Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(Mb) akiongoza kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Kikao hicho kimefanyika leo Mei 30, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma(kulia) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani). Wa pili kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP, John Casmir Minja(kulia) ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, DIGP, Abdulrahmani Kaniki(wa kwanza kushoto) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Adengenye.
Watendaji
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Maafisa Waandamizi wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia kwa makini kikao kazi
kilichofanyika chini ya Uenyekiti wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni leo Mei 30, 2016 Mkoani Dodoma(Picha zote
na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
UONGOZI WA UDSM WAANZA KUWEKA TAA MABIBO HOSTEL.
UONGOZI Chuo Kikuu cha Dar es
salam unatarajia kununua taa za dharura 12 kwa ajili ya kukabiliana na
tatizo la giza katika Hosteli ya Mabibo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Naibu Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) anaeshughulikia masuala ya Utawala Prof.David Alfred Mfinanga
wakati wa mahojiano na Idara ya Habari.
Alisema kuwa tatizo la giza nene
katika eneo hilo la lango kuu la kuingia Hostel za mabibo mpaka eneo
lile la maegesho ya magari lipo mbioni kupatiwa ufumbuzi baada ya
taratibu za ununuzi kukamilika.
Alisema kuwa kukamilika kwa uwekaji wa taa hizo za dharura zitapunguza kabisa tatizo hilo.
Aidha, Prof.David Alfred Mfinanga
alisema kuwa katika mpango wa muda mrefu wa kutatua tatizo hizo
uongozi wa UDSM unatarajia kuweka umeme wa jua ambao utapunguza gharama
za kulipia umeme na hivyo kuwa na umeme wa uhakika.
Hostel hizo za kisasa
zilizojengwa miaka michache iliyopita na Shirika la Hifadhi za
Jamii(NSSF) zimesaidia kupunguza tatizo la makazi lililopo kampasi kuu
ya Chuo kikuu(mlimani) lakini kasoro hizi za kukosa umeme zinahatarisha
eneo hilo kugeuka kuwa la ubakaji na hata ukabaji kwa wanafunzi na
wageni.
RAIS WA ZANZIBAR MH. DK. SHEIN KATIKA ZIARA YA KICHAMA KISIWANI PEMBA
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Wete Abrahmani Makame Shehe alipokuwa akisoma risala ya wilaya wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein alipozungumza na Wanachama wa CCM Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo kwa ajili ya kuwapongeza kutokana na ushindi katika uchaguzi wa marudio wa mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
Baadhi ya WanaCCM wakitetemka gari walipofika Viwanja vya Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein alipozungumza na Wanachama wa CCM Wilaya hiyo leo kwa ajili ya kuwapongeza kutokana na ushindi katika uchaguzi wa marudio wa mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
Viongozi wa Mashina,Wenyeviti na Makatibu wa maskani wakiwa ni Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Wete wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein alipozungumza na viongozi hao leo wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba kuwapongeza na kuwashukuru kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 30/05/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein akipokea risala ya Wilaya kutoka kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Wete Abrahmani Makame Shehe katika mkutano wa Viongozi wa Chama Wilaya ya Wete uliofanyika leo katika ukumbi wa skuli ya Kiislamu Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wete Bw.Kombo Hamadi Yussuf alipokuwa
akiwasalimia Viongozi wa CCM wa Mashina,Matawi na Maskani waWilaya ya
Wete wakati wa Mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed
Shein alipowashukuru wana CCM wa Wilaya hiyo kwa ushindi katika uchaguzi
wa marudio wa Mwezi Machi mwaka huu uliofanyika leo katika ukumbi wa
Skuli ya Kiislamu Wilaya ya Micheweni Pemba,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kasakzini Pemba Khadija Nassor Gulam alipokuwa akizungumza machache na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa wakati wa Mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein alipowashukuru wana CCM wa wilaya hiyo kwa ushindi katika uchaguzi wa marudio wa Mwezi Machi mwaka huu uliofanyika leo katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu Wilaya ya Micheweni Pemba,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipokuwa akiwasalimia Viongozi wa CCM wa Mashina,Matawi na Maskani wa Wilaya ya Wete walipohudhuria katika mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza Viongozi hao uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein leo katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu ya kiuyu Wilaya ya michweani Mkoa wa Kaskazini Pemba,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa katika mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza Viongozi wa CCm wilaya ya wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu ya kiuyu Wilaya ya Michweani Mkoa wa Kaskazini Pemba,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
MUSA MCHEZAJI BORA WA MEI VODACOM
Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Mei 2016.
Musa katika kinganyiro hicho aliwapiku Donald Ngoma wa Yanga na Ali Nassoro wa Mgambo Shooting. Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Musa alicheza mechi zote tatu za timu yake na kufunga jumla mabao manne; mawili katika kila mechi.
Kwa kushinda tuzo hiyo ya Mei ambayo ni ya mwisho kwa msimu huu kwa wachezaji bora wa mwezi, Musa atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Washindi wengine wa tuzo hiyo ya mwezi kwa msimu huu wa 2015/2016 ambao mechi zake za mwisho zilichezwa Mei 22 mwaka huu ni Hamisi Kiiza wa Simba (Septemba), Elias Maguli wa Stand United (Oktoba), Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba), Shomari Kapombe wa Azam (Januari), Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari), Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi) na Juma Abdul wa Yanga (Aprili).
Musa katika kinganyiro hicho aliwapiku Donald Ngoma wa Yanga na Ali Nassoro wa Mgambo Shooting. Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Musa alicheza mechi zote tatu za timu yake na kufunga jumla mabao manne; mawili katika kila mechi.
Kwa kushinda tuzo hiyo ya Mei ambayo ni ya mwisho kwa msimu huu kwa wachezaji bora wa mwezi, Musa atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Washindi wengine wa tuzo hiyo ya mwezi kwa msimu huu wa 2015/2016 ambao mechi zake za mwisho zilichezwa Mei 22 mwaka huu ni Hamisi Kiiza wa Simba (Septemba), Elias Maguli wa Stand United (Oktoba), Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba), Shomari Kapombe wa Azam (Januari), Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari), Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi) na Juma Abdul wa Yanga (Aprili).
RCL YAENDELEA KUTIMUA VUMBIt
Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu wa 2015/2016 inaendelea vizuri katika vituo vinne vya Kagera, Morogoro, Singida na Njombe ambapo itafikia tamati Juni 6 mwaka huu.
