Tuesday, May 31, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMWAKILISHA RAIS DKT JOHN MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA, NCHINI PAPUA NEW GUINEA


ra11 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Papua New Guinea Mhe. Peter O Neil Alipowasili Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. 
rai2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe walipokutana Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. 
rai3 
Wimbo wa taifa ukipigwa katika mkutano huo
rai4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia kwa makini Hotuba ya Waziri Mkuu wa Papua New Guinea Mhe. Peter O Neil alipokua akifungua mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Guinea leo Mei 31,2016  Mkutano huo unaojadili kuhusu masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. 
rai5 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia kwa makini Hotuba ya Waziri Mkuu wa Papua New Guinea Mhe. Peter O Neil alipokua akifungua mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Guinea leo Mei 31,2016  Mkutano huo unaojadili kuhusu masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific waliohudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili  unaojadili kuhusu masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, katika kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. Mkutao huo umefunguliwa leo Mei 31,2016 katika kituo cha mikutano cha ACC mjini Papua New Guinea. (Picha na OMR)
rai7 
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius B. Likwelile.na katibu wake Waziri RajabMakamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius B. Likwelile.na katibu wake Waziri Rajab
rai8 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akichangia baadhi ya mada zilizowasilishwa kwenye mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Guinea leo Mei 31,2016.  Mkutano huo unaojadili kuhusu masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa.
rai9

Serikali yaanza kutumia TEHAMA Kuendesha mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.

mae1 
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Bi. Riziki Abraham (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari Leo jijini Dar es salaam kuhusu utaratibu mpya wa kutumia teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kutangaza nafasi za kazi,kupokea maombi,kuwaita kwenye usaili waombaji wa kazi na kuwapa  taarifa za kazi na kuwawezesha waombaji kupata ajira kwa kutumia mfumo huo (TEHAMA).Kulia ni Kaimu Naibu Katibu wa Sekretarieti hiyo anayeshughulikia TEHAMA Bi. Mtage Ugullum.
mae2 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais  Sekretarieti ya Ajira uliofanyika leo jijini Dar es salaam Ukilenga kutoa taarifa kuhusu matumizi ya  teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuendesha mchakato wa ajira katika utumishi wa umma.
(Picha na Idara ya Habari Maelezo)
……………………………………………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo.
Serikali imeanza kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( TEHAMA) katika kutangaza nafasi za kazi,kupokea maombi,kuwaita waombaji kazi kwenye usaili na kuwawezesha kutumia teknolojia hiyo kupata ajira.
 Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Bi Riziki Abraham wakati wa mkutano na Vyombo vya Habari uliolenga kueleza mikakati ya Serikali kuboresha mfumo wa kupokea maombi ya ajira  na kuyashughulikia.
 “Sekretarieti ya Ajira inatoa rai kwa waombaji fursa za Ajira kujisajili katika mfumo wa Ajira unaopatikana kupitia anuani ya tovuti ya www.ajira.go.tz na mfumo wa” job alert system” au kupitia simu za kiganjani kwa kupiga *152*00# ili kuomba fursa za ajira zinazopatikana” Alisisitiza Riziki.
Akifafanua kuhusu faida za kutumia TEHAMA kuendesha mchakato wa ajira, Riziki amesema kuwa mfumo huo unasaidia kupunguza idadi ya siku za kuendesha mchakato wa ajira kutoka siku 90 hadi 52 kwa sasa.
Aliongeza faida nyingine kuwa ni Serikali inapanua wigo wa utoaji taarifa za uwepo wa fursa za Ajira hasa kwa waombaji wa ajira waishio vijijini.
Alisema mfumo huu unalenga kupunguza changamoto kadhaa zikiwemo malalamiko ya baadhi ya waombaji fursa za ajira kuhusu upotevu wa maombi yao ya kazi.
Hadi kufikia Mei, 2016 jumla ya waombaji wa fursa za Ajira waliokuwa wamejiandikisha kwenye mfumo wa utumaji maombi ya kazi walikuwa (97,765).
Aidha jumla ya waombaji wa fursa za Ajira 89,484 wamejiunga kwenye mfumo wa kupata taarifa za uwepo wa fursa za Ajira kupitia simu za kiganjani.

