Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
na Misitu wa Serikali ya Czech Republic Bw. Dusan Benza akizungumza
katika kongamano la wafanyabiashara wa nchi hiyo na watanzania
lililofanyika leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Mawaziri wawili Kilimo na
Viwanda wa Jamhuri ya Jamhuri ya Czech wakiongozana na wafanyabiashara
zaidi ya thelathini wako nchini kwa ajili ya kutafuta na kujionea fursa
za uwekezaji nchini Tanzaniam Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na
Tanzania Investiment Bank (TIB), Ubalozi wa Szech Republic nchini Kenya
na Tanzania House Of Business Company Limited (THB).
Ujumbe huo metembelea wizara ya
Kilimo na wizara ya Viwanda na Biashara na kusaini mikataba ya
ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hapa nchini na nchi ya Szech
Republic ili kuunganisha masuala ya kibiasha na uwekezaji na kuwezesha
wafanyabiashara wa nchi hizi kuwekeza katika masuala ya biashara,
Teknolojia na Kilimo kwa ujumla.
Balozi wa Heshima na Mwakilishi
wa Ubalozi wa Czech Republic hapa nchini John Chaggama akizungumza na
mmoja wa viongozi wa ujumbe huo huku Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa
Czech akisikiliz kwa makini.
Injinia Michal Basovnik wa
kampuni ya Impuls akitoa mada kuhusu shughuli mbalimbali zinazotolewa
na kampuni yao ambayo ina tawi pia nchini Zambia.
Injinia Martin Adamuska wa
kampuni ya NWT kutoka nchini Czech Republic akifafanua jambo wakati
alipokuwa akielezea mambo mbalimbali yanayofanya na kampuni yao lakini
pia fursa mbalimbali zinazoweza kuwekezwa.
Injinia Petr Pawlica wa wa
kampuni ya PAWLICA pia ametoa mada katika kongamano hilo na kuelezea
teknolojia ya kampuni hiyo katika masuala ya Kilimo.

Bw. Godffrey Kirenga wa SAGCOT
CENTER LIMITED akiwaelezea wafanya biashara hao juu ya fursa mbalimbali
zilizopo hapa nchini katika uwekezaji wa kilimo.
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa
Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza
katika kongamano hilo kulia ni John Chaggama Balozi wa Heshima na
Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania.
Kutoka kulia ni Mr Charles
Chandika Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania House Of Business
Company Limited, Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech
Consolate nchini Tanzania, Elipina Makungu na Bahija Salim
wakijadiliana jambo wakati wa kongamano hilo la wafanya biashara.
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa
Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza
na Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate nchini
Tanzania wakimsikiliza mmoja wa maofisa kutoka wizara ya mambo ya nje
wakati akizungumza nao.
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa
Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye na John
Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic
nchini Tanzania wakizungumza na Injinia Vladmir Pikora wa benki ya
Czech Export Bank mara baada ya nusu ya kwanza ya majadiliano kati ya
wafanya biashara wa Tanzania na Szech Republic katika kongamano
lililofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
John Chaggama Balozi wa Heshima
na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ujio wa wafanyabiashara hao.
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa
Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza na
waandishi wa habari juu ya umuhimu wa ujio wa wafanyabiashara hao na
kongamano hilo kwa wafanyabiashara wa Tanzania ya Czech Republic katika
masuala mazima ya kibiashara na uwekezaji.
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka
nchini Czech Republic wakiwa katika kongamano hilo lililofanyika kwenye
hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
Baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania wakihudhuria kongamano hilo.
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali za Tanzania masuala ya biashara na uwekezaji wakiwa katika kongamano hilo.
John Chaggama Balozi wa Heshima
na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania
akimsikiliza Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate
nchini Tanzania.
