Thursday, March 31, 2016

MFUKO WA PENSHENI LAPF YAKABIDHI MSAADA WA MABATI 300 SHULE ZA WILAYA YA GEITA


6


Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akishuhudia mabati yaliyotolewa ma Mfuko wa Pensheni LAPF kwa ajili ya ujenzi wa madarasa wilayani Geita ikiwa jitihada za Mfuko wa LAPF kuunga mkono jitihada za Serikali kutoa elimu bure. Jumla ya mabati 300 yenye thamani ya Shs. 7,000,000/= yalikabidhiwa.
7 
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akikagua mabati yaliyokabidhiwa kama msaada na mfuko wa Pensheni wa LAPF wilayani Geita, kulia ni Meneja Masoko wa Mfuko wa LAPF Bw. James Mlowe wengine ni maofisa kutoka wilaya ya Geita.
9 
Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa neno la shukrani kwa Mfuko wa Pensheni LAPF kwa msaada wa mabati 300 yanayotosheleza kuezeka vyumba sita (6) vya madarasa yanayoweza kuchukua wanafunzi 45 kwa kila chumba na hivyo kupunguza tatizo la ukosefu wa mazingira bora ya kufundishia.
 
8 
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akiteta jambo na Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni LAPF pamoja na mbalimbali wa Wilaya ya Geita mara baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

PICHA NA MPIGA PICHA WETU

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA

mpanjuMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Ndugu Amon Mpanju wakati Naibu Mpanjo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo March 31, 2016.(Picha na OMR)

SERIKALI KUPITIA UPYA MIKATABA YA TRL

10Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akimsikiliza mmoja wa abiria anayetumia usafiri wa reli ya kati mkoani Kigoma. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Saveli Maketta.
11 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mkoani Kigoma.
12Muonekano wa mabehewa ya treni yakiwa mwisho wa reli ya kati, mkoani Kigoma.
13 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kapteni wa Meli ya MV Liemba ya namna inavyoendeshwa, mkoani Kigoma.
14 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akipata ufafanuzi wa namna ya injini za Meli ya MV Liemba zinavyofanya kazi wakati alipotembelea Meli hiyo mkoani Kigoma.
15 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mwenye kizibao cha njano), akimsikiliza Kapteni Winton Mwassa (wa kwanza kulia), kutoka Kampuni ya huduma za meli mkoani Kigoma mara baada ya kutembelea na kuona hali ya MV Liemba.
……………………………………………………………………
Serikali imeliagiza Shirika la Reli Tanzania (TRL), kupitia upya mikataba ya ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa ili kubaini kasoro zilizojitokeza na kuchukua hatua stahiki kabla ya maboresho ya reli ya Tanga-Moshi-Arusha.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma wakati akikagua miundombinu ya reli na kusissitiza nia ya serikali kufufua reli ya kanda ya kaskazini ili kuimarisha huduma ya uchukuzi katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
“Kama Serikali tumewekeza vya kutosha katika TRL, hivyo tunawataka mfanye biashara itakayolipa nasi tutahakikisha popote reli ilipo inatoa huduma iliyokusudiwa na kuchangia kukuza uchumi wa nchi”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TRL kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kupata bidhaa na abiria wengi wa kuwasafirisha nchini kote.
Amesema Serikali imedhamiria kuliongezea nguvu TRL ambapo baadhi ya mitambo kutoka Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) itakabidhiwa kwa shirika hilo hivyo kulitaka kuwa na mpango madhubuti wa kufanya biashara na kurudisha hadhi ya usafiri wa reli hapa nchini.
“Fanyeni bidii ili mpate mzigo wa kusafirisha kutoka Tanga kwenda Moshi na Arusha ili kufikia lengo la kubeba mzigo wa tani milioni moja kwa mwaka”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Amezungumzia umuhimu wa TRL kuafanya kazi kwa karibu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), ili kuongeza kasi ya huduma za uchukuzi nchini, kuongeza fursa za ajira na kukuza pato la shirika na taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Bw. Masanja Kadogosa amesema TRL imejipanga kutafuta masoko ndani na nje ya nchi ili kuboresha huduma za uchukuzi na kukuza pato lake.
Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua Meli ya MV Liemba na kuitaka Mamlaka ya Usimamizi wa usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kuhakikisha meli za MV Liemba na MV Mwongozo zinakaguliwa na kufanya kazi inavyostahili katika Ziwa la Tanganyika.
“Tumieni fursa ya kuwa karibu na nchi za maziwa makuu kufanya biashara ili meli zetu zipate mzigo wa kutosha na kuongeza mapato kwa taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa ambaye yupo katika ziara mkoani Kigoma amewataka viongozi na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya wizara yake kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuibua fursa za kiuchumi katika ukanda wa magharibi na hivyo kufufua miundombinu itakayochochea uchumi wa mikoa ya magharibi mwa Tanzania yenye fursa nyingi za kibiashara.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

TCRA waikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao ‘malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali’ (Digital Payment Services). 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao ‘malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali’ (Digital Payment Services). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fortunata Mdachi pamoja na Amos Shiyuka (kushoto) wakishuhudia.
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi inayokuja kuwekeza katika huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao ‘malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali’ (Digital Payment Services). Leseni hiyo imekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kwa kampuni ya Agano Safi huku akiikumbusha kufanya shughuli zake kwa kuzingatia vigezo na masharti ya leseni.
Akipokea leseni hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo alisema anaishukuru TCRA kwa kuwaamini na kuwakambidhi leseni ya kufanya biashara ya mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao, hivyo kampuni hiyo itahakikisha inafanya kazi kwa ufanisi na kushirikiana na vyombo husika ikiwemo BoT ili kuhakikisha jamii na taifa linanufaika na shughuli hizo.
Alisema kampuni hiyo inayoundwa na Wanamibia kwa ushirikiano na baadhi ya Watanzania imejipanga kuja na teknolojia ya kisasa katika mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na kampuni ya malipo ya MobiPay iliyojijengea heshima ya huduma zake katika nchi za Kusini mwa Afrika huku ikiwa na makao yake nchini Namibia.
Hafla hiyo ya makabidhiano imehudhuriwa pia na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria ambaye amepongeza Agano Safi kufanikiwa kufanya biashara hiyo nchini Tanzania jambo ambalo linaongeza ushirikiano baina ya nchi hizo huku zikibadilishana teknolojia kwa masuala mbalimbali na ubunifu kibiashara.
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fortunata Mdachi (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kukabidhi leseni ya biashara kwa Kampuni ya Agano Safi itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo kwa njia ya kidigitali’ (Digital Payment Services). 
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa pande zote mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu, Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria, Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu, Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria, Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa TCRA wakiwa katika hafla hiyo.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka (kulia).
Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Agano Safi (kulia) wakiwa na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika.               

No comments :

Post a Comment