Friday, April 29, 2016

Bomba la mafuta kukamilika Juni mwaka 2020.


 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea uzoefu wa Tanzania kwenye
ujenzi wa miradi  ya mabomba ya gesi na mafuta katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi  Irene  Muloni na kulia ni  Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini  Uganda, Dk. Fred Kaliisa (kushoto)
akifafanua  jambo katika kikao hicho. Kulia ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha akifafanua jambo katika mkutano huo.
 Wataalam kutoka Wizara, taasisi na makampuni ya mafuta kutoka Tanzania na Uganda wakifuatilia
kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na mwakilishi kutoka kampuni ya Total
katika mkutano huo.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI KIKAO KAZI CHA MAKAMANDA WA POLISI, WANASHERIA WA SERIKALI WAFAWIDHI WA MIKOA NA WAKUU WA UPELELEZI WA MIKOA NA VIKOSI.

JA1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali,  Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center
JA2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali,  Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center
JA4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na viongozi wengine wakati wimbo wa Jeshi la polisi ukipigwa. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola, Kushoto kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harison Mwakyembe , Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad  Yusuph Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Ernest Mangu.
JA5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convention Center kwa ajili ya ufunguzi wa rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi.
JA6 
Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
JA7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kabla ya kufungua kikao kazi hicho.
JA8 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kufungua kikao kazi hicho.
JA9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa mara baada ya kufungua kikao kazi chao katika ukumbi wa Dodoma Convention Center mjini Dodoma.
JA10 
Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakiimba Wimbo wa Jeshi la Polisi kabla ya ufunguzi wa Kikao kazi hicho.
JA11 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga
JA12 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na

Tafrija ya mchapalo baada ya Tigo na samaki samaki kuingia Ubia yafana

Wadau wakifurahi usiku wa jana wakati wa hafla ya mchapalo baada ya Tigo na mgahawa wa samaki samaki kuingia Ubia ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja  kwa kuleta  bidhaa/huduma zao kwa wateja wa kila mmoja.
 
Vinywaji murua kabisa 
 
Warembo wa Tigo wakiwa tayari kuhudumia wateja na wageni waalikwa wote 
 
Ulinzi ukiimarihwa kwa  wageni waalikwa na  wateja wote
 
Mtaalamu wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo Samira Baamar (kulia ) akiwa katika pozi na wafanyakazi wenzake Ummy Mtiro na Natasha 
 
Mhudumu wa Samaki akitabasamu na kuwakaribisha wageni waalikwa 
 
Blogger na mdau wa mitandao ya kijamii John Kiandika akiwa katika pozi na mkewe wakati wa hafla usiku wa jana 
 
Mmoja ya wageni waalikwa akipata maelezo kuhusu huduma ya Tigo 4g kutoka kwa mhudumu
 
Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos
 
Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout akifurahi jambo na wafanyazi wa tigo wakati wa hafla hii
 
Watangazaji maaruf wa kituo cha Clouds tv Hudson Kamoga na Sam sasali wakiwa pamoja kupata maelekezo kuhusa huduma ya intanet ya kasi ya Tigo 4G kwenye hafla hiyo.
 
 
Mhudumu akiandaa chakula 
 
Wahudumu wa samaki samaki wakiwa katika pozi 
 
wadau wakiwa katika pozi 
 
Taswira ukumbini 
 
Mdau John kiandika na mkewe wakipata maelezo zaidi kuhusu huduma ya Tigo 4g 
wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja 
 
 
 Tigo ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania,ikijulikana kama“nembo ya maisha ya kidijitale yanayojitosheleza”.
 ………………………………………………………………………………………………………
Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedhaza kwenye mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS, Tigo Music ( Deezer)na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.
 
Intaneti ya Tigo ya 3G inatoa huduma bora kwa wateja wake katika mikoa yote nchi nzima, na Hivi karibuni Tigo imezindua mtandao wa 4G ambao kwa sasa unapatikana Dar es Salaam nzima, na unatarajiwa kuzindualiwa nchi nzima.  Kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014 pekee kampuni ilizindua zaidi ya minara mapya 500 yenye mtandao wa Tigo nakufanya kuwa zaidi ya maeneo 2000 ya mtandao na inapanga kuongeza uwekezaji wake mara mbili ifikapo 2017 katika suala la upatikanaji wa mtandao na kuongezauwezo wa upatikanaji wa mtandao kwa maeneo yasiyofikika kabisa vijijini.  
 
Pamoja na kuwa na zaidi ya wateja milioni 10 waliosajiliwa, Tigo imeajiri zaidi ya watanzania 300,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wa wawakilishi wa huduma kwawateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.
 
 Tigo ni nembo kubwa ya kibiashara ya kampuni ya Millicom, kampuni ya kimataifa  inayoendeleza maisha ya kidijitale katika nchi 11 pamoja na shughuli za kibiashara katika Afrika na Amerika yaKusini na ina ofisi kubwa Ulaya na Marekani.
Ukiwa ni mgahawa unaoongoza kwa vyakula  vinavyotokana na mazao ya baharini  na vinywaji  nchini Tanzania, Samaki Samaki  inamiliki migahawa mitatu  ambayo ipo Mlimani City
(Ubungo/Mwenge), City Centre (kwenye makutano ya Barabara ya Samora na Mirambo) na Samaki Samaki  kwenye Barabara ya Haile Selassie.
Tangu kuanzishwa kwa tawi la Mlimani City mwaka 2007 tumeshuhudia kupanuka kwa  Migahawa  ya Samaki Samaki  hadi matawi miwili  zaidi ndani ya jiji la Dar es Salaam katika kipindi cha miaka mitano ya uendeshaji wake,  kuongezeka kwa wateja ambao wanafikia hadi 1,000 kwa siku ndani ya matawi hayo,  kuongezeka  kuimarika  kwa nembo yetu ya biashara  na kutambuliwa na umma,  kupatikana kwa fursa za ajira kwa wazawa, jamii kutuunga mkono kupitia Mfuko wa Samaki Samaki ( Samaki Samaki Foundation) ambao unalenga kuwasaidia  wahitaji  kwa kutoa misaada ya kuwajibika kwa jamii,  jamii imeweza kutufikia  kwa kutumia  video na muziki uliorekodiwa  katika kukuza  nembo yetu kupitia Samaki Samaki Fleva na kuuza  bidhaa zetu nyingine  ambazo hazihusiani na chakula  zikiwemo kofia, fulana  na CD za muziki.
  Dira ya Samaki Samaki ni   kushikilia nafasi yake  nchini Tanzania  kwa kukua hadi mikoa mingine nchini  na hata baadaye  kusambaa hadi  kona nyingine za Afrika na dunia kwa ujumla. Kwa hivi sasa  inaangalia Mwanza na Arusha  kama vituo vya kuanzia kusambaa hadi mikoa mingine.

MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA

G2Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Mbunge  wa Ilala  Azzan  Mussa Zungu, bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
G3 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Angeline Mabula bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
G5 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
G6 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Butiama , Nimrod Mkono kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
G7 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na wabunge Ahmed Shabiby wa Gairo (kushoto) na Suleiman Ahmed  Saddiq wa Mvomero, kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
G8 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Jovago: to reach our goals in 2016, Setbacks in Tourism sector should not be looked into one perceptive

index
With the strategies to increase 2 Million number of Tourist arrivals in 2017; JovagoTanzania explains that the gap in Tanzania’s tourism sector should be one of the core factors for development in 2016/2017.
Addressing  journalists in Dar Es Salaam, Lilian Kisasa, Jovago’s Pr and Marketing Manager, exposed the statistics from Tanzania Tourism board which shows that, the number of tourist arrivals increased to 1,077,058 in 2012, 1,095,884 in 2013 and 1,140,156 (2014). This progress is a promising signs that Tanzania is close to reaching its goal of 2M arrivals in 2017.
We can increase the number of visitors by not looking at just one category; we really need to focus on the purpose of visits, how to improve infrastructure and what kind of hospitality we should provide”. She added
Nevertheless, the statistics from the Tanzania Tourism Board shows that almost 56% of international travelers use airport as a mode of transport, only 38% use roads, while 0.5% opt for railway and the remaining travel by Water. This shows there are still unequal improvements in terms of the transport systems in the country.
However, she added that in order to improve the direct contribution of the tourism sector in 2016, there is need to promote domestic tourism; which covers only 40%.  International tourists contribute to the remaining 60%.
In addition, the Country Manager of JovagoTanzania Mr Andrea Guzzoni noted that 2016 is a year of change and improvements. According to Andrea, there are trends in visitors’ preferences, with the bottom line being value for money.
Jovago has planned to promote the best secured and classic accommodation in Tanzania in 2016. The leading online booking company noted that Wireless services, swimming pools, airport pickup services, Ac, free breakfast and the best customer service are top of the determining factors in the hotel industry.
The statistics shows that 80% of visitors travel for leisure, recreation and holiday, while only 5% travel for business and professional purposes and the rest travel to visit relatives and in transit. There is therefore need to improve services that suits all of the travelers’ needs

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI-MNH- YAWEKA MIKAKATI KUHAKIKISHA WATOTO WANAOZALIWA NA MATATIZO YA KUTOSIKIA WANAPATIA MATIBABU.

C1 
Mtaalam wa masikio Fayaz Jaffer akitoa elimu kwa wazazi / walezi , jinsi ya kutunza kifaa kinachomsaidia mtoto mwenye matatizo ya kusikia kuweza kusikia na kuwasiliana. Mtaalam huyo ametoa elimu hiyo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- alipokuatana na wazazi ambao watoto wao walifanyiwa upasuaji nchini India na kuwekewa kifaa hicho.
C2 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili –MNH- Profesa Lawrence Museru akielezea mipango ya MNH katika kuhakikisha huduma hiyo inakuja kutolewa hapa MNH kwa siku zijazo
C5 
Baadhi ya wazazi wakimsikiliza mtaalam wa Masikio Fayaz Jaffer leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH.
C3Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru pamoja na Mtaala wa masikio Fayaz Jaffer wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto ambao walifanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa maalum cha kuwasaidia kusikia ili kuweza kuwasiliana.
C4 
Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Museru ( katikati) akiwa na Mkuu wa Idara ya Masikio , Pua na Koo Daktari Edwin Liyombo ( kushoto ) na Fayaz Jaffer .
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- imeweka mikakati ya kuhakikisha watoto wanaozaliwa na matatizo ya kutosikia wanapatia matibabu hayo katika Hospitali hiyo ili kuwawezesha watoto wengi wenye matatizo hayo kupata huduma hiyo kwa wakati.
Mikakati hiyo imeelezwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Museru wakati akizungumza na wazazi / walezi ambao walifika MNH kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao ambao wana matatizo ya kusikia sanjari na kupata maoni mbalimbali kutoka kwa wazazi hao.
Akifafanua Profesa Museru amesema kimsingi mahitaji ya matibabu hayo ni makubwa na upasuaji huo haufanyiki nchini  hivyo wagonjwa hutegemea matibabu hayo nje ya nchi na ambayo ni gharma kubwa .
“ Mpango uliopo sasa ni kuhakikisha huduma hiii inafika hapa MNH ili wagonjwa wenye matatizo hayo waweze kutibiwa hapa nchini kwasababu tuna wataalam wa kutosha , pia naamini hatua hiyo itawasaidaia wananchi wengi kupata  matibabu hayo ” amesema Profesa Museru.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masikio ,Pua na Koo wa MNH  Daktari Edwin Liyombo amesema tayari dokezo limeandaliwa ili kuiomba serikali kuanzisha program maalum itakayowasaidia Madaktari kupata mafunzo pamoja na kupata vifaa tiba ili upasuaji huo uweze kufanyika hapa nchini.
Kwa  mujibu wa Daktari Liyombo mgonjwa mmoja akipelekwa nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji hugharimu kati ya Shilingi Milioni 85 hadi Milioni 100  lakini endapo matibabu hayo yatafanyika hapa nchini gharama itapungua kwa kiasi kikubwa.
Akizungumzia kuhusu utaratibu wa kukutana na wazazi  ambao watoto wao wana matatizo ya kusikia, Daktari Liyombo amesema utaratibu huo ni endelevu kwani una lenga kufuatilia maendeleo ya mtoto na kumuwezesha mzazi kupata ushauri wa kitaalam , leo zaidi ya wazazi 40 wamejitokeza MNH kwa ajili ya kukutana na watalaam .

StarTimes yawaletea wateja wake tamthiliya ya ‘Scars’

