Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza rasmi
kwa Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki uliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.PICHA NA
IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe
Magufuli akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza
mazungumzo yaliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe
Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa
mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika
Mashariki Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa
mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe
Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa
mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki
uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya kuanza
kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika
Mashariki uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa pamoja na badhi ya Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya
ya Afrika Mashariki uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Uganda
Yoweri Museven baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani
Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki
EAC,(kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kuwasili
katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa
Nchi za Afrika ya Mashariki EAC,[Picha na Ikulu.]
Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika
ya Mashariki wakisimama wakati wimbo wa umoja wa nchi hizo ukipigwa
katika mkutano wa 17 wa EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto mkoani
Arusha,[Picha na Ikulu.]
Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika
ya Mashariki akiwemo mwenyekiti wa mkutano wa 17 wa EAC Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuanza kwa
mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Ngrdoto Mkoani
Arusha,[Picha na Ikulu.]
Mwenyekiti wa Mkutano wa 17 wa
Afrika ya Mashariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John
Pombe Magufuli (wa tatu kushoto) akiongoza mkutano huo uliofanyika leo
ukumbi wa Ngrdoto Hotel mkoani Arusha,wengine ni Vionngozi mbali wa
Jumuiya hiyokamawanavyoonekanwa,[Picha na Ikulu.]
Baadhi ya waalikwa katika wakiwa
katika ukumbi wa mkutano Ngurdoto Mkoani Arusha leo wakimsikiliza
Mwenyekiti wa Mkutano wa 17 wa Afrika ya Mashariki Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (kulia) akitoa hutuba yake
ya ufunguzi wa mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya
Mashariki EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto Hotel Mkoani
Arusha,{Picha na Ikulu.]
Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
walioalikwa katika mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya
Mashariki EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto Hotel Mkoani
Arusha,(katikati) Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora
Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini,akiwa na Mawaaziri wa Nchi za Jumuiya
hiyo,{Picha na Ikulu.]
18 KUIVAA SIMBA SC
Kocha Mkuu wa Mbeya City Fc,
Kinnah Phiri ametangaza majina ya nyota 18 watakaoivaa Simba Sports Club
kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacoma Tanzania bara uliopangwa
kuchezwa jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Mapema leo Phiri ameuambia
mtandao huu kuwa anatua jijini Dar na kikosi cha nyota hao ambao
aliwaandaa maalumu kwa mchezo huo wa mwishoni mwa juma akiwa na imani
kubwa kuwa wataiwezesha City kuibuka na ushindi kutokana na kuiva
vizuri kimazoezi na mafunzo waliyoyapata katika wiki nzima ya
maandalizianya .
“Nina imani nao kuwa,wamefanya
vizuri sana kwenye mazoezi ya wiki hii, sina shaka na wao kutupatia
matokeo kwa sababu wako sawa tayari kwa mchezo,tutacheza kwenye mfumo
mpya ambao haujawahi kuonekana tukicheza, hii ni kwa sababu tumedhamiria
kupata ushindi kama ambavyo timu imekuwa ikifanya kila inapokutana na
Simba”, alisema.
Miongoni mwa nyota walio kwenye
orodha ya kuivaa Simba siku hiyo ya jumapili ni pamoja na mlinzi Hassan
Mwasapili, mlinda lango Haningtony Kalyesubula pia wamo Temi Felix,
Haruna Shamte,Yohana Moriss,Kenny Ally na wakali wengine 12 ambao
wamepewa majukumu kadhaa kuhakikisha City inaandikisha pointi tatu
muhimu mbele ya timu hiyo ya Msimbazi.
Profesa Lawurence Museru akutana na Mtaalamu wa Mfumo wa Chakula na Ini
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawurence Museru akizungumza na
Mtaalamu wa Mfumo wa Chakula na Ini, Profesa Abdel Meguid Kassem pamoja
na Classen ambao wametoa msaada wa huduma za afya kwa wagonjwa katika
hospitali hiyo. Wataalamu hao wanatoka Ujerumani.
Mtaalamu wa Mfumo wa Chakula na
Ini, Profesa Abdel Meguid Kassem pamoja na Classen wakizungumza LEO na
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa
Lawurence leo kwenye hospitali hiyo.
