Monday, February 8, 2016

PSPF YAZIDI KUJITANUA, WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAZIDI KUMIMINIKA KWENYE MFUKO HUO KWA KUJIUNGA NA MPANGO WA PSS


 Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto, akitoa elimu juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSS, na umuhimu wa wanafunzi wa UDSM kujiunga na Mfuko huo kupitia Mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS. Warsha hiyo iliyokusanya wanafunzi karibu 3,000 ilifanyika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani jijini Dar es Salaam
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani na wale wa Chuo Kikuu Cha
Tumaini, kampasi ya Dar es Salaam, (TUDACO) wameendelea kuchangamkia “fursa”
kwa kujiunga na Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kupitia Mpango wa uchangiaji wa
Hiari, PSS
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, UDSM, Kitapenda Ahadi
na Makamu wake, Irine Deodatus Ishengoma, waliongoza mamia ya wanafunzi pale
mlimani kwa kujaa fomu za kujiunga na Mfuko huo.
Hatua ya kujiunga na Mfuko huo ni baada ya semina iliyotolewa na Maafisa wa Mfuko huo, wakiongozwa na mabalozi wa PSPF, Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanya kazi zake Ulaya na Marekani, Flaviana Matata, na Msanii maarufu wa hapa nchini, Mrisho Mpoto almaaruu kama “Mjomba”.
Akizungumzia huduma zitolewazo na Mfuko huo, Afisa wa Matekelezo (compliance), wa PSPF, Albert
M.Feruzi na Hadji Jamadary, walisema, kuna uchangiaji wa mpango wa lazima,
(mandatory scheme) na ule wa hiari Supplementary Scheme) na kuwataka wanafunzi
hao ambao wengi wao ni wa mwaka wa mwisho, kuchangamkia fursa kwa kujiunga na
mpango wa uchangiaji wa hiari.
Nao mabalozi wa PSPF, waliwaeleza wanafunzi hao kuwa pindi wakijiunga na PSPF,
hawatajutia uamuzi wao, kwani kuna watafaidika na mafao mbalimbali kama vile mkopo
wa elimu, fao la uzazi, mkopo kwa muajiriwa mpya, mkopo wa nyumba na mkopo wa
viwanja.
Chuo Kikuu ChaTumaini, tawi la Dar es Salaam, (TUDACO), ndio waliokuwa wakwanza
kujiunga na Mfuko huo ikiwa ni wiki moja tu baada ya wanafunzi wenzao hapo hapo
kuchukua uamuzi huo. 
Afisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Rahma Ngassa, (wakwanza
kushoto), mhamasishaji, Anthony Luvanda, (wapili kushoto), Mabalozi wa PSPF,
Flaviana Matata, (watatu kushoto) na Mrisho Mpoto, (wane kushoto) na Makamu wa
Rais wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Irine Deodatus Ishengoma, wakifurahia
jambo wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na uongoz wa DARUSO kwa
kushirikiana na Mfuko wa Pensehni wa PSPF, na kufanyika ukumbi wa Nkuruma wa
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mamia ya wanachuo walijiunga na
Mfuko huo kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS) 
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, wakijaza fomu za kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wakati wa semina ya siku moja iliyofanyika Ukumbi wa Nkrumah wa chuo hicho mwishoni mwa wiki.
 Afisa wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Gasper Lyimo, akigawa fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko huo, kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, ambao walijiunga na Mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS
 Rais wa Serikali ya Wanafuzni wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, DARUSO,

WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WATUNUKIWA TUZO ZA HESHIMA KUTOKA CHUO KIKUU AFRICAN GRADUATE UNIVERSITY CHA JIJINI DAR ES SALAA

 
Mkuu wa Chuo hicho kutoka nchini Zambia, Profesa Timothy Kazembe akimvika kofia Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba wakati akimtunuku tuzo ya heshima ya udaktari. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk.Fredrick Ringo akimkabidhi tuzo hiyo.
Waimbaji wa nyimbo za injili, Stella Joel (kulia) ambaye ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano na mwenzake Upendo Mbila (kushoto), aliyetunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma wakiteta jambo kwenye mahafali hayo ya pili ya Chuo cha African Graduate University yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja.
Paul Mbila (kulia), akimvika taji mama yake Upendo Mbila ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili baada ya kutunukiwa tuzo Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma.
…………………………………………………………………. 
Na Dotto Mwaibale
 
Chuo Kikuu cha African Graduate University kimewatunuku tuzo za heshima za stashahada ya uzamili katika ngazi mbalimbali waimbaji wa nyimbo za injili nchini kutokana na mchango wao katika jamii.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hizo kwa waimbaji hao katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa alisema ni jambo jema kuwakumbuka watu mbalimbali waliolifanyia taifa mambo mazuri.
 
“Chuo chetu kimeona ni vema kikawapa tuzo za heshima watu mbalimbali wakiwemo wanamuziki wa nyimbo za injili kwani kupitia uimbaji wao wameweza kutoa mafunzo kwa watu na wengine kuacha kutenda dhambi na kuamua kuokoka” alisema Profesa Nzowa.
Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili waliotunukiwa tuzo hizo ni Rais wa Shirikisho la Muziki  Tanzania, Ado Novemba ambaye alitunukiwa tuzo ya heshima ya udaktari, Stella Joel ambaye ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano na Upendo Mbila aliyetunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma.
 
Akizungumza baada ya kupata tuzo hiyo Stella Joel alisema anamshukuru mungu kwa kumuwezesha kupata tuzo hiyo na kuwa imemtia nguvu kuendelea kufanya kazi ya mungu kupitia uimbaji.
 
Kwa upande wake Upendo Mbila alitoa shukurani zake kwa chuo hicho kwa kutambua mchango wa waimbaji wa nyimbo za injili kwa kuwapa tuzo hizo ambazo

CHUO KIKUU CHA AFRICAN GRADUATE UNIVERSITY CHAFANYA MAHAFALI YAKE YA PILI NCHINI JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu Mkuu wa Chuo cha African Graduate University, Askofu Profesa Stephano Nzowa (kulia), akizungumza katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.Kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Timothy Kazembe kutoka nchini Zambia na mgeni rasmi wa mahafali hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo, ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia katika mahafali hayo.
 Wahitimu wa chuo hicho wakiwa wamejipanga tayari kwa kuingia ndani kuanza kwa shughuli mbalimbali za mahafali hayo.
 Ndugu na jamaa na wageni waalikwa  kwenye mahafali hayo.
 Wahitimu hao wakishiriki kuimba wimbo wa taifa.
 Mahafali yakiendelea.
 Taswira katika ukumbi wa mahafali.
 Waliotoa huduma katika mahafali hayo wakiwa katika pozi.
 Waimbaji wa nyimbo za injili wakitoa burudani.
 Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa akimvika kofia Mwimbaji wa nyimbo za injili, Stella Joel wakati akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano katika mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho kutoka nchini Zambia, Profesa Timothy Kazembe.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo akimpongeza mwimbaji Stella Joel kwa kupata tuzo hiyo.
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
 
WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha African Graduate University katika ngazi mbalimbali wametakiwa kutumia elimu waliyopata kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla.
 
Mwito huo ulitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringomgeni aliye kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.
 
“Nawaombeni sana elimu mliyopata itumieni kwa ajili ya kuinua maisha ya familia zetu, wananchi na taifa kwa ujumla na si vinginevyo” alisema Dk.Ringo.
 
Makamu Mkuu wa chuo hicho Askofu Profesa Stephano Nzowa aliwata wahitimu hao kuendelea kujiendeleza kielimu hadi kufikia ngazi mbalimbali za juu.
 
