RAIS
wa zamani wa Klabuya Simba ya Dar es Salaam, Alhaj Ismail Aden Rage,
(kushoto), akipokea kadi yake ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, kutoka kwa Meneja
Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa PSPF, Bi.Costantina Martin, makao
makuu ya PSPF, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Aprili 14, 2016.
Alhaj Rage akionyesha kadi hiyo
Meneja
wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
Bi. Mwanjaa Sembe, (kushoto), akipokea fomu za kujiunga na uanachama
kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Klabu ya soka ya Simba, Alhaj Ismail Aden
Rage, makao makuu ya PSPF, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Aprili 14,
2016
Alhaj
Rage, (kushoto), akiweka dole gumba kwenye fomu yake ya uanachama huku
akisaidiwa na Bi. Mwanjaa Sembe, (kulia) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa
PSPF, Bw.Abdul Njaidi
Alhaj Rage akijaza fomu, kuliani Bi. Mwanjaa Sembe
Alhaj Rage, akikabidhi fomu kwa Bi. Mwanjaa Sembe, huku Njaidi akishuhudia
Rage akizungumza baada ya kukabidhi fomu kwa Bi. Mwanjaa Sembe (kushoto)
Meneja
wa Mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, wa Mfuko wa Pensehni wa
PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, akiwa mwenye furaha baada ya kupokea mwanachama
mpya, Alhaj Ismail Aden Rage
Alhaj Rage akipokewa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Njaidi alipowasili kujiunga na Mfuko huo
Alhaj Rage, akibadilishana mawazo na Bi. Costantina Martin, na Njaidi baada ya kuwa mawanachama wa Mfuko huo
…………………………………………………………………………………………………
RAIS wa zamani wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Alhaj Ismael Aden Rage, amejiunga
na mpangowa uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Aprili 14,
2016.
Rage ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Tabora mjini, kufuatia kujiunga huko,
amefaidika kuingizwa kwenye fao la huduma ya afya litolewalo na Mfuko huo
kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF ambao una ushirikiano wa kutoa
huduma za afya kwa wanachama wa PSPF wanaotaka kufaidikana huduma hiyo.
“Nitoe wito kwa wanamichezo wakiwemo wa mpira wa miguu, kuchangamkia fursa hiyo kwani
mambo sasa yamebadilia kujiunga na PSPF kupitia mpango huu wa hiari ambao
unamruhusu mtu binafsi au vikundi kujiunga na uanachama, lakini pia kutokana na
kupanda kwa huduma za afya, ukiwa mwanachama wa PSPF unaweza kupata huduma ya
afya wewe na familia yako, hii ni faida kubwa.” Alisema Rage wakati
akikabidhiwa kadi yake ya uanachama na Meneja Masoko, Mawasiliano na Uenezi wa
PSPF, Bi. Costantina Martn.
Rage alisema, yeye kama mwanamichezo atahamasisha wanamichezo hususan wacheza mpira
kujiunga na mpango huu kwani maisha ya sasa yanahitaji kwenda kisasa, na jambo
muhimu ni kuwa na afya bora, na afya bora utaipata kama unapata huduma bora,
nimeambiwa kupitia mpango huu ninaweza kupata matibabu kwenye hospitali yoyote
nchini na wakati wowote, Alisema.
Awali Rage alijaza fomu za kujiunga na uanachama ambapo alipokewa na Meneja wa Mpango
wa Uchangiaji wa Hiari, PSS, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe. Ambaye
alimshukuru Rage kwa kuwa mwanachama wa Mfuko huo.
na mpangowa uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Aprili 14,
2016.
Rage ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Tabora mjini, kufuatia kujiunga huko,
amefaidika kuingizwa kwenye fao la huduma ya afya litolewalo na Mfuko huo
kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF ambao una ushirikiano wa kutoa
huduma za afya kwa wanachama wa PSPF wanaotaka kufaidikana huduma hiyo.
“Nitoe wito kwa wanamichezo wakiwemo wa mpira wa miguu, kuchangamkia fursa hiyo kwani
mambo sasa yamebadilia kujiunga na PSPF kupitia mpango huu wa hiari ambao
unamruhusu mtu binafsi au vikundi kujiunga na uanachama, lakini pia kutokana na
kupanda kwa huduma za afya, ukiwa mwanachama wa PSPF unaweza kupata huduma ya
afya wewe na familia yako, hii ni faida kubwa.” Alisema Rage wakati
akikabidhiwa kadi yake ya uanachama na Meneja Masoko, Mawasiliano na Uenezi wa
PSPF, Bi. Costantina Martn.
Rage alisema, yeye kama mwanamichezo atahamasisha wanamichezo hususan wacheza mpira
kujiunga na mpango huu kwani maisha ya sasa yanahitaji kwenda kisasa, na jambo
muhimu ni kuwa na afya bora, na afya bora utaipata kama unapata huduma bora,
nimeambiwa kupitia mpango huu ninaweza kupata matibabu kwenye hospitali yoyote
nchini na wakati wowote, Alisema.
Awali Rage alijaza fomu za kujiunga na uanachama ambapo alipokewa na Meneja wa Mpango
wa Uchangiaji wa Hiari, PSS, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe. Ambaye
alimshukuru Rage kwa kuwa mwanachama wa Mfuko huo.
WAZIRI WA ARDHI AKUTANA NA WAMILIKI WA MABENKI NCHINI
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
akiwasisitiza Wamiliki wa Mabenki Nchini kuzitambua Hati Miliki za Ardhi
za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali,
kushoto ni Bibi Medelina Kiwayo Meneja Usimamizi wa Taasisi za
Fedha-Benki Kuu na Tuse Joune Kaimu Mkurugenzi Mkuu Chama cha Wenye
Mabenki Tanzania (TBA).
