Friday, June 3, 2016

VIONGOZI WIALAYA YA MFENESINI CCM KICHAMA WAZUNGUMZA NA RAIS DK. SHEIN


JEB1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mfenesini Kichama, Mkoa wa Magharibi wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu,[Picha na Ikulu.] 03/06/2016
JEB2 
Baadhiya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa katika mkutano wa kuwapongeza na kuwashukuru Wananchi na Viongozi wa Chama Wilaya ya Mfenesini Kichama wakiwemo Mabalozi,Wenyeviti wa matawi,Maskani na Makatibu katika ukumbi wa tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere leo mgeni rasmi akiwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]03/06/2016.
JEB3 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akimkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Viongozi wa CCM wakiwemo Mabalozi,Makatibu wa Matawi,Maskani na Wenyeviti katika Wilaya ya Mfenesini katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere,Bububu Mkoa wa Magaharibi Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 03/06/2016.
JEB4Mwanachama wa Umoja wa Vijana UVCCM Rashid Mohamed Othman  alipokuwa akitoa mchango wake uliogusia zaidi uendelezaji wa Matawi ya Chama yaendane na hadhi mchango huo aliutoa leo katika ukumbi wa Chuo cha Tawi la Mwalimi Nyerere Bububu Mkoa wa Magharibi Unguja wakati wa Mkutano wa Kuwashukuru Viongozi wa Mashina,wenyeviyi wa Matawi na Maskani uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.] 03/06/2016.
JEB5 
Balozi kutoka Koani Mwanahamis Iddi Mwanachama cha Mapinduzi wa Jimbo la Mfenesini Wilaya ya Mfenesini  alipokuwa akichangia kuhusu wanachama wanaokiuwa Chama wachukuliwe hatua  wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,alipofanya mkutano wa kuwashukuru  na kuwapongeza wanachama Viongozi wa Wilaya ya Mfenesini kwa ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere,Bububu Mkoa wa Magharibi,[Picha na Ikulu.] 03/06/2016. 
JEB6Mwanachama cha Mapinduzi wa Jimbo la Mfenesini Wilaya ya Mfenesini Mkoa wa Magharibi Mashaka Petro alipokuwa akichangia kukushu matengenezo ya Barabara ya Mwachealale wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,alipokua akizungumza na wanachama hao alipowashukuru  na kuwapongeza kwa ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
JEB7 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mfenesini Bw. Mjumbe Msuri wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa taCCM Mkoa Amani, [Picha na Ikulu.] 01/06/2016.

KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BENKI KUU YA TANZANIA (1966 – 2016) KUFANYIKA JUNI 22, 2016

ful12 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu Benki Kuu ya Tanzania ilipoanzishwa.
Sherehe hizi zitafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam tarehe 22/06/2016 ambapo mgeni rasmi atazindua vitabu viwili na kufuatiwa na kongamano litakaloshirikisha wataalam mbalimbali wa uchumi wakiwemo magavana 20 wa benki kuu kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mada kuu katika Kongamano hilo itakuwa: “Beyond Aid and Concessional Borrowing: New Ways of Financing Development in Africa and its Implications”, (yaani namna ya kupata fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya misaada na mikopo nafuu na athari zake) itakayowasilishwa na Prof. Justin Lin wa Chuo Kikuu cha Peiking, China. Mada hii imechaguliwa kwa kuzingatia changamoto ambazo serikali za Afrika zinakumbana nazo katika kugharamia miradi ya maendeleo wakati ambapo misaada na mikopo nafuu imekuwa ikipungua kwa kiasi kikubwa.
Wachumi waliobobea wa ndani na nje ya nchi, wakiwemo magavana 20 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) na wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) watashiriki katika kongamano hilo.
Vitabu vitakavyozinduliwa siku hiyo ni (i) “Tanzania: The Path to Prosperity” kinachoelezea masuala yanayohusu sera za uchumi nchini Tanzania ambacho kimeandikwa na wachumi waliobobea wa ndani na nje ya nchi, na kimechapishwa na Oxford University Press. (ii) Kitabu cha pili ni cha miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania kiitwacho “50th Anniversary of the Bank of Tanzania: Evolution of the Bank of Tanzania’s Role and Functions”, ambacho kinaelezea historia, majukumu, mafanikio na changamoto za Benki Kuu katika kipindi cha miaka 50 na matarajio ya Taasisi hii ya Umma katika maendeleo ya taifa katika kipindi cha miaka 50 ijayo.
Aidha, Tarehe 11/6/16 Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa atakuwa Mgeni Rasmi kwenye matembezi ya hisani ya wafanyakazi wa Benki Kuu kutoka makao makuu ya Benki hadi viwanja vya Mnazi Mmoja kuchangia ununuzi wa madawati ya shule za msingi kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki. Wafanyakazi wa Benki Kuu walioko matawini Mtwara, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya, Zanzibar na Chuo cha Benki Mwanza nao pia watafanya matembezi ya hisani kwenye mikoa yao.
Pamoja na matembezi kutakuwa na maonesho yaliyoandaliwa na Benki Kuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja yenye lengo la kuwapa wananchi historia ya taasisi hii, ilikotoka, ilipo na inakoelekea katika kutekeleza majukumu yake.
Benki Kuu ingependa kuwakaribisha wananchi kufika kwa wingi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja siku hiyo ya tarehe 11/6/16 kujifunza mengi kuhusu taasisi hii ya umma.
Aidha, tunawaomba wananchi kufuatilia vipindi mbalimbali vya redio na makala kwenye magazeti ambapo mengi kuhusu historia, changamoto, mafanikio na matarajio ya Benki yataelezwa na viongozi mbalimbali wa Benki wa sasa na waliopita.
Benki Kuu ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 1965 na kuanza kutoa huduma rasmi tarehe 14 mwezi Juni mwaka 1966. Katika kipindi cha uhai wake, Benki Kuu ya Tanzania imetimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kulingana na mahitaji ya taifa yalivyojitokeza mwaka hadi mwaka.
Imetolewa na:
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
03/06/2016