Nzowa alisema watu wengi wamekuwa wakijiendeleza kielimu wakiwa na matumaini ya kuja kupata kazi nzuri jambo ambalo alisema ni bahati.
 
“Msisome kwa ajili ya kuja kupata kazi nzuri bali someni ili kujiongezea uelewa wa mambo mengi ambayo yatawasaidieni kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwaingizia fedha” alisema Nzowa.
 
Profesa Nzowa alisema chuo hicho chenye makao makuu yake nchini Sieralaoni kipo katika nchi kadhaa barani Afrika na kwa Tanzania kinajengwa Wanging’ombe mkoani Njombe na kuwa mahafali hayo ni ya 25 na kwa hapa nchini ni ya pili.
Mkuu wa chuo hicho Profesa Timothy Kazembe kutoka nchini Zambia alisema lengo lao ni kufungua chuo hicho katika nchi mbalimbali duniani ili wanafunzi kujua mambo mbalimbali yakiwemo ya kijamii na ya mungu.
 

ZAIDI YA KAYA 60 KIWALALA NA MJIMWEMA ZIMEATHIRIKA NA MAFURIKO

FGM
WATENDAJI wakuu wa mashirika mawili makubwa ya Umoja wa Mataifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) wametoa wito kwa dunia kujipanga vyema kumaliza kabisa tatizo la ukeketaji (FGM) ifikapo mwaka 2030.
Katika kauli zao walizotoa katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini Dar es salaam watendaji hao Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dk. BabatundeOsotimehin, na Mkurugenzi Mtendaji wa UNCEF, Anthony Lake, wamesema ipo haja ya dunia kuadhimisha siku hiyo kwa kulenga kuwa na kiwango sifuri katika vitendo vya ukeketaji.
Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yamesema kwamba ukeketaji ni vitendo vya kikatili vinavyowanyima wanawake haki yao ya msingi na kuwazuia kuchanua inavyostahili kama wanawake.
Viongozi hao wamesema kwamba vitendo vya ukeketaji vimesambaa duniani kote kuanzia Afrika, Mashariki ya Kati ambako imekuwa kama vitu vya kawaida vikiathiri pia familia katika nchi za Asia Australia, Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Kusini.
Wamesema kwamba kama hatua zisipochukuliwa kutokomeza ukeketaji idadi ya mabinti na wanawake wanaoweza kuingizwa katika mkumbo huo itakuwa inaongezeka ikiwapeleka katika mzunguko ule ule wa kushamirisha ukeketaji na kurejesha nyuma maendeleo ya wanawake na binadamu kwa ujumla kama familia.
“ Ili kuhami utu wa mwanamke, tunahitaji kuchukua hatua sasa na kuwajibika kama dunia kutokomeza ukeketaji. “ ilisema sehemu ya taarifa ya viongozi hao kwa vyombo vya habari.
Septemba mwaka jana katika mkutano wa kutengeneza mpango wa kimataifa wa maendeleo endelevu, nchi 193 zilikubaliana kuhakikisha kwamba ukeketaji unakuw aumetokomezwa ifikapo mwaka 2030.
Taarifa hiyo imesema kwamba ili kufanikiwa wananchi wanatakiwa kushawishi familia nyingi duniani hapa kuachana na tabia ya ukeketaji.
“Tunahitaji kufanyakazi na idadi kubwa ya wataalamu wa tiba katika jamii zetu – wakiwemo waganga wa jadi na wataalamu wa kisasa wa matibabu, tukiwashawishi wakatae kutoa huduma ya ukeketaji.” Ilisema taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo hiyo imetaka wanawake waliofanyiwa ukeketaji kusaidiwa huduma mbalimbali zikiwamo za kisaikolojia na nyingine zinazostahili ili kuwapunguzia maumivu waliyoyapata na wanayoendelea kuyapata kutokana na kukeketwa.

KAMPUNI YA MAWASILIANO YA TIGO YAHAMASISHA WATANZANIA KUJALI AFYA ZAO.

Katika ni Robert Paul ambae ni Meneja Masoko ya Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO Kanda ya Ziwa, akizungumza katika zoezi la Utoaji bure wa huduma mbalimbali za Afya ikiwemo upimaji wa Magonjwa ya Moyo, Utoaji wa Matibabu kwenye majeraha(Vidonda) pamoja na Uchangiaji damu lililofanyika juzi jumamosi February 06,2016 katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
 
“Tigo tumeamua kushiriki zoezi hili ili kuonyesha mfano katika jamii namna tunavyojumuika na Watanzania katika shughuli za Kijamii, hivyo kupitia fursa hii ningependa kuwaasa Watanzania kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara ikiwemo kupima shinikizo la damu, saratani lakini kubwa zaidi kuwa na moyo wa kujitolea kuchangia damu ili kuwasaidia wenye uhitaji wa damu. Alisema Paul.
 
Nae Cassim Aziz (Kushoto) ambae ni Meneja Masoko wa Tigo Mkoani Mwanza, alizishauri taasisi pamoja na makampuni mbalimbali nchini kuwa na desturi ya kushiriki katika shughuli za kijamii hususani kuhamasisha watanzania kupima afya zao mara kwa mara ili kuepuka athari za kiafya zinazoweza kuzuilika.
 
Zoezi hilo liliandaliwa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Udaktari Hubert Kairuki cha Jijini Dar es salaam wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni sehemu ya kuenzi Miaka 17 tangu mwasisi wa chuo hicho afariki dunia (Februa 06,1999) ikiwa ni miaka miwili baada ya kuanzisha chuo hicho.
Dkt.Emmanuel Chacha ambae ni Mkurugenzi wa Hospital ya CJ Jijini Mwanza akizungumza katika shughuli hiyo ya upimaji wa afya bure ambapo Hospital ya CF ilikuwa miongoni mwa wadau waliofanikisha shughulio hiyo.
Mwenye Kinasa Sauti ni Dkt.Francis Tegete ambae ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Profesa Paschalis Rugarabamu ambae ni Mlezi wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Picha ya Pamoja ya wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Wadau waliofanikisha zoezi la Upimaji afya bure wakiwa katika Picha ya Pamoja ya wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Kampuni ya Mawasiliano Tigo ikiendelea na Utoaji wa Huduma zake za Simu kwa wateja
Mmoja wa Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo akipatiwa huduma na wahudumu wa Kampuni hiyo.
Wanafunzi na Wananchi mbalimbali walijitokeza kupima bure afya zao
Zoezi la Upimaji na utoaji huduma za afya bure likiwa linaendelea
Bank ya Damu salama Kanda ya Ziwa ikiendelea na zoezi la ukusanyaji damu kutoka kwa wananchi waliokuwa wanajitolea damu.
Katikati ni Alfredy Chibuae ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Taaisi ya Tanzania Rural Health Movement akifuatilia utoaji wa huduma unavyoendelea. Taasisi hiyo inashughulika na utoaji wa huduma za afya bure kwa watu wasiojiweza hususani watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (mitaani) pamoja na utoaji wa huduma za dharura ikiwemo wale wanaopata ajali. Taasisi hiyo inapatikana Bugando Jijini Mwanza.
PROFESA KILLIAN WA CHUO CHA MKWAWA ASHINDA SAFARI KUTAZAMA BUNDESLIGA UJERUMANI NA STARTIMES
 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo, akichezesha droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
 Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia) akiandika namba ya mshindi wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akipiga namba ya simu ya mshindi aliyepatikana katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia). 
 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo akizungumza na mshindi kwa njia ya simu aliyepatikana wakati wa uchezeshwaji wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
 
MKUU wa Chuo cha Ualimu cha Mkwawa cha mkoani Iringa ambacho ni chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bernadeta Killian (50) amefanikiwa kuibuka mteja wa kwanza mwenye bahati kwa kujinyakulia tiketi ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga kutoka kwa kampuni ya StarTimes katika droo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
 
Akizungumza kwa njia ya simu Profesa Killian baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi amesema kuwa anayo furaha isiyoelezeka kupata taarifa hiyo ya ushindi ambao hakufikiria kama kuna ofa hiyo nzuri kwa wateja.
 