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
akiwasisitiza Wamiliki wa Mabenki Nchini kuzitambua Hati Miliki za Ardhi
za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali
alipo kutana nao leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
akiwasisitiza Wamiliki wa Mabenki Nchini kuzitambua Hati Miliki za Ardhi
za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali
alipo kutana nao leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa katika kikao na Wamiliki
wa Mabenki Nchini ili kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika
kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali, kulia ni Bibi
Medelina Kiwayo Meneja Usimamizi wa Taasisi za Fedha-Benki Kuu na Tuse
Joune Kaimu Mkurugenzi Mkuu Chama cha Wenye Mabenki Tanzania (TBA),
kushoto ni David Shambwe Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya
Biashara-NHC na Mary Makondo Kaimu Kamishna wa Ardhi.
Rais Magufuli atengua uteuzi wa Nderumaki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji
wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. Gabriel Nderumaki.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 14
Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi,
imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia tarehe 18
Machi, 2016.
Bi. Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN)
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
14 Aprili, 2016
ASILIMIA 71 YA WATANZANIA HAWATAKI KUFANYA KAZI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista
Mhagama,akizungumza katika katika uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa watu
wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014. Uzinduzi huo ulifanyika
katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam, jana. Kulia ni Mkurugenzi wa
Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mkurugenzi Mkuu
wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista
Mhagama,akionesha ripoti ya matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa
kufanya kazi wa mwaka 2014 katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam,
jana. Wengine wanaoshuhudia ni kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa
Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu
za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi
Duniani,Marry Kawar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista
Mhagama,akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa
kufanya kazi wa mwaka 2014 katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam, .
Wengine wanaoshuhudia ni kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu
nchini,Dk.Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za
Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi
Duniani,Marry Kawar.
………………………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi – MAELEZO
Utafiti uliofanyika hivi
karibuni na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) umebaini kwamba asilimia 71
ya watanzania wanatumia muda mwingi kufanya shughuli zisizokuwa za
uzalishaji mali wala tija binafsi kwao na Taifa kwa ujumla
Akizundua taarifa ya utafiti
huo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
amesema kuwa idadi hiyo hufanya kazi zisizoleta tija kwao na taifa na
muda mwingi huutumia kujihudumia binafsi kwa kulala na starehe nyingine.
Ameeleza kuwa takwimu hizo
zinaonesha wazi ni kwa namna gani watanzania wanashindwa kujishughulisha
katika kufanya kazi zenye kuwaingizia kipato na badala yake wanatumia
muda wao mwingi kufanya shughuli zisizo za uzalishaji hasa kufanya
starehe mbalimbali.
“ Ndugu zangu watanzania
unakuta mtu amekaa baa au anacheza “poll table” kuanzia asubuhi mpaka
jioni na hujui anafanya kazi gani ya uzalishaji, ndugu zangu tuone aibu
basi tujishugulishe tulijenge taifa letu ili kujiletea maendeleo yetu na
nchi yetu.”
Aidha, matokeo hayo
yamebainisha kuwa asilimia 18.5 ya wananchi wanafanya kazi za uzalishaji
na asilimia 10.6 ni wale wanaofanya shughuli za nyumbani zisizo na
malipo huku uchambuzi wa kijinsia ukionesha kuwa wanaume asilimia 23.8,
wanatumia muda mwingi kwenye shughuli za kiuchumi ikilinganishwa na
asilimia 13.5 ya wanawake.
Amefafanua kuwa wanawake ambao
ni asilimia 16.5 katika utafiti huo wanatumia muda mwingi kufanya kazi
za nyumbani zisizo na malipo ikilinganishwa na asilimia 4.4 ya wanaume.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Ofisa ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa
upatikanaji wa Takwimu hizo utaisaidia Serikali kupata mbinu sahihi za
kuondokana na tatizo la ajira nchini kwa kuunganisha nguvu kutoka sekta
isiyo rasmi ili kuleta changamoto katika soko la ajira nchini.
Amesema kuwa hii ni mara ya
tano Tanzania inafanya utafiti huo na kubainisha kuwa ulianza mwezi
Januari hadi Desemba, 2015 ukitumia sampuli ya Sensa ya Watu na Makazi
ya mwaka 2012 iliyotumika kupata taarifa sahihi ya takwimu hizo.
Aidha, amebainisha kuwa ili
kufanikisha utafiti huo NBS imeshirikiana na wadau mbalimbali ikwemo
Wizara ya kazi na Ajira,Shirika la Kazi Duniani (ILO),Benki ya Dunia
(WB),Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) na Asasi zisizo za Kiseikali.
Tigo sasa ya pili kwa ukubwa katika kampuni za simu Tanzania

Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez
Ushindani
unazidi kupamba moto miongoni mwa kampuni za simu nchini ambapo katika
kipindi cha miezi mitatu cha kati ya Oktoba na Desemba mwaka 2015, ni
jumla ya watumiaji wapya 1,448,782 tu ambao walijisali kutumia huduma
zao za mawasiliano.
Ushindani
huu ambao umechochewa na kuingia kwa kampuni mpya katika sekta ya
mawasiliano Tanzania, umefikisha jumla kuu ya watumiaji wa huduma ya
mawasiliano nchini kufikia 39.8 milioni kwa mujibu wa
takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Mamlaka ya Mawasilano Tanzania,
(TCRA).
Kampuni
ya MIC Tanzania Ltd- ijulikanayo kwa jina lingine kama Tigo – ilisajili
juma ya wateja wapya 488,886 katika kipindi hicho cha miezi mitatu sawa
na asilimia 34. Idadi
hii ya wateja wapya inaifanya Tigo kuwa na jumla ya wateja 11,115,991
na kuifanya kampuni hiyo kuwa katika nafasi ya pili kwa ukubwa imiliki
asilimia 28 la soko la mawasiliano nchini na hivyo kuipita
Airtel ambayo imekuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha takriban muongo mmoja.
