Thursday, May 12, 2016

Utafiti wa malaria kuokoa maisha ya Watanzania.


1Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva akiongea na mwandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Luis Velarde wakati wa ziara ya waandishi hao katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
2   Mtaalamu  wa maabara katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga akiendelea na kazi ya kufanya vipimo vya malaria kwa kutumia vipimo vinavyotoa majibu kwa haraka (MRDT) ambayo majibu yake hutolewa baada ya dakika 15.5 
Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa tayari wamewasili Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe.
6 
Mtaalamu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja akifafanua jambo kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
7 
Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakimsikiliza Mtaalamu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja (hayupo pichani) walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
9 
Familia ya Salumu Rashidi wa kijiji cha Masatu kilichopo wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakiwa na mtoto wao Mohammedi Salimu ambaye ni miongoni mwa watoto waliopo kwenye mradi wa kudhibiti malaria wilayani huo. Kushoto ni mama yake Mohammedi Monica Mugunda.
34 
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa, (JKT) wakitumbuiza wakati wa zaira ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani walipotembelea zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Tanga)

WABUNGE WENGI WAIBARIKI BAJETI WIZARA YA AFYA

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim akihitimisha majumuisho ya makadirio ya Bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, bungeni Dodoma usiku huu.
 Waziri Ummy Mwalim akipanga vizuri nyaraka tayari kuhitimisha majadiliano ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.
 Viongozi wa wizara hiyo wakifuatilia majadiliano ya wabunge kuhusu bajeti hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Hamis Kigwangallah akijibu moja ya hoja za wabunge.
 Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda (Chadema), Mkoa wa Mbeya, akichangia hoja wakati wa makadilio ya Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iliyopitishwa bungeni Dodoma
 Naibu Waziri wa Afya, Hamisi Kigwangala akisalimiana na wanafunzi wanaosomea utabibu katika Chuo Kikuu cha Dodoma waliozuru bunge mjini Dodoma
Continue reading →

Wafanyabiashara barani Afrika watakiwa kuunganisha nguvu kupaaza sauti zao

arusha 
Mahmoud Ahmad Arusha
………………………………………………..
Umoja wa wafanyabiashara barani Afrika umewataka wafanyabiasha barani humu kuungana na kupaaza sauti zao ilikuweka mazingira bora ya kufanyabiashara zao kwenye nchi za bara hili.

KATIBU WABUNGE AKUTANA NA WADAU WA HABARI OFISINI KWAKE MJINI DODOMA

Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akizungumza na wadau wa Habari kutoka Jukwaa la
Wahariri, TMF, Sikika, Baraza la Habari Tanzania, Jukwaa la Katiba na TAMWA.
Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akimsikiliza Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw Deus
Kibamba wakati alipokutana na wadau wa Habari Ofisini kwake.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Bw Nevelle  Meena akizungumza wakati wa Mkutano kati ya
Katibu wa Bunge na wadau wa Habari.
 Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akisalimiana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw Theophil Makunga  wakati wa Kikao kati ya Katibu wa Bunge na wadau wa Habari.
Picha na Ofisi ya Bunge

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linafanya uchunguzi juu ya mauaji ya watu saba yaliotokea Wilayani Sengerema.