Timu sita zitapanda daraja
kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2016/2017. Timu hizo ni zile
zitakazoongoza kila kundi, na washindwa bora (best losers) wawili kutoka
makundi mawili tofauti
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limeweka waangalizi wake katika kila kituo, na
litawachukulia hatua watu wote watakaobainika kutumia michuano hiyo
kuchafua viongozi.
Mtwivila City ya Iringa inaongoza
kituo cha Njombe ikiwa na pointi sita baada ya kucheza mechi tatu.
Katika kituo hicho kesho (Mei 31) kutakuwa na mechi kati ya Jangwani FC
ya Rukwa na Nyundo FC ya Katavi kwenye Uwanja wa Amani.
Timu inayoongoza kituo cha
Morogoro ni Namungo FC ya Lindi yenye pointi saba kwa mechi tatu. Kesho
(Mei 31) ni mechi kati ya Makumbusho FC na Sifapolitan, zote za Dar es
Salaam itakayofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kitayose ya Kilimanjaro inaongoza
kituo cha Singida ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi zote
tatu ilizocheza. Kesho (Mei 31) kwenye kituo hicho kutakuwa na mechi
kati ya Stand FC ya Tabora na Murusgamba ya Kagera itakayochezwa Uwanja
wa Namfua
Mpaka sasa vinara wa Kituo cha
Kagera ambacho mechi zake zinachezwa Uwanja wa Vijana mjini Muleba ni
Mashujaa FC ya Kigoma yenye pointi saba.
MKWASA AISHITUKIA MISRI, WANYAMA NA KAZIMOTO WATOA NENO
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba mchezo ujao kati ya Mapharao wa Misri na Taifa Stars, utakuwa ni fainali ya kuamua taifa litakalofuzu katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON hapo mwakani kutoka kundi G.
Akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya mchezo kati ya Harambee Stars ya Kenya na Taifa
Stars ya Tanzania Mei 29, 2016, uliofanyika Uwanja wa Moi Kasarani,
Mkwasa maarufu kama Master anasema kwa msimamo na hali ilivyo kwa sasa,
“Najua Misri wanatufuatilia. Na hata Kenya kwa siku zote tatu
walikuwako. Najua Misri wanahitaji sare ili wafuzu kwa fainali hizi,
lakini hawataipata Tanzania.”
Mkwasa anasema mchezo dhidi ya
Misri, ana uhakika vijana wake watajitahidi ili kupata matokeo mazuri
baada ya Jumapili kufanya vema dhidi ya Harambee Stars waliocheza mechi
hiyo mbele ya mashabiki wao wachache ambao pia hawakuchangamka kama wale
wa Tanzania ambao licha ya kuwa ugenini walichangamsha mji na uwanja.
Wakati Misri wana pointi saba,
Taifa Stars ina pointi moja na hivyo wa kuibania au kupindua matokeo ya
Misri isiende AFCON mwakani, basi ni Tanzania hasa kama itawafunga
Mapharao Jumamosi kabla ya kwenda Nigeria Septemba, mwaka huu kucheza na
Nigeria.
“Kama nilivyosema, Misri
wanakujawanahitaji pointi moja. Lakini sisi tunahitaji pointi tatu.
Mchezo wa leo unatosha kuona mapungufu (upungufu). Maana ilikuwa mechi
ngumu iliuyojaa nyota wote wa Kenya ambao ni professionals, lakini mimi
nilikuwa na local based players na matokeo yamekuwa hayo.
“Tilianza kufunga bao, lakini
wakarudisha. Bora mchezo umeishia hivi maana najua Wakenya hawana
uvumilivu, tungewafunga hapa sijui kama tungetoka salama,” amesema
Mkwasa ambaye baadhi ya waandishi, hususani wale wa Kenya walianguka
kicheko kuashiria kuwa kuna matatizo katika utawala wa soka.
Mkwasa anasema ana taarifa namna
ambavyo Misri wanaifuatilia Taifa Star hususani ukusanyaji wa video kwa
ajili ya kuona aina ya soka la Tanzania, huku akisema: “Hawatafanikiwa
kwa sababu soccer is the game of different approach (Soka ni mchezo
wenye mifumo tofauti). Hivyo tulivyocheza na Kenya sivyo nitakavyocheza
na Misri, nitakuwa na approach yake.”
BASATA, HAANNEEL WAZINDUA MATUKIO YA SIKU YA MSANII KWA MWAKA 2016
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Haakneel Production Emmanuel Mahendeka ambayo ni
waandaaji wa Siku ya Msanii akimwongoza Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel kutia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kuzindua
matukio ya Siku ya Msanii (SYM, 2016) kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa
Alliance Francaise mwishoni mwa wiki.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ndilo mbunifu na mmiliki wa maadhimisho ya Siku ya Msanii nchini Godfrey Mngereza (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bi. Leah Kihimbi (Katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni mwendeshaji wa Siku ya Msanii ya Haakneel Production Emmanuel Mahendeka mwishoni mwa wiki kwenye uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 katika Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam.
Msanii maarufu wa kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto akisaini kitabu cha wageni kabla ya kushuhudia hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise ulioko jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bi.
Vivian Shalua (Kushoto) akifuatilia kwa makini moja ya matukio
yaliyokuwa yakiendelea kwenye hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya
Msanii kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa Alliance Francoise mwishoni mwa
wiki. Kushoto ni Msanii wa Sanaa za Ufundi Gozbetha Rwezaula.
Marais wa Mashirikisho manne ya Sanaa nchini kutoka kushoto Symon Mwakifamba (Filamu), Adrian Nyamangale (Ufundi), William Chitanda maarufu kama MC Chitanda (Sanaa za Maonesho) na Addo November (Muziki) wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali ya uzinduzi wa matukio ya Siku ya Msanii mwaka kwa mwaka 2016
Kikundi cha Sanaa cha Safari kikitoa burudani kwenye hafla ya Uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam
Miss Chang’ombe kuzinduliwa rasmi Juni 02, 2016
Mratibu
Miss Chang’ombe 2016 kutoka Kampuni ya SG Entertainment Adam
Hussein(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam kuhusu uzinduzi wa Mashindano ya Urembo Kitongoji cha Chang’ombe
yanayotarajiwa kuzinduliwa Juni 02, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha
Habari na Mawasiliano wa kampuni hiyo Victor Mkumbo na Kulia ni Meneja
Masoko Geofrey Msala.(Picha Na: Lilian Lundo)
……………………………………………………………………………………………………..
