Monday, April 25, 2016

PSPF yavuna wanachama Wilaya ya Temeke


 Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live kulia Bi. Joyce Kiria kushoto akionyesha kitambilisho  chake cha uchangiaji wa hiari kutoka kwa Menejawa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa  mfuko wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe kushoto wakati
wa mafunzo kwa wajasiriamali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa  mfuko wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe kushoto akimkabidhi  Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live kulia Bi. Joyce Kiria kitambulisho cha uchangiaji wa hiari katika mafunzo kwa  wajasiriamali yaliyofanyika
jijini Dar es Salaam jana.

Maafisa usafirishaji waaswa kuwa wazalendo

US1

Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan akifungua kikao cha maafisa usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Silivester Simfukwe na kulia ni Mhandisi Elirehema Mmari.
US2
Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Silivester Simfukwe akizungumza na maafisa usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika kikao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan.
US3
Baadhi ya cha maafisa usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakifatilia kikao kati yao na Wakala wa Umeme na Ufundi(TEMESA) kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
( Picha zote na Theresia Mwami-TEMESA)
……………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Maafisa usafirishaji kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali wameaswa kuwa wazalendo kwa kufuata kanuni na utaratibu wa matengenezo na shughuli za kiufundi Serikalini.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na  Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan alipokuwa akifungua kikao cha maafisa usafirishaji kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali kujadili changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali.
Kaimu Mtendaji Mkuu huyo amesema kwa hali ilivyo sasa imebainika kuwa Sheria na Kanuni za matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali imekuwa ikikiukwa kwa kiasi kikubwa na hivyo kuilazimu mamlaka husika kutafuta njia mbadala ili kukabiliana na changamoto hiyo.
“Lengo letu ni kupata namna bora ya kutoa huduma ya matengenezo ya kiufundi ya vifaa vya Serikali pasipo kukiuka Sheria na Kanuni zilizowekwa hivyo basi tunaomba ushirikiano kutoka kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali  kuleta magari na vifaa kwetu ili tutekeleze wajibu wetu” alisema Mhandisi Manase.
Mhandisi Manase ameongeza kuwa pamoja na uchache wa Wizara , Idara na Taasisi  za Serikali zinazotekeleza Sheria na Kanuni za matengenezo ya magari ya Serikali kwa kuleta magari TEMESA ila kumekuwa na changamoto katika ulipaji wa gharama za matengenezo hali inayosababisha Wakala usiweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka TEMESA Mhandisi Sylivester Simfukwe amesema Wizara , Idara na Taasisi  za Serikali zinatakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo kwa kupeleka na kulipa gharama za matengenezo ya magari na vifaa vya Serikali kwani Wakala huu ndio mshauri mkuu wa Serikali katika masuala ya kiufundi na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kuongezeka kwa mapato ya Serikali.
Naye Meneja Usafirishaji kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Jonathan Mhagama ameiomba Serikali kuiongezea uwezo TEMESA kwa kuwa na karakana za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambapo kwa sasa uwezo walionao wakala huo ni mdogo ukilinganisha na magari yaliyopo Serikalini.
Mkutano kati ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na maafisa usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za serikali umekuja mara baada ya kauli kutoka kwa  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof  Makame Mbarawa ya kuyataka magari yote ya Serikali kutekeleza Sheria na Kanuni za matengenzo ya vifaa vya Serikali.