Cosmas Cheka kuwania ubingwa wa dunia dhidi ya Mmalawi Jumamosi June 4

index 
Na Mwandishi wetu
Bondia nyota wa ngumi za kulipwa nchini, Cosmass Cheka Jumamosi June 4 anapanda jukwaani kwenye uwaja wa Ndani wa Taifa kupambana na bondia wa Malawi, Chrispin Moliyati katika pambano la kuwania ubingwa wa Dunia wa Universal Boxing Union (UBO) wa uzito wa Super feather.
Pambano hilo la raundi 12 limeandaliwa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Advanced Security, Juma Ndambile kwa lengo la kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.
Ndambile  ambaye ni meneja wa Cheka alisema kuwa ameaua kumtuafutia mpinzani wa nje bondia wake kwa lengo la kumpandisha kiwango ili aweze kucheza mapambano makubwa duniani.
Alisema kuwa ameamua kuondokana na kuwaandalia mabondia wake mapambano dhidi ya mabondia wa hapa hapa kwani hawapati uzoefu wa kimataifa.
Kwa upande wake, Cheka alisema kuwa amejiandaa vyema kwa  pambano hilo na anataka kuonyesh ubora wake katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
Cheka alisema kuwa anatarajia kushinda katika pambano hilo ili kuendeleza rekodi yake katika  ngumi za kulipwa.
“Moliyati ni bondia mzuri na najua atanipa upinzani mkali, lakini sitakubali kupoteza katika ardhi ya Tanzania, nimejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano hilo,” alisema.
Mbali ya mapambano hayo, leo pia kutakuwa na ‘mawe’ ya aina yake katika mapambano ya utangulizi.
Bondia nyota, Japhet Kaseba atawania ubingwa wa Taifa wa TPBC Limited dhidi ya bondia nyota kutoka Zanzibar, Amour Mzungu katika pambano la uzito wa juu,  Pia Alphonce Mchumiatumbo atazipiga na bondia Mussa Ajibu kutoka Malawi katika pambano la uzito wa juu kabla ya Ashraf Suleiman kuonyeshana kazi na Aliki Gogodo wa Malawi katika pambano la uzito wa juu pia.
Pambano lingine la ubingwa litakuwa kati ya bondia Shabani Kaoneka dhidi ya Zumba Kukwe la uzito wa middle raundi 10 ambapo Yonas Segu atazichapa na bondia wa Malawi, Wilson Masamba katika pambano la uzito wa Light-Welter la raundi nane.
Mabondia wa kike, LuluKayage atazichapa na Enelesi Nkwanthi katika pambano la uzito wa bantam la raundi sita.

