Tuesday, March 29, 2016

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu,yafanya ziara yatembelea mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa (JNIA)



 KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, imefanya ziara ya kutembelea mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal Three- TBIII), jijini Dar es Salaam, Machi 29, 2016 ambapo awali wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Profesa Norman Adamson Sigalla King, walipatiwa maelezo ya kina ya maendeleo ya mradi huo unaohusisha jengo la kisasa la abiria na sehemu ya kuegesha ndege kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na sehemu ya maegesho ya magari. Baada ya maelezo hayo ya kina yaliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, (TAA), Mhandisi George Sambali akisaidiana na baadhi ya wakurugenzi wengine wa Mamlaka hiyo, wajumbe hao walitembelea mradi huo na kujionea hatua mbalimbali za ujenzi ambapo kwa sasa ujenzi umefikia karibu asilimia 60. Pichani, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali, (kushoto), akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Norman Adamson Sigalla King, (kulia), na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA
 Mwenyekiti wa Kamati, akizungumza
 Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha, akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kabla ya kutembelea mradi
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo na maafisa wa TAA, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali (hayupo pichani)
 Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga, (kulia), akitoa maelezo ya maeneleo ya mradi huo. (kushoto) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA, Laurent Mwigune
 Mjumbe wa Kamati, Anna Richard Lupembe, akizungumza
 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, na Mbunge wa Fuoni, Zanzibar, Abbas Ali Hassan Mwinyi, (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TAA, Ramadhan Maleta, na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Laurent Mwigune (kushoto)
 Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga(kushoto), akimueleza Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Sigalla, sehemu ya maegesho ya ndege
 Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed
Millanga(kushoto), akimueleza Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Sigalla,
(kulia kwake) na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Sambali, (wakwanza kulia), sehemu ya maegesho ya ndege
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania, ATCL, Johnson Mfinanga akizungumzia hali ya shirika hilo
 Afisa Mkuu wa Masoko wa TAA, Scholastica Mukanjanga, akizungumza
 Mjumbe wa Kamati akizungumza
 Mjumbe wa Kamati akizungumza
 Mjumbe wa Kamati, Abass Ali Hassan Mwinyi, (katikati), akizungumza
Sehemu ya jengo la uwanja huo

KAMATI YA BUNGE YAIOMBA SERIKALI KUTOA VIBALI VYA UINGIZAJI SUKARI KUTOKA NJE YA NCHI

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu Serikali kutoa mapema vibali vya uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuziba upungufu ya bidhaa hiyo nchini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa.
 Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa akizungumza katika mkutano huo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (katikati), akiwa na wajumbe wa kamati hiyo.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Mwanahabari kutoka TBC, Angela Msangi (kulia), akiuliza suala katika mkutano huo.

ASKOFU CHARLES GADI NA WACHUNGAJI WENZAKE WALIOMBEA TAIFA LIPATE MVUA

 Askofu  wa Kanisa la God News for all Ministry, Dk. Charles Gadi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhu kabla ya kuliombea taifa lipate mvua akiwa na wachungaji mbalimbali. Kulia ni Mchungaji Palemo Masawe.
 Mchungaji Martini Ndaki (kushoto), akizungumza katika 
mkutano huo.
 Meza kuu kabla ya maombi. 
Askofu Charles Gadi (wa tatu kutoka kushoto), akiongoza maombi ya kuliombea taifa lipate mvua. Kutoka kushoto ni Mchungaji Denis Komba, Mchungaji Martin Ndaki, Mchungaji Palemo Masawe, Mchungaji Denis Kumbilo, Mchungaji James Manyama na Mchungaji Leonard Kajuna
 

Wizara ya Habari yateua Wajumbe wa Kamati ya Maudhui kwa kipindi cha miaka 3

Nape_Nnauye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye (MB), amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Kamati ya Maudhui kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia Machi 11, 2016.
  1. Joseph Method Mapunda (Mwandishi wa Habari/Mhariri Mtendaji mstaafu wa Magazeti ya Serikali (TSN);
  2. Abdul Ngalawa (Mwandishi wa Habari/Mkurugenzi mstaafu wa Redio Tanzania Dar Es Salaam (RTD);
  3. Derek Kaitira Murusuri (Mwandishi wa Habari/Mhadhiri); na
  4. Zainabu Mrisho Mwatawala (Mwandishi wa Habari na Mwanasheria).

RAIS DK.JOHN MAGUFULI ATOA HATI YA KIWANJA KWA BOHARI YA DAWA (MSD)


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto), akimkabidhi hati ya kiwanja chenye ukubwa wa ekari tano Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu kilichotolewa na Rais Dk. John Magufuli kwa MSD kupitia Wizara hiyo Dar es Salaam leo mchana.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (kulia), akisalimiana Naibu Katibu Mkuu wa  Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Moses Kusiluka wakati wa hafla hiyo ya kukadhiana hati hiyo ya kiwanja. Katikati ni Waziri wa Wizara hiyo, William Lukuvi.
 Salamu zikiendelea. Hapa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango Miji, Profesa John Modestus.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (mbele kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Waziri Lukuvi na Mkurugenzi wa MSD, wakiangalia hati hiyo.
Viongozi wa wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Usanifu Majengo, Amina Ramadhani, Ofisa Ardhi Mkuu, Mwamasage na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya.
 