ST1 
Meneja wa Maudhui na Vipindi wa StarTimes Tanzania, Bi. Paulina Kimweri akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamthiliya ya ‘Scars’ itakayoanza kuonekana siku ya Jumatatu ya Mei 2, 2016 kupitia chaneli ya StarTimes Swahili. Akimsikiliza kwa makini katika uzinduzi huo uliofanyika katika ofisi za kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Uhusiano wa Umma, Bw. Muddy Kimwery.
ST2………………………………………………………………………………………………………….
  •      Ni tamthiliya inayohusu simulizi na visa vya kweli katika maisha ya watu.
  • ·         Itaonekana katika chaneli ya StarTimes Swahili, mahususi kwa vipindi vinavyotumia lugha ya Kiswahili inayoonekana pia nchini Kenya.
  • ·         StarTimes yahamasisha watanzania kuchangamkia fursa kwa kutengeneza filamu na tamthiliya ili ziweze kuonekana kupitia chaneli hiyo ili kupanua wigo wa mashabiki wao.
Katika kuboresha maudhui yanayotumia lugha ya Kiswahili, kampuni ya StarTimes Tanzania kupitia chaneli yake mahususi kwa vipindi vya Kiswahili ya StarTimes Swahili imewatangazia wateja wake ujio wa tamthiliya mpya na ya kusisimua ya ‘Scars au Makovu’ itakayoanza kurushwa siku ya Jumatatu ya mwezi Mei 2, 2016 saa 2:30 usiku.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tamthiliya hiyo Meneja wa Vipindi na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bi. Paulina Kimweri amebainisha kuwa tamthiliya ya ‘Scars’ itakuwa ni ya aina yake na kusisimua zaidi kwani inagusa zaidi maisha halisi ya kila siku.
“Tamthiliya hii ni tofauti na zingine kwani ndani yake ina visa na simulizi za kweli kabisa za maisha ya wahusika waliocheza ndani yake. Masuala kama ya changamoto mbalimbali wanazopitia watu kwenye familia zao kama vile mateso, udhalilishaji na unyanyasaji wanaopitia wanawake katika ndoa zao. Haya yote yatakuwa yakisimuliwa na kuonekana kwa wateja na watazamaji wa chaneli ya StarTimes Swahili.” Alielezea Bi. Kimweri
Meneja huyo wa Maudhui katika kampuni hiyo inayotoa huduma ya matangazo ya luninga kwa njia ya dijitali alifafanua zaidi kuwa, “Lengo kubwa la kuanzishwa na kuwepo kwa chaneli hii mahususi kwa vipindi vya Kiswahili si tu kuwaburudisha wateja wetu kwa maudhui mazuri bila pia kukuza lugha ya Kiswahili kwani chaneli hii inaonekana katika nchi za Tanzania na Kenya. Pia hutoa fursa kwa watayarishaji na wasanii wa vipindi vya Kiswahili baina ya nchi hizi. Hivyo basi hii ni fursa kubwa ya kufurahia wasanii wetu na kuipaisha lugha yetu ya Kiswahili ambayo kwa sasa inazidi kupaa katika anga za kimataifa.”
“Nina imani kubwa na tamthiliya hii ya ‘Scars’ kwamba itapendwa sana na wateja wetu kwani inagusa maisha halisi kwa simulizi zitakazopatikana ndani yake. Katika uchaguzi wa tamthiliya tunazotaka zionekane kwa wateja wetu huwa tunazingatia sana suala la ujumbe na mafunzo yanayopatikana ndani yake na si burudani pekee. Hivyo, basi ningependa kuchukua fursa hii kuwataka wateja wetu na watanzania wapenda tamthiliya tamthiliya kukaa mkao wa kula na kutega macho ya mbele ya luninga zao ifikapo siku ya Jumatatu na zinginezo kila ifikapo saa 2:30 usiku kwenye chaneli ya StarTimes Swahili. Nawaomba walipie kwani malipo yetu ni nafuu ili kila mtu aweze kufurahia huduma zetu.” Alihitimisha Bi. Kimweri
Mbali na tamthiliya mpya ya ‘Scars au Makovu’ pia kupitia chaneli ya StarTimes Swahili ambayo inaonekana kwenye kisimbuzi cha kampuni ya Startimes kwa nchi za Kenya na Tanzania pia kuna tamthiliya moto moto zinazoonekana kwa sasa kama vile; Urembo, Fihi, Majaribu, Kijakazi, Majaribu, Kivuli na Sumu la Penzi.
Chaneli hii imeanzishwa mahususi kabisa katika kuonyesha vipindi vyenye maudhui ya lugha ya Kiswahili ambapo lugha hiyo inazungumzwa katika nchi nyingi za Afrika ya Mashariki na Kati. Kupitia chaneli hii si tu kukuza lugha ya Kiswahili bali pia ni fursa kubwa kwa wasanii kuonekana na kujitangaza kupitia kazi zao ili ziweze kuonekana katika soko la Afrika ya Mashariki. Hivyo basi hii fursa kubwa kwa wasanii wa nchini Tanzania kuchangamkia faida zinazokuja na matangazo ya dijitali kwa kupeleka kazi zao katika kampuni ya StarTimes ili ziweze kuonekana hewani.

Ndugai akabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

B1Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda wake. Alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah
B3Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Bunge la Seniti la Burundi Mhe Reverien Ndikuriyo wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha.
B4 
pika wa Bunge Job Ndugai akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mhe Jeanne Uwimanimpaye wakati wa Mkutano huo.B5 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  (wa kwanza kulia) akifurahia jambo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega  (katikati) na Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha.
………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amemkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda wake.
Spika Ndugai alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Spika wa Bunge la  Seneti la Kenya, Spika wa Bunge la Kenya, Rais wa Bunge la Seniti la Burundi, Naibu Spika wa Bunge la Burundi, Naibu Spika wa Bunge la Rwanda, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki pamoja na Makatibu wa Mabunge ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki.
Akiukabidhi Uenyekiti huo Spika Ndugai aliwashukuru Maspika wenzake kwa ushirikiano walimuonesha katika kipindi chote cha  Uongozi wake na kumtakia kila la kheri Mwenyekiti  mpya wa jukwaa hilo.
Maspika wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hushika Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo Tanzania ilichukua Uenyekiti wa Jumuiya hiyo mwaka jana.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Kidega atashiki Uenyekiti wa Jukwaa hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kuukabidhi kwa Spika mwingine katika mkutano ujao unaotarajiwa kufanyika nchini Kenya.
Pamoja na mambo mengine mkutano huo wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki ulijadili maswala mbalimbali yanayohusiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki lilianzishwa mwaka 2008.

MSAJILI WA HAZINA ATOA UFAFANUZI KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UMILIKI WA HISA ZA SERIKALI KATIKA SHIRIKA LA USAFIRISHAJI DAR ES SALAAM (UDA)

index11 
Msajili wa Hazina Bw. Laurence Mafuru akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu umiliki wa hisa za Serikali katika Shirika la Usafirishaji Dar es salaam (UDA) na kubainisha kuwa Serikali inamiliki hisa 49% katika shirika hilo kinyume na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kuwa Serikali imeuza hisa zote kwa muwekezaji. Kulia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Gerald Chami.
index22 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Msajili wa Hazina leo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu faida za Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika kuongeza uwajibikaji na tija kwenye utumishi wa umma hasa kwa kuzingatia mapendekezo ya ripoti  ya mwaka 2014/2015.

WANANCHI JIJINI MBEYA WAJITOKEZA KUPATIWA DAWA ZA KINGA TIBA KWA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akitoa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa wananchi wa Jiji la Mbeya katika eneo la kituo cha Mabasi madogo(Daladala)Kabwe April 29 -2015 mara baada ya kuzindua rasmi .

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akiongoza zoezi la ugawaji wa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ,Magonjwa hayo ni Minyoo ya Tumbo,Matende ,Ngirimaji na Usubi, ambapo dawa hizo zinatolewa kwa wananchi wote kuanzia miaka Mitano (5)na kuendelea .


Wananchi eneo la kwabwe jijini Mbeya  stendi wakisubiri kwa hamu kupatiwa dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuanza rasmi mei 2 hadi 5 mwaka huu .Picha EmanuelMadafa,Jamiimojablog-Mbeya .

Jiji la Dar es salaa kunufaika na upatikanaji wa maji.

D1 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mahandisi Isack Kamwela akijibu swali la Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es salaam.
D2 
Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu Dkt. Abdallah Possi akijibu la Stella Ikupa Alex (Viti Maalum) alitaka kujua upatikanaji wa zabuni za kazi kwa watu wenye ulemavu leo Bungeni mjini Dodoma.
D3 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akifafanua jambo Bungeni leo mjini Dodoma.
D4 
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiuliza swali leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es salaam.
D5 
Silafu Jumbe Maufi (Mbunge Viti Maalum) akiuliza swali leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali iatamaliza tatizo la upungufu wa vifaa vya kufundishia somo la TEHAMA na walimu wa masomo hayo katika mkoa wa Rukwa.
D6 
Wabunge walio katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
D7 D8 
Baadhi ya wageni wakifuatilia mkutano wa Bunge leo mjini Dodoma.