“Ninajisikia furaha kwa kutangazwa kuwa mshindi kwani sikutarajia kama wateja wa StarTimes tunaweza kupewa kubwa kiasi hiki ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ‘Live’. Naweza kusema mwaka umeanza vizuri kwa kuonyesha dalili ya neema kama hii, ni fursa kubwa kwangu mimi kama mteja kwani kuna maelefu ya wateja ambao wangependa kupata fursa hii. 
 
Nawashukuru kwa hili kwani wameliendesha zoezi bila ya upendeleo na sisi wateja wao tunafurahi na kuwapongeza sana na tutandelea kuwaunga mkono.” Alieleza Profesa Killian
 
Mshindi huyo wa kwanza wa droo iliyopewa jina la ‘Pasua Anga na StarTimes’ alipatikana baada ya kujiunga na kifurushi cha Super ambacho ni shilingi 36,000/- katika dishi. Lakini pia mteja yoyote wa StarTimes anaweza kuibuka mshindi kwa kujiunga na kifurushi chochote kuanzia cha shilingi 5,000/- na kuendelea kwa upande wa ving’amuzi vya dishi na antenna. Na kwa wateja wapya pindi wajiungapo na huduma za kampuni hiyo wamekuwa wameunganishwa moja kwa moja na droo ya bahati nasibu.
 
“Ningependa kutoa wito kwa wateja wenzangu waendelee kujiunga kwani bado nafasi zimebaki kushindaniwa na zote zipo kwa ajili yao, hivyo wasilaze damu. Ninaahidi kuitumia fursa hii ipasavyo kwa kuenda kutazama wenzetu wa ulaya wanafanya nini kwa upande wa soka kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukitazama kupitia kwenye luninga, pongezi tena kwa StarTimes kwa kuifanya ligi ya Bundesliga ionekane kupitia ving’amuzi vyake kwa gharama nafuu kabisa ambayo kila mtu anaweza kuimudu. Wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuipa ligi hiyo umaarufu nchini kwani sasa kwa kiasi kikubwa michezo yote inaonekana ‘Live’ na kufuatiliwa na watu wengi.” alihitimisha Mkuu huyo wa Chuo cha Ualimu Mkwawa
 
Naye kwa upande wake Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa, “Hii si mara ya kwanza sisi kuchezesha droo ya bahati nasibu kwa kuwazawadia wateja wetu ni zawadi mbalimbali, hivyo basi huu ni muendelezo tu wa ofa nyingi zinazoendelea kumiminwa kwa wateja wetu waaminifu. Safari hii wateja wetu tumeamua kuwazawadia safari itakayolipiwa gharama zote na kampuni kwenda Ujerumani kutazama ligi ya Bundesliga ambayo kwa Afrika ndio kampuni pekee yenye hakimiliki ya kuionyesha ‘Live’.”
 
“Makubaliano baina ya wamiliki wa ligi hiyo ya Ujerumani na kampuni ya StarTimes yaliingiwa kwa dhumuni kubwa la kuifanya ligi hiyo maarufu barani Afrika kama ligi zingine. Na ni kwa kupitia StarTimes pekee hilo linaweza kufanikiwa kutokana na wingi wa wateja wetu, ubora wa huduma na gharama nafuu ambazo mwananchi yoyote wa kipato cha chini anaweza kuzimudu,” alisema Bi. Hanif na kumalizia, “Hivyo basi nampongeza mshindi wa leo na nawasihi wateja wetu waendelee kujiunga nasi au walipie vifurushi vyao ili waingie kwenye droo ya bahati nasibu na kujishindia safari hii kubwa kwenda Ulaya kutazama mechi moja kwa moja pamoja na mashabiki wengine ulimwenguni.”
 
Akielezea machache kutokana na ushuhuda wake baada ya kupata fursa ya kutembelea ofisi za Bundesliga na kushuhudia mechi kadhaa nchini Ujerumani, Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda, ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli za michezo, amesema kuwa, “Bahati ya kupata safari ya kwenda Ujerumani ni fursa kubwa sana kwa wateja na ningependa waitumie vema. Kuna mengi tu ya kujifunza licha ya kufurahia safari hiyo. Wenzetu wamepiga hatua kubwa na tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwao, hivyo nawasihi waitumie vemam ili waje kutuhadithia na sie huku.”
 
 
Zoezi zima la uchezeshwaji wa droo ya bahati nasibu ya kumpata mshindi ilichezeshwa kwa uwazi na haki mbele ya waandishi wa habari ikishuhudiwa na mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

JK AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MAALUM MJINI DODOMA


 Mjumba wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli akimkaribisha, Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipowasili, Ikuu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma, kuendesha Kikao Cha Kamati Kuu Maalum ya CCM
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiwa na Mjumba wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli alipowasili, Ikuu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma, kuendesha Kikao Cha Kamati Kuu Maalum ya CCM
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo, Chamwino mkoani Dodoma. Kulia ni Rais Magufuli
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi, baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo, Chamwino mkoani Dodoma
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo, Chamwino mkoani Dodoma
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Mumbe wa Kamati Kuu, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa,  baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo, Chamwino mkoani Dodoma
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu mwenzake, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Maaliwa
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli kabla ya kikao kuanza. Katikati yao ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
 Viongozi hao wakiendelea na mazungumzo ya hapa na pale kabla ya kikao kuanza
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo, kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk John Pombe Magufuli na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Wajumbe wakisimama ukumbini kumlaki Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kabla ya kikao kuanza
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk John Magufuli na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa ukumbini
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Katibu wa NEC anayeshughulikia mambo ya Nje Dk. Asha-Rose Migiro ukumbini. Kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Mohammed Seif Khatib
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhavi akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ally Vuai na Balozi Seif Ali Idd  ukumbini
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana na Asha Aboud wakibadilishana mawazo ukumbini 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kumkaribisha Mwenyekiti kufungua kikao
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu Maalum ya CCM, leo, Ikulu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