Timu nne zatinga nusu fainali katika Mei Mosi

OLI1
Kikosi cha Tamisemi kilichoingia nusu fainali katika michezo ya Mei Mosi.
OLI2
Kikosi cha Uchukuzi SC kilichotinga nusu fainali kwenye michezo ya nusu fainali.
OLI3
Kiungo wa Ukaguzi, Mansour Juma (17) akikokota mpira mbele ya Seleman Kaitaba wa Uchukuzi SC katika mchezo wa soka katika mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma. Uchukuzi SC walishinda 3-1.
OLI4
Kipa wa GGM Emmanuel Charles (mwenye jezi nyeusi) akijiandaa kudaka mpira wa kona uliochongwa na Omar Said ‘Chidi’ wa Uchukuzi (hayupo pichani). Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
…………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU nne za soka zimeingia hatua ya nusu fainali kwenye mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye atika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Timu hizo ni Tamisemi na Tanesco zilizotoka kundi A, wakati za kundi B ni Uchukuzi SC na Geita Gold Mine (GGM).
Nusu fainali hiyo itafanyika keshokutwa kwa kumshindanisha mshindi wa kwanza wa kundi A na mshindi wa pili wa kundi B kwa mechi ya saa 8:00 mchana na mechi ya saa 10:00 mshindi wa kundi B ataumana na mshindi wa pili wa kundi A.
Timu zilizoishia kwenye hatua ya makundi ni TPDC, CWT na UDOM za kundi A na za kundi B ni Ukaguzi, CDA na Mambo ya Ndani.
Kwa upande wa netiboli inayochezwa kwa mtindo wa ligi,  timu ya Tamisemi inaongoza kwa kuwa na pointi sita sawa na Uchukuzi SC, lakini wanamagoli mengi ya kufunga ambayo ni 76 wakati wenzao wanayo 54, wakifuatiwa na CDA yenye pointi tatu, huku Tanesco na TPDC wakiwa hawana kitu.
Katika michezo ya awali ya kuvuta kamba timu ya wanawake ya Uchukuzi SC ilipata ushindi wa chee dhidi ya UDOM, ambao hawakutokea uwanjani, pia Tanesco wanaume walipewa pointi baada ya CWT kushindwa kuonekana ulingoni, nayo TPDC wanawake waliwavuta Tamisemi kwa mivuto 2-0.
Katika mchezo wa bao wanawake Mayasa Kambi wa UDOM alitwaa ubingwa akifuatiwa na Thea Samjela wa Uchukuzi SC na mshindi wa tatu ni Catherine Likunguwa wa CDA; wakati kwa wanaume Omari Said wa Uchukuzi SC alitwaa ubingwa baada ya kumfunga Lameck Mboje wa Tamisemi katika mchezo wa fainali.
Nayo TPDC ilitoshana nguvu na Tanesco katika soka kwa kufungana bao 1-1. Tanesco ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao katika dakika 25 na TPDC walisawazisha katika dakika za nyongeza.
Michuano hiyo itaendelea Jumanne (Aprili 26,2016) katika soka kwa Uchukuzi SC kuwakaribisha CDA Dodoma asubuhi na jioni Ukaguzi watacheza na Mambo ya Ndani.

Vyeti vya kuzaliwa havitolewi kwa misingi ya kisiasa

01ZPBC-IM1001-pemba-crown-hotel-1475
Na Masanja Mabula –Pemba 
SERIKALI ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba imekanusha  taarifa zilizotolewa na wananchi ya kwamba vyeti vya kuzaliwa katika Wilaya hiyo hutolewa kwa misingi ya kisiasa .
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Abeid Juma Ali aliyaeleza hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara  ambao baadhi yao waliodai kwamba kuna ubaguzi juu ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa
Alisema kuwa  kwa kipindi cha miezi mitano tangu ashike wadhifa huo  tatizo la upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa  kwa watoto  katika wilaya hiyo limeanza kupatiwa ufumbuzi .
Alifahamisha kuwa kwa kushirikiana na watendaji wa Ofisi ya Vizazi na Vifo   , ameanza kulipunguza tatizo hilo , ambapo watoto wengi wameweza kupatiwa vyeti kwa wakati na bila usumbufu .
“Mtoto hana chama iweje basi  nimbague kwa misingi ya siasa , natambua wajibu na majukumu yangu kwani mimi ni mtumishi wa umma na ninawatumikia wananchi wote pasi na ubaguzi ”alifahamisha .
Awali mfanyabiashara Ali Salimu Ali (Baraka) wa Wingwi alisema kwamba kunahitaji kuangaliwa upya Ofisi inayohusika na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwani imekuwa ikichelewesha kupatikana kwa vyeti kwa baadhi ya watoto .
Alieleza kwamba wapo watoto wamefikia umri wa kwenda skuli lakini hawana vyeti  vya kuzaliwa , licha ya kwamba kumbukumbu zao zipo katika Ofisi ya vizazi na vifo lakini zimeshindwa kufanyiwa kazi .
“Vyeti vya kuzaliwa bado ni tatizo , kwani kuna baadhi ya watoto wamefikia umri wa kuanza skuli , lakini hawana vyeti , tunaomba hii Ofisi  inayohusika na utoaji wa vyeti uiangalie upya  nahisi kama kuna  ubaguzi fulani hivi  ”alisema  .
Kikao hicho  pia kilihudhuriwa na Madiwani wa Wilaya hiyo ambapo Mkuu wa Wilaya alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara kuwapa ushirikiano wakati wanapokusanya mapato  yatokanayo na biashara zao .

Balozi Amina Salum Ali awataka watendaji Wizarani kuleta mabadiliko katika utendaji wa kazi


aina Na Masanja Mabula – Pemba
 
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar,  Balozi Amina Salum Ali amewataka watendaji wa Wizara hiyo kuleta mabadiliko katika utendaji wa kazi, ili kuifanya Zanzibar iweze kufikia katika uchumi wa kati.
 
Alisema kuwa, Wizara imeandaa sera  mbali mbali ambazo zinaweza kuifanya Zanzibar kufikia uchumi wa kati, ikiwa ni pamoja na sera ya biashara, viwanda na sera ya mpangokazi ambao utekelezaji wake utaanza leo (jana).
 
Akizuzungumza na watendaji wa Wizara hiyo pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti katika ukumbi wa Makonyo Chake Chake, alisema ipo haja kwa watendaji wake kujibadilisha kwa kuwa na sera madhubuti ya  kuwa na viwanda vikubwa, ambavyo vitaifanya Zanzibar kufikia uchumi wa kati.
 
