Monday, May 9, 2016

KONGAMANO LA JESHI LA POLISI (MEDICAL WING) LA KUJIPIMA UTENDAJI KAZI NA CHANGAMOTO LAFANYIKA MJINI TABORA

LAPF imedhamini kongamano la Jeshi la Polisi (Vikosi vya masuala ya tiba) uliofanyika mjini Tabora. Mfuko wa Pensheni wa LAPF umetoa kiasi cha Shilingi milioni  6,200,000/= katika kufanikisha  kongamano la Maafisa wa Polisi kutoka mikoa yote Tanzania maalum kwa ajili ya kujipima na kujadili changamoto mbalimbali za kitengo cha tiba ndani ya jeshi la polisi (medical wing) Wawakilishi kutoka mikoa yote Tanzania walishiriki katika kongamoano hilo wakiwa ni maofisa waandamizi wa jeshi hili la polisi. katika kongamano hilo Mfuko ulipata wasaa wa kuwasilisha mada kuhusu fursa mbalimbali zitolewazo na Mfuko lakini pia mada ya maandalizi kabla ya kustaafu ilitolewa katika mkutano huo , udhamini huu una synergy kubwa na mfuko katika kusajili wanachama wapya ndani ya jeshi la polisi.
mlo1 
Kamanda wa Jeshi la Polisi ACP Paul Kasabago akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya TZS. 6,200,000/= iliyotolewa na Mfuko wa Pensheni LAPF kuwezesha kongamano la Maafisa wa Polisi kutoka mikoa yote Tanzania (medical wing) mjini Tabora. Wanaokabidhi kutoka LAPF ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wanachama Bw. Valerian Mablangeti, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Desdery Sigonda pamoja na Meneja Kanda ya Dar es Salaam Bi. Amina Kassim.
mlo2Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Pensheni LAPF Bw. Valerian Mablangeti akitoa mada kuhusu Mfuko ikijumuisha maandalizi kabla ya kustaafu, Maafisa waandamizi wa jeshi la Polisi wakisiliza kwa makini katika kongamano la jeshi hili lililofanyika mjini Tabora hivi karibuni.
mlo3 
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakifuatilia kwa makini mada toka Mfuko wa Pensheni LAPF kwenye kongamano la Jeshi hili lililofanyika mjini Tabora ambapo maafisa hao walivutiwa na kujiunga na mfuko wa uchangiaji wa hiari ikiwa ni maandalizi kabla ya kustaafu.
mlo4 
Mmoja ya Maafisa waandamizi walioshiriki kongamamo la jeshi la Polisi mkoani Tabora hivi karibuni akiuliza namna ya kujiunga kwa hiari na Mfuko wa Pensheni wa LAPF mara baada Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama kuwasilisha mada kuhusu fursa mbalimbali zitoleawazo na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.

Visa na mikasa,Vilio na majonzi kumbukumbu ya makovu katika filanu ya Scars

sc1 
Ile show ya kijanja sasa imeshaanza ndani ya  Chaneli ya StarSwahili  Ni kila jumatatu saa 2:30 usiku  Hii sio ya kukoksa Ungana na StarTimes leo Hii lipia kifurushi cha Nyota Tsh 5000 tu Kwa Mwezi. Kwa maelezo zaidi

sc2

MATUKIO ZAIDI RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI UZINDUZI WA MAJENGO YA NSSF NA PPF MKOANI ARUSHA LEO

ng1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na wafanyakazi wa PPF na NSSF pamoja na wananchi wa jiji la Arusha kabla ya kufungua rasmi jengo la la Kitega uchumi la Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Arusha. PICHA NA IKULU
ng4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mipango kabla ya kufungua rasmi jengo la la Kitega uchumi la Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Arusha. 
ng6 
Meya jiji la Arusha  mstahiki Calist Lazaro Bukhai akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya ufunguzi rasmi wa Jengo la Kitega uchumi la Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Arusha. 
ng7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia wakati kikundi cha ngoma za asili cha kimasai kilipokuwa kikitumbuiza pembezoni mwa jengo la kitega uchumi la NSSF jijini Arusha.
ng8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la kitega uchumi la NSSF Mafao House jijini Arusha
ng9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mipango, Waziri wa Kazi wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge kazi ajira na vijana Jenista Mhagama wakifunua pazia  kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la kitega uchumi la NSSF Mafao House jijini Arusha. 

MAPITIO YA HOJA MBALIMBALI ZA WABUNGE MJINI DODOMA.

Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard Kalemani akijibu baadhi ya hoja za Wabunge zilizoihusu Wizara ya Nishati na Madini wakati wa kipindi cha jioni Bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) (kulia)
akijibu baadhi ya hoja za baadhi ya Wabunge wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali jioni bungeni mjini Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa mapitio  ya baadhi ya hoja za Wabunge leo jioni Bungeni mjini Dodoma.  
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mhe. Amina Makilagi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali za Wabunge leo mjini Dodoma.
 
Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard Kalemani (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji (Mb) wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) akijibu hoja za Wabunge mbalimbali wakiochangia hotuba ya Wizara yake leo jioni Bungeni mjini Dodoma.
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba wakati wa mapitio ya hoja za Wabunge jioni Bungeni mjini Dodoma.
 
 (Picha zote na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma)

SHAKA: KIKWETE AMETOA JASHO JINGI KUITUMIKIA TANZANI

 Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wananchi wa  tanga
…………………………………………………………………
Na Woinde Shizza,Tanga

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM )umevitaka vyama vya

upinzani wanaopika  maneno ya kipuuzi yenye  lengo la kuwagongajisha
viongozi wa CCM wakome na wamuache Mwenyekiti wa CCM  Dk Jakaya
Kikwete astaafu kwa heshima kwasababu ameitumikia nchi yake kwa kutoa
jasho jingi miaka kumi iliopita
Aidha umoja huo umesisitiza kuwa kazi aliyoifanya Dk Kikwete katika
uongizi wake wa miaka kumi kisiasa na kiserikali utabaki kwenye vitabu
vya kumbukumbu ya historia iliotukuka hususan kila utakapokumbukwa
mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM mwaka 2015.
Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka ameyasema hayo wakati
alipozungumza na viongozi na  wanachama wa uvccm na ccm kwenye ukumbi

wa TANU Hall mjini Tanga.

Alisema baada ya upinzani sasa  kujiona hawana hoja na hakubaliki

katika jamii maadui wa kisiasa wanotimiwa na nafisadi wamekuwa

wqkijaribu kupika uzushi na kutaka kuionyesha jamii kwamba viongizi wa

chama tawala hawana maelewano.

“Nakupeni  usia viongozi wa Ukawa ambao sasa mmekuwa wakiwa , mambo ya

ngoswe waachieni ngoswe wenyewe, viongozi wa ccm hawagombani,

hawajawahi kugombana na kamwe hawatagombana milele “alisema shaka

Aliwataka viongozi hao kutazama mustakabali wao kisiasa na kuachana na

ccm kwasababu chama hicho tawala haiwezekani kubomoka kwa maneno ya

jikoni , vijiweji au vichochoroni.

Shaka alisisitiza kuwa mwenyekiti wa ccm Dk Kikwete wakati akiwa Rais

ameitumikia nchi yake kwa kadri ya uwezo wake kama ambavyo

walivyotenda na kuitumikia nchi viongozi watangulizi wake akiwemo

baba wa Taifa Mwalimu julius Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee

Benjamin Mkapa na yeye ametenda kwa uwezo wake kama atakavyotenda Rais

Dk John Magufuli katika kipindi chake.

“Mtu mwenye akili timamu kila atakaposafiri akiizunguuka nchi yetu na

kupita juu ya barabara za lami, ujenzi wa madaraja, kutanuka kwa

mawasiliano, kukua uchumi wa Taifa na wa mtu mojmoja na wananchi iushi

katika nyumba za kisasa lazima utamkunbuka Kikwete taka usitake

“alieleza Kaimu huyo katibu mkuu .

Alisema kila zama ina kitabu na Nabii wake hivyo mema yaliofanywa na

kiongozi mmoja aliyemaliza muda wake yanahitaji kuheshimiwa kwasababu

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli wote ni watoto wa baba na

mama mmoja.

MATUKIO KUTOKA BUNGENI MIJINI DODOMA

B1 
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini  Mhe.Profesa Anna Tibaijuka na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma .
B2 
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini  Mhe. Zitto Kabwe akichangia mjadala wa hoja  ya hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji  leo mjini Dodoma.
Picha na MAELEZO-Dodoma.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAENDELEA KUPUNGUA.

