Tuesday, March 1, 2016

LAPF KUKUTANISHA WADAU WAKE MKOANI ARUSHA MACHI 10 NA 11 MWAKA HUU

1
Meneja Masoko na Mawasiliano  wa LAPF, James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wao uliofanyika Milenium Tower jijini Dar es salaam wakati alipoelezea kuhusiana na mkutano wa mwaka wa wadau wa LAPF unaotarajiwa kufanyika  kwenye ukumbi wa AICC mwezi huu kwa sikU mbili  jijini Arusha. Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama Bw. Valerian Mablangeti.
2
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyotolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano  wa LAPF, James Mlowe wakati akizungumza nao katika ofisi za Shirika hilo zilizopo Mkumbusho jijini Dar es salaam.
3
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama Bw. Valerian Mablangeti akiwafafanulia jambo waandishi wa habari wakati wa mkutano huo kulia ni Bw. James Mlowe Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF.
………………………………………………………………………………..
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja  na bilioni 87 za thamani ya uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.
Hayo yalibainishwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF James Mlowe wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika Machi 10 na 11 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
Alisema LAPF imeendelea kupiga hatua kila mwaka ukilinganisha na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii hapa nchini.
” LAPF imeweza kutoa mikopo ya masomo kwa watu 800 katika maeneo mbalimbali nchini yenye thamani ya sh.bilioni 1.2 jambo ambalo tunajivunia” alisema Mlowe.
Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika  kwa wadau wa mfuko huo kupatiwa barua za mualiko.
Alisema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene na kuwa mawaziri wengine wakaoshiriki kwenye mkutano huo ni  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Jafo Selemani .
Alisema katika mkutano huo Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atatoa taarifa ya hesabu za mfuko huo na pia kutakuwa na mada inayohusu afya kutoka kwa Daktari wa  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

GAPCO YAWAPA NEEMA WALEMAVU KATIKA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON 2016


Mshindi wa mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathon 2016, Vosta Peter (30) akishangilia mara baada ya kumaliza. Mbio hizo za Kilometa 10 zilidhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mshindi wa kwanza kwa mbio za walemavu kilomita 10, Vosta Peter (30) akipokea cheki ya Shilingi Milioni Moja kutoka kwa kampuni ya GAPCO, wanaomkabidhi ni Meya wa Manispaa ya Moshi Raymond Mboya (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Gapco Afrika Mashariki, Macharia Irungu (anayepiga makofi toka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO Tanzania, Vijay Nair. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

OLDUVAI GORGE IS IN TANZANIA

old map
Tanzania Tourist Board (TTB) has been following up the ongoing discussions on social media following a video clip being posted on YouTube (https://www.youtube.com/watch?v=iveX49WE7fw) which has been circulating through various media channels showing a person claiming that Oldupai Gorge, a site in Tanzania that holds evidence of the earliest existence of mankind is in Kenya.
This video clip has triggered a lot of discussions on the different social media among Tanzanians and other people who have good wishes for Tanzania tourism who know very well that Oldupai Gorge is in Tanzania and NOT in Kenya.
As a public institution, responsible for marketing and promotion of Tanzania tourist attractions, Tanzania Tourist Board is also dismayed by this misleading information which intends to distort the good work the Board has been doing in promoting Tanzania tourist attractions including the Oldupai Gorge.
The Board would like to take this opportunity to strongly refute this statement delivered by the said person from a neighboring country while addressing one of the sessions of the International Young Leaders Assembly (IYLA) in USA, August 2015.
We would like to inform the world that as it is the case for Mt. Kilimanjaro, Serengeti National Park, Zanzibar to mention just a few, Olduvai Gorge which is referred to as the Cradle of Mankind, where Dr. Louis and Mary Leakey discovered important hominid remains of the nutcracker ‘Australopithecus bosel’, who lived nearly two million years ago, is also in Tanzania and not elsewhere in the world. It is located in the eastern Serengeti Plains in the Arusha Region and about 45 km, from Laetoli, another important archaeological site of early human occupation. The paleoanthropologist-archeologist team Mary and Louis Leakey established and developed the excavation and research programs at Olduvai Gorge which achieved great advances of human knowledge and world-renown status. Olduvai Gorge is one of the key tourist attractions for Tanzania.
We call upon Tanzanians and those with good wishes for Tanzania wherever they are to continue supporting the effort’s undertaken by TTB in marketing Tanzania and her all tourism attractions. We believe that it is the role of every single Tanzanian to promote Tanzania as Africa’s best destination and ask them to join and support Tanzania Tourist Board in its efforts to promote destination Tanzania.
We would like to applaud the reaction made by Tanzanians and non-Tanzanian within and out of Tanzania, who through this incident were able to stand up as ‘one voice’ and tell the world that OLDUPAI GORGE is INDEED IN TANZANIA!
Issued by:
Public Relations Office
TANZANIA TOURIST BOARD
March 01, 2016

WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA DAMU KWA HIYARI KUOKOA MAISHA

 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa vipimo na mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kulia) wakati wa zoezi la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari lilifanyika eneo la Karume jijini Dar es Salaam kwa siku mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa wiki.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa vipimo na mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kulia) wakati wa zoezi la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari lilifanyika eneo la Karume jijini Dar es Salaam kwa siku mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa wiki.
 Mfanyakazi wa Maabara ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kushoto) akimfanyia vipimo mmoja ya wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kwa hiyari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura
hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa
hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
  Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakifanyiwa vipimo katika zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa mkazi wa Dar es Salaam akipimwa presha kabla ya kushiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki. 
Mmoja wa mkazi wa Dar es Salaam akishiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.

Shida ya maji jiji la Dar es salaam kuwa historia

 Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Dawasa Mhandisi Romamus Mwang’ingo (Kushoto)  akitoa maelekezo kwa Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kulia) juu ya ufanyaji kazi wa mitambo ya Ruvu chini.
 Mafundi wakiwa katika harakati za kulaza bomba litakalotumika kuleta maji kwenye tanki kubwa lililopo kibamba toka Ruvu chini na juu kwa ajili ya uhifadhi na usambazaji maji katika Jiji la Dar es salaam. 
Mafundi wakikarabati bomba kuu la kusambaza maji toka Ruvu juu katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani.
 Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Katikati) akisikiliza maelezo juu ya ufanyaji wa kazi wa mitambo inayotumika kusambaza maji toka Ruvu juu kutoka kwa Meneja Mradi toka kampuni ya WABAG Mr. Pintu Dutta wakati wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam ilipotembelea mitambo hiyo. 
 Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kushoto) akisikiliza maelezo juu ya ramani inayoonesha usambazaji wa maji toka Ruvu Juu kwenda katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Dawasa Romamus Mwang’ingo.
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO AKABIDHI MICHANGO YA TWIGA STARS
wm1
Naibu Waziri wa  Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi  Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka  jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Fedha hizo zimewekwa  katika Benki ya NMB Bank House akaunti  namba “20110001677 inayojulikana kwa jina la Twiga Stars Special Fund”.
wm2
Naibu Waziri wa  Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimsikiliza Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund mara baada ya kumkabidhi shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka  jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Ijumaa ya wiki hii timu hiyo itacheza na   Zimbabwe  mashindano ya awali ya kufuzu kombe la Afrika kwa wanawake.
wm3
Naibu Waziri wa  Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimweleza jambo   Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund mara baada ya kumkabidhi shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka  jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Mhasibu Osmund alizipeleka fedha hizo  katika Benki ya NMB Bank House akaunti namba “20110001677 inayojulikana kwa jina la Twiga Stars Special Fund”.
Picha na Anna Nkinda