Elipina Makungu na Bahija Salim
wakifurahia jambo wakati wa kongamano hilo la wafanyabiashara wa Czech
Republic na Tanzania kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
SENDEKA ATINGA SINGIDA KUPITIA HANANG
Msemaji
wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na baadhi
ya viongozi alipowasii Ofisi ya CCM wilaya ya Hanang mkoani Manyara
akiwa njioni kwenda Singida leo
Katibu
wa CCM wilaya ya Hanang, Kajoro Vyohoroka akimpeleka Ofisini, Msemaji
wa CCM Ole Sendeka baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya
Hanang leo akiwa njiani kwenda Singida
Msemaji
wa CCM, Christopher Ole Sendeka akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi
ya CCM wilaya ya Hanang mkoani Manyara. Kulia ni Katibu wa CCM wilaya
hiyo, Kajoro Vyohoroka
Msemaji
wa CCM, Christopher Ole Sendeka akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi
ya CCM wilaya ya Hanang mkoani Manyara. Kulia ni Katibu wa CCM wilaya
hiyo, Kajoro Vyohoroka na kushoto ni Mjumbe wa NEC wa Kigoma, na Ofisa
katika Idara ya Itikadi na Uenezi Makao Makuu ya CCM, Kilumbe Ng’enda
Msemaji
wa CCM, Ole Sendeka akisalimiana kwa bashasha na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Manyara, alipowasili kwenye ofisi ya CCM ya
wilaya hiyo leo
Msemaji
wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akizungumza na viongozi
wa CCM wa Wilaya ya Hanang, alipofika kwenye ofisi hiyo akiwa njiani
kwenda Singida leo
Msemaji
wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na baadhi
ya viongozi wa CCM alipowasili leo, Ofisi ya CCM mkoa wa Singia akiwa
katika ziara ya kikazi
MAKABIDHIANO YA WAZIRI OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa
Haji Ussi (Gavu) akikabidhiana Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini katika
ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi IkuluMjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawazi wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.[Picha na Ikulu.]
Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji
Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wakati wa kukabidhi
Ofisi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.[Picha na Ikulu.]
Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji
Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wakati wa kukabidhi
Ofisi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) (katikati) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.[Picha na Ikulu.]
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa
haji Ussi (Gavu) akitoa nasaha zake kwa Wafanyakazi wakati wa
makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa Waziri ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na
Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini leo katika ukumbi wa Ofisi
ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu
Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali,[Picha na Ikulu.]
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa
Haji Ussi (Gavu) na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na
Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini (katikati) wakiombewa
dua baada ya makabidhiano ya Ofisi katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.[Picha na Ikulu.]
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa
Haji Ussi (Gavu) na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na
Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini (katikati) wakipeana na
Makatibu (kulia) Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Salum Maulid Salum na Katibu wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Haroub Shaibu Mussa kwa kuwatakia Kheri na
mafanikio baada ya makabidhiano ya Ofisi katika ukumbi wa Ofisi ya Rais
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
ZIARA YA SENDEKA BABATI MJINI
Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christipher Ole Sendeka akisalimiana na
Katibu wa CCM wilaya ya Babati mjini, Benard Ghati alipowasili Ofisi ya
CCM wilaya ya Babati mkoani Manyara akiwa katika ziara ya kikazi
Viongozi
wa CCM wilaya ya Babati mkoani Manyara wakiwa tayari kumpokea Msemaji
wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka alipowasili Ofisi ya CCM
wilaya ya Babati
Msemaji
wa CCM, Mjmbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisaini kitabu cha
wageni katika Ofisi ya CCM wilaya ya Babati mkoani Manyara
Katibu
Mwenezi wilaya ya Babati mjini Reginard Sanga akizungumza maneno ya
utangulizi kumkaribisha Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole
Sendeka alipofika katika Ofisi ya Wilaya hiyo
Katibu
wa CCM, Babati Mjini Bernard Ghaty akizungumza, Msemaji wa CCM,
Christopher Ole Sendeka alipofika katika Ofisi ya CCM wilaya ya Babati
mjini mkoani Manyara
Katibu wa CCM mkoa wa Manyara, Ndengaso Ndakubali akimkariisha kuzungumza Msemaji wa CCM, Ole Sendeka.
