Kutoka kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer, Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania, Luana Reale wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali katika Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 66 ya EU duniani (Picha na Modewjiblog)
Umoja wa Ulaya (EU) umesema kuwa utaendelea kushirikiana na Tanzania katika shughuli za maendeleo ikiwa kama ni moja ya kazi wanazozifanya kusaidia ukuaji wa maendeleo katika maeneo mbalimbali duniani.
Hayo yamesemwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer, kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani, kuwa kwa kipindi kirefu EU imekuwa ikifanya kazi nchini na hivyo wataendelea kukuza ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya lakini pia kuisaidia Tanzania kuata maendeleo zaidi.
“Tutaendelea kusaidia Tanzania kukuza uchumi, kusaidia kuwepo na usalama na amani na hizo ni kazi ambazo tumekuwa tukizifanya hivyo tunaamini ushirikiano wa Tanzania na EU utaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu,” alisema Van de Geer.
Pia alisema wanatambua kazi aliyoifanya Mwalimu Nyerere wakati akiwa madarakani na hata kasi iliyopo sasa katika kuleta maendeleo katika serikali ya Rais Magufuli hivyo wanaamini maendeleo yatapatikana kwa kasi.
Alisema kwa upande wa EU wataendelea kusaidia maendeleo ambapo kwa sasa watahakikisha mradi wa maendeleo wa miaka mitano (2016-2020) utafanikiwa ili kuifanya Tanzania kufikia malengo ya kuwa moja ya nchi iliyo na maendeleo barani Afrika.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akiamkaribisha Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa chini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akikaribisha wageni waalikwa kwenye halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer baada ya kuwasili kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania, Luana Reale akisalimiana na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa anayeshughulikia dawati la Marekani na Ulaya Marekani, Felista Rugambwa huku Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akiendelea kukaribisha wageni waalikwa.
Afisa Habari wa Umoja wa Ulaya, Susanne Mbise akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Balozi wa Umoja huo, Bw. Roeland Van De Geer kuzungumza na wageni waalikwa katika hafla mchapalo ya siku ya Umoja wa Ulaya iliyofanyika tarehe 9 Mei katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland Van de Geer akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani kwenye sherehe ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa Kiuchumi, Ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jiijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uswiss Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arthur Mattli katika hafla hiyo.
Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan akibadilishana mawazo na Balozi Liberata Mulamula (kushoto) halfa ya siku ya Umoja wa Ulaya katika kuadhimisha miaka 66 ya ukuaji wa kiuchumi, ustawi, Amani na Demokrasia duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
NDANDA, YANGA KUPIGWA DAR MEI 14
Mpaka sasa taarifa kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara
(TPLB), mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Ndanda na
Young Africans umepangwa kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mara
baada ya Yanga kuomba hivyo na Ndanda kama timu mwenyeji kuridhia
kuuhamisha kutoka Nangwanda Sijaona wa Mtwara.
Kwa nyakati tofauti, mwishoni mwa wiki iliyopita Young Africans ilituma maombi kwa Ndanda kadhalika TPLB kuomba ridhaa ya mchezo huo kufanyika Dar es Salaam kwa kuwa inatarajiwa kusafiri Jumapili alfajili kwenda Angola kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidia ya Sagrada Esperanca ya Angola.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TPLB, Ndanda imekubali ombi la Young Africans iliyoomba mchezo huo uhamishwe kwa malengo ya kuisaidia Young Africans kuwahi usafiri ndege kwenda Angola ambako wanatarajiwa kucheza na wapinzani wao ama Mei 17 au 18, mwaka huu.
Barua ya Bodi ya Ligi kwa TFF imesema kwamba Young Africans watatumia mchezo huo ambao Ndanda itakuwa mwenyeji kupokea taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro ameishukuru Ndanda kwa uungwana wao wa kujali maslahi ya taifa na kukubali mchezo huo kufanyika Dar es Salaam, kabla ya Young Africans kwenda Angola.
Kanuni ya pili ya Ligi Kuu Bara toleo la 2015/16 imeeleza wazi kuwa, “Katika mazingira maalumu, timu inaweza kucheza mchezo wake wa nyumbani katika uwanja mwingine endapo kuna sababu nzito na za msingi, utambulisho wa uwanja katika mazingira haya pia unawajibika kufanywa katika kipindi cha uthibitisho wa kushiriki ligi au kwa maombi maalumu kwa TPLB,” inasehemu kanuni hiyo.
Kwa kuzingatia kanuni hiyo na sababu za yanga ambazo Ndanda na Bodi wameona kuwa ni nzito wamekubaliana kucheza mchezo huo Dar es Salaam.
Yanga inatarajiwa kucheza na wapinzani wao, Sagrada Esperanca ya Angola ama Mei 17 au 18, 2016. Katika mchezo wa kwanza ulifanyika Dar es Salaam Jumamosi iliyopita Yanga iliwafunga wageni wake mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga inahitaji ama sare, ushindi na kama kufungwa basi si zaidi ya bao moja ili kuindoa Esperanca katika hatua ya awali, ili kuingia hatua ya makundi katika kusonga mbele.
Kwa nyakati tofauti, mwishoni mwa wiki iliyopita Young Africans ilituma maombi kwa Ndanda kadhalika TPLB kuomba ridhaa ya mchezo huo kufanyika Dar es Salaam kwa kuwa inatarajiwa kusafiri Jumapili alfajili kwenda Angola kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidia ya Sagrada Esperanca ya Angola.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TPLB, Ndanda imekubali ombi la Young Africans iliyoomba mchezo huo uhamishwe kwa malengo ya kuisaidia Young Africans kuwahi usafiri ndege kwenda Angola ambako wanatarajiwa kucheza na wapinzani wao ama Mei 17 au 18, mwaka huu.
Barua ya Bodi ya Ligi kwa TFF imesema kwamba Young Africans watatumia mchezo huo ambao Ndanda itakuwa mwenyeji kupokea taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro ameishukuru Ndanda kwa uungwana wao wa kujali maslahi ya taifa na kukubali mchezo huo kufanyika Dar es Salaam, kabla ya Young Africans kwenda Angola.
Kanuni ya pili ya Ligi Kuu Bara toleo la 2015/16 imeeleza wazi kuwa, “Katika mazingira maalumu, timu inaweza kucheza mchezo wake wa nyumbani katika uwanja mwingine endapo kuna sababu nzito na za msingi, utambulisho wa uwanja katika mazingira haya pia unawajibika kufanywa katika kipindi cha uthibitisho wa kushiriki ligi au kwa maombi maalumu kwa TPLB,” inasehemu kanuni hiyo.
Kwa kuzingatia kanuni hiyo na sababu za yanga ambazo Ndanda na Bodi wameona kuwa ni nzito wamekubaliana kucheza mchezo huo Dar es Salaam.
Yanga inatarajiwa kucheza na wapinzani wao, Sagrada Esperanca ya Angola ama Mei 17 au 18, 2016. Katika mchezo wa kwanza ulifanyika Dar es Salaam Jumamosi iliyopita Yanga iliwafunga wageni wake mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga inahitaji ama sare, ushindi na kama kufungwa basi si zaidi ya bao moja ili kuindoa Esperanca katika hatua ya awali, ili kuingia hatua ya makundi katika kusonga mbele.
RAIS TFF AIPONGEZA YANGA
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi
ameipongeza timu ya soka ya Young Africans kwa kutwaa ubingwa wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya
hivyo msimu uliopita wa mwaka 2014/2015.
Hii ni mara ya 26 kwa Young Africans ambayo kwa sasa inacheza mashindano ya kuwania kutwaa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kutwaa taji hilo tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1965. Simba inafuatia katika rekodi hiyo baada ya kulitwaa taji hilo kwa mara 18.
“Nichukue nafasi hii kuipongeza Young Africans kwa ubingwa. Pia nizipongeze timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya msimu wa Ligi Kuu Bara ya Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio,” amesema Rais Malinzi baada ya Young Africans kufikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 15 zilizoshiriki ligi hiyo.
Kadhalika Rais Malinzi amezikumbusha na kuhamamisha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 kutoa maoni, mapendekezo, marekebisho ya ili kuboresha kanuni za uendeshaji wa ligi hiyo kwa msimu ujao. Maoni hayo yapelekwe kwa njia ya maandishi moja kwa moja kwenye ofisi za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) au kwa njia ya barua pepe tplb.tplb@yahoo.com
Young Africans imefikia rekodi hiyo baada ya kutwaa ubingwa katika miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992,1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006 na misimu ya 2007-2008, 2008-2009, 2010-2011, 2012-2013, 2014-15 na 2015-16.
