Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli
akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi
rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar
es salaam leo Aprili 19, 2016
OSCAR DE LA HOYA AMPATIA USHAURI BONDIA AMIR KHAN
Bondia Oscar De La Hoya amemshauri
bondia Amir Khan kutumia kasi yake ya kurusha masumbwi ili kumshinda
kirahisi Canelo' Alvarez
Amir Khan amekuwa akijifua vikali
kujiandaa na pambano hilo litakalofanyika Jijini Las Vegas Marekani
mwezi Mei mwaka huu.
Amir Khan akijifua katika kambi yake kujiandaa na pambano
Amir Khan akifanya mazoezi huku akijiangalia kwenye kioo
RAIS MAGUFULI ATUMBUA JIPU LINGINE, AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
ametangaza kumsimamisha kazi kuanzia leo Mkurugenzi wa jiji la Dar es
Salaam, Wilson Kabwe kutokana na kuingia mikataba tata ambayo
imeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 3.
Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo wakati akilizindua daraja la Kigamboni ambalo amependekeza liitwe daraja la Nyerere.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda kuweka hadharani mikataba mibovu iliyoingiwa na Mkurugenzi huyo
Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo wakati akilizindua daraja la Kigamboni ambalo amependekeza liitwe daraja la Nyerere.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda kuweka hadharani mikataba mibovu iliyoingiwa na Mkurugenzi huyo
SERIKALI KUCHUNGUZA MKATABA WA JENGO LA MACHINGA COMPLEX
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda (kulia), akikagua vizimba katika
Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, baada ya kufanyika kikao
cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kilichoketi jana kujadili
uendeshaji wa biashara wa katika jengo hilo pamoja na kamati ya mkoa
iliyoundwa kuchunguza mkataba wa jengo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda akizungumza na
wafanyabiashara katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana,
kuhusu uendeshaji wa jengo hilo.
Makonda akiwasili katika viwanja vya Jengo la Machinga Complex
kuzungumza na wafanyabiashara na wadau wengine. Kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Ilala, Raymond Mushi wengine ni viongozi wa jengo hilo.
Makonda akiangalia Uwanja wa Karume akiwa jengo la Machinga Complex.
UCHUKUZI WAENDELEA KUJIFUA KWA KASI
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF AWATEMBELEA WAATHIRIWA WA MAFURIKO WALIOPO KATIKA KAMBI MAALUM YA SEKONDARI YA NYERERE
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
wananchi waliopata majanga ya kuingiliwa na maji katika nyumba zao
wakati alipotembelea kambi maalum iliowekwa katika Skuli ya Sekondari ya
Nyerere, alipofika kuwafariji na kuwapa pole na mtihani huo.
Baadhi
ya Wananchi wa maeneo ya Nyerere, Kwahani Kwa Wazee na Sebleni wakiwa
katika Kambi maalum ilioandaliwa kwa Wananchi waliopata maafa ya
kuingiliwa na Maji Nyumba zao wakati wa mvua ilionyesha juzi jumapili
katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwafariji Wananchi
waliopata maafa ya mvua katika baadhi ya maeneo ya Visiwa vya Unguja,
Katika Kituo hicho kuna Wananchi zaidi ya mia nne waliopata maafa hayo
wakiishi kwa muda katika kituo hicho.

















No comments :
Post a Comment