Mjumbe wa NEC Kigoma, Kilumbe N’genda akizungumza kabla ya Msemaji wa CCM aliyefuatana naye, Ole Sendeka hajazungumza
Msemaji
wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akizungumza na wajumbe
wa Sekretarieti wa CCM Wilaya ya Babati mkoani Manyara
Wahandisi Temesa wapigwa msasa
kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase
Ole Kujan (wa pili kushoto) akipata maelekeo juu ya ufungaji wa moja ya
mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) kutoka kwa Mhandisi Zuhura
Semboji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa wahandisi na
mafundi wa Temesa.
Ole Kujan (wa pili kushoto) akipata maelekeo juu ya ufungaji wa moja ya
mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) kutoka kwa Mhandisi Zuhura
Semboji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa wahandisi na
mafundi wa Temesa.
kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase
Ole Kujan(katikati) akiangalia moja ya kifaa cha kupimia umeme
kinachotumika katika mafunzo kwa wahandisi na mafundi wa Temesa
yaliyofunguliwa leo.
Ole Kujan(katikati) akiangalia moja ya kifaa cha kupimia umeme
kinachotumika katika mafunzo kwa wahandisi na mafundi wa Temesa
yaliyofunguliwa leo.
Mhandisi Amani Mwanga akitoa maelekezo ya namna ya kufunga moja ya
mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya wahandisi na
mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya wahandisi na
mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
Baadhi ya wahandisi kutoka Temesa wakiwa katika harakati za kuchuna
na kuunga nyaja katika moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar)
Katika mafunzo ya wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
na kuunga nyaja katika moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar)
Katika mafunzo ya wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
Fundi Sanifu kutoka Temesa Mganza Juma (Katikati)akiwa makini kufunga
moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya wahandisi
na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya wahandisi
na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
……………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam wanaendesha mafunzo ya wiki mbili kwa Wahandisi na mafundi wa Temesa
ili kuwajengea uwezo katika kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua.
Akifungua mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA
Mhandisi Manase Ole Kujan amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea
uwezo wahandisi na mafundi ili kuweza kutumia teknolojia ya umeme wa
nishati ya jua ambao umekuwa na tija kubwa hasa kwa sehemu ambazo umeme wa
kawaida haujafika.
“Nishati ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana katika
maeneo ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya
wahandisi na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika
Salaam wanaendesha mafunzo ya wiki mbili kwa Wahandisi na mafundi wa Temesa
ili kuwajengea uwezo katika kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua.
Akifungua mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA
Mhandisi Manase Ole Kujan amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea
uwezo wahandisi na mafundi ili kuweza kutumia teknolojia ya umeme wa
nishati ya jua ambao umekuwa na tija kubwa hasa kwa sehemu ambazo umeme wa
kawaida haujafika.
“Nishati ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana katika
maeneo ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya
wahandisi na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika
RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU CHRISTINA LISSU MUGHWAI KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha
Maombolezo kufatia kifo cha Mbunge wa zamani wa Viti Maalum Chadema
Christina Lissu Mughwai aliyefariki Aprili 7 mwaka huu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiaga mwili wa
marehemu Christina Lissu Mughwai aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum
kutoka Chadema katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Mwanasheria
Tundu Lissu (Mb) kufatia kifo cha mdogo wake Christina Lissu Mughwai
aliyefariki Aprili 7 mwaka huu.
PICHA NA IKULU
Wizara YA KILIMO yakanusha kodi ya ng’ombe
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
……………………………………………
Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
imekanusha kodi ya ng’ombe iliyoripotiwa na Umoja wa wafanyabiashara wa
Mifugo na Mazao yake wa Wilaya ya Kinondoni.
Taarifa hii imetolewa na Katibu
Mkuu (Mifugo) wa Wizara hiyo Dkt. Mary Mashingo baada ya kuyaona
malalamiko ya wafanyabiashara hao kwenye baadhi ya vyombo vya habari
nchini.