Pamoja na kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2015/2016, kikosi cha timu ya Young Africans kwa sasa kimebakiza michezo miwili ambayo ni dhidi ya Ndanda unaotarajiwa kupigwa Jumamosi Mei 14, 2016 kadhalika dhidi ya Majimaji Mei 22 ambayo itakuwa ni siku ya kufunga pazia la Ligi Kuu msimu huu wa 2015/16.
Hii ni mara ya 26 kwa Young Africans ambayo kwa sasa inacheza mashindano ya kuwania kutwaa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kutwaa taji hilo tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1965. Simba inafuatia katika rekodi hiyo baada ya kulitwaa taji hilo kwa mara 18.
“Nichukue nafasi hii kuipongeza Young Africans kwa ubingwa. Pia nizipongeze timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya msimu wa Ligi Kuu Bara ya Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio,” amesema Rais Malinzi baada ya Young Africans kufikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 15 zilizoshiriki ligi hiyo.
Kadhalika Rais Malinzi amezikumbusha na kuhamamisha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 kutoa maoni, mapendekezo, marekebisho ya ili kuboresha kanuni za uendeshaji wa ligi hiyo kwa msimu ujao. Maoni hayo yapelekwe kwa njia ya maandishi moja kwa moja kwenye ofisi za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) au kwa njia ya barua pepe tplb.tplb@yahoo.com
Young Africans imefikia rekodi hiyo baada ya kutwaa ubingwa katika miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992,1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006 na misimu ya 2007-2008, 2008-2009, 2010-2011, 2012-2013, 2014-15 na 2015-16.
Pamoja na kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2015/2016, kikosi cha timu ya Young Africans kwa sasa kimebakiza michezo miwili ambayo ni dhidi ya Ndanda unaotarajiwa kupigwa Jumamosi Mei 14, 2016 kadhalika dhidi ya Majimaji Mei 22 ambayo itakuwa ni siku ya kufunga pazia la Ligi Kuu msimu huu wa 2015/16.
RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA RAIS MUSEVENI WA UGANDA KESHO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni
mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Uganda.
……………………………………………………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Mei, 2016 amewasili
Jijini Kampala nchini Uganda ambapo kesho anatarajiwa kuhudhuria sherehe
za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri
Kaguta Museveni.
Rais Magufuli ametua katika
uwanja wa ndege wa Entebe majira ya saa tano za asubuhi na kupokelewa na
Waziri wa Ujenzi na usafirishaji wa Uganda Mheshimiwa John Byabagambi
na kisha kuelekea Ikulu ya Entebe ambako amepokelewa rasmi na mwenyeji
wake Mheshimiwa Rais Yoweri Kaguta Museveni.
Akiwa katika Ikulu ya Entebe Rais Magufuli amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na pia amepigiwa mizinga 21.
Aidha, Viongozi hao wamefanya
mazungumzo ambapo pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano
na uhusiano kati ya nchi hizo mbili, Rais Magufuli amemhakikishia Rais
Museveni kuwa Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha ujenzi
wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka Hoima katika Ziwa
Albert nchini Uganda na kupita kaskazini mwa Tanzania hadi bandari ya
Tanga.
Rais Magufuli ameongozana na
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa Mheshimiwa Suzan Kolimba.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Kampala
11 Mei, 2016
TIGO YATOA MSAADA WA VYANDARUA KWA HOSPITALI YA UKEREWE
MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO
| Baadhi ya Wabunge wa Majimbo mbalimbali wakielekea katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma tayari kwa vikao vya asubuhi leo 11 Mei, 2016. |
| Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akifurahiua jambo pamoja na Wabunge wenzie nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. |
| Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira akiingia ndani ya Bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi mjini Dodoma. |
| Naibu Waziri, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya bunge hilo. |
| Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya Wabunge Bungeni mjini Dodoma. |
| Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Tate William Ole-Nasha akijibu maswali mbalimbali ya Wabunge Bungeni mjini Dodoma. |
| Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisoma bajeti ya Wizara yake mbele ya Wabunge leo 11 Mei, 2016 mjini Dodoma. |
(Picha zote na Benedict Liwenga, Dodoma)
SERIKALI KUKAMISHA MAABARA NNE ZA UPIMAJI KIFUA KIKUU NCHINI.
Wizara ya Afya , Maendeleo ya
Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha
maabara nne za Kanda ili kuboresha huduma za vipimo vya upimaji wa kifuu
na kifuaa kikuu sugu.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha na kusogeza huduma karibu za upimaji wa kifuaa kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha Bungeni hotuba kuhusu makadirio ya
mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka ujao wa fedha 2016/17.
Amezitaja hospitali hiso ambazo
zitakuwa na maabara hizo kuwa ni Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali
ya Rufaa ya Bugando, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali
ya Kibong’oto mkoani Kilimanjaro.
Waziri Ummy aliongeza kuwa
Wizara hiyo itaendelea matibabu ya kifua kikuu sugu katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Bugando.
Aidha ,Waziri huyo aliongeza
kuwa Wizara imefanikiwa kufikia idadi ya vituo 547 vinavyotoa huduma
shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI nchini .
Hatua hii inalenga kuondoa usumbufu kwa wagonjwa wenye maambukizi mseto ya Kifuua Kikuu na UKIMWI kupata huduma sehemu moja.
Waziri Ummy aliongeza kuwa
chini ya utaratibu huo , Wizara imefanikiwa kutoa huduma watu 692,642
wanaoishi na Virusi vinavyosababisha UKIMWI (WAVIU) ili kubainisha
uwepo na kutokuwepo kwa maambukizi ya kifua kikuumiongoni mwao.
Alisema kuwa kati ya hao watu 26,218 waligundulika kuwa na maambukizi ya kifua kikuu na walipatiwa matibabu.
Aidha , Waziri huyo alisema
kuwa katika mwaka ujao wa fedha ,Wizara hiyo itaendelea kutoa huduma za
matibabu ya kifua kikuu sugu kufikia hospitali kumi za mikoa ya Dar es
salaam, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Tanga, Shinyanga, Geita
na Mara.
Alisema kuwa Wizara itaongeza
uwezo mikoa 16 yenye viwango vya chini kabisa vya uibuaji wagonjwa wa
kifua kikuu ili kuongeza kasi ya kudhibiti ugonjwa huo nchini.
Katika mwaka ujao wa fedha
Wizara hiyo iliomba Bunge likubali kuidhinisha makadirio ya matumizi ya
Wizara pamoja na Taasisi zake yenye jumla ys shilingi
845,112,920,056.00.
Kati ya fedha hizo shilingi
317,752,653,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi
527,360,267,056.00 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
BONDIA SAJJAD MEHRAB KUTOKA IRANI AWASILI KUMVAA THOMASI MASHALI MEI 14 TAIFA
| Bondia
Sajjad Mehrab kutoka ‘Iran’ akiongea na wahandishi wa habari mara baada
ya kuwasili nchini kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa Dunia na
Thomas Mashali utakaofanyika mei 14 katika uwanja wa ndani wa Taifa picha na SUPER D BOXING NEWS |
NIRAIS DKT. MAGUFULI AWASILI NCHINI UGANDA KWA AJILI YA KUSHIRIKI TUKIO LA KUAPISHWA RAIS MTEULE WA UGANDA YOWERI KAGUTA MUSEVENI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga
mkono kwenye kikundi cha ngoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
Entebe nchini Uganda. PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa
na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada
ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
zawadi ya maua kama ishara ya Ukaribisho kutoka kwa mtoto katika Ikulu
ya Entebe nchini Uganda mara baada ya kuwasili kutokea Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo
za mataifa mawili pamoja na ule wa Afrika Mashariki ukipigwa katika
Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo
za mataifa mawili pamoja na ule wa Afrika Mashariki ukipigwa katika
Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Maafisa mbalimbali waku wa vyombo vya Ulinzi wa
Serikali ya nchini Uganda mara baada ya kuwasili nchini humo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika Ikulu nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa
heshima wakati akikagua gwaride rasmi la heshima mara baada ya kuwasili
katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga
mkono kwenye kikundi cha ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye
Ikulu ya nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni
mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Uganda.
MAADHIMISHO YA MIAKA SITA YA CHAMA CHA WATANZANIA WALIOSOMEA CHINA (CAAT)
Chama cha Watanzania Waliosoma
China kwa kiingereza China Alumni Association of Tanzania (CAAT)
kinapenda kukukaribisha katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 6
(2010-2016) tokea kilipozaliwa. Sherehe hiyo itafanyika katika ukumbi wa
Cardinal Laurian Rugambwa Social Centre pembezoni mwa kanisa la
Mtakatifu Peter (St Peter), Oysterbay Ijumaa ya tarehe 20-May-2016
kuanzia saa 8 alasiri.
