyumba za Polisi 4136 ambao utakwenda sambamba na ujenzi wa vituo vya Polisi.
Amesema Serikali imechukua hatua za haraka kulishughulikia suala la ukosefu wa nyumba za askari hao katika maeneo mbalimbali nchini ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yenye ukosefu wa nyumba hizo.
Amelieleza Bunge kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa maslahi ya Askari Polisi yanaimarishwa ikiwemo malipo ya Posho ya pango kwa askari wasio na nyumba ambayo ni asilimia 15 ya mishahara yao ili waweze kulipia gharama hizo.
Ameongeza kuwa  askari wenye utalaam maalum wakiwemo madereva na madaktari wamekuwa wakilipwa posho ya asilimia 15 ya mishahara yao na kuongeza kuwa askari wanaoajiriwa katika ajira mpya kama madaktari wamekuwa wakilipwa mishahara sawa na madaktari wengine bila kujali vyeo vyao.
“Serikali tumefanya jitihada kubwa sana kuboresha maslahi ya askari wetu, kama Serikali tumetoa posho za nyumba, posho za utalaam maalum kwa askari wote ambayo ni asilimia 15 ya mshahara wa kila Polisi hii yote ni kuwafanya askari wetu waweze kumudu gharama za maisha” Amesisitiza Mhe. Mpina.
Ameeleza kuwa kwa askari wanaofanya kazi katika mazingira magumu wakiwemo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wamekuwa wakipewa posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu (Hardship allowance) kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kila mwezi.
Mhe. Mpina amebainisha kuwa askari wote wanaohitimu mafunzo yao wamekuwa wakikatiwa Bima ya Afya kwa asilimia 100 na Serikali pamoja na udhamini wa mikopo mbalimbali katika taasisi za kifedha ili waweze kupewa mikopo na taasisi hizo.
Aidha, amesisitiza kuwa serikali imewapandishia kiwango cha Posho ya katikati ya mwezi (Ration Allowance) kutoka shilingi 180,000 za awali hadi 300,000 ambazo wanalipwa kwa sasa nchi nzima.
Katika hatua nyingine Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imetoa ufafanuzi kuhusu vijana wa kidato cha nne kutochukuliwa kujiunga na  Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi  amesema kuwa hatua ya kuwachukua vijana wote wanaomaliza kidato cha nne kwa sasa haiwezekani kutokana na uwezo mdogo wa kifedha wa Serikali.
Amesema kuwa uwezo wa JKT kuchukua vijana wa kujitolea kwa sasa ni 5000 hadi 7000 kwa mwaka kulingana na bajeti inayotolewa na kuongeza kuwa mpango wa Serikali ni kuendelea kutenga fedha na kujenga kambi zaidi za mafunzo ili kuwawezesha vijana wengi kujiunga  na mafunzo hayo kulingana na upatikanaji wa fedha.
Kwa upande wa wahitimu wa kidato cha sita wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa Sheria Mhe. Mwinyi amesema Serikali imewachukua vijana 14,000 na inaendelea kujenga uwezo wa ndani wa kuchukua vijana wengi zaidi.
Amesema Serikali inakusudia kujenga majengo ndani ya makambi ili kuwezesha vijana wote wanaohitimu kidato cha sita kupitia JKT kabla ya kujiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini.
Aidha, Amefafanua kuwa kwa wale wanaojiunga na JKT kwa kujitolea ambao idadi yao inafikia 5000 sio wote wanaopata nafasi ya kuajiriwa katika vyombo vya Ulinzi na Usalama na kuongeza kuwa ni asilimia 71 ndio hupata ajira kwenye vyombo hivyo huku waliobaki wakilazimika kurudi nyumbani.
Amebainisha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaangalia utaratibu wa kuwawezesha vijana hao ili wanaporudi uraiani waweze kupatiwa mitaji ya kuwawezesha kujiajiri wenyewe.

SERIKALI IMEJIPANGA KUKARABATI UWANJA WA NDEGE WA MTWARA.

