Frank Mvungi-Maelezo
Serikali imefanikiwa
kuwaunganisha Watanzania wanaotafuta kazi wapatao 20,000 ikiwa ni moja
ya hatua ya kupunguza tatizo la ajira nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Msemai wa Wakala wa Huduma za Ajira nchini (TaESA) Bi Jamila Mbarouk wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam.
Akizungumzia watafuta kazi
waliongushwa tangu kuanzishwa kwa wakala huo Jamila alisema kuwa wengi
waliounganishwa walikuwa wahasibu, Makatibu muhtasi, wataalamu wa huduma
za jamii.
“Jukumu letu letu ni
kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri ndani na nje ya nchi ili waweze
kupata huduma hii kwa urahisi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Ajira
hapa nchini” alisisitiza Jamila.
Katika kupanua huduma ili
kuwafikia watanzania walio wengi Jamila amebainisha kuwa (TaESA)
imefungua ofisi za Kanda katika Mikoa ya Dodoma,Mwanza, na Arusha .
Mafanikio Mengine ni wakala
kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watafuta kazi 3185 ili kuweza
kuhimili ushindani na changamoto za soko la ajira.
Mafunzo hayo yametolewa
mbalimbali ikiwemo chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha Usimamizi
wa Fedha (IFM), Taasisi ya Uhasibu (TIA), Chuo cha Ardhi na Taasisi ya
Teknplojia Dar es salaam (DIT).
Akieleza Umuhimu wa mafunzo
hayo Jamila amesema kuwa yanalenga kuwajengea uwezo watafuta kazi ili
waweze kuandika barua za maombi ya ajira kwa ufasaha, kuandaa wasifu
binafsi (CV) na kuwajengea uwezo wa namna ya kufanya mahojiano kwa
ufanisi kwa kuzingatia mbinu za kisasa.
Kwa upande wake Afisa Kazi wa
TaEsa Bw. Amani Kasale amesema kuwa baadhi ya watafuta kazi wamekuwa na
kasumba ya kuchagua maeneo ya kufanyia kazi hasa yale yaliyopo katika
miji mikuu hali inayozorotesha juhudi za Serikali kuwaunganisha watafuta
kazi na waajiri katika maeneo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.
Akifafanua Kasale alisema kuwa
huduma ya kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri inatolewa bure kwa
watanzania wote wanaotafuta ajira kwa kuzingatia sheria na Kanuni za
ajira hapa nchini.
Pia Kasale alitoa wito kwa
vijana wote wanaotafuta ajira kuachana na kasumba ya kuchagua maeneo ya
kufanya kazi hasa yale yaliyo katika miji mikuu na kutumia fursa
zilizopo maeneo ya pembezoni.
Wakala wa huduma za Ajira
Tanzania TaESA Ulianzishwa kwa sheria ya wakala Na. 30 ya mwaka 1997
ikiwa na lengo la kuunganisha watafuta kazi na waajiri wenye fursa za
ajira ndani na nje ya nchi.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM)
kimewataka Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuendelea
kushirikiana ili kuunda nguvu ya pamoja itakayosaidia kuharakisha
maendeleo ya nchi kwa ufanisi zaidi.
Kimesema utendaji mzuri wa
viongozi hao ndani ya Baraza hilo ndiyo utakaoweza kukirahisishia kazi
Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa 2020, hali itakayojenga
imani kwa wananchi kuirejesha tena CCM madarakati kutokana na utendaji
mzuri wa viongozi hao.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai wakati akibadilishana mawazo na Katibu
Mpya wa Kamati ya Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi ndani ya Baraza la
Wawakilishi Zanzibar (Mnadhimu) huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini
hapa.
Nd. Vuai alimpongeza kiongozi
huyo kwa kuaminiwa na Wajumbe wa Baraza hilo na kumchagua kuwa Mnadhimu
wa Wawakilishi wote wa CCM ndani ya Chombo hicho cha kutunga sheria za
nchi.
Alisema kuchaguliwa kwa Mnadhimu
huyo pamoja na msadizi wake kutasaidia kuongeza ufanisi wa kusimamia
vyema shughuli za baraza la wawakilishi ili ziende sambamba na mahitaji
ya wananchi majimboni.
Alieleza kwamba mbali na viongozi
hao kuwa na jukumu la kuandaa miswaada, kutunga sheria na kupitisha
Bajeti za nchi bado wana wajibu wa kusimamia kwa vitendo ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya 2015/2020 pamoja na kulinda maslahi ya Chama hicho.
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU NA JAJI MKUU IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefika Ikulu kwa ajili ya
mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza mazungumzo
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana
na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman Ikulu jijini Dar es
Salaam.
SERIKALI YAFAFANUA KUHUSU NDEGE NDOGO ZINAZOENDESHWA NA RUBANI MMOJA
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI imesema kuwa, hakuna
kiwango kinachobainisha wazi kuwa ndege yenye uwezo wa kubeba abiria
kumi au zaidi ni sharti iendeshwe na marubani wawili.
Kauli hiyo imetolewa
leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhe. Eng. Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa
Jimbo la Tambwe, Mhe. Khalifa Issa aliyetaka kujua kuhusu Sheria za nchi
na za Kimataifa zisemavyo kuhusu ndege za namna hiyo kurushwa na rubani
mmoja.
Eng. Ngonyani amesema
kwamba, taratibu zinazoongoza fani ya kuendesha ndege nchini huongozwa
na miongozo inayokubalika Kimataifa na ambayo imeridhiwa hapa nchini na
Bunge.
