Thursday, March 31, 2016

UTOAJI MIMBA USIO SALAMA NI JAMBO LA KAWAIDA NCHINI TANZANIA NA NI SABABU KUBWA YA VIFO VYA WAJAWAZITO

0001
Dr. Neema Lusikamayki Mkurugenzi wa Huduma Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  na Andrea B. Pembe Kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili wakikata utepe wakati akizindua ripoti ya utafiti wa utoaji wa mimba usiosalama uliofanyika nchi nzima ambao umefanyika kwenye ukumbi wa JNICC leo jijini Dar es salaam leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 
001
Dr. Neema Lusikamayki Mkurugenzi wa Huduma Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  na Andrea B. Pembe Kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili wakionyesha utafiti huo mara baada ya kuuzindua rasmi.
1
Dr. Neema Lusikamayki Mkurugenzi wa Huduma Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akisoma hotuba yake kabla ya kuzindua utafiti huo katika uzinduzi uliofanyika kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam.
03
Profesa PS Muganyizi kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Muhimbili   akiungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi huo  katikati ni Sarah Keogh kutoka taasisi ya Guttmacher ya nchini Marekani  na kulia ni Andrea B. Pembe Kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili.
3
Baadhi ya wataalamu na waandishi wa habari mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
4
Baadhi ya wataalamu namaofisa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
…………………………………………………………………………………………………………….
Utafiti mpya Watoa Makadirio ya Kwanza Kitaifa ya Matukio ya Utoaji Mimba Nchini
Katika utafiti wakilishi wa kwanza kitaifa kuhusu matukio ya utoaji mimba na huduma baada ya kuharibika kwa mimba nchini Tanzania, watafiti waligundua kwamba utoaji mimba kwa siri hutokea mara nyingi na huchangia kwa kiasi kikubwa kwenye vifo na kuumia kwa wajawazito. Utafiti huo, uliofanywa na watafiti kutoka taasisi ya Guttmacher iliyoko Marekani, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili zilizoko hapa Tanzania, waligundua ya kwamba makadirio ya mimba 405,000 zilitolewa nchini ndani ya mwaka 2013, nyingi zikitolewa kwa taratibu ambazo si salama na kuhatarisha maisha ya wanawake. Kutokana na mchanganyiko wa sheria tata na yenye vizuizi vingi ya utoaji mimba ya Tanzania, wanawake hutafuta huduma za utoaji mimba zinazofanyika kisiri na ambazo si salama.
Watafiti hao, ambao walifanya utafiti kwenye vituo vya afya, miongoni mwa wataalamu wa afya na kufanya mapitio ya taarifa za idadi ya watu na uzazi, wamekadiria kwamba wanawake 66,600 walipewa huduma baada ya kuharibika kwa mimba kwenye vituo vya afya kutokana na matatizo yaliyotokana na utoaji mimba usio salama ndani ya mwaka 2013. Hata hivyo, karibu wanawake 100,000 ambao walipata matatizo hawakupata matibabu ambayo waliyahitaji. Watafiti wanatumaini kwamba matokeo yao yatasaidia kutaarifu  juhudi zinazoendelea nchini Tanzania kupunguza uwiano wa vifo vya wajawazito, ambao umebaki kuwa miongoni mwa iliyo juu zaidi duniani.
“Kwa kutambua kuwa utoaji mimba usiokuwa salama ni chanzo kikuu cha vifo vya wajawazito, Serikali ya Tanzania imepanua wigo wa upatikanaji wa huduma baada ya kuharibika kwa mimba katika muongo mmoja uliopita, lakini mapungufu makubwa bado yapo na wanawake wengi hawapati huduma wanazohitaji,” alisema Sarah C. Keogh, mtafiti mwanasayansi mwandamizi wa taasisi ya Guttmacher na mwandishi kiongozi wa utafiti huo. “Utafiti huu unabainisha mapungufu hayo na kusaidia kuunda mikakati kuhakikisha kuwa kila mwanamke wa Kitanzania anayehitaji anaweza kupata huduma baada ya kuharibika kwa mimba inayoweza kuokoa uhai.”
Kiwango cha kitaifa cha utoaji mimba nchini Tanzania—36 kwa kila wanawake 1,000 walio kwenye umri wa uzazi—kinafanana na viwango vya nchi nyingine za Afrika Mashariki. Hata hivyo, ndani ya Tanzania viwango vya utoaji mimba vinatofautiana kwa ukanda. Viwango vya juu ya utoaji mimba hupatikana katika Kanda ya Ziwa (51 kwa kila wanawake 1,000) na Nyanda za Juu Kusini (47 kwa kila wanawake 1,000), na kiwango cha chini hupatikana Zanzibar (11 kwa kila wanawake 1,000). Viwango hivi tofauti vya utoaji mimba huhusishwa kimsingi na utofauti katika viwango vya matumizi ya njia za uzazi wa mpango na mimba zisizotarajiwa, na uwezekano wa wanawake kuamua kutoa mimba katika tukio la kupata mimba zisizotarajiwa.
“Mbali na huduma baada ya kuharibika kwa mimba, wanawake wa Kitanzania wanahitaji upatikanaji bora na kamilifu wa huduma mbalimbali za njia za uzazi wa mpango na ushauri nasaha kuhusu uzazi wa mpango  ili waweze kufanya maamuzi sahihi,” alisema Godfather Kimaro, mwanasayansi mtafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania, ambaye alifanya kazi kwenye utafiti. “Ndani ya mwaka 2013, wanawake wa Kitanzania walipata mimba zisizotarajiwa zaidi ya milioni moja, ambazo kati yake 39% ziliishia kwenye kutolewa. Kukabiliana na mahitaji yasiyokidhiwa ya uzazi wa mpango kutapunguza kiwango cha mimba zisizotarajiwa na hivyo kupunguza uhitaji wa kutoa mimba na vifo na majeruhi ambayo kwa mara nyingi hutokea baada ya taratibu zisizo salama.”
Watafiti wamependekeza kuimarisha juhudi za kuhakikisha upatikanaji wa huduma baada ya kuharibika kwa mimba, ambayo kwa sasa inapatikana bila ulinganifu katika maeneo mbalimbali. Wamependekeza uwekezaji katika kufanya huduma baada ya kuharibika kwa mimba inapatikana katika ngazi zote za mfumo wa afya, ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo watoa huduma wa ngazi ya kati na kusambaza kikamilifu dawa na vifaa vyote muhimu kwenye vituo vya afya. Pia, walisisitiza umuhimu wa kujumuisha utoaji wa huduma za uzazi wa mpango  kama sehemu ya huduma baada ya kuharibika kwa mimba na kuhimiza kwamba kila mwanamke anayetibiwa kutokana na matatizo yanayohusiana na kutoka kwa mimba apewe ushauri wa kina na nyenzo za uzazi wa mpango. Hatimaye, walipendekeza kwamba utata katika sheria ya utoaji mimba ya Tanzania ufafanuliwe kuhakikisha kuwa wanawake wanaweza kupata utaratibu salama na wa kisheria  kwa kiasi kamili kinachoruhusiwa. Watafiti wanatumaini kwamba matokeo ya utafiti huu yatasaidia kuleta mwanga kwenye sera na mipango ambayo italeta huduma za kifanisi zaidi na hatimaye kuboresha hali ya afya ya uzazi ya wanawake wote wa Tanzania.
Matukio ya Utoaji Mimba na Huduma Baada ya Kuharibika kwa Mimba Nchini Tanzania” na Sarah C. Keogh wa Taasisi ya Guttmacher et al. inapatikana mtandaoni kupitia PLoSONE.
Utafiti huu uliweza kufanyika kutokana na misaada kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Norway.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii yatembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya TBC-Kisarawe.

