Friday, May 6, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANACHI ALIPOKUWA SAFARINI KUTOKEA DODOMA KUELEKEA ARUSHA



kat01 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha sehemu mbalimbali wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha kwa njia ya barabara leo Mei 6, 2016. PICHA NA IKULU
kat1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha.
kat2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha.
kat3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua karanga kutoka kwa mjasiriamali mara baada ya kuwahutubia mamia ya wakazi wa Babati mkoani Manyara waliojitokeza katika eneo la Stendi ya Mabasi ya Babati Mkoani Manyara.
kat4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Magugu mkoani Manyara wakati akielekea  Mkoani Arusha.
kat5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara wa Stendi ya Mabasi ya Singida wakati alipokuwa njiania kuelekea Arusha.
kat6 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Endasak mkoani Manyara wakati akitokea Dodoma kuelekea Arusha kwa njia ya barabara.
kat7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Dareda mkoani Manyara waliojitokeza kumsalimia wakati akitokea Dodoma kuelekea mkoani Arusha. PICHA NA IKULU

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAZUNGUMZIA KUHUSU UTEKELEZAJI WA AHADI YA UADILIFU KWA WATUMISHI WA UMMA

ut1Mtangazaji wa kipindi cha Rushwa ni Adui wa Haki Bi. Miriam Chisoro (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama (kulia) wakati  wakijadili mada kuhusu Ahadi ya Uadilifu  kwa watumishi wa umma ofisini kwa mkurugenzi huyo mapema leo.
ut2Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi  wa Umma Bw. Mathew Kirama (kulia) akisisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa umma wakati wakijadili mada hiyo na Mtangazaji  wa kipindi cha Rushwa ni Adui wa Haki Bi.Miriam Chisoro (kushoto) ofisini kwa mkurugenzi huyo mapema leo.

TAMKO LA WIZARA KULAANI MAUAJI YA MAMA NA MTOTO, B/MOYO

logo 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inasikitishwa na inalaani vikali tukio la kuuawa kwa kuchinjwa, mwanamke Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emmanuel (3), wakazi wa eneo la Zinga, kata ya Dunda, wilayani Bagamoyo, kutokana na wivu wa kimapenzi.
Wizara inakemea maauji hayo, yanayodaiwa kutekelezwa na Frowin Mbwale  mkazi wa Kawe, Dar es salaam, ambaye ni mme wa marehemu, kwani yamesababisha kukatisha maisha ya mama na mtoto, katika kipindi ambacho Taifa linahimiza uzingatiaji wa mchango na haki za wanawake katika maendeleo ya taifa, na mwitikio wa haki ya kuishi ya Mtoto katika mipango na programu za maendeleo endelevu.
Wizara inasisitiza kutambua kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa wanafamilia liko mikononi mwa kila mwananchi, hivyo jamii inawajibu wa kusaidia udhibiti wa ukatili na mauaji katika familia na jamii zetu. Jamii ikiwa na uelewa wa pamoja katika haki za wanawake na watoto katika jamii, itawezesha kuwekeza katika haki ya kuishi ya Mtoto, na  kuendelea kuwaamini wanawake kwamba wanaweza kutoa mchango mkubwa wa kuendeleza familia zao, na taifa likaweza kupiga hatua kufikia maendeleo endelevu.  
Wizara inapenda kupongeza Polisi mkoa wa Pwani na wananchi walitoa taarifa za kuwakamata watuhumiwa wa mauaji haya, na tunaamini kuwa watakapofikishwa mbele ya vyombo vya sheria haki itaweza kutendeka.
Wizara inapenda kutoa pole kwa familia za marehemu hao waliopoteza maisha kwa kuchinjwa na kuawa, na kuwaombea kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa. Wizara inaitaka jamii itambue kuwa hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mtu mwingine, na mwanamke na mtoto anahaki ya kuthaminiwa utu wake, bila ubaguzi wowote ambao unaweza kukatisha maisha yao.
                Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
          Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee

The Government to issue a quarterly report on maternal death

um1 
Minister for Health, Community Development, Gender, Elderly and Children, Ms. Ummy Mwalimu.
…………………………………………………………………………………………….
By Jonas Kamaleki- Maelezo
The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children is set to give a quarterly report on maternal deaths during delivery in order to minimize mothers’ deaths in the country.
This was revealed by the Minister for Health, Community Development, Gender, Elderly and Children, Ms. Ummy Mwalimu at the opening of the Health Women Leaders Conference in Dar es Salaam. “My ministry will ensure that all District Councils are providing a quarterly report on the deaths that occur during delivery.” Said Ummy Mwalimu. These reports according to the minister will be in line with maternal deaths reduction.
She also said the 5th Phase Government will construct rooms for operations in all health centres countrywide to rescue women’s life at delivery.
On promoting women in the decision making bodies, Ms. Ummy said she will be appointing 30 percent of women in the boards under her ministry. She mentioned such boards as the Tanzania Food and Drug Authority (TFDA), Medical Store Department (MSD) and Pharmacy Board.
She noted that promotion of women depends largely on the level of education, thus she urged girls to study hard and perform well in order to acquire higher leadership positions. “Fifty – fifty in leadership without education is just politics, so girls you need to be educated so as to be considered in high ranking leadership positions,” added Ummy Mwalimu.
Meanwhile, the Executive Chairperson of the Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS), Ms. Fatuma Mrisho urged girls to be busy with studies so as to avoid involving themselves with love affairs thus concentrating with academic issues. She further said that when girls are fully engaged with studies they will be free from HIV/AIDS by about 7 per cent.
Stressing on women empowerment, the Danish Ambassador in Tanzania, Mr. Einar Hebogård Jensen said women need to have equal access to education, healthcare, resources and leadership. He said there was a need to respect and empower them for the betterment of the community.
This was a pre-conference that will be followed by the largest conference on the health, rights and well-being of girls and women that will take place on 16-19 May 2016 in Copenhagen, Denmark. It will attract more than 5,000 people – world leaders, academics, policy makers, activists, media, royalty, civil society and private sector representatives.