Alieleza suala la kukuza viwanda Zanzibar kuwa, Wizara inataka kukiendeleza kiwanada cha sukari Mahonda, kujenga kiwanda cha maziwa, kiwanda cha Zanzibar Milin na kiwanda cha makonyo ambacho hutoa mafuta ya karafuu, makonyo na mafuta mengine ya mimea.
 
 ”Kuna mambo lazima tuyabadilishe, kwanza utendaji wa kazi wa silka ya kawaida ambapo wanataraji matokeo yatakayobadilisha maisha ya wananchi, utendaji utakaotuletea mapato na maendeleo, hii ndio itakayoifanya Zanzibar kufikia uchumi wa kati”, alisema Balozi huyo.
 
Balozi Amina aliwataka watendaji hao kufanya kazi ya ziada katika kubadilisha Zanzibar  na kuwa ya maendeleo zaidi kwa kutumia bidhaa zinazotokana na kilimo.
 
Alisema kuwa, asilimia 85 ya viwanda Zanzibar ni vya wananchi, hivyo ni vyema juhudi zikatendeka katika kuvibadilisha na kufikia viwanda vikubwa, kwani Zanzibar inayo nafasi kubwa ya kuzalisha na kuuza bidhaa zinazotokana na kilimo.
 
”Tunatakiwa tufanye kazi ya kuibadilisha Zanzibar kwa kutumia bidhaa zinazotokana na mimea, kwani uzalishaji unataka bidii kubwa, hivyo ipo haja ya kuwashirikisha wa Zanzibar na nje yake kwa kutembeleanaili kuona wenzetu wanafanya nini na sisi tuweze kufuata”, alieleza Waziri huyo.
 
Waziri huyo alisema, ipo haja ya kutolewa elimu kwa wajasiriamali na kuwezeshwa kwa kupitia sehemu za nje zenye maeneo ya kiuchumi ili kujifunza mambo mbali mbali ambayo wataiga kutoka huko.
 
”Ili tufikie huo uchumi wa kati ni lazima Serikali ijipange kuwawezesha wajasiriamali na wawekeze kupitia sehemu za wenzao ka kuwatembeza, kupatiwa elimu na soko, jambo ambalo ni changamoto kubwa kwetu”, alieleza.
 
Akizungumzia suala la karafuu alieleza kuwa, Zanzibar imefanya vizuri kwa miaka mitano iliyopita kwa uzalishali wa zao hilo, ambapo Serikali imenunua tani elfu 20 kutoka kwa wananchi, ikiwa na thamani ya shilingi billioni 285.89.
 
”Serikali imejiandaa vizuri na bei itaendelea kuwa ile ile kama alivyoahidi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, lengo ni kuivusha Zanzibar kwenda katika uchumi wa kati”, alisema.
 
Alisema bei ya ununuzi wa zao la karafuu haijashushwa kama baadhi ya wananchi wanavyodai, kwani hiyo ni ahadi ya serikali katika kustawisha maisha ya wakulima wa zao hilo.
 
Aliwataka wananchi kuacha kabisa uuzaji wa karafuu kwa njia ya magendo na waendelee kuuza hapa Zanzibar, kwani fedha zinapoingia serikalini huwafaa wananchi wenyewe kutokana na huduma za kijamii.
 
”Pia tufanye biashara inayokubalika kimataifa, karafuu zetu tusuzichanganye na makonyo kwa sababu kuna ushindani mkubwa wa soko, hivyo ni vyema tukazianika sehemu sahihi na kuwa kavu kabisa”, alifahamisha.
 
Aidha alisema kuwa, Wizara itakuwa na utaratibu wa kuangalia bei ya vyakula na kuhakikisha kwamba vyakula vinavyoingia vinakuwa na viwango vya kimataifa pamoja na usafi.
 
”Tuko tayari kuingia katika mapambano, kwa nini tusiwe na viwango vya vyakula vinavyoingia wakati nchi nyengine wanavyo, tutahakikisha zinaingia bidha zenye ubora na viwango”, alisisitiza.
 
Mwandishi wa habari Salim Ali Mselem kutoka redio Istiqama akiuliza swali, alisema serikali itapanga sera ipi ambayo itawawezesha wananchi wote wakati wanapoimarisha upande huu, wananchi hukwama kwa upande wapili.
 
”Zao la karafuu limeongezwa bei lakini na kodi inaongezeka kwa wafanyabiashara siku hadi siku, jambo ambalo wenye kipato cha chini wanaumia, kwa mfano wafanyabiashara wa sokoni hapa Chake Chake wanatozwa kodi elfu 60 badala ya elfu 30, kweli wananchi wanawezeshwa hivi”, alihoji Salim.
 