tib1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Bw.Peter Serukamba katika viwanja vya urushaji wa matangazo ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Kisarawe
tib2
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii Bw.Peter Serukamba akieleza jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kuangalia mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
tib3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (wa pili kulia) akiwasilisha jambo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii walipotembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
tib4
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii Bw.Peter Serukamba akieleza jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kuangalia mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
tib5
Mkurugenzi wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Ayoub Ryoba akiwasilisha  taarifa ya shirika hilo  kwa wajumbe wa wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe Pwani.Wengine pichani ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye,Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi.Anastazia Wambura na mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Peter Serukamba
Picha na Daudi Manongi-Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mwakyembe apokea taarifa ya sheria ya manunuzi.

3 Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi (Kushoto) akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma, katikati ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe na kulia ni katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome. 5 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akipokea taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi.
4 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi na kulia ni katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Sifuni Mchome.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO
………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amepokea taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka Tume ya kurekebisha Sheria.
Akipokea taarifa hiyo leo Jijini Dar es salaam Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amesema taarifa hiyo ya utafiti itasaidia kurekebisha sheria ya manunuzi ambayo inalenga kukuza uchumi wa nchi.
“Mimi na wataalamu wangu tumeipokea taarifa hii, tutaiangalia na kuhakikisha tunaifikisha Wizara ya Fedha na Mipango na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuendelea na utaratibu unaofuata ili mchakato wa marekebisho uweze kufanyika kwa haraka”alisema Dkt Mwakyembe.
Akifafanua juu ya sheria ya manunuzi ya Umma, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi  amesema kuwa Tume imefanya utafiti wa sheria hiyo kwa kushirikisha wadau mbalimbali.
“Tumepata maoni mengi na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi na wasimamizi wa manunuzi ya Serikali kwa namna wanavyoiona sheria ya manunuzi ya Umma,na sisi tumeyachambua maoni hayo kwa kutumia vigezo vya sheria”alisema  Jaji Mujulizi.
Aidha,Tume imetoa maoni kwa Serikali kusimamia sheria ili iweze kuendana na ukuaji wa uchumi nchini kwa kurekebisha baadhi ya sheria ili kuepuka muingiliano uliopo kati ya sheria ya manunuzi na sheria nyingine.
Marekebisho ya sheria hii ni moja ya agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli  lililotolewa Novemba 2015 alipokua akizindua Bunge la 11.

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM (BARA) AWATAKA WATUMISHI WA CCM KWENDANA NA KASI YA MABADILIKO YA SASA

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akisalimia baadhi ya viongozi wa CCM, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi hiyo, akiwa katika ziara ya kikazi leo. Anayemsalimia ni Katibu wa CCM wilaya ya Mbarali Abdallah Mpokwa.  Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo Mwangi Kundya
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhwavi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya leo. Kulia ni Katibu ambaye hajapangiwa kituo, Mariam Yusuf
Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangi Kundya akimsindikiza Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwavi kwenda ukumbini kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya CCM mkoa huo leo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhwavi akiingia ukumbini kuzungumza na wafanyakazi katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya leo. Kulia kwake ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangi Kundya
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rajabu Luhwavi akiwasili ukumbini
Katibu wa UVCCM mkoa wa Mbeya Adiya Mamu akihamasisha watumishi wa Chama, kumkaribisha ukumbini Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Rajabu Luhwavi leo
Watumishi wa CCM Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya wakiwa ukumbini
Katibu wa CCM, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Lobe Zongo akimkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu Bara kuzungumza na wafanyakazi hao wa Chama mkoa wa Mbeya
Continue reading →