index 
Kwamba tarehe 11.05.2016 siku ya jumatano majira ya saa 03:45hrs usiku katika Kijiji na Kata ya Sima Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, watu wawili wasiofahamika majina wakiwa na mapanga walivunja mlango na kuingia kwenye nyumba ya Mama Eugenia Philipo miaka 60, akiwa amelala na familia yake na  kuwakata mapanga sehemu mbalimbali za miili yao hadi kufariki papo hapo, Mama mwenye Kaya Bi Eugeni, Mdogo wake, Watoto, pamoja na watu wengine wawili waliokua wakifanya kazi hapo nyumbani kwao wakitokea Ngara Mkoani Kagera.
Waliouawa 1. Eugenia Philipo miaka 60 Mama mwenye Kaya, 2. Maria Philipo miaka 50, mdogo wa Mama Mwenye Kaya 3.Mabula Makeleja miaka 20 mwanafunzi wa kidato cha nne, 4. Mkiwa Philipo mika 12, mwanafunzi shule ya msingi 5. Leonard Aloyce miaka 13 mwanafunzi shule ya msingi sima wote wa familia moja na 6. Donald miaka 40, pamoja na 7. Samson miaka 23 wakazi wa Ngara waliokuwa wakifanyakazi hapo nyumbani kwa Bi Eugeni.
Aidha katika utekelezaji wa mauaji hayo watu hao walianza kuingia kwenye nyumba walipokuwa wamelala watoto wa familia hiyo pamoja na wafanyakazi, na baada ya kuwakata mapanga hadi kuwaua waliingia kwenye nyumba ya jirani alipokuwa amelala Mama mwenye Kaya na mdogo wake Bi Maria na kuwaua vivyo hivyo, kisha wakaondoka eneo la tukio na kwenda kusiko julikana. Huku watoto wengine wanne wakinusurika kwenye mauaji hayo baada ya kujificha chini ya uvungu wa kitanda.
Jeshi la Polisi linawashikilia watu nane kwa mahojiano dhidi ya mauaji hayo na msako mkali wa kuwasaka wahusika wengine waliohusika kwa namna yeyote katika mauaji hayo bado unaendelea. Chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana, uchunguzi bado unaendelea. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawaomba wananchi wenye mapenzi mema na nchi yao watusaidie kutupa taarifa za wahusika wa  mauaji hayo ili tuweze kuwakamata.
Imetolewa na:
SACP: AHMED MSANGI                          
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

SERIKALI KUTUNGA SERA YA KUSIMAMIA SEKTA NDOGO YA FEDHA NCHINI

jiatu1 
NAIBU Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameliambia Bunge Mjini Dodoma, leo tarehe 12 Mei, 2016, kwamba serikali inaandaa sera ya Taifa ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2016, itakayosimamia na kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo
Alisema kuwa sera hiyo itawasilishwa mbele ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni kabla ya kupelekwa bungeni hatimaye itapatikana sheria ya kusimamia taasisi ndogo za fedha-microfinance Act, 2016.
“Serikali inatambua changamoto ya taasisi binafsi za fedha zinazosumbua wananchi, hivyo sheria hiyo ikitungwa itasaidia kuondoa matatizo hayo” alisisitiza Dkt. Kijaji
Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Rahisa Abdalah Musa (Viti maalumu), aliyetaka kujua serikali ilikuwa na mpango gani wa kudhibiti utitiri wa taasisi za fedha pamoja na mabenki ili yalete tija kwa Taifa kwa kuwakopesha wananchi
Akijibu swali la msingi na maswali ya nyongeza yaliyoulizwa na Mhe. Faida Mohamed Bakar (Viti maalumu) aliyetaka kujua mikakati ya serikali ya kuanzisha benki ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo ili kuwawezesha kupata huduma bora, Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa serikali haina mpango wowote wa kufanya hivyo.
Alisema kuwa badala yake serikali inafanya jitihada za kuimarisha benki zake zilizopo ikiwemo Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) na Benki ya Rasilimali (TIB) ili kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara wa kada mbalimbali.
“Serikali imeiboresha kimuundo, Benki ya Rasilimali (TIB) kwa kuunda kampuni tatu zinazofanyakazi kwa kujitegemea lakini kwa ushirikiano wa karibu” alisisitiza Dkt. Kijaji
Alizitaja kampuni hizo kuwa ni TIB Benki ya Maendeleo itakayotoa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa wafanyabiashara wakubwa na wa kati, TIB Benki ya Biashara itakayowahudumia wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo na TIB Rasilimali itakayohusika na masuala ya ushauri kwenye Soko la Hisa na Mitaji la Dar es salaam
“Pamoja na mambo mengine, kampuni hii inawajibika kuwashauri wafanyabiashara, hususan wa sekta ndogo ya fedha kupata mitaji kupitia Soko la Hisa la Dar es salaam” aliongeza Dkt. Kijaji
Dkt. Kijaji alisema kuwa pamoja na juhudi za serikali za kuboresha benki hizo, ikiwemo Benki ya Posta, Serikali kupitia Benki Kuu (BOT) inaendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwemo kutunga sheria, kanuni na taratibu za kusaidia nguvu za wananchi na sekta binafsi kuanzisha benki au taasisi za fedha katika maeneo yao
“Ni matarajio yetu kuwa wananchi wanatumia fursa ya mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo nchini kuwekeza wao wenyewe au kuzishawishi benki za biashara kuanzisha huduma za kibenki katika maeneo yao” alisema Dkt. Kijaji
Kuhusu ombi la mbunge huyo kuitaka serikali iingilie kati masuara ya riba zinazotozwa na taasisi za fedha na kuwaumiza wananchi, Dkt. Kijaji alisema kuwa serikali haiwezi kudhibiti wala kuingilia jambo hilo.
Alisema kuwa Serikali ilijitoa katika uendeshaji wa moja kwa moja wa shughuli za kifedha tangu mwaka 1991 ili kuruhusu ushindani huru na kuboresha huduma katika sekta ya fedha hivyo viwango vya riba na mikopo vinavyotozwa na benki hizo na taasisi nyingine za fedha zinapangwa kutokana na nguvu ya soko.
Dkt Kijaji alieleza kuwa katika upangaji wa viwango vya tozo na riba mbalimbali benki na taasisi za fedha huzingatia gharanma za upatikanaji wa fedha, halikadhalika gharama za uendeshaji na sifa alizonazo mkopaji”Alisisitiza Dkt Kijaji
Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
DODOMA
12/5/2016

