Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye
foleni kwa katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na mfuko huo katika kampeni
maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya
ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. (Picha na John Dande)
foleni kwa katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na mfuko huo katika kampeni
maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya
ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. (Picha na John Dande)
Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (kulia), akiwajazia fomu baadhi ya wanachama wapya katika
kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia
Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi.
Jumla ya wanachama 214 walijiunga na NSSF.
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (kulia), akiwajazia fomu baadhi ya wanachama wapya katika
kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia
Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi.
Jumla ya wanachama 214 walijiunga na NSSF.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye
foleni katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na NSSF katika kampeni
maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya
ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
foleni katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na NSSF katika kampeni
maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya
ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Amani Marcel (kushoto) akiwakabidhi fulana wanachama wapya, Emmanuel
Joseph na Prisca Mwamsojo katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama
wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini
Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama 214 waliandikishwa.
Joseph na Prisca Mwamsojo katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama
wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini
Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama 214 waliandikishwa.
Ofisa Msajili wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Grace Mutegeki (kushoto) akiwaelekeza jambo baadhi
ya wanachama wapya waliojiunga na mfuko huo katika kampeni maalumu ya kuelimisha
na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilayaya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga
jijini Dar es Salaam.
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Grace Mutegeki (kushoto) akiwaelekeza jambo baadhi
ya wanachama wapya waliojiunga na mfuko huo katika kampeni maalumu ya kuelimisha
na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilayaya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga
jijini Dar es Salaam.
Afisa
Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango
akimjazia fomu ya kujiunga na NSSF mchuuzi wa mayai wakati wa kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha
wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya
Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama wapya 214 walijiunga
na NSSF.
Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango
akimjazia fomu ya kujiunga na NSSF mchuuzi wa mayai wakati wa kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha
wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya
Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama wapya 214 walijiunga
na NSSF.
Baadhi ya wananchi wakisoma fomu
kabla ya kujiunga na NSSF katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama
wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Jijini
Dar es Salaam.
kabla ya kujiunga na NSSF katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama
wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Jijini
Dar es Salaam.
Watu mbalimbali wakisubiri kujiandikisha.
Afisa
Uandikishaji wa NSSF, Amina Kisawaga, kushoto akiwaelekeza jambo baadhi
ya wananchi waliotembelea banda lao katika kampeni maalumu ya
kuelimisha na kuandikisha wanachamawa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya
ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi.
Zaidi ya wanachama 20 walijiandikisha.
RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI TAREHE 03 MEI 2016 MKOANI DODOMA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza
kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 03 Mei, 2016 katika ukumbi wa
TAMISEMI mjini Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kutoka
kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 03 Mei, 2016 katika ukumbi wa
TAMISEMI mjini Dodoma.
PICHA NA IKULU
RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI DODOMA
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakielekea
kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika
Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati
alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya
Halmashauri kuu ya Taifa.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia
jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya
Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao
cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.
Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.
Ali Mohamed Shein.
PICHA NA IKULU
TAARIFA KWA WANACHAMA WA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN)
Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini ‘Tanzania Bloggers
Network’ – TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa ama
habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari (WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kamati Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya kujadiliana na kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya habari ambazo zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii (bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa mbalimbali nchini husambazwa na mitandao hiyo.
TBN iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa aina yoyote kwa taasisi ambazo zinawatenga bloggers.
Tunasikitika kufikia hatua hii ila hamna jinsi.
Kamati Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya kujadiliana na kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya habari ambazo zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii (bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa mbalimbali nchini husambazwa na mitandao hiyo.
TBN iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa aina yoyote kwa taasisi ambazo zinawatenga bloggers.
Tunasikitika kufikia hatua hii ila hamna jinsi.
TBN itasikitika na kumshangaa
mwanachama wake au blogger asiye mwanachama kutounga mkono agizo hili,
na kwenda kinyume na agizo hili. Muda umefika ‘Bloggers’ kudai heshima,
kutambulika na kuthaminika kama tasnia ya habari ingine yoyote.
Imetolewa na;-
Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
03/05/2016
Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
03/05/2016
KATIBU WA BUNGE AKUTANA NA VIONGOZI WA JESHI LA MAGEREZA NA SUMA – JKT,
JIJINI DAR, UTENGENEZAJI WA MADAWATI YA SHULE NCHINI KUANZA MUDA WOWOTE
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashilila akiongea na Viongozi wa
Jeshi la Magereza pamoja na SUMA – JKT kwenye Ofisi za Bunge, Jijini
Dar es Salaam kuhusiana na namna walivyojipanga katika kutekeleza jukumu
la utengenezaji wa Madawati ya shule hapa nchini.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashilila
akiongoza mazungumzo na Viongozi wa Jeshi la Magereza pamoja na SUMA –
JKT(hawapo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja(wa kwanza kushoto)
akiwa pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo wakifuatilia kwa
makini mazungumzo na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Thomas Kashilila(hayupo pichani).
Mtendaji
Mkuu wa SUMA – JKT, Bregedia Jenerali C. Yateri akifuatilia mazungumzo
hayo na Maofisa Watendaji wa Shirika hilo la SUMA – JKT.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja akiteta jambo na
Mtendaji Mkuu wa SUMA – JKT, Bregedia Jenerali C. Yateri walipokutana
leo Mei 3, 2016 katika Ofisi za Bunge, Jijini Dar es Salaam(Picha zote
na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
WANAHABARI SHIRIKIANENI NA WADAU WA AFYA KUELIMISHA JAMII KUHUSU MABADILIKO YA TABIANCHI.
Dkt.
Azma Simba wa Kitengo cha Epidemolojia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye alimwakilisha mgeni rasmi katika
ufunguzi wa Semina kwa Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya
tabianchi akisoma taarifa ya Mkurugenzi toka Wizarani leo 3 Mei, 2016
Jijini Dar es Salaam.
JAJI WA SHINDANO LA TUZO ZA EJAT 2015, NATHAN MPANGALA ALIPONGEZA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT)
Baadhi
ya majaji wa Shindano la Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT)
2015, wakifuatilia utoaji tuzo wa shindano hilo lililofanyika katika
ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Kutoka
kushoto ni Bw. Nathan Mpangala, Bw. Juma Dihule, Bw. Kiondo Mshana, Bi.
Valerie Msoka (Mwenyekiti), Bw. Ndimara Tegambwage na Dkt. Joyce Bazira
Ntobi.
Jaji
wa Shindano la Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) 2015,
Nathan Mpangala (kushoto) akimkabidhi tuzo Bw. Mansour Jumanne wa SAUT
FM ya Mwanza katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini
Dar es Salaam wiki iliyopita.
……………………………………………………………………………………
MMOJA
wa majaji wa Shindano la Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT)
2015, ambaye pia ni mchoraji vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala
amelipongeza Baraza la Habari Tanzania (MCT), kwa kumpa heshima ya kuwa
mmoja wa majaji wa tuzo hizo zilizofanyika wiki iliyopita Jijini Dar es
Salaam.
Akizungumzia
ushiriki wake katika shindano hilo, alisema toka kinyang’anyiro hiko
kianze mwaka 2009 hakijawahi kuwa na jaji mchora vibonzo. Safari hii MCT
wameliona hilo. Ni jambo zuri na la kupongezwa.
“Yanapofanyika
mashindano ya aina yeyote yale, ni vema yakahusisha watu waliobobea
katika eneo husika ili waweze kusaidia kutoa miongozo,” alisema
Mpangala.
Jopo
hilo la majaji liliongozwa na Bi. Valerie Msoka, wajumbe wengine
ni Bw. Ndimara Tegambwage, Dkt. Joyce Bazira Ntobi, Bw. Ali Uki, Bw.
Jesse Kwayu, Bw. Kiondo Mshana, Bw. Juma Dihule, Bw. Godfrey Nago
na Bi. Pili Mtambalike.
UINGEREZA YAIFAGILIA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, JKCI
NA K-VIE MEDIA/Khalfan Said
NAIBU balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, (pichani wapili kushoto), ameisifu
taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), kwa kuratibu kambi ya upasuaji wa
moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka nje kwa mafanikio makubwa.
taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), kwa kuratibu kambi ya upasuaji wa
moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka nje kwa mafanikio makubwa.