Na. Lilian Lundo – MAELEZO
Kampuni ya SG Entertainment
kuzindua mashindano ya urembo ya Miss Chang’ombe Juni 2, 2016 katika
Ukumbi wa MPOA AFRIKA uliopo Davis Corner Tandika jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo
cha Habari na Mawasiliano wa kampuni hiyo Victor Mkumbo alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa watakaoshiriki
mashindano hayo ni wakazi wa Chang’ombe na Temeke peke yake.
“Washiriki wa mashindano haya ni
wakazi wa Chang’ombe na Temeke, nje ya hapo haturuhusu mtu kutoka eneo
lingine kushiriki, lengo ikiwa ni kuwapa fursa wakazi wa maeneo haya”,”
anasema Mkumbo.
Kwa upande wake Mratibu wa Miss
Chang’ombe 2016 Adam Hussein anasema kwamba nafasi za warembo kushiriki
bado zipo na fomu za kujiunga zinapatikana CDS PARK(TCC Club)
Chang’ombe, MPOA AFRIKA Davis Kona na duka la nguo CHILU Latest Wear
Temeke Mwisho kwa gharama ya shilingi 5,000 tu.
Aliongeza kuwa fainali ya
mashindano hayo itafanyika Julai 21, 2016 katika viwanja vya CDS
Park(TCC Club) Chang’ombe ikisindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii
mbalimbali akiwemo Galatone ,mwadada Chemikal.
Washindi watano kutoka Kitongoji
cha Chang’ombe wataungana na warembo kutoka vitongoji vya Kigamboni na
Mbagala ili kutafuta warembo wa Temeke watakao wakilisha katika
mashindano ya kitaifa ya kumtafuta mrembo atakayeiwakilisha Tanzania
katika mashindano ya Mrembo wa Dunia mwaka huu.
DAWASCO YAKANUSHA GARI YA DAWASCO KUJERUHI WATATU
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imekanusha taarifa iliyoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya gari linalodaiwa kuwa la DAWASCO lenye namba za usajili T 369 BUZ ambalo liliparamia kituo cha mabasi cha Mbuyuni kilichopo maeneo ya Namanga Oysterbay na kujeruhi watu watatu.
Akizungumzia
tukio hilo, Kaimu Meneja uhusiano wa Dawasco, Bi. Everlasting Lyaro
amesema kuwa gari hilo sio mali ya Shirika la Majisafi na Majitaka Dar
es salaam, bali ni moja ya gari linalomilikiwa na watu binafsi ambao
wanasaidiana na Dawasco katika kusambaza huduma ya maji maeneo ambayo
huduma hiyo bado haijafika kwa kutumia magari makubwa ya kusambaza Maji
(maboza) ambayo yamesajiliwa na kuwekwa nembo ya Dawasco.
“Gari
hili sio mali ya Dawasco, bali limesajiliwa na Dawasco na kuwekewa
viambatanisho vyote muhimu ili kusambaza huduma ya Maji maeneo ambayo
mtandao wa Maji haujafika haujafika” alisema Lyaro.
Ikumbukwe
kuwa mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, Dawasco ilianza zoezi maalum la
kusajili visima pamoja na magari yote makubwa ya kusambaza huduma ya
Maji jijini Dar es salaam, ambapo tayari magari makubwa takribani 256 ya
kusambaza huduma ya Maji jijini Dar es Salaam yamekwisha sajiliwa.
Dawasco
inapenda kuvikumbusha vyombo vya habari kuzingatia taratibu za kazi
kwa kuandika taarifa zenye uhakika na ukweli ili kuepuka upotoshaji wa
habari kwa wananchi.
Everlasting Lyaro
Kaimu Meneja uhusiano- Dawasco
022-2194800 au 08001164
Dawasco Makao Makuu
SERIKALI YA CHINA YATOA MSAADA WA MADAWATI YA TSH MILIONI 20,YAMPONGEZA RAIS DR MAGUFULI KWA UCHAPA MKAZI
Balozi wa China nchine Dr Lu Yong,ng akifurahia zawadi alizopewa ,kulia ni mbunge Martha Mlata |
Boga lenye kilo 7 alilopewa balozi wa China Iramba Singida |
Waziri
wa kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akihuka katika ndege
aliyoafiria pamoja na ujumbe wa balozi wa china nchini Dr Lu Yong’ng
alipofanya ziara jimboni kwake Iramba leo na kukabidhi madawati 400 |
waziri Nchemba na mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata wakiungana na balozi wa China nchini Dr Lu Yong,ng kucheza ngoma na wasanii wa Iramba baada ya kupokelewa ofisi za halmashauri ya Iramba |
Sehemu ya madawati iliyotolewa na ubalozi wa China wilaya ya Iramba |
MAKAMU WA RAIS AWASILI NCHINI PAPUA NEW GUINEA KUMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Belize Bw. Wilfered Eliringron wakati Makamu wa Rais alipowasili katika Hoteli ya Airways mjini Papua New Guinea. Makamu wa Rais yupo Nchini Papur New Guinea kwa ajili ya kumwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa siku mbili unaotarajiwa kuanza kesho utakaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. Mkutano huo utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwandaaji Mkuu wa mkutano wa The HL MEETING UN WOMEN unaotarajiwa kufanyika keshokutwa mjini Guinea, Makamu wa Rais yupo Nchini Papur New Guinea kwa ajili ya kumwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa siku mbili unaotarajiwa kuanza kesho utakaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. Mkutano huo utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP). (Picha na OMR Papua New Guinea)
YALIYOJILI KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO LEO MJINI DODOMA
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson
Mwansasu akiongoza kikao cha 32 cha Mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa
kikao cha 32 cha Bunge hilo mjini Dodoma
kikao cha 32 cha Bunge hilo mjini Dodoma
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla akijibu maswali ya wabunge kuhusu sekta ya Afya Bungeni
mjini Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Ukonga (CHADEMA) Mhe. Mwita Mwikwabwe akisoma kitabu cha Kanuni za Kudumu za Bunge ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Mbunge
wa Nzega Mhe. Hussein Bashe (CCM) akizungumza jambo na Mbunge wa
Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kulia) nje ya ukumbi wa
Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha 32 cha mkutano wa tatu wa
Bunge leo mjini Dodoma.