V1Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akita taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Aprili 2016 leo jijini Dar es salaam, Kulia ni Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja.Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 umepungua hadi asilimia  5.1  kutoka asilimia 5.4.
V2 
Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja akifafanua kwa waandishi wa Habari kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania.
V3 
Waandishi wa Habari wakiwa kazini, wakati Ofisi ya Taifa ya Takwimu ikitangaza Mfumuko wa Bei Mwezi Aprili 2016 leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………..
Na. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  Dar es salaam.
 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 na kusema kuwa umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.4 iliyokuwepo mwezi Machi, 2016.
Hii inamaanisha kuwa  kasi ya upandaji wa bei ya  bidhaa na huduma kwa mwezi Aprili 2016 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma  iliyokuwepo mwezi Machi mwaka huu.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo ametoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam na kueleza kuwa kupungua kwa mfumuko huo kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema Takwimu zilizokusanywa katika mikoa yote ya Tanzania Bara kwenye bidhaa zinazotumika kupima mfumuko wa bei kwa mwezi Aprili 2016 zimeainisha kuwa bidhaa zisizo za vyakula katika soko zikiwemo Gesi , dizeli na mafuta ya taa zimechangia kupungua kwa mfumuko huo.
Amesema kuwa pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa hizo kwa mwezi Aprili 2016, baadhi ya bidhaa za vyakula ikiwemo mchele, unga wa Mahindi na mkaa ilionyesha kuongezeka katika kipindi hicho.
Akizungumzia Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania kwa mwezi Machi na Aprili Bw. Kwesigabo amesema kuwa zimeongezeka hadi kufikia 102.46 kutoka 101:93 za mwezi Aprili.
Amesema kuwa tofauti na mwezi Machi bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi kwa mwezi Aprili ni unga wa muhogo, dagaa, choroko, maziwa ya ungana na matunda aina ya machungwa.
Aidha,bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na mvinyo, bia kuni na mazulia.
Kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Aprili, 2016 umefikia shilingi 97 na senti 60 ikilinganishwa na uwezo wa shilingi 98 na senti 11  wa mwezi Machi 2016.
“Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Aprili 2016 umepungua, hii ina maana kuwa sasa mtu anahitaji kuongeza  ya shilingi 2.40 ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Machi ” Amesema Kwesigabo.
Kwa upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki mwezi Machi, 2016, Kwesigabo amesema una mwelekeo unaofanana; Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.27 kutoka 6.45 huku Uganda ukifikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 6.2 zIlizokuwepo mwezi Machi 2016.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete AAGWA LEO NA BALOZI WAPYA CHIKAWE NA KISAMBA

J1Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Balozi Mathias Chikawe, Balozi huyo alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo, Mei 9, 2016.
J2 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiagana na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani, Balozi Mathis Chikawe, baada ya mazungumzo yao, Balozi huyo alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo, Mei 9, 2016.
J3 
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba akisaini kitabu cha wageni, alipofika kumuaga Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.
J4Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba,  Balozi huyo alipofika kumsalimia katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo, Mei 9, 2016.
(Picha na Bashir Nkoromo).

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA JENGO LA KITEGAUCHUMI LA MFUKO WA PENSHENI PPF JIJINI ARUSHA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akikata utepe
kuzindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF) lililopo Mtaa
wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira,
Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, (kushoto) ni Meya wa jiji
la Arusha, Calist Lazaro (wa kwanza kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini
ya PPF, Ramadhan Kijjah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.
Picha zote na Mafoto Blog
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, baada ya kuweka Jiwe la Msingi
la uzinduai wa Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo lililopo Mtaa wa Korido
Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.
 Jengo hilo lililozinduliwa leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia wakazi
wa arusha na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipozindua rasmi, Jengo
la Kitegauchumi la Mfuko huo
 (PPF)
lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.
 Sehemu ya wadau kutoka NSSF waliohudhuria uzinduzi huo wa wenzao wa PPF.
 Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mhe. Rais Dkt. Magufuli…..
  Baadhi ya wafanyakazi wa PPF Kanda yas Arusha wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
 Sehemu ya wananchi wa Jiji la Arusha wakimsikiliza Mhe.  Rais Dkt. Magufuli…..
 Wananchi wakimshangilia Mhe Rais wakati akihutubia…..
 Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mhe Rais.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni PPF na Wakurugenzi wa Mfuko wa huo  wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
 Baadhi ya viongozi na wadau wa Mfuko huo na Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro (kushoto) wakimsikiliza Mhe Rais.
Continue reading →

WATANZANIA KUSHUHUDIA COPA AMERICA LIVE KUPITIA STARTIMES

 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Mohamed Kimweri (kushoto), akizungumza katika na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kupata haki za kuonesha michuano ya Copa Amerika moja kwa moja ambayoitafanyika nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka Juni 26 mwaka huu. Kulia ni Meneja Maudhui wa kampuni hiyo, Paulina Kimweri.
 Meneja Maudhui wa kampuni hiyo, Paulina Kimweri, akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
…………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
 
KAMPUNI ya StarTimes Tanzania imefanikiwa kupata haki za kuonyesha michuano ya Copa America moja kwa moja ambayo itafanyika nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka Juni 26 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais wa kampuni hiyo nchini,  Zuhura Hanif alisema kuwa kupatikana kwa haki za kuonyesha michuano hiyo mikubwa na mikongwe ulimwenguni ikiwa inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake ni jitihada za kuhakikisha kuwa wateja wao wanafurahia vipindi bora vya michezo na burudani.
“Leo StarTimes inayo habari njema kuwataarifu kuwa tumepata haki maalum za kuonyesha michuano ya Copa America moja kwa moja kutoka nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka Juni 26 mwaka huu. Ninaposema haki maalumu manake ni kwamba watanzania hawataweza kushuhudia michuano hii sehemu yoyote isipokuwa kupitia king’amuzi cha