WAZIRI WA NISHATI NA MAENDELEO YA MADINI NCHINI UGANDA MHANDISI IRENE MULONI AWASILI NCHINI TANZANIA

Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, aliwasili nchini jana usiku pamoja na Ujumbe wake kwa lengo la kushiriki Kikao cha Kujadili Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Kikao hicho kinafanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, aliwasili nchini jana usiku pamoja na Ujumbe wake kwa lengo la kushiriki Kikao cha Kujadili Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Kikao hicho kinafanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
UG1 
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon  (kulia) akisalimiana na Ofisa kutoka  Ubalozi  wa Uganda Nchini Tanzania  Nyiransanziyera Fredah (kushoto) aliyewasili katika  Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kumpokea Waziri wa  Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini  Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
UG2 
Katibu Mkuu wa  Wizara ya  Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini  Uganda, Dk. Fred Kaliisa (kushoto)  akibadilishana mawazo na  Balozi wa Uganda Nchini  Tanzania,  Dorothy Hyuha (kulia) mara baada ya Waziri wa  Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini  Uganda, Mhandisi Irene Muloni, kuwasili katika  Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ujumbe wake.
UG3 
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon  (kulia) akibadilishana mawazo na  Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya ujenzi wa mabomba kutoka  Uganda, Habumugisha Johnbosco (kushoto)  aliyeambatana na  ujumbe wa Waziri wa  Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini  Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
UG4 
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon  (kushoto) akibadilishana mawazo   na  Balozi wa Uganda Nchini  Tanzania,  Dorothy Hyuha (kulia)  mara baada ya Waziri wa  Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini  Uganda, Mhandisi Irene Muloni, kuwasili katika  Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ujumbe wake.
UG5 
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon  (kulia ) akizungumza na  Waziri wa  Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini  Uganda, Mhandisi Irene Muloni (kushoto) mara baada ya  Waziri  huyo pamoja na  ujumbe wake kuwasili katika  Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

TANZANIA COMMENDED FOR ENHANCING GIRLS EDUCATION IN ICT.

index 
The Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia H.E. Naimi Hamza Aziz(centre) poses for a picture with four student girls from Tanzania who participated in the Girls in ICT Day Celebrations in Addis Ababa under the auspices of International Telecommunication Union ITU held at AU Headquarters yesterday.
From left, Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary school, Dorice Mhanga from Kleruu Secondary School in Iringa, Khudhaima Bedran Sultan from Chasasa Secondary school in Pemba and Elician Yohana Kapi from Nyankumbu Secondary school in Geita .
(photo courtesy of Tanzanian Embassy in Addis Ababa Ethiopia).
……………………………………………………………………………………………..
Tanzania has been commended for its efforts in enhancing girl’s education in the country including rural areas with the aim of achieving gender balance by availing opportunities for girls to acquire skills in science and technical subjects including Information and Communication Technology (ICT).
The compliments were given yesterday (April,28,2016)  by the International Telecommunication Union (ITU) Regional Director for Africa Mr. Andrew Rugege when officiating at the opening ceremony of the International Girls in ICT Day Celebration held at the African Union Headquarters in Addis Ababa, Ethiopia.
“ Your Excellency Tanzanian Ambassador Naimi Aziz, I would like you to convey my regards to your government for its efforts in promoting ICT education for girls as witnessed by four girls who travelled all the way  from Tanzania to join us in this auspicious occasion. The girls, excelled in ICT competition organized by ITU,” he said praising the girls for successful creating useful IT applications that could be used for provision of social services.
The four girl students from Tanzania who were invited for the occasion in the Ethiopian capital, Addis Ababa include, Khudhaima Bedran Sultan from Chasasa Secondary school in Pemba Zanzibar, Elician Yohana Kapi from Nyankumbu Secondary school in Geita, Dorice Mhanga from Kleruu Secondary school in Iringa and Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary school in Dodoma.
Mr. Rugege said ITU estimates a skills shortfall of over two million jobs in the Information and communication technology (ICT) sector within the next five years adding that, Girls and young women who learn coding, apps development and computer science will not only be well-placed for a successful career in the ICT sector, but ICT skills are rapidly becoming a strong advantage for students in just about any other field they might choose to pursue.
“ Girls in ICT Day reminds us that ICTs help to improve the lives of people everywhere and especially in Africa – through better health care, better environmental management, better communications, and better educational systems that transform the way children and adults learn,” he said adding that the technology has been instrumental in creating job opportunities to African youths.
The girls participating in the school workshops were invited to the African Union in Addis Ababa HQ for a half day celebration where they had the opportunity to present their work and what they learned during the workshops to the ITU officials, the diplomatic community, AU Staff and ITU Delegates.
Six girls from various secondary schools in Tanzania who excelled in ICT competition coordinated by the ITU were invited for the ADDIS Girls in ICT Day celebration having emerged winners from zonal and eventually national ICT contests. Two of them could not travel to Addis Ababa to join their colleague due to delay in visa application.
The Four Girls are scheduled to return home on Saturday.
ITU’s Girls in ICT Day, is a global initiative aimed at raising awareness among girls and young women about the importance of digital skills for a successful professional career in all sectors and encouraging them to consider studies and careers in Information and Communication Technologies (ICT).
.ITU is the United Nations specialized agency for information and communication technologies – ICTs.
An organization based on public-private partnership since its inception, ITU currently has a membership of 193 countries and almost 800 private-sector entities and academic institutions. ITU is headquartered in Geneva, Switzerland, and has twelve regional and area offices around the world.
ITU membership represents a cross-section of the global ICT sector, from the world’s largest manufacturers and telecoms carriers to small, innovative players working with new and emerging technologies, along with leading R&D institutions and academia.
Founded on the principle of international cooperation between governments (Member States) and the private sector (Sector Members, Associates and Academia), ITU is the premier global forum through which parties work towards consensus on a wide range of issues affecting the future direction of the ICT industry.
From  Freddy Maro,
Tanzania Embassy Addis Ababa Ethiopia

HALMASHAURI ZA MASASI, NANYAMBA KUANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO SEKTA ZA UMMA AWAMU YA KWANZA MKOANI MTWARA

MKUU wa Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara, Christopher Magala akizungumza wakati wa kuhitisha mafunzo ya utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) yanayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID) na kutekelezwa katika Halmashauri 97 katika mikoa 13 nchini. Uzinduzi wa mradi wa PS3 ngazi ya mkloa wa Mtwara ilifanyika juzi mjini humo.
Mkoani Mtwara mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusisha Halamshauri ya Nanyamba na Halmashauri ya Wilaya Masasi.
Awamu ya pili ambayo itatekelezwa
mkoani mtwara kwa halamashauri saba zilizobaki utafanyika mwezi Februari na
Oktoba mwaka 2017 na utahusisha Halmashauri za Mjiwa Newala, Wilayaya Newala, Mji
wa Masasi, Wilaya ya Nanyumbu, Manispaa ya Mtwara, Wilaya ya Mtwara na Wilaya
yaTandahimba.
 Baadhi ya Maofisa wa Mradi wa PS3 pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Mtwara wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo.
 Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika mafunzo hayo.
 Mshauri wa Mradi katika Masuala ya Rasilimali Fedha, Dk Daniel Ngowi akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
 Mshauri wa Mradi katika Masuala ya Elimu, Dk Rest Laswai akifafanua jambo juu ya uimarishaji mifumo ya sekta za Umma katika nyanja ya elimu.
Continue reading →

Katibu wa Bunge aongoza kikao cha maandalizi ya mkutano wa Maspika wa Afrika Mashariki.