Sherehe hiyo itahudhuriwa na
viongozi wakubwa kutoka serikalini na baadhi ya wageni kutoka ubalozi wa
China. Pamoja na burudani mbalimbali, maadhimisho hayo yatakuwa na
hotuba kutoka viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
viongozi wa ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China. Kwenye sherehe hiyo
pia utafanyika uzinduzi wa tovuti (website) ya CAAT.
Baada ya chakula cha pamoja cha
jioni, vilevile kutakuwa na fursa ya wafanyabiashara, wajasiliamali na
wafanyakazi waajiriwa kuonyesha bidhaa au matangazo ya bidhaa au huduma
wanazotoa. Dhima kuu ya tukio hilo ni;•Utambulisho wa jumuia ya CAAT
ambayo inajumuisha wataalam wa taaluma mbalimbali waliohitimu mafunzo
yao katika Jamhuri ya Watu wa China•Kubaini na Kuainisha fursa
zinazopatikana Tanzania na China kupitia CAAT•
Maonyesho ya bidhaa na huduma
mbalimbali za biashara za wanajumuia. Wote mliopata kusoma China
mnakaribishwa. Hakutakuwa na kiingilio. Unaweza kushiriki kwa
kuthibitisha uwepo wako kwa kupiga simu kwa Katibu Mtendaji wa CAAT kwa
kupitia 0783-992020 au 0715-200090 au email gsoreku@yahoo.com
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI kupitia Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji inashauriana na Wawekezaji wa Viwanda
vinavyofanya kazi kwa kusuasua pamoja na vile vilivyofungwa ili
kuviwezesha viwanda hivyo kufanya kazi.
Kauli hiyo imetolewa leo
Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.
Charles Mwijage wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe.
Savelina Mwijage ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa
kuviboresha viwanda vya kizamani ili viweze kufanya kazi vizuri kwa
faida ya nchi.
Mhe. Mwijage amesema kuwa,
viwanda vingi vinavyotumia teknolojia ya zamani ambavyo havifanyi kazi
au kuzalisha kwa kusuasua ni vile vilivyobinafsishwa ambapo katika
tathmini iliyofanywa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili
wa Hazina inaonyesha kuwa kati ya viwanda vilivyobinafsishwa, viwanda
24 vinafanya kazi kwa kusuasua na viwanda 37 vimefungwa kote nchini.
Aidha, katika mkoa wa Kagera,
Kiwanda cha NMC Old Rice Mill kimefungwa wakati kiwanda cha Kagera Tea
Co. Ltd (MARUKU) kinafanya kazi kwa kusuasua.
“Kusuasua kwa kiwanda hiki na
vingine vyote nchini kunatokana na uchakavu wa mitambo katika baadhi ya
Viwanda, ushindani katika soko, kupungua kwa mtaji na kutopatikana kwa
malighafi”, alisema Mhe, Mwijage.
Ameongeza kuwa, Serikali
inafanya majadilaino na wawekezaji wa viwanda vinavyofanya kazi kwa
kusuasua pamoja na vile vilivyofungwa ili kuviwezesha viwanda hivyo
kufanya kazi tena ambapo katika majadiliano hayo yanayoendelea,
yanahimiza matumizi ya ya teknolojia ya kisasa katika uzalishaji
viwandani.
“Tunawashauri wawekezaji
walioshindwa kuendesha ipasavyo viwanda vyao kuingia ubia na wawekezaji
wengine wenye uwezo wa kuviendesha kwa tija ili tuongeze ajira,
tuzalishe bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na nje na kulipa kodi”,
alisema Mhe. Mwijage.
Amesisitiza kuwa, Wizara yake
kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine itaendelea kulinda viwanda vya
ndani kwa kuhakikisha bidhaa zote ziingiazo zinakidhi viwango na
zinatozwa tozo stahiki.
“Tutahakikisha kuwa tunaboresha
wepesi wa kufanya biashara kwa kuondoa tozo kero na kuhakikisha kuna
umeme wa uhakika wakati wote”, alisisitiza Mhe. Mwijage.
Serikali kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuongeza uzalishaji wa mbegu za mazao ya mafuta.
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI kwa kushirikiana na na
Sekta Binafsi nchini imeandaa mikakati inayolenga kuongeza tija na
uzalishaji wa mbegu za mazao ya mafuta hususan zao la alizeti ambao
uzalishaji wake umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka.
Hayo yamesemwa leo na Naibu
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Tate William Ole-Nasha wakati
akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Jesca Kishoa kuhusu
Serikali kuweka msukumo kwa mazao ya mafuta katika mikoa husika kwa
faida ya nchini na wakazi wa mikoa hiyo.
Mhe. Ole-Nasha amesema kwamba,
Taifa limekuwa likitumia fedha nyingi za kigeni katika kuagiza mafuta ya
kula wakati kuna vyanzo vingi vya mafuta ikiwemo alizeti na michikichi,
hivyo ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali inashrikiana na
Sekta Binafsi kuweka mikakati itayolenga kuongeza tija na uzalishaji wa
mbegu za mazao ya mafuta hususani alizeti.
Amesema kuwa, katika mkoa wa
Singida vikundi mbalimbali vimeundwa na taasisi mbalimbali za Serikali
na zile zisizo za Kiserikali ambapo moja ya malengo ya vikundi hivyo ni
kuongeza thamani ya zao la alizeti na upatikanaji wa pembejeo ili kukuza
tija na uhakika wa soko kwa wakulima.
“Kigoma ni mkoa pekee nchini
unaolima zao la michikichi kwa kiwangho kikubwa ikilinganishwa na maeneo
mengine nchini”, alisema Ole-Nasha.
Ameongeza kuwa, Hadi sasa mkoa
una zaidi ya hekta 18,924 za michikichi zenye tija ya tani 1.6 kwa
hekta, uzalishaji huo bado ni mdogo ikilinganishwa na tani 4 kwa hekta
zinazoweza kuzalishwa.
Amesema pia ili kuongeza tija,
mkoa kupitia Halmashauri zake unaendelea kuhamasisha wananchi kufufua
mashamba ya zamani ya michikichi kwa kuyapalilia, kuondoa majani
yaliyozeeka na kuanzisha mashamba mapya yatakayokuwa yanapandwa mbegu
bora.
“Mkoa kwa kushirikiana na wadau
wengine umeshaanza kuzalisha miche bora ya michikichi ambayo
itasambazwa kwa wakulima kwa gharama nafuu ili kila mkulima apande miche
137 inayotosha hekta moja”, aliongeza Ole-Nasha.
Ametoa wito kuwa, Serikali Kuu na ya Mkoa zinakaribisha
wawekezaji zaidi kuwekeza katika uzalishaji mkubwa na viwanda vya kati
na vikubwa vya kukamua mafuta na bidhaa nyingine zitokanazo na
michikichi.
RAIS MSTAAFU DK. JAKAYA KIKWETE AHANI MSIBA WA MAMA YAKE NA TEDDY MAPUNDA
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk Jakaya Kikwete na Mkewe
Mama Salma Kikwete wakisalimiana na Teddy Mapunda pamoja na Ndugu na
Jamaa wa familia wakati alipofika Mbezi nyumbani kwa wafiwa kwa ajili ya
kuhani msiba wa mama mzazi wa Teddy Mapunda Marehemu Benadette Izengo
ambaye alizikwa juzi katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk Jakaya Kikwete na Mkewe
Mama Salma Kikwete wakisaini kitabu cha Maombolezo mara baada ya
kuwasili Mbezi nyumbani kwa Teddy Mapunda kwa ajili ya kuhani msiba huo.
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk Jakaya Kikwete akisaini
kitabu cha Maombolezo huku Mama Salma Kikwete akiwa amesimama nyuma
kulia ni Teddy Mapunda Mtoto wa Marehemu Benadette Izengo.
RAIS DK. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI WA BODI ZA TAFORI NA TTB
UTEUZI
WA WENYEVITI NA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA MAKUMBUSHO
YA TAIFA, TAASISI YA UTAFITI WA MISITU TANZANIA (TAFORI) NA BODI YA
UTALII TANZANIA (TTB).
……………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi wa Shirika la Makumbusho ya Taifa, Bodi ya Taasisi ya
Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Katika uteuzi huo Mhe. Rais
amemteua Bi. Anna Abdallah (Mbunge Mstaafu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Makumbusho ya Taifa, Dkt. Felician Kilahama (Mbobezi katika
fani ya Misitu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu
Tanzania (TAFORI) na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB).