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
P 
MWANAFUNZI WA DARASA SITA SHULE YA MSINGI TUYOMBO AFARIKI DUNIA NA MWINGINE KUJERUHIWA BAADA YA PIKIPIKI WALIOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGWA NA GARI.
MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO WAKIWA WANASAFIRISHA NA KUPAKIA SUKARI BILA KIBALI.
Katika Tukio la Kwanza:
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Tuyombo darasa la sita iliyopo Wilaya ya Mbeya Vijijini aliyefahamika kwa jina la TIMOTH PHILIMON (14) amefariki dunia baada ya Pikipiki waliyokuwa wakisafiria ikiendeshwa na dereva aitwaye MATHIAS TIELI MARIRA (32) mkazi wa Inyala yenye namba za usajili T. 791 BPM aina ya T-Better kugongwa kwa nyuma na Gari.
Ajali hiyo ilitokea mnamo tarehe 08.05.2016 majira ya saa 19:15 jioni huko Kijiji cha Shamwengo, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya.
Inadaiwa kuwa Gari yenye namba za usajili T. 126 BEL aina ya Mitsubishi Fuso ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la FRANSIS S/O ALEX NYIGU (48) mkazi wa Makambako ilimgonga mwendesha Pikipiki huyo ambaye aliyekuwa mbele yake kusababisha kifo cha mwanafunzi TIMOTH PHILIMON ambaye alikuwa abiria kwenye Pikipiki hiyo.
Aidha katika ajali hiyo mwendesha pikipiki MATHIAS TIELI MARIRA alijeruhiwa na anaendelea na Matibabu. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Chanzo cha ajali ni mwendo kasi. Mtuhumiwa amekamatwa.
Katika Tukio la Pili:
Mtembea kwa miguu mwanamke asiyefahamika jina umri kati ya miaka 30 hadi 40 alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na Gari yenye namba za usajili T. 696 yenye Tela namba T.589 BCG aina ya Scania  ikiendeshwa na dereva DAVID MALILA (28) mkazi wa Makambako.
Ajali hiyo ilitokea mnamo tarehe 08.05.2016 majira ya saa 08:00 asubuhi huko eneo la Nsalaga, Kata ya Nsalaga, Tarafa ya Iyunga, Jiji na  Mkoa  wa Mbeya. 
Inadaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni baada ya tairi ya Gari hilo kuchomoka na kwenda kumgonga mwanamke huyo ambaye alikuwa akitembea kwa miguu pembezoni mwa Barabara. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Dereva alikimbia mara baada ya tukio, upelelezi unaendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi JUSTUS A. KAMUGISHA anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kufuata na kuheshimu sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Lakini pia anatoa wito kwa watumiaji wengine wa barabara wakiwemo watembea kwa miguu nao wachukue tahadhari pindi wanapotumia barabara.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tawi la Mbeya linawashikilia watu watano ambao ni PIUS KIKO (43) mkazi wa Sae Jijini Mbeya ambaye alikuwa akisafirisha sukari katoni 52 kwenye Gari yenye namba za usajili T.724 DCF aina ya Toyota Coaster bila kibali.
Mtuhumiwa akiwa na wenzake alikamatwa mnamo tarehe 08.05.2016 majira ya saa 11:00 asubuhi katika Operesheni hiyo maalum iliyofanyika eneo la Kabwe, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya.
Aidha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tawi la Mbeya waliendelea na Operesheni hiyo eneo la Soweto na kufanikiwa kumkamata mfanyabiashara aitwaye BUSHIRI BONIFACE (45) mkazi wa Soweto akiwa na mifuko 27 ya sukari kila mmoja ukiwa na uzito wa kilogram 50 akiweka katika mifuko midogo ya kilo moja bila kibali.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 08.05.2016 majira ya saa 15:00 alasiri huko eneo la Soweto, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga,  Jiji na Mkoa wa Mbeya katika Operesheni maalum. Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Imesainiwa na:
(JUSTUS A. KAMUGISHA – SACP)
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Dar Kuongeza madampo kukabiliana na uchafu Jijini