images 
Na Fatma Salum- MAELEZO,
 Dodoma.
Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imetenga shilingi bilioni 10 katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani leo Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe. Hawa Ghasia lililohoji kuhusu ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Mhe. Ngonyani alisema kuwa Serikali imeendelea kufanya matengenezo ya mara kwa mara katika uwanja huo na TAA inafanya tathmini ya uchakavu wa matabaka ya lami (Pavement Evaluation) ya njia ya kuruka na kutua ndege ili kubaini ukarabati stahiki unaotakiwa na matumizi ya fedha zinazohitajika na kazi hiyo ya tathmini inatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2016.
Aidha, Mhe. Ngonyani alieleza kuwa katika mpango wa muda mrefu, Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inaandaa Mpango Kabambe (Master Plan & Concept Design) kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa uwanja huo kutoka daraja 3C la sasa kwenda daraja la 4E ili kuweza kuhudumia ndege kubwa zaidi hivyo kuwa kitovu cha usafiri wa anga kwa Ukanda wa Kusini.
“Ukarabati na upanuzi wa uwanja utahusisha miundombinu yote ya kiwanja ikiwemo taa na mitambo ya kuongozea ndege pamoja na majengo. Kazi hiyo ya uandaaji wa Mpango Kabambe na Usanifu wa Awali inatarajiwa kukamilika Julai 2016.” Alisema Ngonyani.
Ikiwa ni mpango wa muda mfupi, Mhe. Ngonyani aliongeza kuwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imeingia makubaliano na Kampuni ya British Gas (BG) kwa ajili ya kutumia taa zake ambazo ni za kuhamisha kwa ajili ya kuongozea ndege pale ambapo ndege itatakiwa kutua usiku katika uwanja huo.

SERIKALI YAZIAGIZA TAASISI ZAKE KUTOA RISITI ZA KIELEKTRONIKI

NGO3 
Na Fatma Salum- MAELEZO.
Dodoma
Serikali imeagiza kuwa kuanzia Mwezi Julai mwaka huu ni lazima mfumo wa kielektroniki utumike katika utoaji wa risiti kwa tozo, faini, ada na malipo mengine yote ya Serikali Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakala wote wa Serikali ili kudhibiti upotevu wa mapato.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Dkt. Mpango alisema kuwa agizo hilo pia linahusisha malipo ya faini za mahakamani, faini za usalama barabarani, viingilio kwenye mbuga za wanyama na vibali vya kuvuna maliasili.
“Naziagiza ofisi zote za Serikali kutoa risiti za kielektroniki kwa malipo yote yatakayofanyika kwani matumizi ya vifaa na mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato yataongeza ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali.” Alisema Dkt. Mpango.
Katika kufanikisha hilo Dkt. Mpango aliongeza kuwa Maafisa Masuuli wote wanaelekezwa kusimamia ipasavyo utekelezaji wa agizo hilo.
Katika hatua nyingine, Dkt. Mpango alisema kuwa Serikali imeamua kufanya uthamini wa majengo kwa mkupuo ili kuongeza mapato yatokanayo na kodi ya majengo na usimamizi wake utakuwa chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Katika hotuba hiyo Dkt. Mpango amefafanua mkakati wa Wizara yake kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano kuanzia 2016/17 hadi 2020/21 ambao umejikita katika kujenga msingi wa uchumi wa viwanda na maendeleo ya watu.

MATUKIO BUNGENI BAJETI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO MJINI DODOMA LEO

NGO1 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2016/2017, Bungeni Mjini Dodoma leo
NGO2 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (Kulia) akifurahia jambo na Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Zanzibar, Tauhida Cassian Galoss Nyimbo, mara baada ya kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 mjini Dodoma leo.
NGO3 
Waziri wa Fedha na MIpango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Naibu Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaji, wakiwa makini kuandika hoja mbalimbali za wabunge wakati wakichangia Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma leo.
NGO4 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo ambapo kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Dorothy Mwanyika na kushoto kwake ni naibu Katibu Mkuu Amina Hamis Shaban.
NGO5 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma mara baara ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo.

Tanzania yasifika kwa Utawala wa Sheria:Waziri Kairuki

index 
Na Immaculate Makilika – MAELEZO
Serikali ya Tanzania yasifika kwa kuwa na uongozi unaozingatiaSheria na Utawala Bora.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki alipokuwa akifungua Mkutano wa siku mbili  wa Kimataifa kuhusu Utawala wa Sheria na Utawala bora.
Lengo la mkutano huo ilikuwa ni  kujadili masuala ya Afrika katika kukuza utawala wa sheria katika utekelezaji wa agenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na agenda ya Umoja wa Afrika ya 2063.
“Mkutano huu wa kistoria nchini Tanzania utasaidia kuleta mageuzi katika Taasisi zinazosimamia masuala ya Sera na Sheria ambayo yatachochea maendeleo mazuri katika nchi za Afrika”, alisema Waziri Kairuki.
Akiendelea kuzungumza Waziri Kairuki alisema uwepo wa Marais wastaafu kama Mhe.Benjamin Mkapa na Dkt. Jakaya Kikwete, katika mkutano huo ni ushahidi tosha wakuwepo na mafanikio ya utawala wa sheria na utawala bora nchini Tanzania.
Kwa upande wa Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa, amesema ili Bara la Afrika liendelee Kiuchumi ni lazima watu wake wapate elimu ya uraia ili waweze kushiriki zaidi katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo yao pamoja na kuwepo na uongozi utakaoleta mabadiliko “transformative leadership”.
Naye, Waziri wa Haki Sudani ya Kusini Mhe. Pwanauwilla Unango amesema pamoja na kuwa Bara la Afrika lina matatizo mengi kama vita, njaa, magonjwa na ndoa za utotoni, dunia isiitazame Afrika kwa mtazamo huo pekee, bali inahitaji msaada kutoka Jumuiya za Kimataifa.
Mkutano huo wenye kauli mbiu “Kufikia agenda ya 2030 na agenda ya 2063:Utawala wa Sheria kwa Maendeleo Endelevu ya Afrika”, (Achieving the 2030 agenda and agenda 2063:The rule of law as a driver of Africa’s suistainable development) , umeandaliwa na  Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Sheria (IDLO) la nchini Italia, kwa Ushirikiano wa Serikali ya Tanzania  umehusisha wadau mbalimbali wakiwemo Mawaziri, kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mabalozi kutoka ndani na nje ya Afrika pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu.