Kufuatia uteuzi huo wa Mhe. Rais,
Waziri wa Maliasili na Utalii kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya
Shirika la Makumbusho ya Taifa Sura ya 281 kifungu cha 4(2) kikisomwa
pamoja na Jedwali aya ya (1a) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi
hiyo;
- Amina Amer Issa, Mkurugenzi wa Makumbusho, Nyaraka na Mambo ya Kale Zanzibar.
- Ali S. Mcharazo, Mkurugenzi wa Tanzania Library Services, Dar es Salaam.
- Godius Kahyala, Dean, College of Arts and Social Sciences University o,f Dar es Salaam.
- Thomas J. Lyimo, Dean, Faculty of Science University of Dar es Salaam.
- Oswald Masebo, Mhadhiri, Mkuu wa Idara ya Historia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
- Lota Melamari, Consult, Management of Natural Resources and Environment and Coordinator of Tanga Botanical Gardens, Arusha.
- Anna M. Kishe, Mtaalam wa lugha za Kiswahili na Kiingereza na Mhadhiri katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dar es Salaam.
- Donatius M. Kamamba, Mkurugenzi wa Mambo ya Kale, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Aidha, kwa mamlaka aliyonayo
chini ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Sura
ya 277 kifungu cha 6(2) kikisomwa pamoja na Jedwali la 2 (1)(a), Mhe.
Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi
hiyo;
- Salim Maliondo, Profesa wa Biologia ya Misitu Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
- Susana Augustino, Mhadhiri Mwandamizi matumizi ya mazao ya misitu, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
- Deusdedit Bwoyo, Kaimu Mkuruenzi Msaidizi, Maendeleo ya Misitu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es Salaam.
- Dismas L. Mwaseba, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
- Charles Maguta Kajege, Business Consulatant (Finance), Dar es Salaam.
- Lemayon Melyoki Mkurugenzi, Shule ya Ujasiriamali, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
- Tuli S. Msuya, Katibu Tawala, Mfuko wa Misitu Tanzania, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es Salaam.
- Emma Liwenga, Mtafiti Mwandamizi, Taasisi ya Tathmini ya Maliasili (IRA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
- Lawrence Mbwambo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Morogoro.
“Pia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Bodi ya Utalii Tanzania Sura ya 364 kifungu cha 3(2) kikisomwa pamoja na Jedwali 1(2), Mhe. Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo;”
- Ibrahim Mussa, Mkurugenzi wa Masoko, TANAPA
- Balozi Joseph Sokoine Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
- Mark Leveri, Mtaalam wa kutengeneza filamu na matangazo ya video, Ex. Tanzania Film Company.
- Richard Rugimbana, Mtendaji Mkuu Tanzania Confederation of Tourism (TCT).
- Zabein Muhaji Mhita, Mbunge Mstaafu na Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi Mstaafu.
- Agustine Kungu H. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera na Uchumi, Wizara ya Fedha na Mipango.
Uteuzi wa Wenyeviti na Wajumbe hao ni wa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 24/04/2016 hadi tarehe 23/04/2019.
IMETOLEWA NA:
Angelina E.A. Madete
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
10 Mei, 2016
JWTZ LAANDAA SEMINA ya Wakuu wa Kamanda wa majeshi ya Nchi kavu Afrika
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa kutakuwa na Semina ya wiki
moja ya Wakuu wa Kamandi wa majeshi ya Nchi kavu Afrika itakayoendeshwa
Mkoani Arusha katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia tarehe 13 hadi 19, Mei
2016.
Lengo la Semina hiyo ni
kuwakutanisha Wakuu wa kamandi hizo Afrika ili kujadili na kuendeleza
ushirikiano katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali
yanayolikabili bara la Afrika katika Nyanja ya ulinzi.
Kauli Mbiu ya Semina hiyo ni Ujenzi wa Usalama Afrika kupitia Ushirikiano.
Semina hii hufanyika kila mwaka
katika mojawapo ya nchi za Afrika, ili kuwajengea makamanda hao
ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali za kiulinzi
zinazotokana na mabadiliko katika Nyanja za kiusalama.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
PIZZA HUT YAFUNGUA MGAHAWA NCHINI TANZANIA KWA KUPELEKA PIZZA KWENYE KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO
Balozi
wa Markani nchini Balozi Mark Childress katikati akishirikiana pamoja
na Bw. Vikram Desai Mkurugenzi wa Dough Works Ltd, Vikram Desai na
Mkurugenzi wa Pizza Hut Afrika, Randall Blackford Afrika, Randall
Blackford kulia kukata utepe kuzindua rasmi mhagawa huo uliopo jengo la
Mkuki Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Balozi
wa Markani nchini Balozi Mark Childress akipata maelezo kutoka kwa Bw.
Vikram Desai Mkurugenzi wa Dough Works Ltd, Vikram Desai mara baada ya
kuzindua rasmi mgahawa wa Pizza Hut uliopo jengo la Mkuki jijini Dar es
salaam.
Balozi wa Markani nchini Balozi Mark Childress akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika leo.
Baadhi ya wageni mbalimbali walioalikwa katika uzinduzi huo wa mgahawa wa Pizza Hut.
Bw.
Vikram Desai Mkurugenzi wa Dough Works Ltd, Vikram Desai akizungumza na
wageni waalikwa na kumkaribisha Balozi wa Marekani Mark Childress ili
kuzungumza na wageni waalikwa.
………………………………………………………………………………………………………………………..
Huduma ya kupeleka pizza
kileleni itatimiza rekodi ya dunia ya Guinness, kwa kutoa pizza kwenye
urefu wa juu kabisa katika ardhi, ili kuashiria ufunguzi wake nchini
Tanzania.
***** ****** *******
Kwa kutambua kuingia katika nchi
yake ya mia moja, Pizza Hut, ambayo ni sehemu ya Yum! Brands, Inc
(NYSE: YUM) na ambayo ni kampuni kubwa duniani ya mgahawa wa pizza,
imesherekea ufungunzi wa mghahawa kwa kupeleka pizza katika kilele cha
mlima Kilimanjaro nchini Tanzania. Kwa kupeleka pizza hii inaweka rekodi
ya dunia ya Guinness, kwa kutoa huduma ya kupeleka pizza katika urefu
mkubwa, juu ya ardhi wenye urefu wa zaidi ya futi 19,000.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Pizza
Hut kwa Afrika, Randall Blackford, timu ya wafanyakazi wa Pizza Hut na
baadhi ya wataalamu waangalizi, walipanda hadi kileleni mwa mlima
Kilimanjaro kwa siku tano ili kuweka rekodi ya dunia. Blackford na timu
kwa pamoja walishiriki kula pizza kubwa inayojulikana kama pepperoni juu
ya kilele cha mlima katika kusherehekea mwendelezo wa kupanuka kwa
Kampuni kimataifa. Mshauri kutoka rekodi ya dunia ya Guinness alikuwepo
nchini Tanzania ili kuthibitisha kwamba Pizza Hut kweli imeweka rekodi
kwa kutoa huduma ya kupeleka pizza kwenye urefu wa juu kabisa katika
ardhi.
Si tu kwamba timu imeweka rekodi
za dunia za Guinness, pia wamechangia kiasi cha shilingi za kitanzania
milioni 15 (karibu dola za kimarekani 7,000) kwa Shule ya Msingi Msasani
jijini Dar Es Salaam,Tanzania kama njia ya kuonyesha dhamira yao ya
kusaidia jamii ambazo zimewazunguka. Fedha hizo zitasaidia kufanya
matengenezo mbalimbali ya shule kwa wanafunzi 1,300 na kutoa mafunzo kwa
walimu wao.
“Tunayofuraha kubwa kuileta Pizza
Hut nchini Tanzania na tunaamini hakuna njia bora ya kusherehekea nchi
yetu ya 100 zaidi ya kuweka rekodi ya dunia kwa kutoa huduma ya kupeleka
pizza juu kabisa ya ardhi kwenye mlima Kilimanjaro, “alisema Milind
Pant, Rais wa Pizza Hut kimataifa. “Pizza Hut iko njiani kuwa ni mgahawa
unaopendwa zaidi na kukua kwa kasi katika kipengele cha pizza na
tunafanya bidiii ili iwe rahisi kwa wateja wetu kupata pizza zetu bora
duniani kote.
Pizza Hut, ambayo ina zaidi ya
mighahawa 16,000 duniani kote na kwa mwaka 2015 jumla ya mauzo yake
yalikuwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 12, ni kampuni ya mghahawa
wa pizza pekee na ya kwanza kuwa katika nchi 100. Pizza Hut iliingia
Afrika mwaka 2014 na inaona fursa ya kukua Afrika kwa miaka kadhaa
ijayo.
Mkurugenzi wa Dough Works Ltd,
Vikram Desai, alishirikisha shauku yake kwa ufunguzi wa mgahawa akisema,
“Timu yetu ina furaha na inajivunia kuileta Pizza Hut kwa watanzania.