VIINGILIO MECHI YA YANGA, ESPERANCA

Uongozi wa Young Africans ya Dar es Salaam, umekamilisha maandalizi yote muhimu ya mchezo dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola wa kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho la Barani Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho Jumamosi Mei 7, saa 10:00 jioni.
Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana ukisimamiwa na kamishna kutoka Ethiopia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa Jukwaa la VIP “A” kuwa ni Sh 30,000; VIP “B” na “C” Sh 20,000 wakati jukwaa la viti Rangi ya chungwa ni Sh 7,000 wakati mzunguko wa viti vya bluu na kijani ni Sh 5,000.
Kwa mujibu wa Muro, Yanga itawakosa wachezaji mahiri wawili, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko ambao watatumia mchezo huo kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano walizoonywa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kushuka kucheza Kombe la Shirikisho.
“Tunawaomba wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga tujitokeze kwa wingi kesho kuishangilia timu yetu kwa nguvu na kasi kubwa,” amesema Muro ambaye alitumia nafasi hiyo kutamba kwamba Yanga ilisajili wachezaji 24 kwenye michuano inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

FIFA YAILIMA FAINI SIMBA, YAPANGA KUISHUSHA DARAJA

imagesShirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (sawa na Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) ya shirikisho hilo.
Kamati ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.
Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe. Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.
Felix Majani, Mwanasheria wa Musoti, ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa FIFA, alifungua kesi katika shirikisho hilo kuwashitaki Simba kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na mteja wake.
Kwa kosa hilo Simba inatakiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016. TFF imekuwa nakala na maagizo kuisimamia Simba inalipa kiasi hicho cha fedha.
Simba imeagizwa kulipa stahiki zote za Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016.
Katika barua hiyo ambayo TFF ina nakala yake, Simba imepewa amri ya kuhakikisha inalipa na isipotekeleza agizo hilo mara moja itakatwa pointi tatu katika mechi zake Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara –VPL.
FIFA imekwenda mbali zaidi ikisema ikiwa klabu hiyo kama haitalipa katika muda uliopangwa yaani siku 30 kutoka sasa, FIFA itaishusha Simba daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara hadi Ligi Daraja la Kwanza au zaidi.
Kwa upande wake, TFF imagizwa kuhakikisha uamuzi huo unasimamiwa vema utekelezwaji wa maagizo hayo vinginevyo itachukuliwa hatua stahiki ikiwamo kuiondoa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE, (JNIA), WAPATA SHIRIKA LINGINE LA NDEGE, NI MAURITIUS AIRLINES

 Mfanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, akiielekeza ndege ya Shirika la
Ndege Mauritius Airlines, kuegesha kwenye daraja la kushukia abiria (Bridge),
kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei
6, 2016. Ndege hiyo aina ya Airbus 319 yenye uwezo wa kubeba abiria 130, imetua
kwa mara ya kwanza na itakuwa ikifanya safari zake kila Ijumaa ikiruka moja kwa
moja kutoka Mauritius kuja Dar es Salaam kasha Nairobi, nchini Kenya.
Magari ya zimamoto yakiipokea ndege hiyo kwa kuimwagia maji ikiwa ni ishara ya ukaribisho
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said, JNIA
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, kupitia uwanja wake wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, imeongeza idadi ya mashirika ya ndege yanayotumia uwanja huo
baada ya ndege ya kwanza ya Shirika la Ndege la Mauritius (Mauritus Airlines),
kutua kwenye uwanja huo leo Mei 6, 2016.
Ndege
hiyo aina ya Boeng Airbus 319, yenye kubeba abiria 130, ilitua kwenye uwanja
huo majira ya saa 5;20 asubuhi ambapo kama ilivyoada ya kupokea ndege mpya
inayoanza shughuli zake kwenye uwanja huo, magari mawili ya zimamoto yalipiga
(saluti), kumwagilia maji ndege hiyo wakati ikielekea kuegesha kwenye daraja la
kushukia abiria.
Kwa
mujibu wa maafisa wa Shirika hilo, ndege hiyo itakuwa ikiruka kutoka Mauritius
moja kwa moja na kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
ambapo itashusha abiria na kuelekea 
uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
“Safari ya kutoka Mauritius kuja Dar es Slaam ni kiasi ya masaa matatu .”alisema rubani
mkuu wa ndege hiyo, Parikshant Nundlol
Maafisa wa TAA walisema  kuwa ndege hiyo itakuwa ikifanya safari yake mara
moja kwa wiki kila siku ya Ijumaa.

