Friday, March 25, 2016

SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA AWAMU YA SABA WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN


 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiwapungia mkono wananchi baada ya zoezi la kuapishwa pamoja na kukagua
gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa unaoashiria mwanzo
wa Uongozi wake kwa kipindi cha pili katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya
kuapishwa rasmi  leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana
mkono na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame wakati
aliposalimiana  na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika
zoezi la kuapishwa  katika Uwanja wa Amaan Studium leo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana
mkono na Mkuu wa KMKM Hassan MUssa Komodoo wakati aliposalimiana  na Wakuu
wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa
katika Uwanja wa Amaan Studium leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana
mkono na Kaimu Mkuu wa JKU Kanali Ali Mtumweni Hamadi wakati
aliposalimiana  na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya
kumalizika zoezi la kuapishwa  katika Uwanja wa Amaan Studium leo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akifuatana na Makamanda wakati alipokuwa akikagua gwaride la Vikosi vya Brass
Band leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,baada ya kuapishwa rasmi
kwa kuongoza Zanzibar katika kipindi cha Pili cha Awamu ya saba,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua
gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa katika Uwanja wa
Amaan Studium baada ya kuapishwa leo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein akitia
saini hati ya kiapo mbele ya Jaji Mkuu Mhe,Omar Othman Makungu baadanya
kumalizikika kwa zoezi hilo lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium
Mjini Unguja(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo
alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wananchi baada ya zoezi la kuapishwa kushika
nafasi hiyo ya Urais kwa kipindi cha pili cha Uongozi katika Uwanja wa Amaan
Studium Mjini Unguja leo, 

SSRA YAKUTANA NA WADAU WA CHAMA CHA WAAJIRI TANZANIA (ATE) KUJADILI MABADILIKO NA MAENDELEO MBALIMBALI KATIKA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII

Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama cha Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Carina Wangwe, akizungumza wakati akiufungua mkutano wa mamlaka hiyo na wadau wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam . 
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na wadau wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama wa SSRA, Carina Wangwe, alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi, akimwakilisha Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, Millenium Tower, Dar es Salaam
Washiriki wa mkutano huo, wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA) na
wadau wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama wa SSRA, Carina Wangwe, alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi, akimwakilisha
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam .
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA) na wadau wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama wa SSRA, Carina Wangwe, alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi, akimwakilisha
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, Millenium Tower, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA), Onorius Njole, akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Kisheria wa usimamizi na
udhibiti wa hifadhi ya Jamii Tanzania wakati wa mkutano huo, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam .
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole, alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Kisheria wa usimamizi na udhibiti wa hifadhi ya Jamii Tanzania wakati wa mkutano huo, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakifuatilia mada kuhusu Mfumo wa Kisheria wa usimamizi na udhibiti wa hifadhi ya Jamii, iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam .
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA), Onorius Njole, akiwasilisha mada hiyo
wakati wa mkutano huo, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Tafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA), Ansgar Mushi, akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Hifadhi ya Jamii Tanzania, Mtazamo wa Waajiri na Mpango wa hifadhi kwa waajiriwa wao, wakati wa mkutano huo,
Millenium Tower, jijini Dar es Salaam.