SERIKALI KUTOA KIPAUMBELE KATIKA KUHAKIKI RASLIMALI NA MADENI YA VIONGOZI

index 
Na Mwandishi wetu.
………………………………………
Serikali imesema kuwa italipa kipaumbele suala la uhakiki wa mali za viongozi wa umma  kwa kuiwezesha Sekretarieti ya Maadili ya viongozi kufanya kazi zake  kwa ukamilifu kwa mujibu wa Sheria ya  Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki amesema hayoleo jijini Dar es Salaam alipokutana na Kamati ya Kudumu yaBunge ya Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imetembelea ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma kujua majukumu, mafanikio na changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo  ili wakifika bungeni waweze kuisemea.
“Suala la uhakiki wa rasilimali na madeni ya viongozi tutahakikisha linapewa kipaumbele katika Awamu hii ya tano ya  uongozi,” amesema.
Kwa mujibu wa Waziri Kairuki, Serikali itajitahidi kuongeza jitihada ili uhakiki wa rasilimali na madeni ya viongozi wa Umma ufanyike,  pamoja na kuiongezea Taasisi hiyo bajeti ya kutosha.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Mhe  Salome Kaganda amesema viongozi wengi wanarejesha fomu za raslimali na madeni, ila wapo wachache wanaoshindwa kurejesha fomu hizo.
Amesema, “Tangu mwaka 2005/06 hadi mwaka 2014/15 tumesambaza  fomu 78,786, lakini fomu zilizorejeshwa ni 60,948 ambazo ni sawa na asilimia 77 ya fomu zote zilizosambazwa.”
Aidha Kamishna huyo amewaambiawajumbe wa kamati hiyo ya Bunge kuwa tangu mwaka 2013 hadi 2015 Sekretarieti yake haikufanya uhakiki wa rasilimali na madeni kwa viongozi wa umma kutokana na  ufinyu wa bajeti.
Kwa upande wao baadhi ya Wajumbe wa kamati wamesema kuwa wataishauri serikali kuiongezea Sekretarieti bajeti iliiweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sharia.
Pia wamependekeza kufanyiwa maboresho Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 ili iwe na nguvu zaidi na kuwaruhusu kuwafikisha mahakamani viongozi wanaokiuka sharia hiyo.
Sekretarieti ya Maadil  ilianza kufanya kazi rasmi mwezi Julai, 1996 ikiwa na jukumu la msingi la kujenga na kukuza uadilifu miongoni mwa Viongozi wa Umma kwa kusimamia utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Maadili ya viongozi wa umma Na 13 ya mwaka 1995.

SPIKA WA BUNGE AKUATANA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA AHMADIYYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA

jam01
. Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana  na Kiongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania Sheik Tahir Mahmoud aliyemtembelea pamoja na viongozi wenzake Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
jam2
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania waliomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Kiongozi wa Jumuiya hiyo nchini Sheik Tahir Mahmoud.
jam3 

WAZIRI WA AFYA AKAGUA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KATIKA MAJIMBO YA MTWARA VIJIJINI, MASASI NA NDANDA

Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) akiwasili katika hospitali ya Rufaa Ndanda Mission.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari wametembelea Hospitali ya Mji wa Masasi (Mkomaindo), Hospitali ya Rufaa Ndanda Mission na Kituo cha Afya cha Nanguruwe kilichopo Jimbo la Mtwara Vijijini.
Katika ziara hiyo ya siku 2 Mh. Ummy alipata fursa ya kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya afya ikiwemo kukagua wodi za wagonjwa, maabara pamoja na kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa watumishi wa idara ya afya na wananchi katika utoaji wa huduma za afya katika maeneo hayo.
Mh. Ummy alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe Dk. John Pombe Magufuli imejikita zaidi katika kuwahudumia wananchi hasa wa kipato cha chini kwa kuimarisha Nidhamu na Uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma. Pamoja na kusimamia Uwazi na matumizi bora ya rasilimali za Taifa.
Licha ya kukiri kuwa sekta ya Afya inakabiliwa na changamoto mbalimbali Mh. Ummy aliwapongeza na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa kazi na nzuri wanayoifanya ktk kutoa huduma kwa wananchi. Alieeleza kuwa Serikali inatambua na kuthamini kazi yao na imedhamiria kutatua changamoto zilizoko katika utoaji wa huduma ikiwemo kuongeza watumishi wa afya na kununua vifaa tiba na kuboresha mazingira ya kazi ya watumishi wa afya hasa walioko pembezoni.
Aliwaasa wananchi kuwathamini madaktari na waaguzi na iwapo kuna malalamiko dhidi ya watumishi hao basi wananchi wazingatie Sheria, Kanuni na Taratibu ktk kuonyesha malalamiko yao badala ya kujichukulia sheria mkononi.
Alisema, Hata hivyo wapo watumishi wachache ambao wanafanya kazi kwa kutozingatia maadili ya kazi na viapo vyao, hivyo aliwataka wabadilike kwani Serikali ya awamu ya 5 haitamvumilia mtumishi yeyote anaejihusisha na vitendo vya rushwa na uzembe kazini.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi Ndanda mission.
Pia aliwaasa watumishi hao kujiepusha na mambo ambao yanaweza kuleta mgongano na hisia mbaya kwa wananchi. Mfano tuhuma dhidi ya mfamasia wa Wilaya kumiliki maduka matatu ya 3 ambapo mhe Waziri ameelekeza uchunguzi wa TAKUKURU ufanyike.
Katika Hospitali ya Mkomaindo, Mhe Ummy ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa mafanikio waliyopata ktk ukusanyaji wa mapato ambapo baada ya kufunga mfumo wa kukusanya mapato wa kielektronik mapato yao yameongezeka kutoka shs 500,000 hadi 1,500,000 kwa siku. Amezitaka Halmashauri zote nchini kuiga mfano wa hospitali ya Mkomaindo kwa sababu hatua hii itachangia sana kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi ikiwemo uwezo wa Halmashauri wa kununua dawa na vifaa tiba.
Katika Kituo cha Afya cha Nanguruwe Mh. Ummy aliihimiza Halmashauri kukamilisha ujenzi wa wodi mbili ili Kituo hicho kiweze kupandishwa hadhi kuwa Hospitali ya Wilaya. Pia aliwataka kuongeza jitihada katika kuingiza wananchi/kaya nyingi katika Bima ya Afya kwani asilimia 5 wa waliojiunga ni ndogo sana.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi ili kujua kero zao katika ziara ya siku mbili mkoani humo.
Katika Hospitali ya Rufaa ya Mission Ndanda Mhe Ummy ameipongeza kwa kufanyia kazi agizo lake la wiki mbili zilizopita la kuzitaka hospitali za Taasisi za Dini zinazopokea ruzuku ya Serikali (Fedha na au Watumishi) kutekeleza kwa vitendo sera za Taifa za Serikali ikiwemo ya Matibabu Bure kwa Wajawazito, Watoto chini ya umri wa miaka 5 na Wazee. Hospitali ya Rufaa Ndanda imekubaliana na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kuanza utekelezaji wa jambo hili kuanzia Julai 1, 2016.
Mh. Ummy pia amepongeza upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu bure ya Ugonjwa wa Kifua kikuu hospitalini hapo ambapo alisema ni asilimia 10 tu ya vituo vya afya/Hospitali binafsi nchini zinazotoa huduma hizo licha ya Serikali kuwa tayari kuvipatia vifaa vya uchunguzi na dawa bure. Mhe Ummy amezitaka hospitali nyingine binafsi kuunga mkono jitihada za Serikali za kutokomeza ugonjwa wa Kifuu kikuu kama sehemu ya mchango wao kwa jamii.
Mhe Ummy pia ametembelea Chuo cha Maafisa Tabibu na Chuo cha uuguzi vilivyoko Masasi.
IMG-20160331-WA0025
Waziri Ummy akiongea na wagonjwa aliowakuta wakisubiri huduma katika hospitali ya Mkomaindo Masasi.
Mohammed Bakari
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari akizungumza na Watumishi wa Afya Ndanda Mission katika ziara aliyoambatana na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu.
Mohammed Bakari
IMG-20160331-WA0023Baadhi ya watumishi wa afya wakimsikiliza kwa makini Waziri wa afya Mh.Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati ziara yake tar 30 Machi.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wakinamama aliyelazwa kwenye wodi ya wazazi alipokua akikagua maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
Mussa Rashid
Kaimu Mganga mkuu Halmashauri ya mji wa Masasi DK. Mussa Rashid akitoa taarifa kwa Waziri wa afya alipotembelea chumba cha vipimo katika hospitali hiyo. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari.
Ummy Mwalimu
Waziri Mh. Ummy Mwalimu akibadilisha mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Bernard Nduta. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa Ndanda, Fr. Silvanus Kessy.