 Rubani mkuu wa ndege hiyo, Parikshany Nundlol, akizungumza na waandishi wa habari wa Mauritius waliofuatana na ndege hiyo
Warembo wa Kitanzania walioshiriki kuipokea ndege hiyo
Wafanyaakzi wa shirika la ndege la Mauritius na wale wa Swissport wakiwa katika picha ya pamoja
 Abiria wa kwanza waliowasili na ndege hiyo

Mahakama Kuu imefuta rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP)

       index   
Na JacquilineMrisho – MAELEZO
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyokuwa ikipinga kuondolewa kwa shitaka la 8 la utakatishaji fedha linalomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya na wenzake wawili.
 
Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Moses Mzuna alipokuwa akitoa majibu ya rufaa iliyokuwa imekatwa na DPP.
 
“Ninafahamu kila kesi inaamuliwa kutokana na mazingira yake lakini nimefuta rufaa hii kwa kuwa hoja zilizotolewa hazina nguvu kisheria” alisema Jaji Mzuna.
 
Aidha Jaji Mzuna amefafanua kuwa hata kama amefuta rufaa hiyo lakini upande wa Jamuhuri bado una nafasi ya kubadilisha shitaka au hati nzima ya mashtaka inayowakabili washtakiwa hao.
 
Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Timony Vitalis amekubaliana na uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo juu ya pingamizi lake ingawa bado anasimamia watuhumiwa kutofutiwa shitaka la utakatishaji wa fedha.
 
Naye Wakili wa Utetezi Majula Magafu amesema kuwa wao wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na Wakili wa Serikali ili wajue namna ya kuikabili kesi hiyo.

Mtafiti wa Hesabu aomba Milioni 12 kufanikisha safari ya Marekani kuwasilisha Utafiti wake.

Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.
Mtanzania aliyevumbua Fomula ya Hesabu yenye uwezo wa kutumika katika Hesabu za Viwandani Mhandisi Mazoleka Maziku awaomba watanzania, Taasisi za Serikali na zisizo za Kiserikali,Kimataifa na za watu binafsi kumchangia kiasi cha Shilingi Milioni 12 kwa ajili ya kuwasilisha utafiti wake katika Mkutano wa Mwaka wa wataalamu wa Hesabu za Viwandani nchini Marekani.
Bw. Maziku ameomba msaada huo alipokuwa akizungumza na waaandishi wa Habari kuhusu utafiti huo aliyoufanya kwa lengo la kuboresha fomula zinazotumika sasa hivi ambapo kama utafiti huu utakubalika na kuanza kutumika basi unaweza kurahisisha ukokotoaji wa hesabu zinazotumika viwandani.
Mbali na hayo mtafiti huyo alisema fomula hiyo aliyogundua inauwezo wa kukokotoa hesabu za aina mbili ambazo hujulikana kama (Arithmetic Progression na Sums of Powers) ambapo hapo mwanzo zilikuwa zikitumia fomula tofauti.
“Baada ya kuwasilisha utafiti wangu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Hesabu (UDSM)kwa ajili  ya kufanya uchunguzi na uhakiki, wataalam hao  walijiridhisha na kuona vyema watume utafiti huo katika  Chuo Kikuu cha Manchester Uingereza, ambapo chuo hicho ni miongoni mwa vyuo bora  Duniani na ndipo nilipotumiwa mwaliko huu,” alisema Mhandisi Maziku.
Hata hivyo mtafiti huyo amewasihi watanzania watakaoguswa kumchangia wanaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0686-632 262 au 0713 037 123 kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo, kwani safari hiyo itasaidia kuitangaza nchi yetu pamoja na kupata mtandao wa wanasayansi Duniani.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika huko Marekani kuanzia tarehe Julai 11 hadi 15 mwaka huu katika Chuo Kikuu cha Massachusetts na Utahushisha wanachama zaidi ya 13,000 Duniani pamoja na Vyuo Vikuu vya Kisayansi takribani 500 Duniani kote.

MAKAMU WA RAIS KATIKA SALA YA IJUMAA DODOMA

IJ1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waumini wa Dini ya Kiislam baada ya Sala Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa GADAFFI Mkoani Dodoma Leo Mei 6,2016. (Picha na OMR)
IJ2

Wizara ya Afya yapokea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4

AF1Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari leo 6 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam kuhusu msaada walioupokea toka Shirika la Afya Duniani (WHO) wenye thamani ya shilingi bilioni 1.4.
AF2Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa tiba leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
AF3Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro wakikabidhiana hati za makabidhiano ya vifaa tiba leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
AF5 
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro (kulia) akikabidhi jokofu kwa kwa jaili ya huduma za chanjo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro (kulia) akikabidhi jokofu kwa kwa jaili ya huduma za chanjo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutoa chanjo kwa akina mama na watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali nchini.
Akiongea na waandishi wa habari Wizarani hapo, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila ameeleza kuwa vifaa tiba hivyo vitasaidia uhifadhi wa chanjo katika mikoa mbalimbali pamoja halmashauri nchini.
‘’Ni msaada mkubwa tulioupata toka WHO na nina amini kuwa utatusaidia sana katika kufanikisha suala la chanjo kwa akina mama na watoto nchini na pia tunaamini wataendela kushirikiana na Wizara ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea’’, alisema Dkt. Rusibimayila.
Ameongeza kuwa, kwa sasa vituo vipya vinavyofunguliwa nchini vikiwemo vile ambavyo havikuwa na majokofu vitakuwa na uwezo wa kupata vifaa hivyo kama vile majokofu na vifaa vingine vya tiba ili huduma za chanjo ziweze kutolewa katika kila kituo nchini.
Akikabidhi vifaa hivyo Wizarani hapo, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro  amesema kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ni pamoja na majokofu 200 pamoja na vifaa vitumikavyo kwa ajili ya kutolea chanjo.
Kwa upande wake Mratibu Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana Emmanuel Yohana ameeleza kuwa, majokofu hayo pia yatapelekewa katika wilaya ambayo yana upungufu wa majokofu pamoja na vituo vipya kwa ajili ya kupunguza umbali kwa wagonjwa wa chanjo na pia ni moja ya kuweka huduma karibu na wananchi nchini.
Aidha, ameongeza kuwa spesimeni za polio na surua zilizotolewa na WHO zitapalekwa pia katika vituo kwa jili ya kuchukua damu kwa ajili ya vipimo na kuletwa Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi wa maabara.
‘’Wanufaika wa huu msaada kutoka WHO ni wananchi wote wa Tanzania kwani utaenda katika vituo vyote vya chini zikiwemo Zahanati’’, alisema Yohana.
Kupitia wadau mbalimbali Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kushirikiana na wadau hao katika kutafuta vifaa tiba mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa sekta ya afya nchini inaimarika kwani Tanzania kwa sasa imeweza kudhibiti polio kwa kiasi kikubwa.