Katika taarifa hiyo wizara
imekanusha kuwa kodi ya ng’ombe siyo shilingi 18,500 kama ilivyoripotiwa
na wafanyabiashara hao bali ni shilingi 12,000 ambayo inatambulika
kisheria.
“Wizara yetu inapenda kutoa
ufafanuzi juu ya kodi inayotozwa katika machinjio ya Kimara kama
ifuatavyo: ushuru wa soko shilingi 5000, ushuru wa kusafirisha mifugo
shilingi 1500, ushuru wa ukaguzi wa wanyama shilingi 2500 pamoja na
gharama za machinjio shilingi 3000 kwa kila kichwa cha ng’ombe ambapo
jumla yake ni shilingi 12,000”alisema Dkt.Mashingo.
Aidha,taarifa hiyo imeelezea
kuhusu kupitisha ng’ombe katika soko la upili la Pugu kabla ya
kuwapeleka katika machinjio ya Kimara kuwa ni kwa ajili ya kuwafanyia
vipimo vya afya ng’ombe hao kabla ya kuchinjwa pamoja na kulipia tozo ya
Serikali.
Taarifa hiyo pia imefafanua baadhi
ya sababu za kufungwa kwa machinjio ya Kimara tangu Aprili 9 mwaka huu
zikiwemo za baadhi ya wafanyabiashara kupeleka ng’ombe katika machinjio
hayo moja kwa moja bila kupitia Pugu ambalo ni kosa kisheria pamoja na
uchafu uliokithiri katika machinjio hayo.
Katika kufanya juhudi za kupambana
na matatizo haya,Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inajipanga kukutana
na wafanyabiashara wa mifugo na mazao yake ili kuwaelimisha zaidi
kuhusu Sheria, Kanuni, na Taratibu zinazopaswa kufuatwa katika ufanyaji
wa biashara hii.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KONGAMANO LA WANAWAKE KATIKA UONGOZI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake waliohudhuria
Kongamano la Wanawake katika Uongozi linalojadili kuendeleza Mazingira
kuwezesha kuinua Wanawake ambao bado hawajapata fursa kufikia nafasi za
Uongozi. Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi limefanyika
leo April 12, 2016 katika ukumbi wa Mwalim Nyerere.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Waandishi wa Vyombo vya Habari baada ya kuzindua
Kongamano la Wanawake katika Uongozi linalojadili kuendeleza Mazingira
kuwezesha kuinua Wanawake ambao bado hawajapata fursa kufikia nafasi za
Uongozi. Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi limefanyika
leo April 12, 2016 katika ukumbi wa Mwalim Nyerere.
(Picha na OMR)
FAO JIPYA LA WOTE SCHEME LA PPF LITASAIDIA KUKUZA UCHUMI WA WATANZANIA
Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa akizungumza wakati wa semina hiyo.
Fao jipya la Wote Scheme ambalo ni mfumo wa hiari kwa wanachama ulioanzishwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF utasaidia kuwapa fursa watanzania waliopo kwenye sekta isiyo rasmi kukidhi mahitaji na kutambua mchango na ushiriki wa sekta hizo katika kukuza uchumi.
Fao hilo pia linatoa fursa kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta iliyo rasmi kuwawezesha kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa alisema hayo juzi wakati semina kwa askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Zimamoto mkoani Tanga uliokuwa na lengo la kuwapa uelewa juu ya mafao yanayopatikana kupitia mfuko huo.
![]() |
| Washiriki wa semina hiyo Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa |
Alisema kupitia fao hilo
mwanachama
anafaidika na huduma za Afya ikiwemo kupata kadi ya Afya mahali popote kwa
kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) mwaka
mzima bure.
mwanachama
anafaidika na huduma za Afya ikiwemo kupata kadi ya Afya mahali popote kwa
kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) mwaka
mzima bure.
Aidha alisema kupitia skimu hiyo mpya ya mfuko huo unachangia na kuwapa uelewa watanzania utamaduni wa kujiwekea
akiba ya baadae ili kuweza kukabiliana na ugumu wa maisha wakati
wanapokuwa wakifikia
umri wa kustaafu.
akiba ya baadae ili kuweza kukabiliana na ugumu wa maisha wakati
wanapokuwa wakifikia
umri wa kustaafu.
