Mbunge
wa Viti Maalum kutoka Tanzania Mhe. Aysharose Matembe akifuatilia kwa
makini ufunguzi wa Mkutano wa Wabunge Vijana kutoka Mabungu yote
Duniani unaofanyika sambamba na Mkutano wa134 wa Umoja wa Mabunge
Duniani ( 34th Inter- Parliamentary Union) unofanyika Lusaka Nchini
Zambia wiki hii.
Spika
wa Zambia Mhe. Patrick Matibini akifungua Mkutano wa Wabunge Vijana
kutoka Mabungu yote Duniani unaofanyika sambamba na Mkutano wa134 wa
Umoja wa Mabunge Duniani ( 34th Inter- Parliamentary Union) unofanyika
Lusaka Nchini Zambia wiki hii.
Picha na Owen Mwandumbya
Wabunge Vijana kutoka Nchi Mbalimbali wakifuatilia kwa makini ufunguzi
wa Mkutano wa Wabunge Vijana kutoka Mabungu yote Duniani unaofanyika
sambamba na Mkutano wa134 wa Umoja wa Mabunge Duniani ( 34th Inter-
Parliamentary Union) unofanyika Lusaka Nchini Zambia wiki hii.
Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa
CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania
(OUT), Prof. Elifas Bisanda (hayupo pichani) kufungua rasmi mafunzo ya
Tehama kwa walimu nchini.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
MAFUNZO kwa walimu watakaotumia
teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya
sayansi ikiwamo hesabu yamefunguliwa katika maabara za Chuo Kikuu Huria
jijini Dar es salaam.
Mafunzo hayo yanayohusisha walimu
kutoka Vyuo vya Monduli, Tabora na Morogoro yamelenga kuoanisha
ufundishaji na matumizi ya Tehama katika program ya Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya kuboresha elimu
Tanzania kupitia ufadhili wa taifa la China.
Programu hiyo inayotoa ushirikiano
mpya kati ya China na shirika hilo la Umoja wa Mataifa inafanyakazi
katika mataifa manane ya kusini mwa jangwa la sahara inatekelezwa kwa
lengo la kuwezesha mafanikio kwa malengo ya 2030.
Nchi zinaozhusika na mpango huo ni Tanzania Kongo ya Kinshasa (DRC), Congo, Liberia, Uganda, Côte d’Ivoire, Ethiopia na Namibia.
Mpango huo ambao kwa ujumla wake ,
awamu ya kwanza na ya pili unachukua miaka minne umelenga kuwezesha vyuo
vya walimu kutoa walimu wa kufunza wenzao kwenye stadi za kufundisha
kwa kutumia Tehama.
Mradi huo unaojulikana kama
UNESCO-China Funds-in-Trust (CFIT) wenye lengo la kuziba pengo la ubora
wa elimu wa kuwawezesha walimu kufundisha kwa kutumia Tehama
ulizinduliwa Novemba 22,2012 kwa nchi tatu za kwanza na baadae kuongezwa
nchi nyingine tano kufikia nane mwaka 2013.
Mpango huo ni wa dola za Marekani milioni 8 kutoka China mahususi kwa mataifa ya Afrika kuboresha elimu kupitia Unesco.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu
Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akifungua mafunzo ya wiki
mbili kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari
(Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yanayoendelea
katika maabara za Chuo Kikuu Huria (out) jijini Dar es salaam. Walioketi
kutoka kushoto ni Basiliana Caroli Mrimi kutoka Wizara ya Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa
CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo pamoja na Kiongozi wa kitaifa wa timu
ya mradi wa CFIT kit, Prof. Ralph Masenge.



No comments :
Post a Comment