TUZILINDE HAKI ZA BINADAMU.

index 
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Tanzania imechukua hatua kadhaa za kulinda na kuhifadhi haki za binadamu nchini. Hatua hizo zinajumuisha kuridhia mikataba kadhaa muhimu ya Kimataifa na Kikanda ya haki za binadamu, kuingiza baadhi yake kwenye sheria za nchi na kuanzisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB).
Aidha, Serikali imeendelea kuimarisha Mahakama, Bunge na Vyombo vyote vinavyosimamia utekelezaji wa Sheria nchini.
Kwa mujibu wa mapendekezo ya Azimio la Vienna la mwaka 1993 na Programu yake ya utekelezaji, kila serikali ulimwenguni inapaswa kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu, ambapo kwa upande wa Serikali ya Tanzania iliamua kuanzisha mchakato huu.
Mnamo mwaka 2009, THBUB iliongoza warsha ya Kitaifa ya Mashauriano yenye lengo la kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu ambapo warsha hiyo ilijumuisha wajumbe mbalimbali kutoka Serikalini, Wanataaluma, Asasi za Kiraia pamoja na Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN).
Mpango Kazi huu unajumuisha mapendekezo mengi ya kimataifa na unatoa mwongozo wa utekelezaji ulio wazi kwa Wizara mbalimbali katika kukuza haki za binadamu nchini. Unaelezea malengo ya jumla na hatu za msingi zinazopaswa kuchukuliwa huku ukibainisha Wizara zinazohusika.
Aidha, Mpango huu unajumuisha Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) wenye viashiria vinavyopimika, ambao pia unaimarisha utekelezaji wa Mpango Kazi.
Mpango Kazi huu utaimarisha haki za binadamu nchini Tanzania kupitia baadhi ya malengo yakiwemo kufanya tathmini kuhusu masuala ya haki za binadamu na kuandaa mikakati ya kukuza utoaji elimu ya haki za binadamu na kuongeza uelewa kwa Watanzania wote.
Halikadhalika, Mpango umebainisha haki 23 zilizoko katika makundi manne ya kimada kama maeneo ya kipaumbele katika kuimarisha ukuzaji na ulinzi wa haki za binadamu nchini. Haki na makundi hayo yanajumuisha Haki za kiraia na Kisiasa, Haki za kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni, Makundi yenye Mahitaji Maalumu, Kuimarisha Taasisi na Msuala yaliyopo ambapo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ikisaidiwa na Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itafuatilia utekelezaji wa Mpango huo.
Continue reading →

TRA kugawa EFD’S 5700 kwa wafanyabiashara

TRA1 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata  akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato nchini kulia ni Kamishna wa kodi za ndani Bw. Yusufu Salum.
(Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………………
Na Lilian Lundo MAELEZO
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejipanga kugawa jumla ya mashine 5700 za (Electronic Fiscal Devices) EFD’s kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za Serikali katika kukusanya mapato nchini.
Akizungumzia mipango hiyo leo, Jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema wameamua kuanza kugawa mashine hizo kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wengi wao hawana uwezo wa kugharamia manunuzi ya mashine hizo.
“ Mamlaka imeona changamoto wanayoipata wafanyabiashara wadogo hivyo imeamua kuanza kugawa mashine hizi ili kuondokana na tatizo la kutotoa risiti za mauzo kwa wafanyabiashara hao ambao walio wengi walikuwa na kisingizio cha kutokuwa na mashine hizo”. Alisema Kidata.
Kamishna Kidata ameongeza kuwa Mamlaka yake imeshaagiza mashine hizo na zipo tayari kuanza kugawiwa mwezi huu kwa wafanyabiashara  hao ikiwa ni awamu ya kwanza ya ugawagaji wa mashine hizo ambao utafanyika nchi nzima.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeazimia kugawa mashine laki mbili kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za kuweza kukusanya mapato yatokanayo na kodi za biashara kwa urahisi na ufanisi mkubwa.

Wafanyabiashara zaidi ya 300 wakamatwa kwa kutotoa risiti za EFD’S.

