Monday, May 30, 2016

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF WAENDELEA NA KAMPENI YA KUELIMISHA MADAKTARI KUHUSU FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAPATAPO MADHARA KATIKA KAZI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Emmanuel Humba, (kulia),  akimkaribisha Naibu Waziri wa Kazi Mhe. Anthony Mavunde alipowasilili kufungua mafunzo kwa Madaktari
yanayohusu ajali na maginjwa yanayosababishwa na kazi Jijini Arusha Leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba
…………………………………………………………………………………………
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umeendelea na kampeni yake ya kutoa mafunzo kwa madaktari ili kujenga uelewa wa kufanya tathmini ya  ajali na magonjwa ayapatayo mfanyakazi yanayotokana na kazi safari hii ikihusisha madaktari kutoka mikoa mitano ya ambayo ni Arusha Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Singida.
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa leo Mei 30, 2016 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Bw. Anthony Mavunde, huko jijini Arusha, ni muendelezo wa mafunzo mengine kama hayo yaliyotolewa wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, ambapo madaktari kutoka mikoa ya Dares Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, lindi na mtwara walihudhuria.
WCF imechukua hatua hiyo ili kujiandaa na UTOAJI WA Mafao kwa mara ya kwanza tangu uanzishwe ifikapo Julai mwaka huu wa 2016.
 

MISS TANZANIA USA AEESHA KAMARA ATEMBELEA, KUONGEA NA KUTOA MSAADA KENTON HIGH SCHOOL

Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara akiongea na wanafunzi wa Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam siku alipotembelea shuleni hapo katika moja ya majukumu yake ya kuhudumia jumuiya. Miss Kamara anadhamini wanafunzi wawili shuleni hapo
Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akimkabidhi msaada mwalimu mipira siku alipotembela shule ya Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania USA Aesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wawili anaowadhamini kwa kuwasomesha shuleni hapo.
Picha ya pamoja

MAJALIWA AWASILI ARUSHA

index 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix  (katikati)  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha May 30, 2016 ambako May 31, 2016 anatarajiwa kufungua mkutano wa  Kimataifa wa ‘Africa  World Heritage’ kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha -AICC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wafanyika mkoani Mtwara

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua.
Baadhi ya watoto wa mkoani mtwara wakishindana kucheza muziki ikiwa ni sehemu ya burudani zilizosindikiza hafla ya uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua.
Wasanii Joe makini na Niki wa pili kutoka kundi la weusi wakitumbuiza hadhara iliyojitokeza katika uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua 
Msanii wa nyimbo za taarab isha mashauzi akiimba moja ya kibao chake wakati akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Msanii wa nyimbo za taarab isha mashauzi akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa mtwara halima dendego akimbeba mmoja ya watoto waliokabidhiwa chandarua chenye viuwatilifu ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akirusha maputo angani kuashiria uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye viuwatilifu mmoja ya mama wajamzito ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye viuwatilifu mmoja ya mama wenye watoto wa chini ya umri wa miezi sita ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
 
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya Malaria wameendelea na jitihada za kupambana na ugonjwa huo ili kufikia lengo la serikali la kupunguza vifo hadi kufikia asilimia moja ifikapo mwaka 2020.
 
Katika kutekeleza azma hiyo, serikali ya Tanzania na wadau hao wamezindua mpango wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu vya muda mrefu kwa akina wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa.
 
Akizindua mradi huo kitaifa, mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego amewataka wanawake kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito ili kupata ushauri na kinga dhidi ya malaria ikiwa ni pamoja na kupata chandaru kitakacho mkinga dhidi ya ugonjwa huo.Amesisitiza suala la kusafisha ameneo yote ili kudhibiti mazalia ya mbu waenezao Malaria ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na kuenea kwa ugonjwa huo unaosababisha vifo vya wakina mama wajawazito na watoto wa chini ya miaka 5.
 
“kwa mujibu wa Takwimu za ugonjwa huo kwa mkoa wa Mtwara, zimeshuka kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka 2011/2012. Hata hivyo takwimu za kitaifa zinaonesha kushuka kwa ugonjwa huo kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 9 mwaka 2015”. Alisema Bi Dendego.“Lengo la kitaifa la mapambano dhidi ya Malaria linaonesha kupunguza vifo hivyo hadi kufikia asilimia 5 mwaka huu na asilimia 1 mwaka 2020 hivyo sisi mkoa wa Mtwara tuna jukumu la kuhakikisha takwimu zetu zinaenda sambamba na takwimu za kitaifa”. Amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
 
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa kutoka ofisi ya Afya ya shirika la misaada la Marekani USAID Bibi Ana Bodipo -Memba amesema, ushirikiano wa serikila ya Marekani na Tanzania katika mapambano dhidi ya Malaria umeonesha mafanikio makubwa kwani wamefanikiwa kupunguza kwa silimia 50 vifo vitokanavyo na malaria kwa upande wa Tanzania Bara na chini ya asilimia moja kwa upande wa Zanzibar.
 