indexCC 
Na Lilian Lundo – Maelezo
………………………………………
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limeazimia kuongeza idadi ya madampo na kurekebisha miundombinu ya dampo la Pugu ili kuhakikisha jiji linakuwa safi.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita alisema Baraza hilo limeazimia kuongeza na kurekebisha miundombinu baada ya ziara walioifanya na kugundua mapungufu katika dampo la Pugu.
“Tumegundua kuna udhaifu mkubwa katika dampo la Pugu, magari yanayopeleka taka yananasa barabarani hivyo tukaona kuna sababu ya kutengeneza miundombinu, hivyo tumetenga milioni 700  kwenye bajeti hii ili kutengeneza barabara hiyo,”alisema Mhe. Mwita.
Aidha, alisema kwamba baraza limetenga kiasi cha shilingi milioni 200 katika bajeti ya 2016/17 ili kununua eneo Mkuranga kwa ajili ya dampo, huku wakiendelea na mchakato wa kuongeza madampo mengine Kigamboni na Kisarawe ili kuhakikisha taka zote zinazozalishwa ndani ya jiji la Dar es Salaam zinapelekwa kwenye madampo badala ya kuzagaa mitaani.
Kwa upande wake, Naibu Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Mussa Kafana alisema kuwa, suluhisho la kumaliza taizo la uchafu si kuwa na dampo tu bali ni kuwepo kwa vifaa maalumu vya kuhifadhi taka. Hivyo baraza likaamua kuwepo na vyombo vya kuhifadhia taka katika mitaa yote ya jiji la Dar es Salaam ili kudhibiti uzagaaji wa taka.
Usafi ni moja ya kipaumbele cha Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambapo kwa mara ya kwanza alitangaza siku ya Uhuru wa Tanzania (Tisa Desemba) iazimishwe kwa kufanya usafi nchi nzima ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu pamoja na kuiweka Tanzania katika hali ya usafi.
`

Wawekezaji Sekta Binafsi wahimizwa kuwekeza katika biashara ya matunda mkoani Tanga.

images 
Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
……………………………………
Wawekezaji kutoka Sekta Binafsi nchini wenye nia ya kufungua Viwanda vya juisi mkoani Tanga ikiwemo Wilaya ya Muheza wamehimizwa kuwekeza katika biashara hiyo mkoani humo.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage wakati wa kipindi cha maswali na majibu, ambapo Mhe. Mwijage alikuwa kijibu swali lililoulizwa na Mheshimiwa Balozi Adadi Mohamed Rajabu, Mbunge wa Muheza lililotaka kujua ni lini Serikali itajenga kiwanda cha matunda wilayani hapo na kuwaondolea usumbufu wakulima katika utafutaji masoko.
Mhe. Mwijage amesema kuwa tafsiri ya Serikali katika kujenga viwanda ni kwa serikali kuweka mazingira sahihi na wezeshi ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje wa sekta binafsi kujenga viwanda.
Aidha, aktika kutekeleza hilo Mhe. Mwijage ameeleza kuwa Sera na Mikakati mbalimbali shirikishi inatoa fursa kwa Sekta na Taasisi za uwekezaji kujenga viwanda na kunufaika na vivutio mbalimbali.
“Mkoa wa Tanga ikiwemo Wilaya ya Muheza wamejaaliwa kuwa na utajiri wa matunda aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na machungwa, maembe, machenza, mafenesi na mananasi, kwa kutambua upatikanaji wa matunda hayo, Wizara yangu inahimiza na kuhamasisha wawekezaji kutoka Sekta Binafsi wenye nia ya kufungua viwanda vya juisi mkoani Tanga wafanye hivo’’, alisema Mhe. Mwijage.
Amefafanua kuwa, mpaka sasa Kampuni ya M/s Sasumua Holding imeanzisha mradi mkubwa wa kulima matunda katika utaratibu utakaoshirikisho wananchi na kufikia mwezi Novemba, 2018 kiwanda cha juisi kitakuwa tayari kinafanya kazi.
“Mradi huu uko kwamsisi, Handeni mkoani Tangam hivyo ni tegemo langu kuwa mafaniko ya Mwekezaji huyo yatawavutia wawekezaji wengine”, alisema Mhe. Mwijage.
Ameongeza kuwa, Wizara kupitia Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) ina utaratibu wa kutoa ushauri jinsi ya kuanzisha mitaa ya viwanda kila mkoa ikiwa ni jitihada za kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuendeleza uzalishaji katika mikoa husika.

Wananchi wahamasishwa kuwekeza kwenye dhamana za Serikali.

G2Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Alexander Ng’winamila (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu uwekezaji kwenye dhamana za Serikali. Kulia ni Meneja Msaidizi Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BOT Bi. Victoria Msina na Kushoto ni Meneja Msaidizi Masoko ya Ndani wa BOT Bw. Genes Kimaro.
G1 
Meneja Msaidizi Masoko ya Ndani wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Genes Kimaro (kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu aina na faida za uwekezaji kwenye dhamana za Serikali.
PICHA NA FATMA SALUM-MAELEZO

SUMATRA YATANGAZA NAULI ZA USAFIRI WA MABASI YAENDAYO HARAKA.