TRA 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata  akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato nchini.
……………………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewakamata zaidi wafanyabiashara 300 kwa kosa la kutotumia mashine za (Electronic Fiscal Devices) EFD’S katika biashara zao.
Akizungumzia na waandishi wa habari  Jijini Dare s Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema mamlaka yake imefanya uchunguzi wa kina na kuwabaini wafanyabiashara hao katika maeneo mbalimbali nchini wakikiuka agizo la kuwa na mashine hizo.
“ Tumeshaanza kuwapeleka mahakamani wafanyabiashara ambao wanakwepa kulipa kodi kwa kuuza bidhaa bila risiti na pia tumetaifisha bidhaa mbalimbali zilizoingizwa nchini kwa njia ya magendo na kukwepa kodi “ Alisema Kidata.
Kamishna Kidata amefafanua kuwa mamlaka haitowavumilia wafanyabiashara wanaoikosesha mapato Serikali kwa kuuza na kutoa huduma bila risiti za EFD’s kwa makusudi na hasa wale wafanyabiashara wanaouza kazi za wasanii bila stempu za kodi pamoja na wafanyabiashara wanaojihusisha na magendo.
Vilevile amefafanua kuwa, kwa wafanyabiashara waliopelekwa mahakamani mara baada ya kumalizika kwa kesi zao na kupewa adhabu ya kulipa faini, wakibainika tena kurudia makosa hayo adhabu kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kifungo cha miaka mitatu jela kwa kukaidi agizo la Serikali.
Aidha, Mamlaka imetoza faini ya Shillingi Mil 746 kwa wafanyabiashara waliokutwa na makosa mbalimbali yakiwemo kutotumia mashine za kielotroniki za EFD’s , kuingiza bidhaa kimagendo na kuuza kazi za wasanii bila ya stempu ya kodi.
Mamlaka inatoa wito kwa wananchi wote  kuwa mabalozi wa kodi na kichocheo cha ukusanyaji wa mapato kwakutimiza wajibu wao wa kudai risiti  wanaponunua bidhaa au kupatiwa  huduma mbalimbali.Na Raymond

TUHUMA DHIDI YA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KUHUSU UTAFUNAJI WA MAMILIONI YA FEDHA

index 
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimesikitishwa na habari zilizochapishwa na gazeti la RAI Toleo la 1249 la tarehe 5 – 11 Mei 2016 ambazo ni za upotoshaji.
Tunapenda kufafanua kuwa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinaeleza kuwa, Chuo cha Usimamizi wa Fedha kilipokea fedha za ziada kutoka Wizara ya Fedha kwa ajili ya mishahara na fedha hizo zilishapangwa kurudishwa ndani ya mwaka wa fedha 2015/2016 kama ripoti ya Mkaguzi ilivyoagiza katika mwaka wa fedha wa 2014/2015.  Kwa hiyo fedha hizo hazijatafunwa wala kupotea.
Kuhusu ukusanyaji wa madeni yaliyoripotiwa, nusu ya deni ni karo ya wanafunzi wanaolipiwa na Bodi ya Mikopo na fedha hiyo ililipwa Chuoni ndani ya mwaka wa fedha 2014/2015.  Madeni mengine ni ya wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali na madeni hayo yanafutwa kwa kufuata taratibu za kifedha (Financial Regulation) kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali alivyoelekeza.
Ufanunuzi huu ulitolewa kwa mwandishi wa gazeti hili (Bwana Gabriel Mushi) mnamo tarehe 04-05-2016 alipoongea na Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala.
Kwa kumalizia Chuo cha Usimamizi wa Fedha kinafanya kazi zake kwa kufuata taratibu zilizowekwa na kwa zaidi ya miaka 30 mfululizo Chuo kimepata hati safi za mahesabu (Clean Audit Report) kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG).
Taarifa hii imetolewa na

3 ZA AZAM FC SAWA, BADO ZA COASTAL UNION

DSC_00225Mwenyekiti wa Mbeya City  fc, Mussa Mapunda amelipongeza shirikisho la  soka Tanzania  TFF kwa hatua yake ya kuipoka  pointi 3 timu ya Azam Fc na  kuziweka kwa timu yake  kufutia  makosa yaliyofanywa na timu hiyo ya  Chamazi Complex  kumchezesha mchezaji Erasto Nyoni aliyekuwa na zuio la kadi tatu za njano.
Muda mfupi uliopita Mapunda ameimbia mbeyacityfc.com kwamba kwa kosa  hilo City ilistahili kupata ushindi huo wa bao 3 na pointi 3 kama ambavyo kanuni za ligi  zinavyoelekeza na kutoa  angalizo kwa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania  bara kuongeza umakini katika  kutunza  kumbukumbu  za adhabu  au makosa mbalimbali kwa wachezaji wake.
“Kwenye hili nalipongeza shirikisho, hakika wametenda haki, na ninawaomba  waendelee kusimama kwenye misingi ya haki, ni haki yetu kupata pointi 3 baada ya Azam fc kuchezesha mchezaji mwenye adhabu ya kadi 3 ambaye ni wazi hakustahili kucheza mchezo ule, hata sisi tumekutana na hali hii katika nyakati tofauti lakini hatukuwahi kuthubutu kumchezesha mchezaji  mwenye adhabu  hata kama alikuwa ni muhimu kikosini” alisema.
Akiendelea zaidi Mwenyekiti Mapunda alisisitiza vilabu kuwa makini na matukio ya aina hii  huku pia  akiikumbusha TFF kuendele kuchukua hatua kama hizi.
Katika hatua nyingine  Mapunda amesema kuwa  bado anaamini TFF itaitendea haki City kwa kuchukua hatua kama hizi kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union uliovunjika  dakika mwisho za kipindi cha pili baada ya kutokea kwa vurugu kubwa  uwanjani zilizosababishwa  na mashabiki wa timu hiyo ya Tanga.
“Naamini TFF watatutendea haki kwenye hili pia,mchezo ule ulikuwa na matukio mengi ya ajabu ambayo yalimfanya mwamuzi kushindwa kumaliza mchezo, risasi za moto zilipigwa  uwanjani, , sisi bado tunasubiri pointi tatu zingine kutoka kwenye mchezo ule, kwa sababu mnyonge mnyongeni  haki yake mpeni”, alimaliza.