“Marekani inafahamu umuhimu wa mapambano dhidi ya Malaria, na hivyo mfuko wa Rais wa Kupambana na Malaria kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo hivyo nah ii ni ishara nzuri katika kufikia malengo ya kuutokomeza kabisa ugonjwa huu.” Alisema Bi Bodipo.
 
Mwakilishi wa wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Bi Helen Semu amesema, serikali itaendelea na uhamasishaji wa jamii kuendelea kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili asilimia 85 iliyofikiwa kwa sasa izidi kuongezeka na kufikia lengo la kumaliza kabisa tatizo hilo nchini.“Sisi Serikalini tutahakikisha tunaongeza jitihada za kuhamasisha jamii kuendelea kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili kila mmoja afahamu umuhimu wa kufanya hivyo na kudhibiti maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa huu” alisema bi Helen
 
Mpango wa utoaji vyandarua vyenye viuwatilifu kwa akina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama CHANDARUA KLINIKI unachukua nafasi ya mpango wa zamani wa HATIPUNGUZO na unasimamiwa na Mradi wa VECTORWORK kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na unfadhiliwa na mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria chini ya usimamizi wa shirika la misaada la nchi hiyo – USAID.

MAANDALIZI YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI TANZANIA 2016/2017 YAANZA RASMI.

CHU1Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akihojiwa na waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016.
CHU2Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Fatuma Mrisho akielezea umuhimu wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 katika mkutano wa wadau wa utafiti huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016.
CHU3Mkurugenzi Mkazi wa ICAP Tanzania Dkt. Fernando Morales akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016.
CHU4 
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) katika Mkutano wa Wadau wa Utafiti huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016. (PICHA NA EMMANUEL GHULA).
……………………………………………………………………………………….
Na Veronica Kazimoto
Wito umetolewa kwa wadau pamoja na wananchi ili kushiriki kikamilifu katika kuwezesha upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
Akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wana mchango mkubwa katika kufanikisha upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
“Leo hii tumekutana na wadau mbalimbali wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu kwa ajili ya kujadili na kushauriana namna ya kufanya utafiti huu kwa ufanisi ili kupata takwimu bora zitakazosaidia katika kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo nchini”, amesema Dkt. Chuwa.
Dkt. Chuwa amefafanua kuwa utafiti huu unategemea sana ushiriki wa wananchi kwani wao ndio wadau na wahusika wakuu ambao wanapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha ili kurahisisha upatikanaji wa takwimu rasmi zitakazosaidia Taifa katika kuboresha huduma za afya kwa manufaa ya watanzania wote.
Dkt. Chuwa amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu ipo katika harakati za kukamilisha maandalizi ya utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania 2016/2017 ambao utaanza kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Aidha Dkt. Chuwa  amesema utafiti huu ni wa kipekee ukilinganishwa na tafiti zilizotangulia kutokana na kuongezeka kwa viashiria vitakavyo chunguzwa ikiwemo kuangalia kiwango cha CD4, kiwango cha maambukizi mpya, upatiakanaji wa huduma zinazohusiana na UKIMWI pamoja na kupima watoto wadogo wenye umri chini ya mwaka mmoja.
Amesisitiza kuwa kukamilika kwa utafiti huu kutasaidia Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini hasa katika kupambana na maambukizi mapya ya UKIMWI na namna ya kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa ICAP nchini, Dkt. Fernando Morales amesema utafiti huu ni wa muhimu katika kupima viashiria na matokeo ya UKIMWI kwa nchi ambazo zimekuwa zikipata msaada wa kupambana na UKIMWI kutoka Serikali ya Marekani.
“Lengo la Utafiti huu ni kupata viashiria ambavyo vinasababisha maambukizi mapya pamoja na kupima jinsi gani Taifa limeweza kupambana na ugonjwa wa UKIMWI nchini”, amesema Dkt. Morales.
Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 unafanyika katika nchi Ishirini (20) Afrika ambapo kwa sasa nchi nane (8) zinaendelea na utafiti huu zikiwemo Zimbabwe, Zambia, Malawi, , Lesotho, Swaziland, Uganda, Namibia na Tanzania.