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATUA MKOANI TANGA, AZUNGUMZA NA WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI, ATEMBELEA MSITU WA MAPANGOPORI YA AMBONI

MAN1 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akichungulia pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MAN2 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo (kulia), mara baada ya kutoka ndani ya pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Katikati ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MAN3 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama vinavyotoa ulinzi katika msitu wa Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri alifanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MAN4 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza kuu) akizungumza katika Kikao cha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Mkoa huo, Martine Shigella. Watatu kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu (wapili kushoto). Viongozi hao wamekutana  mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama mkoani Tanga.
MAN5 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella kabla ya kwenda katika msitu wa Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri alifanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Nishati ya uhakika inahitajika kwa ukuaji wa uchumi – Prof. Muhongo

MH1 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao  kilichoshirikisha watendaji kutoka  kampuni zinazojishughulisha na  utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za Statoil na ExxonMobil pamoja na  Wizara ya Nishati na Madini na  Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)
MH2 
Meneja Mkazi wa Kampuni  inayojishughulisha na  shughuli za   utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta  ya  Statoil Tanzania, Øystein Michelsen, (kushoto) akielezea shughuli zakampuni  hiyo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia)
MH3 
Meneja Mkazi wa Kampuni  inayojishughulisha na  shughuli za   utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta  ya  Statoil Tanzania, Øystein Michelsen akisisitiza jambo  katika kikao hicho.
MH4 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mbele) akiongoza kikao  kilichoshirikisha watendaji kutoka kampuni zinazojishughulisha na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na  gesi za  British  Gas (BG),  Ophir, Pavilion pamoja na  Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo  ya  Petroli Nchini (TPDC)
………………………………………………………………………………………………………
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa   ili  Tanzania  iweze kuwa nchi ya  viwanda, nishati ya uhakika inahitajika  na kutaka makampuni kuwekeza katika uzalishaji wa umeme unaotokana na gesi.
Profesa Muhongo aliyasema hayo jijini  Dar es  Salaam   katika  nyakati  tofauti alipokutana na  watendaji wa kampuni zinazojishughulisha na  Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi  pamoja na wataalam kutoka  Wizara ya Nishati na Madini na  Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) lengo likiwa ni  kupokea taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali  ya makampuni hayo.
Kampuni hizo zinazofanya  kazi kwa kushirikiana na  Shirika la TPDC  ni pamoja na  British  Gas (BG),  Ophir,  ExxonMobil na Statoil.
Profesa Muhongo alisema kuwa hakuna nchi yoyote  duniani iliyopiga hatua kimaendeleo bila kuwa na nishati ya uhakika ya  umeme na kuwataka  wawekezaji kuchangamkia  fursa kupitia  gesi nyingi iliyogunduliwa.
Alitaja maeneo yanayohitaji uwekezaji   katika kuzalisha  umeme kwa kutumia gesi  kuwa ni pamoja na Mtwara,  Lindi, Somanga Fungu, na Mkuranga
Aliongeza kuwa   viwanda  37 pamoja na  vya sementi  vinahitaji  gesi na kusisitiza kuwa  iwapo sekta ya  gesi itatumiwa ipasavyo inaweza kuchangia nchi  kupiga hatua na kuingia katika  kundi la nchi zenye kipato cha  kati ifikapo mwaka 2025 kama  Dira ya Maendeleo  ya Taifa inavyosema.
Wakati huo huo Profesa Muhongo, aliwataka watendaji kutoka  Wizara ya Nishati na Madini  na  Taasisi zake kufanya kazi kwa kasi ili kuendana na kasi ya uwekezaji katika  shughuli za utafutaji na uchimbaji  wa gesi na mafuta.
“Sekta ya gesi na mafuta ambayo ni mpya inahitaji umakini  na kasi  ili kuvutia wawekezaji  zaidi,” alisisitiza Profesa Muhongo.
Akizungumzia   mikakati ya serikali katika kuzalisha  wataalam  katika masuala ya mafuta na gesi Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imekuwa ikitoa ufadhili kwa wanafunzi katika ngazi  za shahada za uzamili na uzamivu katika  vyuo  vilivyopo nje ya nchi  vyenye uzoefu katika  fani hiyo, pamoja na uanzishwaji wa programu hizo katika   Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha  Dodoma (UDOM) na  Chuo  cha Madini.
Alisema kuwa  mpaka sasa kuna idadi ya takribani wanafunzi 98 waliohitimu masomo hayo  na kuziomba kampuni hizo   kuajiri wataalam hao  ili wawe na mchango mkubwa kwenye  sekta ya gesi.
“ Nia ya Serikali ni kuwa na wataalam wazawa ambao  watanufaika  kupitia  uchumi  wa gesi kwa kufanya kazi katika  viwanda vya kuchakata gesi na kuzalisha umeme unaotokana na  gesi,” alisema Profesa Muhongo.
Naye   Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk.  James Mataragio alisema kuwa  shirika  hilo  limekuwa likishirikiana na  kampuni hizo katika  hatua zote muhimu hususan katika kiwanda cha  kuchakata  gesi asilia  kimiminika (Liquefied Natural Gas) na  kuongeza kuwa mpaka sasa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda limeshapatikana.
Alisema kuwa,   Tanzania inatarajia kuwa kitovu kikuu cha gesi barani  Afrika kwani  gesi nyingi  itakayozalishwa  itauzwa katika nchi nyingine.
Aliongeza kuwa nchi kama  Uganda,  Jamhuri ya  Demokrasia  ya Kongo na  Zambia  zimeonesha nia ya  kuhitaji  gesi kwa ajili ya kuzalisha nishati ya uhakika kwa kuwa nchi hizo  zinatumia maji kuzalisha umeme ambapo uzalishaji wake  hupungua hususan  wakati wa kiangazi kutokana na kupungua kwa kina  cha maji.
Naye Meneja Mkazi wa Kampuni  ya  Statoil Tanzania, Øystein Michelsen, alisema kuwa kampuni yake  ipo  tayari kushirikiana na Serikali  kuhakikisha kuwa miradi yake inakamilika kwa wakati.
Alisema  tangu  kampuni hiyo kuanza  shughuli zake nchini,  imekuwa ikishirikiana na  Serikali kwa kutoa ufadhili wa masomo  katika masuala ya  gesi na mafuta nje ya nchi kwa wanafunzi wanaofanya  vizuri.
Aliongeza kuwa kampuni ya  Statoil imekuwa ikitoa elimu ya  ujasiriliamali kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara  ili waweze kushiriki  katika uchumi wa gesi kupitia  utoaji wa  huduma  zake kwa Kampuni hiyo.