1Mwenyekiti wa kikao cha Makatibu wa Mabunge wa Afrika Mashariki Dkt. Thomas Kashilila akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano wa Maspika wa Afrika Mashariki leo jijini Arusha.
2Mwenyekiti wa kamati ya maadalizi ya mkutano wa Maspika wa Afrika Mashariki Dkt. Thomas Kashilila (kushoto) akiongoza kikao hicho leo jijnii Arusha. Kulia ni Katibu wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Bw. Keneth Madete.
6 
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa na Itifaki wa Bunge la Tanzania Jossey Mwakasyuka (kushoto) akiwa na Msaidizi wa Katibu wa Bunge la Tanzania ndugu Emmanuel Mpanda
5 
Makatibu wa Mabunge ya Afrika Mashariki wakitoka ukumbini baada ya ufunguzi wa kikao cha maandalizi ya mkutano wa Maspika wa Afrika Mashariki leo jijini Arusha.
4Mwenyekiti wa kikao cha Makatibu wa Mabunge wa Afrika Mashariki Dkt. Thomas Kashilila (wa kwanza kulia) akiwa na baadhi ya Makatibu wa Mabunge ya Afrika Mashariki wakiwa Jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Bw. Keneth Madete na Katibu wa Bunge la Kenya Bw. Justine Bundi (katikati).
3 
Makatibu wa Mabunge ya Afrika Mashariki na Baadhi ya Maafisa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa kikao cha maandalizi ya mkutano wa Maspika wa Afrika Mashariki leo jijini Arusha.

Tigo yatoa visima 12 vya maji kwa vijiji 12 Singida

 Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) akifungua bomba katika moja ya kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo pembeni yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mtinko  katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. 
…………………………………………………………………………………………………………
 Kampuni ya simu ya Tigo leo imekabidhi visima 12 vya maji  vyenye thamani ya 174m/- kwa vijiji 12 mkoani  Singida  ikiwa ni kuchangia juhudi za serikali  za kupunguza  uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano  iliyofanyika kwenye kijiji cha Mtinko wilayani Singida  mkoani Singida, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata  alisema ufadhili huo  umo kwenye mikakati ya kampuni ya kusaidia  jamii katika kunyanyua hali zao za maisha.
Vijiji vitakavyonufaika kutokana na ufadhili huo pamoja na wilaya zake kwenye mabano ni Lulumba (Iramba), Kisana (Iramba), Kisonzo (Iramba), Songambele (Iramba), Kinyeto (Singida Vijijini) na  Damankia (Ikungi). Vingine ni  Muungano (Ikungi), Ighuka (Ikungi), Kamenyanga (Manyoni), Sasajila (Manyoni), Mtinko (Singida Vijijini) and Kinampanda (Kinampanda).
 “Msaada huu ni sehemu ya uwekezaji wa Tigo kwenye miradi ya kijamii  ambayo inaleta tija kubwa kwa jamii. Tuna imani kwamba kupitia visima hivi, Tigo inasaidia  kutatua uhaba mkubwa wa maji  katika eneo hili la mkoa wa Singida  ambalo kwa kiwango kikubwa  limekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua katika kipindi cha miaka mine  iliyopita,” alisema Lugata.
 Aidha aliongeza kuwa uhaba wa maji  miongoni mwa  wilaya nyingi za Singida  umesababisha wakiazi wake  kupoteza muda mwinmgi kutafuta  bidhaa hiyo muhimu, jambo ambalo  Tigo inaamini  kuwa hivi sasa litafikia ukomo kutokana na upatikanaji wa visima hivyo.
 Makabidhiano ya visima hivyo yalihudhuriwa na kushuhudiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge  ambaye aliishukuru Tigo kwa ufadhili huo uliopatikana kwa wakati mwafaka akisema kwamba visima hivyo vitapunguza kwa kiwango kikubwa  uhaba sugu wa maji  uliolikumba eneo hilo  na kuchangia kukua ustawi wa jamii  kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akikata utepe katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akifungua moja ya bomba katika kisima   katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
 Hata hivyo, alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo  kuchangia kwenye juhudi kama hizo. Waziri Lwenge alisema, “Tunatoa shukrani za dhati kwa Tigo kwa kutuunga mkono kwenye juhudi zetu za kutatua  uhaba wa maji uliopo Singida na hata kwenye mikoa mingine nchini. Tuna imani visima hivi 12  vitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hili linaloikabili jamii kwa sasa”.

TANAPA YAKABIDHI MABATI 2800 KUSAIDIA UJENZI WA MAABARA NA ZAHANATI WILAYANI SERENGETI

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Marwa
Ryoba (kushoto) akipokea msaada wa mabati kutoka kwa Meneja Ujirani Mwema wa
TANAPA Bw. Ahmed Mbugi wilayani Serengeti.
 ……………………………………………………………………………
 
Na Jacquiline Mrisho – Dar es Salaam
 
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limekabidhi jumla ya mabati 2800
kwa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kusaidia ujenzi wa maabara
15 za shule za sekondari na zahanati zilizo katika Kata mbalimbali za wilaya hiyo.
Akikabidhi msaada huo Meneja ujirani mwema wa Tanapa, Ahmed Mbugi amesema
TANAPA imetoa msaada huo kusaidia Maendeleo ya Elimu na Afya katika wilaya
hiyo.
“Mabati haya ni msaada ambao tumeutoa kwa Wilaya ya Serengeti ikiwa ni
muendelezo wa misaada tunayoitoa kwa jamii hii ili kusaidia shughuli za
maendeleo wilayani hapa” alisema Mbugi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Naomi
Nnko aliongeza kuwa ujenzi wa maabara hizo kutawawezesha wanafunzi kusoma
masomo ya sayansi kwa vitendo, na hivyo kuongeza ufaulu katika shule za
sekondari wilayani humo.
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Juma Keya alishukuru
kwa msaada huo toka TANAPA na kuomba mashirika mengine ndani na nje ya Wilaya
ya Serengeti kushirikiana na Halmashauri hiyo kuleta maendeleo katika jamii.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Maftah
Mohammed  aliliomba shirika hilo
kuchangia upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari zilizopo
wilayani humo.
Mpaka sasa TANAPA imeisaidia Halmashauri hiyo kwenye ujenzi wa maabara
katika Kata ya Natta, uchimbaji wa marambo na ujenzi wa mabweni katika shule za
Sekondari.

UVCCM: SUMAYE ACHA KUMBUGHUDHI RAIS DK. MAGUFULI HUNA VIWANGO

 
Na Woinde Shizza, Kilimanjaro
Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema Waziri mstaafu Frederick Sumaye, hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na masuala ya utawala.
 
Sumaye ametakiwa amuache Rais Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwa sababu alipewa dhamana ya kuwa Waziri Mkuu lakini hakufikia hata thekuthi ya utendaji unaofanyika sasa.
 
Hayo yamesemwa jana na Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM wa kata mbili za Kwandele na Mbichi jimbo Rombo mkoani Kilimanjaro.
 
Shaka alisema anachokifanya Sumaye na baadhi ya wanasiasa muflisi wanaojaribu kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani wananchi wameyasahau.
 
Alisema kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika  utendaji na usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita Sumaye.
 
“Amekuwa waziri mkuu kwa miaka kumi kuliko waziri mkuu yeyote na kwa bahari mbaya sana ndiye waziri mkuu zero kuliko mwingine yeyote tokea tupate uhuru mwaka 1961 “alisema shaka.
 
Aidha Kaimu huyo katibu mkuu alimuonya sumaye akimtaka aache kumfuatafuata Dk Magufuli katika mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazichukua dhidi ya mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma nchini.
 
Alisema wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi iuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima alisema  kina sumaye na wenzake  wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi Rais kwa ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa.
 
“Sumaye aacha kufuatafuata Rais na kujifanya unajua wakati mambo yalikushinda wakati ukiwa PM, kama huna maneno ya kusema rudi Hanang ukalime maharage na karanga “alisema
 
Pia shaka aliwataka wananchi wa jinbo la Rombo kujitatayarisha ili kumpiga chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini kwasabahu ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
 
“Siku zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, selasimi hajui anavhokufanya wala hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo lake,lazima adui huyo apigiwe mwaka 2020 “alisisitiza shaka
 
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara moja tabia ya kushiriki na kuchagua vyama na wagonbea wa nafasi mbali mbali kwa ukabila, ujimbo au nasaba.
 