Serikali yalitaka Dira ya Mtanzania kukanusha tuhuma dhidi ya Balozi Ombeni Sefue

mwb1
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw.Assah Mwambene (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa za upotoshaji zilizotolewa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la tarehe 29/02/2016 kuhusu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo Habari, Bw.Jamal Zuberi na Mkurugenzi Msaidizi Habari Bw.Vicent Tiganya wote kutoka Idara ya Habari (MAELEZO).
mwb2
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw.Assah Mwambane (ambaye hayupo katika picha) iliyokuwa ikiutaka uongozi wa Gazeti ya Dira Mtanzania kukanusha habari waliyoitoa hivi karibuni iliyokuwa na kichwa cha habari “Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu”.
Na Anitha Jonas – MAELEZO
…………………………………………………………………………………………………………………
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw.Assah Mwambene ameutaka uongozi wa Gazeti la Dira ya Mtanzania kukanusha haraka na kuiomba radhi Serikali na   Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kutokana na taarifa waliyoitoa katika toleo namba 404  la tarehe 29/02/2016 lenye  kichwa cha habari “Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu.
Hayo  yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi huyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu taarifa kuwa hazikuwa na ukweli wowote kwani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue hakuhusika katika uteuzi wa Mkurugenzi wa MSD wala kuhusika na kampuni ya CRJE katika utoaji wa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma Oktoba 2007  kwani katika kipindi  hicho alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.
“Serikali inautaka uongozi wa Gazeti la Dira ya Mtanzania ukanunushe taarifa hiyo kwa uzito ule uliyotumika kuchapisha habari hiyo na kama wanapinga wakidai wana ushahidi basi waupeleke mara moja kwenye vyombo vinavyohusika  ikiwemo Sekretarieti ya Maadili na TAKUKURU”,alisema Bw.Mwambene.
Aidha,  Bw.Mwambene amesema gazeti hilo liliandika kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipigia chapuo Kampuni ya “UGG”  iliyowahi kuonyesha nia ya kujenga reli ya Kati nchini. Taaarifa hii pia siyo ya kweli na hakuna kampuni  yenye jina la “UGG” ilishawahi kuonyesha nia ya kujenga reli hiyo.
Mkurugenzi aliendelea kusema kuwa gazeti hilo lilimtuhumu pia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kuhusika na kumsafisha Bwana Eliakim Maswi wakati alichokifanya Balozi Sefue ilikuwa ni kusoma matokeo ya uchunguzi ambao hakuufanya yeye. Waliomsafisha ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Kamati ya Uchunguzi iliyoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu kwani ndio waliiyofanya uchunguzi huo.
Hata hivyo serikali imewashauri wamiliki wa vyombo vya habari,wachapishaji,wahariri, na waandishi wa habari wajikite kwenye weledi na ukweli pia wafanye  utafiti wa kina  na kuandika mambo waliyo na uhakika nayo

Wataalamu TPRI wapelekwa Kilombero kufanya uchunguzi

dk rutNa Jacquiline Mrisho
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro imewapeleka wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viuwatilifu ya Kitropiki (TPRI) wilayani Kilombero kufanya uchunguzi wa zao la mpunga linalosadikiwa kuharibiwa na dawa zilizomwagwa na Kampuni ya Kilombero Plantation (KPL) inayomiliki mashamba yanayopakana na mashamba ya wananchi.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mali Mkoa wa Morogoro Bw. Ernest Mkongo kuhusu uchunguzi unaoendelea kufanyika katika mashamba ya wananchi ili kutathmini athari zinazotokana na dawa hizo.