TOUR 2016 MALAWI

city in malawi copy
Wakati siku za kuanza msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania bara zikiendelea  kuhesabika  kufuatia  hitimisho la msimu jana mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu  na   Yanga kuibuka mabingwa, ratiba ya mwanzo ya michezo ya kirafiki ambayo kikosi cha Mbeya City Fc  kitacheza kwa ajili ya matayarisho ya 2016/17 imetoka.
Kwenye ratiba hiyo, City  imepaga kucheza michezo mitatu ugenini, ambapo itaanza kwa kushuka ‘dimbani’ Kamuzu Stadium jijini Blantyre Juni 18  kucheza na vigogo wa soka nchini Malawi, Big Bullets.
KUPATA SAUTI  NA KUJUA ZAIDI KUHUSU  RATIBA KAMILI YA MICHEZO YA KIRAFIKI 2016
FUNGUA  LINK HII:  http://mbeyacityfc.com/tours/

Mfuko wa sheria yatoa ruzuku bilioni 18 kwa mafunzo ya wasaidizi wa sheria

LE1 
Kaimu Afisa Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Bi Scholastica Jullu akizungumza na waandishi wa habari jinsi wasaidizi wa kisheria wanavyosaidia kubadilisha maisha ya watanzania 
LE2 
Jopo la viongozi wa LSF wakionyesha ripoti jinsi wasaidizi wa sheria walivyotatua matatizo ya wananchi nchini, kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano,  Renatus Sona, Afisa Mradi na Haki za wanawake, Bi Fortunata Kitokevya, Kaimu Afisa Mtendaji, Bi Scholastica Jullu, wa pili kulia Meneja Ufuatiliaji na Matokeo, Juma Mwenga na mwisho kulia ni Bw. Masele
……………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa msaada wa kisheria (LSF) umetoa ruzuku kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 18 kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha utoaji wa msaada wa kisheria kwa ajili ya  mafunzo kwa wasaidizi wa sheria 4,000 nchi nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Afisa Mtendaji, Bi Scholastica Jullu amesema kwamba ruzuku imetolewa kuanzia 2012 kwa mashirika hayo ili kuweza kutoa mafunzo kwa wasaidizi wa sheria katika kutatua matatizo yanayowakabili wananchi hasa wa vijijini.
“Dhumuni la uanzishwaji wa mfuko huu ni kulinda haki za binadamu kupitia ujengaji uwezo wa kisheria na kuongeza upatikanaji wa huduma za kisheria kwa watu masikini na wanajamii wengine walio katika hatari ya kukosa haki zao hususani wanawake nchini,” aliongeza Bi Jullu
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011, LSF imechangia katika kukuza na kulinda haki za binadamu huku ikiweka msisitizo katika ulinzi w haki za wanawake na makundi maalum.
Amesema kwamba kutokana na mafunzo waliopata wasaidizi wa kisheria nchini imewezesha upatikanaji wa huduma za usaidizi wa sharia kwa watanzania takribani milioni thelathini na tano (35 milioni).
Alifafanua kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka 2015 takribani watu 90,000 walipata huduma za msaada wa kisheria na watu 300,000 walifikiwa na elimu ya sheria nchini nzima.
Mambo ambayo wasaidizi wengi wa sheria wanayokutana nayo ni matatizo ya ardhi, ndoa, mirathi, watoto na jinsi ambao asilimia 80 yalishughulikiwa na asilimia 9 tu yalipelekwa kwenye vyombo vingine vya utoaji haki kama vile mahakama, mabaraza ya usuluhishi, serikali za mitaa na polisi.