Raibu alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi ya asili au ujamaa.
 
“Tunachotaka kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni kumuasi baba wa Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, haiutuacha tukiwa tumegawahyika  , tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini, chadema acheni kwasabahu hilo ni baa au janga katika jamii “alisema Raib.
 
Jumla ya wananchi wapya 103 wa CCM na jumiya zake walijiunga na chama cha mapinduzi pia shaka alipata nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya timu za kata za makiidi na mahare wilaya Rombo.

JAMII YASHAURIWA KUWAPELEKA WATOTO KWENYE CHANJO

MPOKatibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Mpoki  Ulisubisye akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
………………………………………………………………………………………………………
Na Magreth Kinabo- Maelezo
 Jamii imeshauriwa  kuwapeleka watoto wote wanaostahili kupata chanjo    walio chini ya umri wa miaka mitano katika vituo vya afya ili waweze kupatiwa chanjo  ili kuweza kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vya watoto.
Kauli hiyo ilitolewa Aprili 27, mwaka huu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Mpoki  Ulisubisye wakati wa maadhimisho ya wiki ya chanjo nchini yaliyofanyika  kwenye hoteli ya Serena Jijini Dares Salaam.
Alisema  utoaji wa chanjo hiyo umeaanza Aprili 25 hadi 29 mwaka huu na  kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘ Kumilisha Chanjo,Epuka Ugonjwa wa Polio’. Hivyo  vItuo  vya kutolewa kutolea huduma za afya vinafunguliwa kuanzia saa 2: 00  asubuhi hadi saa 11.00 jioni.
“ Kila mmoja wetu anawajibu wa kuhakikisha  mtoto wake , mtoto wajirani au mlengwa mwingine yeyote anapewa haki ya chanjo ili kumzuia asipatwe na maradhi ambayo yanakingwa na chanjo au asiwe na hatari kwa wengine kwa kuwaletea ugonjwa,” alisema Dkt. Ulisubisye.
Aliongeza kuwa  chanjo  ni mikakati muafaka katika kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vya watoto, hivyo hupunguza gharama kubwa ambazo familia  zetu na taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu maradhi yanatokana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.
Alisema chanjo huzuia takribani vifo milioni mbili hadi tatu kwa kila  mwaka kutokana na maradhi yanayokingwa kwa chanjo duniani.
Aliyataja maradhi hayo kuwa ni Dondakoo, Surua ,Polio,Kifua Kikuu,Kifaduro,PepoPunda,Homa ya ini,homaya uti wa mgongo,kichomi na kuhara.

SERIKALI YAZIDI KUPAMBANA NA UGONJWA WA MALARIA NCHINI

indexNa Beatrice Lyimo-MAELEZO
27/04/2016
Kufanikiwa kwa juhudi za Kutokomeza ugonjwa wa Malaria kutaufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri na salama pa kuishi kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo na kuwawezesha mamilioni ya watu kufikia malengo yao kimaisha.
Hivi karibuni Tanzania imeungana na nchi nyingine Ulimwenguni kuadhimisha siku ya Malaria duniani ambapo ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo katika jamii.
Takwimu kutoka Shirika la Afya ulimwenguni WHO za mwaka 2002 zinaonyesha kuwa kila mwaka watu kati ya milioni 300 hadi 500 duniani wanapata ugonjwa wa malaria, kati yao watu milioni moja na nusu hufariki kutokana na ugonjwa huo.
Kulingana na takwimu hizo katika bara la Afrika watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano ndiyo wanaathirika zaidi na ugonjwa wa malaria ambapo kila mwaka watoto milioni tano wanakufa kwa ugonjwa huo barani Afrika.
Kwa mujibu wa WHO idadi  vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria hadi kufikia mwaka 2013 vilipungua kwa takriban asilimia 20 tu duniani kote katika muongo mmoja uliopita ambapo theluthi moja ya nchi 108 ambazo malaria ilikuwa imeenea zilitarajiwa kutokomeza ugonjwa huo katika kipindi cha miaka 10.
Kufuatia ufanisi mkubwa uliopatikana chini ya malengo ya maendeleo ya milenia, ni muhimu kuuendeleza ufanisi huu na kuutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria chini ya malengo ya maendeleo endelevu.
Kauli mbiu hiyo inaenda sambamba na lengo la kuwa na ulimwengu usio na malaria lilijumuishwa katika mkakati wa kiufundi wa kimataifa kwa ajili ya malaria 2016 hadi 2030, ulioidhinishwa Mei mwaka uliopita na baraza kuu la Afya duniani. Mkakati huo unalenga kupunguza kwa kiwango kikubwa maambukizi ya malaria ulimwenguni katika kipindi cha miaka 15 ijayo.
Continue reading →

Uchukuzi SC yawa ya tatu, kipa adaka penati 3

MO1Kipa Willium Barton wa Uchukuzi SC akikaa tayari kupangua penati ya kipa mwenzake wa Tanesco Hashim Yahya. Uchukuzi ilitwaa ushindi wa tatu kwa penati 3-2.
MO2Abubakar Mwamachi (9) wa Uchukuzi SC akikokota mpira huku mlinzi wa Tanesco Juma Rajabu akiwa ameshika ardhini.
MO3Wachezaji wa michezo mbalimbali wa timu ya Uchukuzi SC wakishangilia baada ya timu ya soka kutwaa ushindi wa tatu kwa penati 3-2 dhidi ya Tanesco.
MO4Omary Kitambo (4) wa Uchukuzi SC akiwania mpira uliopigwa na Stanley Uhagile wa Tanesco. Uchukuzi ilitwaa ushindi wa tatu kwa penati 3-2.
…………………………………………………………………………………………………….
  • Kamba wanaume watwaa ubingwa
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU ya soka ya Uchukuzi SC jana ilitwaa ushindi wa tatu wa mashindano ya Mei Mosi, baada ya kuwashinda Tanesco magoli 3-2 kwa mikwaju ya penati, katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Ushindi wa Uchukuzi SC ulichagizwa na kipa wao mahiri William Barton aliyeweza kudaka penati tatu kati ya tano zilizopigwa na Tanesco.
Baada ya ushindi huo, Barton alimwaga machozi ya furaha, kwani alidaka penati zilizopigwa na kipa mwenzake Hashim Yahya, Khalifa Shekuwe na Abdallah Magubile.
Penati za Uchukuzi SC zilifungwa kwa ufundi stadi na Fidelis Kyangu, Masoud Masoud na Kado Nyoni, wakati waliokosa ni Omary Said ‘Chidi’ na Seleman Kaitaba.
Hatua ya penati ilifuatiwa baada ya timu hizo kutoka suluhu katika dakika 90 za kawaida na kwa mujibu wa sheria za mashindano hayo hakina nyongeza ya dakika 30 na inapigwa mikwaju ya penati moja kwa moja.
Kocha wa Uchukuzi SC, Elutery Muholeli alisema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa, na wachezaji wake walicheza kwa kujituma, na dhamira yao ilikuwa ni kutwaa ubingwa, lakini bahati haikuwa yao na wamebahatika kutwaa ushindi wa tatu.
Naye kocha wa Tanesco, James Washokera alikiri wachezaji wake kukosa umakini kutokana na kikosi chake kukosa wafungaji, na aliamua kuwatumia viungo zaidi, ili kufunga magoli lakini walishindwa kutokana na kucheza nafasi sio yao.
“Unajua hii timu yetu ilitakiwa kuwa ni kombaini ya Tanesco Tanzania nzima, lakini haikuwa hivyo na badala yake wametoka sehemu chache na nilitarajia ningechagua wafungaji kutoka mikoani, lakini sikupata nafasi hiyo, ila hili tatizo huu ndio mwisho wake na mwakani tutakuja kamili kwani nitahakikisha ninazunguka na kupata wachezaji sehemu zote,” alisema Washokera.
Pia Uchukuzi wanaume wameibuka mabingwa wa mchezo wa kamba baada ya kumaliza ikiwa imejikusanyia pointi 10, na haikuwahi kuvutwa na timu yeyote tangu michuano hiyo ianze.
Nayo CDA ‘Watoto wa nyumbani’ wameshika nafasi ya tatu katika mchezo wa netiboli wakiwa na pointi tatu sawa na Tanesco iliyoshika nafasi ya nne , lakini wanatofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa, huku TPDC ikiburuza mkia ikiwa haijapata pointi yeyote.