Mfalme wa Saudia Arabia amuahidi Rais Magufuli ushirikiano mnono

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NEMBO YA TAIFA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mfalme wa Saudi Arabia Mtukufu Salman Bin Abdulaziz Al Saud amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa nchi yake imeichagua Tanzania kuwa nchi ya kipaumbele katika mpango wake wa kuimarisha zaidi mahusiano na Afrika uliolenga kuendeleza na kukuza biashara, uwekezaji na kushiriki katika miradi ya maendeleo.
Ujumbe wa Mtukufu Salman Bin Abdulaziz Al Saud umewasilishwa kwa Rais Magufuli leo tarehe 24 Machi, 2016 na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mheshimiwa Adel Al Jubeir Ikulu Jijini Dar es salaam.
Katika Salamu hizo pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuiongoza Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania, Mfalme Salman Bin Abdulaziz Al Saud amesema Saudia Arabia imedhamiria kukuza zaidi mahusiano kati yake na Tanzania ili kuwaletea manufaa makubwa wananchi.
Kwa upande wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru Mfalme wa Saudi Arabia kwa kumtumia ujumbe na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuiongoza Tanzania na amemhakikishia kuwa Serikali yake itafurahi kuona Saudi Arabia inashirikiana na Tanzania kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kati na barabara.
Maeneo mengine ambayo Rais Magufuli na Waziri Adel Al Jubeir wameyazungumzia ni ushiriakiano kati ya Tanzania na Saudia Arabia katika kuendeleza Elimu, Utalii, Bandari na miundombinu.
Pamoja na kufanya Mazungumzo hayo, Rais Magufuli pia ameshuhudia utiaji saini wa mkataba kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo, ambapo kwa upande wa Tanzania mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga, na kwa upande wa Saudi Arabia umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mheshimiwa Adel Al Jubeir.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
24 Machi, 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA AWAMU YA SABA WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN

1  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Zanzibar, Dkt. Mwinyi Haji Makame mara baada ya kuwasili Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya sherehe za kuapishwa Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein.
4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mamia ya wananchi wa Zanzibar mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kuapishwa kwa Rais wa awamu ya saba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
3 
Gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na usalama vikiimba wimbo wa Taifa kwenye uwanja wa Amaan.
13 
Rais mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi waliofurika katika uwanja wa Amaan  Kisiwani Zanzibar mara baada ya kuapishwa. 

WAOGEAJI WA TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA YA KUOGELEA AFRIKA KUSINI

13Waogeleaji wakichuana katika mashindano mbalimbali yaliyopita.
11……………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Jumla ya waogeleaji 15 wa Tanzania (Tanzania Swim Squad) watashiriki katika mashindano ya kimataifa ya Afrika Kusini yaliyopangwa kuanza Machi 28 mpaka Aprili 3 mjini Johannesburg.

KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI YATEMBELEA MSD

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (mwenye suti nyeusi kushoto), akiwatembeza Wajumbe wa  Kamati Bunge ya Mauala ya Ukimwi waliotembelea MSD Keko Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge ya Ukimwi, Hassna Sudi Katunda Mwilima (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe hao na wageni katika ziara hiyo.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (kulia), akiwatembeza wajumbe hao MSD Keko.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (katikati), akitoa maelekezo kwa wajumbe hao.

WAZIRI MAGHEMBE AMEMSIMAMISHA KAZI MTENDAJI MKUU WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA ( TFS), WAKURUGENZI WATATU PAMOJA NA WAKUU WA KANDA NCHI NZIMA

8Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu na Wakurugenzi watatu wa  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo .  Kushoto  ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani.
9Baadhi ya Waandishi wa habari Waliohudhuria Mkutano huo wa Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.
10Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu na Wakurugenzi watatu wa  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo 

VIJANA WAANDAA MSAFARA WA HISANI KWA KUTUMIA MAGARI KUPINGA UJANGILI NA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI

Mkurungezi mtendaji wa Bongo Ride Idrisa Magesa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuelezea makamilisho ya maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha  ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani,kulia kwake ni Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele na kushoto kwake ni Mkuu wa matukio Kelvin Edes,Pembeni yake ni Mkurungezi wa Teamtezza Kennan Richard.
Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele akiongea na waandishi wa habari kuelezea kukamilika kwa maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha  ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani,kulia kwake ni Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele na kushoto kwake ni Mkuu wa matukio Kelvin Edes,Pembeni yake ni Mkurungezi wa Teamtezza Kennan Richard

Bunge kuanzisha Ushirikiano wa kirafiki na Bunge la Israeli

1Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo naye.
2Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone Plotwakati alipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo naye.
3Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
4Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akimkabidhi zawadi ya trei ya kubebea vinywaji mke wa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Bi. Shosh Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
5Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akipokea zawadi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
6Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashililah (wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot (wa pili kushoto) wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu wa Bunge John Joel
7…………………………………………………………………………………………………..
Na Zuhura Mtatifikolo, Bunge
Katibu wa Bunge Tanzania Dkt Thomas Kashililah leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israeli (KNESSET) Ronen Plot aliyemtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam akitokea Nchini Zambia alikokuwa akishiliki Mkutano wa 134 wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika tarehe 19 hadi 23 Machi, 2016.

