Tuesday, April 19, 2016

Zantel Yakabidhi Computer 21 Kwa Vyuo vya Walimu Zanzibar.

Afisa Mtendaji wa Millcom Africa Bi Cynthia Gordon akimkabidhi Computer Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma, anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Zanzibar  
Afisa Mtendaji wa Millcom Africa Bi Cynthia Gordon akimkabidhi Computer Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma, anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin, Afisa wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha na kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi Khadija Juma Bakari,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Zanzibar  
Maofisa wa Zantel wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhi Computer Vyuo vya Walimu Zanzibar.
Maofisa wa Zantel wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhi Computer Vyuo vya Walimu Zanzibar.
Afisa wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akitowa maelezo wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Computer Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa ajili ya matumizi ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel Tanzania Benoit Janin akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Computer kwa ajili ya Matumizi ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Hyatt Shangani Zanzibar. Na kusema lengo la Zantel ni kushirikiana na Serikali kwa lengo la kukuza na kuboresha elimu ya teknolojia na mawasiliano kusaidia vyuo vya Ualimu vinavyotoa Mafunzo hayoili kuongeza ufanisi
katika ufundidishaji wao..
Afisa Mtendaji wa Millcom Africa, Bi Cynthia Gordon, akizungumza wakati wa hafla hiyo na kusema Walimu ndio msingi wa maendeleo kwenye Taifa na ndio maana Zantel imewapa kipaumbele katika miradi yake ya Kijamii. na Kusema Zantel Daima imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha tunaboresha sekta elimu kwa wazanzibari na kama tunavyojua elimu ya teknolojia na mawasiliano ni muhumu kwa dunia ya sasa. 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Computer na Kampuni ya Simu ya Zantel kwa ajili ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hotel ya Hyatt Shangani Zanzibar, na kuipongeza kampuni hiyo kwa jitihada zake inayofanya kwa kushirikiana na serikali katika kukuza na kuboresha elimu visiwani Zanzibar.
‘Ili kutoa elimu bora kwa walimu wa teknolojia ya mawasiliano wa ngazi zote ni muhimu kuhakikisha mafunzo ya komputa yanajumuishwa kwenye mtaala wa vyuo vya elimu ili kuwajengea uwezo walimu katika kufundisha wanafunzi’ 
Maofisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya makabidhiano ya Computer kwa ajili ya matumizi ya Vyuo vya Walimu Zanzibar.
Mkuu wa Vyo vya Ualimu Zanzibar Maulid Omar Hamad akitowa neno la shukrani kwa Uongozi wa Zantel Tanzania kwa msaada wao wa Computer 21 kwa ajili ya matumizi ya Vyo hivyo katika kutowa mafunzo kwa Walimu hao.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma Afisa wMtendaji Mkuu wa Zantel Benoit Janin.wakifuatilia hafla hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Vyuo vya Walimu akitowa shukrani. 
Viongozi wa meza kuu wakimsikiliza Mkuu wa Vyuo vya Walimu Zanzibar Maulid Omar Hamad, akitowa shukrani kwa niaba ya Vyuo hivyo wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Computer na Kampuni ya Simu za Mkoni Zantel hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Zanzibar. 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma, Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar Bi Khadija Juma Bakari kushoto Afisa Mtendaji wa Millcom Bi Cynthia Gordon na Afisa wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Zantel na Wizara ya Elimu Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amaali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akibadilisha mawazo na Mtendaji Mkuu wa Zantel Benoit Janin na Mtendaji wa Millicom Bi. Cynthia Gordon, baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi Computer kwa ajili ya Matumizi ya Vyuo vya Walimu Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akitowa shukrani kwa Kampuni ya Zantel kwa msaada wao wa Computer kusaidia matumizi katika Vyuo vya Walimu Zanzibar. wakati akizungumza na waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Zanzibar.  
Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya hafla ya kukabidhi Computer 21 kwa ajili ya matumizi ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar.
Imetayarishwa na othmanMapara.Blogspot.com.
Zanzinews.com.