“Lakini pia sisi kama PPF
tunarahisisha
uchangiaji kupitia mitandao yote ya simu kwani hii imesaidia kuweza kuepusha
changamoto mbalimbali ambazo wanaweza wakukumbana nazo wanachama wetu ambao
wamejiunga ma Mfuko huu “Alisema.
tunarahisisha
uchangiaji kupitia mitandao yote ya simu kwani hii imesaidia kuweza kuepusha
changamoto mbalimbali ambazo wanaweza wakukumbana nazo wanachama wetu ambao
wamejiunga ma Mfuko huu “Alisema.
Hata hivyo alisema kuwa
wanaendelea
kutoa mikopo ya elimu na biashara ili kuweza kuwainua wanachama wao kiuchumi
sambamba na kujiendeleza kielimu ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha
na utandawazi.
wanaendelea
kutoa mikopo ya elimu na biashara ili kuweza kuwainua wanachama wao kiuchumi
sambamba na kujiendeleza kielimu ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha
na utandawazi.

“Fao hili lilianzishwa mwezi wa saba mwaka jana ambapo mwanachama
anafaidika na huduma za afya (Kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini
– NHIF),mikopo mbalimbali
na Fao la Uzeeni(Pensheni) “Alisema Meneja huyo.
Semina hiyo ililenga kuwapa
uelewa wa mambo mbalimbali kuhusu mfuko
huo ikiwemo uandikishaji wanachama,mafao yatolewayo na mfuko huo,Wote
Scheme (mfumo
wa Hiari),Mikopo ya Saccos na Fao la Elimu.
uelewa wa mambo mbalimbali kuhusu mfuko
huo ikiwemo uandikishaji wanachama,mafao yatolewayo na mfuko huo,Wote
Scheme (mfumo
wa Hiari),Mikopo ya Saccos na Fao la Elimu.
Picha na Stori kwa Hisani ya blog ya Kijamii ya Tanga Raha
Waziri Makamba akutana na Ujumbe wa Kamati ya Fedha ya Bunge la Finland
………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba hii leo amekutana na
kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Kamati ya Fedha ya Bunge la Finland.
Katika mazungumzo yao
yaliyofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli Dar es Salaam,
wabunge hao wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada inazofanya za
kulinda na kuhifadhi mazingira.
Awali, akiwakaribisha wabunge hao
Waziri Makamba amesema Tanzania inajivunia uhusiano mzuri uliopo baina
ya Tanzania na Finland na kuwashukuru wabunge hao kwa kufanya ziara
hiyo ya kikazi nchini Tanzania.
Waziri Makamba amesema Serikali ya
awamu ya Tano imejikita zaidi katika kuimarisha Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira ikiwa ni pamoja na kuandaa Mkakati Mkubwa wa Kitaifa wa
kupanda miti nchi nzima hususan maeneo kame ili kunusuru nchi na athari
za mabadiliko ya Tabianchi.
“Hivi sasa tuko katika hatua za
kuainisha maeneo yatakayopandwa miti hiyo kwa kuangalia aina za udongo
na miti itakayoweza kuhimili katika maeneo husika” Alisisitiza Makamba.
Waziri Makamba ameiomba Serikali
ya Finland kuendelea kushirikiana zaidi na Serikali ya Tanzania ili
kufikia malengo endelevu ya Uchumi na maendeleo ya Viwanda bila kuathiri
Mazingira.
Naye Balozi wa Finland Nchini
Tanzania Bw Mart Akhtsary aliyeambatana na ujumbe wa wabunge kutoka
Finland amemhakikishia Waziri Makamba kuendeleza na kudumisha
ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
WASHTAKIWA WA TUMBILI WASOTEA DHAMANA.
