Wednesday, June 1, 2016

TBL Group yaibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya mzalishaji bora wa mwaka 2015

TBL1 
Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli akikabidhi tuzo  kwa mshindi  wa kwanza wa Tuzo ya Rais ya mzalishaji bora wa mwaka 2015, kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin  wakati wa hafla ya kutoa  tuzo kwa washindi iliyofanyika jijini katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam . Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia)  na kushoto ni Waziri wa Biashara ,Viwanda na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
TBL2Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
TBL3Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
TBL4 
Rais John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na watendaji wa makampuni ambayo yameshinda tuzo mbalimbali katika kipindi cha mwaka huu
TBL5Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (wa nne mstari wa mbele kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa kampuni hiyo waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo.
…………………………………………………………………………………………………………………
Kampuni ya  TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo  imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es salaam katika  hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla  hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni  kwa kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.
Kampuni ya  TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo  imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es salaam katika  hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla  hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni  kwa kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.

 TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO VYA HABARI

msangi_New1SACP: AHMED MSANGI
…………………….
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU [3] WANAOJIHUSIHA NA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI NA WENGINE [7] WANAOTUHUMIWA KULETA FUJO.
KWAMBA MNAMO TAREHE 30.05.2016 MAJIRA YA SAA 14:00hrs KATIKA MAENEO YA MIHAMA – MNARANI KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA RAYMOND MONGESA MIAKA 18 MKAZI WA MNARANI AKIWA NA MISOKOTO 30 PAMOJA NA KILO 10 ZA BHANGI, NA MWENZAKE DIONIZI ELIAS MIAKA 27 MIHAMA AKIWA NA MSOKOTO 01 WA BHANGI KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA ZA NCHI.
AIDHA BAADA YA KUWAKAMATA WATUHUMIWA HAO ASKARI WALIENDELEA NA DORIA PAMOJA NA MISAKO YA KUWASAKA WAHALIFU AMBAPO NASIBU ABDUL NA WENZAKE 07 WALIKAMATWA WAKIFANYA FUJO NA KUBUGUDHI ABIRIA KATIKA  MAENEO YA MECCO STAND, PAMOJA NA  MATHIAS MSUKUMA MIAKA  30 MKAZI WA NYAKATO SOKONI ALIEKAMATWA NA MISOKOTO  20 YA BHANGI.
WATUHUMIWA WOTE WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI DHIDI YA UHALIFU WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA BHANGI ILI KUWEZA KUKAMATA WAHUSIKA WENGINE ZAIDI WANAOSHIRIKIANANAO KATIKA BIASHARA HIYO, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YANAYOWAKABILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HASWA VIJANA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA KAMA BHANGI NA ZINGINE  KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA ZA NCHI, KWANI JESHI LA POLISI TUMEJIPANGA KUHAKIKISHA TUNAKAMATA WAHALIFU WA  AINA KAMA HIYO  KATIKA SEHEMU ZOTE ZA MKOA WA MWANZA, HIVYO TUNAOMBA WANANCHI WATUPE USHIRIKIANO WA KWA KUTUPA TAARIFA MAPEMA ZA UHALIFU NA WAHALIFU ILI TUWEZE KUWAKAMATA NA KUWAFIKISHA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMESAINIWA NA
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

RAIS UHURU KENYATTA AKUTANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU RAILA ODINGA KATIKA IKULU YA NAIROBI

UH1
Rais wa Jahuri ya Kenya Mh. Uhuru Kenyatta akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mh Raila Odinga wakati alipomkaribisha Ikulu kwa Chakula cha Mchana na Mazungumzo katika Ikulu ya Nairobi kwa mwaliko wa Ikulu ambapo viongozi wa Chama cha CORD walialikwa kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za siku ya Mdaraka (Madaraka Day)inayotarajiwa kufanyika kesho  mjini Nakuru nchini humo, Kulia ni Makamu wa Rais wa Kenya Mh. William Ruto na Kushoto ni Gavana Mosess Watangula.
UH2 
Rais wa Jahuri ya Kenya Mh. Uhuru Kenyatta kulia akiongozana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mh Raila Odinga wakati Waziri Mkuu huyo mstaafu alipoalikwa katika Ikulu ya Nairobi kwa chakula cha mchana na maadhimisho ya Madaraka Day yanayotarajiwa kufanyika Kesho mjini Nakuru, Kushoto ni Gavana Mosess Watangula.
UH3 
Rais wa Jahuri ya Kenya Mh. Uhuru Kenyatta akipozi kwa picha na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mh Raila Odinga wakati Waziri Mkuu huyo mstaafu alipoalikwa katika Ikulu ya Nairobi kwa chakula cha mchana na maadhimisho ya Madaraka (Madaraka Day) yanayotarajiwa kufanyika Kesho mjini Nakuru,  kulia ni Makamu wa Rais wa Kenya Mh. William Ruto na Kushoto ni Gavana MOsess Watangula.