“Serikali haitamvumilia mtumishi wa afya anayefanya kazi bila kuzingatia weledi na maadili ya kazi yake”

AF1 
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi, akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi unaofanyika Mkutano wa Pili wa Neuroradiolojia  jijini Dar es Salaam, unaojadili Jukumu la Neuroradiolojia katika kukapambana na Magonjwa Yasiyoambukiza.
AF2 
Msajili Mstaafu wa Baraza la Wataalamu wa Radiolojia (MRIPC) Euniace Bandio, akizungumza kuwakaribisha Wataalamu na Washiriki wa Mkutano wa Pili wa Neuroradiolojia unaofanyika jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku mbili unajadili Jukumu la Neuroradiolojia katika kukapambana na Magonjwa Yasiyoambukiza.
AF3 
Katibu wa Jukwaa la Neuro-rad Dkt. Mboka Jacob akizungumza na washiriki wa mkutano wa Pili wa Neuroradiolojia  unaofanyika jijini Dar es Salaam.
AF4 
Baadhi ya watalaamu wa Radiolojia na washiriiki wa mkutano huo wakimsikiliza mgeni rasmi.
……………………………………………………………………………………………………………………………………….
Hussein Makame-MAELEZO
SERIKALI imesema haitamvumilia mtumishi yeyote wa sekta ya afya atakayefanya kazi zake bila kuzingatia weledi na maadili ya taaluma za sekta hiyo.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi, wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Neuroradiolojia  ulioanza jijini Dar es Salaam leo, kujadli Jukumu la Neuroradiolojia katika kukapambana na Magonjwa Yasiyoambukiza.
Prof. Kambi alisema ametoa msimamo huo kutokana na ukweli kwamba wataalamu wa sekta hiyo wanashughulikia afya ya binadamu kwa hiyo ni lazima wafanye kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili.
“Mtu yeyote ambaye ni mtumishi katika sekta ya afya ni lazima afanye kazi zake kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma, hivyo ndivyo taaluma zetu kwenye sekta ya afya zinavyotaka” alisema Prof. Kambi na kuongeza kuwa:
“Kwa hiyo mtu ambaye hatafuata weledi na maadili sisi kama Serikali hatutaweza kumvumilia kwa sababu tunashughulikia afya ya binadamu kwa hiyo ni lazima kazi hizi tuzifanye kwa kuzingatia weledi na maadili”
Kuhusu mkutano huo, Mganga Mkuu huyo wa Serikali, aliwaomba washiriki wa mkutano huo kuangalia na kujadili changamoto mbalimbali za taaluma ya Neuroradiolojia ili waisaidie Serikali kupata mawazo na ushauri wa jinsi ya kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.
Akizungumzia vifaa muhimu katika hospitali za Kanda nchini, Prof. Kambi alisema Serikali inafanya jitihada za kuhakikisha hospitali zote za Kanda angalau zihakikishe zinapata vifaa vya Ultrasound, CT Scan na MRI ambazo ni muhimu katika kutoa huduma za afya.
Aliongeza kuwa hali si mbaya katika vituo vya afya kuhusu masuala ya vipimo kwa sababu hospitali nyingi za Serikali zina vipimo vikubwa muhimu kwa utoaji wa huduma ya afya kwenye hospitali hizo.
“Kwa mfano kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tuna Ultrasound, tuna CT Scan,  tuna MRI.Ukienda hospitali ya Bugando baadhi ya vipimo vipo vingine havipo, ukienda kwenye Hospitali ya Kanda ya Mbeya nako kuna baadhi vipo na vingine havipo” alisema na kufafanua kuwa:
“Lakini sisi kama Serikali tunafanya jitihada za kuhakikisha hospitali zote za Kanda angalau zihakikishe zinapata vifaa vyote  hivi ambavyo ni muhimu katika kutoa huduma za afya”.
 Kwa upande wake Mkufunzi Muandamizi wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili na Mwenyekiti wa Baraza la Walaamu wa Radiolojia Nchini (MRIPC) Dkt. Ramadhani Kazema alisema jukumu la baraza hilo ni kuangalia kama wataalum wa Radiolojia wanakidhi mahitaji katika mafunzo na wanafanya kazi zao kwa weledi.
“Changamoto zinazoikabili tasnia hii katika nchi hasa za Afrika ni uhaba wa fedha na kuna jitihada zimefanywa ili kuboresha upatikanaji wa fedha kama unavyojua bajeti za hospitali ni kidogo ziko finyu kwa hiyo inakua na athari kwenye utendaji wetu wa kazi” alisema Dkt. Kazema.
Alifafanua kuwa pamoja na wataalamu wa Radiolojia kuwa si wa kutosha lakini wanaridhisha na vitendea kazi vipo vinaridhisha ,ingawa changamoto ni jinsi ya kuvifanya vitendea kazi hivyo viendelee kufanya kazi kwa muda wote.
Mkutano huo wa siku mbili wa Wataalamu wa Nuerolojia unajadili Mada kuu inayosema “Jukumu la Neuroradiolojia katika kukabialiana na Magonjwa Yasiyoambukiza na kushirikisha wataalamu kutoka Kenya, Marekani, Uganda, Korea Kusini, Uingereza na Tanzania.
Hata hivyo, mkutano huo pia unatarajia kushirikisha wataalamu hao kubadilishana uzoefu na utaalaamu katika masuala ya Neuroradiolojia na kujadili masuala ya ugonjwa ya kansa ya matiti.