“KAMATI YA BUNGE, MALIASILI, UTALII, ARDHI NA MAZINGIRA WAMTAKA WAZIRI LUKUVI KUFUTA HATI MILIKI YA ECO ENERGY”

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Injinia Ramo Makani kulia akiteta
jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili,Ardhi na Utalii,Meja Jenerali
Gaudance Milanzi katikati kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa wa Shirika la
Hifadhi za Taifa(TANAPA),Ibrahim Mussa wakati wa ziara ya siku moja ya
kamati ya Bunge Maliasili,Ardhi na Utalii kwenye hifadhi ya Taifa ya
Saadani,
Wajumbe wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii wakiingia kwenye hifadhi ya
Taifa ya Saadani jana

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii Atashasta
Justus Nditiye akitoa maazimio ya kamati hiyo mara baada ya kuitembelea
hifadhi ya Taifa ya Sadani wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa kamati
hiyo,Marry Chatanda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Injia Ramo Makani akizungumza wakati wa ziara hiyo

Kaimu Mkurugenzi wa (TANAPA),Ibrahim Mussa akizungumza wakati za ziara ya kamati ya Bunge
Maliasili,Utalii na Ardhi Mazingira ilipotembelea hifadhi ya Taifa ya
Saadani.

Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Meja Jenerali Gaudance
Milanzi akizungumza wakati za ziara ya siku moja ya Kamati ya Bunge ya
Maliasili,Utalii na Ardhi

 Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Tanapa,Mtango Mtaniko akizungumza
wakati wa ziara ya kamati ya Bunge Maliasili,Utalii na Ardhi walipofanya
ziara ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani
Mjumbe wa Kamati ya Bunge Maliasili,Utalii,Ardhi na Mazingira,Pauline Gekule
akiulizwa swali wakati ziara hiyo

MJUMBE wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii,Shabani Shekilindi ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga akiuliza swali wakati wa ziara hiyo

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini,Marry Chatanda ambaye pia  ni mjumbe wa kamati
hiyo akichangia hoja kwenye ziara hiyo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudance Milanzi kulia akiteta jambo na Meneja wa Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete wakati kamati ya Bunge Maliasili,Ardhi na Utalii walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani
Picha kwa Hisani ya Tanga Raha Blog

Tume ya Kurekebisha Sheria Yakabidhi Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma

REK1
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi (Kushoto) akimkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dk. Harison Mwakyembe Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma. Wengine pichani ni Katibu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sufini Mchome (wa pili kulia) na Katibu Mtendaji wa Tume Bw. Casmir Kyuki.
REK2
Mwenyekiti wa Tume Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi akizungumza wakati wa makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma. Makabidhiano yalifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Katiba na Sheria Dar es Salaam.
REK3
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dk Harison Mwakyembe akiongea mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.
REK4
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Casmir Kyuki akizungumza wakati wa makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.
REK5
Katibu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi wakati wa makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.
REK6
Sehemu ya Waandishi wa habari waliohudhuria makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma (Picha zote na Munir Shemweta wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania).