Wanafunzi
wa shule ya Sekondari Barbro Johansson iliyoko jijini Dar es salaam
wakiondoka ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya
kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. Sulemani Jafo akijibu maswali ya wabunge yaliyoelekezwa kwenye
wizara yake Bungeni mjini Dodoma.
Wabunge
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge
kufuatia Naibu Spika wa Bunge hilo Mhe. Tulia Ackson kutangaza
kuliahirisha Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza jambo na Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba nje ukumbi wa Bunge.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akizungumza jambo na wabunge leo mjini Dodoma.
Mbunge
wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto)
akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia
ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mbunge wa Kigoma Mhe. Peter Selukamba akijadiliana jambo na Mbunge wa Nzega mjini Mhe. Hussein Bashe (kushoto)Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu nje ya Ukumbi wa Bunge mjini.
Kikao cha 32 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asubuhi.
Wabunge wakiondoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Naibu Spika kutangaza kuahirisha shughuli za Bunge leo.
Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akimweleza jambo Mwenyekiti
wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi
nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum –
DODOMA
DAWASCO YABAINI WIZI WA MAJI MSIMBAZI BONDENI.
Maelezo ya picha kushoto: Fundi kutoka Shirika la Majisafi na
Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) akiondoa Mpira wa Maji uliokuwa
umeunganishwa kwenye kisima kinyume na utaratibu ambapo walikuwa wakitumia huduma
ya Maji bila kuwa na mita wala akaunti namba ambapo walinzi jengo hilo awali walidai
maji wanayotumia ni ya kisima kwenye jengo lilipo eneo la Msimbazi Bondeni
jijini Dar es Salaam.
Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) akiondoa Mpira wa Maji uliokuwa
umeunganishwa kwenye kisima kinyume na utaratibu ambapo walikuwa wakitumia huduma
ya Maji bila kuwa na mita wala akaunti namba ambapo walinzi jengo hilo awali walidai
maji wanayotumia ni ya kisima kwenye jengo lilipo eneo la Msimbazi Bondeni
jijini Dar es Salaam.
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini
Dar es Salaam (Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji katika eneo la kata ya
Ilala mchikichini mtaa wa Msimbazi Bondeni ambapo walinzi wa jengo hilo
walikuwa wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume cha utaratibu nakujifanya kuwa
wanatumia Maji ya Kisima.
Dar es Salaam (Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji katika eneo la kata ya
Ilala mchikichini mtaa wa Msimbazi Bondeni ambapo walinzi wa jengo hilo
walikuwa wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume cha utaratibu nakujifanya kuwa
wanatumia Maji ya Kisima.
Akizungumza kwenye eneo la tukio Afisa
biashara msidaizi wa Dawasco Ilala Sezi
Mavika amesema kuwa jengo hilo haliishi mtu bali wapo walinzi tu na mwenye
jengo hilo anajulikana kwa jina moja tu la Duncan na kueleza kuwa walinzi hao
wamejiunganishia huduma ya Maji kwa muda mrefu na wanatumia kumwagilia maua
pamoja nakufanyia shughuli za usafi kwenye jengo hilo.
biashara msidaizi wa Dawasco Ilala Sezi
Mavika amesema kuwa jengo hilo haliishi mtu bali wapo walinzi tu na mwenye
jengo hilo anajulikana kwa jina moja tu la Duncan na kueleza kuwa walinzi hao
wamejiunganishia huduma ya Maji kwa muda mrefu na wanatumia kumwagilia maua
pamoja nakufanyia shughuli za usafi kwenye jengo hilo.
“Tumekuta walinzi wameunganisha huduma
ya Majisafi kwenye jengo hili linalomilikiwa na bwana Duncan ambapo
wamejiunganishia kwa kupitisha kwenye kisima kisichofanya kazi nakudai kuwa
Maji wanayotumia niya Kisima ndipo tulipo shirikisha ofisi ya serikali ya mtaa
nakuweza kukagua nakuona kuwa wajiunganishia maji yetu na hawana mita wala
akaunti namba na watumia kwa muda mrefu huduma ya maji ya Dawasco” alisema
Sezi.
ya Majisafi kwenye jengo hili linalomilikiwa na bwana Duncan ambapo
wamejiunganishia kwa kupitisha kwenye kisima kisichofanya kazi nakudai kuwa
Maji wanayotumia niya Kisima ndipo tulipo shirikisha ofisi ya serikali ya mtaa
nakuweza kukagua nakuona kuwa wajiunganishia maji yetu na hawana mita wala
akaunti namba na watumia kwa muda mrefu huduma ya maji ya Dawasco” alisema
Sezi.
Kwa upande wa makamu mwenyekiti wa
serikali ya mtaa ya Msimbazi Bondeni bi Cecilia Kasele ametoa rai kwa wananchi
wote wa mtaa wao kujiepusha na tabia ya wizi wa Maji na kuwasihi wananchi
kuwataja wezi wa Maji kwenye maeneo yao kwani hao ndio wanaofanya wakose huduma
bora ya Maji.
serikali ya mtaa ya Msimbazi Bondeni bi Cecilia Kasele ametoa rai kwa wananchi
wote wa mtaa wao kujiepusha na tabia ya wizi wa Maji na kuwasihi wananchi
kuwataja wezi wa Maji kwenye maeneo yao kwani hao ndio wanaofanya wakose huduma
bora ya Maji.
“Napenda kuwasihi wananchi wote wa
mtaa wangu kujiepusha na tabia ya wizi wa Maji na pia nawasihi wale wote
wanaofahamu wezi wa Maji kujitokeza na kuwataja kwani hao wezi ndio wanasabisha
Dawasco kutokuweza kutoa huduma bora kutokana nakuhujumiwa na watu wachache”
alisema Kasele.
mtaa wangu kujiepusha na tabia ya wizi wa Maji na pia nawasihi wale wote
wanaofahamu wezi wa Maji kujitokeza na kuwataja kwani hao wezi ndio wanasabisha
Dawasco kutokuweza kutoa huduma bora kutokana nakuhujumiwa na watu wachache”
alisema Kasele.