Nae Nasra Mohamedi kutoka ZBC televisheni akitoa hoja yake kuwa, kama iliyoelezwa wajasiriamali wapo asilimia  85, hivyo serikali itafute njia mbadala ya kuwawezesha ili kutumia njia ya digital katika kufanya kazi zao ili kufikia maendeleo zaidi.
 
Waziri Amina alikuwa kwenye ziara ya kutembelea vitengo mbali mbali vya Wizara, ambapo aliona jitihada mbali mbali zinazofanywa na wajsiriamali na kujionea mambo mbali mbali ambayo hufanywa katika kiwanda cha makonyo Wawi Chake Chake, ikiwa ni pamoja na mafuta yanayotengenezwa kwa karafuu na makonyo



Serikali yaipongeza Quality Group kwa kuanzisha Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH)

O1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH)   wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHUSM
O2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Qaulity Center leo jijini Dar es Salaam.Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.
O3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti nyeusi) akitembelea bidhaa mbalimbali za Sanaa na Utamaduni mara baada ya kuzindua rasmi Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.
O4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti nyeusi) akitembelea bidhaa mbalimbali za Sanaa na Utamaduni mara baada ya kuzindua rasmi Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.
O5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifurahia jambo na Mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume walipokutaka wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam.
O6
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya picha kutoka kwa uongozi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam.Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.Kituo hicho ni duka ambalo linauza bidhaa za sanaa na utamaduni kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
O7
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya fimbo maarufu kwa jina la Rungu la Kimasai kutoka kwa Mshauri wa masuala ya bidhaa za sanaa na utamaduni Bibi. Caroline Kessy wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam.
O8
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifurahia jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Quality Group Ltd ambao ni wamiliki wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) Bw. Arif Sheikh  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo jijini Dar es Salaam
………………………………………………………………………………………….
Na: Frank Shija;WHUSM
Serikali yaipongeza Kampuni ya Quality Group ltd kwa hatua yake ya kuanzia Kituo cha Uridhi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) ambapo kupitia kituo hicho bidhaa mbalimbali za Sanaa na Utamaduni zinauzwa ndani na nje ya nchi.
Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho kutaiuza nchi, utamaduni wetu, kazi za sanaa na kuongeza ajira miongoni mwa jamii yetu.
Aidha Profesa Gabriel amesema kuwa Serikali itaendelea kuwa pamoja nao na kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha kwamba wanafikia mafanikio na malengo waliyojiwekea katika uwekezaji huo.
Aliongeza kuwa ni vyema sasa Kituo hiko kikafikiria kuanzisha vituo vidogo vidogo katika kanda ili kurahishisha upatikanaji wa bidhaa hizo na kusaidi wasanii walioko pembezoni wapate soko la bidhaa zao kwa Serikali ingependa kuona zaidi wasanii wa ndani wakinufaika na uwepo wa Kituo hicho.
Pia ameuomba uongozi wa Kituo hicho kuangalia namna ya kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwajengea uwezo wasanii hili kujenga soko la uhakika,ubora na viwango vya hali ya juu.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Quality Group Limited Bw. Arif Sheikh ameishukuru Serikali kwa kuonyesha ushirikiano kna imekuwa faraja kubwa kwao kwa kiongozi wa ngazi ya juu Serikalini kukubali kuja kuzindua Kituo chao.
Sheikh amesema kuwa kuanzishwa kwa Kituo hicho kumelenga kukuza sanaa na utamaduni wa Mtanzania kwakuwa kinahusika na uuzaji wa bidhaa za sanaa na utamaduni tu, hivyo wasanii wanayo fursa ya kujipatia kipato kwa kukiuzia Kituo kazi zao.
Hata hivyo Sheikh alisema kuwa kutokana na ushauri uliotolewa Kampuni yao ipo tayari kutoa ushirikiano zaidi kwa Serikali pindi watakapohitajika kufanya hivyo ikiwemoi sualaua la kuwajengea uwezo wasanii wa kazi za mikono.
Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzaia ambacho kwa kingereza kinaitwa  Tanzania Center for Cutural Heritage (TCCH) kipo katika jengo la Quality Center, kinamilikiwa na Kampuni ya Qaulity Group Limited ya jijini Dar es Salaam.

DC HAPI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA ALI HASSAN MWINYI

H1

Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akikagua matengenezo ya  barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016 jijini Dar  es Salaam
H2
 Mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Salum Hapi wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa barabara ya Ali Hassani Mwinyi Halipo tembelea leo kuona maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo
H3
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akiwa na wafanyakazi wa MS ESTIM CONSTRUCTION CO.LTD
H4
Mkuu wa wilaya Mhe.Ally Hapi akiongea na msimamizi wa ujenzi.
H5
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kushoto akiwa na meneja wa Tanroad katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016