Na Dotto Mwaibale
 
RAIS Dk. John Magufuli kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  ametoa kiwanja chenye ukubwa wa ekari 5 kwa Bohari ya Dawa (MSD) kilichopo Luguluni nje kidogo ya jiji la  Dar es Salaam, kwa ajili ya ujenzi wa Bohari ya Dawa ili kuondoa upotevu wa fedha kwa maghala ya kukodi.
 
Ujenzi wa maghala katika kiwanja hicho utaokoa kiasi cha sh. bilioni 4 zilizokuwa zikitumika kila mwaka kwa ajili ya malipo ya maghala ya kukodi yaliyopo Mabibo Ubungo jijini pamoja na kanda mbalimbali  nchini.
 
Akizungumza wakati wa akikabidhi hati hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu Dar es Salaam leo mchana,  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema, Rais ametoa ardhi hiyo ili kuepusha gharama zisizo na sababu kwa MSD.
 

Rais Magufuli aingia Chato kwa mara ya kwanza ataka watanzania washikamane kujitegemea badala ya kutegemea misaada

kal1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Ezikiel Elias Kyunga mara baada ya kuwasili katika viwanja wa Chato Mkoani Geita. Rais aliwasili Wilayani Chato kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
kal2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu  Ezikiel Elias Kyunga kulia ,Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Msukuma kushoto na Naibu waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni mbunge wa Chato Dkt. Medard Kalemani watatu kutoka kulia wakielekea kwenye uwanja wa Mkutano wa mazaina kwa ajili ya kuwasalimia mamia ya wakazi wa Chato Mkoani Geita.
kal3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na kikundi cha ngoma za asili cha Chato mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mkutano Chato Mkoani Geita.
kal4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Chato mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
kal5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru wakazi wa Chato waliofika kumpokea kwenye Uwanja wa Michezo wa Mazaina Wilayani Chato.
kal6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu wa wageni mara baada ya kuwasili Wilayani Chato.
kal7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Chato mara baada ya kuwasili.
kal8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika hotuba yake.
kal9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Chato mara baada ya kumaliza kuwahutubia katika mkutano wa hadhara.
kal10
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
kal11
Wakazi wa Chato wakifurahia Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Michezo wa Mazaina Wilayani Chato. PICHA NA IKULU
……………………………………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefika nyumbani kwake katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais, ambapo akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato, ametoa wito kwa kila mtanzania kuchapa kazi kwa juhudi ili nchi iondokane na utegemezi wa misaada ya wafadhili ambayo huambatana na masharti.
Dkt. Magufuli amesema jukumu kubwa lililo mbele ya watanzania kwa sasa, ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA BOHARI YA DAWA MSD JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo na Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Banakunu (kulia), wakitembea wakati kamati hiyo ilipotembelea MSD Makao Makuu Keko Dar es Salaam leo asubuhi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Mary Lingo (wa pili kulia), akiwaelekeza wajumbe wa kamati hiyo jinsi dawa zinavyotunzwa katika maghala.
 Mkurugenzi wa MSD, Laurean Banakunu (katikati mbele), akiwaongoza wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea MSD leo.
Mjumbe wa kamati hiyo, Azani Zungu akiuliza swali juu ya kuharibika kwa dawa.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
 
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Jamii imetembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa Keko na kuipongeza kwa utendaji wake kazi pamoja na mazingira magumu yanayoikabili.
 
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba amesema Kamati yake itasimamiana kuyafanyia kazi masuala makubwa manne ambayo ni pamoja na bajeti finyu ya dawa, ulipwaji wa deni la serikali, mfumo wa uwajibikaji kati ya Tamisemi na Wizara ya Afya ambao unasababisha utekelezaji na usimamizi wa masuala ya Afya kutokuwa na mtiririko kutoka juu kwenda chini. 
 
Jambo la nne ni kuhakikisha utekelezaji wa kuongeza uzalishaji dawa ndani ya nchi kupitia sekta binafsi (PPP).
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kingwangala alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha Bohari ya Dawa inanunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji kwa bei nafuu, hivyo Serikali imeweka kipaumbele kuhakikisha deni la MSD linalipwa mapema iwezekanavyo.
 
Alisema tayari Wizara ya Afya imeiagiza MSD kuandaa bei elekezi kwa maduka maalum ya dawa (prime vendor) ili vituo vinavyokosa dawa MSD vinunue huko bila usumbufu na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa dawa na vifaa tiba.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu ameviomba vituo vya Afya kuleta mahitaji yao kwa wakati.