Tumewekeza mamilioni ya dola ili kuendeleza biashara ya Pizza Hut nchini
Tanzania na tunampango wa kufungua zaidi ya migahawa minne ya Pizza Hut
ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Tunayofuraha kuendelea kuieneza zaidi
bidhaa hii ya kimataifa katika jamii yetu, kutengeneza zaidi ya ajira
mpya 500 kufikia mwisho wa mwako 2019 na kuendeleza zaidi sekta ya QSR. “
Pizza Hut mpya inapatikana katika
maeneo ya Mkuki Mall barabara ya Nyerere jijini Dar Es Salaam. Mgahawa
umepambwa kwa mtindo wa kisasa, ubao unaoonyesha aina na bei ya pizza ni
wa kidijitali, ina sehemu ya kucheza watoto na ina siti za kukaa watu
90. Bali na ladha ya kimataifa ya Pizza Hut,pia kuna orodha ya menu
yenye ladha inayopendwa nchini kama vile Peri-Peri chicken, Paneer
Vegorama na Tandoori Paneer pizzas.
Serikali kuwaunga mkono Wananchi wa Busiri katika uchimbaji madini.
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
……………………………
Serikali imewaunga mkono
Wachimbaji Wadogo wa Madini wa Busiri kwa kuwatafutia maeneo ya
uchimbaji wa madini, ambapo Wizara ya Nishati na Madini imetenga eneo
lenye ukubwa wa hekta 11,031 lililokuwa chini ya Leseni za Utafutaji
namba PL 3220/2005 ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Bw. Daudi Mbaga pamoja
na PL 5853/2009 iliyokuwa ikimilikiwa na na Meru Minerals Resources
Limited ambazo zilizoisha muda wake.
Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini
Dodoma na Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard
Kalemani wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi
kuhusu mikakati ya Serikali ya kuwaunga mkono Wachimbaji wadogo wadogo
wa Busiri.
Mhe. Kalemani ameeleza kuwa,
hadi mwishoni mwa mwezi Machi, 2016, Wizara yake imegawa kwa wananchi wa
Busiri leseni 81 za Uchimbaji Mdogo wa Madini (PMLs) katika eneo hilo,
sawa na takribani hekta 810 kati ya hekta 11,031 za eneo lililoachwa kwa
ajili ya Wachimbaji Wadogo.
“Wizara imegawa leseni nyingine
30 za uchimbaji mdogo (PMLs) katika eneo lililopo katika kijiji cha
Kuntakama takribani kilomita moja eneo la uchimbaji mdogo wa madini la
Busiri”, alisema, Mhe. Kalemani.
Ameongeza kuwa, mkakati mwingine
wa Serikali ni kuendelea kulitumia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)
kutoa huduma ya ugani kwa wachimbaji madini wadogo wa kijiji cha Busiri
na wengine wote nchini ikiwemo kutoa ruzuku kupitia Mfuko wa Wachimbaji
Wadogo.
“STAMICO pia itaendelea kuwapa
elimu wachimbaji wadogo na kuwahamasisha kuunda Vikundi vya Uchimbaji
ili waweze kusaidiwa kwa pamoja”, alisema Mhe. Kalemani.
Aidha, Serikali imekuwa
ikiwatembelea wachimbaji madini wa eneo tajwa mara kwa mara kwa kutumia
Maafisa na Wataalamu wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi na
Ofisi ya Afisa Madini Mkazi-Bukoba.
Amefafanua kuwa, tarehe 11
Machi, 2016 Afisa Madini Mkazi wa Bukoba alifika na kufanya mkutano na
kikundi cha Busiri Mining Co-operative Society Limited chenye Leseni Na.
PML 001712WLZ.
“Ili kutekeleza ombi la sasa la
Mheshimiwa Mbunge, Wizara yangu itamtuma Afisa Madini wa Kanda ili
awatembelee tena na kuwaelimisha juu ya fursa zilizopo za kuendeleza
wachimbaji wadogo ili uchimbaji uwe wenye tija na kutoa ajira na kuondoa
umaskini kupitia uchimbaji wa madini”, aliongeza, Mhe. Kalemani.
Matukio bungeni Dodoma leo
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Mhe. Ummy Mwalimu
(IMb) akisoma taarifa ya Bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma, 11
Mei, 2016.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akifurahi na Wabunge wenzie nje ya
Bunge mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DODOMA.
VIKUNDI 39 VYA WANAWAKE WILAYANI MOROGORO VYAPATIWA MIKOPO YA SHILINGI MILIONI 23.8
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
……………………………………………….
Halmashauri ya Wilaya ya
Morogoro imeviwezesha Vikundi 39 vya Wanawake pamoja na Vijana vyenye
wanachama 295 kupatiwa mikopo ya jumla ya shilingi milioni 23.8 kupitia
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake.
Taarifa hiyo imetolewa
leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo (Mb) wakati
akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mhe. Tebweta Omary
lililotaka kujua mpango wa Serikali wa kuzibana na kuziamuru
Hallmashauri zote ikiwemo ya Morogoro Vijijini kutenga asilimia 5 ya
fedha za mapato ya ndani kwa Vijana na asilimia 5 kwa ajili ya akina
mama.
Mhe. Jafo amesema
kuwa, katika mwaka wa fedha wa 2015/16, Serikali imetenga shilingi
milioni 175 kwa ajili ya wanawake na vijana kutokana na mapato ya ndani.
Amefafanua kuwa,
mkakati wa sasa wa Serikali ni kuimarisha makusanyo ya mapato ili
kujenga uwezo wa kutenga fedha zaidi ambapo katika bajeti ya mwaka wa
fedha wa 2016/17 sharti la kupitisha makisio ya bajeti ya kila
Halmashauri lilikuwa ni kuonyesha asilimia 10 zilizotengwa kwa ajili ya
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake kutokana na mapato ya ndani.
“Halmashauri zote
zimeagizwa kuhakikisha fedha hizo zinapelekwa kwenye vikundi husika
ikijumuisha walemavu na kusimamia marejesho yake ili vikundi vingine
viweze kunufaika.
Kwa upande mwingine,
Mhe. Jafo amejibu swali la Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Kanyasu
Costantine John ambaye alitaka kujua kwanini Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya Nyankimbo imabaki kuwa shule ya Kutwa wakati mazingira yake
yanafaa kuwa sekondari ya Bweni ambapo alijibu kuwa shule hiyo
ilijengwa chini ya Mradi wa Geita Giold Mining na kupata usajili wa Na.
S.1942 mwaka 2006 ikiwa ni shule ya kutwa kwa kidato cha Kwanza hadi cha
Nne.
Aidha, amesema kuwa
mwaka 2012 shule hiyo iliongezewa kidato cha Tano na Sita hali
iliyoifanya shule hiyo kuwa imesajiliwa ya kutwa kwa kidato cha kwanza
hadi cha nne na Bweni kwa kidato cha Tano na Sita.
“Taratibu zilizotumika
ili kuisajili shule kuwa ya bweni ni Halmashauri yenyewe kuwasilisha
maombi Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ili kupata
kibali”, alisema Mhe. Jafo.
Aliongeza kuwa, kabla
ya kupata usajili, Kamishna wa Elimu atatuma Timu ya Wataalam katika
shule husika kwa ajili ya kuhakiki uwepo wa miundombinu inayohitajika
ilio shule iweze kusajiliwa kuwa ya bweni.
WANANCHI WATOA MAONI JUU YA MABASI YA MWENDO KASI
Na Lorietha Laurence-Maelezo
………………………………………
Baada ya kuanza rasmi kwa mabasi
ya mwendo wa haraka Jijini Dar es Salaam wananchi wameupokea kwa maoni
tofauti huku wengi wao wakisifia hatua hiyo ya serikali katika
kurahisisha hali ya usafiri katika jiji hilo.
Wakitoa maoni yao katika maeneo
mbalimbali ya jiji ,Bw.Kulwa Khamis Mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi
mwisho amesema kuwa huduma hii ya usafiri ni nzuri kwa kuwa haina foleni
na inaokoa muda wa kusafiri.
“nimefurahishwa na huduma hii kwa
kuwa haina foleni na inasaidia kufika kwa wakati maeneo yetu ya kazi na
hata kurudi nyumbani mapema,jambo ambalo linapunguza muda mwingi
uliokuwa ukipotea katika foleni” alisema Bw.Khamis.
Naye Bi.Emmy Jonas mkazi wa
Kibamba amesema kuwa huduma hiyo ni nzuri lakini amedai kuwa nauli ni
kubwa na kuomba uongozi wa Dar es Salaam Rapid Transport (DART) na
taasisi husika kufikiria upya nauli ili wananchi wa hali ya chini
waweze kumudu.