Dawasco inaendelea na operesheni yake
ya kukamata wezi wa Maji kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na hivyo
inawasihi wananchi wote waliojiunganisha huduma ya Maji kinyume na utaratibu
wajitokeze nakusajiwa kihalali pia watumie fursa hii ya zoezi la kuunganishia
wateja wapya kupata huduma ya Maji kihalali, hatua kali za kisheria
zitachukuliwa kwa wale wote watakaokamatwa wamejiunganishia huduma ya Maji
kinyume na utaratibu.
ya kukamata wezi wa Maji kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na hivyo
inawasihi wananchi wote waliojiunganisha huduma ya Maji kinyume na utaratibu
wajitokeze nakusajiwa kihalali pia watumie fursa hii ya zoezi la kuunganishia
wateja wapya kupata huduma ya Maji kihalali, hatua kali za kisheria
zitachukuliwa kwa wale wote watakaokamatwa wamejiunganishia huduma ya Maji
kinyume na utaratibu.
MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAFANYIKA MOROGORO
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Cyprian Kuyava, akitoa neno la shukrani mjini Morogoro, baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu ijayo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uhakiki Mali za Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.
Ezra Msanya, akijibu maswali ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara hiyo, mjini Morogoro, mwishoni mwa juma
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa wilaya hiyo uliofanyika mjini Morogoro, mwishoni mwa juma
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (wa nne kutoka kushoto) akiungana na wafanyakazi wanaounda Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kuimba wimbo wa mshikamano daima, wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza hilo uliofanyika Mjini Morogoro Mwishoni mwa juma. kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Dorothy Mwanyika na kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Amina Hamis Shaban.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakiimba wimbo wa mshikamano daima, mkutano uliopitia bajeti ya Wizara hiyo na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akihutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawako pichani) mjini Morogoro, ambapo amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kufanyakazi kwa bidii na kuacha mazoea ili kutimiza malengo ya kukusanya mapato na kusimamia matumizi yake kikamilifu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (aliyeketi katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika mjini Morogoro, mwishoni mwa juma
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (aliyeketi katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika mjini Morogoro, mwishoni mwa juma
HATIMAYE 19 WAPITA MCHUJO WA KWANZA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA MSIMU WA TANO 2016
Afisa
uhakiki wa ubora kutoka TBS Stela Mroso akisisitiza jambo kuhusu
ushirikiano wao kama Shirika la Viwango la TBS na Oxfam Tanzania
kuhakikisha wanatetea wanawake
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Kilimo Paskarina Kayuma akitoa Shukurani kwa Shirika
la Oxfam Tanzania kwa kuendelea kuwanyanyua wanawake katika kilimo na
amewaomba juhudi hizo ziendelee.
Miongoni
mwa majaji Fredy Njeje kutoka Blogs za Mikoa na Edna Kiogwe mshiriki
wa mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita(ambaye hayupo pichani)
wakielezea namna usaili ulivyofanyika mpaka kuwapata washiriki 19 katika
shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano kwa mwaka 2016
Aliyekuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita Ester
Kulwa akionesha kanda zote ambazo washiriki wametokea.
Kulwa akionesha kanda zote ambazo washiriki wametokea.
Mabalozi
wa Chakula na Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Shirika la Oxfam kwa
upande wa Tanzania Shamim Mwasha ambaye pia ni Fashion Blogger(wa kwanza
kushoto), Jacob Stephen ‘JB’ Msanii Maarufu wa Bongo Movie(wa katikati)
na Khadija Mwanamboka wakitangaza majina 19 ya washiriki wa shindano la
Mama shujaa wa chakula 2016 msimu wa tano.
Baadhi ya wageni wakiwa katika Hafla fupi ya kutangaza majina 19 ya washiriki
katika shindano la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016
katika shindano la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016
Aliyekuwa
Mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pili akizungumza jambo
wakati wa Hafla fupi ya kutangaza washiriki shindano la Mama shujaa wa
chakula msimu wa tano 2016.
Suhaila Thawer ambaye ni ‘Public Forum Officer’ kutoka Shirika la Oxfam Tanzania akitoa neno la Shukurani
Meneja
utetezi kutoka Oxfam Tanzania Eluka Kibona akitoa maelezo kuhusu
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kuwa linaendeshwa Tanzania,Nigeria na
Ethiopia ambapo alisema lengo la shindano ni kutambua mchango wa
wanawake katika mapambano dhidi ya umasikini na kuleta uhakika wa
chakula.
Mabalozi
wa Chakula na Kampeni ya Grow wakiwa katika picha ya pamoja na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Jane Foster (wa kwanza Kulia)
Baadhi ya akina mama waliowahi
kushiriki shindano la Mama shujaa wa Chakula Misimu iliyopita wakiwa na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Jane Foster (wa pili kulia)
……………………………………………………………………………………………………………
Hatimaye 19 watajwa kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa tano kwa mwaka huu 2016,
ambapo fomu 3000 zilizotumwa na wakulima wanawake kote nchini, fomu 1795 zilipitiwa na kuwapata washiriki hao ambao wataanza kutembelewa mmoja mmoja ili kuhakiki iwapo kile walichokijaza kwenye fomu kinaoana na hali halisi.
Mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula 2016, linatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Enguiki kilichopo Monduli mkoani Arusha, kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 16 na kurushwa katika Runinga ya ITV.Baadhi ya akina mama waliowahi kushiriki shindano la Mama shujaa wa Chakula Misimu iliyopita wakiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Jane Foster (wa pili kulia)
Hatimaye 19 watajwa kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa tano kwa mwaka huu 2016,
ambapo fomu 3000 zilizotumwa na wakulima wanawake kote nchini, fomu 1795 zilipitiwa na kuwapata washiriki hao ambao wataanza kutembelewa mmoja mmoja ili kuhakiki iwapo kile walichokijaza kwenye fomu kinaoana na hali halisi.
Mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula 2016, linatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Enguiki kilichopo Monduli mkoani Arusha, kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 16 na kurushwa katika Runinga ya ITV.Baadhi ya akina mama waliowahi kushiriki shindano la Mama shujaa wa Chakula Misimu iliyopita wakiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Jane Foster (wa pili kulia)
Akizungumza wakati wa kutangaza majina hayo, mmoja wa majaji wa shindano hilo Jacob Stephen ‘JB’ ambaye ni
muigizaji maarufu wa Filamu Tanzania alisema katika uchambuzi wa fomu hizo walikuwa ni wanawake wakulima ambao wanaelimu ya juu na baadhi ya viongozi wa kisiasa na wale wadogo wadogo.
muigizaji maarufu wa Filamu Tanzania alisema katika uchambuzi wa fomu hizo walikuwa ni wanawake wakulima ambao wanaelimu ya juu na baadhi ya viongozi wa kisiasa na wale wadogo wadogo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster alisema shindano hilo limeanza
kuendeshwa kuanzia mwaka 2011 na sasa ni msimu wa tano na limefanikiwa
kuwaunganisha wanawake wakulima wadogo wadogo ambao ni asilimia 70 ya
wanawake nchini. Alisema majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na
kuwapata washiriki ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao
ili changamoto zilizopo zitatuliwe.
