Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango kazi wa
Taifa wa Dawa vifaa Tiba na vitendanishi kwa miaka mitano (2015-2020)
leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi
mkutano wa Mpango kazi wa Taifa wa Dawa vifaa Tiba na vitendanishi kwa
miaka mitano (2015-2020) leo jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Mfamasia
Mkuu wa Serikali Henry Irundo na kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali
Muhamad Kambi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya (katikati) akionyesha taarifa ya Mpango kazi wa
Taifa wa Dawa vifaa Tiba na vitendanishi kwa miaka mitano (2015-2020)
baada ya uzinduzi leo jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Mfamasia Mkuu wa
Serikali Henry Irundo na kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Muhamad Kambi.
Wajumbe
waliohudhuria uzinduzi wa Mpango kazi wa Taifa wa Dawa vifaa Tiba na
vitendanishi kwa miaka mitano (2015-2020) leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja
na wajumbe wa mkutano wa taarifa ya Mpango kazi wa Taifa wa Dawa vifaa
Tiba na vitendanishi kwa miaka mitano (2015-2020) leo jijini Dar es
Salaam.
(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)
Waziri Nape awataka wauzaji wa Filamu za Nje kufuata sheria.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wauzaji wa filamu za nje
kuhusu kufuata sheria ya uuzaji wa filamu hizo hapa nchini katika kikao
kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi
ya Filamu Bi.Joyce Fissoo.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi
Joyce Fissoo akieleza jambo wakati kikao kati ya Serikali na wauzaji wa
Filamu za nje(Hawapo Pichani) kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam
.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Bodi hiyo Bw Tairo.
Mwenyekiti wa wauzaji wa filamu
za nje Bw Joseph Lyakurwa akiwasilishwa mada kwa Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wakati wa kikao baina
ya Serikali na wauzaji wa filamu hizo kilichofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
: Baadhi ya wauzaji wa Filamu za
nje walioshiriki katika kikao kati yao na Serikali cha kubadilisha
sheria ya uuzaji wa filamu za nje hapa nchini kilichofanyika leo jijjini
Dar es Salaam
BMT KUANZISHA SEMINA YA WADHAMINI.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Baraza la MichezoTaifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani akielezea Semina ya
masoko na wadhamini wa Michezo Nchini katika mkutano uliofanyika leo
jijini Dar es salaam kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali
ya Pro- Event Masters Ltd Bw. Henry Tandau.
Mkurugenzi
wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Pro- Event Masters Ltd Bw. Henry
Tandau akiongea na waandishi wahabari hawapo pichani akielezea Semina ya
masoko na wadhamini wa Michezo Nchini katika mkutano uliofanyika leo
jijini Dar es salaam kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la
MichezoTaifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja.
PICHA ZOTE NA ALLY DAUD-MAELEZO
PICHA ZOTE NA ALLY DAUD-MAELEZO
NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI-MWANZA
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni,
akisalimiana na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza mara baada ya
kuwasili jijini hapo jana akitokea mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni
akisaini katika kitabu mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la
Polisi jijini Mwanza,mara baada ya kuwasili jijini hapo jana akitokea
Kagera kwa ziara ya kikazi.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,ACP Japhet Lusingu(kushoto), akitoa
taarifa ya hali ya usalama katika mkoa wa Mwanza kwa Naibu Waziri wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati) mara
baada ya Naibu Waziri kuwasili jijini Mwanza jana akitokea mkoani Kagera
kwa ziara ya kikazi.Kulia ni Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai mkoa
wa Mwanza,SSP Augustine Senga.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni,
akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza mara
baada ya kuwasili jijini hapo jana akitokea Kagera kwa ziara ya kikazi.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WAGAWA VIFAA VYA KUSOMEA NA
KUFANYA KAMPENI YA KUHAMASISHA KUACHA MAUAJI KATI YA WAKULIMA NA
WAFUGAJI WILAYANI KILOSA.
Maafisa
Habari na Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kilosa
wakati alipokuwa akiongea nao walipotembelea shule ya palakuyo kutoa
vifaa vya kusomea masomo ya Sayansi na kufanya kampeni ya kuhamasisha
kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Maafisa
Habari na Mawasiliano Serikalini wakifanya kampeni ya kuhamasisha
kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa.maafisa hao
walitoa pia msaada wa vifaa vya kusomea masomo ya sayansi.
