Mkurugenzi
Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius
Kahyarara akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa
NSSF, Yacoub Kidula.
Wataalamu
wa ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisalimiana na Mkurugenzi Mkuu mpya
wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
Barabara za kuingilia darajani upande wa Kurasini.
Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akionyesha njia za kuingia na kutoka darajani
Barabara ya kuingilia darajani upande wa kushoto na barabara ya kutokea mjini upande wa kulia.
Mkurugenzi
Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius
Kahyarara (wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa wahandisi wa
ujenzi wa daraja la Kigamboni wakati wa ziara yake ya kutembelea daraja
la Kigamboni.
Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akifafanua jambo
kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Prof. Godius Kahyarara (katika) alipotembelea daraja wa Kigamboni
jijini Dar es Salaam, daraja hilo linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya kumalizika kwa ujenzi wake
kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Prof. Godius Kahyarara (katika) alipotembelea daraja wa Kigamboni
jijini Dar es Salaam, daraja hilo linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya kumalizika kwa ujenzi wake
MABADILIKO YA RATIBA SHUGHULI ZA KAMATI ZA BUNGE
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
Kufuatia mabadiliko ya tarehe ya
kupokea Mapendekezo ya Mpango na kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali
kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017, Ofisi ya Bunge imefanya mabadiliko ya
tarehe za shughuli za Kamati za Bunge kuelekea Mkutano wa tatu wa Bunge
(Mkutano wa Bajeti) ili kuendana na masharti ya Kanuni za Bunge kuhusu
shughuli hizo. Kwa mabadiliko hayo , ratiba ya shughuli za Kamati
itakuwa kama ifuatavyo:-
- Tarehe 29/3/2016 hadi tarehe 4/4/2016 Kamati za Kudumu za Kisekta zitatembelea na kukagua utekelezaji wa miradi iliyotengewa Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(1) ya Kanuni za Bunge. Hapo awali kazi hii ilipangwa kufanyika tarehe 31/3/2016 hadi 6/4/2016.
- Tarehe 5/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 96 ya Kanuni za Bunge, Serikali itawasilisha Dondoo na Randama za Vitabu vya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Awali kazi hii ilipangwa kufanyika tarehe 29/3/2016;
- Tarehe 6/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 97(1)-(2) ya Kanuni za Bunge kutakuwa na Mkutano wa Wabunge wote ambapo Serikali itawasilisha Mapendekezo ya Mpango na kiwango cha ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Awali kazi hii ilipangwa kufanyika tarehe 30/3/2016;
- Tarehe 7/4/2016 hadi 15/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 98 (2) ya Kanuni za Bunge, kwa kipindi cha siku tisa (9) Kamati za Kudumu za Kisekta zitachambua taarifa za utekelezaji wa Bajeti za Wizara zinazosimamiwa na Kamati hizo. Katika kipindi hicho, Kamati ya Bajeti itafanya uchambuzi wa Mapendekezo ya Mpango na kiwango cha ukomo wa Bajeti kwa Mwaka
wa fedha 2016/2017. Awali Kamati ya Bajeti ingefanya kazi hii kuanzia tarehe 31/3/2016 hadi 6/4/2016;
- Tarehe 15/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 98(3) ya Kanuni za Bunge kutakuwa na Kikao cha pamoja kati ya Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti ili kujadili mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara mbalimbali;
- Tarehe 16 na 17 Aprili, 2016 kama ilivyokuwa imepangwa awali Wabunge wataelekea Dodoma tayari kwa Shughuli za Mkutano wa Tatu wa Bunge ambao utaanza tarehe 19 Aprili, 2016.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
25 Machi, 2016.
WAGOMBEA USPIKA BUNGE LAWAWAKILISHI ZANZIBAR WAMKATAA KIFICHO
……………………………………….
HEKAHEKA
zimeanza Visiwani Zanzibar ambapo wagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la
Wawakilishi wameanza kupigana vikumbo kuwania nafasi hiyo huku sura
mpya za vijana wenye damu mbichi zikijitokeza kuchuana na mkongwe
aliyechukua tena fomu ya kutetea nafasi yake Mhe Pandu Ameri Kificho.
Kificho
ni Spika wa Bunge la Wawakilishi kwa muda wamiaka 25 sasa ambapo
wanachama wa CCM Zanzibar tayari wameanza kutilia mashaka uamuazi wa
spika huyo aliyechukua fomu za kugombea tena akitaka kuendelea na
kuongoza kiti cha uspika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, jambo,
inalozua maswali mengi yasiyo na majibu.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ASHUHUDIA KUORODHESHWA KWA HISA STAHILI ZA MAENDELEO BANK PLC, KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM (DSE)
Naibu
Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji, Mwenyekiti wa Maendeleo
Benki, Amulike Ngeliama (kushoto) na Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na
Mipango wa(CMSA) Nicodemus Mukama wakifuatilia jambo katika hafla hiyo.
Naibu
Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akipiga kengele kuashiria
uorodheshwaji rasmi wa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE jana.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Maendeleo Benki, Amulike Ngeliama na Mkurugenzi
wa Capital Markets na Securities Authoriy (CMSA) Nicodemus Mukama
Emmanuel Nyalali, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji DSE akizungumza katika hafla hiyo.
Naibu
Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akiongea wakati wa hafla
ya kuorodheshwa kwa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE
Mkurugenzi
mtendaji wa Maendeleo Benki, Ibrahim Mwangalaba akitoa hotuba yake
kabla ya kumkaribisah Mwenyekiti wa Benki hiyo kuzungumza na washiriki
wa hafla hiyo.