Alisema
majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki
ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto
zilizopo zitatuliwe. Aliongeza kuwa shindano la mama shujaa wa Chakula
linaendeshwa katika nchi tatu Afrika ikiwemo Nigeria, Ethiopia na
Tanzania.
Ambapo
Tanzania wamepita katika mikoa mbalimbali na kukusanya wanawake
wakulima wadogo wadogo ambao tunaamini kwa kuwa pamoja wanaweza kupaza
sauti kwa watunga sera kuhusu changamoto wanazokutana nazo.
Afisa
Uhakiki wa Ubora TBS, Stela Mroso alisema shirika la viwango nchini
liliungana na Oxfam mwaka jana ili kuhakikisha wanawaleta wanawake
pamoja na kutoa elimu zaidi kuhusu kilimo chenye ubora na mazao
yanayoweza kuwa na viwango vya kimataifa. Alisema bila viwango wanawake
hawawezi kufanya biashara, huku akitoa wito kwao kujitokeza ili
kuangalia ubora wa mazao wanayozalisha. Aliongeza kuwa asilimia 80 ya
wanawake nchini wanajishughulisha na Kilimo kwa hiyo ni muhimu chakula
kinachozalishwa kiwe katika ubora na afya pia kiweze kuzaliswa Kimataifa.
kinachozalishwa kiwe katika ubora na afya pia kiweze kuzaliswa Kimataifa.
Washiriki
wa Mama Shujaa wa Chakula 2016 kuwa ni Betty Nyange (62) Mkoa wa
Morogoro, Monica Charles Mduwile (44) Mkoa wa Dodoma, Neema Gilbet Uhagile (29) Mkoa wa Njombe, Mary Christopher Lyatuu (29) Mkoa wa Arusha, Loyce Daudi Mazengo (39) Mkoa wa Singida, Anjela
Chogsasi Mswete (48) Mkoa wa Iringa, Lucina Sylivester Assey (54) Mkoa
wa Shinyanga, Marta Massesa Nyalama (50) Mkoa wa Kaskazini Unguja,
Christina Machumu (42) Mkoa wa Mara, Happiness Paulo Raulent (35) Mkoa
wa Kagera. Mary Bony Soko (42) Mkoa wa Ruvuma, Mary Ramadhani Mwiru (39)
Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanaid
Alli Abdalla (53) Mkoa wa Mjini Magharibi, Maria Alfred Mbuya (43) Mkoa
wa Mbeya, Eliza Richard Mwansasu (30) Mkoa wa Rukwa, Mwajibu Hasani
Binamu (46) Mkoa wa Mtwara, Eva Haprisoni Sikaponda (40) Mkoa wa Songwe, Hidaya Said Musa (40) Mkoa wa Tanga na
Mwasiti Salim Mazuri (40) Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya Kinondoni.
Mwasiti Salim Mazuri (40) Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya Kinondoni.
Wazee wa Jamii ya Wafugaji na Wakulima Wataka Kulipwa Pensheni kama Wanavyopatiwa Wastaafu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bw. Zubeir Sabatala akizungumza na ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ulioongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi wakati Tume ilipofanya Utafiti wa Mfumo wa Sheria ya Huduma za Jamii kwa Wazee katika mikoa ya Pwani na Morogoro.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Kitongoji cha Mlandizi Kati Bw. Ally Nyambwilo
akizungumza wakati wa Utafiti wa Mfumo wa Sheria ya Huduma za Jamii kwa
Wazee unaondeshwana Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania katika mikoa ya
Pwani na Morogoro
Mwenyekiti
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania mhe. Jaji Aloysius Mujulizi
akizungumza na Wazee wa Kitongoji cha Mlandizi Kati wakati wa Utafiti wa
Mfumo wa Sheria ya Huduma za Jamii kwa Wazee unaondeshwana Tume.
Bw. Kasongo Kilendu wa kijiji cha Magindu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini akichangia maoni wakati wa Utafiti wa Mfumo wa Sheria ya Huduma za Jamii kwa Wazee unaondeshwa na Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Bw. Abeid Ally Mamboleo wa Kitongoji cha Mlandizi Kati katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini akichangia maoni wakati wa Utafiti wa Mfumo wa Sheria ya Huduma za Jamii kwa Wazee unaondeshwa na Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania
Mzee wa Jamii ya ufugaji Bw. Lukunati Moreto wa kijiji cha Magindu katika Halmashauri yaWilaya ya Kibaha Vijijini akichangia maoni wakati wa Utafiti wa Mfumo wa Sheria ya Huduma za Jamii kwa Wazee unaondeshwana Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Mwenyekiti
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania mhe. Jaji Aloysius Mujulizi
akiwa katika picha ya pamoja na wafugaji wa kijiji cha Magindu katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini wakati wa Utafiti wa Mfumo wa
Sheria ya Huduma za Jamii kwa Wazee unaondeshwana Tume ya Kurekebisha
Sheria Tanzania katika mikoa ya Pwani na Morogoro, picha zote na Munir
Shemweta
Vijana nchini watakiwa kuwa huru katika kutoa maoni yao
Vijana nchini watakiwa kuwa huru kutoa maoni yao na wanapo kosea wawe tayari kukosolewa na kukujirekebisha.
Rai hiyo imetolewa na Rais
Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali
ya Pili ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Mkoa wa Dar es
Salaam yaliyofanyika jana katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam.
Kikwete alisema kuwa vijana
wanapaswa kutoogopa kukosea, kwani watu ujifunza kutokana na makosa
hivyo ni vyema wakathubutu kufanya mambo kwa kuzingatia misingi, weledi
na kwa uwazi huku wakiepuka migawanyiko.
Wakati huo huo Kikwete ameahidi
kulisaidia Shirikisho hilo kandana ya Dar es Salaam jumla ya shilingi
milioni 20 kwa ajili ya kusaidia katika kutekeleza mradi wao wa kilimo
na ufugaji wa kuku.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Bi. Zainabu Abdallah alisema
kuwa katika kuenzi na kutambua juhudi za Rais msataafu Jakaya Kikwete
katika kusaidia Vijana wataanzisha Tuzo maalumu kwa Vijana zitakazo
julikana kama “Jakaya Mrisho Kikwete Youth Awards”
Ambapo lengo lake ni kuhamasisha viongozi waendelee kusthamini michango ya vijana katika kukuza na kuendeleza Taifa letu.