WASHIRIKI ISHIRINI BORA WA SHINDANO LA ‘MO ENTREPRENEURS’ WATANGAZWA

Top 20 - Mo Entrepreneurs Competition
Taasisi ya Mo Dewji Foundation wakishirikiana na kampuni ya Darecha Limited wametangaza majina ya washiriki 20 bora wa shindano la Mo Mjasiriamali (Mo Entrepreneurs Competition). Shindano la Mo Mjasiriamali lilizinduliwa mwezi wa Januari, 2016 na mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya MeTL na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Bilionea Mohammed Dewji. Akizindua shindano hilo mweneyekiti huyo alisema,
“Tatizo la ukosefu wa mitaji ni kikwazo kikubwa kwenye ukuaji wa biashara za vijana wengi hapa nchini.Hivyo ni muhimu kuwaongezea vijana fursa za upatikanaji wa mitaji”
Shindano la Mo Mjasiriamali linalenga kuwainua vijana wenye shauku, ari na nia ya dhati ya kukuza biashara zao ili kujiongezea kipato na mchango wao katika ujenzi na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Wakitangaza majina ya washiriki 20 bora, waratibu wa shindano la Mo Mjasiriamali wamesema shindano hili limewafikia maelfu ya vijana katika maeneo mbali mbali ya Tanzania. Vijana wapatao 200 wanaomiliki biashara changa walituma maombi ya ushiriki. Washiriki waliotuma maombi walikuwa na wastani wa umri wa miaka 26, miongoni mwao asilimia 13 ni wa jinsia ya kike. Aina mbalimbali za biashara kama vile, biashara za kilimo, ufugaji, utengenezaji wa mbolea, tehama na nishati zilionekana kupata washirki wengi zaidi.
Majina ya washiriki 20 watakaofanyiwa usaili na jopo la majaji litakaloongozwa na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Ndg. Mohammed Dewji, majina ya biashara zao na mkoa wanaotoka kwenye mabano, ni:
1.Edgar Mwampinge (Spid Express Courier&Logistics, DSM),.
2.Geofrey Boniphace (Brain Bongo Media Network, DSM),
3.Alexander Jokoniah (Mazimbu Agro Enterprises,Morogoro),
4.Raphael Malongo( Malongo Poultry Farm,Singida),
5.Sirjeff Khagolla (Jefren Agrifriend, DSM),
6.Erick Karoli (Tado Travel, Arusha),
7.Ahad Katera (Guavay, DSM),
8.Bonkey Kaigembe (Igale Company, Mbeya),
9.Gerald Reuben(Nitume Sokoni, Pwani),
10.Selenga Kaduma(Agro Forest, Njombe),
11.Saturnin Tarimo (Galaxy Energy Solutions, DSM),
12.Ally Msigwa (Alishati Investments,Iringa),
13.Khadija Liganga (Dida Vitenge Wear, Mwanza),
14.Williard Kaaya (Newhope Cassava Flour, DSM),
15.Doreen Assey (Dee Bakery,DSM),
16.Clemence Makoyola(Easternwind Investment, Morogoro),
17.Emmanuel Ngalewa( Ngama Technologies, DSM),
18.Eric Mutta (Problem Solved, DSM),
19.Francis Saanane( Hub Networks, DSM),
20.Fredrick Swai (Nact Technology Hub, Mbeya)
Washiriki wote ishirini watafanyiwa usaili wa kina kuhusu biashara zao ambapo miongoni mwao watapatikana washindi watatu(3) hadi watano(5). Washindi hao watatangazwa siku ya tarehe 19 Aprili na kupatiwa kiasi cha milioni shilingi milioni 10 kila mmoja ili kukuza biashara zao.Pia washindi hawa watakuwa wakikutana na mkurugenzi mtendaji wa MeTL na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation kwa ushauri kuhusu namna ya kukuza biashara zao.

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA INTANETI, AfPIF 2016

IMG_7655
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba akielezea matumizi ya intaneti yalivyo nchini na changamoto zinazowakabili watumiaji wa huduma hiyo. (Picha na Modewjiblog)
Mwaka 2016 unakuwa mwaka wa neema kwa Tanzania kupata fursa ya kuandaa Mkutano unaowakutanisha wadau wa intaneti (African Peering and Interconnection Forum), mkutano unaotaraji kufanyika Agosti 31 – Septemba 1, jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia mkutano huo, Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi amesema mkutano huo unalengo wa kukutanisha wadau mbalimbali wa intaneti ili kutanua miondombinu ya intaneti katika bara la Afrika.
Amesema taasisi yake inapenda kuona huduma ya intaneti ikipatikana kwa urahisi kwa watumiaji wake Afrika na hivyo kupitia mkutano huo wataweza kutazama jinsi gani wanaweza kushirikiana na kubadilishana takwimu za watumiaji wa mitandao kwa bara zima la Afrika.
“Tunatambua kuwa watumiaji wa intaneti wanazidi kuongezeka na kupitia mkutano huu tutaweza kuangalia jinsi gani tunaboresha huduma ya intaneti iwe bora ili iweze kutumiwa na watu wengi zaidi,” amesema Mwangi.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba amesema mkutano huo una umuhimu kwa Watanzania kwa kupata fursa ya kujifunza na kubadilishana mawazo na watu kutoka mataifa mengine katika huduma ya intaneti.
Amesema kwa sasa Tanzania bado ina changamoto nyingi katika huduma ya intaneti na kupata nafasi hiyo ya kuandaa mkutano kutakuwa na faida kwa mashirika yanayotoa huduma ya intaneti ili kuwawezesha kutambua ni jinsi gani wataboresha huduma kwa wateja.
“Nchi yetu inawatumiaji wengi wa intaneti ila bado kuna changamoto nyingi ikiwepo usalama wa mtandao na serikali inafanya jitihada nyingi kumaliza changamoto hizo na kupitia mkutano huu tunaamini utasaidia zaidi Watanzania kupata kitu kipya katika huduma ya intaneti,” amesema Simba.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary amesema Watanzania wengi bado hawajafahamu umuhimu wa intaneti kutokana na kutokuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu intaneti lakini kupitia mkutano huo ulioandaliwa na Internet Society wataweza kuapata elimu mpya kuhusu intaneti.
IMG_7593
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary.
IMG_7596
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto), Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary, Meneja Mradi wa Tanzania Internet Exchange (TIX), Frank Habicht na Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi wakizungumza jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
IMG_7603
Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary akifungua mkutano huo.
IMG_7613
Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi akizungumzia mkutano wa Intaneti, AfPIF utakaofanyika nchini, Agosti, 30 – Septemba, 1
IMG_7617
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo.
IMG_7629
IMG_7631
IMG_7645
IMG_7622
Baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano huo.
IMG_7667
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