Serikali yawapa motisha wachezaji wa Twiga Stars

TWI1
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake “Twiga Stars” wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) alipowatembelea kambini kwao leo jijini Dar es Salaam.Twiga Stars inatarajiwa kucheza mechi na Timu ya Taifa wanawake ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa tarehe 4 katika uwanjja wa Taifa.
Picha na WHUSM
TWI2
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” alipowatembelea kambini kwa leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Nkenyenge na Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia).
TWI3
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Selestine Mwesiga akitoa shukura kwa Serikali kutokana na jitihada zake za kuitafutia wadhamini Timu ya Taifa ya Mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars) wakati Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura(wapili kutoka kushoto) alipo watembelea wachezaji wa Timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia). Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Nkenyenge.
TWI4
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akisalimiana na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” (Nasra Juma) alipowatembelea kambini kwao leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a.
TWI5
Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a. akisalimiana na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars”  Bibi. Nasra Juma  wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) kambini kwao leo jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKAMILISHA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI TANGA

m1
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliangalia vijana wa kikundi cha sanaa cha Tanga kwanza alipowasili Ofisi  ya CCM Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga.                
m2
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akizungumza nao katika Ofisi ya CCM Mkoa Tanga. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo March 01.2016.
m3
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na vijana wa kikundi cha wasanii cha Tanga kwanza alipokua akiondoka katika Ofisi ya Chama cha  Mapinduzi CCM Mkoa Tanga baada ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016.  (Picha na OMR)        
m4
 Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga Mwanakombo Mwakuru akimvisha Skafu Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili Ofisi  ya CCM Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016. Makamu wa Rais  amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga. Kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Mhe.Henri Shikifu.
m6
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Tanga katika Ofisi ya CCM Nkoa Tanga. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo March 01,2016.
m5
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akizungumza nao katika Ofisi ya CCM Mkoa Tanga. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo March 01.2016.

Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi kwa Rais Mstaafu Kikwete


hal 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha Kaka yake Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kilichotokea leo asubuhi nchini India.
Mzee Selemani Mrisho Kikwete alikuwa nchini India kwa matibabu.
Katika salamu zake Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshituko taarifa za kifo cha Mzee Selemani Mrisho Kikwete na amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete kuombeleza kifo cha mtu muhimu kwa familia hiyo.
“Napenda kukupa pole nyingi wewe Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, familia yenu yote, ndugu jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mtu muhimu katika familia, natambua uchungu mkubwa mlionao lakini nawaomba muwe  uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu” Alisema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amemuombea Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete apumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Arusha
01 Machi, 2016

KUZIONA TWIGA, ZIMBABWE ELFU 2000/=

Kiingilio cha chini cha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake ‘Taifa Stars’ dhidi ya timu ya taifa ya wanawake Zimbambwe kitakua shilingi elfu mbili tu.
Mchezo huo namba 3, unatarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa saa 10 kamili jioni katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, huku kiingilio cha juu kikiwa shilingi elfu tatu kwa jukwaa kuuu.
Waamuzi wa mchezo huo ni Lidya Tafesse, akisaidiwa na Yehuzewdubizua Yehuw, Tsige Sisay, Woinshetkassaye Abera kutoka nchini Ethiopia, huku Kamisaa wa mchezo huo Geneviev Kanjika akitoka Congo DR wote wanatarajiwa kuwasili siku ya Alhamisi mchana kwa shirika la ndege la Kenya (KQ).
Wakati huo huo kikosi cha Twiga Stars kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo wa siku ya Ijumaa, huku kocha mkuu wa timu hiyo Nasra Juma akisema vijana wake wote wapo katika hali nzuri na tayari kuwakabili Wazimbambwe.
Aidha Kocha Nasra amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini na watanzania wote kwa ujumla, kujitokeza uwanjani siku ya Ijumaa kuja kuwapa sapoti katika mchezo huo, ambapo watakua wakiwakilisha na kupeperusha bendera ya Tanzania.

JAFO AMUAGIZA MKURUGENZI WA KISARAWE KUMTAFUTIA KAZI NYINGINE MENJEJA WA MAMLAKA YA BODI YA MAJI

Jafo-30Jan2016
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE PWANI
 NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi na Utawala bora,  Seleman Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kumtafutia kazi nyingine meneja wa Mamlaka ya Bodi ya Maji Kisarawe Listern Materu kutokana na kushindwa kutatua kero ya maji kwa muda mrefu.

No comments :

Post a Comment