UTARATIBU WA UHAKIKI WA ORODHA YA MALIPO HAUCHELEWESHI MSHAHARA

UTARATIBU WA UHAKIKI WA ORODHA YA MALIPO HAUCHELEWESHI MSHAHARA-page-001

TANZANIA NA SAUDI ARABIA ZASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA UCHUMI, BIASHARA, UWEKEZAJI, UFUNDI, VIJANA NA MICHEZO

MA1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 
MA2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akiwa katika mazungumzo  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 
MA3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair.
MA4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia kubadilishana hati baada ya uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair.
MA5
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Al Jubair, Waziri Mahiga, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kulia) na ujumbe uliombatana na Waziri Al Jubair. 
MA6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 

SHEREHE YA KUAPISHWA RAIS MTEULE WA ZANZIBAR

OT1
Viongozi wa Dini na Vikosi vya Ulinzi wakifuatana kuelekea katika jukwa maalum la kuapishwa Rais Mteule wa Zanzibar katika uwanja wa Amaan Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
OT2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma kwa Vikozi vya Ulinzi na Usalama baada ya kuapishwa Rasmi katika wamu ya pili ya Uongozi wa awamu ya 7 leo katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
OT3
Kikosi cha Bendera na Vikosi mbali mbali vya Ulinzi wakitoa heshama kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  baada ya kuapishwa Rasmi katika awamu ya pili ya Uongozi wa awamu ya 7 leo katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
OT4
Kikosi cha KMKM kikitoa salamu ya heshma kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  baada ya kuapishwa Rasmi katika awamu ya pili ya Uongozi wa awamu ya 7 leo katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA WIZARA YA AFYA

2vif
Waziri wa  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh Ummy Mwalimu akizungumza na wageni kutoka UNICEF walipomtembelea ofisini kwake. Wakwanza kushoto ni Maniza Zaman muwakilishi kutoka  Chief UNICEF Tanzania na wapili kushoto ni Sudha Shara afisa kutoka UNICEF.
1vif
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ndg. Michael John akikabidhi vifaa muhimu kwaajili ya udhibiti salama wa taka zitokanazo na huduma za afya na usafi kwa hospitali za mfano za mikoa 12 na Wilaya 2 nchini.

Jeshi la Polisi latahadhalisha kuhusu usalama katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka

BULI
Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka ambayo inaanza kesho Ijumaa Kuu, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi,  kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao. Katika kipindi cha sikukuu baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na pale vitakapojitokeza vitadhibitiwa  kwa haraka

Mshana awaaga wafanyakazi TBC na kumkaribisha mkurugenzi mkuu mpya Dk.Ayoub Ryoba.

MSH1
: Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akimkaribisha rasmi katika ofisi za shirika hilo na kumkabidhi rasmi ofisi Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk.Ayoub Ryoba leo jijini Dar es Salaam.
MSH2
Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Dk.Ayoub Ryoba akitia saini kitabu cha wageni Baada ya kukaribishwa na kukabidhiwa rasmi ofisi za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
MSH3
Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk.Ayoub Ryoba Taarifa ya Makabidhiano ya ofisi leo jijini Dar es Salaam.
MSH4
Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana akizungumza jambo wakati wa sherehe za kuwaaga wafanyakazi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) na kumkaribisha mkurugenzi mkuu mpya Dkt.Ayoub Ryoba (wa pili kulia) leo jijini Dar es Salaam.Wengine Pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya TBC Balozi Herbert E.Mrango na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi Bi.Elimbora Muro (wa kwanza kushoto).
MSH5
Wafanyakazi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) wakimskiliza Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk.Ayoub Ryoba (hayupo Pichani) wakati alipokuwa akiongea nao leo jijini Dar es Salaam.
MSH6
Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Dk.Ayoub Ryoba akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo(hawapo pichani) wakati wa kumuaga mkurugenzi mstaafu wa shirika hilo Bw.Clement mshana.