WAZIRI KITWANGA, VIONGOZI WAKUU UHAMIAJI NA JESHI LA ZIMAMOTO WAFANYA KIKAO CHA MAPITIO YA RASIMU YA BAJETI KWA MWAKA 2016/17

TWA1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Wizara yake ya Mwaka 2016/17 kwa upande wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Idara ya Uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, kilijumuisha Viongozi Wakuu wa Taasisi hizo pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
TWA2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (kulia) wakati alipokuwa anatoa taarifa yake katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Idara ya Uhamiaji kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kikao hicho kilijumuisha Viongozi Wakuu wa Uhamiaji na Wakuu wa Idara ya Wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
TWA3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwafafanulia jambo Viongozi Wakuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Wakuu wa Idara ya Wizara yake katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Jeshi hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wa tatu kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Rogatius Kipali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
TWA4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kulia) akizungumza na Viongozi Wakuu wa Idara ya Uhamiaji katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 ya Wizara yake. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, pia kilihudhuriwa na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akifuatiwa na Mrakibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji, Joseph Mtenga.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KAMATI YA MALIASILI YATEMBELEA HIFADHI YA SAADANI PAMOJA NA KUKUTANA NA TANAPA

BUN1Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti ya TANAPA wakati kamati hiyo iliopotembelea Hifadhi ya Saadani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani.
BUN2Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.
BUN3Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.
BUN4
Mkuu wa Hifadhi ya Saadani Bw. Hassan Nguluma akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Maliasili, Utalii na Ardhi ramani ya Hifadhi hiyo wakati kamati hiyo ilipoitembelea Hifadhi ya Saadani pamoja na kukutana na Menejimenti ya TANAPA. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani (mweye miwani) na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Atashasta Nditiye

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM AANZA ZIARA MKOANI MBEYA LEO

LUH1
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi, akisalimiana na viongozi wa CCM mkoa wa Mbeya baada ya kuwasili mkoani hapa, leo, Machi 31, 2016, kuanza ziara ya kikazi. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangwi Kundya, Katibu wa CCM, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Lobe Zongo na Katibu msaidizi Mkuu wa
mkoa, Adallah Mayomba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwai akiwa na mwenyeji wake, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya, Mwangwi Kundya (kushoto), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani Mbeya.

VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI MKURANGA VYASHAURIWA KUWA KATIKA MWAMVULI WA VICOBA ILI KUPATA SIFA YA KUKOPESHWA

Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa, Bengi Issa mwenye kilemba, akizungumza kwenye kikao cha pamoja na Mbunge wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega kushoto kwake kwa ajili ya kuangalia namna ya kushirikiana naye kuwasaidia na kuwawezesha wananchi wa Mkuranga. Mbunge Mkuranga asaka uwezeshwaji wa wananchi wake
…………………………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani, Abdallah Ulega, jana amefanya kikao na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Taifa (NEEC), Bengi Issa, kwa ajili ya kutafuta fursa ya kuwawezesha wananchi wilayani humo.
Mbunge wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega, akizungumza jambo katika kikao cha pamoja na Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa (NEEC), Bengi Issa, hayupo pichani.
Kikao hicho pia kilihusisha Mkurugenzi wa Uwezeshaji, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuranga, ambapo pamoja na mambo mengine, kilijadili namna ya kusaidia vikundi vilivyosajiliwa 285, vikundi vya vicoba 109, ufugaji wa nyuki, vikundi vya wanawake, vijana na waendesha bodaboda.
Akizungumza baada ya kikao hicho kumalizika, Ulega aliyewahi pia kuwa Mkuu wa wilaya Kilwa, alisema kwamba lengo ni kuona wanananchi wa Mkuranga wanapiga hatua kutoka kwenye hali ya ukata na kufikia kiwango kizuri, sanjari na kufanikisha maendeleo kwa wananchi wote.
Alisema kwamba kikao hicho kimemalizika kwa mafanikio ambapo ilishauriwa kuwa vikundi vya kukopeshana (VICOBA) inabidi viwekwe chini ya mwamvuli mmoja utakaoviwakilisha vyote.
“Hili litakapofanyika, Benki ya Posta Tanzania ina utaratibu wa kutoa mikopo ya riba ndogo kupitia mwamvuli huo unaowakilisha vikundi vyote kwa pamoja, tukiamini kuwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha ndoto zetu.
“Lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunaiweka Mkuranga katika kiwango kizuri ukizingatia kwamba wilaya hii ipo karibu na jiji la Dar es Salaam, hivyo inaweza kukua kwa kasi kwa sababu mtu anaweza kuishi Mkuranga na akafanya kazi au kuingia na kutoka kwa urahisi wilayani kwetu,” alisema.
Aidha imeshauriwa pia kuanzisha SACCOS ya wafugaji wa nyuki ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo ya vifaa kwa ajili ya ufugaji wa kisasa wa nyuki, ambapo wana vikundi wanatakiwa kuandaa mpango kazi wao utakaopelekwa Benki ya Maendeleo kwa ajili ya mkopo, ikiwa na lengo la kuhifadhi misitu na kuacha utafutaji wa kipato kwa njia ya kukata miti ili kuzalisha mkaa.