WAZIRI MKUU: WATAALAMU WA MALIKALE KUWENI WABUNIFU

LIW4 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa mambo ya malikale na uhifadhi wa urithi asilia (natural heritage) watafute mbinu zitakazoimarisha utunzaji wa rasilmali hizo bila kuathiri mifumo ya uchumi ya nchi zinazoendelea.
Ametoa wito huo leo (Jumanne, Mei 31, 2016), wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa siku nne unaojadili Uhifadhi wa Urithi wa Dunia wa Afrika kama Nyenzo ya kuleta Maendeleo Endelevu ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha.
Waziri Mkuu amesema kuna baadhi ya nchi ambazo ni maskini sana lakini zimebarikiwa kuwa na rasilmali kama madini na gesi asilia lakini kwa sababu rasilmali hizo ziko karibu sana na vivutio vya urithi asilia wa dunia, watu wa nchi hizo wanazuiwa kuchuma rasilmali zao ili wasiharibu vivutio hivyo.
“Tunatambua umuhimu wa kutunza rasilmali na vivutio vya urithi asilia. Hivi ni kwa nini zisitafutwe teknolojia zinazofaa ambazo zitaruhusu uvunaji wa gesi asilia na madini bila kuathiri uhifadhi wa vivutio vya urithi asilia wa dunia (world heritage sites)?”, alihoji Waziri Mkuu.
“Serikali za nchi za Kiafrika zinahitaji suluhisho kama hili wakati zikiendelea kutafuta njia sahihi za kuwianisha uhifadhi wa vivutio vya urithi wa dunia na changamoto ya kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake,” amesema.
“Sisi viongozi ambao wengi wetu ni wanasiasa, hatukatai ushauri wa wataalamu lakini tunawasihi baadhi yenu ambao mnashiriki mkutano huu muhimu, mtafute njia mbadala za kufumbua tatizo hili badala ya kuendelea kutegemea njia za kizamani za kukabiliana na changamoto kama hizi ili sote tuweze kunufaika na rasilmali zilizopo ikiwa ni pamoja na kutunza vivutio vya urithi asilia wa dunia,” aliongeza.
Amesema kama rasilmali hizo zitachambuliwa vizuri na kwa njia sahihi bila kuathiri vivutio vya urithi wa dunia, ni dhahiri kuwa zitaingiza mapato ambayo kiuchumi yatasaidia kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi ambao pia watasaidia kwenye uhifadhi wa vivutio hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilmali nyingi zikiwemo za ardhini (madini), misitu, wanyama na maeneo ya kihistoria na kusisitiza kuwa Watanzania wana jukumu la kuzilinda ili zilete tija kwa wananchi wote.
“Tukizitunza rasilmali zetu zitasaidia kupata mapato kutokana na utalii Serikali itapeleka sehemu ya mapato haya katika miradi mbalimbali na hivyo kuchangia kwenye pato la Taifa,” amesema.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na UNESCO hasa katika masuala yanayohusu uhifadhi wa vivutio vya dunia kutokana na umuhimu wake kwenye maendeleo endelevu.
Alisema wizara yake imelenga kusimamia, kuendeleza na kuimarisha utunzaji wa maliasili na uhifadhi wa vivutio asilia na vya kiutamaduni (natural and cultural heritage) kwa kushirikiana na wadau wengine hapa nchini.
Naye Mkurugenzi wa Uhifadhi Malikale wa UNESCO, Dk. Mechtild Rossler aliwataka washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali duniani wawe tayari kupitia upya shughuli zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia wajibu wa nchi za Kiafrika katika kuandaa mwelekeo wa miaka ijayo.
Alisema katika miaka 40 ya utendaji wa UNESCO, idadi ya vivutio vya urithi wa dunia imeongezeka na kufikia 89 ambapo kati ya hivyo viko baadhi vinakavyobiliwa na changamoto ya kufutika kutokana na athari za kigaidi, matukio ya kivita na kazi za kibinadamu.
“Vivutio 16 kati ya 48 viko katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara na hivi vinakabiliwa na tishio la kupotea kutokana na vita, harakati za kigaidi na shughuli za kiuchumi za kibinadamu zikiwemo uchimbaji wa madini na gesi asilia,” alisema.
Aliwataka washiriki wa mkutano huo wakumbuke kuwa vivutio vya urithi wa dunia ni vielelezo vya jamii na pia huchangia uchumi kwa kutoa ajira kwenye jamii husika.
Mkutano huo unaohudhuriwa na washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani, unajumuisha washiriki kutoka nchi 36 zikiwemo nchi 12 ambazo ni za nje ya bara la Afrika.
Waziri Mkuu amerejea mjini Dodoma mchana huu kuendelea na vikao vya Bunge.

Kampuni ya Regency Innovation Solutions na United Bank for Africa [Tanzania] wazindua kadi ya malipo ya kipekee Afrika