WAZIRI MKUU APANGA KUKUTANA NA VIONGOZI WA DINI

915
Waziri kuu, Kassim Majaliwa akiteta na Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT,  Dkt.  Brown Abel Mwakipesile katika Ibada ya kumsimika Askofu  huyo iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West Mjini Dodoma Februari 7, 2016.
……………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ataitisha kikao cha viongozi wa dini zote hivi kar
ibuni ili wapange na kuainisha ni mambo gani ambayo wanaweza kutoa ushauri kwa Serikali na kupata njia bora ya kuwahudumia Watanzania.
Ametoa ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Askofu Dk. Brown Abel Mwakipesile iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT la Mlimwa West nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alisema: “Hivi karibuni nitaitisha kikao cha viongozi wa dini zote kitakachojumuisha Maaskofu Wakuu, Masheikh na baadhi ya wachungaji ili tukae na kubaini ni nini kifanyike ili kuisadia Serikali namna nzuri ya kuboresha maisha ya Watanzania.”
Akijibu risala iliyosomwa na Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Leonard Mwizarubi, Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kufanya mapitio ambayo yatawawezesha Watanzania kupata huduma kwa urahisi.
“Katibu Mkuu pamoja na Baba Askofu Mkuu wamegusia suala la upandaji wa gharama za vifaa vya ujenzi pamoja na suala la makazi bora. Mwezi ujao tunaanza vikao vya Bunge vya kupitia bajeti ya Serikali, tutaliangalia hili kwa kumshirikisha Waziri wa Fedha… tutafanya mapitio katika hili ili mwananchi wa kawaida aweze kumudu maisha,” alisema huku akishangiliwa na waumini hao.
Aliwaomba viongozi wa kanisa hilo pamoja na waumini wake waendelee kuiombea nchi pamoja na viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwani kazi ya kutumbua majipu waliyoianzisha ina mitihani mikubwa.
“Kutokana na maombi yenu kwa viongozi wakuu wa kitaifa nina imani Taifa hili litafika tunakotaka liende. Endeleeni kutuombea kwa sababu kazi ya kutumbua majipu ina mitihani mikubwa. Lakini pia napenda niwahakikishie kuwa Serikali hii itatumbua majipu hayo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. Hakuna mtu ambaye ataonewa,” alisisitiza Waziri Mkuu.
Kuhusu mgogoro wa kiwanja cha kanisa hilo kilichopo eneo la Ipagala, Waziri Mkuu aliahidi kulishughulikia suala lao kesho asubuhi kabla hajaondoka kurejea Dar es Salaam. “Kesho asubuhi nitamuita Mkurugenzi Mkuu wa CDA na kumtaka anipe taarifa sahihi kuhusu mgogoro huu. Najua suala hili liko mahakamani, lakini naamini Mkurugenzi anaweza kuwa kiungo kizuri kati ya wananchi waliojenga eneo hili pamoja na kanisa ambao mnamiliki kiwanja husika”.
“Kama atapata eneo jingine na kupima viwanja, kisha akawapatia hawa wananchi anaweza kuwa amesaidia kuondoa mgogoro huu. Wananchi walienda mahakamani huku wakijua eneo lenu limewekewa uzio, sasa wanagoma kutoka kwa sababu hawana mahali pa kwenda,” aliongeza.
Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Mwakipesile alisema kanisa litaendelea kuiombea Serikali ya awamu ya tano ili nchi idumu katika amani na utulivu.
Aligusia eneo la kanisa lililopo kiwanja na 34, kitalu ‘E’, Ipagala East, Dodoma, ambalo ujenzi wa shule yake umesimama kutokana na mgogoro baina yao na wananchi waliovamia eneo lao kwa kujenga nyumba za kuishi licha ya kuwa eneo hilo lilikwishawekewa uzio.
“Kama kanisa tumeshindwa kukamilisha ujenzi wa shule kwa sababu wananchi hao walifungua kesi mahakamani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Tunaomba uamuzi wa kesi hii uharakishwe,” alisema huku akishangiliwa.
Alisema kanisa hilo lina majengo 4,670 nchini kote na viwanja 420 ambavyo ni vya kujenga makanisa na vituo vya kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Mwizarubi alisema katika risala yake kwamba wanaiomba Serikali ifikirie kushusha bei ya vifaa vya ujenzi ili wananchi waweze kuwa na nyumba bora za kuishi.
“Maisha bora maana yake ni kuwa na nyumba bora. Tunaiomba Serikali yako ipunguze bei ya vifaa vya ujenzi ili Watanzania waweze kuwa na makazi bora,” alisema huku akishangiliwa.

RAIS MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 39 YA CCM SINGIDA JANA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI IBADA YA KUMSIMIKA ASKOFU MKUU WA PILI WA EAGT, DKT MWAKIPESILE

10Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa  Pili wa EAGT, Dkt. Brown Abel Mwakipesile  iliyofanyika kwenye Kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Februari 7, 2016
12 16Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt.  Brown Abel  Mwakipesilie zawadi ya picha yenye maadishi ya neon la Mungu katika Ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West  mjini Dodoma Februari 7, 2016.
9Waziri kuu, Kassim Majaliwa akiteta na Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT,  Dkt.  Brown Abel Mwakipesile katika Ibada ya kumsimika Askofu  huyo iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West Mjini Dodoma Februari 7, 2016.
11
13 14 Baadhi ya Waumini wa EAGT wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt Brown Abel Mwakilpesile kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Feb 7, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS WA ZANZIBA AWAANDALIA CHAKULA VIKOSI VYA ULINZI ZANZIBAR

1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akichukua chakula wakati wa hafla ya chakula maalum iliyofanyika leo katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar kwa Vikosi vya ulinzi vilivyoshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (katikati) Kamishna wa jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makam
2Maaskari wa vikozi vya ulinzi wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
3Maaskari wa vikozi vya ulinzi wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
4Askari wa Vikosi vya Ulinzi wakiwa katika hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja kwa ushiriki wao katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
5Maaskari wa vikozi vya ulinzi wakijipanga kwa mstari wakati wa kuchukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja kwa ushiriki wao katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
6Askari wa Vikosi vya Ulinzi wakiwa katika hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja kwa ushiriki wao katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
7Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)pamoja na viongozi wengine wakiitikia dua iliyoombwa baada ya chakula alichowaandalia askari wa vikosi vya ulinzi leo katika viwanja vya katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Unguja kwa ushiriki wao katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
8Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Kamishna wa jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame leo baada ya hafla ya chakula maalum ilichokiandaa kwa Vikosi vya ulinzi vilivyoshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya mpira Makamo Makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar Mjini Unguja,
[Picha na Ikulu.]