Mmoja wa madaktari wa masuala ya
Mfumo wa Chakula katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
akizungumza kwenye mkutano huo leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawurence akizungumza na wataalamu hao LEO.
MCHEZO MGUMU, MBEYA CITY INANAFASI: REDONDO
Kiungo
mshambuliaji wa City, Ramadhani Chombo Redondo amesema mchezo wa ligi
kuu ya soka Tanzania dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa jumapili hii
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar utakuwa mgumu kutokana na mazingira ya
timu zote mbili.
Akizungumza na mbeyacityfc.com
mapema leo, Chombo amesema kuwa City inakwenda Dar kucheza mchezo huo
ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa uliopita kama ilivyo kwa
simba, jambo ambalo linaufanya mchezo huo kuwa mgumu kutokana na uhitaji
wa matokeo kwa timu zote.
WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA FEDHA WA MIL 220, KWA MATIBABU YA WAGONJWA WA MOYO
Kaimu
Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi akisoma
taarifa fupi juu ya magonjwa wagonjwa wa moyo wanaopatiwa matibabu
katika taasisi hiyo na namna walivyojipanga kutoa matibabu ya upasuaji
kwa watoto hao 101, waliolipiwa gharama za matibabu kutoka BAPS Charity.
Wengine ni Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wa BAPS
Charity.
Waziri
Ummy Mwalimu akiongea na mmoja wa wazazi waliokuwa katika tukio hilo la
kukabidhiwa fedha kiasi cha Mil 220, kwa ajili ya wagonjwa wa moyo 101,
ambao wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika taasisi ya JKCI.
Waziri
wa Afya, Ummy Mwalimu akipata kumjulia hali mtoto Zahara Seleman Muna
(10) ambaye anasumbuliwa na magonjwa ya moyo. Hata hivyo Waziri Ummy
Mwalimu amejitolea kama Waziri kuhakikisha atawasaidia watoto hao katika
kutimiza ndoto zao ikiwemo kuwasomesha na masuala mengine kupitia
Wizara yake ambayo yenye dhamana, Waziri Ummy aliguswa na watoto hao
kutokana na ndoto zao walizokuwa nazo ikiwemo kusoma zaidi.
Mwenyekiti
wa taasisi ya BAPS Charity, Subhash Patel, akizungumza machache
kuhusiana na mchango huo wa Milioni 220, kwa ajili ya matibabu ya watoto
101, ambapo pia aliomba wadau wengine kujitokeza kuchangia ilikuisaidia
Serikali katika kuhakikisha uhai kwa wagonjwa wa moyo hasa watoto hapa
nchini.
Bw.
Alfred D. Dafi mkazi wa Karatu akiwa amembeba mtoto wake, Beatrice
Alfred (13) akitoa shukrani zake kwa Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu
kwa kuweza kuchukua majukumu ya kumsaidia mtoto wake katika masuala ya
kumsomesha na mambo mengine kama Waziri mwenye dhamana. Waziri amechukua
jukumu ya kuwasaidia watoto hao, kutokana na kuguswa na ndoto
walizonazo ikiwemo kusoma wafike mbali. Mtoto huyo Beatrice hadi sasa
anasoma darasa la sita, katika shule ya Sumawe, iliyopo Karatu.
Dk.
Naiz Majani, ambaye ni daktari wa watoto wa magonjwa ya moyo akitoa
ufafanuzi kwa wanahabari juu ya matatizo ya magonjwa ya moyoo ambapo
amebainisha kuwa kati ya asilimia 10, pekee magonjwa ya moyo yanabainika
kwa mwanamke huku miongoni mwa wazazi wanaozaa watoto wenye matatizo ya
moyo ni wale waliokosa chanjo mbalimbali ikiwemo ya Lubela na mambo
mengine.
Watoto
Beatrice Alfred (13) na Zahara Seleman Muna (10) wakiwa katika picha ya
pamoja. Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu ameamua kujitolea kuwasaidia
kutimiza ndoto zao ikiwemo suala la kuwasomesha na mahitaji mengine kama
Waziri mwenye dhamana. Kushoto ni Baba wa mtoto Beatrice, Bw. Alfred
Dafi ambaye anatokea Karatu.