Amefafanua kuwa,
Katika taratibu hizo, kuna matakwa ya kisheria na kiufundi ambayo
yakifuatwa yanawezesha kuwa na uwezekano mdogo sana wa kukumbwa na
athari ya kiafya na kushindwa kumudu kuendesha ndege.
Ameeleza kuwa,
Marubani hupimwa afya zao na madaktari bingwa kila muda maalum kulingana
na umri kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 140 mpaka 177 ya The Civil
Aviation (Personnel Licensing) Regulations, 2012.
“Serikali inaruhusu
ndege kuendeshwa na rubani mmoja kwa kuzingatia taratibu hizo, Aidha,
Kanuni 32(5) inasema kwamba ndege iliyoandikishwa katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na kuruka kwa shughuli za kibiashara yenye uzito
unaozidi kilo 5,700 itakuwa na marubani wasiopungua wawili”, alisema
Eng. Ngonyani.
Pia amefafanua kuwa,
shughuli za Usalama wa Anga nchini zinaongozwa na Sheria Namba 80 “Cvil
Aviation Act. 80” na Kanuni zilizotengenezwa chini yake, ambapo urushaji
wa ndege yenye abiria tisa au zaidi unaongozwa na Kanuni ziitwazo “The
Civil Aviation (Operation of Aircraft) Regulations, 2012” ambapo ndege
inayotimiza vigezo vilivyowekwa kwenye vifungu (2), (3) na (4) vya
Kanuni ya 32 kuwa na uzito wa chini ya kilo 5,700 inaruhusu kuendeshwa
na rubani mmoja.
Ameongeza kuwa,
katika viwango vinavyotolewa na Shirika la Kimataiaf la Usafiri wa Anga
(ICAO) kwenye kiambatanisho namba 19, chini ya Mkataba wa Kimataifa wa
Usafiri wa Anga (Chicago Convention) hakuna kiwango chochote
kinachobainisha wazi kuwa ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 10 au zaidi
ni sharti iendeshwe na marubani wawili.
“Pia hakuna hata
mapendekezo ya kiutekelezaji kwenye suala hilo, na hata katika
Kiambatanisho cha 6 chenye sehemu tatu kianchohusiana na uendeshaji wa
ndege ambacho ndicho kinachozungumzia idadi ya marubani katika
uendeshaji wa ndege hakina katazo hilo”, alisisitiza Eng. Ngonyani.
WIZARA YA KUDHIBITI MIGOGORO YA ARDHI KWA KUFUNGUA MABARAZA YA ARDHI
Jengo la Baraza la Ardhi Kiteto.
…………………………………………………………………………………………..
Katika azma ya kuimarisha huduma
ya utatuzi wa migogoro ya ardhi nchini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imeendelea kuboresha na kufungua Mabaraza ya Ardhi
na Nyumba ya Wilaya yatakayohusika na migogoro katika maeneo mbalimbali
nchini.
Kwa upande wa Mabaraza ya Ardhi
na Nyumba ya Wilaya mapya, Baraza ambalo limeshaanzishwa rasmi, ni lile
lililopo katika wilaya za Kahama na tayari limepatiwa vitendea kazi
muhimu na watumishi.
Wizara imeunda Mabaraza ya Ardhi
na Nyumba ya wilaya mapya 47 kupitia GN 544/2016, kati ya mabaraza hayo
mapya 47, Mabaraza ya Lushoto, Kiteto, Kasulu, Kibondo na Bagamoyo
yamepatiwa vitendea kazi na yataanza kufanya kazi mwishoni mwa mwaka huu
wa fedha.
Aidha, uimarishaji wa Mabaraza
hayo utapunguza mlundikano wa mashauri katika Mabaraza ya Ardhi na
Nyumba ya Wilaya kwa kuwa migogoro isiyo ya lazima kwenda ngazi ya
wilaya itasuluhishwa katika ngazi ya kijji au kata.
Katika picha ni baadhi tu ya
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ambayo yapo tayari kufunguliwa;
Kiteto, Lushoto, Kigoma mjini na Kibondo.
Serikali yakamata kilo 140 za dawa za kulevya nchini
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.
Serikali imefanikiwa kukamata
takribani kilo 139.69 za dawa za kulevya ikiwemo kilo 53.49 za Heroin,
Cocaine kilo 86.2 kuanzia mwaka 2015 mpaka Aprili mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo
vya habari kutoka Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya
iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Habari na Takwimu wa tume
hiyo, Amani Msami, pia tume hiyo imekamata tani 97 za bangi na mirungi.
Alisema mbali na kukamata kilo
hizo, takwimu zinaonesha kuwa watumiaji wa Heroin nchini wanakadiriwa
kuwa kati ya 200,000 hadi 425,000 ambapo kati ya hao 30,000 hutumia dawa
hizo kwa njia ya kujidunga sindano.
“Serikali imefanikiwa kukamata
takribani kilo 53.49 Heroin, Cocaine kilo 86.2 kuanzia mwaka 2015 mpaka
Aprili mwaka huu” alisema Msami na kuongeza kuwa:
“Watumiaji wa Heroin nchini
wanakadiriwa kuwa kati ya 200,000 hadi 425,000 ambapo kati ya hao 30,000
hutumia dawa hiyo kwa njia ya kujidunga”.