WAZIRI MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI KURUDI KAZINI

1Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mvomero Sadick Murad (kushoto) wakati akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani yenye urefu wa Km 48.6. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani.
2Sehemu ya juu ya daraja la Diwale lenye urefu wa mita 75 likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake kama linavyoonekana.
3Mbunge wa Mvomero Sadick Murad akimwongoza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia) kuelekea katika daraja la Diwale, wa tatu kulia ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Mtenga.
4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa Turiani kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa Darajala Diwale.
5Muonekano wa Daraja la Diwale linalounganisha wilaya ya Mvomero na Kilindi.
6Mafundi wanaotengeneza vichwa vya treni katika karakana kuu ya TRL, Mkoani Morogoro.
7Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi Sanayejenga.
8Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawsiliaano Prof.Makame Mbarawa (Wa pili kushoto), akitoa maelekezo kwa Meneja bishara wa kampuni ya Malaysia inayojenga vichwa vya treni Srinivasan Rajmohan (Wa kwanza kulia) kuhusu kufanya kazi hiyo kwa haraka ( Wa pili kushoto) ni katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Eng.Leonard Chamuriho na (Wapili kulia) ni Naibu Waziri Eng.Edwin Ngonyani.
9Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa akizungumza na Wafanyakazi wa TRL (Hawapo pichani), Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Ucukuzi na Mawasiliano Eng.Wdwin Ngonyani, akifuatiwa na Kaimu Meneja wa TRL Morogoro Eng.Yusto Goima na Meneja TANROADS Morogoro Eng.Dorothy Mtenga.
10Wafanyakazi wa karakana kuu ya Reli Mkoani Morogoro wakimsiliza Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa (Hayupo pichani), akiwapa muongozo wa kufanya kazi.
……………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka Makandarasi waliosimamisha kazi za ujenzi wa barabara nchini kuendelea na ujenzi baada ya Serikali kuanza kuwalipa madai yao.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani yenye urefu wa kilomita 48.6 Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, Prof. Mbarawa amesema tayari Serikali imeshalipa makandarasi mbalimbali nchini shilingi bilioni 400 na itaendelea kufanya hivyo ili kumaliza madeni yao kwa haraka.
“Hakikisheni mnarejea kazini na kuwapa mikataba ya ajira wafanyakazi wenu katika kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa ili ujenzi wa barabara na madaraja ukamilike kwa mujibu wa mkataba na hivyo kuondoa usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii”, amesema Prof Mbarawa.
Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation anayejenga barabara ya Magole-Turiani kuwa tayari serikali imeshamlipa zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya laki 735 na Shilingi za kitanzania zaidi ya Milioni 795 hivyo ni wakati wa kukamilisha ujenzi huo hususan sehemu za madaraja kabla ya mvua za masika kuaanza.
Akizungumza katika ukaguzi huo Mbunge wa Mvomero Mhe. Sadick Murad ameiomba Serikali kumalizia daraja la Diwale lenye urefu wa mita 75 ili liweze kupitika.
Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua karakana ya ujenzi wa vichwa vya treni mjini Morogoro na kumtaka mkandarasi anayekarabati vichwa hivyo kufanya kazi hiyo kwa haraka na kutoa kazi nyingine kwa watanzania ili kuwajengea uwezo wa kazi hizo.
Amewataka wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Kufanya kazi kwa ubunifu, uadilifu na uwazi ili kufufua hadhi ya Shirika hilo ambalo ni muhimu kwa uchumi wa nchi hii.
Amesema takribani asilimia 96 ya mizigo inayoshushwa katika Bandari ya Dar es salaam husafirishwa kwa njia ya barabara hivyo ni jukumu la TRL kuhakikisha inapata mizigo ya kutosha ya kusafirisha ili kupunguza mizigo hiyo kusafirishwa na barabara lakini kufufua uchumi wa TRL na taifa kwa ujumla.
“Fanyeni kazi kwa bidii, uwazi na kwa kushirikiana ili kujenga Shirika la Reli la kisasa lenye uwezo wa kujitegemea acheni vitendo vya hujuma na migomo vinavyoweza kudhoofisha shirika hili”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amekemea vitendo wa wizi wa mafuta na kuhujumu Reli vinavyofanywa na watumishi wasio waaminifu na kuwataka kuwa wazalendo kwa nchi yao ili kuchochea kasi ya maendeleo.
Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino (Sekta ya Uchukuzi) Eng. Dkt. Leonard Chamuriho amewataka watumishi wa TRL Kuepuka migomo itakayoathiri utendaji wa Shirika hilo, kubuni mikakati ya kuwezesha shirika hilo kujiendesha kwa faida, kupambana na ubadhirifu wa mali na miundombinu na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta tija inayokusudiwa.
Profesa Mbarawa alikuwa kwenye ziara ya kukagua utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambapo amepata fursa ya kukagua ujenzi wa mizani ya kisasa ya Mikese na kituo cha mtandao wa mawasiliano ya simu vijijini ya Halotel unaosambazwa katika taasisi za Serikali ikiwemo Hospitali, Polisi, Mahakama na Shule hapa nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano

PPF WAKABIDHIWA RASMI JENGO JIPYA LA KISASA WALILOJENGA JIJINI ARUSHA LENYE THAMANI YA BILIONI 32.5

Kiongozi Mkuu wa mfuko wa PPF (Director General) William Erio (kushoto) akipokea michoro ya jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo,  Arch. Dudley Mawalla (kulia) kutoka kampuni ya   MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa kichina CREJ (EA) Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya PPF, Injinia Marko Kapinga.
DG William Erio (pichani juu) ameisifu timu yote iliyoshiriki kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika ubora uliotakiwa na katika bajeti iliyopangwa mwaka 2012 bila kuongezeka pesa yoyote, kuanzia kitengo cha miradi ya PPF makao makuu, wabunifu na wasimamizi, mamlaka za Jiji, idara nyingine za Serikali na wakandarasi wenyewe. 
Jengo hilo maalumu kwa shughuli za ofisi na biashara lenye ghorofa 10 sambamba na eneo la basmenet yenye uwezo wa kupaki magari 168, lina thamani ya shilingi bilioni 32.5. Limejengwa eneo la Corridor, Kitalu Na. 15 Barabara ya zamani ya Old Moshi Jijini Arusha. lina huduma zote muhimu kwa majengo ya kisasa zikiwemo ‘lifti’ za kutosha, majenereta makubwa, mataki ya maji na mafuta ya jenerato, mfumo wa kukabiliana na moto na bila kusahau camera 90 za usalama na eneo kubwa la kuegesha magari ndani ya jengo.
Kwa mujibu wa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi huo wa kisasa, Arch Mawala, ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi Agosti 2 mwaka 2018 ukitarajiwa kukamilika miezi 104 baadae na ulikamilika rasmi (practica completion) mwishoni mwa mwezi Disemba mwakaa jana. Hata hivyo imewachukua miaka miwili na miezi 3 kuweza kukamilisha kila kitu katika ubora wa kiwango cha juu, ambapo miezi hiyo mitatu ni ya ngongeza ya muda kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika. 
Sehemu ya muonekano wa mbele wa jengo
Mpaka kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, tayari ukaguzi wa mamlaka za Jiji na Usalama wa Majengo umeshakamilika na ruhusa ya matumizi kutolewa. Tayari jengo hilo limeshapata wapangaji watatu ambao wapo kwenye jengo tayari zikiwemo benki za TIB na FBNB, huku asilimia 21 ya wapangaji wengine wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na wapangaji wengine 24 wakiwa katika mazungumzo.
Aidha kwa maelezo ya Mratibu wa PPF Kanda ya Kasakazini, Bw Onesmo Rushahi, Ofisi za Kanda ambazo kwa sasa ziko maeneo ya Kaloleni Jijini hapa zitahamishiwa katika Jengo hili jipya, huku mkakati wa PPF ukiwa ni kuhakikisha baada ya mwaka mmoja jengo hilo liwe limefanikiwa kupata wapangaji maeneo yote kwa shughuli za ofisi na biashara. 
Mkandarasi Mkuu ni kampuni ya CRJE (EA) Ltd akisaidiwa na wakandarasi wengine kwa huduma za jengo kama vile ICT na Usalama – SSTL Group Ltd, Lifti – S.E.C (EA) Ltd, AC – M.A.K Enginering Co. Ltd, Mfumo wa maji safi na maji taka – Jandu Plumbers Ltd, na Umeme ni Central Electrical International Ltd. Pia kulikuwa na mamlaka za kiserikali kama wasimamizi wa usalama makazini OSHA, Idara ya maji Asurha – AUWSA, NAESCO, Halmashauri ya Jiji na Bodi za Ukaguzi kama AQRB na CRB. 
Injinia Marko Kapinga, Meneja wa Utekelezaji wa Miradi ya PPF akikagua makabrasha yaliyokabidhiwa na mkandrasi kama michoro halisi ya namna jengo lilivyo kwa sasa
Kiongozi mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, Bw Hu Bo (kulia) ambaye kamapuni yake ndio ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi akikabidhi funguo kwa Director General wa PPF Bw William Erio kama ishara ya makabdihiano ramsi ya jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo. Kwa mbali anashuhudia Meneja wa jengo hilo kutoka PPF Bw..
Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini Bw Onesmo Ruhasha (kulia) akishuhudia makabidhiano rasmi ya jengo jipya la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo
Meneja wa PPF Uwekezaji Bw Selestine Some (kushoto) akimkabidhi ufungua kama ishara ya kuhamishia usimamizi wa jengo la PPF Plaza kwa Menenja Rasilimali, Bw Selemani Kituli wa PPF Kanda ya Kaskazini
Continue reading →

ZAWADI DOTTO AIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA URIMBWENDE YA “MISS ALBINISM 2016”.