UCHAGUZI YANGA, MWISHO WA KUCHUKUA, KUREJESHA FOMU JUNI 6

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Klabu ya Young Africans imeridhishwa na mwenendo wa wanachama kwa namna wanavyochukua na kurejesha fomu.
Katika kikao chake cha kufanya tathmini kilichoketi jioni ya leo Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Msomi Alloyce Komba kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu mpaka Jumatatu Juni 6, 2016 saa 10:00 jioni. Isipokuwa Jumamosi na Jumapili ya Juni 4 na 5, 2016.
Hadi sasa wanachama tisa (9) wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.
Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar ambao wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.
Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz
Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji. Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni tarehe 6 Juni, 2016. 

TANZANIA ELECTED CHAIR OF THE AFRICAN GEOLOGICAL BODY

AM1 
The Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia H.E. Naimi Hamza Aziz Delivers her speech during the opening session of the African Minerals and Geosciences Centre(AMGC) 36th Annual Meeting hels at United Nations Economic Commission for Africa(UNECA), Conference Centre in Addis Ababa Ethiopia
AM2 
From Freddy Maro
Tanzania Embassy Addis Ababa Ethiopia.
May,31,2016.
Tanzania has been elected a Chair of the Governing Council of African Minerals and Geosciences Center (AMGC) during its 36th annual meeting held at United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) conference Centre in Addis Ababa, Ethiopia over the weekend.
Tanzania was represented by The Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia H.E. Naimi Hamza Aziz who read the Member country’s statement on behalf of Minister for Minerals and Energy Prof. Sospeter Muhongo.
In her speech, ambassador Naimi urged Member States to consider the development of other strategic minerals such as graphite; lithium and Rare Earth Elements (REEs) which she said were not only economically viable but also important.
“The mining sector is seriously affected by the drop of mineral prices in the global market especially for precious and base metals which are mostly mined by our countries. The decline of mineral price has resulted to low exploration activities to Member States especially my country, which has led to the decline of income to the centre (AMGC),” she said.
The Tanzania Permanent Rep. further advised the African Minerals and Geo-Sciences Center(AMGC) to be more creative and diversify its economic activities for its future and sustainability.
In order for Member States to catch up with fast growing technologies, the Ambassador said it was high time for AMGC to invest in Research and Development (R&D), in which the findings would be shared with Member States for optimal utilization of mineral rich resources found in the continent.
 She said that Member States should endeavor to make AMGC a truly Pan African Center of Excellence and to achieve this more needs be done in terms of marketing, which would increase the center’s visibility and capability and promote the tremendous work it does.
“It is therefore crucial that Member States pay their respective annual contributions to the center, in order to allow it to operate more efficiently and effectively and successfully implement its programs and activities,” She emphasized.
Ambassador Naimi said Tanzania was very proud to host the AMGC and stands committed to continue to honor and fulfill its obligation which aims inter alia, to facilitate and ensure that the center fulfills its mission and mandate to serve all African countries.     
In his opening speech the outgoing AMGC chairman who is also The Ethiopian Minister of Mines, Petroleum and Natural Gas H.E. Tolesa Shagi said Ethiopia and many African countries were adopting effective mineral management policies and strategies for the exploitation of mineral resources which were vital in boosting economic growth.
“The Mining sector in Ethiopia is providing support for the development of small and medium scale and artisanal mining enterprises and encourage greater participation of women in mining activities as a strategy for enhancing the development impact of mineral resources,” he said.
The Minister highlighted challenges facing mining industry in Ethiopia and Africa in general including shortage of capacity in negotiating, administering and monitoring the mining contracts as well as lack of sufficient geo-science information.
He said for African countries to overcome the challenges facing the mining industry they should opt for coordinated efforts as envisaged in the Africa Mining Vision (AMV) that was adopted by African Heads of States in February 2009, the long term goal of the vision is to create a Transparent Equitable and optimal exploitation of mineral resources to underpin broad-based sustainable growth and socio-economic development.
Speaking during the same occasion, the Deputy Executive Secretary and Chief Economist of ECA said that the Economic Commission for Africa(ECA) was acutely aware of the strategic importance of the AMGC as a partner to African Countries to collectively implement a transformative agenda for mineral resources development which would be instrumental for sustainable development.
African Minerals and Geosciences Centre (AMGC) formerly known as the Southern and Eastern African Mineral Centre (SEAMIC) started as a sub-regional development Centre for Eastern and Southern African nations namely, Angola, Comoros, Ethiopia, Mozambique, Tanzania and Uganda.
The Centre is located in Kunduchi Dar es Salaam Region, Tanzania.