MWANAHABARI MTOTO NA MWANAMAZINGIRA WA UN, GETRUDE CLEMENT ALIVYOPOKELEWA JIJINI MWANZA.

Shujaa Wetu,
Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa Umoja wa Mataifa UN kutoka Mwanza Tz, Getrude
Clement (16) jana amewasili nyumbani Jijini Mwanza majira ya saa tatu usiku na
kupokelewa kwa shangwe na ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege Mwanza.
 
………………………………………………………………………………………………….
Alihudhuria
Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliohusu Mabadiliko ya Tabia nchi
(Climate Change) ambapo alihutubia õakiwakilisha kundi la Watoto na Vijana
duniani.
 
Kutoka Kushoto Pichani ni Brightius Titus ambae ni Katibu wa Mtandao wa Watoto na Vijana Mkoani Mwanza MYCN, Katikati ni Getrude mmoja wa Watoto wa Mtandao huo na Kulia ni Shaban Magana ambae ni Mwenyekiti wa MYCN.
“Kitu ambacho nimejifunza ni kupata kujiamini zaidi kwa sababu ule Mkutano ulihudhuriwa na watu wengi, wakiwepo viongozi kutoka zaidi ya nchi 170 wanachama wa Umoja wa Mataifa. Wameniasa kusoma zaidi ili kufikia malengo yangu ambapo nitaendelea kuzungumza na wananchi pamoja na viongozi wao juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo nitakuwa balozi wao”. Alisema Getrude.
“Wazazi wawaruhusu watoto wao katika kushiriki shughuli mbalimbali za vikundi ili waweze kujiamini zaidi katika kufikia ndoto zao”. Anasema Mtoto Mwanahabari Getrude.
Shabani Njia (Kulia) ambae ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana na Watoto Mkoani Mwanza MYCN akizungumzia mapokezi ya Mwanahabari na Balozi wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa akiwakilisha kundi la Watoto na Vijana Getrude Clement
Clement Leon ambae ni baba mzazi wa Getrude akizungumzia mapokezi ya mwanae katika Uwanja wa ndege Mwanza.
Rizik Athman ambae ni mzazi wa Getrude akizungumzia mapokezi ya mwanae katika Uwanja wa ndege Mwanza ambapo anafurahishwa na hamasa aliyonayo mtoto wake ikiwemo kujiamini katika masuala mbalimbali ikiwemo ya habari.
Getrude (Katikati) akiwa na Wazazi wake, Clement Leon (Kushoto) pamoja na Rizik Athman (Kulia).
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN, mapema wakifurahia jambo wakati wakimsubiria Getrude
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN wakiwa pamoja na Getrude.
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN, wakifurahia na Getrude katika picha ya pamoja.
Mapokezi ya Mtoto Getrude
Mapokezi ya Mtoto Getrude
Mapokezi ya Mtoto Getrude, Wengi walimsubiria kwa hamu kubwa.
Shuja, Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa UN Getrude Clement baada ya kuwasili Jijini Mwanza.
Tazama HAPA Getrude akihutubia katika Mkutano wa UN

NICO NJOHOLE NA RENATUS NJOHOLE WAWASILI DALLAS, MTANANGE WA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI

Renatusi Njohole akiwa katika picha ya pamoja na kaka yake
 Benchi la ufundi la Yanga Bwn. Gerry Mshana(kulia) akipata picha ya kumbukumbu na Nico Njohole siku ya Alhamisi Dallas, Texas. Nico na Renatus wamekuja maalum kuhudhuria mkutano wa DICOTA na kuchezea Simba kwenye mtanange wa watani wa jadi.
  Kutoka kushoto ni Gerry Mshana, Mary Maswanya (dada mkubwa wa Nico na Renatus), Renatus, Nico na Rais wa DICOTA, Ndaga Mwakabuka walipopata picha ya kumbukumbu. 
 Rais wa DICOTA Bwn. Ndaga Mwakabuta akiwa katika picha ya pamoja Nico na Renatus
 Kutoka kushoto ni Jerry, Nico, Ndaga Mwakabuta, Renatus, na Gerry Mshana wakiwa kwenye picha ya pamoja

DC KINONDONI AANZA MAPAMBANO DHIDI YA WATUMISHI HEWA

 
NA BASHIR NKOROMO
Mkuu wa Wilaya a Kinondoni, Dar es Salaam,  Salum Hapi amesema, Serikali katika wilaya hiyo imebaini kuwa  imepoteza zaidi ya sh. bilioni 1.331 kwa kuwalipa wafanyakazi hewa wapatao 89.hadi sasa.
Amesema, baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo siku saba zilizopita, amesimamia maofisa wake kufanya uchunguzi na kubaini kuwa pamoja na wafanyakazi hao hewa ambao wameisababishia serikali kupoteza sh. 1, 331, 734, 881 pia wapo watumishi vivuli wapatao 8823 ambao wanalipwa mishahara wakati  hawafanyi kazi katika maeneo husika kutokana na sababu mbalimbali.

Hapi amesema wafanyakazi hao vivuli ni pamoja na waliohamia idara nyingine lakini wakati wanalipwa huko walikokwenda bado wanalipwa katika idara walizokuwepo mwanzo na kwamba wengi wao wapo katika Idara ya Elimu.

Akzungumza na waandshi wa habari Ofisini kwake, leo, Hapi amesema, amebaini hatua hiyo baada ya kufanya uchunguzi wa kinaa na kuwabinya wasimamizi katika idara mbalimbali za utumishi, na kwamba ameelekeza mwanasheria kuchukua hatua haraka ili wahusika wachukulie hatua za kisheria.
Katika hatua nyingine, Hapi amewataka wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la machinga, kuwa kuanzia kesho ni marufuku kufanya shughuli zao katika maeneo yasiyo mahsusi kwa biashara katika wilaya ya Kinondoni.

Amesema, agizo hilo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kutaka ifanyike hivyo kwa lengo la kulifanya jiji liwe safi kuunga mkono agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuhimiza usafi nchi nzima.
Hapi amesema, machinga wote kama wahanitaji kufanya biashara zao ni lazima waende katika maeneo yaliyopangwa, ambayo alisema, hapo mengi na bado yana nafasi za kutosha kwa ajili ya kutumika kufanyia biashara.

Waziri wa Afya Afunga Mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Dar

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo, akifunga rasmi Mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) leo jijini Dar es Salaam.  
 