Airtel ambayo imekuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha takriban muongo mmoja.
Airtel
kwa upande mwingine ilisajili jumla ya wateja wapya wapatao 32, 839
katika kipindi hicho cha miezi mitatu na kufikisha jumla ya wateja wake
kuwa 11,047, 505 ambayo ni sawa na asilimia 28 lakini kiwa imezidiwa na
Tigo kwa idadi ya wateja 68,486. Licha
ya kuendelea kupungua kwa idadi ya wateja wake mwaka hadi mwaka, kwa
mujibu wa takwimu za TCRA, Vodacom bado inaongoza kwa kuwa na idadi
kubwa ya wateja wapatao 12,714,297 sawa na asilimia 32 ya jumla
ya watumiaji wote wa huduma za mawasiliano Tanzania.
ya watumiaji wote wa huduma za mawasiliano Tanzania.
Idadi ya wateja wa Vodacom imeonekana kushuka kutoka asilimia 45 mwaka
2007 hadi asilimia 41 mwaka 2008 na kufikia asilimia 39 Desemba 2009.
Wadadisi
wa sekta ya mawasiliano wanaelezea hali hii kushuka kwa idadi ya wateja
wapya miongoni mwa kampuni hizi kuwa kunachangiwa na mabadiliko ya
kimikakati ambapo msizitizo mkubwa miongoni mwa kampuni ni kuwalenga
Zaidi wateja watumiaji wa huduma za Intaneti kupitia simu zao
kama nyenzo kuu ya kukuza mapato tofauti na matumizi ya kuongea na
kutuma sms kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Meneja
Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez, kwa upande wake ameelezea kukua haraka
kwa kampuni hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kusema
kumechangiwa na sababu mbalimbali zikiwemo ubunifu mkubwa ambao
unafanywa katika kendesha kampuni kibiashara.
“Mafanikio
ya Tigo yameletwa na sababu nyingi kama vile kuwapa wateja wetu huduma
bora na kwa bei nafuu, upatikanaji wa mtandao wetu nchi nzima, utumiaji
wa teknolojia ya kisasa, ubunifu na kuwa karibu na wateja,” Gutierrez
anasema.
Akifafanua
Zaidi kuhusu ubunifu huo, Gutierrez ametaja baaadhi ya huduima na
bidhaa zilioanzishwa na kampuni hivi karibuni kama vile kuwapa wateja
uwezo wa kufanya miamala ya kibenki kupitia simu zao za mikononi, uwezo
wa kutuma na kupokea fedha kutoka mitandao mingine ya mawasiliano,
kutuma na kupokea fedha kimataifa na mgao wa faida utolewao kwa
watumiaji wa huduma ya Tigo Pesa kila baada ya miezi mitatu.
Aidha meneja huyo mkuu ametaja vichocheo vingine vya kukua hara kwa Tigo kuwa ni “kubuni
huduma zinazolenga kuwapa wateja wetu fursa ya kuishi maisha ya kidijitali zikiwemo
huduma kama vile upatikanaji wa Facebook kwa lugha ya Kiswahili, simu zenye menu ya Kiswahili, WhatsApp ya bure na zinginezo,” amesema. Kampuni ya Tigo kwa mujibu wa Gutierrez inawekeza kiasi cha dola za kimarekani $ 120 milioni kwa mwaka katika kuboresha mtandao wake na kupanua upatikanaji wa huduma zake
nchini.
huduma zinazolenga kuwapa wateja wetu fursa ya kuishi maisha ya kidijitali zikiwemo
huduma kama vile upatikanaji wa Facebook kwa lugha ya Kiswahili, simu zenye menu ya Kiswahili, WhatsApp ya bure na zinginezo,” amesema. Kampuni ya Tigo kwa mujibu wa Gutierrez inawekeza kiasi cha dola za kimarekani $ 120 milioni kwa mwaka katika kuboresha mtandao wake na kupanua upatikanaji wa huduma zake
nchini.
Ametoa
mfano wa huduma ya 4G LTE ya Tigo ambayo kwa sasa inapatikana katika
miji sita – Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi na
Mwanza – na kuelezea kuwepo kwa mkakati wa kufikisha huduma hii katika
mji mikubwa yote nchini ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Kwa
upande wake kampuni ya Zantel ambayo ni kampuni dada ya Tigo, zote kiwa
zinamilikiwa na Millicom, ilirekodi wateja wapya 320, 483 katika
kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ta mwaka 2015 na kufikisha jumla ya
wateja 1, 839, 391. Nayo kampuni mpya ya Haloteli ndiyo iliyoongoza
kwa kuvuna wateja wengi kipindi hicho wapatao 793, 383 na hivyo
kufikisha jumla kuu
ya waetja wake kuwa 1,226,678 hadi kufikia mwisho wa Desemba 2015.
ya waetja wake kuwa 1,226,678 hadi kufikia mwisho wa Desemba 2015.
Ikiwa
na wateja milioni 1.56 hadi kufikia mwishoni mwa Desemba 2015, Smart
ilikuwa na asilimia nne (4) la soko la mawasiliano ya simu nchini sawa
na Zantel wakati kampuni inayomilikiwa na serikali (TTCL) ikiwa
inashikilia asilimia moja (1) ya soko hilo.
MAKABIDHIANO YA OFISI KATIBA NA SHERIA ZANZIBAR
Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji
Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wa Wizara ya Katiba,Sheria,Utumishiwa Umma na Utawala Bora wakati wa makabidhiano ya Ofisi na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishiwa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun
Ali Suleiman leo katika ukumbi wa Jengo la Wizara ya Utumishi wa Umma
Shangani Mji Mkongwe wa Zanzibar, baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheun,[Picha na Ikulu.]
Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji
Makeme Mwadini akikabidhiana Ofisi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Katiba,Sheria,Utumishiwa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman
leo katika ukumbi wa Jengo la Wizara ya Utumishi wa Umma Shangani Mji
Mkongwe wa Zanzibar, baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheun,[Picha na Ikulu.]
Mwakilishi WHO atembelea Wizara ya Afya Zanzibar kupata tarifa za Kipindupindu
Waziri wa Afya Mhe, Mahmoud
Thabit Kombo kulia akisalimiana na Muakilishi wa Shirika la Afya Duniani
WHO alioko Zanizbar Dk, Ghirmay Andemichael mara baada ya kuwasili
Ofisini kwake Mnazi mmoja Mjini Zanzibar, kupata taarifa ya maradhi ya
kipindupindu yalioanza mwezi Septemba mwaka jana hapa Zanzibar.
Waziri wa Afya Mhe, Mahmoud
Thabit Kombo akizungumza na muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO
nchini Tanzania Dk, Rufaro Chatora kushoto yake pamoja na ujumbe
aliofuatana nao Ofisini kwake Mnazi mmoja Mjini Zanzibar. Muakilishi
huyo alifika kuangalia hali ya maradhi ya kipindupindu Zanzibar.
Muakilishi wa Shirika la Afya
Duniani WHO Dk, Rufaro Chatora katikati akizungumza na Wakuu wa sekta
mbalimbali katika Wizara ya Afya Zanzibar kuhusiana na Maradhi ya
Kipindupindu Zanzibar. Kushoto yake ni Muakilishi wa WHO aliopo
Zanzibar Dk, Ghirmay Andemichael na kulia yake ni Katibu Mkuu wizara ya
Afya Zanzibar Mohd Saleh Jidawi.
………………………………………………………………………………………………….
NA RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR
Mwakilishi wa Shirika la Afya
Duniani (WHO) nchini Tanzaia Dkt. Rufaro Chatora amezishauri taasisi za
Serikali, taasisi za kiraia na watu binafsi kila mmoja kutekeleza
wajibu wake katika kukabiliana na maradhi ya kipindupindu nchini.
Amesema maradhi ya kipindupindu
yanapotokea katika nchi moja yanagusa nchi nyingi duniani kutokana na
watu kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyengine katika harakati zao za
maisha.
Dkt. Chatora ameeleza hayo
alipokuwa akizungumza katika mkutano na watendaji wakuu wa Wizara ya
Afya na waandishi wa Habari katika ziara yake ya kuangalia hali ya
maradhi ya kipindupindu Zanzibar tokea yalipoanza mwezi Septemba mwaka
jana hadi hivi sasa ambapo watu 2703 wamepata ugonjwa huo.
Amesema maradhi ya kipindupindu
ni rahisi kutibika iwapo kila mtu atatimiza wajibu wake na kufuata
ushauri wa wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kuacha kutumia maji
yasiyo salama ambayo ni moja ya chanzo kikubwa cha kupata maradhi hayo.
Mwakilishi huyo wa WHO amesema
Shirika hilo kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Kimataifa
litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
katika kukabiliana na maradhi hayo ili kuhakikisha yanamalizika.
Akieleza hali ya kipindupindu
ilivyo hivi sasa Zanzibar katika mkutano huo uliofanyika Wizara ya Afya
Mnazimmoja, Mkurugenzi Kinga na ELimu ya Afya Dkt. Mohd Dahoma amesema
hali bado sio nzuri na wanaendelea kupokea wagonjwa wengi katika kambi
ya Chumbuni.
“Tunapokea wagonjwa kati ya 10
hadi 15 kwa siku katika kambi ya Chumbuni, kwa bahati mbaya jana
tulipokea wagonjwa 20 na kambi moja mpya imefunguliwa katika kisiwa
cha Tumbatu,’’ alisema Dkt. Dahoma.
Amesema jumla ya Kambi 17 za
wagonjwa wa kipindupindu zimefunguliwa katika maeneo mbali mbali ya
Unguja na Pemba na kumi kati yao zimefungwa baada ya kukosa mgonjwa wa
maradhi hayo.
Ameongeza kuwa kati ya wagonjwa
2703 waliogunduliwa na maradhi hayo 34 wamefariki ikiwa ni sawa na
asilimia 1.3 na vijana wenye umri kuanzia miaka 17 ndio walioathirika
zaidi.
Dkt. Dahoma amesema kisiwa cha
Unguja kimekuwa na wagonjwa wengi zaidi wa kipindupindu asilimia 52.3
na Pemba ni asilimia 47.3 huku Mkoa Mjini Magharibi ukiongoza ukifuatiwa
na Mkoa Kaskazini Pemba.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya
amewashauri wananchi kuwawahisha mapema vituo vya afya watu
wanaobainika na dalili za maradhi ya kipindupindu kwa vile imeonekana
wagonjwa wengi wanapopelekwa vituoni afya zao zinakuwa mbaya na matibabu
yanakuwa magumu.
Wizara ya Afya Zanzibar yaadhimisha siku ya afya Duniani kwa kutoa elimu ya maradhi yasiyoambukiza skuli mbali mbali.
Mkuu wa Kitengo cha maradhi
yasiyoambukiza (NCD) Omar Mwalimu Omar akitoa elimu kwa wanafunzi wa
Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki juu ya njia bora za kujikinga na
maradhi yasiyoambukiza ikiwa ni maadhimisho ya siku ya afya Duniani.
Muuguzi kutoka kliniki ya
wagonjwa wa kisukari Hospitali ya Mnazimmoja Bi. Mwanaharusi Shaaban
akitoa elimu ya ugonjwa wa kisukari kwa wanafunzi wa Skuli ya
Mwanakwerekwe C katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afya Duniani
zinazoadhimishwa kila ifikapo tarehe 7 April. Zanzibar imeadhimisha
siku hiyo April 13 kwa kutoa elimu skuli za serikali na binafsi.