1 
Bw.Tesha Philemon Kaimu Mkurugenzi wa KItengu cha Huduma za Kibenki Mtandaoni Benki ya UBA kushoto akibadilishana mikataba na Bw. Mike Raymond Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Regency Innovation Solutions baada ya kusaini mkataba wa kutoa huduma ya kadi ya malipo ya kipekee ya Visa inayoitwa  Mimosa Black Card leo kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es salaam.
3 
Bw.Tesha Philemon Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Kibenki Mtandaoni Benki ya UBA kushoto na Bw. Mike Raymond Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Regency Innovation Solutionswakionyesha  kadi ya malipo ya kipekee ya Visa inayoitwa  Mimosa Black Card iliyozinduliwa leo baada ya kampuni hizo kutiliana sahihi mkataba wa kufanya biashara kwa pamoja.
4 
Bw.Tesha Philemon Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Kibenki Mtandaoni Benki ya UBABw.Takizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………………………………..
Kampuni ya uvumbuzi na suluhisho inayoitwa Regency Innovation Solutions na benki ya UBA ya Tanzania wamesaini mkataba wa maelewano wa kutoa huduma ya kadi ya malipo ya kipekee ya Visa katika bara zima la Afrika wakianzia nchini Tanzania. Taarifa hii imetolewa leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kadi mpya ya malipo itakayoitwa Mimosa Black Card, kadi ambayo itaruhusu mteja kuweka na kutoa fedha bila ya kuhitaji akaunti ya benki.
Mkurugenzi Mkuu wa Regency Innovation Solution Mike Raymond alisema “Tumefurahi kushirikiana na benki ya UBA Tanzania katika uendelezaji wa uvumbuzi ambao utaanzia hapa Tanzania. Lengo letu ni kuleta suluhisho zilizo salama na kuaminika kwa wateja wetu. Kadi hii ya Mimosa ni ya kisasa ambayo sio tu ni salama na inayorahisisha huduma bali ina huduma nyingine nyingi na zawadi kwa wateja. Kupitia huduma hii tunaongeza wigo wa huduma za kifedha katika nchii ya Tanzania haswa kwa sababu kadi hii imeunganisha na huduma za pesa kupitia mitandao ya simu.”
Kadi hii mpya ni sawa na kadi ya kawaida ya malipo ya kabla ila ni ya kipekee kwa sababu haiunganishwi na akaunti ya benki hivyo kuifanya kuwa ya gharama nafuu na pia urahisi wa kuweka na kutoa fedha. Kadi hii pia italindwa kwa neno la siri (PIN) na teknolojia ya juu ya ulinzi. Kwa maana hiyo watumiaji wa kadi ya Mimosa wanaweza kutoa fedha katika mashine za kutolea fedha (ATM), kufanya malipo ya kutumia kadi katika maeneo yote yenye huduma hiyo na pia kufanya manunuzi mtandaoni mahali popote duniani kupitia mtandao wa Visa.  Vile vile wateja wanaweza kuweka pesa katika kadi zao kupitia tawi lolote la UBA Tanzania au mitandao ya simu M-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na pia katika akaunti za kukusanya fedha katika benki za CRDB na Exim.
“Tanzania tayari ina mfumo wa teknolojia ya kuwa jamii isiyotumia fedha. Kupitia kadi zetu tunawahamasisha wateja wetu kupokea mfumo huu wa kufanya malipo bila kutumia fedha. Zaidi ya hapo wateja wetu watapata punguzo la bei katika baishara mbalimbali sio tu Tanzania bali barani Afrika na baadaye ulimwengu mzima watakapofanya manunuzi kupitia kadi hizo. Wateja pia wanaweza kupata fedha za dharura hadi shillingi Milioni moja kwa riba ya asilimia sifuri,” aliongeza Raymond.
Naye Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha za Kielektroniki wa UBA Tanzania, Tesha Philemon, alisema kuwa “ Lengo letu kuu ni kubadilisha mfumo wa jinsi watu wanavyotumia huduma za kibenki haswa kwa kujikita katika kundi la wale ambao hawatumii huduma za benki kwa kupitia teknolojia kama hizi. Tunaamini kuwa ushirikiano huu kati ya UBA Tanzania na Regency Innovation Solutions utafanikisha lengo letu la kuwafikia wale wasiotumia huduma za benki na kuwajumuisha katika huduma hizi katika Tanzania na bara la Afrika.
Tanzania ni nchi ya kwanza katika ushirika huu kuanza kutumia teknolojia hii. Kampuni ya Regency Innovation Solutions tayari ina miradi kama hii katika nchi za Zambia na Uganda na wana mpango mkubwa wa kuleta mabadiliko makubwa katika kutoa vitambulisho kwa kutoa vitambulisho vya ushirika vya Visa kwa wanafunzi na makampuni na katika siku za karibuni pia watazindua kadi za malipo kabla za Visa za Dhahabu na Platinum.
Fursa
  • Kuwa wakala wa usambazaji wa kadi hizi tafadhali tuma barua pepe kwa Meneja wa Akaunti kupitia : RegencyInnovation@gmail.com
  • Kusajili kampuni yako kuwa katika orodha ya biashara zitakazotoa punguzo kwa wateja zaidi ya 500 wa kadi za Mimosa, tutumie barua pepe kwa Meneja wa Akaunti kupitia :

Balozi Herbert Mrango akagua ukarabati MV Magogoni.

KIV1 
Kaimu Mtendaji wa TEMESA Mhandisi Manase Ole kujan (Kushoto) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Balozi Herbert Mrango (katikati) wakati Bodi hiyo ilipotembele ukarabati wa kivuko cha magogoni.
KIV2Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Balozi Herbert Mrango( wa tatu kulia) akiongoza na wajumbe wa bodi hiyo wakati Bodi hiyo ilipotembele ukarabati wa kivuko cha magogoni.
KIV3Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Silvester Simfukwe (katikati walio chuchumaa) akiwaonesha Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) sehemu ya kivuko cha Magogoni inayoendelea kufanyiwa ukarabati.
KIV4 
Kivuko cha Magogoni kikiwa katika ukarabati katika Bandari ya Dar es Salaam.
Picha na Theresia Mwami-TEMESA.
………………………………………………………………………………………………………………
Na Theresia Mwami- TEMESA
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imetembelea na kujionea maendeleo ya ukarabati wa kivuko cha Mv Magogoni chini ya kampuni ya Songoro Marine katika Bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Balozi Herbert Mrango ameeleza kuridhishwa na kasi ya ukarabati wa kivuko hicho na kuushauri uongozi wa TEMESA kuharakisha malipo yanafanyika kwa wakati ili kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa.
“Nakuagiza Kaimu Mtendaji uhakikishe malipo kwa kampuni hii yanafanywa kwa wakati na ukarabati huu kukamilika mapema ili kuwapa fursa wananchi kutumia kivuko hiki”alisema Balozi Mrango.
Aliongeza kuwa ni muhimu wananchi kurejeshewa huduma ya kivuko hicho ili kuondoa kero inayowakabili kwa sasa kwa kuwa na kivuko kimoja chenye uwezo wa kubeba magari ambapo kukamilika kwa ukarabati wa huu utakuwa umerahisiha shughuli ya usafirishaji.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji wa TEMESA Mhandisi Manase Ole kujan amesema atahakikisha malipo yanafanyika kwa wakati ili kuwezesha mkandarasi huyo kumaliza kazi hiyo kwa muda uliopangwa na kurejesha huduma ya kivuko hicho kwa wananchi.
Aidha aliongeza kuwa kazi ya ukarabati wa kivuko hicho imegawanywa katika sehemu mbili ambazo ni, ukarabati wa “Body” pamoja na mifumo ya umeme unaofanywa na Mkandarasi kutoka kampuni ya Songoro Marine huku TEMESA ikihusika na ukarabati wa mitambo ya kuongozea kivuko.
Kivuko cha Mv Magogoni kinachotoa huduma katika maeneo ya kigamboni na Magogoni Jijini Dar es Salaam kilisimamisha rasmi kutoa huduma hiyo mapema Mei mwaka huu kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati mkubwa chini ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kampuni ya Songoro Marine kukiongezea ufanisi katika kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi.