Timu ya Taifa ya mchezo wa Roll yaenda Kenya


ROL1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nadia House of Beuty ,Nadia Azmat akionesha viatu vitakavyotumika kuchezea mchezo wa Roll kwa nchi zaAfrika utakakaofanyika Kenya.
ROL2Meneja Mauzo wa Kampuni ya Isere Sports inayouza vifaa vya michezo, Ismail Bura (kulia) akionesha Kocha Mkuu wa mchezo wa Roll, Aurher Haule sampuli ya sare za Taifa zinazofaa kuvaliwa na wachezaji wanapokuwa nje ya nchi.
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa ya Mchezo wa mpira wa kuteleza(Roll Ball) imeondoka jana ikiwa na wachezaji 12 kwenda Kenya kwenye mashindano ya kimataifa ya Afrika yatakayoanza leo mjini Nairobi.
Kocha Mkuu wa timu hiyo,Arthur Haule alisema jana Dar es Salaam kuwa wamejiandaa kutwaa ubingwa wa mchezo huo utakaoshirikisha timu kutoka mikoa sita.
Alisema safari yao ambayo imedhaminiwa na Kampuni ya Nadia House of Beuty inaondoka na wachezaji 12 na viongozi wawili.
Aliwataja wachezaji watakaowakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ni Mohammed Athumani, Emmanuel Thomas, Hamisi Salum, Rajab Kassim, Omari Madohola, Yakhe Shaaban,Jonas Emmanuel, Fahadi Waziri, Said Abdallah,Kassim Rajab, Feruzi Juma na Clement Andrea.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nadia House of Beuty, Nadia Azmat akikabidhi vifaa vya michezo kwa safari hiyo aliwataka watanzania wengine kusadia michezo ambayo haina umaarufu ili kuibua vipaji mbalimbali vya vijana.
Nchi zinazoshiriki mashindanoi hayo ni wenyeji Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania, Afrika Kusini na Zambia.

MTOTO WA KITANZANIA ASHIRIKI KATIKA FILAMU YA KIMAREKANI

Tasnia ya filamu Tanzania inazidi kukua kwa kasi, si tu nyumbani hata nje ya nchi watanzania wanazidi kungara.
Safari hii mtoto wa watanzania wenzetu aitwaye Evan Byarushengo amabahatika kupata nafasi ya kushiriki katika filamu ya kimarekani iitwayo THE REAL MVP: The Wanda Durant Story.
Filamu hii inajaribu kuonyesha jinsi mama wa mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Kevin Durant alivyohangaika kuwakuza watoto wake mpaka kufikia kuwa mastaa. Evan anaigiza kama Kevin Durant akiwa mtoto wa miaka 7. Waigizaji wakuu wa filamu hii ni pamoja na Cassandra Freeman anayeigiza kama mama Evan; Pauletta Washington (mke wake Denzel Washington) ambaye anaigiza kama bibi 
yake Evan na wengine wengi.
Juu, katika clip mojawapo Evan akifanya mazoezi ya kucheza mpira wa kikapu. Nyuma ni director wa filamu George Nelson na wasaidizi wake. 
Juu, Evan akiwa anaongea na bibi yake (Pauletta) na mtoto anayeigiza kama kaka yake Kevin aitwaye Tony. 
Juu Evan(aliyechuchumaa) akipitia script mbele ya wenzake. 
Evan na mwenzake mwishoni walipata bahati ya kuonana na mama yake Kevin ambaye stori ya filamu inamuigiza.
Unaweza kuona clips za hiyo movie kupitia links hizi za youtube. 
Kwa walio Marekani na Canada, movie hiyo itaonyeshwa siku ya Ijumaa na Jmosi kupitia Lifetime Channel 8/7c
Tuendelee kumwombea mtanzania mwenzetu aende mbele zaidi ili tuzidi kuipeperusha bendera yetu. Evan amefanya audition nyingi kwahiyo Mungu akipenda ataonekana kwenye matangazo ya kibiashara na filamu zaidi. 
Asante sana,
Dr. Philomena Ishengoma & Godfrey Byarushengo
Wazazi wa Evan

JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA AFUNGUA MAFUNZO MAALUMU KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza. Mafunzo hayo yameanza leo na yanatarajia kufikia tamati kesho Mei 07,2016.
……………………………………………………………………………………
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba, amewataka watumishi wa Mahama Mkoani
Mwanza kutimiza wajibu wao kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na kwa wakati.
Mhe.Makaramba ameyasema hayo hii leo Jijini
Mwanza, wakati akifungua Mafunzo Maalumu ya huduma kwa  Watumishi
wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza.
Amesema Mafunzo hayo yamekuja kwa
wakati ikizingatiwa kwamba Mahakama ya Tanzania kwa sasa inaendelea na
maboresho ya Utendaji kazi wake kama sehemu ya kuhakikisha kwamba inatoa huduma
iliyo bora kwa wananchi.
 