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya
Mwanakwerekwe C wakimskiliza kwa makini mtoa elimu ya maradhi yasiyo
ambukiza Bi. Mwanaharusi Shaaban (hayupo pichani) wakati wa sherehe za
siku ya Afya Duniani zinazoadhimishwa kila ikifika tarehe 7 kila mwaka.
Mwanafunzi Shadia Issa Juma akiuliza swali kwa Muuguzi kitengo cha wagonjwa wa kisukari Bi. Mwanaharusi Shaaban.
Mkufunzi kutoka kitengo cha
maradhi yasiyoambukiza (NCD) cha Wizara ya Afya Rabia Ali Makame
akifundisha wanafunzi wa Skuli ya SOS kuhusiana na visababishi
vinavyopelekea maradhi yasiyo ya kuambukiza katika sherehe za
kuadhimisha siku ya Afya Duniani.
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya
Mwanakwerekwe C wakimskiliza kwa makini mtoa elimu ya maradhi yasiyo
ambukiza Bi. Mwanaharusi Shaaban (hayupo pichani) wakati wa sherehe za
siku ya Afya Duniani zinazoadhimishwa kila ikifika tarehe 7 kila
mwaka.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLYOVER) YA TAZARA NA KUFUNGUA DARAJA LA KIGAMBONI JIJINI DARA ES SALAAM
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara
ya juu (Flyover) katika makutano ya TAZARA na ufunguzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Siku ya Jumamosi tarehe 16
Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais ataweka jiwe na msingi la ujenzi wa
barabara ya juu katika makutano ya barabara Nyerere na Mandela (Flyover ya TAZARA).
Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016
Mheshimiwa Rais atafungua rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita
680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini
na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5. Ujenzi huu umefanywa na
Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China
Bridge Engineering Group.
Aidha wakati tunasubiri uzinduzi
rasmi, Wananchi na magari yenye uzito usiozidi tani 10 yataruhusiwa
kutumia Daraja la Kigamboni kuanzia Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 ili
kuwawezesha kuelewa vizuri miundombinu na matumizi ya daraja.
Utekelezaji wa miradi hii ni
mojawapo ya jitihada za Serikali za kuboresha miundomninu na kupunguza
msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.
Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
14 Aprili, 2016
NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KUTEMBELEA MRADI WA MABWAWA YA SAMAKI GEREZA KWAMUGUMI, KOROGWE
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi Mhe. William Ole Nasha (Mb) anatarajia kufanya ziara ya kikazi
Gereza Kwamugumi, Korogwe Mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi
iliyotolewa na kusainiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John
Casmir Minja inaeleza kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea
maendeleo ya mradi wa mabwawa ya samaki yaliyopo gerezani hapo ambayo
hadi sasa yamepandwa vifaranga wa samaki 18,800 tangu tarehe 16/12/2015.
Kabla ya kutembelea eneo la mradi
wa mabwawa ya samaki, Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha atapokea taarifa
fupi ya maendeleo ya mradi wa uzalishaji samaki Gereza Kwamugumi,
Korogwe.
Miradi ya ufugaji samaki ipo
katika Magereza ya Karanga, Njombe, Masasi, Tukuyu ambapo nia ya Uongozi
wa Jeshi la Magereza ni kuieneza katika Magereza mbalimbali yenye fursa
za kuendesha mradi huo.
Mradi wa uzalishaji samaki katika
Gereza Kwamugumi ni mojawapo ya miradi mbalimbali ya uzalishaji mali
iliyoanzishwa na Uongozi wa Jeshi katika kukabiliana na changamoto
mbalimbali zinazolikabili Jeshi la Magereza, hususan katika kuipunguzia
Serikali gharama za kuhudumia Magereza na kuongeza pato la kodi kwa
Taifa.
Dk. Kigwangalla akutana na afisa miradi kutoka Shirikala la Kimataifa la nguvu za Atomiki (IAEA)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla (wa
pili kushoto) akisikiliza kwa makini mazungumzo na Afisa miradi
anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa
wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile (wa kwanza kulia). Wengine
ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba anayeshughulikia magonjwa yasiyo
ambukiza, Profesa Ayoub Magimba (katikati), akifutiwa na Mkurugenzi
taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaisalage na kushoto Mratibu wa
Magonjwa ya Saratani Kitaifa pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kwa watu
wazima, Dk. Sara Maongezi. (Picha na mpiga picha wetu).
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla
amekutana na Afisa miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika
kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon
Haile katika mazungumzo yaliyofanyika leo asubuhi Aprili 14.2016,
Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Dk.
Kigwangalla ameomba Tanzania ipatiwe kibali cha kununua mashine mpya ya
kutibu saratani (LINAC) Sambamba na sehemu ya msaada iliyoahidiwa na
Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Bw.Yukiko Amano mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu,
Mh. Mizengo Kayanda Pinda miaka mitatu iliyopita.
Tanzania tayari imetenga kiasi
cha Euro 1.65 Milioni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya mchango wake kwa
asilimia 50 kama mradi ulivyokuwa awali.
Mh. Kigwangalla alisema:
“Bahati mbaya sana kutokana na ucheleweshwaji, Bajeti ya msaada huo
kutoka IAEA ilipitwa na wakati na kusababisha Tanzania kukosa fursa
hiyo. Malengo ya Tanzania ni kununua mashine hizo mbili kwa ajili ya
kuboresha huduma za tiba ya Mionzi nchini”.
Ujenzi wa jengo kwa ajili ya
kufunga mashine hizo mbili umesha kamilika na mashine moja itakamilika
mwaka huu na ya pili mwakani ili kuboresha huduma za Saratani nchini.