Mwenyekiti wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Geofrey Semu akizungumza katika mkutano wa THERIA leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulioshirikisha wanachama wa THERIA kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania umefanyika kwa siku mbili mfululizo, Aprili 27 na 28, 2016 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wake kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa THERIA uliofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.
 
Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (kulia) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu, akimkabidhi cheti cha shukrani mmoja wa wanachama waanzilishi wa THERIA kwa kufanikisha mkutano huo.
 
Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (kulia) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu, akikabidhi cheti cha shukrani kwa baadhi ya wanachama waliojitoa kufanikisha mkutano wa THERIA.
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa katika mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa katika mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS)leo jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa katika mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS)leo jijini Dar es Salaam.

Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (hayupo pichani) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu. Mkutano huo wa siku mbili umefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja kati ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (katikati mwenye suti ya kijivu) pamoja na viongozi wa chama hicho na wageni wengine waalikwa.

Picha ya pamoja kati ya meza kuu, mgeni rasmi na viongozi na kamati ya mkutano huo.

UONGOZI WA WANAFUNZI WA CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA ZANZIBAR (ZIFASO) WACHAGUA VIONGOZI WAPYA.

z1Wagombea  wa nafasi  ya Rais wa ZIFASO Juma Shirazi Hassan a Makamu wake Zuwena Jaku Hassan (wa katikati) wakiongozwa kuingia katika kampasi ya Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar kiliopo Chwaka Mkoa Kusini Unguja tayari kwa ajili ya kupiga kura.
z2Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi  ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar Sabrina Yussuf Shaaban akielezea juu ya utaratibu mzima wa kupiga kura ili kupata viongozi wapya wa ZIFASO .
z3 
Mlezi wa wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar Maalim Wazir Hamad akitoa nasaha  zake kwa wapiga kura ambao ni wanafunzi wote wa chuo hicho.
z4 
Mgeni rasmi katika uchaguzi huo ambae ni Afisa kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mohd Ali Abdalla akiwanasihi  wasimamizi na wapiga kura kuendesha uchaguzi katika misingi ya haki.
z5Mgombea  pekee wa nafasi ya Rais wa ZIFASO  Juma Shirazi Hassan akipiga kura yake  katika uchaguzi huo uliofanyika chuoni Chwaka Mkoa Kusini Unguja.
z6Wasimamizi wa uchaguzi wakiwa pamoja na mawakala wa wagombea wakihesabu kura mara baada ya kukamilika zoezi la upigaji kura.
z7 
Mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wakijumuisha kura ili kujua mshindi katika uchaguzi huo.
z8 
Rais mpya wa ZIFASO na Makamu wake Juma Shirazi Hassan na Makamu wake Zuwena Jaku Hassan wakitoa shukrani na nasaha zao  baada ya kuchaguliwa kuongoza Jumuia hiyo kwa mwaka 2016/2017. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo.

Supastaa wa Malawi Tay Grin awapania Diamond na Vanessa

unnamed
Rapper na supastaa wa Malawi, Tay Grin, amedai kuwa ana mpango wa kuwashirikisha Diamond Platnumz na Vanessa Mdee. Tay ambaye hivi karibuni aliachia video ya wimbo ‘Chipapapa’aliomshirikisha msanii wa Nigeria, 2 Face Idibia, amesema kuwa hao ni wasanii wa Tanzania anaowakubali zaidi.
“Ningependa sana kufanya kazi na wasanii wa Tanzania,” anasema Tay.
“Napenda jinsi wasanii wa Tanzania wanavyoimba. wako kimuziki sana hata kama sizungumzii Kiswahili, muziki wao unasikika vizuri na ni mtamu. Nimesikiliza wasanii kama Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Alikiba na muziki wao wa Bongo Flava. Nadhani Nyau Music inaweza kuchanganyikana vizuri na wasanii hawa wakali. Kwa sasa ninafanyia kazi wimbo na Vanessa Mdee na nina matumani ya kumpata Diamond Platnumz kwenye wimbo huo,” ameongeza.
Tay amesema anawakubali wawili hao kutokana na jinsi wanavyojituma na mapenzi yao makubwa kwenye muziki.
“Nimekuwa nikifuatilia kazi zao kwa muda sasa na naweza kusema kuwa wamenishika.”
Tay ni msanii anayeheshimika zaidi nchini Malawi na amewahi kutumbuiza mara mbili kwenye shindano la Big Brother Africa na amewahi kutajwa zaidi ya mara tano kuwania tuzo za Channel 0.
Amewahi kushirikisha wasanii kama Sway (UK), Brick & Lace (Jamaica),  Naeto C, Ice Prince,  na 2face wa Nigeria), Wahu na Nameless  wa Kenya,  Double HP, Da Les na Lira wa Afrika Kusini na wengine.

WANANCHI WA ITOBO, ITIRIMA – SIMIYU WAASWA KUZAA KWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO

Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima – Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.


Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima – Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima.
 —
Na Cathbert Kajuna – Itirima, Simiyu.
Wananchi wa Kijiji cha Itobo, Itirima – Simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasio kuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi.
Akizungumza katika mafunzo ya Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio vijinini kuacha dhana ya kuzaa ovyo kama wanyama bila mpangilio jambo linalowafanya kuendea kuwa maskini.
“Nawaasa wananchi wa Kijiji cha Mitobo kuache mila potofu za kuzaa kila mwaka mimba kila mwaka mtoto maana mtakosa kuwa na maendeleo, nnakuta mtu anawatoto 10 – 15 jambo linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa kuwahudumia,” alisema Meena.
Bi. Meena aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mitobo kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango.
Akiongea mara baada ya kumaliza mafunzo hayo Bi. Ester Meena alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa jambo linaloleta faraja kwa vile linaweza kupunguza idadi ya watu.

Kongamano la Uwekezaji Tanzania na Urusi

me1Makamu wapiliwa Rais waSerikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. BaloziSeif  AliIddiakifunguakongamano la kujadili FursazaUwekezajikati ya Tanzania na Urusi lililofanyika jana jijini Dar es salaam ambalolimewakutanishawafanyabiasharambalimbaliwaMataifahayomawili
me2Waziri waViwandaBiashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijageakifafanuakwawaandishiwahabari janaJijini Dar es salaam kuhusufaidazaushirikianowakibiasharakati ya Tanzania na Urusiutakaochangiamaendeleo katika sektazaKilimo,Usafirishaji na Nishatihapanchini.
me3WaziriwaViwanda na BiasharawaUrusi Mhe. Denis Manturovakizungumzakwenyekongamano la kujadilifursazaUwekezajikati ya Tanzania naUrusilililofanyikaleoJijini Dar es salaam.
me4 
Baadhi ya washirikiwakongamano la kujadilifursazaUwekezajikati ya Tanzania na urusiwakifuatiliamadawakatiwakongamanohiloleoJijini Dar es salaa.
me5MakamuwaPiliwa Rais waSerikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. BaloziSeif  AliIddi(kushoto) akizungumzajambo na MwenyekitiwaTaasisi ya SektaBinafsi Tanzania Bw. Reginald MengileoJijini Dar es salaam marabaada ya kufunguakongamano la Uwekezajikati ya Tanzania na Urusi.
me6MakamuwaPiliwa Rais waSerikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. BaloziSeif  AliIddi(wannekutokakushoto)akiwa na WawakilishiwaSerikali ya Urusi,anayefuatani Waziri waViwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijageakifuatiwana  WaziriwaViwandaBiashara na MasokowaSerikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amina Salum Ali.
Pichazote na (Fatma Salum- MAELEZO)

No comments :

Post a Comment