TRA KUGAWA MASHINE ZA EFD BILA MALIPO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO MKOA WA DAR ES SALAAM

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alfayo Kidata

NHIF YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WAKAZI WA JIJI LA TANGA KWENYE MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA.

MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOAN TANGA(NHIF) ALLY MWAKABABU AKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MWANANCHI ,BURHUANI YAKUB MWENYE TISHETI YA BLUU ALIYEKATA UFFANUZI KUHUSU HUDUMA ZAO.

KUSHOTO NI AFISA MATEKELEZO WA NHIF MKOA WA TANGA,MIRAJI KISILE AKIMUHUDUMIA MKAZI WA JIJI LA TANGA ALIPOTEMBELEA BANDA LAO LILILOPO KWENYE MAONYESHO YA PILI YA KIMATAIFA YA BIASHARA YANAYOFANYIKA ENEO LA MWAHAKO JIJINI TANGA.

AFISA UHAMASISHAJI WANACHAMA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA(NHIF) VISTUS TILUSASILA KUSHOTO AKITOA ELIMU KUHUSU MFUKO HUO KWA MKAZI WA JIJI LA TANGA.
MWENYEKITI WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI TANGA,HASSANI HASHIM AKIMULIZA JAMBO MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA(NHIF) ALLY MWAKABABU WAKATI ALIPOTEMBELEA BANDA LAO KUPIMA SUKARI NA PRESHA.
MENEJA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA(NHIF) ALLY MWAKABABU WA PILI KILIA AKIPIMWA NA NESI WAKATI WA MAONYESHO YA PILI YA KIMATAIFA YA BIASHARA YANAOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA MWAKIDILA JIJINI TANGA.

UPIMAJI WA WANANCHI UKIENDELEA KWENYE BANDA LA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA


Picha kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHA 33 CHA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge
leo kusikiliza Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mbunge wa
Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi akichangia kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Mawaziri wakifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wa mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa leo mjini Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvu akizungumza na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mh. Peter Msigwa mara baada ya kikao cha bunge kuahirishwa mchana leo, Kushoto anayecheka  ni Mh. Balozi Augustino Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.

WAAMUZI WA TAIFA STARS V MISRI

Waamuzi wanne kutoka Gabon, ndio watakochezesha mchezo wa kimataifa kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mapharao wa Misri utakaofanyika Jumamosi Juni 4, 2016 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni ni wa kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Gabon ambako mwamuzi wa kati atakuwa ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric.
Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia kesho Juni mosi, 2016 ambako wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.
Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei 30,2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Serikali kuanzisha benki ya maendeleo ya viwanda nchini.

MS2 
Na Lilian Lundo-MAELEZO
Serikali ya awamu ta Tano imedhamiria kuifanya sekta ya Viwanda nchini kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 7.3 ya sasa
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema kuwa jambo hilo linawezekana hasa kwa kuzingatia nchi yetu ina rasilimali zinazohitajika katika kujenga uchumi wa viwanda.
“Nafahamu kwamba tunakila aina ya rasilimali inayowezesha uwepo wa viwanda hapa nchini ikiwemo umeme wa kutosha pamoja na malighafi zake na kwa maana hiyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuifanya sekta ya viwanda kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka 7.3 ya sasa”. Alisema Rais Magufuli.
Aidha Dkt. Magufuli aliwatoa wasiwasi wadau hao kuhusu uwepo wa soko la uhakika kwa bidhaa zitakazozalishwa kwani Tanzania imezungukwa na nchi zenye uhitaji wa bidhaa mbalimbali na pia ni Mwanachama wa jumuiya mbalimbali ndani na nje ya Afrika.
Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage aliwataka wamiliki wa Viwanda Nchini kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.

UZINDUZI WA MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOANI MARA

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ally Maftah akizindua mradi wa Uboreshaji wa mifumo ya sekta za Umma (PS3 Mkoani Mara leo. Maftah alizindua mradi huo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo. PS3 inatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania Bara kupitia Halamshauri 97 chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Mwakilishi wa  Mkurugenzi wa Mradi wa PS3, Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula akizungumza ambapo alisema kuwa PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha
mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. 
 Kaimu Katiobu Tawala Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akizungumza.
 Baadhi ya washiriki ambao ni Wakurugenzi na watendaji wengine kutoka Mara wakifuatilia uzinduzi huo.
Mtaalam kutoka TMA, Paul Chikira ambae ni mmoja wa wawezeshaji akifuatilia tukio hilo la uzinduzi wa mradi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
 
Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Felix Lyniva akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi
 Washiriki wakipitia nyaraka wakati wa uwasilishaji mada.
 Mtaalam wa masuala ya Rasilimali watu kutoka Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Remmy Moshi akiwasilisha mada.
 Mtaalam wa Mawasiliano na Takwimu wa Mradi wa PS3, Desideri Wengaa akitoa mada juu ya mawasiliano na utoaji takwimu sahihi.
 Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
 Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.