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA ‘AFRICA WORLD HERITAGE JIJINI ARUSHA

  LIW1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Vitambu kutoka  Rais wa Bermuda Emmissions Control Limited, Bw. Donal Smith katika mkutano wa ‘Africa World Heritage’ aliounfungua kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Mei 31, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIW2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Vitambu kutoka  Rais wa Bermuda Emmissions Control Limited, Bw. Donal Smith katika mkutano wa ‘Africa World Heritage’ aliounfungua kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Mei 31, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LAW11 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Bermuda Emmissions Control Limited, Bw. Donal Smith baada ya kufungua mkutano wa ‘Africa World Heritage’ kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Mei 31, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LAW13 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wasanii waliojitokeza kumlaki wakati alipowasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kufungua mkutano wa ‘Africa World Heritage’  mjini Arusha Mei 31, 2016. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIW3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe wakati alipomkaribisha kufungua Mkutano wa “Afrca World Heritage’ kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa  cha Arusha  (AICC) Mei 31, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIW4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua mkutano wa ‘Africa World Heritage’ kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Mei 31, 2016. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumaane Maghembe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIW6 
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa  wa’ Africa World Heritage ‘ wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipofungua mkutano wao kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Mei 31, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LIW7 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa ‘Africa World Heritage’  baada ya kuufungua kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Mei 31, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na kushoto ni Mkuu wa Arusha, Felix Tibenda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LAW8 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa ‘Africa World Heritage’  baada ya kuufungua kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Mei 31, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na kushoto ni Mkuu wa Arusha, Felix Tibenda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LAW9

WANAHABARI WALIA NA UKOSEFU WA MIKATABA.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Wamoja Ayubu (Kushoto) akipokea moja ya Ipad toka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel kwa msaada wa kampuni ya Star Times kwa ajili ya Maafisa Habari wa Mkoa na Halmashauri za Mkoa wa Iringa.
……………………………………………………………………………………………………
Na Zawadi Msalla- Iringa.
Wanahabari wa Mkoa wa Iringa  wameeleza masikitiko yao ya ukosefu wa Mikataba ya ajira ambayo  inasababisha upotevu wa haki zao za msingi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Wakieleza masikitiko hayo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel jana alipotembelea mkoa huo kujionea shughuli mbalimbali za kisekta za Wizara hiyo, walisema ni kwa kipindi kirefu sasa tatizo hilo limekuwa  kilio chao.
Walisema kwamba, kukosekana kwa Mikataba ya Kazi imekuwa ni kikwazo kikubwa kinacho wakatisha tamaa  na hivyo kuitaka Wizara iangalie kwa umakini suala hilo na kuliingiza katika Sheria tarajiwa ya Habari.
Akiwakilisha maoni yake, Bwana Leonard Frank alisema Waandishi wengi wanategemea bahasha katika kuendesha maisha yao ya kila siku kwakuwa hawana mikataba ya ajira hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa maisha ya wanahabari hao kuwa duni.
“Hakuna mishahara, malipo, stahili sawasawa na kazi zetu wala maslahi nyingine zozote”alisema.
Aidha, wameiomba Serikali kuangalia namna ya kukaa na Wamiliki wa vyombo vya habari ili kuweza kujadili suala hilo na kutafutia ufumbuzi wa kudumu.
Naye Katibu Mkuu akijibu hoja hiyo aliwataka wamiliki wa vyombo vya Habari wasisubiri mpaka sheria mpya ya habari itoke ili waweze kutatua suala hilo, kwani ni haki ya msingi ya mtu yeyote anaye fanya kazi.
Alisisitiza kuwa kulipa vizuri waandishi wa habari itasaidia waandishi kufanya kazi kwa moyo na kukuza vyombo vyao.
“Sheria isishurutishe watu, haki ya msingi ya kibinadamu lazima ibaki kuwa haki ya msingi kama kweli wamiliki mnahitaji matokeo mazuri zingatieni suala zima la mikataba”Alisema Prof. Gabriel.
Pia aliwataka waandishi wa habari wajiweke vizuri ili thamani yao ionekane na kuongeza kuwa imefika wakati wa waandishi kuhakikisha jamii inatambua kuwa bila uwepo wao mambo hayawezi kwenda vizuri.
“Hakuna atakaye kuthamini kama hauoneshi kwanini una umuhimu wa kuwepo hapo, kama Mwajiri wako haoni tofauti ya uwepo wako au kutokuwepo kwako basi haina haja ya kulilia mkataba” Aliongeza Prof. Gabriel.
Aliwaambia Wizara yake ipo katika mkakati wa kuinua sekta zake nne ili ziweze kutambulika na kuonekana katikati ya jamii.