Meneja
Uhusiano na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi.sylvia
Lupembe(kushoto) akikabidhi vifaa vya kusomea masomo ya sayansi kwa mkuu
wa wilaya ya kilosa Bw.John Henjewele wakati wakati wa kampeni ya
kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akigawa msaada wa
vitabu kwa watoto wa shule ya Mabwerebwere wilayani kilosa wakati
walipotembelea walayani hapo kusaidia masuala ya elimu pamoja na kufanya
kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Mkurugenzi
Idara ya Habari- MAELEZO Bw.Assa Mwambene(wa tatu kushoto) akikabidhi
madawati kwa watoto wa shule ya msingi Tindiga wakati maafisa habari na
mawasiliano wa serikali walipotembelea shule hiyo kugawa madawati na
kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na
wafugaji wilayani kilosa.Wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya kilosa
Bw.John Henjewele(wa pili kulia).
Picha na Daudi Manongi.
Picha na Daudi Manongi.
ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA – CHATO
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Joyce Thobias na mwanae Jonathan
Mbarak ambaye amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Chato akimuuguza
mwanae majeraha ya moto Machi 16,2916. mheshimiwa Pinda alikuwa katika
siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Geita.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha gari la wagonjwa likiwa ni oja kati ya
mawili yaliyotolewa msaada na Bibi Merete Trolle wa Denmark akisaidiwa
kulisafilisha had hapa nchini na Mgodi wa Geita Gold Mine. Makbidhiano
hayo yalifanyika kwenye hospitali ya wilaya ya Chato Machi 162016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua duka la dawa la MSD baada ya kulizindua
kwenye hospitali ya wilaya ya Chato Machi16, 2016. Kulia ni Mwenyekiti
wa Bodi ya MSD, Profesa Mtulia.Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanachama wa Ushirika wa kiwanda
cha kuchambua pamba cha Biharamulo Cooperative Union mjini Chato ,Machi
16, 2016
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ACCESS BANK WATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM WANAOSOMA SHULE YA MSINGI MTAMBANI
Meneja
Masoko wa AccessBank Mr.Muganyizi Jonas Bisheko Akikabidhi Vifaa
Mbalimbali kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum wanaosoma shule ya
Msingi Mtambani Iliyopo Boko Manispaa ya Kinondoni.
Benki
ya Access Bank imetoa Msaada wa Wanafunzi Wenye Mahitaji maalumu
wanaosoma Shule ya Msingi Mtambani Manispaa ya Kinondoni.Meneja Masoko
kutoka Access Bank alisema Msaada huo ni sehemu ya faida ya Benki hiyo
Ambayo Wnarudisha kwa Jamii ya Watanzania hivyo waliguswa na Changamoto
Kubwa Zinazowakabili Wanafunzi hao ikiwwemo Ukosefu wa Miundo mbinu
Rafiki kwajili ya Wanafunzi hao kama Madarasa vyoo na Vitendea kazi
vingine.Akieleza zaidi Bw Muganyizi
Jonas Bisheko Ameomba Makampuni Mbalimbali Kujitokeza Kuwasidia
wanafunzi wao wenye mahitaji Maalum kwa lengo la kuwezesha kupata elimu
Bora kawa Wanafunzi wengine.Benki
hiyo imetoa Vifaa mbalimbali vya kujifunzia pamoja na Michezo kwajili
ya kusaidia kutatua Changamoto zinazowakabili wanafunzi hao
Msaada
huo unajumuisha vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya kujifunzia pamoja na
Michezo,akieleza zaidi Meneja Masoko wa Benki hiyo amesema Accessbenk
imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii ya watanzania hasa kupitia sekta
ya elimu kwa kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo kama vile
ukosefu wa vifaa na mazingira rafiki ya kuwezesha kutoa elimu bora
Mwalimu
wa shule ya Msingi mtambani anayehusika na Kitengo cha wanafunzi wenye
Mahitaji Maalum akitoa neno la shukrani Mara baada ya Kupokea Msaada
huo.Ameishukuru sana Accessbenki kwa msaada wao amesema kwa kiasi utatua
Changamoto zinazowakabili wanafunzi hao.