MKE WA RAIS MAMA JANETH AWATAKA WATANZANIA KUWASAIDIA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU.

mae1 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkaribisha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam. Mama Majaliwa alifika Ofisini hapo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na mke wa Rais.
mae2 
Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Magogoni jijini Dar es Salaam.
MAE3 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimuonesha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa mafuta maalumu yanayotumiwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino ambayo atayagawa hivi karibuni kwa baadhi  walemavu wa ngozi katika maeneo mbalimbali nchini.  Pia Mke wa Rais mama Janeth amewaomba watanzania kuwajali Wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi. PICHA NA IKULU

LUHWAVI AKAGUA JENGO LA MIKUTANO LA CCM DODOMA LEO

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi (wapili kushoto) akikagua jengo la Mikutano la CCM, Dodoma Convetion Centre leo ikiwa ni maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai mwaka huu katika ukumbi huo. Kushoto ni  Ofisa Miliki wa Jengo hilo Tegemeo Saambili 
Luhwavi akitazama hali ya maua kwenye bustani za jengo la ukumbi huo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Tegemeo Saambili (kushoto), alipokagua jengo hilo leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akihoji kuhusu hali ya bustani zinazozunguka jengo hilo
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi hali ya maua kwenye bustani za jengo hilo, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi hali ya maua kwenye bustani za jengo hilo, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi hali ya maua kwenye bustani za jengo hilo, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.
Luhwavi akielekeza namna ya kuboreshwa bustani zinazozunguka jengo la ukumbi huo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akizunguka jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Cetre, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu
Luhwavi akiingia ndai ya ukumbi wa jengo hilo kuona hali halisi
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison (kushoto), akimpa maelezo kuhusu hali ya ndani ya jengo hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipolikagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison (kushoto), akionyesha baadhi ya viti ambayo hutumiwa na wajumbe, katika ukumbi huo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (hayupo katika picha), alipolikagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.  Mkuu wa Idara ya Usalama na Maadili Makao Makuu ya CCM, Masudi Mbengula
Bendera ya Taifa na bendera ya CCM zikipepea kwenye jengo hilo la Mikutano la CCM, kama ilivyo kawaida. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Katibu Mkuu Wizara ya Afya azindua Baraza la Wafanyakazi Muhimbili

MP1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo  Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu wa baraza hilo, Dk Kissa Mwambene. Kushoto ni Mwenyekiti wa baraza hilo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)
MP2 
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakipiga makofi wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo  Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya wakizungumza na wajumbe wa baraza hilo Leo kwenye hospitali hiyo.
MP3 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi LEO kabla ya kupiga kura za kuwachagua viongozi wapya wa baraza hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani wa hospitali hiyo.
MP4 
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la MNH wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru katika kikao hicho.
MP5 
Wajumbe wakipiga kura LEO za kuwachagua viongozi wapya wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali hiyo.
MP6 
Dk Kissa Mwambene akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua Leo kuwa Katibu wa baraza hilo.
MP7 
Wakili Eneza Msuya akiwashukuru LEO wajumbe baada ya kumchagua kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.
MP9 
Kutoka kushoto ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo, Dk Kissa Mwambene, Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Lawrence Museru, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu Msaidizi wa baraza hilo, Wakili Eneza Msuya na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.
………………………………………………………………………………………………….
Katibu   Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.  Mpoki   Ulisubisya  ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili  kwa kuboresha maslahi ya watumishi wake  na kuendelea kuweka miundombinu bora ya kiutendaji.
Akizindua Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  Dk. Ulisubisya amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa kwani inampa motisha mtumishi kufanya kazi kwa bidii.
 