Pongezi hizo amezitoa leo May 3, 2016, baada ya kutembelea kambi
hiyo maalum iliyoko kwenye taasisi hiyo, na kujionea madaktari wakiendelea na
kazi ya kuwafanyia upasuaji watoto wa Kitanzania kutoka sehemu mbalimbali
nchini.
hiyo maalum iliyoko kwenye taasisi hiyo, na kujionea madaktari wakiendelea na
kazi ya kuwafanyia upasuaji watoto wa Kitanzania kutoka sehemu mbalimbali
nchini.
“Nimefurahishwa sana na uamuzi wa JKCI wa kuratibu zoezi hili
kwa ushirikiano na wataalamu wa magonjwa ya moyo kutoka nje ya nchi, najua
taasisi ya hiari kutoka Uingereza imekusanya fedha na kwa kushirikiana na
madaktari wengine, wamewezesha zoezi hili kufanyika kwa mafanikio.” Alisema
Balozi Sutherland.
kwa ushirikiano na wataalamu wa magonjwa ya moyo kutoka nje ya nchi, najua
taasisi ya hiari kutoka Uingereza imekusanya fedha na kwa kushirikiana na
madaktari wengine, wamewezesha zoezi hili kufanyika kwa mafanikio.” Alisema
Balozi Sutherland.
Taasisi ya Muntada Aid, ni taasisi ya Kiislamu yenye makazi yake
nchini Uingereza, ambayo ndiyo iliyowezwesha kuwaleta madaktari na vifaa, na
hatimaye kwa kushirikiana na madaktari na wataalamu wengine kutoka JKCI
wameweza kufanya upasuaji wa watoto 20 hadi sasa.
nchini Uingereza, ambayo ndiyo iliyowezwesha kuwaleta madaktari na vifaa, na
hatimaye kwa kushirikiana na madaktari na wataalamu wengine kutoka JKCI
wameweza kufanya upasuaji wa watoto 20 hadi sasa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Janabi alisema, chini ya
uratibu wa taasisi yake, wataalamu kutoka Australia kupitia Open Heart
International, wakishirikiana na wataalamu kutoka JKCI waliendesha kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto 15 kuanzia
Aprili 25 hadi Aprili 30.
uratibu wa taasisi yake, wataalamu kutoka Australia kupitia Open Heart
International, wakishirikiana na wataalamu kutoka JKCI waliendesha kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto 15 kuanzia
Aprili 25 hadi Aprili 30.
“Kambi hii ya sasa, inaundwa na wataalamu kutoka Saudi Arabia
chini ya uratibu wa taasisi ya hiari ya Muntada Aid, yenye makazi yake nchini
Uingereza, na hadi leo hii Mei 3, 2016, tayari watoto 20 wameshafanyiwa
upasuaji na hivyo kufanya jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji tangu kambi
hizi mbili zianze.” Alifafanua Profesa Janabi kwenye mkutano na waandishi wa
habari.
chini ya uratibu wa taasisi ya hiari ya Muntada Aid, yenye makazi yake nchini
Uingereza, na hadi leo hii Mei 3, 2016, tayari watoto 20 wameshafanyiwa
upasuaji na hivyo kufanya jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji tangu kambi
hizi mbili zianze.” Alifafanua Profesa Janabi kwenye mkutano na waandishi wa
habari.
Profesa Janabi alisema, malengo yao ni kuwafanyia upasuaji
watoto 70 Ifikapo Mei 7. “Tunawashukuru wenzetu hawa kwa kuja kutshirikiana
nasi kwani upasuaji unaofanyika ni huu wa kisasa, ambapo hakuna kumpasua kifua
mgonjwa bali tunafanya upasuaji kwa kutumia matundu na hili ni jambo muhimu kwa
wataalamu wetu ambao wamepata fursa ya kujifunza kutoka kwao.” Alisema.
watoto 70 Ifikapo Mei 7. “Tunawashukuru wenzetu hawa kwa kuja kutshirikiana
nasi kwani upasuaji unaofanyika ni huu wa kisasa, ambapo hakuna kumpasua kifua
mgonjwa bali tunafanya upasuaji kwa kutumia matundu na hili ni jambo muhimu kwa
wataalamu wetu ambao wamepata fursa ya kujifunza kutoka kwao.” Alisema.
Profesa Janabi (wapili kulia), wengine kutoka kulia, ni Balozi Sutherland, Dkt. Shem, na Dkt.Delila Kimambo
Wataalamu wa JKCI wakiwa kazini kwenye mojaya vyumba vya upasuaji
Balozi Sutherland, katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka JKCI na wale wa Muntada Aid
Profesa Janabi, akimsikiliza mgeni wake, Balozi Sutherland
Dkt.StellaMongella.
(kushoto, akimpatia maelezo Balozi Sutherland, alipotembelea wodi ya
watoto waliofanyiwa upasuaji (Post Operative Recovery Word), Kulia ni
Profesa Janabi
Balozi
Sutherland, akiwapongeza wataalamu wa moyo kutoka Muntada Aid,
wanaoshuhudia ni Profesa Janabi (kulia na Dkt. Tulizo Shem kutoka JKCI.
Baadhi ya Watanzania wakisubiri huduma ya matibabu ya moyo
Kiongozi wa timu ya madaktari kutoka Muntada Aid, (katikati)
Dkt. Tulizo Shem akiongea
Balozi Sutherland akipokewa kwenye taasisi alipowasili
Uswahilini Bingwa Mama Shija Cup
Mchezaji
Sultani Kasikasi wa Uswahilini wa pili kushoto akipongezwa na wenzake
kupiga picha na mpira aliozawadiwa baada ya kufunga mabao matatu Hat
Trick katika mchezo huo.
Mwenyekiti
wa timu ya Bodaboda ya Mbagala,Ali Omari akipokea jezi seti mbili na
mpira mmoja kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilungule baada ya klushika
nafasi ya tatu katika mashindano ya Mama Shija Cup juzi Dar es Salaam.
Muaandaji
wa mashindano ya Mama Shija Cup, Fatuma Shija akikabidhi mpira kwa
waamuzi wa mashindano yake baada ya kumaliza fainali za Kombe la Shija
zilizofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kingunge, Mbagala na Uswahilini
kuibuka mabingwa.
…………………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Soka ya Uswahilini FC imeibuka
mabingwa wa Kombe la Mama Shija baada ya kuichapa Wamangati zote za
Mbagala katika fainali ilijaa ushindani mkubwa iliyofanyika uwanja wa
Shule ya Msingi Kingunge, Mbagala Dar es Salaam.Katika fainali hizo ambazo zilidhaminiwa na Kampuni ya Simu ya Vodacoma, mshambuliaji Sultani Kasikasi wa Uswahilini aliibuka mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kuifungia timu yake mabao 3 yaliyoipatia timu yake ubingwa na kuzawadiwa mpira “hat Trick”.
Mabao ya Kasikasi yalipatikana dakika ya 32 , dakika ya 41 na 59 na mabao ya WAmangati yaliyungwa na Salum Gava dakika ya 39 na bao la pili lilifungwa na Musa Madebe aliyeunganisha krosi safi ya Shaaban Pazi.
Muandaaji wa mashindano hayo, Fatuma Shija akizipongeza timu zote 20 zilizoshiriki Kombe hilo aliwataka vijana kutumia muda wao mwingi kwenye michezo ambayo itachukua muda wao mwingi kujenga miili yao badala ya kuvuta bangi na kufanya vitendo vya kihuni mitaani.
Mashindano hayo yalishirikisha timu kuoka Mkuranga mkoa wa Pwani, Wilaya Mpya ya Kigamboni na Temeke, Mshindi wa nne ilikuwa timu ya Kisemvule FC iliyezawadiwa mpira mmoja, mshindi wa tatu ni Bodabdoda iliyopata jezi seti moja na mpira mmoja na mshindi wa pili alipata medali 15 za shaba, jezi seti mbili na mpira mmoja.
Ilikuwa furaha kubwa kwa
mashabiki wa Uswahili baada ya kuzawadiwa Kombe na medali 15 za dhahabu
kwa wachezaji wake, jezi seti mbili na mpira mmoja walishangilia na
kucheza uwanja mzima huku kuimba nyimbo za ushindi na kuwavutia
mashabiki wake na wapita njia.