JESHI LA POLISI LAKEMEA JAMII KUHUSU MATUKIO YA UBAKAJI WA WATOTO NCHINI

AD 
Ndugu zangu waandishi wa habari, kwanza niwashukuru kwa ushirikiano ambao mmeendelea kutupatia, pia niwashukuru wananchi wote kwa ujumla kwa ushirikiano wao wa kudumisha amani na usalama hapa nchini. Tumewaiteni hapa leo kuzungumzia matukio ya ubakaji
Katika siku za hivi karibuni, Matukio ya ubakaji hasa kwa watoto wadogo yamekuwa yakiongezeka kwa kiwango kikubwa, ongezeko hili limebainika kutokana na ufuatiliaji tulioufanya kupitia matukio yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi ambapo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2016 kumeripotiwa matukio 1765 ukilinganisha na matukio 1585 katika kipindi kama hicho mwaka 2015 ikiwa ni ongezeko la matukio 180.
Katika matukio ya Januari hadi machi 2016, jumla ya watuhumiwa 823 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani ingawa bado kumekuwa na tabia ya wazazi na walezi kuficha watuhumiwa wa ubakaji na  kumaliza kesi hizo kirafiki au kifamilia jambo ambalo ni kinyume cha sheria bila kuzingatia madhara aliyoyapata mtoto.
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linakemea vikali wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo viovu vya ubakaji na wazazi ama walezi wanaofumbia macho vitendo hivyo na kuingia makubalino na watuhumiwa kwa kupeana fedha kama fidia ili wamalize kesi kiundugu au kifamilia.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa  Wazazi, walezi, Viongozi wa dini, Asasi za kiraia, walimu na Wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano katika kushughulikia vitendo hivyo ikiwemo kuwafichua wazazi au walezi wanaofanya makubaliano ya kumaliza kesi za ubakaji kirafiki au kifamilia ili kukomesha vitendo hivyo.
 Imetolewa na:
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.        

ANDIKO LA JK KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA MALARIA DUNIANI

Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete ametoa andiko lake kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani. andiko hilo ambalo ameliandika kwa lugha ya Kiingereza na ambalo limo katika Tovuti ya gazeti la Huffington Post, Dk. Kikwete anasema “ When I was President of Tanzania, I remember visiting a district where 70 percent of the children were absent from school. They told me the problem was malaria. I sent my minister of health to investigate, and he confirmed it was true: a majority of children were missing school and falling behind because they had malaria. That was a wake-up call for all of us…

NHIF YAPELEKA HUDUMA YA MADAKTARI BINGWA MKOANI NJOMBE

2
Mganga Mkuu wa  mkoa wa Njombe Dokta Samuel Mgema akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma  za madaktari bingwa mjini Njombe wanaowafanyia upasuaji na matibabu  wagonjwa mbalimbali kwa  mikoa husika, kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed Bakari
3
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dokta Frank Lekey akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma  za madaktari bingwa mjini Njombe wanaowafanyia upasuaji na matibabu  wagonjwa mbalimbali kwa  mikoa husika,kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed Bakari.
5
Baadhi ya watumishi na madaktari pamoja na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo.
6
Mkuu wa mkoa wa NJOMBE  Mh. Rehema  Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja viongozi mbalimbali mara baada ya uzunduzi huo uliofanyika mjini Njombe leo.
………………………………………………………………………………………………..
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirkiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, wiki hii inaendesha zoezi la huduma za madaktari bingwa katika mikoa ya Njombe na Iringa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo mkoani Njombe Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed Bakari amesema serikali itaendelea kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhakikisha kuwa huduma hizo zinapelekwa katika maeneo mengi ambako wananchi wanahitaji huduma za madaktari  bingwa ili kukabiliana na upungufu uliopo.
Amesema pamoja na kuendelea kutumia huduma hizo za muda za madaktari Bingwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya, itajitahidi kujenga miundo mbinu bora ya sekta ya afya na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi walio wengi.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mganga Mkuu wa Serikali, Mganga Mkuu wa  mkoa wa Njombe Dokta Samuel Mgema, amesema hospitali yake inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na uchakavu wa majengo na ufinyu wa nafasi ikilingwanishwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaohudumiwa katika hospitali hiyo.
Ameomba Serikali iharakishe mchakato wa kujenga Hospitali mpya ya mkoa ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa mkoa wa Njomba, kwani hospitali inayotumika hivi sasa ya Kibena ilikuwa na hadhi ya hospitali ya wilaya na kupandishwa hadi baada ya kutangazwa kwa mkoa mpya wa Njombe, miaka minne iliyipita.
  
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dokta Frank Lekey amesema huduma hizo za madaktari bingwa zimekuwa zikitolewa na Mfuko wake kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya kupeleka huduma bora za matibabu kwa wanachama wa NHIF na kwa wananchi kwa ujumla.
Asema hadi sasa huduma hizo zimeshatolewa katika mikoa 14, ambazo zaidi ya wagonjwa 11,400 wamepatiwa huduma, miongoni mwao zaidi ya wagonjwa 340 walifanyiwa upasuaji wa kitaalamu.
Amesisitiza kuwa huduma hizo zinatolewa kwa wananchi wote bila ubaguzi kwa kufuata taratibu za kawaida za malipo za hospitali husika.