Bi Jullu alisisitiza mchakato umeanza kwa wadau wa sheria, mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali ili kuja na sheria itakayowatambua wasaidizi wa kisheria kwenye mifumo ya serikali.
Kwa upande wake, msaidizi wa kisheria kutoka wilaya ya ilala, Bi Beatrice Bange amesema kwamba changamoto kubwa ni uelewa mdogo wa watanzania wengi kuhusu huduma za wasaidizi wa kisheria na msaada wa kisheria.
Aliongeza kwamba matatizo mengi anayokutana nayo katika wilaya ya ilala ni ndoa, mirathi na matatizo ya ajira kwa wafanyakazi wa kada ya chini.
Utafiti uliofanywa na shirika hilo mwaka jana ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya watanzania hawana uelewa kuhusu msaada wa kisheria na uwepo wa wasaidizi wa sheria.

Hifadhi ya Selous yapoteza asilimia 90 ya Tembo wake

images 
Na Daudi Manongi
Hifadhi ya Taifa ya  wanyamapori ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania imepoteza asilimia  90 ya Tembo waliopo katika hifadhi hiyo kutokana na ujangili uliokithiri.
Ripoti ya mfuko wa hifadhi ya wanyapori na mazingira duniani (WWF) imesema kufikia mwaka 2022 kama hakutakuwa na hatua zozote kali zitakazochukuliwa kuwalinda tembo kutokana na ujangili  basi  watatoweka kabisa.
Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa kwa miaka ya nyuma mbuga ya Selous ilikuwa mojawapo ya mbuga kubwa kabisa katika bara la afrika yenye tembo wengi ambapo kulikuwa na tembo zaidi ya 110000 lakini kutokana na ujangili uliokithiri katika miaka 40 iliyopita tembo hao wamepungua na kubakia 15000 tu uku mahitaji makubwa ya pembe za ndovu katika nchi ya china yakitajwa na ripoti hiyo kuwa kichocheo kikubwa cha ujangili na mauaji ya idadi kubwa ya tembo hao.
Aidha ripoti hiyo inaonyesha hathari kubwa  kiuchumi itakayotokea  kutokana na kwamba Tanzania kupitia Mbuga ya Selous inaingiza dola milioni 6 kwa mwaka ikilinganishwa na Sekta ya Viwanda inayochangia dola bilioni 5 katika pato la Taifa.
Pamoja na Hayo Serikali ya awamu ya tano  kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka mikakati madhubuti ikiwemo kuunda kitengo chake cha intelijensia na kuunda kanda nane za doria za ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya mbuga ya Selous ambayo imeanza kuwa na mafanikio  ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau wa uhifadhi kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi na zana kwa ajili ya doria.
Mwaka 2014 Shirika la Kimataifa la Sayansi,Elimu na Utamaduni la umoja wa mataifa(UNESCO) liliiweka Mbuga ya Selous katika Urithi wa asili ulio hatarini Duniani.

TAARIFA KUTOKA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO (TASWA)

index 
A;KAMATI YA TUZO
 
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imemteua Makamu Mwenyekiti wa TASWA, ambaye pia Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Egbert Mkoko kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania mwaka 2015/2016.
 