DK. SHEIN ALA KIAPO CHA URAIS WA ZANZIBAR

DK1
Rais Mteule wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo na Jaji Mkuu wa Zanzibar  Mhe,Omar Othman Makungu katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Vituo binafsi vya kutoa huduma za afya vyashauriwa kutoa huduma tiba ya Kifua Kikuu

WAZEE
Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mhe. Ummy Mwalimu ametoa Rai kwa wamiliki wa vituo binafsi vya kutoa huduma za afya kupanua wigo wa huduma n

Mfuko wa wazee wanukia

UMMM
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy mwalimu akizungumza na viongozi na baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es salaam katikati ni Mwenyekiti wawazee hao Mzee hemed Mkali na kulia ni Katibu wa wazee hao Mzee Mohamed Mtulia.

Serikali yataka kuwepo kwa mikataba kati ya makampuni ya utengenezaji na usambazaji wa filamu Tanzania

MWAK1
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fissoo akizungumza na wawakilishi wa kamouni ya usambazaji wa filamu Proin promotion(hawapo pichani) kuhusu mkataba kati ya kampuni hiyo na watengenezaji wa filamu Tanzania kushoto ni Rais wa shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba.
MWAK2
Mwakilishi wa kampuni ya Proin promotion Abraham Kesulie akizungumza wakati wa kikao kati ya kampuni hiyo na Bodi ya Filamu Tanzania kuhus mkataba kati ya watengenezaji wa filamu na kampuni hiyo katikati ni Mumbe wa Bodi ya Filamu Hussein Kim na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Patrick Kipangula.
MWAK3
Mwakilishi wa kampuni ya Proin promotion Abraham Kesulie(Kushoto), hiyo katikati ni Mumbe wa Bodi ya Filamu Hussein Kim na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Patrick Kipangula wakimsikiliza  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fissoo9Hayupo Pichani)  wakati wa kikao kati ya kampuni hiyo na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu mkataba kati ya watengenezaji wa filamu na kampuni.
Picha zote na Shamimu Nyaki WHUSM

TAIFA STARS KUWASILI DAR LEO USIKU

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kuwasili leo saa 8 usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere kikitokea nchini Chad kilipokuwa na mchezo dhidi ya wenyeji jana jioni.
Msafara wa Taifa Stars unaongozwa na mkuu wa msafara ambaye pia ni Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ravia Idarus Faina utaondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa N’Djamena saa 8 mchana kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia, kabla ya kuunganisha ndege saa 4 usiku tayari kwa safari ya kurejea nyumbani Tanzania.
Stars inarejea nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya wenyeji Chad, bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta katika mchezo uliochezwa uwanja wa Omnisport Idriss Mahaymat Ouya jijini N’Djamena katika mchezo wa kundi G kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.
Mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam, kikosi cha Taifa Stars kitaingia moja kwa kwa moja kambini katika hoteli ya Urban Rose iliyopo eneo la Kisutu kujiandaa na mchezo wa marudano utakaochezwa siku ya Jumatatu ya Pasaka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 

RITHA KABATI (CCM) KUTOKA MKOA WA IRINGA ARUDI BUNGENI

rita
WABUNGE wa Viti Maalum watatu wameingia baada ya uchaguzi majimbo yote  kukamilika ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata viti maalum viwili na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mmoja

BODABODA MKOANI MWANZA WAADHIA KUANZISHWA KWA UMOJA WA KITAIFA WA BODABODA.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) akuzungumza katika Mkutano Mkuu Muhura wa Kwanza wa mwaka 2016 wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Mwanza uliofanyika Jumamosi Machi 19,2016 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Pamba Jijini Mwanza. Kushoto kwake ni viongozi wa bodaboda Mkoa wa Mwanza