……………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Bank
PLC ni benki iliyoanzishwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania,
Dayosisi ya Mashariki na Pwani na inamilikiwa na Wananchi mbalimbali
kwa njia ya HISA bila kujali, kabila, itikadi, dini wala rangi, kwani
benki hii imesajiliwa na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE), kupitia
dirisha dogo yaani Enterprise Growth Market (EGM) na inaendeshwa kwa
kufuata taratibu zote za BOT na Soko la Hisa la Dar es S alaam.
Maendeleo Bank ilianza kutoa huduma za kibenki tarehe 9/9/2013 baada ya
kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania na tarehe 05/11/2013 ilisajiliwa
rasmi katika soko la hisa la Dar es Salaam baada ya kukidhi vigezo vyote
vilivyowekwa na mamlaka husika. Benki hii ilianza na mtaji wa shilingi
bilioni 4.5 kutoka kwa wanahisa zaidi ya 3,000 wa rika na itikadi
mbalimbali walionunua wakati wa mauzo ya awali (IPO) yaliyofanyika mwaka
2013.
Tarehe
9/11/2015 benki ilipata kibali cha kuuza hisa stahili ambapo matarajio
yake yalikuwa kupata shilingi bilioni 3.06 ambazo zitatumika kuimarisha
shughuli za uendeshaji wa benki pamoja na kuongeza matawi. Katika zoezi
la uuzaji wa hisa stahili benki imeweza kupata jumla ya shilingi bilioni
2.8 na kufikisha jumla ya mtaji wa benki kuwa shilingi bilioni 7.3.
Kusudi
kubwa la kuanzishwa kwa Maendeleo Bank PLC ni kufikisha huduma za
kibenki kwa wananchi wa kipato cha chini na cha kati kwani hao ndio
walio wengi na upatikanaji wa huduma za kibenki kwao ni changamoto
kubwa. Benki hii imepata mafanikio mengi tangia kuanzishwa kwake
takribani miaka miwili iliyopita ambapo mpaka tarehe 31/12/2015, benki
imefikisha wateja zaidi ya 12,000, amana zaidi ya shilingi bilioni 46.0,
mali za benki zimefikia zaidi ya shilingi bilioni 55, imetoa mikopo
zaidi ya shilini bilioni 21.0 na mwaka 2015 imepata faida ya takribani
shilingi milioni 200.0 baada ya kodi.
Benki
hii inatoa huduma mbalimbali za ubunifu ambazo zinawalenga wananchi wa
kada mbalimbali, zikiwemo: huduma za kibenki kwa njia ya simu, huduma za
BIMA, ATM kupitia mtandao wa UMOJA Switch, akaunti mbalimbali zenye
gharama rafiki, kutuma na kupokea pesa kutoka nje na ndani ya nchi, na
kutoa mikopo ya aina mbalimbali, ikiwemo kwa wajasiliamali wadogo ambayo
haina dhamana, yaani mikopo ya vikundi.
DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA MOYO, STEPHAN P. MASATU KUENDESHA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA MARADHI YA MOYO MKOANI KIGOMA
DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo, Dkt. Stephan P. Masatu
………………………………………………………………………
………………………………………………………………………
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WATU
wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo mkoani Kigoma, watapata faraja kubwa
mapema Aprili 4 hadi 9, 2016, kufuatia uwepo wa huduma za uchunguzi wa
maradhi hayo utakaofanywa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo, Dkt.
Stephan P. Masatu, kutoka jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam, Dkt. Masatu alisema,
huduma zote za magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na vipimo vya ECG na
ECHO zitatolewa kuanzia asubuhi kwenye hospitali ya kibinafsi ya Upendo
iliyo jirani na soko kuu la mkoani Kigoma.
Mkoa
wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi na
zinakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa kushughulikia magonjwa kama ya
Moyo na kutokana na uchache wa wataalamu hao, itakuwa ni nafasi nzuri
kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na vitongoji vyake, kujitokeza ili
kuhudumiwa ambapo kliniki hiyo itadumu kwa muda wa siku sita mfululizo.
Dkt. Masatu akitumia mashine ya kupima ECHO, mmoja wa wagonjwa wa moyo
WANAFUNZI WA FEZA BOYS HIGH SCHOOL WATEMBELEA VIRGINIA INTERNATIONAL UNIVERSITY
Wanafunzi
wa Feza Boys High School kutoka jijini Dar es Salaam wakipata picha ya
pamoja walipokua Virginia International University iliyopo jimbo la
Virginia siku ya Alhamisi March 24, 2016, wanafunzi hao wapo kwa ziara
maalum ya kuangalia uwezekano wa kujiunga na chuo hicho katika masomo ya
juu.
Makamu Rais wa Chuo hicho Dr.
Suleyman Bahceci (kulia) akiwaeleza wanafunzi hao taratibu za kufuata
kwa ajili ya kujiunga na VIU

Kushoto ni Alex Luketa Mtanzania
anayefanyakazi chuoni hapo kwa ajili ya kusajili wanafunzi kutoka Afrika
Mashariki akiwa pamoja na wanafunzi wa Feza Boys High School
wakimsikiliza Makamu Rais wa chuo (hayupo pichani) alipokua akielezea
wanafunzi hao utaratibu wa kujiunga na masomo VIU.
Wanafunzi wa Feza Boys wakipata mulo.
Mazungumuzo yakiendelea.
Picha ya pamoja










No comments :
Post a Comment