Aidha Bi. Jonas ameiomba serikali
kumalizia miundombinu ya barabara ya mabasi yaendayo kwa haraka (BRT)
ili yaweze kufika mpaka Kibaha, badala ya Kimara mwisho ili kuepukana na
usumbufu wa kupanda magari.
Kwa upande wake Mtaalam wa
Mawasiliano wa BRT, Bw. Abraham Nyatori ameiomba jamii ibadilike
kuhusu utunzaji wa miundombinu,“hakuna kitu kinaitwa mali ya
umma”,amesisitiza Nyatori.
Mtaalam huyo alikuwa na maana
kwamba kila mwananchi anatakiwa kulinda na kuitunza miundombinu ili
itumike kwa muda mrefu na kuiona kama mali yake na siyo ya umma.
Serikali imekuwa ikijenga barabara
katika maeneo mbalimbali jijini na baadhi ya barabara hizo kuharibika
baada ya muda mfupi na hivyo kuigharimu serikali mamilioni ya fedha
kwa ajili ya matengenezo badala ya kujenga barabara zingine .
JUMLA YA SILAHA 36 ZAZUILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA
| Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo |
Na Woinde Shizza,Arusha
Kufuatia zoezi la kuhakiki silaha linaloendelea hapa nchini jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa
kuhakiki jumla ya silaha 2640 na jumla ya silaha 36 zilizosalimishwa
zimefutiwa leseni za umiliki kutokana na sababu mbalimbali .
kuhakiki jumla ya silaha 2640 na jumla ya silaha 36 zilizosalimishwa
zimefutiwa leseni za umiliki kutokana na sababu mbalimbali .
Akiongelea swala hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa
silaha silaha hizo zimebaki chini ya uangalizi wa jeshi la polisi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo na baadhi ya
wamiliki kupitisha umri wa kumiliki silaha ,wengine wakiwa wagonjwa pamoja na wengine kukosa sifa ya kumiliki silaha
hizo.
silaha silaha hizo zimebaki chini ya uangalizi wa jeshi la polisi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo na baadhi ya
wamiliki kupitisha umri wa kumiliki silaha ,wengine wakiwa wagonjwa pamoja na wengine kukosa sifa ya kumiliki silaha
hizo.
Alisema
kuwa umri wa kumiliki silaha mwisho ni miaka 70 ambapo kuna baadhi ya
wananchi ambao walikuwa wanamiliki silaha hizo tayari wameshafikia ukomo
wa umri wa kumiliki silaha hizo kisheria.
Aidha
alisema pia kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wanamiliki silaha zaidi
ya moja bila sababu yeyote nao wamenyang’anywa huku wengine wakiwa
wamechukuwa silaha hizo bila kujua matumizi halali ya umiliki wa silaha
hizo.
Alitaja aina ya silaha ya silaha mbalimbali ambazo tayari
zimekaguliwa na kukabidhiwa kwa wamiliki kuwa ni bastola 1434,Raifo 540 pamoja na Shortigun 666.Alisema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea kuhakiki silaha hizo hivyo wananchi wote ambao wanamiliki silaha wajitokeze na silaha zao kwa ajili ya kuhakikiwa kwani zoezi likiisha wataanza upekuzi wa silaha zote ambazo hazijahakikiwa na mtu akikutwa nayo akiwa ajahakiki ataokana ametenda kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria
zimekaguliwa na kukabidhiwa kwa wamiliki kuwa ni bastola 1434,Raifo 540 pamoja na Shortigun 666.Alisema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea kuhakiki silaha hizo hivyo wananchi wote ambao wanamiliki silaha wajitokeze na silaha zao kwa ajili ya kuhakikiwa kwani zoezi likiisha wataanza upekuzi wa silaha zote ambazo hazijahakikiwa na mtu akikutwa nayo akiwa ajahakiki ataokana ametenda kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria
Mkumbo pia aliwasihi watu wote ambao wanataka kumiliki silaha kwenda kupata mafunzo kwanza
kabla ya kukabidhiwa silaha na ambaye amesahamu matumizi ya silaha basi arudi kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi
juu ya matumizi sahihi ya silaha.
kabla ya kukabidhiwa silaha na ambaye amesahamu matumizi ya silaha basi arudi kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi
juu ya matumizi sahihi ya silaha.
wanamiliki silaha wajitokeze na silaha zao kwa ajili ya kuhakikiwa
kwani zoezi likiisha wataanza upekuzi wa silaha zote ambazo
hazijahakikiwa na mtu akikutwa nayo akiwa ajahakiki ataokana ametenda
kosa la kumiliki silaha kinyume cha
sheria .
sheria .
Mkumbo
pia aliwasihi watu wote ambao wanataka kumiliki silaha kwenda kupata
mafunzo kwanza kabla ya kukabidhiwa silaha na ambaye amesahamu matumizi
ya silaha basi arudi kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi juu ya matumizi
sahihi ya silaha.
SEREKALI YATAKIWA KUAJIRI NA KUPELEKA WAGANGA ,WAUGUZI NA WAKUNGA KATIKA MAENEO YA VIJIJINI
Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Taifa Shaka Hamdu Shaka Akizungumza Katika
Mkutano Ulio Fanyika Katika Ukumbi Wa Ccm Mkoa Lakini Pia Katika
Mazungumzo Yake Alimtaka ,Mstahiki Meya Kutopokea Hongo Za Wapinzani Ili
Kujiuzuru Alisema ”Mstahiki Meya Tunatambua Chama Cha Cuf Kinataka
Kukupa Hongo Ili Ujizuru Nafasi Hiyo Nnakutahadharisha Kamwe Usijaribu
Kukichezea Chama Cha Mapinduzi Na Sisi Kama Vijana Wa Ccm Tunakutaka
Kupuuza Yote Na Kufanya Kazi Bila Vishawishi Vyovyote Ili Tufikie
Malengo Ya Kuitekeleza Ilani Ya Ccm 2015-2020 Uchaguzi Umekwisha Sasa
Ni Muda Wa Kazi”
Mkutano Ulio Fanyika Katika Ukumbi Wa Ccm Mkoa Lakini Pia Katika
Mazungumzo Yake Alimtaka ,Mstahiki Meya Kutopokea Hongo Za Wapinzani Ili
Kujiuzuru Alisema ”Mstahiki Meya Tunatambua Chama Cha Cuf Kinataka
Kukupa Hongo Ili Ujizuru Nafasi Hiyo Nnakutahadharisha Kamwe Usijaribu
Kukichezea Chama Cha Mapinduzi Na Sisi Kama Vijana Wa Ccm Tunakutaka
Kupuuza Yote Na Kufanya Kazi Bila Vishawishi Vyovyote Ili Tufikie
Malengo Ya Kuitekeleza Ilani Ya Ccm 2015-2020 Uchaguzi Umekwisha Sasa
Ni Muda Wa Kazi”
Wanachama Wapya Wakila kiapo cha Chama na Jumuiya
Na Woinde Shizza, TangaSerikaki umeshauriwa kusomesha , kuajiri na kupeleka waganga, wauguzi na
wakunga katika maeneo ya vijijini ili ukokoa maisha ya kina mama
wajawazito, iiiweko kutoa huduma bora za afya na tiba . Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM )umetoa ushauri huo baada
ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kutembelea hospitali kuu ya
Bombo katika Manispaa ya Mji wa Tanga.
Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka alitoa ushauri huo alipomaliza
kutembelea hospitali hiyo , kusikiliza kero , kupata maelezo toka kwa
muuguzi wa zamu Atose Kiluvia katika hospitali ya Bombo mkoani hapa .
Shaka aliueleza Muuguzi Kiluvia amueleze mganga mkuu wa wilaya kwamba
ili kufikia malengo ya mil enia kuna ulazima wa kuhakikisha maisha ya
kina mama wajawazito yanawekewa utaratibu bora wa kudumu ili kunusuru
maisha yao , kupata ushauri wa maendeleo yao nyakati za ujauzito
wakipata huduma katika vituo vya huduma ya afya.
Alisema ili huduma hizo ziweze kuimarika na kutolewa kwa wakati, mkakati
pekee ujaohitajika na kupewa kipaumbele ni kuweka mazingira bora
kuanzia halmahsuri za wilaya hadi serikali kuu ili kusomesha, kuajiri na
kupeleka wakunga, waganga na wauguzi maeneo ya vijijini.
“Mikakati ya maendeleo ya uimarishaji huduma za msingi za kijamii
ziibuliwe katika ngazi za halalmshauri za wilaya kabla ya Serikali kuu
haijaweka mkono wake, madiwani na wakurugenzi wa halmashauri watenge
muda wankushughulikia nw kuondosha kero mapema” alishauri Shaka.