Simon Berege, amesema mafunzo hayo yanaendeshwa katika Kanda zote za
Mahakama nchini, baada ya utafiti uliofanyika mwaka 2014 kuonyesha kwamba kuna ugumu
katika upatikanaji wa habari za mahakama kwa umma hata kama habari hizo siyo za
siri.
“Tunaipongeza Mahakama kwa hatua hii
ya kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wake na kutoa taarifa muhimu kwa
wananchi maana mihimili mingine imekuwa ikiminya upatikanaji wa taarifa zake
hata kama taarifa hizo siyo za siri”. Amesema Berege.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo
hayo wamesema wanatarajia kujifunza mambo mengi ikiwemo kuongeza ujuzi zaidi wa
namna ya kuwahudumia wateja (Wananchi) ili kuwafanya watambue kwamba Mahakama nchini
zinatenda haki.

Mafunzo hayo ambayo yanafadhiriwa na
Shirika la Misaada la Ujerumani FES, yamefanyika Mkoani Mwanza baada ya mafunzo
kama hayo yaliyofanyika katika Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Tabora kuonyesha
yameongeza ufanisi na utendaji wa Watumishi wa Mahakama katika kuwahudumia
wananchi hususani katika utoaji wa taarifa kwa umma ambapo yanawajumuisha
Mahakimu, Watunza Kumbukumbu pamoja na Maafisa Utumishi wa Mahakama.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Continue reading →

RAIS DK. SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI MTEULE NCHINI JAPAN

chk1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza  na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan Mhe,Mathias M.Chikawe  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais,leo,[Picha na ikulu.]
chik2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan Mhe,Mathias M.Chikawe  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao,[Picha na ikulu.]
…………………………………………………………………………………………………

MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WATU WASIOFAHAMIKA JIJINI MBEYA.

ju 
Mtu mmoja mwanaume asiyefahamika jina, mwenye umri kati ya miaka 25 hadi 28 alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

TAHAFE YATANGAZA TAASISI 31 ZITAKAZO PELEKA MAHUJAJI KWENDA KUHIJI MAKKA

Mwenyekiti wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE), Sheikh Abdallah Khalid (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu mchakato wa kwenda kuhiji mwaka huu 2016. Kushoto ni Katibu wa Taasisi hiyo, Dk. Ahmed Twaha na kulia ni Mjumbe, Hassan Ali. 
Katibu wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE), Sheikh Abdallah Khalid , akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
……………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoa Taarifa ya vifo vya uzazi kila robo mwaka.

um1 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam 5 Mei, 2016.
um2 um4 
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen akiongea na Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam, 5 Mei, 2016.
um5 
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen akiongea na Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam, 5 Mei, 2016.
um6 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) pamoja na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen wakifurahia burudai toka kwa Vijana wakiotumbuiza stejini (hawapo pichani) wkaati wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya uliofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam 5 Mei, 2016.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

MAMIA WAMZIKA ANDREW NICKY SANGA (KING DREW) DODOMA

Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga Enzi za Uhai wake
Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga (King Drew) ukiwa unawasili katika uwanja wa Mashujaa kwa ajili ya Ibada na Kutoa kutoa Heshima za mwisho
Ibada ikiwa inaanza Baada ya Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga kuwasili
 Kwaya wakiwa wanaimba wimbo wao wakati wa kujiandaa na ibada

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI

Z1 
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed ambae alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Profesa Amina Abdulkadr, (kulia) Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu  Wizara hiyo Halima Maulid Salum.
Z2Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Profesa Amina Abdulkadr akisoma risala ya wakunga katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Z3Mwakilishi wa Shirika linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) akitoa salamu za Shirika hilo kwenye maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Z4 
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani.

WAAMUZI MECHI YA YOUNG AFRICANS, ESPERANCAWAAMUZI MECHI YA YOUNG AFRICANS, ESPERANCA

CAF

Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey, Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaozikutanisha timu za Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na GD Sagrada Esperanca ya Angola.
Lamptey kutoka jiji la Accra, Ghana atasaidiwa na raia wenzake wa nchi hiyo kuchezesha mchezo huo Na. 99. Mwamuzi Msaidizi Na. 1 (line 1) ni David Laryea wakati Mwamuzi Msaidizi Na. 2 (line 2) ni Malik Alidu Salifu.
Mwamuzi Msaidizi mezani (Fourth Official) ni Cecil Amately Fleischer huku Kamishna wa mchezo huo, akiwa ni Asfaw Luleseged Begashaw wa Ethiopia.
Viingilio na upatikanaji wa tiketi utatangazwa kesho Ijumaa Mei 6, 2016 na uongozi wa klabu ya Young African mara baada ya mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili. Mkutano wa makocha hao utafanyika saa 5.00 mchana kwenye Ukumbi wa mikutano wa TFF.
Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey, Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaozikutanisha timu za Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na GD Sagrada Esperanca ya Angola.
Lamptey kutoka jiji la Accra, Ghana atasaidiwa na raia wenzake wa nchi hiyo kuchezesha mchezo huo Na. 99. Mwamuzi Msaidizi Na. 1 (line 1) ni David Laryea wakati Mwamuzi Msaidizi Na. 2 (line 2) ni Malik Alidu Salifu.

