Msafara wa Rais John Pombe Magufuli ukiwasili mtaa wa Samora kwenye tawi la benki ya CRDB la Hilland House jijini Dar es salaam.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipokuwa akiondoka katika tawi hilo.
………………………………………………………………………………………….
RAIS John Magufuli amezua mjadala
baada ya kuvamia tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari namba
T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya “Adamu na Hawa” wala bendera ya
Rais.
Tukio hilo lililochukuwa dakika
25, limetokea majira ya asubuhi jijijni Dar es Salaam katika tawi hilo
ambalo liko katika makutano ya barabara za Ohio na Samora, bila
kutarajiwa.
Mara baada ya Rais Magufuli
kufika katika eneo liliko tawi hilo, makutano ya barabara hizo
yalifungwa ndipo Rais aliposhuka kwenye gari na kuingia ndani ya benki
hiyo.
Wakati akikaribia kuingia ndani
ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki
hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao
waliyokwishaingia.
Aidha, baada ya kuingia ndani
baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa
huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile.
Baadhi ya wananchi walisema hawajaona tukio kama lile kwa Marais wote
waliyopita.
James Charles, ambaye ni dereva
wa taxi, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya
kuona ulinzi unaimarishwa walishituka na mara wakamuona Rais Magufuli
akishuka kwenye gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea
ofisi yake ya zamani.
“Lakini kufumba na kufumbua
tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB, tukajiuliza vipi rais leo
kaamua kuwa kama mteja? Hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa
inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu. Haiwezekani aende akachukue fedha
kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,”alisema
Charles.
Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi
wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema kuja kwake kumewashtua
wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa
ajili ya kutumbua majipu.
“Mimi wakati Rais Magufuli
anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma. Kwa ujumla
kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,” alisema.
Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.
Habibu Day yaadhimishwa wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu
Foundation, Juma Mndeme, mwenye miwani akizungumza jambo baada ya
kumaliza kukabidhi misaada ya mabenchi ya kukalia, sabuni na vinywaji
kwa Kituo cha afya Mwanga, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Aliyeshika majaketi ni Mganga Mkuu Msaidizi wa Kituo hicho Honest Temba
na aliyeshika simu ni Meneja Uhusiano wa Habibu Foundation, Julysiza
Mangiseni.
Habibu Foundation yaadhimisha siku yao kwa kutoa misaada wilayani Mwanga
Habibu Foundation yaadhimisha siku yao kwa kutoa misaada wilayani Mwanga
……………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Mwanga
MAADHIMISHO ya Siku Maalum ya Habibu Day wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro yamefanyika kwa mafanikio kwa kushirikisha matukio mbalimbali yakiwamo ya kutoa misaada katika kituo cha Afya Mwanga, kutoa misaada jeshi la Polisi, pamoja na kufanyika mijadala mbalimbali ya kielimu iliyoendeshwa na wanafunzi wa shule za sekondari wilayani humo.
Katika muda wa mijadala, wanafunzi hao walitumia muda mwingi kuzungumzia mfumo wa kielimu nchini Tanzania sanjari na upangaji wa matokeo ya mitihani kutoka Division na GPA iliyoondolewa rasmi katika mfumo huo nchini hapa, huku mgeni rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyata kilichopo Arusha, Profesa Ward Mavura.

Meneja Uhusiano wa Taasisi
ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu Foundation,
Julysiza Mangiseni, akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo
yaliyoanzia kutoa zawadi mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa Habibu Foundation akizungumza
Mkuu wa Polisi wilayani Mwanga, Pili Mande akipokea sehemu ya zawadi kutoka kwenye Taasisi ya Elimu ya Green Bird
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo cha Green Bird kilichopo wilayani Mwanga
wakielekea kwenye Kituo cha Afya cha Mwanga kwa ajili ya kupeleka zawadi
mbalimbali kama ishar ya kumuenzi muasisi wao marehemu mzee Habibu
Mndeme. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.
Awali ratiba ilianza rasmi saa 12 asubuhi kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Green Bird Girls, Green Bird Boys, Green Bird Collage zinazomilikiwa na taasisi ya Habibu Foundation kutembelea katika maeneo ya Ofisi ya polisi Mwanga na kituo cha afya Mwanga, pamoja na kutoa misaada kama vile mabechi ya kukalia wagonjwa, sabuni, vinywaji pamoja na vifaa ya ofisi kwa jeshi la Polisi Mwanga.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu Foundation,, Juma Habibu Mndeme, alisema kwamba lengo la kufanyika kwa maadhimisho hayo ni kukutanisha pamoja wadau wa elimu wilayani Mwanga sanjari na kumuenzi mwanzilishi wa taasisi yao marehemu Habibu Mndeme aliyefariki Dunia mwaka 2010) na kuacha taasisi hiyo inayomiliki pia shule wilayani Mwanga.
“Tumekuwa tukiadhimisha matukio haya kila mwaka lakini tunaendelea kuboresha hatua kwa hatua, maana lengo la taasisi ni kukuza kiwango cha elimu kwa wilaya ya Mwanga na Tanzania kwa ujumla, ndio maana mijadala ya kielimu ilihusisha wanafunzi mbalimbali kutoka ndani ya Mwanga na nje pia, ikiwamo jijini Arusha.
“Sisi kama waendeshaji wa shule zote za Green Bird tunajivunia kufanyika maadhimisho haya kwa mafanikio makubwa, bila kusahau ulinzi madhubuti kutoka kwenye jeshi la polisi kuanzia asubuhi hadi usiku, huku tukiona ushindani mkubwa, uzoefu na umakini kwa kila aliyeshiriki kuonyesha ujuzi na uwezo wake, hususan katika suala zima la kielimu,” Alisema Mndeme.
Naye Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Profesa Ward Mavura ambaye pia ni Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Jomokenyata cha jijini Arusha, aliitaka jamii ya wilaya Mwanga kuiunga mkono taasisi hiyo kwa ajili ya kuiweka katika mazingira mazuri katika utoaji wa huduma zake.
Akizungumzia tukio hilo na utoaji misaada kwenye jeshi la Polisi wilayani Mwanga, Mkuu wa Polisi Mwanga, Pili Mande, aliishukuru Taasisi ya Habibu kwa kuwekeza katika elimu na kuisaidia jamii kwa mambo mengi, jambo linalotakiwa kuungwa mkono na kuendelezwa kwa manufaa ya Mwanga na Tanzania kwa ujumla.
Naye Meneja Uhusiano wa wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu Foundation,, Julysiza Mengiseni, alisema kwamba kufanyika kwa mafanikio kwa maadhimisho hayo ni hatua nzuri ya kuhakikisha dira ya kuifanya taasisi yao iwe kioo cha elimu wilayani Mwanga na Tanzania kwa ujumla.
“Taasisi inaendelea kutoa elimu bora kwa kuweka miundo mbinu mizuri katika shule zake za sekondari na chuo pia hapa wilayani Mwanga, ambapo kwa pamoja tunasonga mbele kutolkana na ushirikiano mkubwa tunaopata kutoka serikalini na kwa wananchi wote,” Alisema Julysiza.
Kwa mujibu wa Julysiza, elimu inayotolewa kwenye shule zinazomilikiwa na taasisi yao ni bora na imechangia katika uandaaji wa watoto kwa makundi mengi ya kielimu kama vile sekondari na chuo kinachofundisha biashara, elimu na afya.