Waziri Mbarawa azitaka taasisi na idara kutumia kituo cha kuifadhi taarifa cha Taifa

Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akielezea namna Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kinavyofanya kazi kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akifafanua jambo kwa kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipozungumzia wadau hao kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kuhifadhia taarifa zao.
Mkuu wa Idara ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Adin Mgendi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo juu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kinavyofanya kazi kwa usalama mkubwa wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipozungumza na wadau hao juu ya matumizi ya kituo hicho kuhifadhia taarifa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya kukitumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ ili kuhifadhia taarifa zao.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya matumizi ya ‘National Information Data Centre’
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya kukitumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ ili kuhifadhia taarifa zao. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura pamoja na Ofisa Mkuu Idara ya Ufundi TTCL, Senzige Kisonge wakifuatilia mazungumzo hayo. 
Mkuu wa Idara ya Compyuta NSSF, Yahaya Madenge (kulia) akiuliza swali kupata ufafanuzi juu ya usalama wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi akiuliza kupata ufafanuzi juu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kinavyofanya kazi na kumlinda mteja wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye tai ya mistari miekundu) akizunguka na baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali vitengo vya IT kuwaonesha miundombinu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ ilivyojengwa kisasa kumlinda mteja wake na taarifa zinazohifadhiwa katika kituo hicho.
Baadhi ya mashine kubwa za kisasa za kufua umeme katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Baadhi ya mitungi ya gesi ya kuzimia moto endapo ukitokea inayofanya kazi kwa kujiongoza yenyewe mara tukio la moto linapojitokeza katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akimuonesha Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi moja ya vyumba maalumu vya usalama katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (katikati) akimuonesha Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi (kulia) moja ya mitambo ya kisasa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Baadhi ya mitambo ya kuhifadhia taarifa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Baadhi ya mitambo ya kuhifadhia taarifa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Baadhi ya mashine zinazofanya kazi ya kupooza mitambo katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (wa tatu kushoto) akifafanua jambo kwa kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipozungumzia wadau hao kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kuhifadhia taarifa zao.

Vivuko vya MV Magogoni na MV Kigamboni viko katika hali nzuri

mv1
Tunapenda kuutarifu umma kuwa Vivuko vya MV Magogoni na MV Kigamboni viko katika hali nzuri na vinaendelea na kazi yake ya kuhudumia wananchi kama kawaida.
Kumekuwa na malalamiko kuwa Vivuko vya MV Kigamboni na MV Magogoni havifanyi kazi kwa muda sasa hivyo kusababisha usumbufu kwa wananchiwanaotu
mia huduma hiyo.
Tunapenda kuutarifu umma kuwa taarifa hizo sio za kweli na kwamba Vivuko vyote viwili yani MV Magogoni na MV Kigamboni vinaendelea na kazi zake za kutoa huduma kwa wanachi kama kawaida na kusisitiza kuwa katika kipindi cha usiku kutokana na kutokuwepo kwa wananchi kwa muda huo vivuko hivyo hupumzika.
MV. Magogoni ina uwezo wa kubeba tani 500, ambayo ni sawa na kubeba abiria 2000 na magari madogo 60 kwa wakati mmoja. Kivuko hiki kiko katika hali nzuri, kinafanya kazi saa 20 kwa siku, na kupumzika kuanzia saa 6:00 usiku mpaka saa 10:00 alfajiri kila siku ili kufanyiwa matengenezo ya kinga (service).
Vile vile MV. Kigamboni inauwezo wa kubeba tani 160, ambayo ni sawa na kubeba abiria 800 na magari madogo 21 Kwa wakati mmoja. Kivuko hiki kinafanya kazi kwa saa 22 kwa siku, na kupumzika kuazia saa 4:00 usiku mpaka saa 6:00 usiku kila siku ili kufanyiwa matengenezo ya kinga (service).
Aidha TEMESA inatoa rai kwa watu wote wanaotumia mazingira ya vivuko vya MV Magogoni na Kigamboni kuyatunza mazingira ya vivuko hivyo katika kuvipa maisha marefu, ili kuepusha adha ya usafiri wa vivuko na inawashauri watumiaji wa Vivuko vya MV Magogoni na Kigamboni kufuata taratibu zote za kivuko kama inavyoelekezwa ili kutoathiri utoaji wa huduma hiyo.
Vivuko vya Mv Magogoni na Kigamboni vinasimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya usafiri kutoka katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano

KUFUTWA USAJILI KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (110) KWA KUJIENDESHA KINYUME CHA SHERIA KUANZIA TAREHE 30/03/2016