Katika mazungumzo hayo, Maafisa
waandamizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Woto
walishiriki, akiwemo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba
anayeshughulikia magonjwa yasiyo ambukiza, Profesa Ayoub Magimba,
Mratibu wa Magonjwa ya Saratani Kitaifa pamoja na magonjwa
yasiyoambukiza kwa watu wazima, Dk. Sara Maongezi pamoja na Kaimu
Mkurugenzi taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage.
WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA USAJILI LA MAZINGIRA
Waziri afya ,maendeleo ya
jamii,jinsia ,wazee na watoto Ummy Mwalimu akiongea na wajumbe wa
baraza jipya la usajili wa wataalam wa afya ya mazingira nchini(hawapo
pichani) kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof: Bakari Mohammad
Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo pamoja na maofisa mazingira wakifuatilia hotuba ya Mh. Waziri Ummy Mwalimu
Mwenyekiti mpya wa baraza la
usajili wa wataalam wa afya ya mazingira nchini Bartholomayo
Ngaeje(katikati) akitoa neon la shukrani kwa waziri wa afya,maendeleo ya
jamii,jinsia,wazee na watoto(hayupo pichani) mara baada ya kuzinduliwa
kwa baraza hilo,kulia ni msajili wa baraza hilo Iddy Hoyange na kulia ni
njumbe wa baraza hilo toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,hafla
hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa wizara hiyo
Waziri wa afya,maendeleo ya
jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akimkabidi cheti cha Uongozi
kwa kuthamini mchango wake kwa baraza hilo aliyekuwa mwenyekiti wa awamu
ya pili Bi.Mary Swai
Filamu za Bi Kidude kuoneshwa katika kumbukumbu ya kifo chake
Kushoto ni mmiliki wa ukumbi wa
ZANCINEMA Mohammed Bajbeir, akiwa pamoja na Andy Jones, raia wa
Uingereza, mtengenezaji wa filamu za ‘As Old sa My Tongue’ na ‘I shot
Bi. Kidude’, zinazoonesha historia ya maisha hadi kufa kwa msanii
mkongwe marehemu Fatma Baraka ‘Bi. Kidude’, wakizungumza na waandishi wa
habari juu ya kumbukumbu ya msanii huyo aliyefariki dunia Aprili 17,
2013. (Picha na Yussuf Simai-MAELEZO, ZANZIBAR.
Kamati ya Muda ngumi za kulipwa yaundwa.
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la
Michezo Taifa(BMT) Bw. Mohamed Kiganja wa kwanza kushoto akiongea na
waandishi wa habari hawapo pichani leo jijini Dar es salaam kuhusu
viongozi waliochaguliwa wa kamati ya muda ya mchezo wa Ngumi za kulipwa ,
kulia ni Katibu Mkuu wa kamati hiyo Bw. Yassin Ustaadh.
Katibu Mkuu mpya wa Kamati ya
Muda ya Mchezo wa Ngumi za kulipwa Bw. Yassin Ustaadh akisisitiza jambo
mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani baada ya kukabidhiwa kamati
hiyo leo jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza
kwa makini Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa(BMT) Bw.
Mohamed Kiganja hayupo pichani alipotambulisha viongozi waliochaguliwa
wa kamati ya muda ya mchezo wa Ngumi za kulipwa , kulia ni Katibu Mkuu
wa kamati.
WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAZIRI WA BIASHARA WA OMAN
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda kama mkakati wa
kukuza uchumi ili nchi iweze kutoka kwene umaskini na kufikia uchumi wa
kati.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU UTAPELI WA AJIRA KATIKA TAASISI MBALIMBALI
Katika siku za hivi karibuni
katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kumejitokeza makundi ya watu ama
mtu binafsi kutumia mwamvuri wa taasisi fulani kujipatia kipato kwa njia
za udanganyifu (utapeli) kwa kuwaahidi vijana kwamba watawapatia ajira
katika taasisi hizo.
Makundi haya ya kihalifu
imebainika kwamba yapo katika maeneo mbalimbali, hivyo, ni suala ambalo
linahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi ili kukomesha vitendo
hivyo. Juhudi za makusudi zinaendelea kufanyika na jeshi la polisi ili
kuwatia mbaroni watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kitapeli.
Aidha, kufuatia kuibuka kwa
vitendo hivyo, tayari Jeshi la Polisi limewakamata matapeli wawili
wakiwa wamekusanya vijana katika mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya,
uchunguzi dhidi yao unaendelea na pindi utakapokamilika watafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabiri.
SENDEKA AWASILI MKOANI KILIMANJARO LEO
Msemaji
wa CCM, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa
Kilimanjaro, Deogratius Ruta alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa
Kilimanjaro, mjini Moshi leo
Mjumbe
wa NEC na Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Mawasilino na Umma Makao
Makuu ya CCM, Kilumbe Ng’enda akisalimiana na Mwenyekiti wa CCN mkoa wa
Kilimanjaro Iddi Juma alipowasili na Sendeka, Ofisi ya CCM mkoa huo leo.
Katikati ni Mkuu wa Wialaya ya Moshi Novatus Makunga
Msemaji
Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka akibadilishana mawazo na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Juma Iddi alipowasili katika
Ofisi ya CCM mkoa huo leo kuanza ziara ya kikazi. Kulia ni Mkuu wa
wilaya ya Moshi Novatus Makunga.
Msemaji
Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiiingia ukumbini kuzungumza na
wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kutoka wilaya za mkoa wa Kilimanjaro,
leo.
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kutoka wilaya za mkoa wa Kilimanjaro wakimpokea Ole Sendeka alipoingia ukumbini
Ole Sendeka baada ya kuingia ukumbini
Msemaji
Mkuu wa CCM, Ole Sendeka akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili
ukumbini kuzungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kutoka wilaya za
mkoa wa Kilimanjaro leo
Msemaji
Mkuu wa CCM, Ole Sendeka akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili
ukumbini kuzungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kutoka wilaya za
mkoa wa Kilimanjaro leo
Wajumbe wakiwa ukumbini kusmikiliza Ole Sendka
Msemaji
wa CCM, Cheristopher Ole Sendeka akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti
ya CCM wilaya za mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuwasili akiwa katika
ziara ya kikazi leo.