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AKUTANA NA MAKUNDI MAALUMU,AWAPA MISAADA
![]() |
| Watu wenye ulemavu wa ngozi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Arusha,Ndg Fadhili Nkurlu |
![]() |
| Mwenyekiti wa Chama cha wenye ulemavu wa Ngozi mkoa wa Arusha,John Kivuyo akizungumza katika mkutano huo. |
MABADILIKO YA MUDA WA MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI SIKU YA JUMANNE TAREHE 19 APRILI 2016
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa Daraja la Kigamboni kesho, Jumanne
tarehe 19 Aprili, 2016.
Kutokana na ufunguzi huo, Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataarifu watumiaji barabara na
Wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma ya magari kutumia
daraja hilo itafungwa kwa muda kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 8:00
mchana ili kuwezesha kufanyika kwa sherehe hiyo ya ufunguzi wa daraja.
Aidha, huduma katika Daraja la Kigamboni itarejea kama kawaida kuanzia
saa 8:00.
Daraja la Kigamboni lililoanza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.
Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
18 Aprili, 2016
MKUU WA MKOA WA MWANZA AAGIZA ALIYEDHULUMIWA KIWANJA AREJESHEWE
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John
Mongella ameuagiza uongozi wa Jiji la Mwanza kuhakikisha linakabidhi
kiwanja namba 28-A kilichopo katika eneo la Bugando ifikapo Aprili 25,
2016 kwa mmiliki halali wa kiwanja hicho bwana Justine Eminoga ambacho
amekuwa akikidai kutoka kwa mfanyabiashara wa Jijini humo kwa zaidi ya
miaka sita sasa.
Mongella amefikia hatua hiyo mara
baada yakupokea malalamiko kutoka kwa bwana Justine ambaye alifika
katika Jiji la Mwanza kwa ajili kufatilia suala lake ambalo limedumu kwa
zaidi ya miaka sita sasa. Akitoa malalamiko yake mbele ya mkuu huyo wa
mkoa, bwana Justine alidai kuzulumiwa kiwanja hicho na mfanyabiashara
aliye mtaja kwa jina Shanif Mansour ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Kwimba.
Katika hatua nyingine mkuu huyo
wa mkoa ametoa siku saba kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kuhakikisha
wanakamilisha zoezi la kuhakiki watumishi, ili kubaini endapo kuna
watumishi hewa waliosalia katika zoezi la awali, zoezi la sasa ambalo
linasimamiwa na Ofisi ya katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kwa kamati
maalumu zilizo undwa na mkuu wa Mkoa huo,
Akiwa katika ziara hiyo mkuu huyo
wa mkoa aliagiza kukamatwa kwa Afisa Utumishi msaidizi wa jiji la
Mwanza Henry Sedetale, ambaye alisaidia watumishi hewa watano kuchukua
mikopo ya zaidi ya Mil.90 kutoka katika benki tofauti tofauti, hata
hivyo taarifa kutoka Taasisi yakupambana na kuzuia rushwa mkoani
Mwanza iliyotolewa wakati wa kikao hicho na mkuu wa Takukuru mkoani
humo, ilisema mtuhumiwa huyo tayari alikuwa ametiwa nguvuni na taasisi
hiyo kwa mahojiano zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza yupo
katika ziara kujitambulisha katika mkoa huo na hii ikiwa ni Wilaya yake
ya tatu mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi na Magu hapo awali.
Imetolewa na
Atley J. Kuni
AFISA HABARI NA MAHUSIANO –RS MWANZA. 18 Aprili, 2016

No comments :
Post a Comment