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAHIMIZA WAKAZI WA TANGA KUJIUNGA NA MFUMO WA WOTE SCHEME

 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PFF mara baada ya kufungua maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Tanga yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwakidila jijini
 Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile akiwa kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesho
hayo
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile wa pili kulia akitoa elimu kwa mkazi wa Tanga
namyanatolewa na mfuko huo. na ya mafao
WAKAZI wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kutumia fursa ya kujiunga na Mfumo
wa wote scheme unaotolewa na Mfuko wa Pensheni PPF ili kuwawezesha kukithi mahitaji kwa sababu unalengo kuu la kutambua mchango wa ushiriki kwenye sekta isiyo rasmi katika kuinua uchumi.
 Hayo yalisemwa jana na Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile wakati alipozungumza na gazeti hili katika maonyesho ya nne ya biashara ya kimataifa ya Tanga yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwakidila jijini hapa ambapo alisema mfumo huo utasaidia kufikia wananchi wengi.
 Alisema kuwa fao hilo likuwa likitoa fursa mbalimbali kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta iliyo rasmi na isiyorasmi ili kuwawezesha kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa mustakabali wa maendeleo yao. 
“Niwaambieni kila mtu au kikundi chenye mlengo wa kiuchumi kilichopo kwenye sekta isiyorasmi kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, mama lishe, waendesha pikipiki, wajasiriamali wadogo wadogo kwa lengo la kuhakikisha wananufaika kupitia mfumo huo “Alisema. 
Aliongeza kuwa pia mfumo huo unawagusa wasanii, wana michezo, wachimbaji madini wadogo wadogo wanaweza kujiunga na mfumo huo kwa lengo la kupata manufaa yanayotokana na mfuko huo. 
Sambamba na hilo pia alisisitiza uwepo wa mafao yanayotolewa na mfuko huo kuwa ni ule wa Afya, Fao la Uzeeni, Mkopo wa elimu ambao unalengo la wanachama kukopa na kujiendeleza kielimu na PPF na mkopo ambao unakuwezesha kutimiza ndoto yako.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MDAU OTHMAN MANGUBE NA MKEWE BI MARIAM WAWASHUKURU WADAU,WASHEREHEKEA MWAKA MMOJA WA NDOA YAO 

Pichani Mdau Othman Mangube akiwa sambamba na mkewe Bi Mariam Swedy wakiwa katika nyuso za furaha,mara baada ya kufunga ndoa yao hapo mwaka jana,ambapo leo Wanamshukuru Mungu kwa kuvuka milima na mabonde mengi katika mazingira tofauti tofauti ya maisha na sasa Wanatimiza mwaka mmoja wa Ndoa yao,ambayo wao bado wanaamini ni changa,lakini kwa rehma na baraka za Mwenyezi Mungu atawasimamia na kuwaongoza katika mstari ulio nyoofu na kuwafikisha miaka mingi zaidi.
“Pia tunawakia heri ndugu jamaa na marafiki popote pale mlipo,tunawashukuru sana kwa ushirikiano wenu mlioutoa wakati wa kuifanikisha ndoa hii,nawashukuru sana na tuendelee na ushirikiano huo,sina cha kuwalipa lakini Mwenyezi Mungu atawalipa zaidi.”Asanteni sana
Bwana Othman Mangube akiwa na Mkewe Bi Mariam Swedy katika pozi la picha

UWANJA WA NDEGE SINGIDA NI ‘JIPU’ NANI WA KULITUMBUA?

Mfanyakazi  wa  kikosi  cha zimamoto na uokozi katika  uwanja  wa  ndege wa mkoa wa Singida akijiandaa  kwa kukifanyia majaribio  kifaa chake  cha  kuzimia moto wakati  ndege  iliyombeba balozi wa China nchini Dr  Lu Yong,ng ikiwasili katika  uwanja  huo jumapili ya May 29 wakati wa  ziara  yake wilayani Iramba
Hapa mfanyakazi  huyo akiwa pekee yake  huku akifanya kazi  tatu kwa  wakati mmoja kuelekeza ndege  hiyo ,kushika kifaa cha  kuzimia moto iwapo  hitirafu  itajitokeza na tatu kuweka gogo kwenye taili la ndege  baada ya kutua

Hapa  akielekea  kuelekeza eneo la  kutua
Hapa  akimwelekeza rubani wa  ndege hiyo huku  kulia kifaa kinachotumika kama gari la zimamoto na uokozi likiwa limeegeshwa kulia
Hapa  anakamilisha  kuelekeza eneo la  kutua anajiandaa kurudi  kuchukua kigogo kwenye gari  hili maalum ambalo kweli  bado mamlaka  ya  viwanja  vya ndege  vinapaswa  kulitazama   hili pasipo kusubiri majanga  ili  kuunda tume ya uchunguzi wa kitakachotokea
Ndege  ikiwa  imetua huku kifaa kinachotumika kama  gari la zimamoto na uokozi  kikiwa pembeni na mhudumu wa kifaa hicho  kushoto
Rubani  akimtazama  mfanyakazi  huyo mmoja anayefanya kazi  tatu kwa  wakati mmoja katika  uwanja wa ndege Singida
Hapa  akielekea  kuweka kigogo kwenye ndege  ushauri  wetu matukiodaimaBlog kwanza kwa kamati ya  ulinzi na usalama mkoa  wa Singida  kulitazama suala   hili la kiusalama kwa jicho la tatu kwani hatuombi jambo basi kutokea  ila ni  vema kinga  kuliko  tiba ,pili uongozi wa kiwanja  hicho  cha ndege kuongeza  wafanyakazi na hata  kuomba gari la kisasa katika uwanja  huo , tatu wizara  husika  kulitazama   hili na mwisho uongozi wa viwanja vya ndege nchini kutoka ofisini na kuzungukia  viwanja  vyote kikiwemo  hiki  cha Singida kuangalia changamoto  zake vinginevyo hili ni  jipu sasa ni nani wa  kujitolea  kulitumbua ?