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo
Vikuu (CCM) Seneta ya Dar es Salaam linaundwa na jumla ya matawi 34
ambapo katika mahafali hayo ya pili jumla ya wahitimu 640 walitunukiwa
vyeti kutambua mchango wao katika kuimarisha uhai wa Chama chao vyuoni.
KITUO CHA MIKUTANO CHA AICC CHAKABIDHI MADAWATI 100
Kituo cha Mikutano cha KimataifaArusha (AICC)kimemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Daudi Ntibenda madawati 100 yenye thamani shilingi milioni nane ili kupunguza tatizo
la upungufu wa madawati katika mkoa huo.
Daudi Ntibenda madawati 100 yenye thamani shilingi milioni nane ili kupunguza tatizo
la upungufu wa madawati katika mkoa huo.
Akipokea
madawati hayo jijini Arusha jana, Ntibenda amesema kwamba msaada huo ni
sehemu ya juhudi za serikali mkoani Arusha kuwashirikisha wadau wa
maendeleo ili kuhakikisha shule
zote za mkoa huo zinakuwa na madawati ya kutosha.
zote za mkoa huo zinakuwa na madawati ya kutosha.
“Napenda niishukuru sana AICC kupitia kwa Mkurugenzi Mwendeshaji Elishilia Kaaya kwa kuitikia
vema wito wa serikali ya mkoa wa kuomba wadau wasaidie kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa wetu”, alisema Mkuu wa Mkoa.
vema wito wa serikali ya mkoa wa kuomba wadau wasaidie kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa wetu”, alisema Mkuu wa Mkoa.
Alitoa wito kwa wadau mbalimbali mkoani Arusha wakiwemo wafanyakazi
wa ofisi ya Mkoa wa Arusha nao kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi ana kaa katika dawati.
wa ofisi ya Mkoa wa Arusha nao kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi ana kaa katika dawati.
Akizungumza
baada ya kukabidhi madawati hayo, Afisa Mwandamizi waItifakina Uhusiano
wa AICC, Catherine Kilinda amesema kwamba AICC kama shirika la umma
linawajibu wakuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya
elimu hapa nchini.
“Sisi kama shirika la umma linalojiendesha kibiashara tunaona fahari kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzaia wa kuhakikisha watoto wetu wa shule hawakai chini na ndio maana leo hii tumekabidhi msaada huu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuinua
sekta ya elimu”, alieleza Catherine.
ya Muungano wa Tanzaia wa kuhakikisha watoto wetu wa shule hawakai chini na ndio maana leo hii tumekabidhi msaada huu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuinua
sekta ya elimu”, alieleza Catherine.
AICC ambayo inajihusisha na kutoa huduma za Mikutano, upangishaji w ofisi na nyumba pamoja
na kutoa huduma za afya, imekuwa ikitumia sehemu ya faida katika kusaidia jamii hasa katika sekta ya elimu.
na kutoa huduma za afya, imekuwa ikitumia sehemu ya faida katika kusaidia jamii hasa katika sekta ya elimu.
JIJI LA DAR ES SALAAM KUJENGEWA MFUMO WA KISASA WA UONDOAJI NA USAFISHAJI WA MAJITAKA
Ramani inayoonesha Mpango wa upanuzi wa mfumo wa uondoaji wa majitaka katika jiji la Dar es salaam utakaotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuondoa wastani wa uondoaji wa majitaka kutoka asilimia 10 hadi asilimia 30 ifikapo mwaka 2017.
Mtambo mpya wa kusafishia maji katika chanzo cha maji Ruvu chini mara baada ya kukamilika.Mtambo huo sasa unazalisha maji lita milioni 270 kwa siku.
…………………………………………………………………………………………………….
Na.Aron Msigwa- MAELEZO.
Serikali
imesema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 itatekeleza mradi wa
ujenzi wa mfumo mpya wa uondoaji na usafishaji wa majitaka
yanayozalishwa katika jiji la Dar es salaam ili kuliweka jiji hilo
katika hali ya usafi na kuongeza wastani wa huduma hiyo kutoka asilimia
10 ya sasa hadi asilimia 30 ifikapo mwaka 2017.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema mradi huo
utatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Korea ya Kusini na Serikali
ya Tanzania kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 89.
Amesema
mradi huo utahusisha upanuzi wa miundombinu ya maji taka kwenye maeneo
ya katikati ya jiji, ujenzi wa miundombinu mipya ya kupitishia maji hayo
katika maeneo ya Ilala, Magomeni hadi Ubungo pamoja na maeneo ya Sinza,
Kinondoni , Mwananyamala, Oysterbay na Masaki.
Maeneo
mengine yatakayoguswa na mradi huo jijini Dar es salaam ni Msasani,
Kawe, Mbezi Beach, Kurasini,Keko, Chang’ombe, Temeke, Hananasif,
Tandale, Kijitonyama, Makumbusho, Mabibo, Ubungo, Manzese, Sandali,
Tandika na Miburani.
Mhandisi
Lwenge amesema mradi huo wa kipekee utahusisha ujenzi wa mitambo mitatu
ya kisasa ya kusafisha majitaka katika maeneo ya Jangwani, Kurasini na
Mbezi Beach.
Aidha,
Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Korea ya Kusini na Benki ya
Dunia itatekeleza mradi wa huduma ya uondoaji wa majitaka na ujenzi wa
miundombinu ya uondoaji wa maji ya mvua katika jiji la Dar es salaam
ambayo yamekuwa kero kwenye miundombinu ya jiji hilo.
“Serikali
tumeanza kutekeleza mpango wa kupanua mfumo wa uondoaji na usafishaji
wa majitaka yanayozalishwa na watumiaji maji , usanifu wa awali wa
miradi mipya ya majitaka umekamilika,kazi inayoendelea ni usanifu wa
kina ili kuweza kupata vitabu vya zabuni na michoro itakayotumika
kumpata mkandarasi wa ujenzi” Amesisitiza Mhandisi Lwenge.