Waandishi wa habari kutoka taasisi ya Malaria no More wawasili Tanga

be1 
Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha Dkt. Mohammed Alawi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
be2 
Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha Dkt. Mohammed Alawi akiongea na baadhi ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
be3 
Mwandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Lyndsey Wajert akiwa tayari kufanyiwa vipimo vya malaria na Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha wakati wa ziara ya waandishi wa Habari hao ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
be4 
Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi anayefanya kazi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Katy Migiro wa Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara mkoani Arusha kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
be5 
Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa tayari uwanja wa ndege wa Arusha kwa safari ya kuelekea mkoani Tanga.
be6 
Eneo la ukingo wa Bahari ya Hindi mkoani Tanga ambapo karibu na eneo walipofikia waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara yao mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Tanga)

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA UAPISHO WA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI

uh1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala.Picha na IKULU
uh2 
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.
uh3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa wa Sudani Kusini Salva Kir mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.
uh8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda.
uh9 uh10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
uh11 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Mwinyi alihudhuria pia sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
uh12 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Kikwete pia alihudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
uh13 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa mataifa mbalimbali katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.
uh14 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa viongozi wa dini wa Taifa la Uganda katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA WAKADIRIAJI MAJENZI, AFRIKA UTAKAOFANYIKA MWEZI AGOSTI 2016 JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Chama cha Wakadiriaji Majenzi Tanzania (TIQS), Samuel Marwa (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo (hawapo pichani), kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa wakadiriaji majenzi, Afrika utakaofanyika Agosti 2016. Kutoka kulia ni Mjumbe wa chama hicho, Neema Shabani na Bahati Mbambe.
 Rais wa Chama cha Wakadiriaji Majenzi Tanzania (TIQS), Samuel Marwa (katikati), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa chama hicho, Joseph Mhonda, Katibu wa chama hicho, Bernard Ndakidemi, Mjumbe wa Chama hicho, Bahati Mbambe na Mjumbe, Neema Shaban.
 Mjumbe wa Chama hicho, Bahati Mbambe (kulia), akisisitiza jambo.
 Mjumbe wa Chama hicho, Neema Shabani akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mjumbe wa chama hicho, Joseph Mhonda akitoa ufafanuzi kadhaa baada ya waandishi wa habari kuuliza maswali.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
……………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale CHAMA Cha WakadiriajiMajengo Tanzania (TIQS) kwa kushirikiana na Chama cha wakadiriaji majenzi Afrika (AAQS), watakuwa wenyeji wa mkutano mkuu wa Wakadiriaji Majenzi wa Afrika utakaofanyika tarehe 18 na 19 Agosti 2016 jijini Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine chama hicho  kimemuomba Rais John Magufuli,awape kazi katika miradi ya ujenzi