KUAHIRISHWA KWA USAILI WA NAFASI ZA KAZI KWA TANGAZO LILILOTOLEWA TAREHE 1 JUNI, 2016

logo 
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Tanzania Metrological Agency (TMA), Tanzania Meat Board (TMB), The Local Government Training Institute (LGTI) na Registration, Insolvency And Trusteeship Agency (RITA) alitoa tangazo katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira la kuita kwenye usaili tarehe 1 Juni, 2016 waombaji wa kazi waliowasilisha maombi na kukidhi vigezo kwa taasisi zilizoanishwa hapo juu.
Kupitia tangazo hili Waombaji kazi wote waliotangaziwa kuitwa kwenye usaili kwa tangazo hilo wanafahamishwa kuwa usaili huo umeahirishwa mpaka watakapotangaziwa tena hapo baadaye.  
Kwa Matangazo ya nafasi za kazi yaliyotolewa mnamo tarehe 6 Mei, 2016, 11 Mei, 2016, 18 Mei, 2016 na tarehe 26 Mei, 2016 nayo waombaji kazi watakaokidhi vigezo watataarifiwa hapo baadae kuhusu mchakato wake unavyoendelea.
Aidha, Kupitia tangazo hili, Sekretarieti ya Ajira kwa niaba ya Serikali inaomba radhi waombaji kazi wote waliowasilisha maombi na wale waliokuwa wamejiandaa kuhudhuria usaili huo kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na
X.M. DAUDI
KATIBU
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma.

Mama Janeth Magufuli aahidi kuendelea kusaidia Jamii ya Wazee na walemavu nchini.

JEN1 
Wananchi wa Kijiji cha Nandagwa Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wakimlaki Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa kwa ajili ya Kambi ya Wazee ya Nandanga iliyopo katika kijiji hicho.
JEN2 
Mratibu wa kambi ya Kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga Bw. Agnerus Chiamba akimpa maelezo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kuhusu nyumba za malazi katika kambi hiyo, aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa.
JEN4 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akifungua kitambaa kwenye jiwe la msingi cha zahanati ya kijiji cha Nandanga itakayorahisisha upatikanaji wa huduma ya afya kwa wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
JEN5 
Baadhi ya Vitu vilivyotolewa kwa ajili msaada katika kambi ya kulea Wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga.
JEN6 
Mratibu wa kambi ya Kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Nandangwa Bw. Agnerus Chiamba akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli taarifa ya kambi ya Kulea Wazee ya Nandanga
JEN7 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla ya utoaji misaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
JEN8 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mama Mary Majaliwa Wakicheza Ngoma na kikundi cha Vijana wakati wa hafla ya utoaji misaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
JEN9 
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mama Mary Majaliwa akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nandanga na kumshukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kwa kutoa msaada katika kambi ya Wazee na watu wenye ulemavu iliyopo katika kijiji hicho.
JEN10 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli(kushoto) akikabidhi misaada kwa wawakilishi wa kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mama Mary Majaliwa.
JEN11 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi na kuahidi kuendelea kusaidia kambi hizo za wazee na watu wenye ulemavu wa ukoma ambapo mpaka sasa meshatoa msaada katika kambi 4 katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Lindi na Mtwara yenye thamani ya Takribani shilingi 250.
JEN12 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi kutoka wawakilishi wa kijiji cha Nandanga kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi

JEN13

JEN14 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiagana na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi baada ya kutoa msaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo eneo hilo.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

No comments :

Post a Comment