IN LOVING MEMORY OF OUR BELOVED PROF. HELEN I. LUGINA

Helen, though it is five years today since God called you, the memories are still strong as the One pm Shining light.  Your unconditional love truly brightened our lives just like the meaning of your name.
Every day in some small way, memories of you come our way. Living without you is the hardest part of all but with the peaceful memories you left us, you will walk with us forever. Each one of us still remembers your infectious laugh, it keeps us going when the going gets tough. Nothing can ever take away, the love you gave us and the family bond you built for us.
You are loved beyond words and missed beyond measure by your husband (Max), children (Emma, Mary, Richard, Roselinda and Kelvin) and grandchildren (Gabriella, Nathan and Joanna)

WANANCHI WA KATA YA MABATINI JIJINI MWANZA WATAKIWA KUUNDA ZAIDI VIKUNDI VYA KIJAMII.

Diwani wa Kata ya Mabatini, Deus Mbehe, akizungumza katika
uzinduzi wa Kikundi cha Ushirikiano People’s cha Mabatini.

Serikali yajadili Rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Kukabiliana na Maafa

ke1Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Naima Mrisho akitoa neno la ufunguzi katika mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Mei 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ke2Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Bw. Christopher Chusi akichangia hoja wakati wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa uliofanyika Mei 30, 2016 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ke3 
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wakifuatilia mada ya Menejimenti ya Maafa kutoka kwa Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. John Kiriwai (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Morogoro tarehe 30 Mei, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ke4Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Naima Mrisho akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya maafa katika zoezi la ukakamavu katika kujiandaa na kukabili maafa wakati wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa Wilayani Kilosa tarehe 30 Mei, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ke5 
Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Fadhili Mtengela akiwasilisha mada ya kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa katika mkutano wa kujadili mpango huo uliofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro tarehe 30 Mei, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)index 
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. John Henjewele (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo Wilayani kilosa Morogoro tarehe 30 Mei, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………………
Na. Mwandishi Wetu
Ofisi ya Waziri Mkuu imejadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wilayani Kilosa Mei 30, 2016.
Rasimu hiyo imejikita katika kutoa miongozo ya uratibu katika kukabili dharura za aina zote za majanga yanapotokea katika ngazi zote za Kitaifa.
Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Maafa Wilayani Kilosa Mkurugenzi wa Tafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Naima Mrisho alieleza kuwa muongozo huo ni sehemu ya kuisaidia jamii katika kupata mbinu bora za kujiandaa, kukabili, na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea ili kuzisaidia jamii zetu. 
“Ni muhimu kuwa na mpango huo kwa kuzisaidia Halmashauri zetu katika kupambana na maafa yanayotukabili,”alisema Bi. Naima 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. John Henjewele alibainisha umuhimu wa Mpango huo ikiwa ni sehemu ya kuanzia na inayotoa muongozo mzuri unaosaidia katika Halmashauri yake katika kukabiliana na Maafa.
 “Tangu mpango kuanza kutumika Desemba 2013 Wilaya ya Kilosa imeweza kuwa na mbinu za kuyakabili maafa yanapotokea hususani yale ya mafuriko” Alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bw. Idd Mshili aliipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuona umuhimu wa kuitembelea Halmashauri yao kwa kuupitia Mpango na kuuboresha ili kusaidia kurahisisha uelewa kwa kua lugha ya Kiswahili inaeleweka kwa urahisi hususani ngazi ya chini na kwa wanavijiji wanaokumbana na maafa pindi yanapotokea.
 “Nichukue fursa hii kuwapongeza Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kuona umuhimu wa kuubadili mpango kutoka lugha ya Kingereza kuwa katika lugha ya Kiswahili ili kufikia makundi yote ya jamii kwa urahisi.”
AWALI: Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa ulianza kutumika mwaka 2013 ikiwa na lengo la kuziwezesha Halmashauri kujiandaa na kuyakabili maafa yanapotokea, Ofisi ya Waziri Mkuu imefanikiwa kufanya Tathimini kwa Halmashauri za baadhi ya Mikoa kwa kuangalia ubora wa mpango tangu uanze kutumika katika Mikoa ya Mtwara, Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma, Singida na Shinyanga kuanzia Mei 23 hadi 30, 2016.