Amesema
kuwa kupitia mpango huo bomba linalomwaga majitaka baharini litaacha
kutumika na badala yake maji hayo yatapelekwa katika mtambo mpya wa
kisasa wa kusafisha majitaka utakaojengwa maeneo ya Jangwani ambao pia
utasafisha majitaka kutoka maeneo yote ya katikati ya jiji Dar es salaam
yaliyo jirani ambapo maji hayo ambayo yatakua yamesafishwa yatauzwa na
kutumiwa katika shughuli mbalimbali za upozaji wa mitambo na
umwagiliaji.
Amebainisha
kuwa katika kulishughulikia tatizo la majitaka jijini Dar es salaam
Serikali itajenga mitambo mingine miwili eneo la Kurasini na Mbezi Beach
itakayotumika kuzalisha gesi asilia kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya
kusafishia maji hayo hivyo kupunguza matumizi na gharama za umeme.
Katika
hatua nyingine Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge
amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017, Serikali itafanya ukarabati na
upanuzi wa mfumo wa kusambazia maji safi katika jiji la Dar es salaam.
Ujenzi
wa mfumo huo unalenga kuongeza idadi ya wananchi wapya
watakaounganishwa na mtandao wa mabomba ya maji safi kutoka Mradi wa
Ruvu Juu na ule wa Ruvu Chini ulioigharimu Serikali bilioni 141 ambao
sasa maji yake yanaingia katika matanki ya maji yaliyoko Chuo Kikuu
Ardhi jijini Dar es salaam.
Amesema
kukamilika kwa mradi wa Ruvu Chini na Ruvu Juu mpaka sasa kumeyawezesha
baadhi ya maeneo ya jiji hilo yakiwemo ya Segerea, Kimara, Kibangu na
Kinyerezi ambayo yalikua na mabomba ya maji maarufu kama mabomba ya
mchina kuanza kupata huduma ya majisafi.
Aidha,
kupitia miradi hiyo mikubwa Serikali inaendelea kuishughulikia kero ya
uhaba wa maji katika maeneo ya Bunju,Mabwepande, Boko,Tegeta,Kunduchi,
Mbezi Beach, Mbezi Juu, Salasala, Kawe, Makongo, Mikocheni, Msasani,
Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Sinza, Manzese, Ubungo,
Mabibo, Kigogo, Buguruni na maeneo yote ya katikati ya jiji hilo.
Mhandisi
Lwenge amefafanua kuwa Kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 32.93
kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa mfumo wa
kusambaza majisafi katika jiji hilo na kuongeza kuwa wananchi wasiopata
huduma ya maji kutoka mtandao wa maji wa DAWASCO wataendelea kuhudumiwa
na mradi wa visima vilivyochimbwa.
”
Hadi mwezi Machi, 2016 tumechimba visima 52 na kati ya hivyo visima 32
vinatumika kutoa huduma ya majisafi katika maeneo mbalimbali ya jiji la
Dar es salaam” Amesema Mhandisi Lwenge.
Wakazi
wa jiji la Dar es salaam wapatao milioni 4.5 wamekuwa wakipata huduma
ya majisafi kutoka chanzo cha Ruvu Chini ambacho kwa siku kinazalisha
mita za ujazo 270,000 kwa siku, Mtambo wa Ruvu Juu unaozalisha mita za
ujazo 182,000, Mtambo wa mtoni 9000 na Visima Virefu 27,000 na kufanya
jumla ya mita za ujazo zinazozalishwa kwa siku kufikia 502,000 kutoka
300,000 za awali.
NAPE AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KUBANGUA KOROSHO MTAMA NA KUFANYA MIKUTANO MIWILI YA HADHARA
Mbunge
wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungmza na wafanyakazi wa kiwanda cha
kubangua Korosho cha Mtama ambapo wafanyakazi hao walitoa malalamiko
mbali mbali ikiwemo kutokuwa na mikataba na vifaa vya kufanyia kazi.
Mmoja kati ya vijana wanaofanya kazi kwenye kiwanda cha kubangua akielezea matatizo yanayo wakuta kiwandani hapo.
Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na viongozi wa kijiji cha
Rondo Mnaramara baada ya kuwasili tayari kuwahutubia wakazi hao
waliojitokeza kwa wingi.
Sehemu
ya wakazi wa kijiji cha Rondo Mnara wakiwa tayari kumsikiliza Mbunge wa
jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye
Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipitia moja ya jambo la msingi
pamoja na diwani wa kata ya Rondo Mama Halima Mwambe muda mfupi kabla ya
kuanza kuhutubia wakazi wa Rondo Mnara.
taifa STARS NA HARAMBEE stars zatoana sare 1-1.
Kikosi cha kwanza cha timu ya Soka ya Tanzania -Taifa Stars kilichoanza dhidi ya Harambee Stars ya Kenya Jumapili.
Ben Pol Akonga Nyoyo za maelfu wa mashabiki katika Tamasha la Nyama Choma Jijini Dar es salaa
BEN POL akicheza na mashabiki zake jukwaani wakati wa tamasha la nyama choma katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam |
Mashabikiwa muziki wa bongo fleva wakishangilia wakati Benpol anatumbuiza kibao chake cha MOYO MASHINE |
Benpol akihojiwa na mtangazaji wa Clouds fm Askofu Tza baada ya kutumbuiza katika tamasha la Nyama choma mapema jana katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam. |
Baadhi ya mawakala wa tigo waliokuwepo katika viwanja vya Leaders kutoa msaada na huduma mbali mbali toka tigo ikiwemo huduma za intaneti ya kasi ya Tigo 4G LTE |
Wakala wa tigo akisajili laini ya mteja katika tamasha la Nyama choma mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam. |
Mtangazaji
wa Choice fm na mshindi wa Bigbrother 2014 Idris sultan akifurahi jambo
na Mcheza kikapu wa kimataifa Hasheem Thabit wakati wa Tamasha la Nyama
Choma lililofanyika mapema jana usiku katika viwanja vya leaders jijini
Dar es salaam.
|
Msanii
mahiri wa Bongo fleva Vanessa Mdee akiongea jambo na mmoja wa shabiki
zake katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam |
Mabanda ya tigo yaliyokuwepo uwanjani katika kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wa tigo waliofika katika tamasha la Nyama Choma |
Mmoja wa wapishi wa nyama akichoma nyama wakati wa tamasha la Nyama Choma mapema jana katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam. |
Wadau wakiendelea kufurahia muziki na kula nyama choma katika tamasha liliofanyika mapema jana |
No comments :
Post a Comment