Msemaji
wa CCM, Cheristopher Ole Sendeka akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti
ya CCM wilaya za mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuwasili akiwa katika
ziara ya kikazi leo. Picha na Bashir Nkoromo).
TAKUKURU MKOANI PWANI YAZITAJA TAASISI NA IDARA 11 ZINAZOONGOZA KWA MALALAMIKO YA VITENDO VYA RUSHWA
Kamanda wa taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Rymond akiwaonyesha
waandishi wa habari ofisini kwake hawapo pichani orodha ya majina ya
taasisi na idara ambazo zimeongoza kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa
(Picha na Victor Masangu)
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo wa Takukuru.
……………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, PWANI
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani
Pwani imezitaja taasisi na idara zipatazo 11 ambazo zimelalamikiwa
kuhusika katika matukio mbali mbali ya vitendo vya kupokea rushwa
kinyume kabisa na
TAMISEMI MKOANI MWANZA YAONGOZA KWA RUSHWA.
Mkuu
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha Mkoani Mwanza (Pichani)
Mhandisi Ernest Makale, leo ametoa taarifa ya Utendaji kazi wa taasisi
hiyo mbele ya Wanahabari katika kipindi cha robo mwaka (Januari hadi
Machi) mwaka huu.
Katika
taarifa hiyo, Mhandisi Makale amebainisha kuwa Takukuru imepokea jumla
ya malalamiko 45 yanayohusiana na vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi
ambapo katika malalamiko hayo, 27 yameelekezwa kwa watumishi wa idara
za Serikali za Mitaa TAMISEMI hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 60. Kati ya
malalamiko hayo 27, malalamiko 13 yameelekezwa katika idara ya ardhi.
(TUMA) KIMELITAKA BARAZA LA SANAA LA TANZANIA KUTOFUNGIA MATAMASHA YA WASANII BILA KUSHIRIKISHWA
RAIS SHEIN AKUTANA MAKAMO WA RAIS WA KOICA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Rais
wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini “KOICA GLOBAL” Bw.Kwon Taemyon
akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo pamoja na
mwenyeji wa Ujumbe huo Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi
Mhe,Hamad Rashid Mohamed(hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini “KOICA
GLOBAL” Bw.Kwon Taemyon akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini
Zanzibar leo pamoja na mwenyeji wa Ujumbe huo Waziri wa
Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed(hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na
Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini “KOICA GLOBAL”
Bw.Kwon Taemyon (wa pili kushoto) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu
Mjini Zanzibar leo pamoja na mwenyeji wa Ujumbe huo Waziri wa
Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed(wa pili kulia)
akiwepo Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee(kulia),[Picha na
Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini “KOICA
GLOBAL” Bw.Kwon Taemyon baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ukumbi
wa Ikulu Mjini Zanzibar leo (katikati) Waziri wa
Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed,[Picha na Ikulu.]
MBUNGE WA CHAMA CHA WAZALENDO ACT-TANZANIA AKUTANA NA WATANZANIA NEW YORK CITY
Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma
Kaskazini akisisitiza jambo mbele ya vijana wa Kitanzania waishio New
York. Zitto alipata nafasi ya kuongea na vijana hao waliotaka kujua
maendeleo ya nchi yao na changamoto zake ndani ya bunge la jamhuri
anavyowakilisha hoja zake kwa faida ya wananchi kupitia upinzani, pia
yeye kama mwana siasa alie upande wa upinzani nini mtazamo wake juu ya
kasi ya rais wa wamu ya 5. Zitto ni mmoja ya vijana kwenye Bunge la
jamhuri ya muungano wa Tanzania na ni Mbunge mwenye nguvu na uwezo wa
kuwakirisha hoja zenye mashiko ndani ya bunge la jamhuri na kuitikisa
serikali ya chama tawala. Mfano mmoja ni suala la Escrow yeye ndiyo
alikuwa chanzo cha habari hiyo iliyotikisa serikali na kupelekea
wananchi kukosa imani na mwenendo mzima wa serikali ya chama tawala. Na
pia alisha wasilisha hoja ya Buzwagi ilisababisha Zitto kusimamishwa
ubunge kwa miezi 4. Zitto yupo New York City kwa kivuli cha World Bank
na pia alipata nafasi ya kutembelea Columbia University New York na
kuongea na wasomi wa huko na pia atapata nafasi ya kutembelea Harvard
University huko Boston. MA. Picha na Vijimambo Blog New York
Zitto akipata ukodak baada ya kukutana na Watanzania New York City. Kwa taswira zaidi nenda soma zaidi.
MWAKILISHI MPYA WA UNHCR NCHINI AJITAMBULISHA KWA WAZIRI KITWANGA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), akimkaribisha
ofisini kwake Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya wakati alipokuwa anawasili
ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha kwa Waziri huyo mara baada ya
kuteuliwa na Shirika lake kuja kuiongoza UNHCR nchini. Hata hivyo,
viongozi hao katika mazungumzo yao walijadiliana masuala mbalimbali
jinsi wa kuwahudumia wakimbizi waliopo nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia), akimfafanulia
jambo Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia
Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea
Waziri Kitwanga ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha baada ya
kuteuliwa na UNHCR kuja kuwa kiongozi wa Shirika hilo nchini.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto),
akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kulia) wakati Mwakilishi
huyo alipomtembelea Naibu Waziri huyo ofisini kwake kwa lengo la
kujitambulisha baada ya kuteuliwa na UNHCR kuja kuwa kiongozi wa Shirika
hilo nchini. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi
nchini, Harrison Mseke. Katikati ni Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika
hilo, Yoko Akasaka, na Afisa wa Shirika hilo nchini, Daria Santoni (wa
pili kulia).