S1Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. David Mziray akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau wa usafiri wakiwamo SUMATRA, UDA, DART na Jeshi la Polisi.
S2Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu nauli zitakazotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka unaotarajiwa kuanza rasmi Mei 10, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi kutoka SUMATRA Bw. Nahson Sigala.
S3Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Nahson Sigala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu viwango vipya vya nauli baada ya SUMATRA kufanya tathmini ya viwango vya nauli iliyopendekezwa awali na Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT na kubaini kuwa gharama zilizopendekezwa ni kubwa mno. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe.
S4Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe (Kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu DART Bw. Ronald Lwakatare wakimkabidhi leseni ya usafirishaji Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Katikati).
S5Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Kushoto) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe baada ya kupokea leseni ya usafirishaji kutoka SUMATRA.
PICHA NA FATMA SALUM-MAELEZO

Serikali Mkoani Manyara kujenga Kituo cha Michezo cha Mkoa.

nWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akijibu swali toka kwa Mheshimiwa Martha Umbulla ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum lililokuwa likiuliza ni lini Serikali itasikiliza kilio cha muda mrefu na kujenga Senta ya michezo ya riadha mkoani Manyara ili vijana wengi wenye vipaji waweze kunufaika, leo Bungeni mjini Dodoma.
………………………………………………………………………………..
Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
 
Serikali inaendelea kuendeleza sekta ya michezo nchini ikiwemo kutafuta maeneo ya kuwawezesha vijana kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana ikiwemo kuwapatia ajira vijana.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati akijibu swali toka kwa Mheshimiwa Martha Umbulla ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum lililokuwa likiuliza ni lini Serikali itasikiliza kilio cha muda mrefu na kujenga Senta ya michezo ya riadha mkoani Manyara ili vijana wengi wenye vipaji waweze kunufaika.
Mhe. Nnauye amesema kuwa Mkoa wa Manyara pamoja na Wilaya zake una vijana wenye vipaji vya riadha na michezo ambapo Serikali inatambua pia umuhimu wa kuwa na kituo kikubwa cha michezo hasa ya riadha ambacho pamoja na mambo mengine kitasaidia kuibua, kukuza na kuviendeleza vipaji vya vijana ikiwa ni pamoja na kuwapatia ajira vijana mkoani humo.
Amesema kuwa, Serikali ya Mkoa wa Manyara imepanga kujenga Kituo cha Michezo cha Mkoa, mara bada ya kukamilisha mazungumzo na kukiubaliana na wananchi wanaomiliki ardhi mkoani humo.
Aidha, ameeleza kuwa kwa kipindi hiki ambacho Uongozi wa mkoa hauna Kituo cha Michezo, mkoa umepanga kutumia kambi ya michezo ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kwa muda, wakati wanasubiri kupatikana kwa eneo la kudumu la mkoa.
“Hii inatokana na sababu kuwa hifadhi ya Taifa ya Tarangire ina hosteli za kutosha na viwanja vya michezo vya kutosha”, alisema Mhe. Nnauye.
Aliongeza kuwa, kujengwa kwa kituo hicho kutaongeza ajira na kupanua shughuli za kibiashara na hata kukua kwa uchumi wa mkoa wa Manyara.
“Serikali inaendelea na mazungumzo na wananchi wamiliki wa ardhi ili kupata eneo la ujenzi”, aliongeza Mhe. Nnauye.
Kwa upande mwingine ameziomba Halmashauri kuisadia Serikali katika kulinda maeneo ya michezo ambayo baadhi ya watu pasipo utaaratibu wanavamia na kugeuza kuwa maeneo yao ya kufanyia shughuli zao ikiwemo makazi.

NI 5000 TU,DAKIKA 90 ZA CITY VS YANGA KESHO – Mbeya City Council FC

Picture-0551Maandalizi ya mchezo namba 218 wa ligi kuu ya soka Tanzania  bara  kati ya Mbeya City fc na Yanga ya Dar es Salaam uliopagwa  kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Sokoine  jijini hapa yamekamilika  na kinachosubiriwa ni dakika 90 hapo kesho.
Kwa mujibu wa msimamizi wa kituo cha Mbeya ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha soka mkoa, Haroub Suleiman, mchezo huo  utafanyika kama ulivyopangwa kwa sababu timu zote mbili tayari zisharipoti (kuwepo) kituoni na tayari makubaliano juu ya kiingilia  yashafikiwa.
“Yanga wamewasili asubuhi ya leo, hii ina maana kuwa mchezo  upo kama ulivyopangwa, kutokana na uzito wa mchezo wenyewe,tumekubaliana kiingilio kitakuwa  shilingi 5000, nawaomba mashabiki wote wa soka katika kanda  hii ya nyanda za juu kusini  wajitokeze kwa wingi  kuzishangilia timu zao huku pia  wakitakiwa kudumisha amani kabla na baada ya mchezo” alisema.
Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Mbeya  City Fc, Mussa Mapunda amewatakia kila la kheri na kuwashukuru mashabiki wote wa timu yake popote walipo ndani na nje ya nchi kwa jinsi walivyojitolea  kuisapoti  timu yao tangu ilipopanda daraja  na kuwataka  kujitokeza kwa wingi hapo kesho  kuja  kuisapoti na kushuhudia  City ikiandikisha  ushindi wa kwanza mbeya ya Yanga.