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali amefuta usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiesrikali (NGOs) 109 kwa kuendesha shughuli zao kinyume cha Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005. Mashirika hayo ni yale ambayo hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa kipindi cha miaka miwili pasipo kutoa sababu za msingi, kutolipa ada ya mwaka au kuendesha shughuli za NGOs bila kusajiliwa chini ya Sheria ya NGOs.
Kwa taarifa hii, Mashirika yaliyotajawa hapa chini yamefutiwa usajili na yataarifiwa kusitisha shughuli zao kuanzia tarehe ya tangazo hili (30/03/2016). Baada ya kipindi hicho, Msajili wa NGOs atayachukulia hatua stahiki Mashirika ambayo yatakaidi amri hii na kuendelea na shughuli za NGOs kinyume na Sheria husika.
MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (109) YALIYOFUTIWA USAJILI KUANZIA TAREHE 30/3/2016  NI KAMA IFUATAVYO:
  1.             THE MEDICAL WOMEN ASSOCIATION OF TANZANIA (MEWATA)
2.             AFRICAN GENDER AND GOOD GOVERNANCE ALLIANCE
3.             AFRICAN WILDLIFE FOUNDATION
4.             AGENDA FOR ENVIRONMENTAL AND SUSTAINABLE DEVELOPMENT
5.             ANTIOKIA MISSION INTERGRATED SOCIAL DEVELOPMENT
6.             BUSEGWE DEVELOPMENT ASSOCIATION
7.             BUTIAMA DEVELOPMENT ASSOCIATION
8.             CARE FOR THE CHILD (CFC)
9.             CHAKUFAA DEVELOPMENT FOUNDATION
10.          CHAMA CHA KUSAIDIA WATOTO YATIMA MAKAMBAKO
11.          COMFORT WOMEN RELIEF FOUNDATION
12.          COMMUNITY AGRICULTURAL ACTION SERVICES CENTRE
13.          COMMUNITY SERVICES SUPPORT OF TANZANIA (COSESU-T)
14.          DAUGHTERS OF ZION FOUNDATION LTD
15.          DEFENCE OF HUMAN RIGHTS CITIZEN RIGHTS
16.          DEVELOPERS OF SUSTAINABLE COMMUNITY BASED ACTIVITIES (DESCOBA)
17.          DIANA WOMEN EMPOWERMENT ORGANIZATION
18.          EDNA DEVELOPMENT FOUNDATION
19.          EMPOWERMENT AGAINST POVERTY AND HIV/AIDS
20.          EMPOWERMENT FOR THE DISADVANTAGED COMMUNITY (EDC)
21.          ENVIRONMENTAL MANAGEMENT AND NUTRITIONAL SERVICES AGENCY (EMA-NUSA)
22.          GLOBAL VISION TANZANIA (GVT)
23.          GRASSROOTS INITIATIVE FOR YOUTH AND ELDERLY DEVELOPMENT ORGANIZATION (GIYEDO)
24.          HOPE MISSION OF DEVELOPMENT FOR THE DISABLED (HOMIDED)
25.          HURUMA CHILD MINISTRY CENTRE
26.          HURUMA REHABILITATION PROGRAMME
27.          IMANI WOMEN ECONOMIC EMPOWERMENT ASSOCIATION (IWEA)
28.          INTERNATIONAL MEDICAL CORPS
29.          IZAAZ MEDICAL PROJECT
30.          JUMUIYA EDUCATION BAGAMOYO (JEBA)
31.          JUNIOR ACHIEVEMENT OF TANZANIA
32.          KAMACHUMU IN NGEMU AGENDA (KINGA)
33.          KILIMO HAI TANZANIA (KIHATA)
34.          KUZA EDUCATION DEVELOPMENT
35.          MANDATE AFRICA FOUNDATION
36.          MASASI FARMERS ADVOCACY ASSOCIATION (MAFADA)
37.          MAZINGIRA INSTITUTE OF TANZANIA (MAI-TANZANIA)
38.          SUMBAWANGA ESCARPMENT ENVIRONMENTAL CONSERVATION ORGANIZATION (SEECO)
39.          MFUKO WA MAENDELEO YA WAISLAM MKOA WA RUVUMA
40.          MKONGO MLOKA DEVELOPMENT ASSOCIATION
41.          MOROGORO ENVIRONMENTAL CONSERVATION ACTION GROUP
42.          MOROGORO ENVIRONMENTAL CONSERVATION ACTION GROUP
43.          MUUNGANO DEVELOPMENT ASSOCIATION (MUDEA)
44.          MWAKALELI COMMUNITYDEVELOPMENT ORGANIZATION (MWACODO)
45.          MWALIMU NYERERE UWC FOR SELF RELIANCE
46.    MWANANYAMALA WOMEN LDEVELOPMENT GROUP (MWAWODE)