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiwa katika
picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (katikati), pamoja na
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. Kapaya
ameteuliwa na UNHCR kuwa Mwakilishi wa Shirika hilo nchini na
amemtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha,
hata hivyo katika mazungumzo yao walijadiliana masuala mbalimbali ya
jinsi ya kuwahudumia Wakimbizi waliopo nchini.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA KWANZA UNAOJADILI SEKTA BINAFSI KATIKA KULETA MAENDELEO ENDELEVU NCHINI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akifungua mkutano wa kwanza unaojadili kuhusu kuangalia Biashara na
Sekta Binafsi katika kuleta Maendeleo endelevu Nchini kwa ajili ya
kufikia malengo 17 ya Maendeleo kwa Jamii. Mkutano huo ulioandaliwa na
AFRIKA SUSTAINABLE BUSINESS umefunguliwa Leo April 14,2016 katika Hoteli
ya Hyatt jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa AFRIKA SUSTAINABLE BUSINESS Bw.
Raymond Mubayiwa kabla ya kufungua mkutano wa kwanza unaojadili kuhusu
kuangalia Biashara na Sekta Binafsi katika kuleta Maendeleo endelevu
Nchini kwa ajili ya kufikia malengo 17 ya Maendeleo kwa Jamii. Mkutano
huo umefunguliwa Leo April 14,2016 katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es
salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja na watendaji na washiriki wa Mkutano wa
kwanza unaojadili kuhusu kuangalia Biashara na Sekta Binafsi katika
kuleta Maendeleo endelevu Nchini kwa ajili ya kufikia malengo 17 ya
Maendeleo kwa Jamii baada ya kufungua Mkutano huo Leo April 14,2016
katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam.
(Picha na OMR)
KAIMU KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA SHAKHA HAMDU SHAKA AWASILI WILAYA YA NGORONGORO KUHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shakha Hamdu Shakha akihutubia wafugaji
katika wilaya ya Ngorongoro katika wilaya hiyo
katika wilaya ya Ngorongoro katika wilaya hiyo
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shakha Hamdu Shakha (wanne kushoto) akiwasili
katika wilaya ya Ngorongoro ambapo alifanya mkutano wa hadhara na kuzindua
matawi ya chama katika wilaya hiyo.wakwanza mstari wa mbele ni Mwenyekiti
wa UVCCM Arusha Lengai Ole Sabaya .
katika wilaya ya Ngorongoro ambapo alifanya mkutano wa hadhara na kuzindua
matawi ya chama katika wilaya hiyo.wakwanza mstari wa mbele ni Mwenyekiti
wa UVCCM Arusha Lengai Ole Sabaya .
(PICHA NA WOINDE SHIZZA,NGORONGORO)
CZECH KUBORESHA UHUSIANO NA TANZANIA
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Jamhuri ya Czech, Zdenek Adamec
ak
iweka sahihi kwenye kitabu cha wageni Ofisini kwa Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (Hayupo pichani).
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akizungumza katika
kikao chake na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Czech, Zdenek Adamec
(Hayupo pichani) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati
na Madini Dk. Meldad Kalemani akizungumza na Dk. Mturi Arnold Meneja
miradi ya Czech Republic katika kampuni ya Tanzania House of Business
Company Limited huku Bw. Zdenek Adamec katikati Naibu Waziri wa Viwanda
wa Jamhuri ya Czech akisikiliza.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (mwenye tai nyekundu),
akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
kutoka Jamhuri ya Czech, Zdenek Adamec (Kushoto kwake), Meneja Mradi wa
Czech nchini, Dkt. Mturi Arnold (mwenye suti ya kahawia), kulia ni Mrs.
Olivia Maboko wa idaraya Ulaya na Americas katika wizara ya mambo ya
nje wakiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa wizara ya Nishati na
Madini.
……………………………………………………………………………………
TAA WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA MIFUMO YA PESA KWA NJIA YA SIMU ILI WAWEZE KUKUZA UCHUMI WAO
Mwenyekiti wa Africa Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu akizungumza kuhusu mkutano huo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitoa hotuba katika mkutano huo.
Baadhi ya washiriki walioshiriki mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili.
Meneja Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Dadi akitoa taarifa kuhusu matumizi ya mobile banking nchini.
Mkurugenzi mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha akiwasilisha mada katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkakati wa Jackson Group Ltd, Kelvin Twissa akitoa mada katika mkutano huo.
Fastjet yatoa ofa nauli za Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam, 12 Aprili 2016-Shirika
la ndege la bei nafuu, fastjet, limetangaza punguzo la nauli la sh.
22,000/- kwa mwezi huu wa Aprili kwenye safari zake za Kilimanjaro,
Mbeya na Mwanza.
Kulingana
na Afisa Masoko na Uhusiano wa Umma wa fastjet, Lucy Mbogoro, ofa hiyo
ijulikanayo kama JET10 imeanza kuanzia mwanzo wa April na itamalizika
tarehe 30 Aprili 2016.
“Ofa
hii kutoka fastjet inaashiria kwa mara nyingine tena jinsi shirika letu
linavyosikiliza matakwa ya wateja wake”, alisema Mbogoro.
Mbogoro
alisema kwamba wateja wanaweza kilipia nauli zao kupitia mitandao ya
Tigo-Pesa, Airtel Money, M-Pesa and pia kupitia NMB Mobile Cash katika
tawi lolote la Benki ya NMB.
“Wateja
wanashauriwa kukata tiketi mapema ili kufurahia nauli za bei nafuu
zaidi na pia wanaweza kulipia kupitia m.fastjet.com or www.fastjet.com.” alishauri Mbogoro.






















No comments :
Post a Comment