Thursday, May 12, 2016

MAJALIWA AMWAKILISHA Rais John Magufuli KWENYE MKUTANO WA KUPAMBANA NA RUSHWA LONDON

 J3 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa kuingia kwenye ukumbi wa Lancaster House, London nchini Uingereza kuhudhuria mkutano  wa Wakuu wa Nchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, May 12, 2016.  Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.
J1 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki katika​ mazungumzo rasmi ya Wakuu wa Nchi katika Mkutano unaojadili mapambano dhidi ya rushwa kwenye ukumbi wa Lancaster House, London, nchini Uingereza May 12, 2016. Wa tatu kushoto ni Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron. Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA RAJABU LUHWAVI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA CCM MKOA WA PWANI LEO

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Rajab Luhwavi akivishwa Skafu na Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Omari Salum, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, Wilayani Kibaha mkoani humo leo.  Katikati ni Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga na kulia ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Kibaha,  David Malecela.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rajab Luhwaavi, akiongozana na  Katibu wa CCM mkoa wa Pwani, Joyce Masunga, kwenda Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, wilayani Kibaha leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwai akisalimia baada ya viongoi baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, kuzungmza na wafanyakazi wa CCM mkoa wa Pwani wilayani Kibaha leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwai akisalimia baada ya viongoi baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, kuzungmza na wafanyakazi wa CCM mkoa wa Pwani wilayani Kibaha leo 

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwavi akisaibi kitabu cha wagei katika Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, wilayani Kibaha leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Pwani, Joyce Masunga.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) YAKANUSHA UTAPELI.

CCC…………………………….
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimelaani vikali tabia ya baadhi ya watu wanaotumia vibaya jina la Chama hicho kuwatapeli wananchi kutoa fedha ili wapatiwe nafasi za ajira katika Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) jambo ambalo sio sahihi.

ZANZIBAR YASHEREHEKEA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI

 Brasbendi ya Chipkizi ikiongoza matembezi ya wauguzi yakipita katika maeneo
ya Kisonge kuelekea Studio za Rahaleo ambapo sherehe hizo ziliadhimishwa rasmi.
Waandamanaji wakiingia kwa furaha eneo la Studio za Rahaleo ambapo sherehe za
sikuya Waguzi Duniani ziliadhimishwa.
Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo aliemuwakilisha Mke wa Rais wa Zanzibar
akisoma hotuba katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika
Ukumbi wa Sanaa Rahale Mjini Zanzibar.
Mrajis Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Vuai Kombo Haji akiongoza kiapo
cha wauguzi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika Ukumbi
wa Sanaa Rahaeo.
Mkurugenzi Tiba Katika Wizara ya Afya Dkt. Salhia Ali Muhsin akimkaribisha
mgeni rasmi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliemwakilishi Mke wa Rais wa
Zanzibar Mama Mwanamwema Shein katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya wauguzi walioshiriki maadhimisho hayo wakifuatilia hotuba zilizokuwa
zikitolewa katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo, Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa wauguzi na Mgeni rasmi, Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo.
 Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.

MAKALA YA MABASI YAENDAYO HARAKA.

3……………………………………………………………….
Hussein Makame-MAELEZO
UIMARISHWAJI wa miundombinu na uboreshaji wa sekta ya usafiri ni baadhi ya  mihimili inayopewa umuhimu nchini katika kuleta maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla hasa pale usafirishaji unapowezesha abiria na mizigo kufika sehemu kwa wakati na kwa gharama nafuu.

WATANZANIA KUZIAMUA ETHIOPIA, GHANA

CAF Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limewateua waamuzi wanne kuchezesha mchezo Na. 27 kati ya Ethiopia dhidi ya Ghana kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana 2017 utakaofanyika Uwanja wa Addis Ababa (Gazon Nature), jijini Addis Ababa huko Ethiopia.
 Mchezo huo utaochezwa Mei 22, 2016 majira ya saa 10.00 jioni kwa saa za Ethiopia, utaamualiwa na Mfaume Ali Nassoro ayesimama katikati wakati walioteuliwa kuwa waamuzi wa pembeni ni Josephat Deu Bulali (line 1) na Alli Kinduli na mezani atakuwa Martin Eliphas Sanya. Kamishina wa mchezo huo kwa mujibu wa CAF ni Julius Elly Mukolwe kutoka Kenya.

SERENGETI BOYS YATUA GOA, KUANZA NA MAREKANI J’PILI

serengeti 
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys imetua salama jijini Goa, India kwa ajili michuano maalumu ya soka ya kimataifa kwa vijana (AIFF Youth Cup 2016 U-16) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIFF).

TANZANIA KUWA WENYEJI MKUTANO WA WAKADIRIAJI MAJENZI

index 
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO DAR ES SALAAM.
…………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa wakadiriaji majenzi Afrika unaotarajiwa kufanyika tarehe 18-19 Agosti, 2016 jijini Dar es salaam.