BARABARA YA KIGOMA-NYAKANAZI KUKAMILIKA MWEZI MEI.

1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kigoma tayari kuanza ziara ya ukaguzi wa miundombinu katika mikoa ya ukanda wa magharibi.
2 
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kigoma, Eng. Narcis Choma akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa kofia) kuhusu ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 inayojengwa na China Railway 50 Group.
3 
Ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 inayojengwa na Kampuni ya  China Railway 50 Group ukiendelea.
4 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa kofia) akitoa maelekezo kwa wataalamu wa ujenzi wa kampuni ya China Railway 50 Group baada ya kukagua mitambo yao ya kupima na kutafiti udongo kabla ya kujenga barabara.
5 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa kofia) akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wilaya ya Kasulu mara baaada ya kukamatwa kwa vijana wawili (waliokaa chini) kutokana na wizi wa nyaya za mkongo wa taifa, mkoani Kigoma.
6 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa koti la kaki) akiangalia athari za mmonyoko wa udongo zilizoathiri mkongo wa taifa wa mawasiliano katika eneo la Kidahwe mkoani Kigoma.
……………………………………………………………..
Makandarasi wanaojenga barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 na Kibondo-Nyakanazi Km 50 wametakiwa kukamilisha ujenzi huo mwezi Mei mwakani badala ya Novemba ili kuharakisha mkakati wa Serikali wa kuufungua mkoa wa Kigoma kwa barabara za lami.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo uliyogawanywa sehemu mbili, Kidahwe-Kasulu inayojengwa na China Railway 50 Group na Kibondo-Nyakanazi inayojengwa na Nyanza Road Works.
Prof. Mbarawa amewataka makandarasi hao kuongeza kasi ya ujenzi, vifaa na  wafanyakazi wenye sifa ili barabara hizo zikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.
“Tutahakikisha ifikapo Juni mwaka huu tutakuwa tumelipa madeni yote mnayoidai Serikali hivyo fanyeni kazi kwa uhakika kwa kuwa katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano tayari tumeshawalipa makandarasi zaidi ya shilingi bilioni 725”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesisitiza kwamba nia ya Serikali ni kuifungua mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa kwa barabara za lami ili kufungua ukanda wa magharibi mwa nchi kibiashara kutokana na ukanda huo kuwa sehemu muhimu ya nchi katika uzalishaji na kiungo kikuu kwa nchi za Congo DRC, Burundi na Rwanda.
Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Shirika la Reli (TRL), kulinda miundombinu ya reli na kujiepusha na vitendo vya hujuma ili kuliwezesha shirika hilo kupata shehena kubwa ya mzigo kufuatia wadau mbalimbali kuonesha nia ya kusafirisha mizigo kwa njia ya reli.
“Serikali imewekeza vya kutosha katika Shirika la Reli hivyo mfanye kazi kibiashara ili mpate mzigo mkubwa wa kusafirisha”, amesisitiza Prof. Mbarawa
Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kigoma na taasisi zilizo chini ya wizara yake Prof. Mbarawa amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuzuia uvamizi na uhujumu wa miundombinu ya barabara, reli, na mkongo wa taifa wa mawasiliano na wote watakaokiuka agizo hilo wachukuliwe hatua za haraka na za kisheria.
Prof. Mbarawa ametoa wiki moja kwa taasisi zilizo chini ya wizara yake kuhakiki wafanyakazi ili kubaini kama kuna wafanyakazi hewa.
Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kigoma, Eng. Narcis Choma amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa mkoa wa Kigoma umejipanga vizuri katika kudhibiti uvamizi wa miundombinu ya barabara na wale waliojenga ndani ya mita 22 kwenye barabara kuu wataondolewa maramoja bila kulipwa fidia.
Prof. Mbarawa yuko katika ziara ya kukagua miundombinu katika mikoa ya kanda ya magharibi ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa uiboreshaji wa miundombinu ya kanda hiyo ili kuiwezesha kufanya biashara kiurahisi na mikoa mingine ya Tanzania na nchi za Congo DRC, Rwanda na Burundi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Tanzania yapata medali mbili zaidi katika mashidano ya kuogelea ya kimataifa ya Afrika Kusini

