Tuesday, April 12, 2016

KONGAMANO LA UWAJIBIKAJI KWA WADAU WA SEKTA YA MAFUTA NA GESI LAFANYIKA DAR ES SALAAM

16

Waziri wa Fedha Dkt.Philip Mpango akizungumza na wadau  (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la uwajibikaji katika sekta ya Mafuta na Gesi lililoandaliwa na taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability leo Aprili 11,2016 jijini Dar es Salaam.
17Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability Bw.Ludovick Utouh akizungumza na wadau waliyoshiriki Kongamano linalohusu uwajibikaji katika sekta ya Mafuta na Gesi (hawapo pichani)  kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi leo jijini Dar es Salaam.
18 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango (kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi  rasmi  wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability na (kushoto) ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw.Ludovick Utouh,sherehe hizo zimefanyika leo jijini Dar es Salaam.
19 
Baadhi ya wadau waliyoshiriki Kongamano linahusu Uwajibikaji katika sekta ya Gesi na Mafuta wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na  Mkurugenzi wa Taasisi ya TWAWEZA Bw.Aidan Eyakuze (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika leo jijini Dar es Salaam
21 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability Bw.Ludovick Utouh wakiwa  wanaonesha kibao kinacho onyesha ufunguzi rasmi wa taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
20 
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (wanne kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliyoshiriki Kongamano la Uwajibikaji katika sekta ya Mafuta na Gesi,(watatu kulia ni)aliyekuwa  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue  na (watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability Bw.Ludovick Utouh.
Picha na Anitha Jonas – MAELEZO.

Mhe. Kairuki afungua Mafunzo JUU YA Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) Dodoma

15 
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mh. Angellah Kairuki (Mb) akifungua Mafunzo juu ya Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania yaliyofanyika mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza wakati wa Mafunzo kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania yaliyofanyika mjini Dodoma.
14Mmoja wa washiriki wa Mafunzo kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) akiuliza swali wakati wa mafunzo yaliyofanyika mjini Dodoma.
13 
Mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Bibi. Sipora J. Liana akiuliza swali wakati wa mafunzo yaliyofanyika mjini Dodoma.
12  Washiriki wa Mafunzo hayo  wakimsikiliza mgeni rasmi Mh. Angellah Kairuki (Mb), (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo –Dodoma.10 
Mkutano ukiendelea

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA YAKUTANA NA WAZIRI WA MUUNGANO NA MAZINGIRA

7Mwenyekiti wa  Kamati ya bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira Dkt.Dalaly  P.Kafumu (katikati) akifafanua Jambo kwa wajumbe wa Kamati hiyo wakati wa kikao cha  Kujadili Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira ,kulia kwake ni Katibu wa kamati hiyo Ndg.Godfrey Magova na kushoto ni Bi. Zainabu Mkamba .
8 
Waziri wa nchi Ofis ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.January  Makamba akielezea jambo  kwa wajumbe wa Kamati ya bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira wakati Wakijadili bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira kwa mwaka wa fedha 2016/ 2017.  
9 
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira Wakimsikiliza kwa Makini Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh.Dkt.  Dalaly P. Kafumu walipokutana Kujadili taarifa ya Utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira kwa Mwaka wa fedha 2016/2017.    

MKE WA WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA MASHUKA KWA AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA

1 
Waziri Mkuu, Kassim Majalaiwa akizungumza  na  Madaktari, Wauguzi na watumishi wa hospitali ya wilaya ya  Ruangwa  Aprili 11, 2016.  Kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Lindi, Mzee Mtopa.
2 
Mke  wa  Waziri Mkuu, Mary Majalaiwa akizungumza baada ya kukabidhi msaada wa shuka kwa wazazi wanaosubiri kujifungua na waliojifungua kwenye hospitali ya wilaya ya  Ruangwa  Aprili 11, 2016.  Kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Lindi, Mzee Mtopa.
5Wanawake  wa  Ruangwa wakimshangilia Waziri Mkuu,   Kassim Majaliwa wakti alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu mjini Ruangwa Aprili 11, 2016.
6 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na wanwake  wa Ruangwa  baada ya kuzungumza nao kwenye  ukumbi wa  Chama cha Walimu  mjini Ruangwa  Aprili  11, 2016.
3 
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitembelea soko  kuu la mji wa Ruangwa  kukagua hali ya chakula na bei zake Aprili  11, 2016. Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa.
4  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na  mabingwa wa soka wa mkoa wa Lindi , timu ya   Namungo FC ya Ruangwa baada ya kukabidhiwa kombe  la ubingwa huo na kuzungumza nao kwenye uwanja wa michezo wa Ruangwa akiwa katika ziara jimboni kwake , Aprili 11, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
…………………………………………………………………………………………………….