Msami alifafanua kuwa mbali na kukamata dawa hizo, tume hiyo ilikamata tani 81.3 za bangi na Mirungi tani 15.7.
Aliongeza kuwa mbali na hayo
idadi ya watuhumiwa waliyokamatwa wakijihusisha na usafirishaji wa dawa
za kulevya zikiwemo Bangi,Mirungi, Heroin na Cocaine walikuwa 14,503.
Hata hivyo, alisema takwimu hizo
zinaonyesha jitihada za serikali katika kukabiliana na biashara ya dawa
za kulevya nchini na si ukubwa wa usafirishaji wa Heroin na Cocaine
nchini.
“Moja ya jitihada za Serikali
katika kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya ni kutungwa kwa Sheria
ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Na.5 ya mwaka 2015.”
Alisema Msami.
Alifafanua kuwa sheria hiyo
imeweka adhabu kali kwa makosa ya kujihusisha na matumizi na biashara ya
dawa ya kulevya ikiwemo kifungo cha maisha kwa yeyote atakayesafirisha
dawa za kulevya.
Atakeyehusisha watoto na dawa za kulevya jela miaka 30
Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.
SERIKALI imesema kuwa mtu yeyote
atakayekamatwa kwa kosa la husisha au kushawishi mtoto kujiingiza katika
matumizi au biashara ya dawa za kulevya atahukumiwa kifungo cha miaka
isiyopungua 30.
Hayo yamesema na Mkuu wa Kitengo
cha Elimu, Habari na Takwimu wa Tume ya kuratibu na kudhibiti wa Dawa za
Kulevya, Amani Msami kupitia Taarifa ya tume hiyo kwa vyombo vya
habari.
Msami alisema adhabu hiyo ni kwa
mujibu wa Sheria ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Na.5 ya
mwaka 2015 tofauti na Sheria ya Kuzuian Biashara Haramu ya Dawa za
Kulevya Na. 9 ya mwaka 1995 iliyokuwa na mapungufu.
Alisema mbali na adhabu hiyo,
sheria hiyo mpya imeweka adhabu ya kifungo cha maisha na faini ya
shilingi Milioni 200 kwa kumiliki mitambo ya kutengeneza dawa za
kulevya.
Msami aliongeza kuwa Sheria hiyo
pia imeweka adhabu kali ya kifungo cha maisha pamoja na faini
isiyopungua Shilingi Bilioni moja kwa watu wanaofadhili biashara ya Dawa
za Kulevya.
“Aidha, sheria hii imeweka adhabu
kali ya kifungo cha maisha pamoja na faini isiyopungua Shilingi Bilioni
moja kwa watu wanaofadhili biashara ya Dawa za Kulevya ambao mara
nyingi ni watu wenye uwezo,”alisema Msami.
Mkuu huyo wa Kitengo, alisema
Serikali kupitia vyombo vya Dola iliwabaini, kuwakamata na kuwachukulia
hatua za kisheria baadhi ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa wa dawa za
kulevya.
Aliwataja baadhi ya watuhumiwa
wakubwa wa dawa hizo waliokamatwa na kuchukuliwa hatua kuwa ni Ali
Khatibu haji (maarufu kwa jina la Shkuba, Mohammed Mwarami (maarufu kwa
jina la Chonji na Mwanaidi Mfundo (maarufu kwa jina la Mama Leila).
Msami alisisitiza wito wa
Serikali kwa wananchi kutoa ushirikiano wa dhati kwa ajili ya kutoa
taarifa kuhusu watu wanaojihusisha na biashara ya dawa ya kulevya ili
waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
SERIKALI KUENDELEA KUONGEZA BAJETI KWA AJILI YA BARABARA.
Na Benedict Liweng, MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI imesema itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya barabara kadri uwezo wa kifedha utakavyoongezeka.
Hayo yamesemwa leo
Bungeni Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Miko na
Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa
Viti Maalum. Mhe. Sophia Mwakagenda aliyetaka kujua utayari wa Serikali
katika kukubali ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya na
kuongeza fedha katika Bajeti ya mwak 2016/2017.
Mhe. Jafo amesema
kwamba, Halmashauri ya Rungwe iliandaaa makisio ya bajeti ya Shilingi
bilioni 7.9 kwa ajili ya matenegenzo ya barabara katika bajeti ya mwaka
2016/17, hata hivyo kutokana na ukomo wa bajreti fedha zilizoidhinishwa
ni shilingi milioni 920 ambazzo zitatumika kwa ajili ya matenegenezo ya
barabara na ujenzi wa madaraja.
“Katika mwaka wa
fedha wa 2015/16, Halmashauri hiyo ilitengewa shilingi milioni 870 na
tayari Serikali imeshapeleka milioni 157.9”, alisema Mhe. Jafo.
Aliongeza kuwa, fedha
za Mfuko wa Barabara katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/17 ni
shilingi bilioni 247.5 ambazo endapo zingegawanywa sawa kwa Halmashauri
zote 181 zilizopo, kila Halmashauri ingekuwa na bajeti ya shilingi
bilioni 1.3.
Amefafanua kuwa mara
zote mahitaji yamekuwa ni makubwa kuliko uwezo wa rasilimali fedha
kukidhi mahitaji hayo ndiyo maana Serikali inaweka vipaumbele ili
kutekeleza mambo machache kwanza kulingana na uwezo uliopo kibajeti.
“Serikali itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya barabara kadri uwezo wa kifedha utakavyoongezeka”, alisema Mhe. Jafo.