NAPE AMJULIA HALI BABA WA DIWANI WA CHADEMA

 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na  Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile (CHASEMA) mara baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Nyangao kumjulia hali Baba wa Diwani huyo aliyelazwa hapo. .
 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipewa maelezo juu maendeleo ya hali ya Mzee Omary Nyimbile, baba wa Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile (CHADEMA) aliyelazwa katika Hospitali ya Nyangao.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimuangalia Mzee Omary Nyimbile, baba wa Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile aliyelazwa katika hospitali ya Nyangao.
 ………………………………………………………………………………………
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amemjulia hali Mzee Omary Nyimbile, baba wa Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile .
Mhe. Nape ambaye yupo kwenye ziara ya utekelezaji wa ahadi zake jimboni kwake na kuonana na wananchi alifika kwenye hospitali ya Nyangao mwishoni mwa wiki iliyopita na kupokelewa na Diwani huyo wa kata ya Mtama kupitia Chama Cha Chadema.
Mheshimiwa Mbunge wa Mtama alimjulia hali Mzee Omary na kumtakia heri ya kupona haraka.
Kitendo cha Mhe. Mbunge kumjulia hali baba wa Diwani wa Chadema kimewashangaza wengi ambao walidhani viongozi hawa hawatoweza kuzungumza kutoka na hali ilivyokuwa wakati wa uchaguzi.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI MBALI MBALI LINDI VIJIJINI

 Mwenge wa Uhuru ukiwasili kwenye uwanja wa mpira wa Mchinga I,wilaya ya Lindi vijijini ambapo ulizindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika Majimbo mawili wa wilaya hiyo, jimbo la Mchinga na jimbo la Mtama.
 Viongozi mbali mbali wakiwa wamesimama tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Lindi Vijijini
 Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Bw. George Jackson kitaifa akizindua mradi wa maji katika shule ya msingi Mchinga I.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda wakiwaongoza waongoza Mwenge wa Uhuru kitaifa kupita juu ya daraja lililofunguliwa rasmi na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Daraja hili linawaunganisha wakazi wa Mchinga II na Mchinga I.
 Wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya Mnonela wakihushuhudia Mwenge wa Uhuru kwa kuushika ulipowasili shuleni hapo jimbo la Mtama , Lindi Vijijini.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) , mkimbiza Mwenge Kitaifa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda wakiwa wamekalia moja ya madawati 50 yaliokabidhiwa kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi  Mnolela.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa heshima kwa Mwenge wa Uhuru kwenye viwanja vya shule ya msingi Madangwa.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Madangwa waliojitokeza kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru ambapo aliwaambia kuwa utekelezaji wa yale aliyoahidi umeanza na kuwahakikishia wananchi wa jimbo lake ahadi zake zitakamilika mapema zaidi.

Vijana nchini washauriwa kujiunga na mashirika ya kujitolea ili wajiongezee ujuzi na maarifa

1Vijana nchini Tanzania wameshauriwa kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea ili kujiongezea ujuzi, uwezo, maarifa na kuleta mabadiliko katika jamii zao,hayo yalielezwa na Meneja wa Maendeleo ya Vijana wa shirika la Raleigh Tanzania, Genos Martin wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.
Martin alisema kuwa ni vyema kwa vijana kujiunga na mashirika ya kitaifa na ya kimataifa ya kujitolea kwani kwa kufanya hivyo kutawapa vijana fursa ya kuongeza ujuzi na maarifa ambao utawasaidia katika sehemu mbalimbali.
Martin alisema, “Kufanya kazi kwa kujitolea ni kitu kigeni nchini kwetu tofauti na Mataifa ya nchi zilizoendelea, watu waliowahi jitolea wanapewa kipaumbele kwenye maombi ya kazi tofauti na nchini kwetu. Hii inafanya kujitolea kuwa jambo la muhimu sana kwenye mataifa ya wenzetu” 
 “Vijana wengi wanalalamika kuwa nafasi nyingi za kazi zinawataka wawe na uzoefu wa miaka mitatu nakuendelea, hawajui ni vipi wanaweza kupata uzoefu lakini kama wakijiunga na haya mashirika ya kujitolea wanaweza pata huo uzoefu na kuwafanya wawe na nafasi nzuri pindi waombapo ajira” aliongezea Martin.
Aidha, Afisa Mawasiliano wa Raleigh Tanzania, Kennedy Mmari alieleza kuwa ni kawaida ya shirika hilo kutafuta vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao huungana na vijana wenzao kutoka mataifa ya mbali mbali ya Ulaya na Amerika.
Mmari aliongezea, “Raleigh tuna programu kwa vijana zinazohusu ujasiriamali, usafi, maji na utunzaji wa mazingira, kijana yeyote anaweza kujjiunga nasi na kufanya program zetu. Hatutoi malipo yoyote wala hawatulipi chochote isipokuwa tunagharamia mahitaji yao yote ya msingi pindi wakiwa kwenye programu”
2 
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chibe iliyopo kata ya Old Shinyanga mkoani Shinyanga wakishuhudia ufunguzi wa kituo cha elimu ya awali kilichojengwa na na vijana wa kujitolea kwa msaada wa shirika la Raleigh Tanzania.
Kwa upande wa vijana waliofanya programu na shirika hilo  wameshukuru kwa nafasi waliyopewa kwani imewasaidia kupata ujuzi na ufahamu wa mambo tofauti ikiwemo jinsi ya kuandaa na kusiammia biashara.
Mmoja wa vijana ambao wamepata fursa hiyo, Sia Malamsha,  alisema kuwa anajiona wa tofauti baada ya kumaliza programu, hakuwahi fikiria kama kuna watu Tanznaia hawana huduma za maji safi na salama lakini kupitia programu za Raleigh nimeweza fika kwenye jamii hizo na kuwasaidia kutatua matatizo hayo.
“Nimekuwa sehemu ya mabadiliko makubwa katika nchi yangu, najivunia kuona nimefanya kitu kuikomboa jamii ya Watanzania” aliongezea Bi. Malamsha.
3 
Vijana wa Shirika la kujitolea la Raleigh wakishiriki ujenzi wa choo katika moja ya miradi yao
Naye kijana Ashiru Said aliyefanya programu ya ujasiriamali amesema kua programu za Raleigh zimemsaidia kupata elimu ya kusimamia na kuendesha biashara.
“Nimeweza kupata elimu ya ujasiriamali, baada ya kurudi nyumbani jamii imefaidika na elimu niliyoipata kwani nimeweza waelimisha vijana wenzangu jinsi ya kuanzisha na kusimamia biashara zao wenyewe” alimalizia Said.
Raleigh Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali lenye ofisi zake mkoani Morogoro na kufanya programu za kujitolea kwa lengo  la kuisaidia jamii ya Tanzania sehemu mbalimbali.