TIB imetoa mikopo ya bilioni 550 kwa Watanzania.

10 
Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji akijibu maswali mbalimbali kuhusu Benki ya TIB na TADB katika kupunguza umaskini, leo Bungeni mjini Dodoma.
Picha na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
 
Hadi kufikia mwaka jana (2015) Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) imewawezesha Watanzania wengi kupambana na umaskini kwa kutoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 550 katika sekta mbalimbali za kiuchumi.
Taarifa hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali toka kwa Mbunge wa Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) lililotaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kuwa Benki za TIB na TADB zinajielekeza kwenye utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Mhe. Kijaji ameeleza kuwa, madhumuni ya kuanzishwa kwa benki ya TIB na TADB kama benki za maendeleo ni kutoa mikopo ya muda wa kati na muda mrefu kwa lengo la kufadhili miradi ya kimkakati, hivyo katika kutimiza azma ya kufadhili miradi ya kimkakati ya kufungua fursa za kiuchumi na kupunguza umaskini, TIB imetoa mikopo katika maeneo ya miji kupitia NHC, Viwanda vya kubangua korosho, maghala, mabomba ya maji, sukari na kilimo cha miwa, kukoboa na kusindika kahawa, kusindika matunda, mifuko ya kuhifadhia mazao na nyaya za umeme; vinu vya pamba na uzalishaji wa mafuta yatokanayo na mbegu za pamba na hoteli.
Aidha, TIB imetoa mkopo wa shilingi bilioni 489.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 181 ya kusambaza umeme vijijini kupitia REA na kaya 257,000 zimenufaika na mradi huo. Pia vikundi 17 vya wachimbaji wadogo wadogo vimenufaika na mikopo jumla ya shilingi bilioni 8.
“Mikopo ya TIB kwa sekta na taasisi mbalimbali imesaidia kwa kiasi kikubwa kutoa ajira na kuendeleza zilizopo. Pia mikopo ya TIB imetumika kuongeza uzalishaji wa bidhaa zinazouzwa nje kama vile maua, kahawa na dhahabu”, alisema Kijaji.
Aliongeza kuwa pamoja na benki ya Kilimo kuchelewa kuanza kutoa mikopo, ni wazi kuwa benki ya TIB imejielekeza kwenye utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na utekelezaji wa Mipango na mikakati mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Dira ya Taifa ya 2025, FYDB, SDGs 2030 pamoja na Afrika 2063.
TIB imewekeza katika mashirika ya umma kama vile Shirika la Reli (TRL), pia imeiwezesha TPDC katika mradi wa gesi na kuipatia Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO) mkopo kwa ajili ya fidia kwa wananchi ili kuweka njia mpya ya kusafirisha umeme.

Serikali yawataka wananchi kutumia mpango wa msaada wa kisheria.

98 
Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Charles Mmbando akiwaeleza waaandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi ambao ni wahitaji wa msaada hiyo juu ya masuala mbalimbali yanayowakabili, Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Bi. Sheiba Bulu.
8 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano huo
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.