 “Nimefarijika sana  kuoana suala la maslahi ya watumishi linapewa kipaumbele hapa MNH kwa kweli mnastahili pongezi na taasisi nyingine hazina budi kuiga mfano huu,  lakini  napenda kusisitiza kuwa kila mtumishi  ni vema akanufaika na maboresho haya amesema,”  Dk Ulisubisya.
Akizungumza kabla ya uzinduzi wa baraza hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema hivi sasa hospitali hiyo imeongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 2 hadi kufikia Bilioni 4.
Pia amesema katika kuendelea kuboresha huduma za matibabu MNH ina mpango wa kuongeza ICU   ya watoto wadogo pamoja na ICU ya kina mama wenye matatizo ya uzazi ili kuokoa maisha ya mama na mtoto .
Kwa mujibu wa Profesa Museru Hospitali hiyo ipo katika hatua za mwisho za kupata mkopo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkopo ambao utasaidia kupanua  huduma  za afya ikiwamo kununua vifaa tiba vya upasuaji.
Katika kikao, wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wamemchagua Dk. Kissa Mwambene kuwa Katibu wa Baraza hilo pamoja na Eneza Msuya kuwa Katibu Msaidizi.

Serikali kuanzisha benki ya maendeleo ya viwanda nchini

MS 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda  PMAYA The President’s Manufacure of the Year  pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU / HASSAN SILAYO-MAELEZO
MS2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
MS3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
MS4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wadau wa Viwanda nchi mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
WAF1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda ya bidhaa zinazotoka viwandani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF4 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiongea na wadau wa sekta ya Viwanda wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 na kuwataka kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.
WAF5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo ya shirikisho la viwanda nchini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga na wa pili ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe.
WAF6 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wadau wa sekta ya viwanda nchini(hawapo pichani) na kuwaahidi kuwaunga mkono katika harakati za kuendeleza sekta ya viwanda ikiwamo kuanzisha banki ya maendeleo ya viwanda nchini itakayosaidia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wale wenye nia ya kuanzisha viwanda.
WAF7 
Wadau wa Sekta ya Viwanda nchini wakimsilkiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.

Zanzibar yaadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani

index 
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt. Ghirmany akitoa taarifa ya Shirika hilo kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.
………………………………………………………………………………………………….
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Inakadiriwa zaidi ya watu milioni sita duniani kote hupoteza maisha kila mwaka kutokana na athari za matumizi ya tumbaku na wanaoathirika zaidi ni vijana wenye umri wa miaka 30 hadi 39.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Wizara ya Afya kwenye maadhimisho ya siku ya kupinga  matumizi ya tumbaku Duniani, Meneja wa Kitengo  cha maradhi yasiyoambukiza Zanzibar ndugu Omar Mwalimu Omar amesema mbali na kusababisha vifo, matumizi ya tumbaku yamekuwa chanzo kikubwa cha maradhi.
Amesema tafiti zilizofanyika zimeonyesha kuwa matumizi ya tumbaku yanachangia kwa asilimia 71 kupata saratani ya mapafu, asilimia 42 magonjwa ya njia za hewa na asilimia kumi magonjwa ya moyo.
Ndugu Omar amesema pamoja na kuwa Zanzibar haizalishi tumbaku na haina viwanda vya sigara, bado matumizi ya bidhaa hizo ni ya kiwango cha juu.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya mwaka 2011ulionyesha asilimia 7.3 ya wazanzibari kati ya miaka 25 hadi 64 ni watumiaji wa sigara na asilimia 4.1 wanatumia tumbaku kwa njia za kunusa na kuvuwata.
Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza amezitaja athari nyengine zinazotokana na matumizi ya tumbaku ni kuanguka kwa uchumi wa nchi.
“Kama nilivyotangulia kusema, rika linaloathirika zaidi ni vijana wa miaka 30 hadi 39 ni wazi kuwa nchi zinapoteza nguvu kazi ambayo ipo katika umri wa kuongeza kipato cha nchi,” alisisitiza Ndugu Omar.
Amekiri kuwa katika vita vya kupambana na matumizi ya tumbaku kumejitokeza changamoto ya viwanda vinavyotengeneza bidhaa za tumbaku kuwa na nguvu kubwa ya kifedha na matumizi ya tumbaku imekuwa moja kati ya starehe hususan katika jamii ya vijana.
Amewataka waandishi wa habari kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Wizara ya Afya ya kudhibiti  matumizi ya tumbaku kwa kuitanabahisha jamii juu ya athari zinazotokana na tumbaku.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) aliepo Zanzibar Dkt. Ghirmany amesema Umoja wa Mataifa umepanga kila ifikapo tarehe 31 Mei ya kila mwaka iwe ni siku ya kupinga matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku ili kuitanabahisha jamii juu ya athari inayotokana na tumbaku.
Ameishauri Serikali kuandaa kanuni ya matumizi ya tumbaku ili sheria iliyotungwa ya kudhibiti uvutaji wa sigara katika maeneo ya wazi iweze kufanya kazi.
Ujumbe wa mwaka huu katika kuadhimisha siku ya kupinga  matumizi ya tumbaku Duniani ni ‘kuwa tayari kuondosha  vivutio katika paketi za kuhifadhia sigara’.