WAKANDARASI WAPIGA MARUFUKU MAGARI YENYE UZITO MKUBWA KUPITA DARAJA LA NYERERE,WAWATAKA WATANZANIA KULITUNZA DARAJA HILO.

 
Hivi ndivyo mandhari nzuri na ya kuvutia ya Daraja la Nyerere lionekanavyo kwa juu pamoja na flai ova yetu ya kuingilia darajani hapo ndani ya Wilaya mpya ya Kigamboni.
Sehemu ya mageti ambapo magari yanapaswa kupita wakati wa kufanya malipo yanayotarajiwa kuanza Mei Mosi 2016.
Mhandisi wa Mradi kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group and Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV) Jamal Mruma akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari kuhusiana na ubora wa daraja hilo.Mhandisi Mruma alisema kuwa Daraja hilo limejengwa kwa ubora mkubwa na lina uwezo wa kuhimili uzito zaidi ya tani 50,lakini kwa sasa magari yanayoruhusiwa ni yale yenye tani kumi kushuka chini,”kwa sasa tunadhibiti uzito mkubwa kwa sababu kuna baadhi ya maeneo bado hayajakamilika ikiwemo na barabara ya kuingilia Kigamboni,ambako hakuwezi kumudu kupitishwa uzito mkubwa”,alibainisha Mhandisi Jamal.
Meneja Mradi kutoka NSSF,Mhandisi Karim Mataka akizungumzia namna baadhi ya Madereva ambao wamekuwa wakikiuka taratibu/sheria na alama zilizowekwa katika daraja hilo kubwa Afrika Mashariki ambalo linatarajiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 100 iwapo litapata matunzo stahiki.Mhandisi Karimu amebainisha kuwa magari yanayopaswa kupita hapo kwa sasa yawe chini ya tani 10,kwa sababu kwa upande wa Kigamboni bado baadhi ya barabara hazijakamili,hivyo ni vyema Madereva wote wakawa makini.
Daraja hilo ambalo litaanza kutumika rasmi kwa kulipia Mei Mosi 2016,Mhandisi Karimu amewataka Watanzania kulinda miundo mbinu ya daraja hilo ikiwemo kutii sheria zote za Daraja hilo ili kuepuka kusababisha uharibifu wa aina yoyote ile,kwa sababu limejengwa kwa gharama kubwa na linahitaji matunzo.
Mhandisi alibainisha pia kuwa Daraja hilo la Kigamboni ambalo lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na kulibatiza jina la Daraja la Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Moja ya Lori likikatiza darajani hapo kwa kukiuka taratibu na sheria za Daraja hilo.
DCIM100MEDIADJI_0006.JPG
Muonekano wa Daraja la Mwal Nyerere kama lionekanavyo kwa mbaali kidogo unapoelekea kwenye mageti ya kutokea upande wa pili wa Kigamboni.Daraja hilo limerahisisha usafiri wa kutoka Kigamboni mpaka kati kati ya jiji la Dar.
DCIM100MEDIADJI_0011.JPG
CgMM5g4UAAA8hhP
Daraja la Kigamboni linavyoonekana usiku.
DCIM100MEDIADJI_0053.JPG
Daraja la Kigamboni linavyoonekana mchana.
DCIM100MEDIADJI_0060.JPG
Makutano ya barabara za kutoka na kuingia katika daraja la Kigamboni yanavyoonekana.

DCIM100MEDIADJI_0069.JPG

SERIKALI YAUNDA KAMATI YA KUANZISHA TUME YA TEHAMA

 