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI FROF. JAMES MDOE AFUNGA MKUTANO WA JOTOARDHI JIJINI DAR ES SALAAM

ta1 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  madini, Prof. James Mdoe ( wa nne kutoka kulia) akisoma hotuba ya ufungaji wa mkutano wa siku tatu uliokutanisha wataalam wa  masuala  ya jotoardhi kutoka katika nchi  za Tanzania,  Kenya,  Uganda, Rwanda, Ethiopia, Eritrea, Marekani, New Zealand na Djibouti kwa ajili ya kujadili  taarifa ya mtaalam mwelekezi  kuhusu utafiti uliofanywa katika Ziwa Ngozi lililopo mkoani Mbeya ambapo kuna  viashiria  vya  jotoardhi pamoja na eneo la  Kibiro nchini Uganda.
ta2 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  madini, Prof. James Mdoe (kushoto) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akifunga mkutano huo. Kulia ni Mjiolojia Mkuu kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Jacob Mayalla.
ta3 
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  madini, Prof. James Mdoe (hayupo pichani)

Tiketi za Bahati Nasibu ya Taifa kuanza kuuzwa mwezi huu

b1Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya  Murhandziwa Limited,Profesa Bongani Aug Khumalo akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na kuanzishwa na mchezo wa Bahati Nasibu ya Taifa itakayoendeshwa na kampuni hiyo nchini  katika hoteli ya SeaCliff jijini Dar es Salaam
b2 
kurugenzi Mkuu wa Bodi ya Taifa  ya Michezo ya Kubahatisha nchini,Abbas Tarimba  (kulia) na wadau wengine wa michezo ya kubahatisha wakisikiliza maelezo ya Professa Khumalo 
…………………………………………………………………………………………………….

TAMKO LA WIZARA KULAANI MAUAJI YA WATU 7 MWANZA

logo 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imesikitishwa na tukio la mauaji ya watu saba wa familia moja waliokatwakatwa mapanga baada ya kuvamiwa nyumbani, katika kijiji cha Sima wilayani Sengerema, mkoani Mwanza, siku ya Jumatano usiku. 
Wizara inalaani vikali mazingira ya mauaji ya watu hao wa familia moja, ambapo wauaji walivamia nyumba ya mama mjane na kumuuwa yeye mwenyewe, na watu wengine sita wakiwemo watoto watatu.  
                     Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
                      Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
          12/5/2016

Chama cha Ushirika NANYUM Lindi chadaiwa milioni 433 na wakulima

nanuNa Raymond Mushumbusi MAELEZO
Chama cha Ushirika (NANYUM) wilayani Lindi kitatakiwa kulipa deni la sh. milioni 433 kwa wakulima wa korosho wilayani humo baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tukio la wizi wa fedha hizo lililodaiwa kufanyika Januari, mwaka huu

Matukio mengi ya ukatili dhidi yao yamekuwa yakifanyika ama shuleni au nyumbani

index 
Na. Immaculate Makilika, MAELEZO
Utafiti ulofanywa mwaka 2009 na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya watoto hapa nchini ulionyesha  kuwa kuna kiwango kikubwa cha ukatili dhidi ya watoto.

No comments :

Post a Comment