Baadhi ya Washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi ya usafirishaji wa
wanyama Hai 61 aina ya Tumbili wakiongozwa na asakari Polisi walipokuwa
wakiwasili katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Moshi.
Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi ,Artem
Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakisindikizwa na askari Polisi
kuingia mahakamani,Nyuma yao ni mshtakiwa mwingine Idd Misanya
wanyama Hai 61 aina ya Tumbili wakiongozwa na asakari Polisi walipokuwa
wakiwasili katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Moshi.
Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakisindikizwa na askari Polisi
kuingia mahakamani,Nyuma yao ni mshtakiwa mwingine Idd Misanya
Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakiwa katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Moshi ,kulia ni aliyekua Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt Charles Mulokozi.
mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, kutoka kulia ni Eduard Vardanyan ,ArtemVardanian na Idd Misanya.
mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, wakizungumza jambo na wakili
Majura Magafu anyewatetea katika shauri hilo.kutoka kulia aliyeshika
nondo ni aliyekua Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Wanamapori Dkt Charles
Mulokozi, mfanyabiashara raia wa Uholanzi Artem Vardanian na ndugu yake
Eduard Vadanyan.
KAMPUNI YA TRICSTER YAANDAA SHINDANO LA WAZO LA BIASHARA
………………………….
Kampuni ya Kijapani inayofanya
shughuli zake nchini (Tricster) imeandaa shindano la wazo la biashara
litakalozishirikisha nchi tano za Afrika zikiwemo
Kenya,Rwanda,Zambia,Zimbabwe na Tanzania mwenyeji wa mashindano hayo
kwa mwaka 2016.
Akiongea na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam Meneja Mradi kutoka kampuni ya Afrika New
Business Development Department(DMM) Bw.Alex Kapungu ambao ndio
wadhamini wa shindano hilo ameeleza kuwa lengo la shindano hilo ni
kusaidia kuboresha ujasiriamali katika bara la Afrika.
“Shindano hili linafanyika kwa
mara ya kwanza na hivyo ni fursa nzuri kwa wajasiriamali na wale
wanaotaka kuwa wajasiriamali kushiriki na baadaye kufanikisha wazo hilo
kiutendaji kwa kuwa biashara halisi”alisema Bw.Alex.
Aidha ameongeza kuwa vigezo vya
kushiriki shindano hilo ni mshiriki awe amefikisha miaka 18 na
kuendelea, awe anajua kuongea na kuandika lugha ya kiingereza na kuwa na
hati ya kusafiria.
Naye Mkurugenzi wa Trickster
Bw.Sonobe Atsushi amesema washindi watakaoingia nusu fainali watapata
fursa ya kutembelea nchi ya japani ambapo mshindi wa kwanza atapata
fedha taslimu Dola elfu tano za kimarekani.
Pia ametoa wito kwa watanzania
kujitokeza na kushiriki kwa wingi ili wapate fursa ya kuanzisha biashara
kupitia mawazo watakayoyatoa na hivyo kupanua wigo wa biashara.
fastjet yashinda kwenye Tuzo Za Usafiri Duniani
TAARIFA KWA NYOMBO VYA HABARI
…………………………………
Dar es Salaam – 11 April 2016 –fastjet,
shirika la ndege la gharama nafuu barani Afrika imeshinda Tuzo ya
Shirika la Ndege Linaloongoza Afrika kwa Gharama Nafuu kwenye Tuzo
ya 23 ya Mwaka ya Usafiri Duniani iliyotolewa Zanzibar,
Tanzania Aprili 9, 2016.
Tuzo
ya Usafiri ambayo inatambulika duniani imepangwa kwa kutambua,
kutuza na kusherehekea mafanikio kwenye sekta zote muhimu za
usafirishaji wa kwenye sekta ya utalii.
Tuzo
ya Shirika la Ndege Linaloongoza kwa Gharama Nafuu ambayo hutolewa kwa
wataalamu wa usafiri na utalii pamoja an watumiaji duniani
kote inatokana na kutambua huduma za fastjet za kufanya watu wamuumudu
usafiri wa anga, usalama na kuaminika kwenye mtandao yote barani
Afrika.