Alisema haiwezekani madiwani wakashiriki vikao vya Baraza la madiwani
ambalo ni bunge la wilaya bila kujadili huduma zznjamii lama vike ujenzi
wa vituo vya afya, masuala ya kilimo, mifugo, miundombinu au ajira za
wakunga, waganga na wauguzi.
Aidha alisema haiwezekani kuzungumzia mpango wa maendeleo ya nchi huku
kukiwa na hali ya kuzorota kwa huduma za jamii kama tiba , chanjo na
kinga au kuwepo upungufu wa wauguzi, wakunga na waganga .
“Zijengwe nyumba bora za kisasa ambazo waganga, wakunga na wauguzi
wataishi na kuridhika, walimu na wataalam wengine wa maendeleo ya kiseta
pia wawe na nyumba za uhakika maeneo ya vijijini. “Alisema
Halmashauri ikipeleka umeme, zikajengwa barabara, nyunba za wataalam
wetu , hakuna atakayekataa kuishi vijijini, siasa ya ujamaa na
kujitegemea haina maana watu waishi katika nyunba za nyasi, hata
mkienga nyumba za roshani bado mtabaki kuwa wajamaa.
Alisema serikali kuu haiwezi kufanya kila kitu katika vitongoji, vijiji,
kata na kwenye wilaya,kazi hiyo lazima ifanywe na halmashauri zetu
wakiwemo wataalam na madiwani.
“Kazi ya serikali kuu ni kupeleka ruzuku, fedha za ruzuku zisitafunwe
na mchwa , kazi ya madiwani ni usimamizi wa matumizi bora ya fedha za
umma, yakipatikana mafanikio kila kijiji ndiyo maendeleo ya Taifa
“alisema Shaka ambaye emeanza ziara ya siku sita mkoani hapa.
wakunga katika maeneo ya vijijini ili ukokoa maisha ya kina mama
wajawazito, iiiweko kutoa huduma bora za afya na tiba . Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM )umetoa ushauri huo baada
ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kutembelea hospitali kuu ya
Bombo katika Manispaa ya Mji wa Tanga.
Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka alitoa ushauri huo alipomaliza
kutembelea hospitali hiyo , kusikiliza kero , kupata maelezo toka kwa
muuguzi wa zamu Atose Kiluvia katika hospitali ya Bombo mkoani hapa .
Shaka aliueleza Muuguzi Kiluvia amueleze mganga mkuu wa wilaya kwamba
ili kufikia malengo ya mil enia kuna ulazima wa kuhakikisha maisha ya
kina mama wajawazito yanawekewa utaratibu bora wa kudumu ili kunusuru
maisha yao , kupata ushauri wa maendeleo yao nyakati za ujauzito
wakipata huduma katika vituo vya huduma ya afya.
Alisema ili huduma hizo ziweze kuimarika na kutolewa kwa wakati, mkakati
pekee ujaohitajika na kupewa kipaumbele ni kuweka mazingira bora
kuanzia halmahsuri za wilaya hadi serikali kuu ili kusomesha, kuajiri na
kupeleka wakunga, waganga na wauguzi maeneo ya vijijini.
“Mikakati ya maendeleo ya uimarishaji huduma za msingi za kijamii
ziibuliwe katika ngazi za halalmshauri za wilaya kabla ya Serikali kuu
haijaweka mkono wake, madiwani na wakurugenzi wa halmashauri watenge
muda wankushughulikia nw kuondosha kero mapema” alishauri Shaka.
Alisema haiwezekani madiwani wakashiriki vikao vya Baraza la madiwani
ambalo ni bunge la wilaya bila kujadili huduma zznjamii lama vike ujenzi
wa vituo vya afya, masuala ya kilimo, mifugo, miundombinu au ajira za
wakunga, waganga na wauguzi.
Aidha alisema haiwezekani kuzungumzia mpango wa maendeleo ya nchi huku
kukiwa na hali ya kuzorota kwa huduma za jamii kama tiba , chanjo na
kinga au kuwepo upungufu wa wauguzi, wakunga na waganga .
“Zijengwe nyumba bora za kisasa ambazo waganga, wakunga na wauguzi
wataishi na kuridhika, walimu na wataalam wengine wa maendeleo ya kiseta
pia wawe na nyumba za uhakika maeneo ya vijijini. “Alisema
Halmashauri ikipeleka umeme, zikajengwa barabara, nyunba za wataalam
wetu , hakuna atakayekataa kuishi vijijini, siasa ya ujamaa na
kujitegemea haina maana watu waishi katika nyunba za nyasi, hata
mkienga nyumba za roshani bado mtabaki kuwa wajamaa.
Alisema serikali kuu haiwezi kufanya kila kitu katika vitongoji, vijiji,
kata na kwenye wilaya,kazi hiyo lazima ifanywe na halmashauri zetu
wakiwemo wataalam na madiwani.
“Kazi ya serikali kuu ni kupeleka ruzuku, fedha za ruzuku zisitafunwe
na mchwa , kazi ya madiwani ni usimamizi wa matumizi bora ya fedha za
umma, yakipatikana mafanikio kila kijiji ndiyo maendeleo ya Taifa
“alisema Shaka ambaye emeanza ziara ya siku sita mkoani hapa.
Taasisi za Umma zatakiwa kutumia mifumo ya kiutendaji
Wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma nchini wakifuatilia mada
……………………………………………………………………………………………….
Taasisi za Umma zimehimizwa kutumia ipasavyo mifumo ya utendaji kazi iliyowekwa ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi Msaidizi ,Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Veila Shoo alisema hayo wakati
akitoa takwimu za matumizi ya mifumo hiyo katika kikao kazi
kilichohusisha wawakilishi kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea
na Wakala za Serikali na kufanyika katika ukumbi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi.
Bi. Veila alieleza kuwa
ufuatiliaji wa mifumo umefanyika katika Idara Zinazojitegemea 16 ambapo
imebainika baadhi ya mifumo inatukima ipasavyo wakati mingine bado.
Awali, akifungua kikao kazi hicho
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Bw. Mick Kiliba
alisema kuwa zoezi la kufanya ufuatiliaji wa mifumo ni endelevu na
watendaji wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa
kutumia mifumo hiyo.
Alisema lengo la tathmini hiyo ni
kupata takwimu za utekelezaji wa mifumo na viwango vya utendaji kazi,
kutambua mifumo yenye changamoto za utekelezaji, kutoa hamasa ili
kuboresha utoaji huduma na kutoa mrejesho kwa taasisi jinsi ya
kuimarisha mifumo.
Mifumo iliyofanyiwa tathmini ni
pamoja na:- Mpango mkakati Mkataba wa Huduma kwa Mteja; Mfumo wa wazi wa
Tathmini ya Utendaji kazi; Uboreshaji wa michakato ya Utoaji huduma;
Tathmini ya Utoaji huduma wa Taasisi; Tathmini ya ndani ya Taasisi;
Ushirikiano wa Taasisi ya Umma na Asasi za Kiraia(AZAKI); Waraka Namba 1
wa mwaka 2012 kuhusu Ununuzi wa Samani za Ofisi; na Usimamizi wa Fomu
za Serikali.
SHIWATA kumkabidh Samatta eneo Juni 4
BABA
Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati)
akiwa na Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael
Kagondela kulia na Mhasibu wa mtandao huo, Asha Salvador baada ya
kumkabidhi kadi ya uanachama na katiba baada ya kikao cha kuthibitisha
mwanae kukubali kupewa ekari tano za kujenga kituo cha wanamichezo,
Mkuranga
BABA
Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati)
akijaza fomu za kukubali masharti ya kujiunga na Mtandao wa Wasanii
Tanzania (SHIWATA) mbele ya Mhasibu wa mtandao huo Asha Salvador.
………………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania
(SHIWATA) umeandaa sherehe za kumkabidhi eneo la kujenga kituo cha
michezo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta katika sherehe
zitakazofanyika Juni 4, 2016 kwenye kijiji cha Wasani Mwanzega Mkuranga.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim
Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa maandalizi ya sherehe hizo
itaambatana na ugawaji nyumba 31 kati ya hizo moja kubwa, tatu ndogo na
misingi 27 ya nyumba hivyo kufikisha jumla ya nyumba 150.
Alisema baba yake Mbwana Mzee
Ali Samatta amethibitisha kuwepo kwa mwanae katika sherehe hizo ambazo
naye ametunukiwa kuwa mwanachama wa heshima wa mtandao huo na kukubali
kushirikiana kuhakikisha michezo inakuwa nchini.