New PictureMrimbwende Zawadi Dotto (Pichani) ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa Kuamkia leo Jijini Mwanza.
Miss Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshiki katika Mashindano hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya urimbwene hii ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.
Mashindano hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi katika Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, Washindi wa Kanda hizo watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata Mshindi wa Kitaifa wa MISS ALBINISM 2016.
New Picture (1)Wshiriki Saba wa Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa na umri wao katika mabano ambapo kutoka Kushoto ni Hajra Sadru (22), Antonia Mathias William (17), Furaha Edward John (17), Pendo Faustine (15), Zabibu Abdallah (18), Zawadi Dotto (17) pamoja na Asteria Christopher.
New Picture (2)Washiriki walioingia Nne bora ambapo kutoka kushoto Hajra Sadru, Furaha Edward, Zabibu Abdallah na Zawadi Dotto
New Picture (3)Baada ya Mtifuano mkali hatimae majaji wakatangaza washini. Furaha Edward mshindi wa tatu (Kushoto), Hajru Sadru mshindi wa pili (katikati) na Zawadi Dotto akaibuka kuwa mshindi wa Kwanza (aliepiga magoti).
New Picture (4)Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.

New Picture (6)Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu.
New Picture (7)Kampuni ya Visimbuzi (Ving’amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni yaliyosaidia kufanikisha mashindano hayo. Mwenye Kinasa sauti ni Erick Makonya ambae ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja zawadi zilizotolewa kwa washindi na Kampuni hiyo ambapo Mshindi wa Kwanza amejinyakulia Simu ya StarTimes aina ya Solar5, Mshindi wa Pili simu aina ya P40 StarTimes na Mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya B27 zote zikiwa ni android kutoka StarTimes.
New Picture (8)Baadhi ya Wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi.

DC MAKONDA ATOA SIKU 20 WENYEVITI WOTE WA SERIKALI ZA MITAA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM WAPEWE RAMANI ZA MITAA YAO

New PictureMkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa wilaya hiyo kwenye mkutano uliofanyika Dar es Salaam leo kuhusu jinsi ya kutatua na kukomesha kero za ardhi
New Picture (1)Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda (hayupo pichani)
……………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ametoa siku 20 kwa Wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa Manispaa hiyo kuwa na ramani ya mitaa ili kuyatambua maeneo ya wazi.
Makonda amewataka watendaji wa Manispaa hiyo kwenda na kasi ya serikali ya kuwatendea haki wananchi katika kumaliza migogoro ya ardhi.
Akizungumza Dar es Salaam leo mchana na Wenyeviti zaidi ya 100 wa Serikali za Mitaa ya9 Manispaa ya Kinondoni ,Makonda alisema baadhi ya watendaji wanatanguliza maslahi mbele kuliko mahitaji ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Alisema migogoro ya ardhi ni kero kila sehemu misibani, harusini na kwenye mazishi suala kubwa ni la ardhi na kuongeza kuwa mabaraza ya ardhi ya Kata hayana uhalali wa kuamua kesi hizo kwa kuwa baadhi yao hata uelewa wa masuala hayo hawana na yamekuwa yakiongeza matatizo.
“Leo tumekutana hapa kwa sababu ya migogoro ya ardhi na kuanzia sasa ndani ya Wilaya ya Kinondoni nataka kurudisha heshima ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa nawaagiza kuanzia sasa mtu yeyote kutoka Wizarani,Manispaa au hata mwekezaji lazima apitie kwanza kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa,”alisema.
Alisema watendaji wengi Manispaa ndio chanzo cha migogoro ya ardhi kwa kutotimiza wajibu wao na wameshindwa kuonyesha dira ya kuwasaidia wananchi.
“Kibaya zaidi ili kujitengenezea mazingira ya ulaji wenyeviti hawashirikishwi katika hatua za awali wanahusika zaidi pale kunapotokea mgogoro,”alisema.
Aliongeza kuwa “Sina hofu wala uoga wala sina sifa ya kupendwa wala kutafuta kupendwa hivyo nitahakikisha ninatumia Mamlaka niliyopewa kufanya migogoro hii ya ardhi Kinondoni na kuwa historia na nikitaka jambo huwa sishindwi”alisema.
Alisema baada ya wenyeviti hao kupewa ramani atahakikisha anakutana na Wazi ri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilium Lukuvi na maofisa wa ardhi.
“Hapo sasa watakaobainika kuhusika katika michezo michafu na kuchochea migogoro basi Waziri Lukuvi aondoke nao maana wameshindwa kazi”alisema
Makonda aliwataka wenyeviti hao kuonesha maeneo ya wazi na yale yaliyovamiwa ili kuchukua hatua kwani wenye dhamana wapo ofisini huku wananchi wakiwa wanateseka na migogoro hiyo.
Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Manispaa ya Kinondoni Juliana Letara alisema Wenyeviti wote watapewa ramani za mitaa yao ndani ya wiki mbili kwa kuwa zipo kwenye kompyuta ofisini hivyo atawapatia ramani hizo.
Alisema kutokana na migogoro mingi ya ardhi anapendekeza kufanyike mapendekezo ya mabadiliko ya sheria kwa kuwa kesi zote za mabaraza ya kata zinaigharimu serikali zaidi ya milioni tatu kwa siku.
Alizitaja kesi hizo kuwa ni za ardhi ya hifadhi,ardhi ya kawaida na ile ya kimila
“Tulikopa benki ya TIB mkopo kwa ajili ya kupima Viwanja likiwemo eneo la Mabwepande lakini kila siku tunatozwa riba ya sh.milioni tatu jambo ambalo ni gumu na ipo siku litashindikana na ndio maana tunauza Kiwanja hadi milioni 20 na 30,”alisema.
Baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa ambao walipata nafasi ya kuzungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo walimtaka Makonda kuondoa majipu sugu katika Manispaa hiyo likiwemo la maofisa mipango miji.
Alisema wako tayari kufanyazi na Makonda lakini sio wafanyakazi hao kitengo cha ardhi kwa kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya ardhi.
Imeandaliwa na  www. habari za jamii.com-simu 0712-727062

Rose Muhando naye amafuata Mwaitege Tamasha la Pasaka

imagesNa Mwandishi Wetu
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, Rose Muhando amekuwa wa pili kuthibitisha kushiriki katika Tamasha la Pasaka linalotarajia mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama Muhando ameungana na mwenzake Bonny Mwaitege ambaye alikuwa wa kwanza kuthibitisha katika tamasha hilo.
Msama alisema tamasha hilo mwaka huu linatarajia kufanyika Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28) ambako alitoa wito kutoa wito kwa wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.
Aidha Msama alisema dhamira ya Tamasha la Pasaka ni wenye uhitaji maalum ambao ni yatima, walemavu na wajane.
Msama alisema sababu ya kupeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya ziwa ni kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo sambamba na kupiga vita mauaji ya walemavu wa ngozi ‘albino’.
“Tunalipeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya ziwa kwa sababu ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo ambayo miaka iliyopita iligubikwa na mauaji ya walemavu wa ngozi ‘albino’,” alisema Msama.

RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI ATUMA SALAMU KWA WATENDAJI WA SERIKALI, ASEMA MNATEKELEZA ILANI YA CCM

9
Leo sio siku yangu ya kutoa hutuba, leo ni siku ya bosi wangu, mheshimiwa Mmwenyekiti wetu wa chama cha mapinduzi, chama
tawala ambapo sisi viongozi tunatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi. Lakini nataka nichukue nafasi hii chanya ambayo nimepewa niwashukuru wananchi wa Singida na watanzania kwa ujumla kwa kunipa kura nyingi na kuwa Rais wenu. 
Napenda kukuthibitishia mwenyekiti wetu, mimi pamoja na serikali ninayoiongoza tutaendelea kukienzi chama cha mapinduzi na tutatekeleza ilani ya uchaguzi ili wananchi wote waweze kuondolewa kero zao.Kero zote zinazowakabili wananchi tutahakikisha tunazitafutia ufumbuzi wa haraka, lengo likiwa ni kufuta kabisa ndoto za wapinzani kushika dola.
 Na nitoe wito kwa watendaji wote wa serikali, watendaji wote wa serikali kuanzia juu mpaka chini, anaejijua ni mtendaji wa serikali ana jukumu moja tu la kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi. 
Asieweza atupishe pembeni, uwe mkuu wa wilaya, tekeleza ilani ya CCM, uwe katibu tarafa, wewe uko ndani ya CCM kwa sababu tunaoteua ni sisi, mimi ni Rais lakini ni Rais niliechaguliwa na chama cha mapinduzi. Kwa hio nitoe wito kwa watendaji wa serikali ambao wanapokuwa kule wanajifanya wao ni watendaji wa serikali, wajue serikali hii inaongozwa na Rais mwana CCM ambae yuko hapa kwa ajili ya kutekeleza. 
Nilitaka hili niliweke wazi, tumedhamiria kufanya kazi na ninasema tutafanya kazi kwelikweli na ndio maana kauli yetu ni hapa kazi tu, lakini pia imeungwa mkono na chama changu na mheshimiwa mwenyekiti kwamba kazi ipo pale.

MAADHIMISHO YA KUTIMIZA MIAKA 39 YA CCM MKOANI SINGIDA

1
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi na wanahama wa jumbe wa CCM alipowasili Uwanja wa Namfua Mkoani Singida kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho ya miaka 39 ya CCM leo Februari 6,2016.
2
Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye, kwenye maadhimisho ya kutimia miaka 39 ya CCM iliyoadhimishwa leo Februari 06,2016 katika Uwanja wa Namfua Mkoani Singida, katikati Mhe. Lazaro Nyalandu.
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishauriana Jambo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa waliposimama kwa muda katika kijiji cha Isunna Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida lilipotokea tukio la ajali ya kuanguka gari ya Polisi iliyosabababisha Vifo vya Askari Polisi watatu leo Februari 06,2016.
3 4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi madawati 1000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Paraseko Kone kwenye maadhimisho ya kutimia miaka 39 ya CCM yaliyoadhimishwa leo Februari 06,2016 katika Uwanja wa Namfua Mkoani Singida. Kushoto Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
5 6
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati, katibu Mkuu wa CCM Mhe. Abdulrahman Kinana kushoto, katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mkuu wa Mkoa Singida Mhe. Paraseko Kone kulia, wakitoka nje ya Uwanja wa Namfua Mkoani Singida baada ya kuhudhuria maadhimisho ya kutimia miaka 39 ya CCM yaliyoadhimisho leo Februari 06,2016.
(Picha na OMR)

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA KILELE CHA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI SINGIDA.

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Namfua mkoani Singida kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM.
2
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wanachama wa CCM pamoja na wakazi wa Singida kwenye uwanja wa Namfua waliohudhuria kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM.
6
Rais Mstaafu wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete akihutubia mamia ya wanachama wa CCM mkoani Singida.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete kulia pamoja na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Singida.
5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abruhamani Kinana.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa katika sherehe hizo mkoani Singida.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abrahamani Kinana pamoja na Makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Philip Mangula mara baada ya kuhutubia wakazi wa Singida.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete wakiondoka mara baada ya kuisha kwa sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Singida-
Picha na IKULU

RAIS WA ZANZIBAR AWAANDALIA CHAKULA VIJANA WA HALAIKI

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na viongozi mara alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo katika chakula maalum kwa Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na viongozi mara alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo katika chakula maalum kwa Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na viongozi wakiimba wimbo maalum alipokaribishwa na vijana wa halaiki chakula maalum kwa Vijana hao walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar alipowaandalia katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
10
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Boara DKt.Mwinyihaji Makame Mwadini akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa viongozi na vijana wa halaiki walioshiriki katika sherehe za Mapinduzi ya mwaka 2016 kutimiza miaka 52 katika viwanja wa Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakitia chakula wakati wa hafla maalum ya chakula aliyowaandalia Vijana walioshiriki katika Halaiki ya sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyofanyika leo katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,
5
Baadhi ya Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakichukua Chakula katika hafla ya iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,
6
Baadhi ya Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakichukua Chakula katika hafla ya iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
7
Baadhi ya Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
8
Hawa ni miongoni mwa Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya chakula kilichondaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo
9
Baadhi ya Viongozi walioshiriki katika hafla ya chakula cha mchana alichokiaandaa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Vijana wa halaiki walioshiriki katika sherehe za Mapinduzi ya mwaka 2016 kutimiza miaka 52 katika viwanja wa Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,
Picha na Ikulu.

TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU KUFANYIKA MACHI 28 WILAYANI KAHAMA


Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Pasaka litakalofanyika  Mkoani Shinyanga Wilayani Kahama Machi 28 mwaka huu ambapo Tamasha la Pasaka mwaka huu halitafanyika jijini Dar es Salaam na baadala yake kufanyika mikoani. 

Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
……………………………………………………………………………………………
TAMASHA la Pasaka mwaka huu kufanyika Machi 28 Mkoani Shinyanga katika viwanja kahama wilaya ya Kahama, ambapo tamasha hilo limewapa kipaumbele waimbaji wa ndani ya nchi yetu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Msama amesema kuwa Kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu ni “UMOJA NA UPENDO HUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU”. ambayo itatawala katika tamasha hilo hapa nchini.
Msama amesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Bonfasi Mwaitege amethibisha kutumbuiza katika tamasha hilo pamoja na Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Rose Mhando.
 Aidha Msama amelishukuru  Balaza la Sanaa Tanzinia(BASATA) kwa kuruhusu kufanyika Tamasha la Pasaka wilayani Kahama pia amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika tamasha hilo mkoani humo.

Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kufadhili Michuano ya Kimataifa ya Timu za JKU