TZ 
Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, ameunda Kamati ya mpito ya kusimamia uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  (TEHAMA) ambapo ameipa miezi sita kufanya kazi kuanzia mwezi Aprili, 2016 ya kuhakikisha kuwa Tume ya TEHAMA inaanza kazi rasmi.
Katika kuhakikisha kuwa Tume ya TEHAMA inaanza kazi mara moja, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano, Prof. Faustin Kamuzora, amewakabidhi wajumbe wa Kamati hiyo Amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na.532 iliyotolewa kupitia gazeti la Serikali Na. 47 la tarehe 20 Novemba, mwaka 2015 iliyoanzisha Tume na Hadidu za Rejea zinazoainisha majukumu yao. Majukumu hayo ni pamoja na kusimamia uanzishwaji wa Tume, kuandaa sheria ya kuanzisha Tume, na kutengeneza Mpango Mkakati wa Tume. Prof. Kamuzora amewataka wajumbe wa Tume hiyo  kuepuka kuweka mitazamo au maslahi binafsi ya wao wenyewe au ya taasisi zao katika kipindi cha kuanzisha Tume, bali waishauri Serikali namna nzuri ya kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaanza kazi ya kusimamia na kuratibu masuala ya TEHAMA nchini. Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao na Katibu wa Kamati ya Kuanzisha Tume ya TEHAMA nchini ni kama ifuatavyo:
  • James Kilaba (Mwenyekiti), Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
  • Samson Mwela (Katibu), Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
  • Idris Rai (Mjumbe), Makamu Mkuu wa Chuo, SUZA,
  • Joan Mbuya (Mjumbe), Mkurugenzi wa Sera na Mipango-Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali,
  • George Mulamula (Mjumbe), Mkurugenzi Mtendaji-DTBi,
  • Juma Rajabu, (Mjumbe), Mkurugenzi Mtendaji-Maxcom Africa,
  • Maharage Chande, (Mjumbe), Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Ofisi ya Rais-President’s Delivery Bureau, na
  • Nicolaus Mhonyiwa (Mjumbe), Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA-Ofisi ya Msajili wa HAZINA.
Aidha, Tume ya TEHAMA inatarajiwa kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na yafuatayo: Kushiriki katika kushauri juu ya uwekezaji wa TEHAMA nchini kwa ubia na sekta binafsi; kuwatambua, kujenga uwezo na kuwaendeleza wataalam wa TEHAMA; kushauri na kushiriki pamoja na wadau katika tafiti za TEHAMA, uwekaji viwango na ubunifu katika sekta ya TEHAMA; na kushiriki katika kusimamia miundombinu na programu za kitaifa za TEHAMA.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano, Dkt. Eng. Maria Sasabo, alisisitiza kuwa Kamati ina kazi kubwa ya kuona namna bora zaidi ya kuhakikisha kuwa Tume itatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na masuala ya uwekezaji; na kusimamia vema  viwango vya wataalamu wa Sekta. Naye Mwenyekiti, Inj. James Kilaba, kwa niaba ya Kamati alishukuru kwa kuaminiwa na Serikali na pia aliahidi kuwa watatekeleza majukumu yao kikamilifu. Pia alimalizia kwa kusema, “hatutawaangusha”.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikali

CHAMA CHA UDP CHAPATA PIGO VIGOGO WAKE WAWILI WAKIMBILIA CCK

 Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akiwapokea waliokuwa viongozi wa Chama cha UDP, waliokihama chama ambao ni  Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara na Mkurugenzi wa Uchaguzi  Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na aliyekuwa Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho , Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK jijini Dar es Salaam leo asubuhi mbele ya waandishi wa habari.
 Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma (kulia), akizungumza wakati wa kuwapokea viongozi hao. Kushoto Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara aliye hamia CCK. 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam, Joachim Mwakitiga aliyejiunga na chama hicho na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya aliyehamia chama hicho.
…………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha United Democratic Party (UDP) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake wa Taifa, John Momose Cheyo, kimepata pigo baada ya wenyeviti wawili wa mikoa ya Mtwara na Dar es 
Salaam kukihama na kujiunga na Chama Cha Kijamii (CCK).
Viongozi waliokihama chama hicho ni  Salum Makunganya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara,  Mkurugenzi wa Uchaguzi  Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmshauri Kuu, Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa 
habari.
Wenyeviti hao baada ya kujitoa walikabidhi kadi zao za UDP kwa Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi ambaye naye aliwakabidi kadi ya CCK na kuwatangaza rasmi  kuwa wanachama wa chama hicho.
Makunganya alikabidi kadi yake ya UDP yenye namba 4544 na kukabidhiwa ya CCK namba 1597 huku Mwakitiga akibidhi kadi yake ya UDP namba 2852 na kukabidhi ya CCK yenye namba 01599 katika tukio lililofanyika ofisi za CCK.
Wakizungumzia sababu zilizowafanya wajitoe UDP walisema ni kutokana na chama hicho kutokuwa na mwelekeo wa kimaendeleo ambacho kwa zaidi ya miaka sita viongozi wake wa kitaifa hawajaitisha mikutano ukiwamo wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu.
Walisema sababu nyingine ni kwamba viongozi wa kitaifa wa UDP wamekigeuza chama hicho kama kampuni binafsi ambapo wamekuwa wakitoa maamuzi mbalimbali ambayo hayajaamuliwa na wanachama kwenye vikao .
“Nyie waandishi si mnaishi Dar es Salaam tangu lini mlishaona Mwenyekiti wa Taifa wa UDP, John Cheyo akiitisha hata mkutano wa hadhara hapa Dar es Salaam kuzungumzia mambo mbalimbali ya chama na taifa kwa ujumla kama vinavyofanya vyama vingine…jibu ni hakuna, UDP inabuka tu wakati wa uchaguzi na tena kwenye eneo moja tu,”alisema Mwakitiga.
Muabhi akizungumza baadhi baada ya kuwakabidhi kadi wenyeviti hao alisema CCK inawapokea kwa mikono miwili viongozi hao na kwamba wakiwa ndani ya chama hicho wataona utofauti na vyama vingine kwa kuwa chama kimejiwekea misingi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Muabhi aliitaka serikali kulitazama upya suala la vikao vya Bunge kutotangazwa kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kufanya hivyo kunawanyima haki wananchi ya kupata habari na hivyo kushindwa kujua nini kinaendelea Bungeni.
“Serikali ijitathimini, wananchi wasipojua nini kinaendelea Bungeni kuna haja gani kwa wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kwenda Bungeni, wananchi watajuaje kama wawakilishi wao wamezifikisha kero zao serikalini,”alisema.
Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma, alisema ujio wa wanachama hao wapya ambao ni wakongwe katika siasa na hivyo CCK itajifunza mambo mengi kutoka kwao.