“Baba yake Samatt alisema
wakati akiwa kijana alikuwa mfungaji mzuri kwa timu alizowahi kuchezea
miaka ya sitini kama vile timu ya shele ya Sekondari ya Mzumbe, timu ya
mkoa wa Morogoro, timu ya Polisi na badaye aliwahi kuichezea Simba akiwa
na akina Hamisi Kilomoni” alisema Taalib.
Alisema sherehe hizo pia
zitapambwa na wasani kutoka vikundi mbalimbali vya ngoma na sarakasi
kutoka jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani..
Alisema SHIWATA ilimzawadia
uanachama wa heshima mchezaji huyio baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji
bora wa Afrika na kutangaza kumpatia eneo la ekari tano kwa ajili ya
kujenga kituo cha wanamichezo.
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete atembelea daraja la Nyerere Kigamboni
Mweneyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya
awali na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipowasili
kukagua daraja lla Nyerere, leo Mei 10, 2016. Kulia ni Msemaji wa CCM,
Christopher Ole Sendeka.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph
Nyamhanga, akimpokea Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
alipowasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na viongozi
mbalimbali waliompokea, kabla ya kukagua daraja la Nyerere, Dar es
Salaam, leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara
zinazopishana ya chini na ya juu mwanzoni mwa daraja la Nyerere,
alipokagua daraja hilo, leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara
zinazopishana ya chini na ya juu mwanzoni mwa daraja la Nyerere,
alipokagua daraja hilo, leo
Msafara wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ukipita
kwenye daraja la Nyerere kwenda Kigamboni, alipokagua daraja hilo leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu jakaya Kikwete akiangaza mandhari ya darala la Nyerere alipokagua daraja hilo leo
Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde atembelea kambi tiba ya GSM Dodoma
Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde leo
amefanya ziara ya kushtukiza katika kambi tiba ya GSM Foundation
inayofanywa na kikosi cha Madaktari bingwa kutoka hospitali ya MOI,
ambayo kuanzia leo imepiga kambi Dodoma baada ya kutoka katika mikoa ya
Mwanza, Singida, na Shinyanga.
Akieleza
sababu za kuitembelea kambi hiyo ambayo iko katika hatua zake za mwisho
kumaliza awamu ya kwanza, Mheshimiwa Mavunde amebainisha kwamba kwanza,
ni kwa sababu alisikia kambi iko katika jimbo lake, lakini jingine
kubwa na la msingi likawa ni kupeleka shukrani zake kwa Maafisa wa
Taasisi ya GSM wanaoambatana na madaktari kuweka kambi tiba hizo katika
kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na migongo wazi
kila mwaka.
“Nimeshtushwa
na takwimu za mwaka juzi, kwamba wanaozaliwa ni 4000 na wanaorudi
hospitali kwa ajili ya tiba hawazidi 600. Hii ni hatari, ilipaswa mtu
kuchukua jukumu la haraka na nimeshukuru kusikia GSM mmefanya hilo,
hongereni sana”, alisema Mavunde.
Mavunde
amewataja Maafisa wa GSM na Madaktari kuwa ni watu wenye moyo wa
kizalendo ambao wanatakiwa kuigwa na jamii, wameacha familia zao, na
wameamua kuokoa maisha ya watoto ambao hata hawawajui, kwa sababu moja
tu kubwa na ya msingi ya utanzania.
PICHANI JUU: Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony
Mavunde(Wa Pili kutoka kulia) akikaribishwa eneo la Hospitali na Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw Jordan Rugimana(Wa tatu kutoka kulia) na
Naibu Mkurugenzi wa MOI ambaye ndio mratibu wa kambi tiba ya GSM DK
Othman KIloloma(Wa nne kutoka kulia) na Meneja wa Taasisi ya GSM BI
Shannon Kiwamba(kushoto)
Mh Mavunde akisikiliza maelezo ya mmoja kati ya wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
Mratibu wa Kambi Tiba ya GSM, Dk Othman Kiloloma akimpa taarifa za wagonjwa Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini
Mh Mavunde akiongea na wanahabari waliokuwa hospitalini hapo kufuatilia habari za wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
Mh
Mavunde akibadilishana mawazo na mratibu wa kambi tiba ya GSM, Dk
Othman Kiloloma, wanaosikiliza ni Kibwana Matukio kutoka GSM, na Mganga
mkuu wa mkoa Bw Jordan Rugimana
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aondoka nchini kwenda Uingereza
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka
kwenda London Uingereza Mai 10 , 2016, kumwakilisha Rais John Magufuli
kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi wa kujadili masuala ya kupambana na
rushwa duniani.
(Picha n Ofisi ya Wziri Mkuu)
WARAMI WAMPONGEZA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUWATETEA WANYONGE, WASEMA ANAPIGWA VITA NDANI YA BUNGE NA NJE YA BUNGE
Kuna tani nyingi za sukari
zimekamatwa katika msako maalum ambao Rais aliamrisha vyombo vya dola
kufuatilia wafanyabiashara wasio waaminifu walioficha sukari, baada ya
zoezi hilo kuanza sukari nyingi imeendelea kukamatwa maeneo mbalimbali
nchini ikiwa imefichwa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.
WARAMI inapongeza jitihada zote
za dhati anazozifanya Rais Magufuli na Serikali yake za kuhakikisha
watanzania wanaishi kwenye usawa, lakini pamoja na hayo wanapendekeza
mambo kadhaa yafanyika na jeshi la polisi
Mratibu huyo wa Taasisi ya WARAMI
amelitaka jeshi la polisi kutoa taarifa rasmi juu ya wafanyabiashara
wanaotamba barabarani kuwa wameliweka jeshi hilo mfukoni kwamba hakuna
wa kuwafanya lolote katika nchi hii.
Taasisi za kiserikali zifafanue
juu ya tabia hii ya wafanyabiashara kutumia picha za viongozi kwa
maslahi yao kama, ni haki ama si haki.
Kiongozi huyo wa WARAMI akaongeza
kwamba hivi sasa Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli anayo vita kubwa
kutokana na kazi anayoifanya ya kuwatetea watanzania waliowanyonge anayo
vita ndani ya bunge na nje ya Bunge
Kutokana Na Hoja Ambazo Zimekuwa
Zikitolewa Na Baadhi Ya Wabunge Zikikosoa Utendaji Wa Rais, kuna baadhi
ya watu wamekuwa wakifaidika na baadhi ya mambo hivyo wasingependa
mabadiliko ya kumkomboa mwananchi wa kawaida yatokee, katika picha
kushoto ni Makdeo Makeja mratibu msaidizi WARAMI
Tozo daraja la Nyerere kuanza Jumamosi
(Picha na Raymond Mushumbusi) MAELEZO
……………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali
imetangaza rasmi kuanza kwa tozo kwa vyombo vya usafiri vitakavyopita
katika daraja la Nyerere kuanzia Jumamosi tarehe 14 ,mwezi huu.
Akizungumzia na
waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa
kuanzia siku hiyo , vyombo vyote vya usafiri vitatakiwa kulipia
ushuru wa kupita katika daraja la Nyerere.
“ Tumeanza kutoza
tozo hii mara baada ya kufunguliwa kwa daraja hili na kuanza kutumika
kwa kupita bila kulipa kwa vyombo vya usafiri tangu Aprili 19 mwaka huu
na sasa tunaanza rasmi kutoza tozo kwa ajili ya kukusanya gharama za
usimamizi, utunzaji na uendeshaji wa daraja hili.” alisema Mhandisi
Nyamhanga.
Mhandisi
Nyamhanga amefafanua kwamba watembea kwa miguu watapita bure katika
daraja hilo huku wenye baiskeli wakilipia Sh. 300, pikipiki Sh. 600,
waendesha maguta ,bajaji na magari ya kawaida(Saloon Cars) watatakiwa
kulipia Sh.1500.
Mabasi yanayobeba
abiria 15 yatalipia Sh. 3,000, yale ya abiria zaidi ya 15 Sh. 5,000
na yale yanayobeba abiria zaidi ya 29 yatalipia Sh. 7,000.
Aidha magari
yenye tani zaidi ya mbili mpaka saba yatalipia Sh. 7,000, tani 7 hadi 15
watalipa Sh.10,000, tani 15 mpaka 20 watalipa Sh.15,000 na yale yenye
tani 20 mpaka 30 yatalipia Sh. 20,000.
Mhandisi
Nyamhanga ameongeza kuwa magari yenye namba za Jeshi la Wananchi(JWTZ),
Jeshi la Polisi(PT), Jeshi la Magereza(MT), gari za wagonjwa, magari ya
zimamoto na magari yenye vibali maalum yataruhusiwa kupita bure
















No comments :
Post a Comment