WAZIRI MKUU KUHUDHURIA MKUTANO WA ADB ZAMBIA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumatatu, Mei 23, 2016)
kwenda Lusaka, Zambia kuhudhuria Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (51st Annual Meeting of the Board of Governors of the African Development Bank – AfDB) utakaofanyika kesho (Jumanne, Mei 24, 2016).
Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.
Mkutano huo ambao utafunguliwa na
Rais wa Zambia, Edgar Lungu utajadili masuala ya Nishati na Mabadiliko
ya TabiaNchi. Pia utahudhuriwa na Marais Idriss Deby wa Chad, Paul
Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya. Nigeria itawakilishwa na
Makamu wake wa Rais, Yemi Osinbajo huku Msumbiji ikiwazilishwa na Waziri
wake Mkuu, Carlos Agostinho do Rosário.
Watu maarufu waliothibitisha
kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Kofi Annan, Ashish Thakkar, John
Kufuor, Mary Robinson, Mo Ibrahim, Nancy Lee, Ngozi Okonjo-Iweala na
Tony Elumelu.
Mkutano huo utakaofanyika kwenye
kituo cha mikutano cha kimataifa cha Mulungushi (Mulungushi
International Conference Centre) utahudhuriwa na washiriki zaidi ya
5,000 kutoka nchi 54 ambao ni wanachama wa benki hiyo, washiriki kutoka
nchi 26 ambazo si za bara la Afrika (non-regional member countries),
wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, wadau wa maendeleo na wawakilishi
wa asasi za kiraia. Wengine ni Mawaziri wa fedha, biashara na uchumi na
wataalamu kutoka vyuo vikuu.
Waziri Mkuu amefuatana na Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji, wachumi kadhaa pamoja na
wataalamu wa sekta ya fedha.
DAR YAONGOZA KWA AJALI ZA BARABARANI
Na Fatma Salum- MAELEZO, Dodoma.
Serikali
imesema kuwa Jiji la Dar es Salaam linaongoza kwa kuwa na ajali nyingi
za barabarani kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2013 hadi 2015
zilizosababisha vifo vya watu pamoja na majeruhi.
Taarifa hiyo
imetolewa leo bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Mhe. Hamad Yusuf Masauni wakati akijibu swali la Mbunge wa
Biharamulo Magharibi Mhe. Oscar Rwegasira kuhusu kuongezeka kwa vifo
vitokanavyo na ajali za barabarani.
Kwa mujibu wa
takwimu zilizotolewa na Mhe. Masauni kwenye taarifa hiyo Jiji la Dar es
Salaam limeongoza kwa kuwa na ajali 18,506 kati ya ajali 46,539
zilizotokea nchi nzima kwa kipindi cha mwaka 2013 hadi 2015.
“Takwimu za
nchi nzima zinaonesha kuwa Mwaka 2013 zilitokea ajali 23,842
zilizosababisha vifo 4,002 na majeruhi 20,689. Mwaka 2014 zilitokea
ajali 14,360 zilizosababisha vifo 3,760 na majeruhi 14,530 na mwaka 2015
zilitokea ajali 8,337 zilizosababisha vifo 3,468 na majeruhi 9,383.”
alisema Masauni.
Mhe. Masauni
alieleza kuwa kwa mwaka 2013 Mkoa wa Kipolisi Kinondoni uliongoza kwa
kuwa na ajali zipatazo 6,589 ukifuatiwa na Mkoa wa Kipolisi Ilala
uliokuwa na ajali 3,464 wakati Mkoa wa Simiyu na Tanga kulikuwa na ajali
chache ambapo Simiyu zilitokea ajali 67 na Tanga ajali 96.
Mwaka 2014
Kinondoni na Ilala ziliongoza tena kwa kuwa na ajali 3,086 zilizotokea
Kinondoni na Ilala ajali 2,516 na mikoa iliyokuwa na ajali chache ni
Simiyu ajali 55 na Kagera ajali 29.
Aidha, Mhe.
Masauni alisema kuwa mwaka 2015 Mkoa wa Kipolisi Ilala uliongoza kwa
kuwa na ajali nyingi za barabarani ambapo ajali 2,516 zilitokea mkoani
humo ikifuatiwa na Temeke uliokuwa na ajali 1,420 wakati mikoa ya Rukwa
na Arusha ilikuwa na ajali chache.
Mhe. Masauni
alibainisha kuwa mfumo endelevu wa wazi uliopo wa kutoa takwimu hizo ni
kupitia taarifa za mwaka za Jeshi la Polisi (Polisi Annual Report)
ambapo kila mtanzania anaweza kupata taarifa hizo za ajali.
SERIKALI KUJENGA NYUMBA 9500 KWA AJILI YA ASKARI MAGEREZA
Na Fatma Salum- MAELEZO, Dodoma.
Serikali
kupitia jeshi la Magereza imesaini Mkataba na Kampuni ya Poly
Technologies ya China kujenga nyumba 9,500 kwenye vituo vyote vya
Magereza nchini.
Hayo yamesemwa
na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yusuf Masauni
wakati akijibu swali kuhusu kuboresha makazi ya askari lililoulizwa na
Mhe. Devota Minja (Mb) leo bungeni mjini Dodoma.
