Jiwe
la Msingi la Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi lililowekwa na
Rais Dk. John Magufuli. Kituo hicho kimefadhiliwa na Benki ya CRDB kwa
gharama ya zaidi ya shilingi milioni 300. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiteta jambo na
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Esther Kitoka.
Brass Band ya Polisi ikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza kwa
makini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akisalimia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (wa kili kulia) akifurahia
jambo na Naibu wake (kulia), IGP,Ernest Mangu, wapili kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisalimia na Rais John Magufuli.
THE SILOAM CHURCH LAWATIA BARAKA WAANDSHI WA HABARI KUBARIKI KAZI ZAO ZA KILA SIKU
Wakili
wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam, Elisha Eliya akiendesha sala
maalum ya kuuombea amani tanzania na pia kuwatia baraka Waandishi wa
habari, ambao walihudhuria kwenye ibada iliyoongozwa na kiongozi huyo wa
The Siloam, leo katika Kanisa hilo, Mbezi Beach, eneo la Makonde Dar es
Salaam..
Baadhi ya waumini na Waandishi wa habari wakiwa kweye ibada hiyo.
Waumini walifanya Ingagement ya ndoa wakitekeleza nadhiri hiyo wakati wa ibada hiyo
Waumini walifanya Ingagement ya ndoa wakitekeleza nadhiri hiyo wakati wa ibada hiyo
Waumini walifanya Ingagement ya ndoa wakitekeleza nadhiri hiyo wakati wa ibada hiyo
Waumini walifanya Ingagement ya ndoa wakitekeleza nadhiri hiyo wakati wa ibada hiyo
Waumini walifanya Ingagement ya ndoa wakitekeleza nadhiri hiyo wakati wa ibada hiyo
MTANZANIA ALIYEIBUKA MSHINDI WA KWANZA AFRIKA NA WA SITA DUNIANI KATIKA MASHINDANO YA KUSOMA QUR-AN KWA NJIA YA TAJ-WEED AWASILISHA TUNZO KWA MZEE MWINYI LEO
Mwanazuoni
kutoka Kondoa, Tanzania, Sheikh Rajay Ayub ambaye ameibuka mshindi wa
kwanza Afrika na wa sita Duniani katika mashindano ya 37 ya Kimataifa ya
usomaji Qur-an kwa njia ya Taj-weed, yaliyofanyika mwezi uliopita
nchini Iran akikabidhi tuzo zake kwa Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan
Mwinyi, wakati wa hafla ya kumpongeza iliyofanyika leo, kwenye Viwanja
vya Makao Makuu ya Baraza la Waislam Tanzania-BAKWATA, Kinondoni, Dar es
Salaam. Kulia ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Aboubakary Bin Zubeir
na Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa, Alhaj Omary
Kariati ambaye aliratibu hafla hiyo. KWA PICHA KEM-KEM ZA HAFLA HIYO>>BOFYA HAPA
MCHEZAJI BORA WA UMMISETA MUSA SAID KUONDOKA JUMATANO JUNI 28, 2016 KWENDA NCHINI UFARANSA
Meneja
Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, akizungumza na
waandishi wa habari kuwaelezea juu ya safari ya mchezaji Musa Said
anayetarajia kuondoka Jumatano ya Juni 28, 2016 kwenda nchini Ufaransa
kwenye kambi ya kimataifa ya Copa Coca-Cola. Pembeni ni Katibu Mkuu wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, Mchezaji Musa Said
Bakari na Mwalimu wake wa Kibasila.
Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
—
Na Devotha Kiwelo.
—
Na Devotha Kiwelo.
MCHEZAJI
bora wa mashindano ya UMMISETA yaliyofanyika mwaka jana mkoani Mwanza,
Said Musa Jumatano ya Juni 28, 2016 kuelekea Ufaransa katika kambi ya
Kimataifa ya Copa Coca – Cola ambayo imeandaliwa na kampuni ya kinywaji
cha Coca – Cola .
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT),
Mohamed Kiganja alisema udhamini wa kampuni ya Coca – Cola imetambua
umuhimu wa michezo hivyo kukubali kudhamini michezo kupitia shule za
sekondari ili kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi ambao wanamalengo
makubwa katika kuitumikia nchini yao kupitia michezo.
“Kwetu
sisi imekuwa faraja kwa kuibua kipaji kichanga ambacho kitakuwa ni
mfano wa kuigwa kama ilivyo kwa Samatta ambaye amekuwa kioo kwa jamii ya
wanamichezo na hivyo kuomba makampuni mengine kujitokeza kwa ajili ya
kusaidiana na Coca – Cola”, alisema.