Mv Magogoni yasitisha huduma zake kwa ajili ya matengenezo
Mtendaji
Mkuu wa Temesa Mhandisi Manase Ole-Kujan akitoa taarifa juu ya
kusimamia kwa huduma za Mv Magogoni inayofanyiwa Matengenzo makubwa.
Wananchi
wakipita katika daraja la Nyerere lilopo Kigamboani Jijini Dar es
Salaam mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli hivi karibuni.
Kivuko cha Mv Magogoni kikiwa katika shughuli zake za kila siku za kutoa huduma kwa wananchi.
(Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Kivuko cha Mv Magogoni kinachotoa
huduma kwa wananchi kutoka upande wa bahari eneo la Magogoni kuelekea
Kigamboni Jiji la Dar es Salaam kimesitisha kutoa huduma kwa ajili ya
kufanyiwa matengenezo makubwa.
Katika taarifa iliyotolewa na
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase Ole
Kujan kwa niaba ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imesema kuwa
kuanzia Mei 5 2016 kivuko hicho kitakuwa katika matengenezo makubwa
ambayo yatafanya kusitisha huduma zake kwa muda.
Taarifa hiyo imesema kuwa huduma
za kivuko zitaendelea kama kawaida kwani wananchi watatumia huduma ya
kivuko cha Mv Kigamboni pamoja na kivuko kilichokodishwa na Serikali
kutoka kampuni ya Azam Marine vitavyokuwa vinasaidia kutoa huduma kwa
wananchi kwa muda wote ambao Mv Magogoni itakuwa katika matengenezo.
“ Muda wake wa matengenezo
umefika na ni wakati muafaka kwa kivuko kwenda kwenye matengenezo ni
muda mrefu kimetumika na kusimama kwa kivuko hiki hakutaleta madhara
makubwa kwani mara baada ya kuzinduliwa kwa daraja la Nyerere hivi
karibuni tuna imani wananchi watatumia daraja hili ili kendelea na
shughuli zao za kila siku” imesema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo
wananchi wenye magari wanaotumia vivuko hivyo wameshauriwa kutumia
daraja jipya la Nyerere ili kuepukana na usumbufu wa kusubiri kivuko
pekee cha Mv Kigamboni chenye uwezo wa kubeba magari na kufafanua kuwa
kivuko kutoka Azam Marine kina uwezo wa kubeba watu peke yake.
Taarifa hiyo imeendelea kusema
kuwa matengenezo ya kivuko cha Mv Magogoni yatafanyika Jijini Dar es
Salaam chini ya usimamizi wa Temesa katika matengenezo ya mitambo na
ukarabati na ujenzi utafanywa na kampuni ya kizawa ya na Songoro Marine
Transport Yard yenye makao makuu yake Jijini Mwanza.
Aidha kivuko cha Mv Magogoni
kitakabidhiwa kesho kwa kampuni ya Songoro Marine Transport Yard kwa
ajili ya matengenzo hayo na mara baada ya mkandarasi kuangalia hali ya
kivuko atatoa muda kamili wa kumalizika kwa matengenezo ya kivuko hicho.
Serikali katika katika jitihada
za kupunguza msongamano katika vivuko hivyo imeamua kwenda kukifanyia
ukarabati mkubwa ili kukiongezea uwezo na ufanisi wa kuhudumia wananchi
kwa kusaidiana na daraja jipya la Nyerere lililozinduliwa na Mhe. Rais
wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt john Pombe Magufuli hivi karibuni
ili kuondoka na tatizo la msongamono kwenye vivuko vya Kigamboni.
RATIBA YA KUWASILI NA MAZISHI YA MPENDWA WETU ANDREW NICKY SANGA HAPA TANZANIA.
RATIBA YA KUWASILI NA MAZISHI YA MPENDWA
WETU
WETU
ANDREW NICKY SANGA
Ndugu zetu pamoja na Marafiki; Kwa niaba ya Familia ya
Bwana Nicky Amon Sanga, Kamati ya Maandalizi inapenda kuwajulisha Ratiba ya
Safari ya Mpendwa wetu ANDREW NICKY SANGA hapa Tanzania kuanzia kuwasili kwa
mwili wa Marehemu hadi tutakapomweka kwenye nyumba yake ya Milele
Bwana Nicky Amon Sanga, Kamati ya Maandalizi inapenda kuwajulisha Ratiba ya
Safari ya Mpendwa wetu ANDREW NICKY SANGA hapa Tanzania kuanzia kuwasili kwa
mwili wa Marehemu hadi tutakapomweka kwenye nyumba yake ya Milele
Muda
|
Tukio
|
Mahali
|
Wahusika
|
DAR ES SALAAM
|
|||
Jumanne 3 Mei 2016
|
|||
3:55 Usiku
|
Mwili kuwasili
|
Uwanja wa Ndege: Julius Nyerere
|
Familia, Ndugu, Marafiki na Jamaa Wote
|
4:30-5:30 Usiku
|
Kuelekea Kuhifadhi Mwili
|
Hospitali ya Taifa Muhimbili
|
Familia, Ndugu na Marafiki na Jamaa Wote
|
Jumatano 4 Mei 2016
|
|||
4:00-6:00 Asubuhi
|
Ibada ya Kuaga
|
Kanisa la Kilutheri Ubungo (Nyuma ya Ubungo Plaza)
|
Familia, Ndugu, Marafiki na Jamaa Wote.
|
6:30 Mchana
|
Safari ya Kuelekea Dodoma
|
Kanisa la Kilutheri Ubungo
|
Wote Waliojiandaa.
|
DODOMA
|
|||
5:00:-6:00 Asubuhi
|
Chakula
|
Nyumbani- Kizota
|
Waombolezaji Wote
|
6:00
|
Kuelekea Uwanja wa Mashujaa
|
Waombolezaji Wote
|
|
6:30-7:20 Mchana
|
IBADA
|
Uwanja wa Mashujaa
|
Waombolezaji Wote
|
7:30-8:45 Mchana
|
Heshima za Mwisho
|
Uwanja wa Mashujaa
|
Waombolezaji Wote
|
8:46 Mchana
|
Kuelekea Makaburini
|
Waombolezaji Wote
|
|
9:20 Mchana
|
Mazishi
|
Makaburi ya Hijra Chinangali
|
Waombolezaji Wote
|
Kamati ya maandalizi siku ya Utamaduni Duniani yaanza maandalizi
Mkurugenzi
Msaidizi Sanaa Hajjat Shani Kitogo (aliyesimama) akiongoza majadiliano
jana Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya
siku ya Utamaduni Duniani inayoadhimishwa kila tarehe ya 21 Mei.
Afisa
Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.
Sefania Motela (aliyesimama) akichangia wakati wa kikao cha kamati ya
maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe
21 Mei mwaka huu.
Mwenyekiti
wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Bw. John Mponda (kulia)
akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya
Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
Afisa
Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.
Fransis Songoro (aliyesimama) akiwasilisha mchango ulitolewa katika
kamati ndogo ndogo zilizoundwa wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi
ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei
mwaka huu.
Baadhi
ya Maafisa Utamaduni na Wadau wa Utamaduni wakifuatilia kwa makini
majadiliano yaliyokua yakiendelea wakati wa kikao cha kamati ya
maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe
21 Mei mwaka huu.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
Tume ya Kurekebisha Sheria Yakutana na Wataalamu Kutoka Marekani
Mwenyekiti
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi
akiongoza kikao cha pamoja baina ya Tume na Wataalamu kutoka Marekani
kujadili Mfumo wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Tanzania.
Kamishna
wa Tume Prof. Sufian Bukurura akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja
baina ya Tume na Wataalamu kutoka Marekani wakiongozwa na Prof Allen
kujadili Mfumo wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Tanzania.
Sehemu
wa washiriki wa kikao cha pamoja baina ya Tume na Wataalamu kutoka
Marekani kujadili Mfumo wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai
Tanzania.
Mmoja
wa washiriki kutoka Marekani akijitambulishwa wakati wa kikao cha
pamoja baina ya Tume na Wataalamu kutoka Marekani kujadili Mfumo wa
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Tanzania.