Mhe. Masauni
alibainisha kuwa kupitia mkataba huo Serikali itapunguza kwa kiasi
kikubwa changamoto iliyopo ya uhaba wa nyumba kwa ajili ya askari wa
jeshi hilo ambapo mahitaji kwa sasa ni nyumba 14,500 wakati zilizopo ni
nyumba 4,221 hivyo kupelekea upungufu wa nyumba 10,279.
“Serikali
inafahamu kuwa lipo tatizo la baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza na
Polisi kuishi katika nyumba chakavu zisizokuwa na hadhi, hivyo katika
kukabiliana na tatizo hili Serikali imeendelea kuzifanyia ukarabati
mkubwa baadhi ya nyumba na pia kujenga nyumba mpya”. Alisema Masauni.
Mhe. Masauni
alifafanua kuwa mgawanyo wa ujenzi wa nyumba hizo mpya ni Makao Makuu
ya Magereza nyumba 472, Arusha nyumba 377, Dar es Salaam nyumba 952,
Dodoma 356, Kagera 364, Kigoma 272, Kilimanjaro 390, Lindi 233, Manyara
206, Mara 378, Mbeya 622, Iringa 336, Morogoro 669, Mtwara 215, Mwanza
398, Pwani 384, Rukwa 358, Ruvuma 320, Shinyanga 337, Singida 299,
Tabora 408, Tanga 382, KMKGM Dar es Salaam 219, Chuo cha Ukonga 115,
Chuo cha Kiwira 183, Chuo cha Ruanda 62, Chuo KPF 27, Bohari Kuu 82 na
Bwawani nyumba 84.
Aidha, Mhe.
Masauni aliongeza kuwa kwa upande wa Jeshi la Polisi, Serikali
inakusudia kujenga nyumba 4,136 katika mikoa 17 ya Tanzania Bara na
Zanzibar zitakazosaidia kupunguza tatizo la makazi kwa askari wa jeshi
hilo.
Mhe. Masauni
alilieleza bunge kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto ya uhaba wa
nyumba kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mikopo yenye riba nafuu,
Miradi Shirikishi (PPP) na kwa kutumia fedha za bajeti ya Serikali kadri
hali ya uchumi itakavyokuwa inaimarika.
MWENYEKITI WA MTAA WA BABALE ULIOPO WILAYA YA NYAMAGANA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WASIOFAHAMIKA WAKATI AKIELEKEA NYUMBANI KWAKE.
MNAMO TAREHE 22.05.2015 MAJIRA
YA SAA 20:00HRS KATIKA MTAA WA BULALE KATA YA BUHONGWA WILAYA YA
NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MWENYEKITI WA MTAA WA BUBALE
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ALPHONCE MUSSA NYINZI MIAKA 48, MSUKUMA
MFANYABIASHARA NA MKAZI WA BULALE ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA
KUTOKEA CHINI YA KWAPA UPANDE WA KULIA NA WATU WAWILI WASIO FAHAMIKA.
RISASI HIYO PIA ILIMJERUHI NEEMA MARANGULA MIAKA 23 MKAZI WA BULALE
KATIKA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA.
INAELEZWA KWAMBA SIKU HIYO
JIONI ALIKUA AMETOKA KWENYE KIKAO ALICHOFANYA NA WAJUMBE WA KAMATI YA
ULINZI NA USALAMA WA MTAA WA BULALE, KATIKA MUDA WA SAA 20:00HRS USIKU
AKIELEKEA NYUMBANI AKIONGOZANA NA WAJUMBE WAWILI ALIKUTANA NA NEEMA
MARANGULA AKIWA NA MUME WAKE AMBAO WALIKUA WANAWAFUATA MAREHEMU NA
BALOZI KWA AJILI YA KUZUNGUMZIA MZOZO WA NDANI YA NDOA YAO KWA HIYO
WALIKUA WANAHITAJI KUSULUHISHWA, MAREHEMU NA WAJUMBE WAKE WAWILI WAKIWA
PAMOJA NA BI NEEMA PAMOJA NA MUMEWE WAKIWA WANAJADILI TATIZO HILO HAPO
BARABARANI MARA GHAFLA WAKATOKEA WATU WAWILI AMBAO WALIKUA WAKIPITA
BARABARANI NA KUWAAMBIA MKO CHINI YA ULINZI NA MMOJA WAO AKATOA BUNDUKI
NA KUMPIGA RISASI MAREHEMU AMBAYE ALIANGUKA CHINI HUKU WENZAKE
WAKIKIMBIA KUJIOKOA KUTOKA ENEO HILO LAKINI PIA WALE WAHALIFU
WAKAKIMBIA NA KUTOKOMEA GIZANI VICHAKANI.
NDIPO WANANCHI WA ENEO HILO
WALIJITOKEZA KWA MSAADA WA KUMSAIDIA MAREHEMU, WALIMCHUKUA MAREHEMU
KUMKIMBIZA HOSPITALI KWA MATIBABU LAKINI ALIFARIKI DUNIA WAKIWA NJIANI.
MAJERUHI BI NEEMA MARANGULA AMELAZWA HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA SEKOU
TOURE KWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI. MWILI WA MAREHEMU UPO
HOSPITALI MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA DAKTARI.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, UCHUNGUZI TUKIO HILO BADO
UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA JESHI LA POLISI AHMED MSANGI
ANAWAOMBA WANANCHI WENYE TAARIFA ZOZOTE KUHUSIANA NA TUKIO HILO
ZITAKAZO SAIDIA KUFANIKISHA KUKAMATA WAHUSIKA WAZITOE POLISI LAKINI PIA
KUTOA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WAO NA KUHAKIKISHA WANATENGENEZA MAKAZI
SALAMA HUKO WANAPOISHI NA MAENEO YA SHUGHULI ZAO. MSAKO MKALI UNAFANYIKA
NA KUHAKIKISHA WAHUSIKA WA TUKIO HILO WANAKAMATWA.
IMETOLEWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA
Mbunge
wa CCM, Mhe. Mary Mwanjelwa akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma
kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Mbunge
wa Nkasi Kaskazini, Mhe. Ally Keissy akiwasili viwanja vya Bunge mjini
Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini
Dodoma.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa
ameongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Jumanne Maghembe
wakielekea Bungeni kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 23 Mei, 2016
mjini Dodoma.
Naibu
Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Masiliano, Mhe. Eng. Edwin
Ngonyani akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani
ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Naibu
Waziri, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Hamis Kingwangalla akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma
kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Eng. Hamad Masauni
(kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mhe. Halima
Bulembo wakiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani
ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.
Selemani Jafo akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao
ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DODOMA.
MBUNGE MWIGULU NCHEMBA AANZA KUTIMIZA AHADI ZAKE JIMBONI IRAMBA
| Mbunge wa jimbo la Iramba Bw Mwigulu Nchemba wa pili kushoto akikabidhi bati zaidi ya 450 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu ,zahanati na nyumba vya madarasa |
| Wananchi wa jimbo la Iramba wakimpongeza mbunge wao Bw Nchemba kwa utekelezaji wa ahadi zake |
TAARIFA YA MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI ILIYOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU
Serikali
kupitia Wizara yangu inaendelea na utaratibu wa kutoa taarifa ya
mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini kila wiki kama
tulivyoahidi. Takwimu za ugonjwa huu zinaonyesha kuwa hadi kufikia
tarehe 22 Mei 2016, kulikuwa na jumla ya wagonjwa 21,585 ambao
wametolewa taarifa ya kuwa na ugonjwa huu, na kati ya hao, ndugu zetu
338 wamepoteza maisha.
Tumefarijika kuona takwimu za
wiki iliyopita kuanzia tarehe 16 hadi 22 Mei 2016 zinazoonyesha kuwa,
kasi ya ugonjwa wa kipindupindu imepungua kwa asilimia 49 (karibu nusu
ya wagonjwa), ambapo idadi ya wagonjwa wapya walioripotiwa ni 108, na
hakuna aliyepoteza maisha, ikilinganishwa na wagonjwa wapya 212
walioripotiwa wiki iliyotangulia ya Mei 9 hadi 15.
Mikoa ambayo imeripoti wagonjwa
wiki hii ni Morogoro (47), Manyara(16), Lindi (14), Mara (11) Dar es
Salaam (9), Pwani (6), Kagera (2), Kilimanjaro (2) na Iringa (1).
Halmashauri zilizoongoza kutoa
wagonjwa wengi ni Kilosa (27), Mvomero (15), Kilwa (14), Tarime Mjini
(11), Babati Vijijini (10), Kinondoni (9), Babati Mjini (5), Morogoro
Mjini (5), Kibaha Mjini (4), Bukoba Mjini (2), Chalinze (2), Same (2),
Iringa Mjini (1) na Mbulu (1).
Katika wiki iliyopita, mikoa
ambayo haikuwa na wagonjwa wa kipindupindu ni Kigoma, Dodoma, Mwanza,
Geita, Singida, Shinyanga, Arusha, Tanga, Tabora, Rukwa, Katavi, Mbeya,
Simiyu na Mtwara. Na mikoa ambayo haijawahi kuripoti mgonjwa wa
kipindupindu tangu mlipuko uanze ni Ruvuma na Njombe
Kupungua kwa idadi ya wagonjwa
kusirudishe nyuma juhudi za kuuzuia ugonjwa huu, bali tunatakiwa
kuzidisha jitihada ili tuweze kuuondoa, tusiwe na wagonjwa kabisa. Ni
vema kuchukua tahadhari zaidi, hasa katika msimu wa masika, ambapo kuna
uwezekano mkubwa wa maji ya mvua kusambaza vimelea vya ugonjwa huu.
Tuendelee kuzuia maambukizi, na pia kuendelea kutoa taarifa za ugonjwa
kila siku, hata kama hakuna wagonjwa, na kusimamia kikamilifu hatua
mbalimbali za udhibiti wa mlipuko huo
TBC yafanikiwa kufanya upembezi yakinifu wa kufunga mitambo ya FM eneo la Mbambabay.
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
SHIRIKA la
Utangazaji la Taifa (TBC) limefanya upembuzi yakinifu wa kufunga mitambo
ya FM yenye uwezo wa Kilowati moja katika eneo la Mbambabay Wilayani
Nyasa Ili kuongeza usikivu wa Redio za TBC.
Kauli hiyo
imetolewa leo Bungeni Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbinga
Vijijini, Mhe. Martin Msuha aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa
kuongeza uwezo wa kurusha matangazo ya Kituo cha TBC Songea ili wananchi
wa tarafa hizo wapate habari kupitia TBC.
Mhe. Nape ameeleza kuwa Matangazo ya Redio ya Taifa kupitia mtambo wa masafa ya kati yaani ‘’Medium Wave’’
wenye nguvu ya Kilowati 100 yalikuwa yakisikika vizuri katika Wilaya
mbalimbali za Mkoa wa Ruvuma wakati mtambo huo ulipokuwa ukifanya kazi.