SERIKALI ITAHAKIKISHA INAENDELEA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI IKIWEMO URITHI WA DUNIA

 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa
…………………………………………………………………………………………….. 
Woinde shizza,Arusha

SERIKALI ya awamu ya tano  imesema kuwa itaendeleza jitihada za
kutunza na kulinda urithi wa dunia ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi
wanaoishi maeneo ya uhifadhi ili watanzania wote waweze kunufaikana
rasilimali za nchi .



Hayo yalisemwa na  waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua
mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo
endelevu unaoendelea jijini Arusha


Majaliwa alisema kuwa rasilimali zilizopo ni za watanzania na ili
kuhakikisha kuwa wananufaika nazo serikali itahakikisha  inatunza na
kulinda uhifadhi ili yawe endelevu na  kusaidia vizazi vijavyo.


Alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi tajiri yenye urithi na hivyo ili
kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika haswa waishio maeneo ya uhifadhi
serikali itatoa elimu ya kutosha ili waepuke kuchangia uharibifu wa mazingira
unaotokea kwenye hifadhi za taifa .

“Rasilimali hizi ni zetu na hivyo hata wanaoishi maeneo ya hifadhi
watusaidie kwa wale wanaoingilia na kuharibu  kwani hata hizo mali
asili zinatusaidia sote na ndiyo sababu  tumewekea mikakati ya kutunza maeneo
hayo ili yawe endelevu’alisema


Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara
ya Mali asili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi Alisema kuwa
madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo
yanatishia  na kuathiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia
katika afrika .


Aidha mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kupitia upya shughuli
zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa
miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.


Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi
wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi
wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku
inayotokea kwenye maeneo ya urithi wa dunia  kutokana na makundi ya
kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.


Aliongeza kuwa pia  mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO  ya
mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa
uridhi wa dunia.


“mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia utakuwa na
manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa bali
pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageni watakao
huthudhuria  mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na
kujenga mitaji wa kijamii”alisema Malinzi


Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa
na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote
za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa
ya Ngorongoro

SERIKALI YAITAKA RITA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU UMUHIMU KUANDIKA WOSIA WA MIRATHI

index 
Na Mahmoud Ahmad Arusha.
SERIKALI imeitaka wakala wa usajili,Ufilisi na Udhamini, RITA, kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuelewa umuhimu wa kuandika wosia na mirathi ,ili kuondoa migogoro kwa familia wakati wa kugawa mirathi ya marehemu.
Rai hiyo imetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu, alipokuwa akifungua kampeni ya siku NNe ya kisheria inayotolewa bure na RITA, kuhusu kuandika mirathi na wosia na kuwaelekeza eneo salama la kuhifadhi wosia ukisha andikwa na mhusika   ili kuondoa migogoro mingi kwa familia pindi mhusika anapofariki dunia.
Mkuu huyo wa wilaya, alisema,wananchi wengi hawana elimu juu ya wosia na mirathi hivyo RITA, ambayo ni wakala wa  serikali ina jukumu kubwa la kuhakikisha elimu inawafikia wengi na hivyo kuwezesha wajane na watoto ambao ndio waathirika  kupata mirathi .
Alisema wosia unasaidia kutatua migogoro ambayo ingelijitokeza wakati wa kugawa mirathi ya marehemu na mtu kuandika wosia sio uchuro bali ni kuweka utaratibu wa mali za muhusika zitakavyogawiwa pindi akisha fariki dunia.
Aliikumbusha jamii kuwa msimamizi wa mirathi sio mrithi wa mali ya marehemu bali jukumuake ni kukusanya mali yote na madeni yote ya marehemu na kusimamia ugawaji na ulipaji wake na kamwe msimamizi yeyote asijihusishe na urithi .
Jamii nyingi zimekuwa zikiingia kwenye migogoro ya kugawana mirathi kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha ya kuandika wosia  kabla ya kifo na matokeo yake wanaoathirika ni wajane na watoto ambao hukosa haki yao .
Awali mratibu wa kampeni hiyo,msajili na wosia kutoka makao makuu ya RITA, Augostino Mbuya, alisema migogoro mingi imekuwa ikijitokeza kwenye familia wakati wa kugawa mirathi kutokana na kutokuwepo kwa wosia ambao ni mwongozo wa jinsi ya kuigawa mali ya marehemu kwa wahusika na matokeo yake watoto na wajane hukosa haki yao ya kurithi.
Alisema kutokana na hali hiyo RITA, ipo tayari kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma hiyo ya kuandika wosia kutokana na wananchi wengi kutokuwa na elimu na kufahamu wapi watapata huduma hiyo ya kuandika wosia na ugawaji wa  mirathi za marehemu
Mbuya,alisema mkakati uliopo ni kusogeza huduma ya kuandika wosia na mirathi ngazi za mikoa na wilaya pamoja na kuhakikisha wanakuwepo wanasheria wa kutosha lengo ni kuiwezesha jamii kuondokana na migogoro ambayo inaweza kuepukwa wakati wa kugawa mali za marehemu.
Alisema tangia kuanzishwa kwa huduma hiyo ya Rita, imeweza kusajili wosia zaidi ya 300 na 30 kati yake zimeshachukuliwakwa  utekelezaji .
Akisoma taarifa ya kazi za Rita, msajili wa mirathi na wosia, kutoka makao makuu ya Rita, Joseph Mwakatobe amesema mahakama kuu imeiteua RITA, kusimamia utatuzi wa migogoro  ya urithi na uandishi wa wosia lngo ni kuondoa migogoro inayojitokeza pindi mtu anaofariki dunia.
Alisema Rita, itaendesha kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi kuhusu kuandika mirathi na wosia katika mkoa wote wa Arusha,ili kuwezesha wajane na watoto wanapata haki yao ya kurithi mali za marehemu .
Aliongeza kuwa kuandka wosia ni swala lahiari ya mtu,na Rita, imekuwa ikikumbana na changamoto mbaimbali zkiwemo za kutokuwepo na wosia wakati wa mirathi .
Aliongeza kuwa mirathi inatolewa kulingana na sheria za dini ya kiislamu, mila na sheria ya India ya mwaka 1865 ambayo inahusisha makundi yote ambayo hayapo kwenye makundi ya kidini na mila.