47.          NATIONAL LIFE DEVELOPMENT ASSOCIATION
48.          NJOMBE DEVELOPMENT ORGANIZATION (NDO)
49.          NORWEGIAN PEOPLE AID
50.          OLOF PALME ORPHANS CENTRE
51.          DEVELOPMENT AGENCY PROBATION TIME RESEARCH
52.          PANGOLIN ELITE SPORTS FOUNDATION
53.          PARTGAGE TANZANIA
54.          PERIPHERY AREAS DEVELOPMENT ASSOCIATION (PADA)
55.          POVERTY ALLEVIATION AND AGRICULTURAL DEVELOPMENT (PADEFO)
56.          POVERTY FIGHTERS AND CHARITABLE GROUP
57.          POVERTY FIGHTERS AND DEVELOPMENT SOCIETY OF TANZANIA (POFIDESO)
58.          PRICESS AGNES FOUNDATION
59.          PROGRESS ASSOCIATION TANZANIA (PATA)
60.          PROMOTION OF FARMING AND ORPHANS EDUCATION IN TANZANIA (PROFOET)
61.          RESTE YOUTH TRAINING TRUST FUND
62.          RIDHIKA SHIRIKA LA ULINZI NA MAZINGIRA
63.          RURAL ACCESS TECHNOLOGY INORMATION AND INSTITUTIONAL SERVICES (RATHS)
64.          RURAL FAMILY LIFE PLANNING ASSOCIATION
65.          RURAL INITIATIVES FOR DEVELOPMENT OF TANZANIA – RIDE(T)
66.          RURAL ORIENTED SUSTAINABLE DEVELOPMENT ORGANIZATION (ROSDO)
67.          RURAL WOMEN DEVELOPMENT ASSOCIATION
68.          SAMORSES EDUCATION FOUNDATION
69.          SANTA MERINA EDUCATION FOUNDATION
70.          SAVE LIFE ASSOCIATION
71.          SHINYANGA FOUNDATION FUND (SFF)
72.          SOCIETY FOR RURAL DEVELOPMENT INITIATIVES (SRDF)
73.          SOLIDARITY WOMEN GROUP (SWG)
74.          SOLUTION AND OPPORTUNITIES FOR DISADVANTAGED IN AFRICA (SODA)
75.          SOUTH DEVELOPMENT IN TANZANIA (YODIT)
76.          SUSTAINABLE INTERGRATED FARMING AND HEALTH IMPROVEMENT
77.          TAMADA
78.          TANZANIA ACTION FOR PASTORAL EDUCATION ADVOCACY (TACEA)
79.          TANZANIA ASSOCIATION OF ENVIRONMENTAL ENGINEERS (TAEES)
80.          TANZANIA DEVELOPMENT AND AIDS PREVENTION (TADEPA)
81.          TANZANIA GIRL’S EMPOWERMENT (TAGE)
82.          TANZANIA HURUMA AIDS ORGANIZATION (THAO)
83.          TANZANIA INITIATIVES FOR POVERTY ALLEVIATION (TIPA)
84.          TANZANIA JOURNALIST ASSOCIATION (TAJA)
85.          TANZANIA MANGROVE PROTECTION ASSOCIATION (TAMPA)
86.          TANZANIA MARGINALIZED AREAS COMMUNITY SERVICES FOUNDATION
87.          TANZANIA ROAD ASSOCIATION (TRA)
88.          TANZANIA SOCIETY FOR THE BLIND (TASODEB)
89.          TANZANIA SUPPORT AND TRAINING YOUTH AND WIDOWS ASSOCIATION
90.          TANZANIA TENANTS ASSOCIATION
91.          TANZANIA YOUTH MUSLIM ASSOCIATION (TAYMA)
92.          TARIME – SIRARI GROUP (TARSI)
93.          TAX SERVICES TANZANIA
94.          TECHNOWLEDGE TANZANIA (TKTZ)
95.          TELECOMS AND ELECTRONICS TECHNICIANS ASSOCIATION (TETA)
96.          TEMEKE DISTRICT YOUTH FOUNDATION (TEYOFO)
97.          THE HUMAN DEVELOPMENT PROJECTS AND TANZANIA
98.          NAMTUMBO NETWORK OF CIVIL SOCIETY (NANECISO)
99.          THE SURVIVAL AFRICA TRUST (SAT)
100.      THE TANZANIA HERALDS YOUTH SERVICES (THEYS)
101.      THE VOICE OF THE AIDS AND ORPHANS (VOTAO)
102.      THE WOMEN WIDOW CHILDREN AND FISHERIES DEVELOPMENT
103.      TUMAINI ORPHANS AND VULNERABLE CHILDREN CENTRE
104.      UMOJA WA DOUYA NA MAKANGAWE (UDOMA)
105.      UMOJA WA MADEREVA WA MABASI TANZANIA (UWAMATA)
106.      WATOTO CARE ORGANIZATION (WACO)
107.      WOMEN AND YOUTH ECONOMIC DEVELOPMENT INITIATIVE (WOYEDE)
108.      WOMEN DEVELOPNMENT AND GENDER
109.      SAIDIA JAMII YA WAZEE KAGERA SAJAWAKA)
110.      UKIMWI ORPHANS ASSISTANCE (UKOA)
 