‘’Tangu mwezi
Julai, 2013 mtambo huo haufanyi kazi kutokana na uchakavu na hivyo
kuathiri usikivu wa matangazo ya TBC katika maeneo kadhaa”, alisema Mhe.
Nape.
Alisema kwamba,
kwa kutambua umuhimu wa Wananchi katika kupata matangazzo, TBC
ililazimika kuhamisha mitambo yake miwili ya Redio yenye uwezo wa
Kilowati moja kwa kila moja iliyokuwa imefungwa eneo la Mshangano,
Songea na kuifunga eneo la juu la mlima wa Matogoro-Songea ili usikivu
Wake usambae katika eneo kubwa zaidi.
‘’Baada ya kufunga mitambo hiyo, matangazo ya TBC Songea yameboreshwa”, aliongeza Mhe. Nape.
Ameongeza kuwa
katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 Wizara yake imetenga fedha za
maendeleo kwa ajili ya kufunga mtambo eneo la Mbambabay.
‘’Kazi hiyo ya
uboreshaji wa matangazo katika eneo Hilo itaanza mara tu fedha za
kununua na kufunga mitambo hiyo zitakapotolewa”, alisema Mhe. Nape.
Aidha, alisema
kwamba kutokana na uwezo mdogo wa mitambo ya FM inayotumika kwa sasa,
mawimbi yake ya sauti hayafiki mbali sana ukilinganisha na yale ya
mitambo ya ‘’Medium Wave’’ iliyokuwa ikitumika awali ambayo yanafika eneo kubwa zaidi la Mkoa wa Ruvuma zikiwemo Tarafa za Hagati, Mbuji na Mkumbi.
‘’Kukabiliana
na changamoto za usikivu hafifu katika maeneo kadhaa Mkoani Ruvuma, TBC
imeshafanya upembuzi yakinifu wa kufunga mitambo ya FM yenye uwezo wa
Kilowati moja katika eneo la Mbambabay Wilayani Nyasa Ili kuongeza
usikivu wa Redio za TBC,”alisema Mhe. Nape.
WAZIRI NCHEMBA ATUMBUA MAJIPU JIMBONI KWAKE AVUNJA BODI YA MAJI ILIYOFANYA UFISADI WA MAMILIONI
| Waziri wa kilimo , mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akipokelewa na wananchi wa kata ya Tulia jimboni kwake Iramba jana |
| Waziri Mwigulu akilakiwa na wapiga kura wake wakati wa mikutano yake ya kuwashukuru |
| Waziri Nchemba akiwapungia mikono wananchi wake |
| waziri Nchemba akiteta jambo na mmoja kati ya walemavu katika kata ya Tulia jimboni Iramba |
| Waziri wa kilimo ,chakula na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akitangaza kuwasimamisha kazi viongozi wa bodi ya maji Mingela Iramba kwa ufisadi wa mamilioni ya maji |
WASIFU WA TIMU ZA MEXCO, ARGENTINA NA CHILE KABLA YA KOMBE LA COPA AMERICA
Timu
ya taifa ya Chile ni maarufu kama “La Roja”. Timu hii ilitengeneza
historia kwa mara ya kwanza mwaka jana ilipoifunga Argentina magoli 4-1
katika fainali ya Copa America na kuchukua ubingwa wa ligi hiyo tangu
kuanziashwa kwa Ligi hii.
Timu ya taifa ya Chile “La Roja” yenyewe iko kwenye kundi D ikijumuishwa na timu za taifa za Panama, Bolivia na Argentina, bado hili ni moja kati ya kundi gumu kwenye michuano ya mwaka huu. Je itafanikiwa kuingia fainali mwaka huu na hata kuchukua ubwingwa tena katika kombe hili? Majibu yote tutayapata katika Copa America 2016 StarTimes pekee
Timu ya taifa ya Chile “La Roja” yenyewe iko kwenye kundi D ikijumuishwa na timu za taifa za Panama, Bolivia na Argentina, bado hili ni moja kati ya kundi gumu kwenye michuano ya mwaka huu. Je itafanikiwa kuingia fainali mwaka huu na hata kuchukua ubwingwa tena katika kombe hili? Majibu yote tutayapata katika Copa America 2016 StarTimes pekee
Timu ya taifa ya Mexico ni
maarufu kama “El Tri”, ni timu yenye historia ya kipekee kwenye fainali
za kombe la dunia. Imeshiriki mara 14, haijawahi kushinda taji hili, iko
katika nafasi ya 19 kwenye viwango vya FIFA
Katika copa America iko kundi C ambalo ni kundi gumu haswa! Ikiwemo Uruguay, Jamaica na Venezuela. Mwaka 1991 ilifanikiwa kuingia fainali na kucheza na Argentina lakini wakagonga mwamba na kupigwa bao 2-1. Hivyo hivyo kwa mwaka 1999 ilipocheza na Colombia katika fainali na kupigwa 1-0.
Je mwaka huu watajitahidi kuchukua ubingwa? Yote utayapata StarTimes
Katika copa America iko kundi C ambalo ni kundi gumu haswa! Ikiwemo Uruguay, Jamaica na Venezuela. Mwaka 1991 ilifanikiwa kuingia fainali na kucheza na Argentina lakini wakagonga mwamba na kupigwa bao 2-1. Hivyo hivyo kwa mwaka 1999 ilipocheza na Colombia katika fainali na kupigwa 1-0.