Mwenyekiti
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi (
wan ne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Marekani
wakioongozwa na Prof Allen ( kulia kwa Mwenyekiti) wakati wa kikao cha
pamoja baina ya Tume na Wataalamu kutoka Marekani wakiongozwa na Prof
Allen kujadili Mfumo wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Tanzania.
(Picha na Munir Shemweta, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania)
MBUNGE ABDALLAH ULEGA ADHAMIRIA KULIKOMBOA JIMBO LA MKURANGA KIMAENDELEO
Mbunge
wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akichangia Bajeti ya Serikai
katika Mpango pili wa wa miaka mitano ijayo wakati wa vikao vya bunge
la bajeti linaloendelea mjini Dodoma hivi karibuni.
Mbunge
wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akiendelea na uchangiaji wa
hoja katika Mpango huo wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano ijayo.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akizindua kisima cha maji Mkamba katika jimbo lake la Mkuranga mkoani Pwani.
…………………………………………………………………………………………………….
SERIKALI ya awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imedhamiria kuwa Serikali ya
mageuzi ya Viwanda ukilinganisha na zilizotangulia.
Rais Dkt.Magufuli hata katika
kampeni zake za uchaguzi 2015 wakati akipita kuomba kura alisisitiza
dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa Viwanda.
Wakati Serikali ikisisitiza
kujenga uchumi wa Viwanda huku ikipata sapoti kupitia Ilani ya Chama cha
Mapinduzi wabunge nao katika kuunga mkono hilo kila mmoja amekuwa na
kiu ya Jimbo lake kuwa la mfano katika eneo hilo.
Abdallah Ulega ni Mbunge wa
Jimbo la Mkuranga lililopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kwa upande
wake tangu achaguliwe na wananchi wake ameonesha dhamira na kiu ya
kutaka kuwakomboa wananchi wake Kwa kutaka jimbo hilo kuwa na viwanda.
Anasema kuwa lazima wao kama
wawakilishi wa wananchi Kwa maana ya wabunge wanaotokana na Chama cha
Mapinduzi CCM wapokee Kwa mikono miwili mageuzi haya kwani wameahidi
hivyo lazima watende.
Ulega anasema kuwa Jimbo la
Mkuranga ni kubwa na linarutuba ya kutosha hivyo anakaribisha
wawekezaji kuingia na kukubali Kuwekeza viwanda vidogovidogo na vikubwa
katika kilimo hasa cha mazao mbalimbali Kwa ajili ya maendeleo ya watu
wake.
Anasema kuwa kuna jitihada kama
Mbunge amekuwa akizifanya za kuhakikisha kwamba jimbo lake ni miongoni
mwa majimbo ambayo yanafaidika na mikakati ya Serikali ya kutaka mageuzi
ya viwanda.
“Kimsingi jimbo langu la Mkuranga ni kubwa kama nilivyosema na uzuri zaidi lina ardhi nzuri sana na ndiyo maana naomba wahisani na wawekezaji wa ndani kujitokeza kuja Kuwekeza na zaidi kijenga viwanda.”anasema ulega
Anasema kuwa kutokana na utajili
wa Ardhi yenye rutuba wanaweza kujenga viwanda vya kusindika mazao
lakini pia kwa sababu eneo lao ni kubwa basi hata viwanda vya kubangua
korosho na kujengwa Kwa viwanda hivyo kutasaidia kuleta ajira katika
eneo hilo.
Anasisitiza kuwa ndio maana
wakati akichangia mpango wa wa maendeleo wa Serikali Kwa miaka mitano
ameomba Serikali na wahisani kujitokeza Mkuranga lakini Kwa upande wa
Serikali kuiweka Mkuranga kuwa sehemu yenye hitaji la ujenzi wa viwanda.
Anasema amebainisha wazi kiu ya
wananchi wa jimbo lake la kutaka maendeleo na ajira hivyo bila kuwepo
na viwanda hakuna ajira inayoweza kuwepo na zaidi vijana watazidi
kulaumu serikali yao.
“Nimesema wazi kuwa Mkuranga
kuna matatizo ya miundombinu mbalimbali ikiwamo barabara.Maji .kilimo na
mambo mengine na katika baadhi ya maeneo haya nashukuru baadhi ya
marafiki wameitikia mwito wangu na wameweza kusaidia katika kichimba
visima ambapo wananchi wangu wameaza kupata Maji safi na salama.”anasema
Ulega
Anasema kuwa anawashukuru
African Foundation Reflection Kwa kuonesha moyo wa kusaidia na juhudi
hizo zote zimetokana na jitihada zake za kutaka kuona siku moja Mkuranga
inakuwa ya kutolea mfano tofauti na ilivyo sasa.
Aidha katika mpango huo wa
maendeleo Kwa miaka mitano Kwa Serikali ameomba kujengewa barabara
Kutoka Kisiju hadi Mkuranga Kwa kiwango cha lami kwani barabara hiyo ni
muhimu Kwa wananchi wa wilaya hiyo lakini hata wale wanaotoka Mafia.
Pia anasema katika mpango
mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano Kuhusu maendeleo ya
miundombinu nchini na hapo aliangalia wilaya ya Mafia kwa sababu pale
kuna bandari na watu wake pia ndiyo wazalishaji wakubwa wa korosho na
samaki.
Anasema kuwa pia kwenye kata
yake ya mbezi kwaniaba ya wananchi wake wa Mkuranga wangeishauri
Serikali kuwa eneo la viwanda ili wananchi wake wawe sehemu ya
uzalishaji wake.
Aidha Ulega anazungumzia suala
la kuondoa kero ya uhaba wa upatikani wa Maji katika jimbo hilo ambapo
Serikali ingefanya bidii ya kutoa maji hayo kutoka katika mto rufiji
kupitia kibiti hadi kufika Mkuranga na hatimaye Dar es Salaam.
Anasema haiwezekani Kwa miaka
nenda rudi tatizo la Maji halipatiwi ufumbuzi wakati Mkuranga inapitiwa
kwa karibu na Mto Rufiji ambapo mikakati madhubuti ya kuleta Maji
ikifanyika tatizo hilo litabaki kuwa historia katika eneo hilo.
Anasema tatizo la ajira Kwa
vijana ni kubwa mno hivyo wanashukuru Serikali Kwa kutambua umuhimu wa
kutilia mkazo uazishwaji na ufufuaji wa viwanda kwani eneo hilo ndilo
linaweza kuwa.msaada Kwa vijana kuweza kupata ajira.
“Mimi kama Mbunge wao kama
nilivyosema awali nitaendelea kupambana na kufanya kila linalowezekana
Kwa kuhakikisha Mkuranga inakuwa sehemu ya viwanda na naendelea kitoa
rai Kwa wawekezaji kuchangamkia Ardhi yetu Kwa kujenga viwanda vingi ili
vijana wangu wapate ajira.”anasema
Anaongeza kuwa mkuranga
ilisahaulika mno pamoja kwamba ni miongoni mwa wilaya za siku nyingi
lakini imekuwa nyuma kimaendeleo hivyo niwakati mwafaka wa kushirikiana
Kwa pamoja Kwa ajili ya maendeleo.
Anasema kuwa wananchi wake
waendelee kumuombea Kwa Mungu na wazidi kudumisha Umoja na mshikamano
ili Kwa pamoja wapambane Kwa lengo la kuona jimbo la mkuranga linakuwa
la mfano.
Akizungumzia kilimo cha korosho
anasema kuwa pamoja na zao hilo kuwa ndio zao linalotegemewa kuendesha
maisha ya wananchi wake lakini bado kwasababu ya ukosefu wa kuwepo Kwa
viwanda hususani vya ubanguaji kunafanya pasiwepo na tija sana
wanayoipata wananchi wake katika kilimo hicho.
Anasema kuwa kutokana na hali
hiyo ana kazi kubwa ya kuendelea kuzungumza na watu mbalimbali ili
kuleta ushawishi wa kukubali Kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda hivyo.
Pia akizungumzia Elimu anasema
anatambua changamoto zilizopo katika eneo hilo hivyo amedhamiria Kwa
dhati Kwa kushirikiana na Halmashauri wanaongeza hamasa Kwa wanafunzi
ili waweze kufanya vema katika masomo yao na hatimaye kuweza kupata
wataalamu wa baadae.