1 
Muogeleaji Marin de Villard wa Tanzania akishindana katika staili ya backstroke kwenye mashindano ya kimataifa ya kuogelea ya Afrika Kusini.
2 
Muogeleaji wa Tanzania Celina Itatiro akionyesha ufundi wake katika staili ya backstroke kwenye mashindano ya kimataifa ya kuogelea ya Afrika Kusini.
3 
Muogeleaji wa Tanzania, Adil Bharmal akiwa katika staili ya breaststroke kwenye mashindano ya kimataifa ya kuogelea ya Afrika Kusini.
4Waogeleaji Josephine”Jojo” Oosterhuis aliyenyosha mkooi juu akiwa na wenzake, Isabella Kortland (wa pili waliosimama kutoka kushoto), Jacqulline Kortland ambaye ni pacha wa Isabella (wa tatu kutoka kulia waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kunyakua medali tatu katika mashindano ya kuogelea ya Afrika Kusini. Wengine katika picha ni kocha Michael Livingstone (wa kwanza kushoto waliosimama), kocha  Alex Mwaipasi (wa pili kulia waliosimama) na meneja wa timu, Inviolata Itatiro wa kwanza kulia waliosimama. Pia katika picha ni Marin de Villard na Celina Itatiro (waliokaa).
5Nyuso za furaha: Meneja wa timu ya Tanzania Swim Squad (TSS), Inviolata Itatiro akiwa na makocha, Alex Mwaipasi (kushoto) na Michael Livingstone mara baada ya ushindi wa medali tatu katika mashindano ya kuogelea ya Kimataifa ya  Afrika Kusini.
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Nyota ya Tanzania katika mchezo wa kuogelea imeanza kung’ara baada ya kupata medali tatu katika mashindano ya kimataifa ya kuogelea ya Afrika Kusini yanayondelea katika mji wa Johannesburg.
Walioshinda medali katika mashindano hayo ni, Josephine Oosterhuis, Isabella Kortland na Jacqueline Kortland  katika mashindano hayo ambayo yanashirikisha waogeleaji zaidi ya 750 kutoka nchi mbalimbali kusini mwa Afrika.
Mbali ya Tanzania na wenyeji, Afrika Kusini, mashindano hayo pia yalishirikisha timu kutoka Zimbabwe, Msumbiji, Angola,  na Namibia. Josephine alishinda medali ya dhahabu katika fainali ya mita 100 breaststroke kwa kutumia muda wa 1.21.79 huku Jacqueline alishinda medali ya shaba kwa kushika nafasi ya tatu kwa kutumia muda wa 1.22.91.
 Nafasi ya pili ikikwenda kwa Deane Toerien wa Afrika Kusini aliyetumia muda wa 1.22.70 na kutwaa medali ya fedha. Isabella Kortland alishinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya mita 50 katika staili ya backstrokes kwa kutumia muda wa 33.25 kuwashinda Georgy Turner na Zantia Bainabridge wa Afrika Kusini ambao walifungana kwa kutumua muda wa 33.84 kila mmoja.
Waogeleaji Celina Itatiro hakuweza kutwaa medali pamoja na kumaliza akiwa wa tisa kwa kutumia muda wa 1.29.26 katika mita 100 butterfly, Marin de Villard  alimaliza wa tisa katika staili ya backstroke kwa kutumia muda wa 37.43.
“Tumefanya vizuri sana, si unajua mashindano haya ni magumu kutokana na ushindani uliopo, Afrika Kusini na nchi nyingine inatumia kutafuta waogeleaji wao ambao watakwenda kushindana katika mashindano ya Cana na wameleta waogeleaji wengi, sisi tumeleta 15 na mpaka sasa tuna medali 3, ni mafanikio,” alisema meneja wa timu hiyo Inviolata Itatiro.
Kocha Alex Mwaipasi alisema kuwa wamefurahishwa na matokeo hayo na wanaamini kuwa wakiendelea na msimamo wao wa kushiriki mashindano mengi ya kimataifa, basi watafika mbali sana ndani ya miaka mitano au kumi.
“Mbali ya medali, hapa waogeleaji wanasaka nafasi ya Cana, baadhi ya waogeaji wetu ndiyo kwanza wanaogelea katika bwawa la mita 50, wengine mara ya kwanza, hivyo kuna changamoto,” alisema Mwaipasi.
Kocha Michael Livingstone aliwashukuru wazazi wa waogeleaji kwa kufanikisha safari hii na kuifanya Tanzania kuingia katika chati ya mchezo wa kuogelea. “Wazazi wamejitahidi kwa kweli, wengine wameshindwa na wengine wameambatana na watoto wao kuja hapa kwa ajili ya kuitangaza Tanzania, tumefanikiwa,” alisema Michael.

SHULE YA AWALI YA SUNRISE YA MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM YAWAFARIJI WATOTO YATIMA WA KITUO CHA WATOTO WETU TANZANIA NA KUFANYA USAFI COCO BEACH


 Mkurugenzi wa Kituo cha Yatima na wale waliotoka katika mazingira magumu cha Watoto Wetu Tanzania (WWT), Evans Tegete akizungumza na wanahabari mwishoni mwa wiki wakati akipokea misaada mbalimbali kutoka Shule ya Awali ya Sunrise.
 Mwalimu wa Shule hiyo, Suma Mwasuka (katikati), akizungumza na wanahabari.
 Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo, Anne Nyokabi (mbele), akiongoza wenzake kufanya usafi Coco Beach ikiwa ni kuunga mkono kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
 Shughuli za usafi zikiendelea.
 Uhamasishaji wa usafi ukiendelea.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa wamekaa na wenzao wa Kituo hicho cha Watoto Wetu Tanzania walipofika kuwajulia hali na kuwapa misaada mbalimbali iliyolewa na wazazi, walimu na mwanafunzi mmoja mmoja

ASKARI POLISI ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUGUNDULIKA ALIJIPATIA AJIRA KWA VYETI VYA KUGUSHI, AKAAMUA KUKIMBIA.

Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia katika jeshi la Polisi mkaoni Ruvuma F 5425 PC Emmanuel Nyagoli ( 35), anatafutwa na Jeshi hilo kwa
kosa la kujipatia ajira kwa vyeti vya Kugushi, Na kwasasa hajulikani alipokimbilia. Taarifa zaidi hii hapa RUVUMA TV.

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MABENKI (TBA)

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job
Ndugai akiongea na viongozi wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) wakati
walipomtembelea ofisini kwake 30 Machi, 2016 jijini Dar es Salaam.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Tulia Ackson akiongea na viongozi wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA)
wakati walipomtembelea Spika ofisini kwake 30 Machi, 2016 jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wajumbe wa Chama cha Mabenki (TBA) Bwana Neech Msuya
(kushoto) akifafanua jambo mbele ya Spika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Job Ndugai (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake
30 Machi, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wajumbe wa Chama cha Mabenki (TBA) Bwana Shani
Kinswaga (kushoto) akifafanua jambo mbele ya Spika Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini
kwake 30 Machi, 2016 jijini Dar es Salaam.
 
(Picha zote na BenedictLiwenga)

No comments :

Post a Comment