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

SAU1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na maafisa wa Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara aliyoifanya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.  Katikati ni Mkuu wa wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Abuu Mvano.
SAU2
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi, alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kukagua shughuli zinazofanywa na Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege,  ACP Martin Otieno.
SAU3
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waandishi wa Habari wakati wa ziara yake aliyoifanya kutembelea Idara za Wizara hiyo zilizomo katika Uwanja huo.
SAU4
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro alipotembelea Kituo cha Polisi Buguruni wakati wa ziara yake katika Kituo hicho.
SAU5
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (katikati), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea Uwanja huo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno.
SAU6
Mkuu wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Abuu Mvano (kulia), akiongozana  na Naibu Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), alipotembelea Idara za Wizara hiyo zilizopo katika Uwanja huo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

UZINDUZI WA MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA WAFANYIKA MKOANI DODOMA

RC wa Dodoma, Jordan Rugimbana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3
RC wa Dodoma Jordan Rugibana akiteta na Mkuturenzi wa Mradi wa PS3, Dk. Emmanuel Malangalila, wakati wa uzinduzi
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma wakifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa Mradi wa PS3 mkoani humo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia majadiliano wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma
Dk. Conrad Mbuya wa PS3 akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mradi mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Mradi wa PS3, Dk. Emmanuel Malangalila, akitoa mada kwenye uzunduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais (Utumishi) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3
Matiko Machonchoryo wa PS3 akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma
***************
Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Dodoma siku ya Jumanne na Jumatano, Machi 22-23, 2016. 

 Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd  Ismail Mzava (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu udhamini wa bonanza lililoandali na Kituo cha Mazoezi cha Power or Fitness cha Mwenge litakalofanyika Viwanja vya Leaders Klabu Jumamosi. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Sas  Sangandele. 
Mazoezi yakiendelea katika  Kituo cha Mazoezi cha Power or Fitness cha Mwenge  kilichopo katika Jengo la Tanzanite House lililopo jirani na Kanisa la Full Gaspel.
 Mazoezi yakiendelea kwenye kituo hicho.
 Vyuma vikiinuliwa kwenye kituo hicho.
 Mazoezi yakifanyika.
Hapa ni kazi tu na mazoezi kwa kwenda mbele.
 …………………………………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
 
KITUO cha Mazoezi cha Power or Fitness cha Mwenge kimeandaa bonanza la michezo mbalimbali litakalofanyika Jumamosi Viwanja vya Leaders Klabu jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Sas Sangandele alisema bonanza hilo liwatawahusisha watu wa rika zote wakiwepo watoto.
 
“Bonaza letu litawashirikisha watu wa aina zote na litakuwa la bure na litaanza saa 12 asubuhi hadi jioni hivyo wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongaji vyake tunawaomba wafike kwa wingi kushiriki” alisema Sangandele.
 
Alisema bonanza hilo ambalo limedhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd kupitia kinywaji chake cha Windhoek linakuwa na michezo ya mpira wa miguu, kufukuza kuku, karate kwa watoto, mazoezi ya viungo na mbio za kilometa tano.
 
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo, Ismail Mzava alisema wameamua kudhamini bonanza hilo kutokana na umuhimu wa michezo ambayo inaleta afya kwa jamii.
 
“Kampuni yetu imekuwa ikitoa udhamini mbalimbali katika shughuli za jamii ndio maana tukaona ni vema tukawaunga mkono hawa wenzetu katika jambo hilo muhimu litakalohusisha michezo mbalimbali” alisema Mzava.
 

TRL KUSAFIRISHA SARUJI YA TANGA KWA NJIA YA RELI

SHI1
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela akitoa taarifa ya hali ya miundombinu katika mkoa wa Tanga kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ofisini kwake.
SHI2
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa pili kulia) akimwonesha moja ya nyaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (wa pili kushoto) kabla ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza.
SHI3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa tatu kulia) pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa.
SHI4
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (kushoto) wakisaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Huku Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakishuhudia.
SHI5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia) kabla ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart.
SHI6Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa tatu kulia) pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa
SHI7
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo baada ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart na (Kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela.
SHI8
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akisaidiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa pili kulia) wakipakia mfuko wa saruji kwenye kontena kabla ya kuanza kusafirishwa kwa njia ya reli kutoka katika kiwanda cha Simba Cement kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza.

No comments :

Post a Comment