Muhimbili Kutoa Tiba Wagonjwa wa Homa Sugu ya Ini

H1 
Mtaalamu kutoka Marekani, Dk Brian McMahon akizungumza na madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kuhusu tiba ya homa sugu ya ini inayosababishwa na virusi vya Hepatitis B.
H3 
Dk Aaron Haris kutoka Marekani akielezea jinsi mradi huo utakavyowanufaisha Watanzania ambao wameambukizwa virusi vya vya Hepatitis B.
H6 
Dk Edwin Masue wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwasilisha mada kuhusu dalili za homa sugu ya ini inayosababishwa na virusi vya Hepatitis B.
H2 H4 
Madaktari na wauguzi wakimsikiliza Dk McMahon wakati akielezea kuanza kwa mradi wa tiba ya homa ya ini kwa watu mbalimbali.
H5 
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Tumbo, Dk John Rwegasha (kushoto) akifuatilia mada iliyowasilishwa na Dk Edwin Masue na Dk Eva Uiso wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Wengine ni Dk McMahon na Dk Haris kutoka Marekani.

Tume ya Kurekebisha Sheria yaendelea na Mapitio ya Sheria za Uwekezaji

E 
Afisa Sheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Hemed Lusungu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maboresho ya sheria mbalimbali yanayofanywa na tume hiyo. Kushoto ni Afisa Sheria wa Tume hiyo Bw. Fredy Kandonga.
D 
Afisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Fredy Kandonga akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tafiti za kisheria zinazotarajiwa kufanyiwa kazi kwa kipindi cha Mwaka 2016/2017 ikiwemo Mapitio ya Sheria za Uwekezaji. katikati ni Afisa Sheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Hemed Lusungu na kulia ni Afisa Habari wa Tume hiyo Bw. Munir Shemweta.
PICHA NA FATMA SALUM- MAELEZO
…………………………………………………………………………………………………

WAZIRI NAPE NNAUYE PAMOJA NA WAZIRI JANUARY MAKAMBA WAKUTANA NA WASANII BUNGENI DODOMA.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) (wa pili kulia) akiwa pamoja na Wasanii wa kizazi kipya ambao walitembelea Bunge mjini Dodoma akiwemo Msanii Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz pamoja na Mafikozolo 12 Mei, 2016.

Wasanii wa kizazi kipya, Nasib Abdul (Diamond Platinumz) (wa tatu kushoto) pamoja na Mafikizolo wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Mbunge Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Babu Tale (katikati). Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba Bungeni Dodoma.

Mhe. Nape Nnauye (wa pili kulia) pamoja na Mhe. January Makamba (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wasanii
Nasib Abdul (Diamond Platinumz) (katikati) pamoja na Mafikizolo
Bungeni mjini Dodoma.
Mhe. Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Mhe. January Makamba (kulia) na Mbunge mwingine (mwenye suti nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja na Wasanii Nasib Abdul (Diamond Platinumz) (katikati) pamoja na Mafikizolo Bungeni mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Dodoma)

Benki ya Kilimo yajipanga kusaidia utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa.

BMkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw. Thomas Samkyi akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkakati wa Benki hiyo wa kusaidia utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano kwa kipindi cha kuanzia 2016/17 hadi 2020/21. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Sera Bw. Francis Assenga.
AMkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Sera kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw. Francis Assenga (Kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu matarajio ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo katika kusaidia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw.Thomas Samkyi na kulia ni Mkurugenzi wa Mikopo na Usimamizi wa Biashara Bw. Robert Pascal.
PICHA NA FATMA SALUM-MAELEZO

KUTOKA BUNGENI- MJINI DODOMA.

index 
Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango akijibu hoja mbalimbali za Wabunge Bungeni mjini Dodoma, 12 Mei, 2016.

SERIKALI MKOANI MBEYA YAFUTA HATI YA KIWANJA CHA MAKAZI KILICHOTOLEWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA

DSC_0357 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Picha Maktaba
……………………………………………………………………………………………..
Na EmanuelMadafa,Mbeya(Jamiimojablogu
SERIKALI Mkoani Mbeya  imeagiza kufutwa kwa hati ya  kiwanja
kilichotolewa na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenye chanzo kikuu cha maji
kilichopo eneo la Nyibuko kata ya Mwakibete kwa matumizi ya makazi.

NHIF LINDI YAWAPA ELIMU YA TOTO AFYA KADI AKINA MAMA WA HALMASHAURI YA (W) LIWALE

1 
Meneja wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi akitoa elimu ya mpango mpya na wa gharama nafuu utakaomuwezesha mzazi kumlipia bima ya Afya mtoto chini ya miaka 18 unaojulikana TOTO AFYA KADI,kwenye kliniki ya mama na mtoto (RCH) Hospitali ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
2 
Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Liwale akitoa rai kwa akina mama walioudhuria kliniki kwa kuchangamkia fursa kwani ni mpango wenye manufaa zaidi na una uwigo wa mafao kwa 50,400 tu.
3 
Akina mama wakifuatilia elimu ya kitita cha mafao yanayotolewa kwenye mpango wa Toto afya kadi kutoka kwa meneja wa NHIF Lindi hayupo pichan

No comments :

Post a Comment