Wanafunzi Wenye mahitaji Maalum kutoka Shule ya msingi mtambani walionufaika na msaada huo kutoka accessbenki.
JAJI MKUU ASEMA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR NI HALALI KISHERIA
Jaji
Mkuu wa Zanzibar akiwa katika ukaguzi wa maendelea ya idara hii ya
mahakama visiwani Pemba ameongea hayo katika mahojiano maalumu na Focus
Media juu ya hali ya kisiasa na uchaguzi wa marudio Zanzibar mapema
tarehe 16 March 2015
Amesema hadi sasa hakuna
pingamizi lolote la kisheria lililoletwa mezani kwa ajili ya pingamizi
kisheria la uchaguzi wa Marudio,amesema wananchi wamegubikwa na ushabiki
bila kufuata kanuni na sheria za uchaguzi,uchaguzi utafanyika kwa
mujibu wa sheria na amewataka wananchi kujitokeza kwa amani na utulivu
kuhakikisha wanapata viongozi bora.
WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI MAAFISA WAWILI CHATO
Aagiza TAKUKURU na Polisi kuanza uchunguzi mara moja
WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya
ya Chato kwa tuhuma za ubadhirifu, rushwa na matumizi mabaya ya
madaraka.
Watumishi hao ni Mkuu wa
Idara ya Kilimo na Ushirika, Bw. Mwita Mirumbe Waryuba pamoja na Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Bw. Dioniz Mutayoba.
TANZANIA RED CARPET YAFANA SEATTLE, WASHINGTON STATE
Mama
mitindo Asya Idarous Khamsini (kati) akiwa katika picha ya pamoja na
mashabiki wake wa mitindo kwenye usiku wa Tanzania Red Carpet
uliofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 mjini Seattle jimbo la
Washington na kuhudhuriwa na Watanzania wanaoishi jimbo hilo na marafiki
zao.
Mama mitindo Asya Idarous Khamsini akipata ukodak moment.
Wavaaji nguo za mitindo wakipata picha ya pamoja na mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
RC MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA APOKELEWA OFISI KWAKE NA KUZUNGUMZA NA WAKUU WA IDARA NA VITENGO MBALIMBALI NA KUTOA MAAGIZO MAZITO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda akishukua kutoka kwenye gari lake la Ukuu wa Mkoa wakati
alipokuwa akifika kwa mara ya kwanza ofisini kwake Dar es Salaam leo
mchana.
Katibu
Tawala Msaidizi- Utawala, Ellha Mcha (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumpokea rasmi jana
alipofika kwa mara ya kwanza katika ofisi yake.
Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shabani Mhando akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkurugenzi mpya wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli akisalimiana na Mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kushoto),
akizungumza wakati wa kumakribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na RC Paul Makonda.
Wakuu wa Idara mbalimbali katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye hafla ya kumpokea mkuu wao wa mkoa.
Mkutano ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, akimkabidhi kadi ya kumkaribisha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, Raymond Mushi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali katika ofisi yake
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YATEMBELEA TAKUKURU NA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki
(Mb) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala yaliyoulizwa wakati wa kikao.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw.
Valentino Mlowola akitoa maelezo kuhusu taasisi anayoiongoza kwa wajumbe
wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jason
Rweikiza (Mb) akitambulisha kamati anayoiongoza.
Mmoja
wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
Mhe. Ruth Mollel (Mb) akitoa mchango wake katika kikao.
Sehemu
ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
(mkono wa kushoto) wakisalimiana na wafanyakazi wa Sekretarieti ya
Ajira katika Utumishi wa Umma kabla ya kikao.
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xvier Daudi
akiwasilisha mada kuhusu taasisi anayoiongoza kwa wajumbe wa kamati ya
Bunge, hawapo pichani.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro, kushoto, akitoa
ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi wakati wa kikao na
kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kilichofanyika
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Waziri
wa Nchi, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kulia,
akifafanua jambo wakati wa kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala
na Serikali za Mitaa kilichofanyika Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma.
No comments :
Post a Comment