Waziri
Ummy Mwalimu akimpa pole dada wa Zahara Seleman Muna (10), Editha
Foi,(kulia) aliyekuwa akilia kwa uchungu baada ya Waziri Ummy Mwalimu
kuamua kujitolea kuwasaidia watoto hao iliwatimize ndoto yao ya elimu na
mahitaji mengine kama Waziri Mwenye dhamana.
“Uchungu
wa Mama”, Waziri Ummy Mwalimu akiwa na watoto Beatrice na Zahara ambao
wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo, ambapo baada ya kuwajulia hali na
kuguswa na ndoto zao za kielimu, Waziri Ummy Mwalimu ameguswa na watoto
hao na kuamua kuwasaidia katika elimu na mambo mengine kama Waziri
mwenye dhamana.
.
Waziri
Ummy Mwalimu akiwa akipeana mkono na baada ya kukabidhiwa hundi ya sh.
Mil 220, iliyotolewa na taasisi ya BAPS Charity kwa ajili ya kusaidia
matibabu ya watoto 101, wa magonjwa ya moyo waliopo katika taasisi ya
JKCI.
.
WAZIRI JANUARY MAKAMBA AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA MATUMIZI SALAMA YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba
(kulia), akizungumza na wajumbe wapya wa kamati ya kitaifa ya matumizi
salama ya bioteknojia ya kisasa wakati akiizindua rasmi Dar es Salaam
leo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI). Kushoto ni
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour.
Msimamizi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph
Ndunguru (kushoto), akitoa mada kuhusu zao la muhogo na changamoto za
magonjwa yanayolishambulia.
Baadhi ya wanakamati hao wakiwa ukumbini katika hafla
hiyo ya uzinduzi.
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa bize wakati wa uzinduzi huo.
Wajumbe wa kamti hiyo
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dk. Julius Ningu
(kulia), akizungumza kwenye mkutano huo wa uzinduzi
Mkutano ukiendelea.
Waziri
Makmba (kulia), akiwaongoza viongozi wengine kutembelea maabara ya
kisasa ya utafiti ya MARI. Kutoka kushoto ni Msimamizi Mkuu wa Taasisi
ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru, Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour na Profesa Raphael Chibunda.
Picha ya pamoja na Waziri Makamba.
Msimamizi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph
Ndunguru (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Makama na wajumbe wa
kamati mpya jinsi maabara ya kisasa ya utafiti ya MARI inavyofanya kazi.
Mimea mbalimbali inayofanyiwa utafiti ikiwa katika chupa maalumu katika maabara hiyo.
Mbegu ya migomba iliyooteshwa baada ya kufanyiwa utafiti katika kituo hicho cha MARI.
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MHE. ANASTAZIA WAMBURA AZIDI KUPOKEA MICHANGO YA TIMU YA TWIGA STARS
Mhasibu wa Wizara ya Habari ,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Godfrey Osmund akimweleza Naibu waziri wa
wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura jinsi atakavyozikatia risiti fedha
ambazo wadau wa michezo wamezitoa kwa ajili ya kuichangia Timu ya Taifa
ya wanawake ya Mpira wa miguu ya Twiga Stars.
Naibu Waziri wa Habari ,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi leo
Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund shilingi milioni mbili
zilizotolewa na Mohammed Dewji kwaajili ya kuisaidia timu ya Taifa ya
wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Hadi sasa wadau wa michezo
wameshaichangia timu hiyo shilingi milioni 17.
Picha na Anna Nkinda
Spika Job Ndugai amtembelea na kumpa pole Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuafuatia kifo cha kaka yake Mzee Selemani Mrisho Kikwete.