Kiganja
alimtaka Musa kuzingatia nidhamu kipindi chote atakachokuwepo kwenye
kambi ili kujijengea heshima katika kukuza kipaji chake kwa kipindi
chote ambacho atakuwa chini ya walimu wageni ambao hajawahi kukutana nao
na hiyo italeta heshima nchini.
Kwa
upande wa Meneja msaidizi wa chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga,
alisema wamefurahi kupata nafasi ya kudhamini mashindano hayo kwa kuwa
ndiyo mara yao ya kwanza na imefanikiwa kufikia malengo ya kupata
mchezaji ambaye atakuwa muwakilishi wa Tanzania katika kambi ya
Kimataifa ya Copa Coca – Cola iliyopo jijini Paris nchini Ufaransa.
Alisema
Musa ataondoka kwa kupitia Nairobi kwa kuwa kozi inaanza kesho na
kumalizika Julai 4, hivyo aliwataka wanafunzi wengine kujituma ili
kufikia malengo kama aliyofikia Mussa.
“Sisi
kama kampuni imekuwa ni faraja kwani tutakuwa tumeitangaza nchini kwa
kupitia Mussa na hii itakuwa ni muendelezo katika michezo
inayoendelea,”alisema.
Mussa
ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Kibasila ambaye alizaliwa Agosti
11, 2000 huku akiwa ni mchezaji tegemeo katika timu ya shule na Mkoa wa
Temeke ambapo walitumia jina hilo kwa kupitia michezo.
Waziri Nape Nnauye azindua Studio ya Redio ya Jamii katika Chuo Kikuu Huria Tanzania.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa
ameongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof.
Elifas Bisanda kwenda kuzindua Studio ndani ya Chuo hicho 27 Juni, 2016
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akikata
utepe wakati wa Uzinduzi wa Redio ya Jamii ya ‘’Community Media Network
of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto)
akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa toka Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira
Rodrigues wakati wa Uzinduzi wa ‘’Community Media Network of Tanzania
(COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia)
akiwa ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania
(COMNET)’’ akijibu baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa Habari mara
baada ya kuizindua rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa
ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’
akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua
rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
……………………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amezindua studio ya redio ya jamii ya
‘Community Media Network of Tanzania’ (COMNET) katika Chuo kuku Huria(
OUT ) itakayotumika kusambaza habari maeneo yenye uhaba wa redio.
Uzinduzi huo umefanyika leo
jijini Dar es Salaam,ambapo Mhe. Waziri amesema kuwa studio hiyo
itasaidia idadi kubwa ya wanachi wanaoishi vijijini kupata habari
kutoka Serikalini na kutoa mrejesho wa kile watakachosikia kwa urahisi.
“Ni Studio muhimu kwa ajili ya
kusambaza demokrasia kwa watu hasa wale waliopo vijijini kwa vile redio
nyingi bado hazijawafikia”Alisema Mhe.Nape.
Aidha amewataka wanafunzi wa
taaluma ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma katika chuo
hicho kutumia studio hiyo kujifunza zaidi kwa vitendo na kuzingatia
maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari zenye ukweli kutoka
vyanzo sahihi ili kutoa ujumbe wenye manufaa mazuri kwa jamii.
Kwa upande wake Makamu mkuu wa
Chuo hicho Prof. Elifas Bisanda amesema studio hiyo imeanzishwa kwa
ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na
Utamaduni(UNESCO) kwa lengo kutoa elimu kwa jamii ambayo imekuwa
haipati habari kwa urahisi.
Amewataka wanahabari na wananchi
kwa ujumla kufikisha habari katika studio hizo kwa kuwa inatumia njia
ya haraka na rahisi katika kufikisha ujumbe kwa kushirikiana na redio
mbalimbali za jamii.
Naye mwakilishi kutoka Shirika la
umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi,na Utamaduni(UNESCO)
Bi. Zulimira Rodrigues amesema studio ya redio ya ‘Community’ ipo kwa
ajili ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu maendeleo ya wanawake na vijana
ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Mpaka sasa Shirika hilo
limefanikiwa kuanzisha redio za jamii katika baadhi ya mikoa ya Tanzania
bara ambayo ni Mwanza,Arusha na Tanga na katika baadhi ya maeneo ya
Unguja na Pemba.
No comments :
Post a Comment