SERENGETI BOYS KUJIPIMA NA MAREKANI, KOREA KUSINI

Timu ya taifa ya Tanzania vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inatarajiwa kushiriki mashindano maalumu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini India, yatakayozishirikisha nchi za Marekani, Malasyia na Korea Kusini na wenyeji mapema mwezi Mei, 2016.
Chama cha Soka nchini India (AIFF) kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.
umla ya nchi tano zitashiriki mashindano hayo yatakayofanyika katika mji wa Goa kuanzia Mei 15-25, 2016 ambapo michezo itachezwa kwa mfumo wa ligi kwa kila timu kucheza michezo minne, kabla ya mchezo wa mwisho wa fainali wa kumpata Bingwa wa mashiandano hayo.
Serengeti Boys ambayo imeshacheza michezo mitatu ya kirafiki ya kimataifa mpaka sasa, mmoja dhidi ya Burundi na miwili dhidi ya timu ya vijana wa Misri (The Pharaohs) inatarajiwa kuingia kambini mwishoni mwa mwezi Aprili, 2016 katika hosteli za TFF zilizopo Karume kujiandaa kwa safari ya kuelekea nchini India kushiriki michuano hiyo.
Kikosi cha Serengeti Boys kinachonolewa na kocha Bakari Shime, akisaidiwa na Sebastian Mkomwa chini ya mshauri wa ufundi wa timu za vijana Kim Poulsen, kinatarajiwa kuwa kambini kwa muda wa wiki mbili kabla ya safari kuelekea Goa India kushirki mashindano hayo.
Kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo maalumu ya vijana kimataifa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Serengeti Boys, kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijanaa barani Afrika dhidi ya Shelisheli Juni 25 – 2 Julai, 2016.

TIMU YA UCHUKUZI YAENDELEA NA MAZOEZI

k1
Dr. Hawa Senkondo (mbele) akikiongoza kikosi cha wanawake cha kuvuta kamba cha Uchukuzi SC katika mazoezi. Wengine ni Germana Vicent, Janeth Komba na Tatu Cosmas.
k2Kocha Abuno Issa (kustoto) akitoa maelekezo kwa timu ya wanawake ya Uchukuzi SC.
k3Kocha Abuno Issa (kulia) akitoa maelekezo kwa timu ya wanaume ya Uchukuzi SC.
k4
  1. Kocha Abuno Issa (kulia) akielekeza timu ya wanawake ya Uchukuzi SC jinsi ya kuvuta kamba, wakati kushoto haonekani vizuri katika picha ni Nagalali Mollel.
k5Nicas Luanda akiongoza timu ya wanaume ya Uchukuzi SC kuvuta kamba katika mazoezi.
k6Timu ya wanawake ya Uchukuzi SC wakishangilia baada ya kuwavuta wanaume katika mazoezi.
k7
:  Sharifa Mustafa (mwenye mpira) akiangalia wa kumrushia wakati (katikati) Mayasa Hamidu  akitazama.

SERIKALI KUCHUNGUZA MKATABA WA JENGO LA MACHINGA COMPLEX

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda (kulia), akikagua vizimba katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, baada ya kufanyika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kilichoketi jana kujadili uendeshaji wa biashara wa katika jengo hilo pamoja na kamati ya mkoa iliyoundwa kuchunguza mkataba wa jengo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, kuhusu uendeshaji wa jengo hilo.
 Makonda akiwasili katika viwanja vya Jengo la Machinga Complex kuzungumza na wafanyabiashara na wadau wengine. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wengine ni viongozi wa jengo hilo.
Makonda akiangalia Uwanja wa Karume akiwa jengo la Machinga Complex.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro akimuaga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi.
………………………………………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kufanyika kwa uchunguzi katika ujenzi wa jengo la Machinga Ciomplex ili kubaini uhalali wa mkataba uliotumika kujenga jengo hilo.
 
Aidha, amebainisha kuwa jengo la Machinga Complex kwa sasa linadaiwa zaidi ya Sh bilioni 36 kiasi ambacho ni mara tatu ya thamani halisi ya jengo hilo ambayo ni Sh 12 ambazo zinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara wa jengo hilo.
 
Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam  jana wakati alipotembelea jengo hilo lililopo Manispaa ya Ilala ili kujionea mazingira ya kufanyia biashara. Alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itaanza kufanya uchambuzi wa mikataba ili kupata uhalali wa gharama na kujua kiwango kinachostahili kulipwa na wafanyabiashara hao.
 
Alisema kamati hiyo ya ulinzi na usalama imekubali kutengeza kamati ndogo itakayoanza kazi leo ya kuchambua na kuanza mikataba.
 
“Ingekuwa vyema tungekuwa na mkutano wa kuwasikilizeni na kujua kero zenu, lakini tunayo sababu moja ya msingi ya kutowasikiliza , kwanza tunatafuta uhalali na utaratibu wa jengo hili lilivyojengwa.
 
Katika maelezo ya awali tuliyoyapata jengo hili uko mkanganyiko mkubwa,  inawezekana ni miongoni mwa mradi mkubwa uliofanyiwa ufisadi Tanzania, sasa hatuwezi kukaa kusikiliza habari ya kizimba change, kwanza tupate uhalali wa mkataba uliopelekea kujenga jengo hili,” alisema Makonda.
 
Alisema kamati ya wafanyabiashara wa soko hilo itakayoundwa chini ya usimamizi wake itaanza kazi ya kuchunguza ili kubaini uhalali wa mkataba na kujua kama waliongia mikataba hiyo walikuwa sahihi.
 
Makonda alitoa rai kwa wafanyabiashara kuwa rai ya Rais Magufuli ni kuwapigania wanyonge na kuhakikish awanatoka sehemu moja kwenda nyingine, hivyo wasaidiza wake kwa kupenda au kutokupenda wana jukumu la kuhakikisha wanafanikisha hilo.
 
Hivi karibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene aliifuta bodi inayosimamia jengo hilo na kumsimamisha kazi meneja anayesimamia jengo hilo na kumtaka kwenda katika ofisi za jiji kwa ajili ya kumpangia kazi nyingine.
Katika hatua nyingine, Simbachawene alilikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabiashara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara hao.
Katika mkutano wake na Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Simbachawene alisema, jengo hilo limekuwa likitumiwa kinyume na lengo ambalo walitakiwa wafanyabiashara kulitumia kwa gharama kidogo lakini limekuwa likitumiwa na watu wengine tofauti na wafanyabiashara jambo ambalo limesababisha kushindwa kulipa deni linalodaiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

UFAFANUZI JUU YA UVUMI KUHUSU HALI YA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII (NSSF)

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zisizo rasmi kuhusu hali na mwenendo wa
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikieleza
kwamba mali za Mfuko huo zimetumiwa vibaya na hivyo kuathiri mafao kwa wanachama.
Taarifa hizi zimesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wa NSSF na wadau
wa Sekta ya Hifadhi ya jamii kwa ujumla kwa kuhofia usalama wa wa fedha na mafao yao. 


Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kuwaondoa
hofu wanachama wote wa Mfuko wa NSSF na Wananchi kwa ujumla na kuwahakikishi
kwamba Mfuko wa NSSF upo katika hali nzuri kifedha na unaendelea kulipa mafao ya
wanachama kama kawaida. Kama mnavyofahamu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
alikwishateuliwa na anaendelea na majukumu ya kusimamia shughuli zote za Mfuko. Vilevile,
taratibu za kupata Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko huo zipo katika hatua za mwisho. 
Aidha, SSRA kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa mamlaka waliyopewa chini ya
Kifungu cha 6(2) (c) cha Sheria Na.8 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na kifungu cha 40 na
cha 48 wanaendelea kufanya kaguzi za Mifuko yote ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa lengo la
kuhakikisha kwamba muda wote Mifuko yote inakuwa katika hali nzuri kwa maslahi ya
wanachama na taifa kwa ujumla. 


Mwisho, Mamlaka inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama walioathirika na taarifa hizi
pamoja na wanachama wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuwahakikishia kwamba fedha
na mafao yao yapo salama na Mamlaka inazifanyia kazi kero zao kwa bidii kubwa.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam.

No comments :

Post a Comment