Imetolewa na, M.S. Katemba
MSAJILI WA NGOs
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
29 Machi, 2016

RAIS MAGUFULI APATA CHAKULA CHA MCHANA MGAHAWANI UWANJA WA NDEGE WA MWANZA AKIWA NJIANI KUELEKEA CHATO

MWZ1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakijipatia chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi. Pamoja nao mezani hapo ni Meya wa Ilemela Mstahiki Renatus Mulunga, Meya wa jiji la Mwanza Mstahiki James Bwire, Mkuu wa Mkoa wa MWanza  Mhe John Mongella na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Ndg Anthony Diallo.PICHA NA IKULU
MWZ2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakijipatia chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi. Pamoja nao mezani hapo ni Meya wa Ilemela Mstahiki Renatus Mulunga, Meya wa jiji la Mwanza Mstahiki James Bwire, Mkuu wa Mkoa wa MWanza  Mhe John Mongella na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Ndg Anthony Diallo.
MWZ3 MWZ4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakiondoka baada ya kupata  chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi. 

RAIS MAGUFULI AWASILI MWANZA, AAMURU BARABARA UWANJA WA KAYENZE IFUNGULIWE MARA MOJA

1
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege mara baada kwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati alipopitaka mkoani humo akielekea Nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko, hii ni mara ya kwanza kwenda kupumzika kijijini kwake toka alipchaguliwa na kauapishwa kushika madaraka ya kuongoza Jamhuri ya Muungano ya Tanzania mwezi Oktoba mwaka jana.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela amemshukuru Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kuamuru kufunguliwa kwa barabara inayopita kandokando ya uwanja wa ndege kuelekea Kayenze iliyokuwa imefungwa kwa miezi miwili na kuleta adha kubwa kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo.
Mara baada ya Rais Magufuli kuamuru barabara hiyo ifunguliwe mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza  Uongozi mzima wa mkoa huo waliongozana kwenda Kayenze na kuwatangazia wananchi kwamba wako huru kutumia barabara hiyo kwakuwa Mh. Rais ameamuru ifunguliwa na sisi tumekuja kutekeleza agizo la rais na sasa barabara hii imefunguliwa. 
(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-MWANZA)
2
Mke wa Rais Mama Janet Magufuli akishuka kwenye ndege wakati Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli alipowasili uwanjani hapo akielekea Chato Mkoani Geita kwa mapumziko.
3
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mwanza leo.
4
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza leo.
5
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza.
6
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa kamati ya Amani mkoani Mwanza wakati alipowasili uwanjani hapo akielekea Chato.
7
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mh.Altaf  Mansour  mlezi wa shirikisho la Vyuo vikuu CCM  Kanda ya Ziwa, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela.
9
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mh.Altaf  Mansour  mlezi wa shirikisho la Vyuo vikuu CCM  Kanda ya Ziwa, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela.
10
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana wana  CCM  waliofika uwanjani hapo kumpokea, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela.
11
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipigiwa saluti na mmoja wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na  usalama mkoani Mwanza waliofika uwanjani hapo kumpokea.
12
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana afisa habari wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw. Atley Kuni .
13
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akielekea kukagua vikundi vya ngoma na kwaya.
14
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na Mkewe mama Janet Magufuli wakiangalia vikundi vya ngoma wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza leo wakielekea Chato kwa mapumziko.
15
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  na Mkewe Mama Janet Magufuli wakiwapungia wachenza goma wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza.
16
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na askari wa kikozi cha Zimamoto uwanjani hapo.
17
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiangalia kwaya ya AIC Makongoro ambayo iliimba wimbo wa kuhamasisha kuitunza amani ya nchi na kumhamasisha kiasi cha kumfanya kujumuika nao na kuimba pamoja na wanakwaya hao.
18
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiimba pamoja na wanakwaya wa AIC Makongoro ya jijini Mwanza wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza.
19
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiimba pamoja na wanakwaya wa AIC Makongoro ya jijini Mwanza wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza.
20
Wadau Issa Michuzi kulia na Pius Lugonzibwa kushoto walikuwepo katika mapokezi hayo.
21
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akwapungia mkono wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Mwanza.
22
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa mwanza katikati ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela  na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga.
23
25
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela akimshukuru Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kuamuru kufunguliwa kwa barabara inayopitka kandokando ya uwanja wa ndege kuelekea Kayenze.
26
Mh.Altaf  Mansour  mlezi wa shirikisho la Vyuo vikuu CCM  Kanda ya Ziwa alikuwepo katika mapokezi hayo , Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga.
27
Baadhi ya wanahabari waliokuwepo uwanjani hapo wakifurahia kwa kugonganisha chupa za soda kinywaji ambacho Mh. Rais Dk John Pombe Magufuli alitoa ofa kwa wananchi wote waliokuwepo uwanjani hapo, kulia ni Shila Kutoka ITV Mwanza na kushoto ni Atley Kuti afisa habari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
28
Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli akiondoka kwenye kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza mara baada kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa Victoria Catering.
29
Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na kwaya ya AIC Makongoro na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza kabla ya kuelekea Chato mkoani Geita.

TANZANIA NA KUWAIT ZASAINI MAKUBALIANO YA SAFARI ZA ANGA

1Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya safari za Anga kati ya Tanzania na Kuwait. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan.
2Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya safari za Anga kati ya Tanzania na Kuwait. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
3Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan mara baada ya kusainiwa kwa hati ya makubaliano ya safari za Anga kati ya Tanzania na Kuwait leo jijini Dar es salaam.
4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait (Kushoto katikati).Wengine katika picha hiyo ni Maafisa kutoka Tanzania na Kuwait. 
Picha na Eleuteri Mangi –MAELEZO.

Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
index 
TAARIFA KWA UMMA
Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (9) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali katika Mkutano wa Pili wa Bunge uliomalizika Februari 2016.
Mikutano hiyo ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Sheria Ndogo inatarajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 4 Aprili, 2016 na Jumanne tarehe 5 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Sheria Ndogo ambazo Kamati inakaribisha wadau na umma kwa ujumla kutoa maoni yao ni pamoja na zifuatazo:-
  1. The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations, 2015
  1. The Public Private Partnership Regulations, 2015
  1. The Copyright and Neighboring Rights (Copyrighted Works – Communication to the Public) Regulations, 2015
  1. The National Examinations Regulations, 2015
  1. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ General Welfare, Conduct and Disciplinary Matters) Regulations, 2015
  1. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ Performance Assessment) Regulations, 2015
  1. The Fire and Rescue Force (Fire Precautions in Buildings) Regulations, 2015
Sheria Ndogo zilizotajwa hapo juu pamoja na nyingine ambazo zinashughulikiwa na Kamati, zinapatikana kwa kupakua (downloadable) katika tovuti ya Bunge la Tanzania ya www.parliament.go.tz pamoja na tovuti ya Serikali ya www.tanzania.go.tz
Aidha, maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya posta au barua pepe kwa anuani ifuatayo:-
Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge,
  1. L. P. 9133, DAR ES SALAAM
Barua pepe: cna@bunge.go.tz
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
29 Machi, 2016.

SUMATRA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI, KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WAFANIKIWA KUKAMATA MABASI 105

3Meneja Mawasiliano wa  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) bw. David Mziray  akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu kukamatwa kwa mabasi yaliyobainika kukiuka masharti ya Leseni  nyakati za asubuhi na jioni katika jiji la Dar es salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO bw. Frank Mvungi.
4Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano  wa  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga kuhamasisha wadau wa Sekta hiyo kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta hiyo.
 (Picha na Maelezo)
……………………………………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,Kikosi cha Usalama Barabarani wamefanya ukaguzi katika Jiji la Dar es salaam,ambapo wamefanikiwa kukamata mabasi  105 na kati hayo 36 yamefikishwa mahakamani  baada ya  kukiuka wa masharti ya leseni ya usafirishaji abiria.
Hayo yamwebainishwa leo  na Meneja Mawasiliano wa SUMATRA Bw. David Mziray wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo katika kutatua kero zinazowakabili abiria nyakati za asubuhi na Jioni.
Akifafanua Mziray amesema kati ya Machi 21-24 , 2016  ilifanya ukaguzi huo  na ili sheria iweze kuchukua mkondo wake Kwa wale wanaokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.
“Katika kuimarisha huduma za usafiri Mamlaka  imeweka utaratibu maalum wa kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo katikati ya jiji,Ubungo,Buguruni na Kariakoo ili kubaini wale wote wanaovunja sheria”.alisisistiza Mziray.
Akizungumzia baadhi ya makosa yalibainika kutendwa na mabasi hayo Mziray alisema kuwa ni pamoja na kuongeza nauli,kukata njia,kutoa huduma bila leseni ya usafirishaji,kutoa huduma katika njia ambazo hawakupangiwa.
Wamiliki na wafanyakazi katika sekta ya usafirishaji kote nchini  hasa wa mabasi ya daladala wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji wanapotoa huduma hiyo kwa umma.
Mziray  aliongeza kwamba  wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale wanapobaini  basi walilopanda linakiuka masharti ya leseni ikiwemo kuongeza nauli,kukata njia,kutoa huduma bila leseni ya usafirishaji na kutoa huduma katika njia ambazo hawakupangiwa ambapo wananchi wanaweza kutoa taarifa kupitia namba za simu za bure ambazo ni 0800110019 na 0800110020.

TANESCO MKOANI PWANI YAWANASA WEZI SABA KWA TUHUMA ZAKUIBA UMEME KINYEMELA

1Afisa Usalama wa shirika la ugavi wa umeme Tanesco Mkoa wa Pwani Henry Byarugaba akionyesha moja ya eneo ambalo wameiba umeme  kwa kujiunganishia bila ya kuzingatia taratibu.
2Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika hilo wakiwa katika eneo hilo mara baada ya kubaini kuwepo kwa wizi huo wa umeme.
(PICHA NA VICTOR MASANGU)
………………………………………………………………………………………..

Serikali ya Tanzania kujenga bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Uganda

1Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akiongea na baadhi waandishi wa habari  mara baada mkutano ya wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini leo jijini Dar es salaam.
2Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Sekta ya Mafuta nchini Dkt. Gideon Kaunda akiongea na baadhi waandishi wa habari  mara baada mkutano ya wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini leo jijini Dar es salaam.
Picha na Ally Daud- Maelezo
……………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Imeelezwa kuwa Tanzania ina vigezo mbalimbali ambavyo vinaifanya nchi ijiamini kwa asilimia 98 kuwa mradi wa bomba la kusafirishia mafuta kutoka Ziwa Albert nchini Uganda utapitia  Kaskazini mwa Tanzania hadi Bandari ya Tanga badala ya nchini Kenya.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa wakati wa kikao chake na wafanyabiashara wa mafuta nchini ambacho kililenga kujadiliana nao kuhusu fursa za uwekezaji zitakazotokana na mradi huo endapo utapita nchini.
Profesa Ntalikwa alivitaja vigezo hivyo kuwa ni uzoefu wa Tanzania katika ujenzi wa mabomba ya kusafirisha nishati mbalimbali ikiwemo Bomba la Mafuta la kutoka Tanzania hadi Zambia (TAZAMA), Bomba la kusafirisha gesi kutoka  SongoSongo hadi Dar es Salaam, Bomba la kusafirisha gesi kutoka eneo la Mnazi Bay hadi Mtwara, pamoja na Bomba kuu la gesi kutoka mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam lenye kipenyo cha inchi 36 hivyo uzoefu huo utasaidia katika kupunguza muda wa ujenzi wa bomba la mafuta ambalo kipenyo chake ni inchi 24.
“Tumewaeleza wenzetu kuwa Serikali ya Tanzania pia ilishajenga uwezo mkubwa katika masuala ya kutwaa, kumiliki na kulipa madai ya wananchi wanaopisha miradi ya mabomba na shughuli hizi zimekuwa zikifanywa kwa wepesi na umakini mkubwa ikiwemo umakini katika kufuata kanuni na sheria za mazingira, hivyo haitatuwia ngumu katika kutekeleza mradi huu,” alisema Profesa Ntalikwa.
Continue reading →

RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI KUTOKA KWA MKAGUZI NA MDIBITI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) IKULU DAR ES SALAAM LEO

J1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
J4 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakipitia Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali iliyokabidhiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
J2 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakiwa na watendaji wakuu  wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkafuzi Mkuu wa hesabu za serikali  baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
PICHA NA IKULU

waogealeaji nane wa Tanzania kushindana kesho (jumanne)

C3Kocha wa TSS, Michael Livingstone akiwafundisha  waogeaji Celina Itatiro na Marin de Villard kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg Afrika Kusini kwa ajili ya Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South Africa level 2
C4 
Kocha wa TSS, Alex Mwaipasi akiwafundisha waogeaji wa TSS, kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg Afrika Kusini kwa ajili ya Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South Africa level 2
C5Adil Bharmal na Pieter De Raadt wakionyesha ufundi wao katika ku-dive wakati wa mazoezi ya timu ya TSS kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park kabla ya mashindano ya South Africa level 2
C2Waogeleaji wa Tanzania Swim Squad (TFF) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg Afrika Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South Africa level 2
C1
C6 
Viongozi wa timu ya Tanzania Swim Squad (TSS), Thauriya Diria (wa kwanza kushoto) na Inviolata Itatiro (Katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na kocha  Michael Livingstone wakiwa katika picha ya pamoja TSS kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park kabla ya mashindano ya South Africa level 2

JOH MAKINI NA G-NAKO NDANI YA 102.5 LAKE FM MWANZA.

Weusi @Joh Makini (L) & @Gnako Warawara (R) Wakiwa Rock City,
Raha Yao ni Kusikiliza 102.5 Lake Fm, Radio Ya Wananzengo.
JE WEWE RAHA YAKO YA ROCK CITY NI NINI?
‪#‎Tune
102.5 LakeFm
‪#‎Raha
Ya Rock City
‪#‎Radio
Ya Wananzengo
Follow Facebook, Twitter & Instagram @lakefmmwanza

IZZO BIZNESS APAGAWISHA WAKAZI WA MBEYA KWENYE TAMASHA LA PASAKA

Msanii Emmanuel Simwinga maarufu “ Izzo Bizness “ akitumbuiza
kwenye tamasha la pasaka la home sweet home lililodhaminiwa Tigo jijini Mbeya
jumapili iliyopita.
 Izzo Bizness  akishow love kwa mashabiki zake tamasha la pasaka la home Sweet Home lililodhaminiwa Tigo jijini Mbeya
jumapili iliyopita
Mamia ya mashabiki wakifurahia burudani toka kwa Izzo  Bizness
Yani ilikuwa shangwe wakati Izzo Bizness akitumbuiza jukwaani kwenye  tamasha la pasaka la home sweet home lililodhaminiwa Tigo jijini Mbeya jumapili iliyopita.
.

Milioni 37 zatengwa kukarabati barabara ya Kata ya Panzuo/Mkuranga

Na Mwandishi Wetu,
Mkuranga
JUMLA ya Sh Milioni 37 zimetangwa kwa ajili ya kukarabati
barabara ya Mbogo na Mbezi Muungwana, inayopita katika vijiji kadhaa vya Kata
ya Panzuo, wilaya Mkuranga, mkoani Pwani kwa ajili ya kupunguza adha za ubovu
wa barabara wanazokutana nazo wananchi wa maeneo hayo hali inayopelekea wakati
mwingine akina mama kujifungulia njiani.
Mwendesha bodaboda Ramadhan Rajab akijaribu kupita katika barabara mbovu inayotokea Kimanzichana kuelekea vijiji vya Mnyonzole na Kibesa, Kata ya Panzuo, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.

No comments :

Post a Comment