2
Makamu Mwenyekiti wa Balraza la Michezo Zanzibar BMZ akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fedha kwa timu za JKU na Mafunzo za mchezo wao wa Kombe la CAF inayotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
1
Meneja wa Makampuni ya Hoteli za Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akizungumza na Waandishi wa habari na Viongozi na Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakati wa kukabidhi fedha za ununuzi wa tiketi wa michuano hiyo inayoandaliwa na CAF Championc Leagua na Confederation Cup 2016. na kuahidi kutowa gharama zote za michezo hiyo. inayotarajiwa kufanyika tarehe 13-2-2016 na 14-2-2016 katika uwanja wa amaan Zanzibar.
  3
Viongozi wa Timu za JKU na Mafunzo wakimsikiliza Meneja wa Makampuni ya Zanzibar Ocean View Zanzibar akizungumza wakati wa hafla hiyo na kutoa ahadi kwa kilia Timun ikishinda mchezo wao huo wa awali itazawadiwa shilingin Milioni Tano kwa ushindi wowote ule,wakati wa hafla ya kukabidhi fedha za tiketi za mchezo huo Kampuni yake imenunua tiketi zote zenye thamani ya shilingi miliono tano kila moja na kutowa fursa kwa Wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar kuona mapambano hayo bure bila ya kiingilio.
4
Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhiwa Tiketi ya Mchezo wa JKU na Gaborone United Club na Kiongozi wa Timu ya JKU Khamis Mohammed, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar.
5
Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa JKU na Timu ya Gaborone United Club Kiongozi wa Timu ya JKU Khamis Mohammed, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar.
6
Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa Mafunzo na AS Vita Club ya Congo Kiongozi wa Timu hiyo Khamis Ali Machenga, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar.
7
Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa Mafunzo na AS Vita Club ya Congo Kiongozi wa Timu hiyo Khamis Ali Machenga, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar.New Picture (7)
Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakiwa katika hafla hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
New Picture (8)
Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakiwa katika hafla hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Imetayarioshwa na OthmanMapara.Blogspot Zanzinews.com
=
indexMENEJA wa hoteli za Zanzibar Ocean View Jacob Makundi (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Idara ya Michezo wa Vyuo vya Mafunzo Khamis Ali Machenga, shilingi 5,000 zikiwa gharama za tiketi za mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya klabu ya Mafunzo na AS Vita ya DRC itakayochezwa Februaei 13, 2016, ambazo zilikwishachapishwa na kuanza kuuzwa. Kampuni ya hoteli za Zanzibar Ocean View imeamua kubeba gharama hizo pamoja na za mechi ya JKU na Gaborone United ya Botswana kuwania Kombe la Shirikisho.
(Picha na Ameir Khalid).
……………………………………………………………………………..
Na Salum Vuai, ZANZIBAR
UONGOZI wa kampuni ya hoteli za Zanzibar Ocean View (ZGH), umeamua kubeba mzigo wa gharama za mechi za wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya klabu barani Afrika zitakazochezwa mwishoni mwa wiki ijayo.
Mechi hizo za kwanza za raundi ya awali, ni ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Mafunzo wataikaribisha AS Vita kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na JKU dhidi ya Gaborone United ya Botswana.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 6, 2016 katika ukumbi wa Nyerere ulioko hoteli ya Zanzibar Ocean View mjini hapa, Meneja wa hoteli hizo Jacob Makundi, amesema hatua hiyo inalenga kuwafanya mashabiki wafike kwa wingi uwanjani siku ya mechi hizo.
Alifahamisha kuwa, tayari kampuni yake imezinunua tiketi elfu kumi (elfu tano kwa kila mechi) zilizobaki baada ya nyengine kuuzwa, kwa gharama ya shilingi elfu kumi, na zitagaiwa kwa mashabiki watakaofika uwanja wa Amaan siku za michezo hiyo bila malipo yoyote.
Makundi alifahamisha kuwa, kampuni yake pia itatoa fulana maalumu kwa wachezaji na viongozi wa klabu hizo, ambazo watavaa kabla ya mechi ya kwanza na watakaposafiri kwenda DRC na Botswana kwa ajili ya michezo ya marudiano.
Meneja huyo amezitaja gharama nyengine ambazo kampuni hiyo itazibeba, ni kutoa punguzo la asilimia 75 kwa waamuzi, makamisaa, viongozi na wachezaji wa timu za wageni kwa huduma ya malazi na chakula kwenye hoteli zake.
Ili kuwapa nguvu wachezaji wa Zanzibar, Makundi aliahidi kuwa kampuni hiyo itatoa zawadi ya shilingi milioni tano iwapo timu itashinda hapa nyumbani, na kuongeza kuwa ushindi huo utakuwa chachu kwao kufikiria motisha zaidi kwa mechi za ugenini.
“Kwa kuwa sisi ni wadau wakubwa wa michezo, tumeona iko haja ya kuwashajiisha wawakilishi wetu hawa ili wafanye vizuri na kuinua jina la Zanzibar katika soka la kimataifa na tunatoa wito kwa taasisi nyengine zijitokeze kuongeza nguvu,” alieleza.
Mapema, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) Khamis Abdallah Said, aliushukuru uongozi wa kampuni hiyo, akisema unaonesha uzalendo kwa nchi katika kuunga mkono juhudi za kuendeleza michezo.
Naye Abdallah Juma Mohammed, aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa kampuni hiyo yenye hoteli tano kubwa Unguja na Pemba Amani Ibrahim Makungu, alisema Zanzibar Ocean imeanza lakini mlango uko wazi kwa wengine kuzisaidia timu hizo na pia michezo mingine.
Akitoa shukuani kwa niaba ya timu zote mbuli, Mkuu wa Michezo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKU) Khamis Mohammed Suleiman, alisema ufadhili waliopata utawatia nguvu ya kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya Zanzibar kwenye michuano hiyo.
Jumamosi Februari 13, Mafunzo wataikaribisha AS Vita katika mechi ya Ligi ya Mabingwa, wakati siku inayofuata JKU watakuwa wenyeji wa Gaborone United kutika Botswana kuwania Kombe la Shirikuso.
Mechi zote hizo zitachezwa katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kuanzia saa 10:00 jioni, na zile za marudiano zitapigwa wiki mbili baadae.

MWENYEKITI WA CCM DK JAKAYA KIKWETE AOGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM SINGIDA, RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU KWA WATENDAJI SERIKALINI

1
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akipokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya CCM yanayofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida ambapo viongozi mbalimbali wamehudhuria wakiongozwa na Mh. Rais Jaohn Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mh.Mama Samia Hassan Suluhu pamoja naye Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-SINGIDA.
2
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mh. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
3
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singinda Mh. Parseko Kone.
5
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na Mh. Rais John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mh.Mama Samia Hassan Suluhu, Kushoto ni Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
06
Msafara wa Mh. Rais John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida tayari kwa kuhudhuria sherehe hizo.
6 7
Mh.Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singida Mh. Dk. Parseko Kone  
8
Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
10
Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili uwanjani hapo katikati ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
11
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono wana CCM na wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja huo.
12
Malkia wa Mipasho mwimbaji wa Taarabu  Khadija Kopa akiongoza kundi la TOT kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya CCM mkoani Singida.
14
Baadhi ya wasanii wa Bongo Move waliohudhuria katika maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.
15
Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.
16
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akitambulisha viongozi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho hayo.
17
Umati wa wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo.
18 19 20 21
Mwimbaji Peter Msechu kulia akiongozana na kundi la bendi ya Yamoto Band tayari kwa kutumbuiza katika maadhimisho hayo.
22
Kundi la Yamoto Band likitumuiza kwenye maadhimisho hayo.
23 24
Kundi la TOT likitumuiza wimbo maalum wa kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi.
25 26
Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rechel Mashishanga aliyekuwa mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA mkoani Singida na sasa amerejea CCM.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AMOS MAKALLA -AKAGUA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA

New Picture (1)Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Amos Makalla na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wamekagua mpaka wa Tanzania na Kenya amekagua alama za mpaka (mawe) ameridhishwa na hali ya usalama wa mpaka na kuagiza kamati ya ulinzi na usalama wiilaya kuwa na mikutano ya ujirani mwema
Aidha Mkuu wa Mkoa ameshiriki kuteketeza mitambo 6 ya kutengeneza pombe haramu ya Gongo, lita 140 za gongo, pipa 33 za maloweko ya gongo
Pia amewataka wananchi kuacha unywaji na upikaji gongo.
New Picture (2)New Picture (3)Baadhi ya mitambo  ya kutengeneza pombe haramu ya Gongo,

MWENYEKITI WA CCM, KIKWETE AOMBA WAZEE KUUNGA MKONO UONGOZI WA RAIS MAGUFULI

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akilakiwa na  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo, kaba ya kukutana na kuzungumza na wazee wa Singida Mjini. Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Mary Maziku.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisubiri kuvalishwa skafu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo. Kushoto ni Mama Salma Kikwete. na Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Singida Mary Maziku na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
 Chipukizi wakimvalisha Skafu Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akienda katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, akiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete, Nape na Mary Maziku

No comments :

Post a Comment