RAIS DK. MAGUFULI AMTEUA JAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA

IMG-20160530-WA0020

ZIARA YA LUHWAVI MANYARA LEO

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM,-Bara, Rajab Luhwavi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara, Luccas Ole Mukusu, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo, mjini Babati, leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa huo Ndegesu Ndekobali. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM,-Bara, Rajab Luhwavi akisalimiana na baadhi ya watumishi wa CCM mkoa wa Manyara, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo, mjini Babati, leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa huo Ndegesu Ndekobali. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili mjini Babati  leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Ndegesu Ndekobali.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili mjini Babati  leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Ndegesu Ndekobali.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Afisa Tawala wa mkoa huo, Eliakim Maswi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30, 2016. 
Katibu wa CCM wa mkoa wa Manyara Ndekobali akishukuru baada ya mazungumzo hayo
wakiagana baada ya mazungumzo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akiagana na Afisa Tawala wa mkoa wa Manyara Eliakim Maswi baada ya mazungumzo na mkuu wa mkoa huo Joel Bendera (Katikati), alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30, 2016. AKAGUA JENGO LA OFISI YA CCM LILILOUNGUA MWEZI MACHI MWAKA HUU

Tuna kila sababu ya kulinda na kuendeleza utamaduni wetu

images 
Benjamin Sawe
Maelezo Dar es Salaam
Watu wengi katika jamii yetu ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi, vijana na watoto hawana uelewa mzuri kuhusu dhana ya utamaduni. Neno “Utamaduni” lina uwanda mpana na linaelezwa kwa namna tofauti na watu mbalimbali. Wataalamu, wanazuoni na wanajamii mbalimbali wametoa maelezo na tafsiri mbalimbali za dhana ya utamaduni. Tafsiri hizi tofauti zinatokana na sababu za kijiografia, kihistoria, kimazingira, kijamii na kipindi au muhula husika.
‘Utamaduni’ ni shughuli au kazi zote afanyazo mwanadamu na namna anavyokabiliana na mazingira yanayomzunguka ili kukidhi mahitaji yake muhimu ya kumwezesha kuishi. Mahitaji hayo muhimu ni Chakula, Makazi na Mavazi. Katika kumwezesha kupata mafanikio aliyotarajia katika kupata mahitaji hayo, binadamu alijiwekea utaratibu (nguzo) za msingi katika kutekeleza shughuli zake za kila siku.
Utaratibu (nguzo) huo ulikuwa ni ule wa kuandaa mazingira ambayo kila mtu alipaswa  kuyafuata kila mara anapofanya shughuli zake. Utaratibu huo ni ule wa kuwa na mila na desturi. Mila na desturi hizi ambazo mababu zetu wamekuwa wakizifuata kwa miaka mingi ni uridhi ambao tunapaswa kuuheshimu, kuulinda na kuuendeleza. Kwa maneno mengine, mila na desturi hizo ambazo ni sehemu ya utamaduni ni rasilimali muhimu sana katika maendeleo ya taifa letu.
Wahenga walinena ‘mkataa kwao mtumwa.’ Usemi huu unatufundisha mambo mengi sana ukizingatia mwenendo wa maisha ya Watanzania katika mazingira ya sasa. Kifupi, usemi huu una maana kwamba, mtu ambaye anadharau maisha na tamaduni ambazo amekulia nazo, ametekwa kimawazo na yuko tayari kutumikishwa au kufuata mila na desturi za jamii nyingine kutokana tu na tofauti ya tamaduni hizo.
Hivi sasa nchi yetu inasura mbili. Kuna sura ambayo inaonyesha jinsi ambavyo baadhi ya Watanzania baada ya kupata elimu yao, hususan elimu ya juu ambayo wameipata hapa nchini au nje ya nchi, wanajiona ni tofauti kabisa na Watanzania wengine. Wasomi hawa wanajiona wako katika nchi ngeni kabisa na sio ile waliyozaliwa.
Kundi hili linaonekana kudharau mila na desturi zetu na kuziona kama zimepitwa na wakati. Kundi hili ambalo linaonekana kuongezeka hapa nchini, linaonekana kutotambua na kutothamini kabisa utamaduni wetu na mchango wake kwa taifa. Mara nyingi kundi hili linaonekana likitumia lugha ya kigeni (Kiingereza) zaidi kuliko Kiswahili, kudhihirisha kuwa ni tofauti na jamii iliyopo

No comments :

Post a Comment