BUNGE LAWASIMAMISHA WABUNGE KWA KUFANYA VURUGU BUNGENI JANUARI 27 ,2016

IMG-20160530-WA0065 IMG-20160530-WA0066

BREAKING NEWS – BUNGE LAWASIMAMISHA WABUNGE 7 KWA KUFANYA VURUGU BUNGENI JANUARI 27 ,2016.

Mwenyekiti wa kamati  ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mhe.George Huruma Mkuchika akiwasilisha taarifa ya Kamati hiyo kuhusu uchunguzi es vitendo vya baadhi ya wabunge kufanya vurugu.
 ………………………………………………………………………..
 Na. Aron Msigwa -Dodoma.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge limepitisha azimio la  kuwasimamisha kuhudhuria vikao vya Bunge
baadhi ya wabunge wa Kambi ya Upinzani waliohusika katika kufanya vitendo vya
vurugu ndani ya ukumbi na kudharau Mamlaka ya Spika Januari, 27, 2016.
Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni Mhe.Kabwe Zubeiri Ruyangwa
Kabwe, Mhe.John Heche, Mhe.Halima Mdee,Mhe.Tundu Lissu, Mhe.Halima Mdee,
Mhe.Pauline Gekul  na Mhe. Ester Bulaya.
 Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya
Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na kanuni ya 74 (4) na (6).
Akisoma adhabu hizo Mwenyekiti wa kamati hiyo yenye
wajumbe 15 Mhe.George Huruma Mkuchika amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na
Kamati hiyo kwa kuwaita na kuwahoji wahusika ulibaini kuwa wabunge hao walitenda kosa kwa kukiuka kanuni zinazoliongoza bunge hilo.
 Imebainishwa kuwa Mhe.Zitto Kabwe alivunja masharti ya Kifungu cha 24(c), (d) na (e) cha Sheria ya Haki na

MAHAKAMA KUU KUANZISHWA KATIKA MKOA WA MARA

jaji 
Na Lydia Churi- Musoma
………………………………………
Mahakama ya Tanzania inakusudia kuanzisha Mahakama Kuu katika mkoa wa Mara ambapo ujenzi wa jengo la mahakama hiyo unatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka huu.
Akizungumza leo mjini Musoma katika ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za kimahakama katika kanda ya Mwanza, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman alisema mkoa wa Mara unayo haki ya kuwa na Mahakama Kuu kwa kuwa nia ya Mahakama ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Alisema mahakama hiyo itajengwa kwa haraka na itamalizika katika kipindi cha mwaka moja kwa kuwa fedha kwa ajili ya ujenzi huo tayari imeshatengwa ambapo nyingine imetokana na msaada waliopewa kutoka Benki ya Dunia.
Alisema kuanzishwa kwa mahakama hiyo katika Mkoa wa Mara kutawapa fursa wananchi wa Mara ya kupata huduma kwa karibu zaidi na pia itasaidia kupunguza kesi zilizoko mahakamani kwa haraka.
Awali akimkaribisha Jaji Mkuu ofisini kwake alipomtembelea, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo alimwomba Jaji Mkuu kuanzisha Mahakama Kuu katika mkoa wake kwa kuwa asilimia 55 ya kesi zote za mauaji katika Mahakama kuu kanda ya Mwanza zinatoka katika mkoa wa Mara hivyo mkoa huo unayo haki ya kuwa na Mahakama Kuu.
Pamoja na mkoa huo kuwa na kesi nyingi za mauaji, Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa wa Mara pia unakabiliwa na kesi nyingi zinazohusu masuala ya ardhi kwa kuwa ni asilimia 38.3 tu ya eneo zima la mkoa huo ndiyo eneo linalotuwa kwa ajili ya makazi ya watu na shughuli za maendeleo
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Mkoa wa Mara una wakazi zaidi ya milioni 1.3.
Alisema Mkoa wa Mara una eneo lenye kilometa za mraba 30,150 ambapo asilimia 36 ya eneo hilo ni maji wakati asilimia 25.7 ni eneo lenye mapori na hifadhi za Taifa ikiwemo mbugaya wanyama ya Serengeti.
Aidha, Mkuu huyo wa mkoa aliisifu Mahakama ya Tanzania kwa kufanya kazi yake kwa weledi ya kuzimaliza kesi zilizohusu mapigano ya koo zilizokuwepo katika siku za nyuma mkoani humo kwa kuwa zimesaidia maeneo ya mkoa huo kuwa salama hivi sasa na hayaonyeshi dalili za kujirudia. Aliongeza kuwa eneo la haki likitulia hata masuala ya utawala yakuwa rahisi.
Jaji mkuu Leo amehitimisaha ziara yake katika kanda ya Mwanza yenye mikoa ya Mara, Geita na Mwanza ambapo alikuwa akikagua shughuli mbalimbali za kimahakama katika kanda hiyo.

No comments :

Post a Comment