“Kutambuliwa
na kupata tuzo hii sio tu kunaonesha kujituma kwa ufanisi kwenye
usafiri wa anga, lakini kunaonesha matokeo ya juhudi zetu tunazojaribu
kulifanyia bara la Afrika,” alisema Meneja Mkuu wa fastjet
Tanzania, John Corse na kuongeza, “tunajivunia sana kupokea
kutambuliwa huko na sekta hii kubwa na fastjet itaendelea kuufanya
usafiri wa anga kuwa wa gharama za chini ambazo watu wengi
watazimudu barani Afrika.”
Shirika
hilo la ndege la bei nafuu lilizinduliwa Novemba 2012 na linafanya
safari kadhaa za ndani ya Tanzania kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya,
Mwanza na Kilimanjaro. Kukua kwa mtandao wa fastjet pia kunatoa
huduma kwa njia ya kutoka Dar es Salaam na Zanzibar na kwenye vituo vya
kimataifa kama vile Johannesburg, Harare, Victoria falls, Entebbe,
Nairobi na Lusaka.
Fastjet
inatarajia abiria wake wengi kwenye njia hizo inakotoa huduma kuwa
ndio wanasafiri kwa mara ya kwanza kwa kutumia ndege kutokana na sababu
ya kukwazwa na tozo za nauli ya juu ambazo awali hawakumudu kulipa
kwa ajili ya usafiri huo.
Huduma
hii ya nauli nafuu imeungwa mkono kwenye utafiti uliofanywa na shirika
hilo hivi karibuni, unaoonesha kuwa asilimia 40 ya abiria kwenye njia
zote walikuwa ndio mara yao ya kwanza kusafiri kiumudu kusafiri kwa
ndege kwa mara ya kwanza hivyo pongezi ziende kwa gharama nafuu za
fastjet.
Jambo
jingine ambalo linapatikana kwenye njia inamopita fastjet ni
kuboreshwa kwa mbadala wa mzigo ambako kunajulikana kama ‘freighty’
kunakoruhusu abiria kusafirisha hadi kilo 80 zilizofungwa kwenye
mabegi kwa gharama ya shillingi 88,000. Mbadala huo wa kusafirisha
mizigo kimsingi umekuwa ni maarufu kwa wafanya biashara wanaosafiri na
fastjet kwenda kununua bidhaa za jumla kimataifa na kuzisafirisha kwa
ajili ya kuziuza kwenye masoko ya nyumbani mwao.
Tuzo
hii inaongeza idadi ya tuzo ambazo fastjet
imeshazipata zikiwemo kushinda Tuzo ya Ubunifu kwenye Usafiri kwenye
utoaji wa nane wa tuzo hiyo mwaka 2015, na hali kadhalika kutangazwa
kuwa shirika la ghama nafuu barani Afrika katika
kulinganishwa mengine kwenye usafiri wa anga kupitia mtandao wa
safiri WhichAirline.com in 2016.
Waandishi wa habari waaswa kujiendeleza kuelimu
Na Beatrice Lyimo – MAELEZO
…………………………………………
Waandishi wa habari waaswa
kujiendeleza kielimu katika fani ya uandishi wa habari na taaluma
nyingine ili waweze kukabiliana na kutatua changamoto mbalimbali
zinazoikabili jamii.
Wito huo umetolewa leo jijini
Dar es Salaam na Mhadhiri Chuo Kikuu Huria Dr. Hamza Kondo alipokuwa
akizindua kitabu chake kiitwacho Watchdog Journalism in Tanzania a
Sustainable Struggle ambapo kwa Kiswahili ni “Uandishi Habari Huru
Tanzania ni mapambano endelevu”.
Dr Kondo amesema lengo la kitabu
hicho ni kuwaelimisha na kuwaasa waandishi wa habari na wataaluma ya
habari kuzidi kuithamini taaluma hiyo licha ya changamoto
zinazowakabili.