Baadhi ya waomborezaji waliohudhuria kuhani msiba nyumbani kwa marehemu mzee Selemani Mrisho Kikwete kwa ajili ya kutoa pole leo Jijini Dar es Salaam. |
(Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo)
TANZANIA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA KUAJIRI MAHOTELI..RIPOTI YA JOVAGO
Afisa habari na uhusiano wa
kampuni Jovago Tanzania Lilian Kisasa akizungumza katika uzinduzi huo
ambapo alisema hapa Tanzania sekta ya utalii imeweza kuajiri watu zaidi
ya laki sita na endapo huduma nzuri zitaboreshwa katika sekta hiyo upo
uwezekano wa kuajiri watu zaidi ya hapo jambo ambalo litapunguza hata
tatizo la ajira hapa nchini.(Pamela Mollel jamiiblog)
Wanahabari wakiwa katika uzinduzi wa ripoti
Meneja mkazi wa kampuni ya Jovago Tanzania Andrea Guzzoni alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi wa ripoti ya mwisho yenye utafiti inayohusiana na sekta ya utalii ili kuweka wazi hali inayoikabili sekta hiyo.
IMEBAINIKA kuwa Tanzania
inakabiliwa na changamoto ya kuwaajiri mahotelia wasio kuwa na ujuzi wa
kutosha katika sekta ya utalii haswa kwenye hoteli hali ambayo
inarudisha nyuma uchumi wa nchi tofauti na nchi nyinginezo za nje ya
nchi
BMT kuadhimisha siku ya wanawake Duniani kwa Kushiriki katika Michezo.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Michezo Tanzania (BMT) Bi. Zaynab Matitu akiongea na waandishi wa Habari
hawapo pichani kuhusu kushiriki katika michezo itayofanyika Machi 5
mwaka huu ili kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani katika uwanja wa
Uhuru jijini Dar es salaam kushoto ni Mwenyekiti wa wa Baraza hilo Bw.
Diomiz Malinzi.
Mwenyekiti wa wa Baraza la
Michezo Tanzania (BMT) Bw. Diomiz Malinzi akiongea na waandishi wa
Habari hawapo pichani kuhusu kushiriki katika michezo itayofanyika Machi
5 mwaka huu ili kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani katika uwanja
wa Uhuru jijini Dar es salaam kulia ni Makamu Mwenyekiti Bi. Zaynab
Matitu.
Picha zote na Ally Daud – Maelezo
DK. AWATAKA WAFANYABIASHARA KUTOKWEPA KULIPA KODI
Mahmoud Ahmad Arusha
WAZIRI wa Fedha na Mipango ,
Dakta Philipo Mpango, amesisitiza wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa
kodi zao kwa wakati na kuwaonya wale wote ambao watakwepa
watashughulikiwa kwa mjibu wa sheria ili kuboresha huduma za jamii na
maendeleo ya taifa.
Alisema kuwa serikali mkakati
wa serikali ni ni kuongeza makusanyo na kulinda utulivu wa uchumi
ukuaji wake kwa kasi zaidi kwa kuwa wafanyabiashara ndio injini ya
chumi wa taifa.
Alisema nchi yetu ina utajiri
mkubwa wa raslimali ila bado nchi ni masikini akasisitiza umuhimu wa
kila mmoja kulipa kodi na kuwahakikishia kuwa serikali haitamuonea
mfanyabiashara yeyoyte na badala yake kutajengwa mazingira ya
kuwawezesha kulipa kodi bila usumbufu
Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan mgeni rasmi tamasha la wanawake
Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark
Bi. Agnes Mgongo (katikati) akiongea na waandishi wa habari kuhusu
tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia
litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016, ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi kushoto kwake ni Mratibu wa tamasha hilo Bi. Anawery Phares
na kulia ni mshehereshaji (MC Pilipili) Bw. Emanuel Mathias.
Mratibu wa Tamasha la pamoja la
kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016
Bi. Anawery Phares(katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo ambapo Mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Bi. Samia Suluhu Hassan,Kushoto ni Mwanamuzi wa Taarabu Bi. Patricia
Hillary na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Bi.Agnes Mgongo.
Mchekeshaji na Mshehereshaji Bw.
Emanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili akito kionjo cha mojawapo ya
kichekesho atakachokifanya siku ya tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku
ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016,kushoto ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo na kulia ni Mwakilishi wa
Children Survial Hut Tanzania (CSI) Bi.Stella Mranda.
Msanii wa Muziki wa Taarabu
Nchini Bi .Patricia Hillary akieleza jambo wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kwa tamasha la
pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5
Machi, 2016 ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.(Picha na
Lorietha Laurence-Maelezo).