WAZIRI WA AFYA MHE.UMMY MWALIMU ATOA TAMKO KUHUSU SIKU YA KUPINGA MATUMIZI YA TUMBAKU DUNIANI, TAREHE 31 MEI 2016

images 
Siku ya kupinga matumizi ya Tumbaku Duniani, huadhimishwa duniani kote kila mwaka tarehe 31 Mei.
Kaulimbiu  ya  Maadhimisho ya  Siku ya kupinga matumizi ya tumbaku mwaka 2016 ni “jiandae kwa pakiti zisizo na matangazo wala vivutio”
Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha jamii juu ya kujiepusha au kujikinga na vivutio mbalimbali vya matangazo yanayo hamasisha matumizi ya sigara ambayo ina madhara mengi kiafya.
Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani inaadhimisha siku hii, kwa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na kujikinga na matumizi ya sigara na bidhaa za tumbaku.
Tafiti nyingi zinathibitisha madhara yatokanayo na matumizi ya tumbaku ni pamoja na magonjwa yasiyoambukiza  kama vile saratani, magonjwa ya mishipa ya damu na moyo, kiharusi, magonjwa ya njia ya hewa.
Tafiti pia zinaonyesha takriban watu 6,000,000 hupoteza maisha duniani kwa mwaka kwa utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake.
 
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani kwa mwaka 2016, inalenga kuelimisha na kuhamasisha jamii kuachana na matumizi ya tumbaku na kusisitiza kwa wazalishaji kutokuweka maandishi au nembo zinazovutia ili kuishawishi jamii kutumia bidhaa hizo. Aidha tumbaku imekuwa ikisababisha madhara kiafya kama vile magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza. Magonjwa hayo ni magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, saratani, ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya njia ya hewa.
Mambo mengine yanayoongeza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na ulaji usiofaa hasa matumizi ya chumvi kupita kiasi, kutofanya mazoezi, unywaji pombe kupita kiasi na msongo wa mawazo.
Ili kuzuia maradhi yasiyoambukiza yatokanayo na matumizi ya tumbaku na bidhaa zake ni muhimu kufuata kanuni za afya ambazo ni kutovuta sigara na kama wewe ni mvutaji, kutovuta sigara hadharani maana madhara yake ni sawa hata kwa mtu asiyevuta ambaye anapata moshi kutoka kwa mvutaji, kuendelea kuielimisha jamii juu ya madhara mbalimbali yatokanayo na utumiaji wa tumbaku hususani kwa vijana.
Serikali inaendelea na mkakati wa tiba kwa watu wenye uraibu wa  matumizi ya tumbaku, ikiwa na lengo kupunguza matumizi hayo miongoni mwa jamii. Kuhakikisha pakiti za tumbaku na bidhaa zake ziwe na tahadhari ya madhara ya utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake. Aidha, serikali, inaendelea kurekebisha sheria, kanuni na taratibu za udhibiti wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatumia  maadhimisho   haya kuwa sehemu ya uhamasishaji kwa jamii kama ilivyo kwenye nchi zote duniani.