CHAPTELE WA UCHUKUZI SC AIBUKA BINGWA MARA SABA

1 
Thea Samjela wa Uchukuzi SC (kuilia) akichuana na Regina Mutimangi wa TPDC katika mchezo wa bao.
2 
Omar Said wa Uchukuzi SC (kushoto) akicheza bao dhidi Hamisi Rahis wa Tanesco.
3 
Neema Makassy  wa Uchukuzi SC (kulia) akitafakari katika mchezo wa bao dhidi ya Joyce Kimondi wa Ujenzi.
4 
Ally Sule wa Uchukuzi SC(kushoto) akicheza mchezo wa fainali dhidi ya Salum Simba wa Tamisemi. Simba aliibuka bingwa.
5 
Timu ya wanawake ya kamba ya Uchukuzi SC wakiwavuta wenzao wa Ukaguzi kwa mivuto 2-0.
6 
Timu ya wanaume ya Uchukuzi SC wakiwavuta wenzao wa Tamisemi kwa mivuto 2-0.

MARIA STOPES YAWANOA WAANDISHI WA HABARI WA JIJI LA MWANZA NA DAR JUU YA UZAZI WA MPANGO

Mchambuzi wa Sera na bajeti wa asasi ya Health Promotion Tanzania (HPT), Bw. James Mlali akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliokutanishwa pamoja jijini Mwanza na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliokutanishwa pamoja jijini Mwanza na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Mwandishi wa wandishi na Muandaaji wa vipindi wa habari wa Redio Free Afrika ya Mwanza, Migongo akiuliza swali kwa mwezeshaji wa mafunzo hayo.
Wasimamizi wa Mafunzo hayo kutoka Maria Stopes Tanzania.
Mtaalamu wa uzazi wa mpango, Bi. Shida Masumbi akiwaonyesha waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam moja ya njia mojawapo inayotumika katika uzazi wa mpango.
Mhadhiri wa SJMC- UDSM, Bw. Abdallah Katunzi akitoa mwongozo kwa waandishi wa habari juu ya mafunzo waliyoyapata waweze kuyafanyia kazi ipasavyo.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Citizen, Bernard Lugongo akiuliza maswali. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog – Mwanza.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Cathbert Angelo Kajuna, Mwanza.
 
ASASI ya Health Promotion Tanzania (HPT) inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango imeiomba Serikali kuongeza bajeti ya uzazi wa mpango ifikie Sh. bilioni sita.
 
Kauli hiyo imetolewa na Mchambuzi wa Sera na bajeti wa asasi hiyo, James Mlali wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Maria Stopes Tanzania kuhusu ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango.
 
Alisema asilimia 27 ndiyo inayotumia uzazi wa mpango na asilimia 25 wanakosa huduma hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti inayotengwa na Serikali.
 
Mlali alisema bajeti ikiwa ndogo hata elimu inakuwa ndogo kutokana na ukosefu wa vitendea kazi.
 
“Bajeti inayotengwa inatakiwa iendane na ongezeko la idadi ya watu kwa kuzingatia upatikanaji wa huduma za kijamii ambazo ni elimu,afya, na ajira.
 
“Pia ongezeko hili alizingatie hali ya uchumi kwasababu asilimia 42 ya watoto wamedumaa akili kutokana na ukosefu wa lishe bora,” alisema Mlali.
 
Mtaalamu wa uzazi wa mpango, Shida Masumbi alisema kuna njia tatu za uzazi wa mpango ambazo ni njia ya muda mfupi, muda mrefu na njia ya kudumu.
 
Alisema njia za muda mrefu ni kitanzi, kipandikizi na njiti, njia za muda mfupi ni sindano, vidonge na kondomu.
 
“Pia ipo njia ya kudumu ya uzazi wa mpango ambayo ni mume na mke kufunga kizazi.
 
“Baadhi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango husababisha maudhi kwa kukosa hedhi, kuongezeka siku za hedhi au kuona matone madogomadogo ya damu,”alisema Masumbi.
 
Alisema pamoja na maudhi hayo lakini kuna faida ambazo ni kuzuia vifo kwa mama na mtoto, mama kupumnzika kwa muda mrefu na kujishughulisha na kazi nyingine za kimaendeleo.
 
Masumbi alisema mwitikio wa matumizi ya uzazi wa mpango ni mkubwa na wanaume 300 walijitokeza kufunga kizazi kwa mwaka jana.

No comments :

Post a Comment