“Najua kuna Changamoto ya
madawati na hili tunalishugulikia Kwa kushirikiana na kamati mbalimbali
za Shule,wazazi,pamoja na walimu ili kuona namna ya kukabiliana na
tatizo hilo na hata uchakavu wa majengo .”anasema Ulega.
Anahitimisha Kwa kuwataka wananchi wa Mkuranga kila mmoja kujielekeza katika kuzalisha Mali huku wakienda na Kauli mbiu ya Rais Dkt.Magufuli ya Hapa Kazi Tu.
Anahitimisha Kwa kuwataka wananchi wa Mkuranga kila mmoja kujielekeza katika kuzalisha Mali huku wakienda na Kauli mbiu ya Rais Dkt.Magufuli ya Hapa Kazi Tu.
MAAZIMISHO YA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ DUNIANI YAFANA
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza
akizungumza na wadau wa Sanaa kwenye maadhimisho ya Siku ya Muziki wa
Jazz duniani yaliyofanyika mapema wiki hii katika Ukumbi wa Baraza hilo
ulioko Ilala Sharif Shamba jijinI Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Msanii
mkongwe John Kitime na Mkuu wa Kitengo cha Matukio kutoka BASATA
Kurwijira Mareges.
Mwakilishi
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) Maximilan Chami akitoa elimu kwa wasanii na wadau wa Sanaa
kuhusu maadhimisho ya siku ya Muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika
mapema wiki hii kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
ulioko ofisi za Baraza hilo Ilala Sharif Shamba. Kushoto kwake ni Katibu
Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza.
Msanii
mkongwe na mchambuzi wa masuala ya Sanaa John Kitime akifafanua juu ya
kwa nini bendi nyingi nchini zilitumia jina la jazz wakati akiwasilisha
mada kwenye maadhimisho ya siku ya muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika
Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba
jijini Dar es Salaam. Wengine kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA
Godfrey Mngereza, Mwakilishi kutoka UNESCO Maximilan Chami na Afisa
Habari wa BASATA Aristides Kwizela
Msanii
Mkongwe wa muziki wa reggae na mchambuzi wa masuala ya Sanaa Innocent
Nganyagwa (Katikati) akiimba sambamba na Katibu Mtendaji wa Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (Kushoto) na Mkuu wa Kitengo
cha Matukio kutoka BASATA Kurwijira Mareges kwenye maadhimisho ya siku
ya Muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa BASATA ulioko
Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
limewaongoza zaidi ya wasanii na wadau wa Sanaa mia moja katika
maadhimisho ya siku ya Jazz duniani yaliyofanyika makao makuu ya Baraza
hilo yaliyoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Maazimisho hayo ambayo
yameazimishwa kwa mara ya kwanza nchini yalipambwa na burudani
mbalimbali kutoka kwa Bendi ya muziki wa Jazz huku wataalam na wasanii
wakongwe wakiwasilisha mada mbalimbali katika kongamano maalum
lililobeba mijadala na hoja mbalimbali kuhusu muziki huo.
Akizungumza kwenye kongamano hilo
Msanii Mkongwe John Kitime alisema kuwa muziki wa jazz una historia ya
aina yake duniani hasa katika kujenga diplomasia baina ya mataifa,
kuunganisha tamaduni mbalimbali duniani na kushiriki katika ukombozi
dhidi ya ukandamizaji na utumwa.
“Sifa kubwa ya muziki huu wa jazz
ni namna ulivyopokelewa na kuvuka mipaka katika tamaduni mbalimbali. Ni
muziki unaoeleza hisia na matukio ya kweli yanayotokea. Ni aina ya
muziki ambao ni urithi wa Dunia kwani una mchango wa pekee” alisema
Kitime.
Awali akielezea historia ya
muziki huu, Mtaalam wa muziki ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Matukio
kutoka BASATA Kurwijira Mareges alieleza kwamba muziki wa jazz una
mizizi yake barani Afrika kabla baadaye kupitia biashara ya utumwa
haujasambaa sehemu mbalimbali duniani na kugeuka urithi wa Dunia nzima.
“Watumwa waliotoka Afrika ndiyo
waliusambaza muziki wa jazz duniani. Walitoka nao Afrika ukachanganywa
na tamaduni za Marekani na baadaye kuzalika jazz tunayoisikia leo.
Waliutumia muziki huu katika kujiliwaza, kutetea haki zao, kupinga
dhuluma na manyanyaso yaliyotokana na utumwa” alisisitiza Mareges
Akizungumza katika maadhimisho
hayo, mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Bw. Maximilan Chami alisema shirika hilo limetenga
siku maalum kwa ajili ya kuadhimisha muziki wa jazz kutokana na mchango
wake katika diplomasia ya utamaduni (cultural diplomacy), kutetea usawa
miongoni mwa jamii na kuwa alama ya urithi wa tamaduni mbalimbali
duniani.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji
wa BASATA Godfrey Mngereza aliwapongeza wasanii na wadau wa Sanaa kwa
kujitokeza kwa wingi katika kuadhimisha siku hiyo huku akisisitiza
kwamba BASATA kwa kushirikiana na wadau litaendelea kuadhimisha tukio
hilo muhimu kila mwaka na kuahidi kuboresha zaidi.
“Nawapongeza sana kwa kujitokeza
kwa wingi katika maadhimisho haya. Huu ni mwanzo mzuri. Tunaahidi
kuendelea kuadhimisha siku hii kila mwaka na kwa ubora zaidi” alisema
Mngereza.
Siku ya muziki wa jazz duniani
imekuwa ikiazimishwa kila mwaka tarehe 30 mwezi Aprili kutokana na
muziki huu kutambuliwa rasmi na Shirika la Umoja wa mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kama urithi wa dunia na ni kwa mara ya
kwanza imeazimishwa nchini Tanzania.
NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015
Na Benedict Liwenga-Maelezo.
Kamati Maalum iliyoundwa kutoka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu
wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015
imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume.
Akizungumza Katika kikao cha
Tume mara baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza, Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa niaba ya Wajumbe
wa Tume amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya
majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume hiyo kwa sasa.
Jaji Lubuva ameeleza kuwa Tume
imeridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa ya kuandaa Rasimu hiyo ikiwa ni
pamoja na muda mfupi uliotumika katika kukamilisha kazi hiyo.
Aidha, ameongeza kuwa lengo ni
kuhakikisha kuwa taarifa hiyo inakamilika na kukabidhiwa kwa Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema
mwezi Julai mwaka huu.
Pongezi hizo pia zimetolewa na
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Ramadhan
Kailima wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo muda mfupi baada ya
kumalizika kwa mkutano wa Tume akieleza kufurahishwa kwake na namna
ambavyo dhana ya ushirikishwaji ilivyotumika katika kuandaa Rasimu hiyo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
iliratibu na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kuanzia Otoba 25
mwaka jana na kuhitimisha rasmi zoezi hilo Machi 20 mwaka huu kwa
Uchaguzi wa Jimbo la Kijitoupele mkoa wa Kaskazini Unguja.
MAPOROMOKO YA ARDHI WILAYA YA MOSHI YAMSHTUA MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ,JAMES MBATIA.
Mbunge
wa Jimbo la Vunjo akisalimiana na mmoja wa waathirika wa mvua kubwa
iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha kufusi kilichokuwa kando ya
nyumba yake kuporomoka na kuhatarisha maisha yake katika kijiji cha Iwa
,Kirua Vunjo katika wilaya ya Moshi.
Mbunge
wa jimbo la Vunjo James Mbatia akizungumza jambo mara baada ya
kutembelea familia ambazo nyumba zao zimeathirika na mvua zilizonyesha
hivi karibuni baada ya kuangukiwa na vifusi na kunusulika vifo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo akitizama zoezi la uondoaji wa Vifusi vilivyo poromoka kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha.
Sehemu ya Kifusi kilichoporomoka kando ya nyumba .
Mkazi
wa kijiji cha Iwa ambaye nyumba yake iliathirika na maporomoko ya
udongo yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha akimuonesha maeneo
yaliyoathirika kuzunguka nyumba hiyo.
Continue reading →MRADI WA KUKUZA TEKNOLOJIA KUPITIA WATOTO XPRIZE WAZINDULIWA DODOMA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa
Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza
teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa
wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka
Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim
Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira
Rodrigues.
Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza
teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa
wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka
Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim
Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira
Rodrigues.
(Picha na Modewjiblog)
Kwa kutambua uwezo walionao watoto katika kubuni vitu mbalimbali, Taasisi
ya XPRIZE iliyo na makazi yake nchini Marekani, imezindua mradi wa
XPRIZE nchini ambao utahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na
malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao watoto
wa miaka 5-12.Akielezea mradi huo, Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, alisema
kuwa wameanzisha mradi huo kwa kutambua uwezo ambao wanao watoto na
kama wakiwezeshwa wanauwezo wa kufanya mambo makubwa.Alisema
dunia ina watoto wengi ambao hawapo shuleni kwa sababu mbalimbali na
hivyo mradi huo utakwenda kufanyika kupitia watoto ambao hawapo
mashuleni na watawapatia vifaa mbalimbali ili waweze kupimwa uwezo wao
katika kazi zinazohusiana na teknolojia.“Dunia
ina watoto Milioni 57 ambao hawapo shuleni tutawatumia kama hao kwa
sababu tunaamini watoto wanaweza kufanya mambo mengi lakini
wanachohitaji ni kuwezeshwa ili waweze kukamilisha mambo wanayofanya,”
ya XPRIZE iliyo na makazi yake nchini Marekani, imezindua mradi wa
XPRIZE nchini ambao utahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na
malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao watoto
wa miaka 5-12.Akielezea mradi huo, Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, alisema
kuwa wameanzisha mradi huo kwa kutambua uwezo ambao wanao watoto na
kama wakiwezeshwa wanauwezo wa kufanya mambo makubwa.Alisema
dunia ina watoto wengi ambao hawapo shuleni kwa sababu mbalimbali na
hivyo mradi huo utakwenda kufanyika kupitia watoto ambao hawapo
mashuleni na watawapatia vifaa mbalimbali ili waweze kupimwa uwezo wao
katika kazi zinazohusiana na teknolojia.“Dunia
ina watoto Milioni 57 ambao hawapo shuleni tutawatumia kama hao kwa
sababu tunaamini watoto wanaweza kufanya mambo mengi lakini
wanachohitaji ni kuwezeshwa ili waweze kukamilisha mambo wanayofanya,”
Wambura-Sitakubali Rasilimali za Taifa hili zichezewe.
Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(wa
pili kushoto) akipata msaada wakati akiteremka toka katika kiwanja cha
shirika la utangazaji Tanzania(TBC) kulipojengwa nyumba za watumishi wa
shirika hilo ambazo hazijaisha kwa zaidi ya miaka 20 sasa na kutoa
maagizo ya kumalizia nyumba hizo au kuwapa Halmashauri ya Kisarawe ili
wajenge Hostel za wanafunzi.(Picha na Daudi Manongi-WHUSM)
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC)
Bi.Joselin Lugola akitoa mrejesho kuhusu nyumba za shirika hilo zilizo
kisarawe mkoani Pwani ikiwemo kukamilisha upatikanaji wa hati wa eneo
hilo na kuliendeleza ili watumishi wa TBC wa kisarawe walitumie kwa
makazi.
Kaimu
mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi.Nahya Mansour(wa kwanza kushoto)
akimskiliza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe
Anastazia Wambura(hayupo pichani) wakati akitoa maagizo juu ya nyumba za
Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) zilizopo eneo la kimani Kisarawe
mkoa wa Pwani.wengine pichani ni Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Kisarawe
Bi.Mwanamvua Mrindoko(wa pili kushoto).
Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura
akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika
la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola wakati alipofanya ziara
katika nyumba za shirika hilo zilizopo kisarawe mkoani Pwani.
……………………………………………………………………………………….
Na.Daudi Manongi-WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura ametoa wito kwa
Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kutunza Rasilimali za Taifa kwa kuwa
ni pesa inayotoka na jasho la mlipa Kodi na ingeweza kutumika kwa kazi
nyingine kuliko uharibifu unaofanyika katika kiwanja cha Shirika hilo
kilicho eneo la kimani ambako zimejengwa nyumba za wafanyakazi wa
shirika hilo waliopo kisarawe mkoa wa Pwani.
Mhe.Wambura alisema hayo wakati
alipotembelea eneo la shirika hilo ili kupata mrejesho wa maagizo
aliyotoa wakati alipofanya ziara ya kwanza katika eneo hilo Aprili 2011
mwaka huu na kuipatia siku saba Idara ya Miradi ya shirika hilo
ikishirikiana na Halmashauri ya kisarawe kufanikisha upatikanaji wa hati
miliki ya eneo hilo la makazi ya wafanyakazi wa shirika hilo.
“Taratibu za Kisarawe za
upatikanaji wa hati zimekamilika na sasa wamepeleka ile Rasimu kwa
kamishna wa hati kanda ya mashariki ,na maelezo tumeyaskia kwamba
kulikuwa na kupishana katika uaandaaji wa hati ndo maana ikachelewa
lakini kwa sasa hivi bado tunaitaji kulinda rasilimali za
Taifa.Tunaitaji kuzuia uhalibifu”,Alisema Mhe Wambura.
Aidha Mhe Wambura ametoa maagizo
kwa shirika hilo kuangalia uwezekano wa kuendeleza makazi hayo kwa kuwa
mpaka sasa imepita miaka 20 eneo hilo halijaendelezwa na shirika hilo au
kufanyiwa uwekezaji wowote au wakabidhi eneo hilo kwa halmashauri ya
kisarawe ili wajenge hostel za wanafunzi na kuongeza kwamba yeye
hatakubali eneo hilo lipotee kwa uharibifu kwa wananchi kubomoa nondo
na kuuza kama vyuma chakavu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali watu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)
Bi.Joselin Lugola alimwahidi waziri huyo kuwa watahakikisha kwenye
bajeti ya mwaka 2017/18 suala hilo linashughulikiwa na kudai kwamba
mara nyingi wanaweka pesa ya ukarabati lakini inakatwa lakini wataanza
ukarabati kwa awamu kwa mikoa ya Arusha na Mwanza na makao makuu kwa
hiyo hata izi za kisarawe zitakarabatiwa mara moja.
TAARIFA KWA WATANZANIA WOTE WAISHIO NCHINI UINGEREZA [TUJUMUIKE UK].
Kikosi kazi cha watanzania wanaoishi Falme za UINGEREZA na EIRE YA KASKAZINI (TZUK Diaspora Taskforce, kwa kifupi, TZUK-DTF) kiliasisiwa na Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe mwaka 2014, kutokana na kutokuwepo na chombo/Jumuiya madhubuti ya kuwaunganisha Watanzania waishio hapa Uingereza
TZUK-DTF
ilianza na wajumbe 11 wakiwemo maofisa wa ubalozi 2 kikiwa na majukumu
makubwa ya kuwa kiunganishi kati ya watanzania na ubalozi wao hapa
Uingereza pamoja na kupanga na kuratibu ufufuaji wa Jumuiya ya
watanzania ambayo itakuwa shirikishi zaidi na endelevu. Mnamo mwishoni
mwa mwaka 2015, chini ya Naibu Balozi, Mheshimiwa Msafiri Marwa,
ilikubaliwa kwamba ili kutimiza malengo yake kwa ufanisi zaidi
yaliyohusisha kuratibu ufufuaji wa Jumuiya ya watanzania Uingereza na
kuhakikisha kwamba Jumuiya hiyo inakuwa na Katiba iliyo bora zaidi,
ilionekana ni vyema TZUK-DTF ikawa na wajumbe zaidi watakaojumuisha
watanzania wa kada mbalimbali walioko Uingereza wakiwemo waliokuwa
viongozi wa mikoa wa Jumuiya na baadhi ya wale walioshiriki katika
michakato ya uasisi wa katiba na uundwaji wa Jumuiya ya watanzania
Uingereza.
Kikosi
Kazi hiki kipya kilikutana rasmi tarehe 05 Mwezi wa Kumi na Mbili,
2015, chini ya uongozi na ulezi wa Mheshimiwa Naibu Balozi, Msafiri
Marwa, ambapo kiliainishiwa majukumu yake kama ifuatavyo:
1. Kujadili na kuziwekea mikakati ya ufumbuzi changamoto mbalimbali zilizokabiliwa na TZUK-DTF katika kutimiza majukumu yake ikiwemo na zile ambazo ziliikabili Jumuiya ya watanzania iliyokuwepo.