Je mwaka huu watajitahidi kuchukua ubingwa? Yote utayapata StarTimes
Argentina
ni nchi inayopatikana barani America ya kusini. Mwaka jana timu hii
ilifanikiwa kuingia katika fainali na kutolewa na mabingwa Chile
waliochukua ushindi wa bao 4-1 katika kombe la COPA America na kuifanya
chile iibuke kidedea katika fainali hiyo. Mwaka huu Argentina itashiriki
katika mashindano ya Copa America, bila kumsahau kiungo mchezaji Messi
ndani, je watafanikiwa kuingia katika fainali au hata kuchukua Ubingwa?
StarTimes tutarusha mechi zote LIVE ndani ya channel za michezo
Samatta sasa kupewa eneo Juni 5
Mwigizaji maarufu nchini, Ahmed Olotu maarufu kama mzee Chilo akizungumza na wanachama wenzake wa SHIWATA katika mkutano huo
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umesogeza mbele kwa
siku moja sherehe za kumkabidhi eneo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana
Samatta hadi Juni 5, 2016 ili kupisha pambano kati ya Timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars) na timu ya Taifa ya Misri.
Akizungumza katika mkutano wa
wanachama kujiandaa na sherehe hizo walimuomba Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye awe mgeni rasmi ambapo pia
waliomba dua la kumuombea Rais John Pombe Magufuli katika juhudi zake za
kupambana na wabadhirifu wa mali ya umma.
MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO SAID MECKY SADICK AFANYA ZIARA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA)
Mkuu
wa Mko wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidick akiwa ameongozana na Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi
(MUWSA) John Ndetico (mwenye tai) alipofanya ziara katika mamlaka hiyo .
Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi
(MUWSA) John Ndetico akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro Said Mecky Sadick alipotembelea ofisi za MUWSA.
Baadhi
ya Viongozi wa Serikali pamoja na Wakuu idara katika Mamlaka ya maji
safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakisikiliza kwa makini
taarifa iliyokuwa ikitolewa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na viongozi wengine wakiwa katika chanzo cha maji cha Nsere .
Chanzo cha Maji cha Nsere ambacho kiwango cha maji kinatajwa kushuka kutoka lita za ujazo Milioni 12 hadi Milioni 9.5.
Mkuu wa mkoa Saidi Mecky Sadick akitembelea maeneo ya chanzo hicho.
Mkuu
wa Mko wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidick akiwa ameongozana na Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi
(MUWSA) John Ndetico (mwenye tai) alipofanya ziara katika mamlaka hiyo .
Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi
(MUWSA) John Ndetico akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro Said Mecky Sadick alipotembelea ofisi za MUWSA.
Baadhi
ya Viongozi wa Serikali pamoja na Wakuu idara katika Mamlaka ya maji
safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakisikiliza kwa makini
taarifa iliyokuwa ikitolewa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na viongozi wengine wakiwa katika chanzo cha maji cha Nsere .
Chanzo cha Maji cha Nsere ambacho kiwango cha maji kinatajwa kushuka kutoka lita za ujazo Milioni 12 hadi Milioni 9.5.
Mkuu wa mkoa Saidi Mecky Sadick akitembelea maeneo ya chanzo hicho.
WEMA AZINDUA MOBILE APLICATION YAKE, HABARI ZAKE ZITAPATIKANA HUMO
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na Miss
Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa Filamu nchini Wema Sepetu
wakifunua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa Wema Sepetu Mobile
Application ya msanii Wema Sepetu kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini
Dar es salaam jana , Katika Aplication hiyo kutapatikana habari
mbalimbali za msanii huyo mwigizaji wa filamu pamoja na habari
zinazohusu masuala mbalimbali ya kazi zake hii ni kwa mara ya kwanza
katika nchi za Afrika Mashariki kwa msanii kuwa na Mobale Aplication
yake hivyo msanii mwingine atakayekuja atakuwa anafuata nyayo za Wema
Sepetu.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimpongeza
msanii Wema Sepetu mara baada ya kuzindua Mobile Application ya msanii
huyo jana.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia
wakati wa uzinduzi wa Wema Sepetu Mobile Application ambapo alimpongeza
Wema kwa hatua kubwa aliyofikia ya kuwa msanii wa kwanza wa Filamu
nchini kuwa na Mobile App na kuwataka wasanii wengine kuwa wabunifu na
kuja na mipango ambayo itawanufaisha zaidi.
Msanii wema Sepetu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mobale Aplication yake kwenye hoteli ya Hyyat Regency.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimpongeza
msanii Wema Sepetuwakipiga picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
Mtaalamu wa Mobile Application Ndugu Haji Yussuf akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wema Sepetu Mobile Application
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza
jambo na Miss Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa Filamu nchini Wema
Sepetu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
akipiga picha ya pamoja na Miss Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa
Filamu nchini Wema Sepetu
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipiga picha
ya pamoja na Miss Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa Filamu nchini
Wema Sepetu na mama yake kushoto pamoja Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Hartman Traders Ndugu Cecil na Mtaalamu wa Mobile Application Ndugu Haji Yussuf wa
pili kutoka kushoto wakati wa uzinduzi wa mobile Application yake
ambayo itawasaidia wapenzi na mashabiki wake kupata habari sahihi na za
uhakika.







No comments :
Post a Comment