WAFANYAKAZI WA NHC WAPANDA MITI KATIKA MAKAZI YALIYOUZWA WANANCHI KIBADA NHC

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susani Omari akizungumza na Mameneja wa NHC na Wakurugenzi wakati wa zoezi la kupanda miti katika Estate ya Kibada ikiwa ni jitihada za NHC kuboresha mazingira ya eneo hilo linalokaliwa na wakazi takribani 1,000 katika nyumba zipatazo 218 za gharama nafuu. EMT wote(Directors, Regional Managers &  Line Managers) pia wametembelea miradi ya Kawe, Morocco Square, Victoria Place, Eco Residence na Kibada ambako kumefanyika shughuli hiyo ya upandaji miti.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, James Rhombo akipanda mti wa mchikichi katika eneo la makazi la NHC Kibada Kigamboni maarufu kama Kigamboni Housing Estate.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TAMICO), Lilian Reuben na Meneja wa NHC, Mtwara, Joseph John wakipanda mti katika eneo la makazi la NHC Kibada Kigamboni maarufu kama Kigamboni Housing Estate.
Zoezi la kupanda miti likiendelea katika eneo la makazi la NHC Kibada Kigamboni maarufu kama Kigamboni Housing Estate.
 Mandhari ya kupendeza ya nyumba za makazi za  NHC Kibada Kigamboni maarufu kama Kigamboni Housing Estate inavyoonekana mchana huu, hizo ni barabara, mataa na mitaro ya nyumba hizo zinavyoonekana leo hii.
 Mandhari ya kupendeza ya nyumba za makazi za  NHC Kibada Kigamboni maarufu kama Kigamboni Housing Estate inavyoonekana mchana huu, hizo ni barabara, mataa na mitaro ya nyumba hizo zinavyoonekana leo hii.
Wajumbe wa ziara hiyo wakisikiliza kwa makini maenelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, NHC, Haikamen Mlekio wakati wajumbe hao walipotembelea eneo hilo la makazi.
 Mandhari ya kupendeza ya nyumba za makazi za  NHC Kibada Kigamboni maarufu kama Kigamboni Housing Estate inavyoonekana mchana huu, hizo ni barabara, mataa na mitaro ya nyumba hizo zinavyoonekana leo hii.
 Mandhari ya kupendeza ya nyumba za makazi za  NHC Kibada Kigamboni maarufu kama Kigamboni Housing Estate inavyoonekana mchana huu, hizo ni barabara, mataa na mitaro ya nyumba hizo zinavyoonekana leo hii.

Timu ya Menejimenti ya NHC nchi nzima yatembelea miradi ya shirika hilo jijini Dar es salaam

1 
Meneja Mradi wa Shirika la nyumba la Taifa  NHC Kawe unaokwenda kwa jina la 711 Injinia Samwel Metil akitoa maelezo kwa  Timu ya Menejimenti ya NHC wote(Directors, Regional Managers &  Line Managers) wakati walipotembelea miradi ya 711 Kawe , Morocco Square, Victoria Place, Eco Residence na Kibada ambapo ambapo pia watafanya pia kazi katiia miradi hiyo Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni  kuwafahamisha juu ya maendeleo na changamoto za miradi hiyo.
2
Mmoja wa Mainjinia wa Mradi wa 711 Kawe Bw.Kishor Hirani akimelezea jambo Meneja mradi Injinia Samwel Metil wakati menejimenti ya shirika hilo ilipotembelea katika mradi huo.
3
Wakuu wa vitengo mbalimbali na mameneja wa mikoa wakitembelea mradi wa 711 Kawe leo.
4
Mmoja wa Mameneja wa NHC kutoka mkoani Dodoma Bw. Itandula Gambalagi pamoja na wenzake wakiwasili kutembelea mradi wa Morocco Square.
5 6Wakipatiwa maelezo katika mradi wa Morocco SquareMorocco Square
7 
Mameneja hao wakifuatilia maelezo ya mradi wa Morocco Square
8
Muungano Saguya kulia Yahya Charahani kushoti na Itandula Gambalagi wakijadiliana jambo wakati walipotembelea mradi wa 711 Kawe pamoja na wenzao.
9
Jengo la Mradi wa Eco Residents ambalo limekamilika kwa asilimia  99%.
11 
Ujenzi wa mradi wa 711 Kawe ukiendelea.

CCM YAKANUSHA UZUSHI ULIOENEA KUHUSU MCHAKATO WA UENYEKITI WA CCM

index 
Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi.
Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti.
Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu.
Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale. Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo. Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa.
Tunawataka wana-CCM wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu wenye nia mbaya na CCM. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila ya mafanikio.
Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.
Aidha, tunapenda kukanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. Hapajawahi kufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. Hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya Viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM hayana msingi wowote.
Kamati Kuu iliteua Wabunge wanne kugombea na kuwaachia Wabunge wa CCM kuamua. Kuhusisha Viongozi na hasa kuzua kuwepo kutokuelewana ni jambo la kusikitisha.  Ni taarifa ya uongo yenye nia ovu kwa CCM na Viongozi wake.
Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli. Waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza kwa watu. Waheshimu maadili ya kazi zao.
Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhi kijiti cha uenyekiti katika CCM na wala hautakuwepo.
Imetolewa na;
Ndugu Christopher Ole Sendeka   
                  MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
05/05/2016

No comments :

Post a Comment