2. Kupitia
maoni ya watanzania yaliyokuwa yamekusanywa tayari, ikiwemo na katiba
za Jumuiya ili Jumuiya iwe na katiba bora zaidi itakayoongeza ufanisi
katika shughuli zaJumuiya.
3. Kuhakiki na kuboresha muundo wa Jumuiya utakaokidhi mahitaji ya sasa ya watanzania waishio Uingereza.
4. Kuzikusanya
na kuzipitia taarifa zote zitakazopatikana za fedha za Jumuiya enzi za
uhai wake na kuzijumuisha kwenye Jumuiya mpya itakayoundwa
5. Kutengeneza na kuratibu njia bora zamawasiliano miongoni mwa wanajumuiya.
6. Kusimamia
kipindi cha mpito kitakachopelekea kuundwa kwa Jumuiya ya watanzania
Uingereza ikiwemo kuratibu uanzishaji/uimarishaji wa Jumuiya za
watanzania za mikoani kwa mujibu wa katiba mpya, na
7. Kuandaa
na kusimamia mkutano mkuu wa watanzania wote wa Uingereza wenye
madhumuni ya kutoa ripoti nzima ya TZUK-DTF, kupitisha katiba mpya,
kutambulisha Kamati Kuu na uongozi mpya wa Jumuiya, kujadili na kuhakiki
mipango na mikakati ya shughuli mbalimbali za Jumuiya kwa mwaka ujao,
na Kikosi Kazi kuvunjwa rasmi na kukabidhi madaraka ya usimamiaji na
uendeshaji wa Jumuiya ya watanzania kwa uongozi mpya wa Jumuiya.
Kama watanzania wa Uingereza mlivyoshiriki katika upendekezaji wa katiba mpya na kutoa maoni juu ya Jumuiya yenu, tunaendelea kuwatia moyo kushiriki kwa moyo mmoja na wa kizalendo pindi tutakapoitisha mikutano ya watanzania kwenye mikoa mliyoko mwezekuhakikisha safari hii ya kuwa na Jumuiya iliyo/zilizo imara inafikia mwisho ulio mwema
Ahsanteni
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. ALI MOHAMED SHEIN AAPISHWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman akimuapisha Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa mjumbe wa
Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake
kwenye Baraza hilo huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo katika Ikulu ndogo ya
Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein mara baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri katika
Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman mara
baada ya tukio la uapisho. PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………………………………………
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei,
2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na
kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo.
Rais Shein ameapishwa na Jaji
Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman katika Ikulu ndogo ya
Chamwino Mkoani Dodoma, tukio ambalo limeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Viongozi wengine walioshuhudia
tukio hilo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa
Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Wakati huo huo, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo mchana
ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Baraza la Mawaziri, uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI Mjini
Dodoma.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
02 Mei, 2016
KIKAO CHA KAMATI YA NIDHAMU MEI 3, 2016
Kikao
cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kinafanyika kesho Jumanne Mei 3, 2016 kwenye ukumbi wa ofisi za
shirikisho zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es
Salaam.
Kikao hicho cha kupitia mashauri
mbalimbali yaliyowasilishwa TFF, ilikuwa kifanyike Jumapili Mei Mosi,
lakini kiliahirishwa kwa sababu ya wajumbe wengi walikuwa na udhuru.
Wadau watakaojadiliwa kesho ni
pamoja na Kocha Mkuu wa Azam FC ya Dar es Salaam, Stewart Hall na
wachezaji wake wakiwamo John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula na
Kipre Tchetche.
Wengine ni nyota wa Young
Africans SC ya Dar es Salaam ambao ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma
wakati kutoka timu ya JKT Rwakoma ya Mara wamo Paulo Jinga, Zephlyn
Laurian na Idrisa Mohamed.
Wengine ni Ismail Nkulo, Said
Juma, Idd Selaman na Edward Amos wa Polisi Dodoma, kadhalika Abel
Katunda wa Transit Camp ya Dar es Salaam na daktari wa Coastal Union ya
Tanga, Dk. Mganaga Kitambi.
Pia Herry ‘Mzozo’ Chibakasa wa
Friends Rangers ya Dar es Salaam naye atajadiliwa na Bunu Abdallah
ambaye ni Kocha Msaidizi wa JKT Oljoro ya Arusha.
MECHI YA NDANDA VS YANGA
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda FC
ya Mtwara na Young Africans umerudishwa nyuma kwa siku moja na sasa
itachezwa Mei 14, 2016 badala ya Mei 15, 2016 kama ratiba ya awali
inavyosomeka.
Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema sababu za kurudisha nyuma mchezo huo Na. 218 utakaofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ni kuipa timu ya Young Africans nafasi ya kujiandaa na kusafiri kwenda nchini Angola kwenye mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mbali ya mechi hiyo, kuna michezo miwili ambayo imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hizo ni kati ya Simba na Mwadui ambayo sasa itachezwa Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni kwamba Mei 7, 2016 kutakuwa na mchezo wa kimataifa utakaozikutanisha Young Africans dhidi ya Esperanca ya Angola kuwania Kombe la Shirikisho.
Mchezo mwingine uliosogezwa mbele ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC ambao sasa utafanyika Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni Uwanja wa Kambarage Shinyanga. Mei 7, 2016 uwanja huo utakuwa na mchezo kati ya Stand United ya Shinyanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Kadhalika Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea kesho Mei 3, 2016 kwa mchezo mmoja ambao Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Jumatano Mei 4, 2016 Azam FC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Michezo hiyo itaanza saa 10.000 jioni na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni ya Azam.
Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema sababu za kurudisha nyuma mchezo huo Na. 218 utakaofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ni kuipa timu ya Young Africans nafasi ya kujiandaa na kusafiri kwenda nchini Angola kwenye mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mbali ya mechi hiyo, kuna michezo miwili ambayo imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hizo ni kati ya Simba na Mwadui ambayo sasa itachezwa Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni kwamba Mei 7, 2016 kutakuwa na mchezo wa kimataifa utakaozikutanisha Young Africans dhidi ya Esperanca ya Angola kuwania Kombe la Shirikisho.
Mchezo mwingine uliosogezwa mbele ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC ambao sasa utafanyika Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni Uwanja wa Kambarage Shinyanga. Mei 7, 2016 uwanja huo utakuwa na mchezo kati ya Stand United ya Shinyanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Kadhalika Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea kesho Mei 3, 2016 kwa mchezo mmoja ambao Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Jumatano Mei 4, 2016 Azam FC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Michezo hiyo itaanza saa 10.000 jioni na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni ya Azam.
KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU
Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kesho Jumanne Mei 3, 2016 saa 5:00
asubuhi itatangaza uamuzi wa rufaa nane zilizowasilishwa na kujadiliwa
za viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza
Tanzania Bara 2015/2016.
Kamati hiyo itatangaza uamuzi
huo mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi za
TFF, zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es
Salaam.
Jumla ya rufaa nane zinazohusu
timu, kocha, viongozi na mchezaji mmoja zilijadilikuwa na kamati hiyo
kwa Jumapili Mei mosi, 2016 kwenye ofisi za TFF jijini.
Rufaa zilizojadiliwa kwenye kikao hicho ni za:
- Timu ya Geita Gold
- Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC
- Denis Richard Dioniz – Kipa wa Geita Gold
- Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
- Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma
- Timu ya Soka ya Polisi Tabora
- JKT Oljoro Fc ya Arusha
- Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora
Wadau hao wa soka walikata rufaa
dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia
hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi
Daraja la Kwanza. Wakata rufaa wote walihudhuria kikao cha rufaa zao.
Waziri Makamba awasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka
wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka
wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi kuhusu wizara hiyo leo Bungeni mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla (kushoto) akiwa Bungeni
leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Dkt.
Ashatu Kijaji.
Baadhi
ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mazingira na Muungano January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa
fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Mwanafunzi
wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini
Mwanza Getrude Clement akiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa mwaliko wa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January
Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wake kwenye
utunzaji wa mazingira. Mwanafunzi huyo alihutubia viongozi mbalimbali wa
dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia
nchi, uliofanyika New York Marekani.