Amesema kitabu hicho
kinazungumzia uhalisia wa uhuru wa habari nchini, hivyo kinafaa
kufundishia taaluma ya habari katika vyuo vikuu na vyuo vya kati nchini.
Aidha, Mhadhiri huyo ameongeza
kuwa ili fani ya taaluma ya habari iheshimike ni lazima iwe na bodi ya
wataalamu waliobobea ambayo itaundwa na wasomi wa taaluma husika ili
kusimamia maadili ya taaluma hiyo na kuchukua hatua kwa wanataaluma
watakaokiuka maadili.
Mbali na hayo Dr Kondo ametoa
zawadi ya vitabu kwa baadhi ya vyombo vya habari nchini likiwemo gazeti
la Jamuhuri, gazeti la majira, gazeti la Habari Leo, gazeti la Mwananchi
na gazeti la Nipashe.
LANCET TANZANIA LIMITED YAFUNGUA MAABARA YA KISASA MJINI MOSHI.
Maabara
ya kisasa ya Lancet iliyofunguliwa mjini Moshi jirani na YMCA kwa
ajili ya kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya
Saratani.
Mtafiti
wa Magonjwa,Dkt Hemed Kalebu akimuonesha Kaimu mganga mkuu wa mkoa ,Dkt
Japhet Boniface ,maeneo mbalimbali alipotembelea maabara hiyo
iliyofunguliwa mjini Moshi.
Dkt
Kalebu akileza jambo kwa kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt
Josephat Boniface katika eneo ambalo hutumika kumpokea mgonjwa anayefika
kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Dkt Kalebu akionesha sehemu ya vifaa mbalimbali katika maabara hiyo ambavyo vimekuwa vikitumika kwa ajili ya kufanya vipimo.
Baadhi
ya vifaa mbalimbali vilivyoko katika maabara hiyo ya kisasa
iliyofunguliwa mjini Moshi itakayotumika kufanya vipimo vya magonjwa
mbalimbali ambayo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakivifuata nje ya nchi.
Kaimu
Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Josephat Boniface akiwa katika
picha ya pamoja na Dkt Hemed Kalebu pamoja na watumishi wengine wa
maabara hiyo .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
TANZANIA OMAN BUSINESS FORUM TO BE HELD ON 13TH APRIL, 2016 AT HYATT REGENCY KILIMANJARO HOTEL, DAR ES SALAAM
On
the occasion of the state visit by the Minister for Industry and Trade
of Oman Dr. Ali Masoud Al Sunaid, the Ministry of Foreign Affairs
Regional and International Corporation and the Ministry of Industry,
Trade and Investment with corroboration with Tanzania Chambers of
Commerce Industry and Agriculture (TCCIA) are co-organizing a business
forum which will take place on Wednesday, 13th April, 2016 starting from 9:00 AM at Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel.
The objective of the forum is to
create a convenient platform for Tanzanian business community to meet,
share experiences and establish business relations with the Oman
business community. The forum will be graced by Her Excellence Samia
Suluhu Hassan the Vice President of United Republic of Tanzania and Dr.
Ali Masoud Al Sunaid Minister for Industry and Trade of Oman.
The Forum will also provide the
opportunity for business to business (B2B) meetings between the Oman
businessmen and their Tanzanian counterparts in various sectors such
as; Banking & Finance, Oil & Gas, Construction & Real
Estates, Posts & Telecommunications, Information Technology,
Electrical & Electronics, Furniture, Tourism, :Agriculture& Agro
Processing, Food & Beverages, Pharmaceuticals, Textiles, Footwear
and General Trading.
As we value your participation in
the growth of trade and investment in Tanzania, we feel honoured to
extend this invitation to you and we hope you will reserve a place to
exchange useful information to participants during the B2B Meetings
Session.
You are kindly requested to
confirm your participation to TCCIA via; Fatma Hamisi (fhamisi@tccia.com
) or to Mr. James W. Kyejo (james.kyejo@mit.go.tz, +255 675 417 813)





















No comments :
Post a Comment