Pia TASWA imeteua wajumbe tisa wa kamati hiyo. Majina yao na vyombo vyao katika mabano ni Mahmoud Zubeiry (Bin Zubeiry Sports- Online), Jane John (TBC), Baruani Muhuza (Azam Media), Limonga Justine (Redio Uhuru), Maulid Kitenge (E-FM Redio), Deogratias Rweyunga (Redio One/ITV), Shaffih Dauda (Clouds Media), Asha Muhaji (Bingwa) na Nelly Mtema (Daily News).
 
Kamati inaweza kuongeza wajumbe wengine au kupunguza kwa kadri itakavyoona inafaa. Utaratibu wa kuizindua kamati hiyo unaandaliwa na sekreterieti ya TASWA. Jukumu la kamati itakuwa ni kuandaa utaratibu wa kuwapata wanamichezo watakaowania tuzo hiyo na pia kuteua washindi kwa kila mchezo.
 
Tuzo za Wanamichezo Bora zinazotolewa kila mwaka na TASWA zimepangwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu, Dar es Salaam zikihusisha michezo mbalimbali.
 
B; ZIARA YA MAFUNZO NAIROBI
 
TASWA kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya, vimeanzisha program ya ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu baina ya vyama hivyo viwili, ikiwa katika makundi tofauti ya wahariri/waandishi waandamizi na kundi lingine la waandishi wa habari chipukizi.
 
Kwa kuanzia wahariri wa habari za michezo 18 au wale wenye uzoefu katika uandishi usiopungua miaka kumi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wataenda Nairobi kwa ziara ya mafunzo kuanzia Julai 6-9 mwaka huu.
Tunaamini wakirudi wataendelea kuwa waalimu wazuri kwa wale chipukizi, ambao nao watapata fursa kama hiyo siku za usoni.
Ahsanteni,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
01/06/2016

Tatizo la hewa ya Ukaa kupungua hapa nchini.

nyu 
Frank Mvungi-Maelezo
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) umeanza kufanya utafiti utakaosadia kupunguza kiwango cha Hewa ya Ukaa (green house gases) kinachozalishwa  kutokana na shughuli za ujenzi ili  kupunguza uharibifu wa mazingira.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mhandisi Heri Hatibu kutoka wakala huo amesema utafiti utasaidia kupunguza gharama za Ujenzi hapa nchini.
Akizungumzia Malengo ya Utafiti huo Hatibu amesema kuwa, utasaidia kupunguza kiwango cha nishati kinachotumiwa kwenye nyumba kwa ajili ya kupooza hewa hivyo kuokoa fedha inayoweza kutumika kufanya mambo mengine.
“Sekta ya Ujenzi inachangia asilimia 40 ya hewa ya ukaa hivyo lengo la utafiti huu ni kusaidia kuondoa tatizo hili mara baada ya utafiti wetu kukamilika.” Alisisitiza Mhandisi Hatibu.
Aidha Hatibu amesema kuwa, utafiti huo utawezesha kusanifu majengo yatakayotumia nishati kidogo kwenye hatua ya ujenzi na hata wakati wa matumizi ya majengo husika. Pia utachochea matumizi ya vifaa vya Ujenzi vinavyopatikana katika maeneo ya karibu na shughuli za ujenzi.
Pia utafiti huo utasaidi kutoa elimu kwa wadau wa ujenzi kuhusu nishati mbadala katika kutekeleza shughuli za ujenzi, ikiwemo kuacha kukata miti.
Vile vile wananchi wataelimishwa kuhusu njia bora za uchomaji wa matofali ili waweze kutumia vifaa vingine badala ya kukata miti kwa ajili ya uchomaji matofali.
Matokeo ya utafiti huo unaotarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu yatasaidia wadau wa sekta hii kupanga mipango ya ujenzi itakayosaidia kupunguza athari katika mazingira zinazosababishwa na matumizi makubwa katika uzalishaji vifaa vya ujenzi na hata katika ujenzi.Utafiti huo unafanyika katika Mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Morogoro na Tanga.

DKT SHEIN KUZUNGUMZA NA MABALOZI WILAYA MJINI

zan11 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,  wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan12 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,  wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan1zan2Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan3 
Katibu wa CCM Wilaya ya Mjini Kichana Bi,Fatuma Shomari Juma alipokuwa akisoma risala ya Chama Wilaya ya Mjini Kichama wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanywa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani, [Picha na Ikulu.] 01/06/2016
zan6Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Kichama Bw. Juma Fakih Choum akiwasalimia wanachama cha mapinduzi waialaya hiyo wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan7 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Kichama Bw. Juma Fakih Choum  wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani, [Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan8Mwanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama Bi.Rukia Omar kutoka    jimbo la Kikwajuni alipokuwa akitoa mchango wake wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,alipowapongeza na kuwashukuru Wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan9Mwanachama cha Mapinduzi wa umoja wa Vijana UVCCM Ashrak Saleh Zingo katika shehia ya kiponda mji Mkongwe wa Zanzibar alipokuwa akitoa mchango wake uliogusia zaidi uvunywaji wa katiba ya Zanzibar unaofanywa na Wanachama cha Upinzania,mchango huo aliuotoa leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani wakati wa Mkutano wa Kuwashukuru Viongozi wa Mashina,wenyeviyi wa Matawi na Maskani uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
zan10Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakinyoosha mikono juu kuunga mkono hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwashukuru kuwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI NCHINI PAPUA NEW GUINEI LEO