Mashududa
walihusika katika zoezi la kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, wakiwa Bungeni leo mjini Dodoma
kwa mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na
Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango
wao katika kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanzania.
Mwanafunzi
wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini
Mwanza Getrude Clement (wa pili kushoto) ambaye alihutubia viongozi
mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu
mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani akiwa na
wanafunzi wenzake Bungeni leo mjini Dodoma.
Naibu
Spika Dkt Tulia Ackson na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,
Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakiwa katika picha ya pamoja
na mashuhuda waliohusika katika zoezi la kuchanganya udogo wakati wa
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. Mashuhuda hao
walikuja kutembelea Bunge leo Mei 2, 2016.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
………………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.
Serikali inaendelea kusimamia
mazingira na kuhakikisha mifuko ya plastiki inayotumika nchini iwe ni
ile inayokidhi viwango vianvyokubalika ili kuondokana na changamoto ya
kuzagaa kwa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni
mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na
Muungano January Makamba alipokuwa akitoa hoja ya wizara yake
kuidhinishiwa maombi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Makamba amesema kuwa sababu kubwa
ya kusambaa kwa mifuko plastiki inatokana na mifuko hiyo kutolewa bure
na hivyo kuchafua mandhari na kuziba mifereji sehemu mbalimbali hali
inayosababisha athari kubwa katika mazingira.
“Asilimia kubwa kwenye mito,
maziwa na fukwe za bahari imejaa mifuko ya plastiki, hali hii ni hari
kwa usalama wa mazingira yetu” alisema Makamba.
Akiwasilisha hotuba yake, Waziri
Makamba amesisitiza kuwa mifuko ya plastiki isiyotakiwa kutumika nchini
ni ile yenye unene chini ya maikroni 50 ambayo hairuhusiwi kuzalishwa
wala kuingizwa.
Kwa mujibu wa maelekezo ya bajeti
ya mwaka wa fedha 2015/2016, Waziri huyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu
wa Rais imekamilisha kanuni mpya ya mifuko ya plastiki zinazorekebisha
viwango vya unene unaoruhusiwa kutoka Maikroni 30 kwenda Maikroni 50.
Waziri Makamba amesema kuwa
kanuni hizo tayari zimesainiwa kupitia tangazo la Serikali Na.271 la
mwaka 2015 na kutolewa katika Gazeti la Serikali Julai 17, 2015 na
kupewa Na. 29.
Kwa upande wake mwanafunzi mwenye
umri wa miaka 16 wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari
Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement ambaye alihutubia viongozi
mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu
mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani amewahimiza
Watanzania kutunza mazingira na kufauata maelekezo yanayotolewa na
Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.
Getrude amesema kuwa amefarikjika
kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia kwenye mkutano wa
mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana kusaini
makubaliano ya Paris.
Katika kuwahimiza vijana kujenga
tabia ya kutunza mazingira, Getrde amewaasa vijana hasa wanafunzi
kusimamia sauala la utunzaji wa mazingira wakiwa shuleni kwa kwa
kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na klabu ya “Mali
Hai” iliyopo shuleni anaposoma.
Kwa upande wa Watanzania kwa
ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude amesema kuwa ni vema
wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia utunzaji wa mazingira
hasa matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mwanafunzi huyo amekaribishwa na
kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa heshima ya kuliwakilisha
vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano ya namna ya kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki
moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao na kusema “Ni furaha yangu
kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi
Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana”.
Wafanyakazi TBL Group Dar,Mwanza , Mbeya,Arusha walivyosherehekea Mei Mosi
Wafanyakazi
wa TBL Dar es salaam katika maandamano wakiandamana wakati wa
maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Duniani Mei Mosi zilizofanyika
jana Duniani kote Kitaifa sherehe hizo zimefanyika mkoani Dodoma huku
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiongoza sherehe hizo.
Wafanyakazi
wa TBL mkoani Arusha katika maandamano wakiandamana wakati wa
maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Duniani Mei Mosi zilizofanyika
jana
Wafanyakazi
wa TBL mkoani Mbeya katika maandamano wakiandamana wakati wa
maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Duniani Mei Mosi zilizofanyika
jana
Wafanyakazi
wa TBL mkoani Mbeya katika maandamano wakiandamana wakati wa
maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Duniani Mei Mosi zilizofanyika
jana
Wafanyakazi wa TBL wakiwa katika sherehe hizo mkoani Mwanza
Vyeti vya kuzaliwa wilayani Micheweni Pemba havitolewi kwa misingi ya kisiasa
Na Masanja Mabula –Pemba
SERIKALI ya Wilaya ya Micheweni
Mkoa wa Kaskazini Pemba imekanusha taarifa zilizotolewa na wananchi ya
kwamba vyeti vya kuzaliwa katika Wilaya hiyo hutolewa kwa misingi ya
kisiasa .
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Abeid
Juma Ali aliyaeleza hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara ambao
baadhi yao waliodai kwamba kuna ubaguzi juu ya utoaji wa vyeti vya
kuzaliwa
Alisema kuwa kwa kipindi cha
miezi mitano tangu ashike wadhifa huo tatizo la upatikanaji wa vyeti
vya kuzaliwa kwa watoto katika wilaya hiyo limeanza kupatiwa ufumbuzi .
Alifahamisha kuwa kwa
kushirikiana na watendaji wa Ofisi ya Vizazi na Vifo , ameanza
kulipunguza tatizo hilo , ambapo watoto wengi wameweza kupatiwa vyeti
kwa wakati na bila usumbufu .
“Mtoto hana chama iweje
basi nimbague kwa misingi ya siasa , natambua wajibu na majukumu yangu
kwani mimi ni mtumishi wa umma na ninawatumikia wananchi wote pasi na
ubaguzi ”alifahamisha .
Awali mfanyabiashara Ali Salimu
Ali (Baraka) wa Wingwi alisema kwamba kunahitaji kuangaliwa upya Ofisi
inayohusika na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwani imekuwa ikichelewesha
kupatikana kwa vyeti kwa baadhi ya watoto .
Alieleza kwamba wapo watoto
wamefikia umri wa kwenda skuli lakini hawana vyeti vya kuzaliwa , licha
ya kwamba kumbukumbu zao zipo katika Ofisi ya vizazi na vifo lakini
zimeshindwa kufanyiwa kazi .
“Vyeti vya kuzaliwa bado ni
tatizo , kwani kuna baadhi ya watoto wamefikia umri wa kuanza skuli ,
lakini hawana vyeti , tunaomba hii Ofisi inayohusika na utoaji wa vyeti
uiangalie upya nahisi kama kuna ubaguzi fulani hivi ”alisema .
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na
Madiwani wa Wilaya hiyo ambapo Mkuu wa Wilaya alitumia fursa hiyo
kuwataka wafanyabiashara kuwapa ushirikiano wakati wanapokusanya
mapato yatokanayo na biashara zao.
RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza
kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo
Mei 2, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini
Dodoma leo Mei 2, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini
Dodoma leo Mei 2, 2016
PICHA NA IKULU
Serikali kutumia dola milioni 690 kuimarisha miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Alois
Matei akiwaeleza waandishi habari kuhusu mradi wa maboresho ya Bandari
ya Dar es Salaam utakaogharimu kiasi cha Dola za Marekani milioni 690
ambapo mradi huo unafadhiliwa na Serikali, Benki ya Dunia,Trade Mark
East Afrika na DFID, kulia ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka
hiyo Bw. Focus Mauki na mwisho Kapteni Abdullah Mwingamno wa TPA Bandari
ya Dar es Salaam.
Mhandisi
Mkuu wa TPA Bi Mary Mhayaya akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa Flow
meter mpya ya Kigamboni ambao umeshakamilika na hivyo kuwezesha mafuta
yote yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam kupimwa na
kujulikana kiasi halisi kilichoingizwa hapa nchini ili kuiwezesha
Serikali kupata mapato stahiki ikiwemo kodi .
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia taarifa ya Mamlaka ya Bandari TPA iliyokuwa ikitolewa na
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Injinia Alois Matei kwenye ukumbi wa
Idara ya Habari Maelezi leo
No comments :
Post a Comment