Kipaumbele chetu ni kuboresha reli ya TAZARA- Balozi Kijazi

5 
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
………………………………….
Serikali  imesema iko tayari kuboresha reli ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA) ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi kwani ni jambo la msingi na itashirikiana na nchi za Zambia na China ili kufanikisha azma hiyo.
Akizungumza  leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Kiongozi,  Balozi  John Kijazi wakati akizindua kikao kazi kilicho shirikisha nchi tatu ambazo ni  Tanzania, Zambia na China kuhusu maboresho ya kiutendaji ya reli ya TAZARA.
“Kipaumbele chetu ni kuboresha reli ya TAZARA ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi, kikao hiki kitajadili kwa kina changamoto mbalimbali zinazoikabili reli hii, pamoja na fursa zilizopo na namna ya kutatua changamoto hizo ili kufufua uchumi wetu kupitia reli ya TAZARA” amesema Balozi Kijazi.
Balozi Kijazi amesema kwa muda sasa reli hii imekua ikifanya kazi bila ufanisi kutokana na sababu mbalimbali licha ya kuwa kiwango cha mizigo kutoka bandari ya Dar es salaam kimeongezeka kutoka tani milioni  6 mwaka 2006 hadi kufikia tani milioni 15 mwaka 2015, reli ya TAZARA imeshindwa kuwa na uwezo  wa kusaidia kusafirisha mizigo hiyo, ambapo mwaka kila mwaka uwezo wake unashuka kutoka kusafirisha mizigo tani 601,229 mwaka 2005/2006 hadi tani 87,860 kwa mawaka 2014/2015.
Vile vile, licha ya kuwa nchi za Zambia  na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeongeza uzalishaji wa shaba  bado TAZARA haikuwa na uwezo wa kuhudumia ama kusafirisha shaba hiyo, utendaji huu wa kiwango cha chini lazima ubadilike.
Aidha, Serikali imesema ina ya dhati ya kuibadilisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati, na yenye viwanda, kwa kujua kuwa uanzishwaji mzuri wa mtandao wa miundombinu hasa reli, barabara, usafiri wa anga, usafiri wa majini ni chanzo muhimu ya kutimiza azma hiyo.
Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Mawaziri la Zambia Dkt. Rowland Msiska amesema kuna haja kubwa ya kuboresha reli ya TAZARA kwa kuwa reli hiyo ina msaada mkubwa kiuchumi si tu kwa nchi za Tanzania, Zambia na China bali hata nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya  Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Aidha, amesema kuna faida nyingi za kuboresha reli ya TAZARA ikiwemo ya gharama nafuu. Usafirishaji mizigo kwa njia ya reli ni wa gharama nafuu kuliko barabara kwani inagharimu senti 5 kwa tani moja kwa umbali wa kilometa moja, huku gharama za usafirishaji kwa barabara ikiwa ni senti 12 kwa tani moja kwa umbali wa kilometa moja.
Naye, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Biashara ya China, Bwana. Liu Junfeng amesema Serikali yake  itaendelea kushirikiana na nchi za Tanzania na Zambia ili kuboresha utendaji wa reli hiyo, huku akisisitiza uhusiano wa nchi hizi tatu umeendelea kuimarika  na unazalisha fursa nyingine za ushirikiano.
Reli ya TAZARA ilijengwa mwaka 1970 hadi 1976 kwa msaada wa Jamhuri ya watu wa China kama zawadi kwa mataifa ya Tanzania na Zambia, kwa lengo la kusaidiza kuongeza njia za usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

Wadau wa maji kujadili rasilimali za bonde la Mto Rufiji.

index         
Na Jacquiline Mrisho MAELEZO
………………………………………….
Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeandaa warsha kwa wadau wake juu ya tathmini ya kimkakati ya athari za kimazingira na jamii juu ya mpango jumuishi wa usimamizi na maendeleo ya rasilimali maji za bonde la Mto Rufiji zitakayofanyika Jijini Dar es salaam na mkoani Iringa.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mbogo Futakamba alipokua akifafanua kuhusu mpangilio wa warsha hizo zitakazofanyika katika mikoa miwili ambapo kwa Jijini Dar es salaam warsha hiyo itafanyika Mei 20 mwaka huu na mkoani Iringa itafanyika Mei 23 mwaka huu kuanzia sa 3 kamili asubuhi hadi sa 10:30 jioni.
“Wizara yetu inawakaribisha wadau wake wote kushiriki warsha hii na mada zitakazotolewa zitahusisha maelezo ya jumla juu ya mipango ya maendeleo ya muda mrefu ya rasilimali za maji ya bonde la mto Rufiji na athari zake tarajiwa za kimazingira na kijamii, kuwapa fursa ya kutoa maoni na mitazamo yao juu ya mipango inayokusudiwa pamoja na kutoa ufafanuzi kuhusu maamuzi na taratibu zinazofuata,”alisema Mhandisi Futakamba.
Aidha, Mhandisi Futakamba ameongeza kuwa warsha hizo zitaandaliwa na kuwezeshwa na washauri elekezi kutoka Kampuni ya uingereza ijulikanayo kama Environmental Resource Management ikishirikiana na kampuni za JSB Envi-Dep na eMjee Consult za Tanzania.
Warsha hizo zitaruhusu wadau kujadiliana kwa pamoja na kutoa maoni ya kutosha juu ya mada zitakazoongelewa ili kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania kupitia rasilimali maji zilizopo kwenye bonde la mto huo.

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI, ENG. JOHN WILLIA MKIJAZI AFUNGUA MKUTANO WA WATAALAM KUTOKA NCHI YA CHINA, TANZANIA NA ZAMBIA

1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leonard Chamuriho (kulia), akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi kwenye Jengo la Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere, wakati alipofika kufungua Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA).3 
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John WilliamKijazi (kushoto), akisalimiana na ujumbe kutoka Nchini China ambao wanahudhuria  Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere. Kushoto kwake ni Balozi wa China NchiniDkt. LU Youqing.
4 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leornard Chamuriho (kulia), akitoa hotuba yake kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere.
5Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi,akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku nne unaozikutanisha Nchi Tatu China, Tanzania na Zambia kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere

No comments :

Post a Comment