un1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mzungumzaji Mkuu wa Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye mkutano huo uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea.
un2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipongezwa na  Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo wakati Makamu wa Rais alipomaliza kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano huo. Katikati Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Mhe. Natumbo Nandi Ndaitwah.
un3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo wakati Makamu wa Rais alipomaliza kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano huo. Katikati Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Mhe. Natumbo Nandi Ndaitwah.
un4 
Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo akimpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya  kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
un5 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mzungumzaji Mkuu wa Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye mkutano huo uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.

Heri ya Kuzaliwa Mwanalibeneke wa Lukaza Blog – Josephat Lukaza

Kwanza Napenda kuchukua Nafasi hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kuniwezesha kuiona siku ya Leo maana Si kwa uwezo wangu bali ni kwa Uwezo wake Muumba wetu aliye Juu.

Leo ni siku muhimu sana kwangu maana inanikumbusha siku niliyoletwa Duniani na Mungu kupitia Mama yangu kwa kusudi maalumu hapa duniani.
Napenda Kumshukuru Mungu kwa maana neema na rehema zake ni Za milele. Nasema asante kwa kunifanya kuongeza mwaka mwingine huku nikiwa na afya njema.

Kiukweli Sina cha Kumlipa Mwenyezi Mungu zaidi ya Kumsifu na Kumwabudu yeye kwa maana Sio kwa uwezo wangu.Napenda kuwashukuruni wote Ambao Mmekuwa mkiniombea na kunitakia heri ya kuzaliwa kwangu Nasema asante na Mungu awabariki sana.

Nakukabidhi wewe bwana njia zangu na kukutumainia kwasababu umeagiza kila akukabidhie njia zake na kukutumainia unaenda kumtendea. Zaburi 37: 5 Leo nasema asante sana kwa Maana kila napokuita Wewe unaitika.
Naomba pia uendelee kuziimarisha hatua zangu kwa maana uliagiza katika Zaburi 37:23 Kuwa “Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake”
Hakika wewe ni Mungu wa Wote.
Nachukua fursa hii kuwa shukuruni wote Ambao mmenitakia baraka na heri katika siku hii muhimu sana kwangu ambayo inanifanya nitafakari matendo yangu hapa duniani, Uhusiano wangu na Mungu wangu, Uhusiano wangu na Ndugu zangu, Uhusiano na Jamii yangu pamoja na rafiki zangu hakika Namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kupatana na Ndugu zangu, jamii yangu na hata marafiki zangu. Kiukweli Namshukuru Mungu kwasababu Ni kwa neema zake na Rehema zake ndio zimenifikisha hapa wala sio kwa ujanja wangu wala mimi sio mwema sana kuzidi wengine.
Wewe Ni Mungu wa wote, Huchelewi wala Huwahi Hakika nitakusifu na kukuabudu siku zote za maisha yangu kwa maana matendo yako makuu uliyonitendea Nayaona na kuyafurahia.

Asante sana Mungu wangu naomba uendelee Kutimiza haja za Moyo wangu. Nitaendelea Kukushangilia na Kukusifu kwa maana kila napokuita unaitika.
Happy Birthday to You Josephat Lukaza – Lukaza Blog