AFRICA DIGITAL BANKING SUMMIT WILL BE HELD ON 13TH & 14TH APRIL, 2016 AT JNICC, DAR ES SALAAM

 Africa Digital Banking Summit will be held on 13th & 14th April, at Julius Nyerere International Convention Centre, Dar es Salaam from 8.30am- 4.30pm. 
 
Topics that will be discussed: 
 
1. E- commerce/M-commerce in East Africa,
 
2. Mobile Money & Digital Payment, 
 
3. Payment Security & Regulation , 
 
4. The Future of Mobile Money & Digital Platforms. 
 
Guest of Honour: Dr. Ashatu Kijaji, Assistant Minister, Ministry of Finance. Speakers include: Mr. Bernard Dadi, Director, National Payment System, Bank of Tanzania, Kelvin Twissa, Telecommunications Expert, Imeke Bassemaker, CEO, NMB, Sameer Hirji, Executive Director, Selcom Tanzania. Visit www.africadbs.com for registration detail

SENDEKA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI BABATI

1 
Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akionyshwa na Katibu wa CCM mkoa wa Manyara, Ndengaso Ndakubali (kulia), jinsi Jengo la Ofisi ya CCM mkoa huo, lilivyoungua moto hivi karibuni, Sendeka alipokagua jengo hilo, leo Aprili11, 2016, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Manyara.
2Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya za Babati Mjini na Babati Vijijini, katika ukumbi wa CCM mkoawa Manyara, leo Aprili 11, 2016, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo.
(Picha na Bashir Nkoromo).

KIKAO CHA BARAZA LA MAPINDUZI (BLM)

index 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM) mara baada ya kuwaapisha Viongozi hao hapo jana, kikao kilichofanyika leo kiliwajumuisha Mawaziri pamoja na Naibu Mawaziri wote wa wizara 13 katika ukumbi wa Baraza hilo Ikulu Mjini Unguja,
 [Picha na Ikulu.]

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO AFRIKA MASHARIKI

DSC_0002
Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam.
.
Shyrose Bhanji
Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji akizungumza jambo.
DSC_0018
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakichukua habari.

JESHI LA MAGEREZA NA SUMA – JKT WAKABIDHIWA JUKUMU LA KUTENGENEZA MADAWATI YENYE THAMANI YA BILIONI 6, JIJINI DAR

mboj1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akionesha mfano wa hundi aliyokabidhiwa na Ofisi ya Bunge leo Ikulu, Jijini Dar es Salaam ambapo fedha hizo ameelekeza zitumike kutengenezea madawati ya shule hapa nchini(kulia)ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.
mboj2
Muonekano wa Madawati ambayo yanatarajiwa kutengenezwa na yaliyoidhinishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kama yanavyoonekana katika picha.
mboj3
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Bregedia Jenerali, Michael Isamuhyo(katikati) wakifuatilia hotuba ya Rais Magufuli(kulia) ni Mtendaji Mkuu wa SUMA – JKT, Bregedia Jenerali C.Yateri.
mboj4
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akiongea na Wandishi wa Habari kuhusu namna Jeshi hilo lilivyojipanga kutekeleza jukumu lililopewa.
mboj5
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa waliohudhuria hafla hiyo.
mboj6
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akisalimiana na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila wakipokutana katika Viwanja vya Ikulu, Jijini Da es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
……………………………………………………………………………………………….

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu azindua taasisi ya (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation)

1
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy
Mwalimu (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation)
yenye lengo la kusaidia wanawake kuinua uwezo wao wa kibunifu ili
kujiinua kiuchumi  hasa Mama Lishe kwa kushirikiana na wadau mbali
mbali. Uzinduzi huo umefakika leo Aprili 11, 2016 kwenye Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni
Mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Basila Mwanukuzi (kulia), Kaimu Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Jinsia, Timoth Mgonja pamoja na Mwakilishi wa Mama
Lishe, Bi. Grace Foya.
2
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy
Mwalimu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
3
Basila Mwanukuzi Mkurugenzi wa Taasisi ya  (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation) akimkaribisha Waziri Ummy Mwalimu ili kuzungumza na wageni waalikwa na kisha kuzindua rasmi taasisi hiyo.
4
Baadhi ya ndugu na wanafamilia wa Basila Mwanukizi wakiwa katika hafla hiyo
5
Mrisho Mpoto kushoto na Miriam Ikoa mmoja wa waliowahi kuwa Miss Tanzania wakiwa pamoja na wageni wengine katika hafla hiyo.
7
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy
Mwalimu akisalimiana na Basila Mwanukuzi mara baada ya kuwasili katika uzinduzi huo Katikati ni Kaimu Mkurugenzi  wa Maendeleo ya Jinsia, Timoth Mgonja
8
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy
Mwalimu akisalimiana na baadhi ya akina mama Lishe waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi.
9
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
10
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy
Mwalimu akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga.
11
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy
Mwalimu na Basila Mwanukuzi wakipiga picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.

No comments :

Post a Comment