Serikali yaahidi kuwapatia vijana mitaji kwa ajili ya kilimo cha kisasa
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu
ya kilimo cha mbogamboga toka kwa Mwenyekiti Kinondoni Saccoss Neema
Urio (Kulia) katika ufunguzi mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana
kulia mwa Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana ni Mkurugenzi Msaidizi Mafunzo
Idara ya Vijana Venerose Mtenga na kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji
Idara ya Vijana Esther Riwa.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu
ya matumizi ya jiko linalotumia nishati ya jua toka kwa Meneja wa
Tanzania Agriculture Productivity Programme Praygod Mushi (Kulia) katika
ufunguzi mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kushoto ni Mkurugenzi
Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther Riwa.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi, Ajira,Vijjana
na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (mwenye koti la Draft) akitoa
ushauri kwa wajasiriamali toka Pop Up the Best Tailoring wa Sinza Dar es
Salaam walioshiriki mafunzo ya usajasiriamali yaliyofanyika Jijini Dar
es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther
Riwa.
Mkurugenzi Uhamasishaji, Idara ya
Vijana Esther Riwa akizungumza na washiriki (Hawapo pichani) wa mafunzo
ya ya kilimo cha kisasa kwa vijana yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya vijana wakimsikiliza
mtoa mada(Hayupo pichani) juu ya juu ya kilimo cha kisasa kwa vijna
katika mafunzo yaliyofanyika Jiji Dar es salaam na kushirikisha vijana
toka Dar es salaam na pwani.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya
kilimo cha kisasa kwa vijana Bi. Jasmin John akitoa neno la shukrani kwa
mgeni rasmi mara baada ya kufungua mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku
tatu Jijini Dar es salaam.
MIKOA NANE NCHINI INATISHIWA KUWA JANGWA – MPINA
NAIBU
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Bw.
Luhaga Mpina amesema mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa nane hapa
nchini ambayo inakabiliwa na tishio la kugeuka jangwa kutokana na tatizo
la ukataji miti hovyo.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Simiyu, Mwanza, Mara, Singida na Arusha. Mingine ni Kilimanjaro, Dodoma na Manyara.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumanne, Machi 2, 2016) alipopewa nafasi na waziri Mkuu Kassim Majaliwa
awasalimie wananchi waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi
kwenye jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani
Simiyu.
Alisema kila wilaya imepewa agizo
la kupanda miche milioni 1.5 kwa mwaka na kwa sababu hiyo watawapima
wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurudenzi wa halmashauri na
Manispaa ambao hawatafikisha idadi hiyo ya miche na kuwasilisha majina
yao kwa Waziri Mkuu.
“Ilani ya Chama cha Mapinduzi
imeagiza kila wilaya ipade miche milioni 1.5 kwa mwaka. Kwa hiyo kuanzia
Machi 3, mwaka ambayo ni siku ya upandaji miti, tutawamoniter Wakuu wa
Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote ili kubaini ni nani hajatekeleza agizo
hili. Tutakuletea mezani kwako majina ya wale ambao watashindwa
kutekeleza agizo hili ambalo liko kwenye Ilana ya CCM,” alisema.
Kwa upande wake, Naibu Waziri
huyo alisema amekuja na miche 7,000 ya matunda aina ya miembe, michungwa
na mifenesi ambayo ameahidi kuigawa kwa kila wilaya. “Tunataka katika
ziara yako hii tusambaze miche 5,000 kwa kila jimbo la mkoa huu na
wakati unamaliza ziara yako tutakuwa tumesambaza miche 35,000,” alisema.
Naibu waziri Mpina alisema
kupandwa kwa miti mbalimbali ya matunda, kutawasaidia wananchi kupata
matunda ya kula, ya kuuza na kupata fedha lakini pia itawasaidia kuwa
chanzo cha mali ghafi kwenye viwanda vya kusindika matunda.
WAZIRI MKUU AAGIZA WATUMISHI WOTE WAHAMIE BUSEGA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa wodi ya Wazazi katika kijiji
cha Nyashimo wilaya ya Busega akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu
Machi 2, 2016. Kushoto ni Mbunge wa Busega, Dkt, Raphael Chegeni na
Kulia nI Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Titus Kamani. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………………………………
No comments :
Post a Comment