WAZIRI NCHEMBA AAGIZA MAOFISA USHIRIKI SINGIDA KUCHUKULIWA HATUA

mbunge  wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu (kulia) akimpokea  waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba alipofanya ziara ya  kikazi wilaya ya Manyoni jana
Waziri Nchemba  akisalimiana na mbunge Nyalandu (kulia)
Waziri  wa  kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali  kuingia  ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku Manyoni
Mbunge Lazaro  Nyalandu kulia akiwa na waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba wakati akisaini kitabu cha  wageni  ofisi ya mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida
Waziri Nchemba  akiingia ukumbi wa mkutano kati yake na  wakulima wa Tumbaku manyoni
Wakulima wa Tumbaku  wakisalimiana na waziri Nchemba 
Baadhi ya madiwani  wakulima wa Tumbaku manyoni wakimpokea  waziri Mwigulu Nchemba
Baadhi ya  wakulima wa Tumbaku  wakiwa  ukumbi wa mkutano kati yao na waziri Nchemba
Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu  akitambulisha  viongozi mbali mbali kabla ya  mkutano wa  wakulima wa Tumbaku kuanza
Waziri wa  Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  akizungumza na  wakulima wa Tumbaku wilaya ya manyoni mkoa wa Singida jana
Diwani  wa kata ya Mitundu wilaya ya Manyoni Bw Andrea Madole  akimkabidhi nyalaka mbali mbali za uthibitisho wa michango kandamizi  wanayobambikizwa  wakulima wa Tumbaku na Kitengo  cha AMIS   waziri wa  kilimo ,mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ambae alitangaza   kufuta michango  hiyo
Wakulima wa Tumbaku  wakitoa kero  zao kwa  waziri Nchemba (hayupo pichani)
Wabunge  wakisikiliza kero  za  wakulima wa Tumbaku
Waziri wa Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu  wakati  akieleza kilio  cha wakulima wa Tumbaku  wilaya ya Manyoni wakati wa  mkutano wa  waziri Nchemba na wakulima wa Tumbaku  uliofanyika  ukumbi wa CCM Manyoni jana
…………………………………………………………………………………………….
Na MatukiodaimaBlog,Manyoni
WAZIRI wa  kilimo ,mifugo na  uvuvi  Bw Mwigulu  Nchemba amefuta michango  hewa iliyokuwa ikichangiwa na wakulima wa Tumbaku  kwa  UNION kwa  kupitia  kitengo  cha AMIS huku akiagiza serikali  ya  wilaya ya Manyoni  kuwachukulia hatua  kali aofisa  ushirika mkoa  Andru Msafiri na afisa  ushirika Wilaya   hiyo Bw Alfred Sekiete iwapo watabainika  kuhusika  deni la bilioni  7  ambalo wanadaiwa benki wakulima  wa tumbaku.
 
Waziri Nchemba  alilazimika kutoa maagizo  hayo  baada  ya  wakulima  wa zao hilo la Tumbaku  kulalamikia utaratibu mbaya wa baadhi ya  viongozi wa UNION na APEX pamoja na baadhi ya maofisa  ushirika   kujinufaisha  kupitia mgongo  wa  wakulima hao.
 
Akitoa agizo  hilo  jana mjini Manyoni  wakati wa  mkutano  wa  pamoja kati yake na  wakulima wa  Tumbaku na viongozi  mbali mbali  wa Serikali  ya  wilaya ya Manyoni na wabunge  wanaotoka  wilaya ya Maeneo  yanayolimwa Tumbaku  mkoani Singida.
 
Waziri Nchemba  alisema  kuwa  baadhi  ya mambo  ambayo serikali  ya Rais Dr John Magufuli  haipendi  kuona ni  pamoja na  wakulima kubebeshwa mizigo mikubwa ambayo kimsingi haiwasaidii kupiga hatua kimaendeleo  zaidi ya  kuwatesa .
 
Alisema  inashangaza  kuona   wakulima  hao  kuendelea  kuumizwa na  viongozi  wachache ambao  wamegeuza  wakulima ni  kichaka cha  wao  kujificha  kujinufaisha  kupitia wakulima.
 
“ Mambo  ya ajabu  sana  hiki kitu  kinaitwa AMIS ni kuwatoza  wakulima michango ya ajabu ajabu  eti  wakulima  kutozwa  dola 1200 kwa  ajili  ya kusafirisha Tumbaku toka  Dar es Salaam kwenda UNION   pia  wanachangia dola 10 kwa  kutunza  kumbukumbu zao  ,dola 3 kupakia na  kushusha mara mchango kwa ajili ya ADMIN   mambo ya ajabu kabisa wakulima wanahusika  vipi na malipo maadmin yani wanatumia lugha  za  kijanja kijanja  kuwaibia  wakulima ADMIN wa makundi kama yale ya Whatsap kwa wakulima  tena…sasa kuanzia leo natangaza  kufuta michango  hii isiyo na maelezo ya kutosha na kuagiza  kujipanga upya kwa  kuwashirikisha   wakulima na taarifa  hiyo ndani ya siku 7 niipate “
 
Waziri chemba  alisema  kuwa kabla ya  kuanza  kuwatoza  wakulima hao michango ni  vizuri  makubaliano ya  michango  hiyo yafanyike  upya kwa kuwashirikisha  wakulima na sio kuendelea  kutumia taratibu  za  zamani ambazo ni mzigo kwa  mkulima.
 
Kuhusu maafisa  ushiriki  kudaiwa  kukopa  benki  kupitia mgongo wa  wakulima  wa  tumbaku na  kupelekea  wakulima hao  kudaiwa  deni  benki  la Tsh bilioni 7 aliagiza mkuu wa  wilaya ya Manyoni kuagiza wakaguzi  na wataalam wake  kufanya  uchunguzi  na iwapo itabainika  kuwa maofisa  hao  walihusika na deni  hilo  hatua  stahiki  kuchukuliwa dhidi

No comments :

Post a Comment