Na. Lilian Lundo – Maelezo
…………………………………
Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imejizatiti katika kuhakikisha kuwa
utoaji wa huduma kwa wateja wake zinakidhi kiwango cha kimatiafa
ifikapo mwaka 2020.
Hayo
yalisemwa na Meneja Kiongozi Uhusiano na Masoko NSSF Eunice Chiume
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu
ya mabadiliko ya mifumo ili kuboresha utoaji huduma kwa wanachama na
wadau wa mfuko huo.
“Miaka
miwili iliyopita NSSF ilikuwa na mapungufu mengi kuliko ubora ambao
ulipelekea NSSF kuboresha mifumo ya huduma zake na kufanikiwa kupata
Tuzo ya utoaji bora wa huduma mwaka 2014 iliyotolewa na British Standars
Institute (BSI),” alisema Chiume.
Chiume
alitaja maboresho yaliyofanyika kuwa ni pamoja na mfumo mpya wa kupokea
malalamiko ya wanachama ambapo kwa sasa malalamiko yanapokelewa na
kutatuliwa kwa haraka tofauti na ilivyokuwa awali.
Katika
mfumo huo mpya unamuwezesha mlalamikaji kutoa taarifa za kutoridhika na
huduma kwa viongozi wakubwa wa NSSF kama vile meneja kiongozi masoko na
uhusiano na mkurugenzi mkuu ikiwa malalamiko yake hayajafanyiwa kazi
ndani ya muda uliopangwa.
Chiume
aliongeza kuwa maboresho mengine yamefanyika kwenye uchukuaji wa
michango kwa mwanachama tofauti na awali ambapo mwanachama alitakiwa
kuonyesha barua kutoka kwa mwajiri wake ndipo mchakato wa malipo
ufanyike lakini kwa sasa NSSF huendelea na mchakato wa malipo kwanza
huku barua ikifanyiwa kazi.
Anaendela
kubainisha kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na changamoto ya
waajiri kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa mwanachama hivyo NSSF
iliamua kubadirisha mfumo huo, huku barua toka kwa mwajiri ikiendelewa
kufuatiliwa.
NSSF
pia imefungua kituo cha huduma kwa wateja pamoja na akaunti katika
mitandao ya kijamii kama vile facebook na twitter ili wanachama na wadau
wa NSSF waweze kutoa maoni au ushauri na kuwaondolea watu kero ya
kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma.
No comments :
Post a Comment