TANROADS yakanusha kudaiwa fidia

3 
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wamekanusha kudaiwa fidia na wananchi wa Kijiji cha Mazingira,Wilaya ya Handeni mkoani Tanga waliovunjiwa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja wa TANROADS Mhandisi Alfred Ndumbaro alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii juu ya malalamiko ya wananchi wa Kijiji hicho kuhusu kutolipwa fidia zao.
”Sheria iko wazi kuwa wanaojenga karibu na barabara wakivunjiwa hawalipwi fidia yoyote lakini wale ambao ujenzi wa barabara uliwafuata katika maeneo yao wana haki ya kulipwa fidia”, alisema Mhandisi Ndumbaro.
Mhandisi Ndumbaro ameongeza kuwa zoezi la malipo ya fidia kwa wanakijiji waliokuwa na uhalali wa malipo hayo lilishakwisha zamani kwa hiyo, wanaodai sasa ni wale ambao nyumba zao zilivunjwa kutokana na kujenga eneo la barabara.
Aidha, Mhandisi huyo ametoa rai kwa wananchi kufuata sheria za ardhi ili kupata uhalali wa viwanja vyao pamoja na kuepuka usumbufu na gharama za kuvunjiwa nyumba zao.
Nyumba hizo zilivunjwa ili kupisha ujenzi wa barabara ya lami yenye Kilomita 54 kutoka Mkata hadi Handeni iliyojengwa na Kampuni ya Synohydro Corporation Limited ya China.

ZIARA YA RAIS KUTEMBELA SEHEMU ZILIZOHARIBIWA NA WAPINZANI (CUF)

zi1Wanachama cha Mapinduzi CCM Tawi la Tibirinzi Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipotembelea tawi lao lililochomwa moto na Wapinzani kwa sababu za kisiasa kuona hali ya uharibifu uliotokea, [Picha na Ikulu.] 31/05/2016.
zi5 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimianana Sheha wa Shehia ya Maziwa Ngombe Bi,Asha Yussuf Hassan, aliyevunjiwa Nyumba yake na Wafuasi wa Chama cha CUF hivi karibuni kwa sababu za kisiasa pamoja na kukatiwa Migomba yeke wakati alipomtembelea leo kuangalia maafa hayo, [Picha na Ikulu.]31/05/2016.
zi6 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimianana Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Micheweni wakati alipomtembea Sheha wa Shehia ya Maziwa Ngombe Bi,Asha Yussuf Hassan, aliyevunjiwa Nyumba yake na Wafuasi wa Chama cha CUF hivi karibuni kwa sababu za kisiasa pamoja na kukatiwa Migomba yeke wakati alipomtembelea leo kuangalia maafa hayo, [Picha na Ikulu.]31/05/2016.
zi7 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo ya ushuhuda kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Maziwa Ngombe wilaya ya Micheweni Pemba, Bi,Asha Yussuf Hassan (katikati) aliyevunjiwa Nyumba yake na Wafuasi wa Chama cha CUF hivi karibuni kwa sababu za kisiasa pamoja na kukatiwa Migomba yeke wakati alipomtembelea leo kuangalia maafa hayo, [Picha na Ikulu.]31/05/2016.
zi8 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi Tawi la Tibirinzi Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba ambalo lilichomwa Moto na wapinzani  hivi karibuni,akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maeneo mbali mbali yaliyopata matukio ya kisiasa,[Picha na Ikulu.] 31/05/2016.
zi2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Shehia ya Maziwa Ngombe wilaya ya Micheweni Pemba leo wakati alipomtembelea Sheha wa Shehia hiyo Bi,Asha Yussuf Hassan (katikati) aliyevunjiwa Nyumba yake na Wafuasi wa Chamacha CUF hivi karibuni kwa sababu za kisiasa pamoja na kukata Migomba yeke, [Picha na Ikulu.]31/05/2016.
zi3 
Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe,Rasshid Hadid (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipofika Kijiji cha Shengejuu shehia ya Pembeni kutembelea ujenzi wa Nyumba ya Nd,Said Khamis Iliyobomolewa na Wafuasi wa Chama cha CUF kwasababu za Kisiasa,(kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe,Vuai Ali Vuai,[Picha na Ikulu.]31/05/2016.

No comments :

Post a Comment