Tuesday, February 2, 2016

Over 500 magistrates censured over case delays

FAUSTINE KAPAMA and ROSE ATHUMANI
MORE than 500 magistrates from different levels are to be reprimanded for poor performance in disposal of cases, the Chief Justice (CJ) Mohamed Othman Chande, announced in Dar es Salaam.

The CJ said this at a news conference held at Mnazi Mmoja grounds in the city, where he disclosed that names of 508 magistrates would be forwarded to the disciplinary committee for action.
“We have already directed all judges in charge of each zone to give seven days to the concerned magistrates to show why disciplinary action should not be taken against them.
We want this action to be completed within 21 days,” he insisted. According to him, the Judiciary had set a target for each resident and district magistrate to determine 250 cases a year and each magistrate at Primary Court level should determine 260 cases yearly. But, he said, the said 508 magistrate underperformed for having handled below 100 cases.
“This is not acceptable. We are operating like a boat which is moving at high speed to ensure early disposal of cases, but there is an anchor which is preventing us from moving. The only option we have is to pull it up so that we can stir the motion,” the CJ said.
The head of the judiciary congratulated all other magistrates who surpassed the target, saying they deserved to be praised for the good job. He gave an example of two magistrates in Dar es Salaam who handled over 900 cases each, another one from Mwanza who determined 789 cases and another in Arusha who judged 778 cases within a year.
“Our target is to start with fresh cases each year. We want all cases that are filed in a year to be determined within the same year and not otherwise. This move is of paramount importance as the people want their cases to be determined early,” he said.
He, therefore, called upon other stakeholders, notably the prosecution to handle the cases with due diligence, the police on their part to complete investigations in time and the advocates to avoid employing technicalities aimed at hindering timely determination of cases.
The CJ also requested the citizens to volunteer themselves to come to court to give testimony, while other key players, like the prison department should ensure inmates are brought to attend their case without failure wherever required.
Speaking on overview of acceleration of determination of cases, he said 222,815 cases were determined last year. At the Primary Court level, the CJ said that 141,025 cases were lodged in the country and 149,757 (including old cases) were determined.
He pointed out that a total of 1240 magistrates handled the cases at all levels and 74.4 per cent of the cases determined were at Primary Courts.
Meanwhile, the CJ told the press conference that the Law Day is expected to be held at national level in Dar es Salaam on February 4, and President John Magufuli is expected to be the guest of honour

Mwamuzi wa kwanza mtanzania wa mchezo wa Baseball.

kij
Kijana Innocent Kennedy ni mtanzania mwenye umri wa miaka 19 tu na kwasasa amekuwa ni gumzo kwa vyama vya kulipwa vya mchezo huu wa baseball barani Asia hususani nchini Japan.
Innocent ameonyesha umahiri mkubwa wa kuamua na kwa mara ya kwanza alishiriki katika kuamua mashindano ya Africa ya kutafuta uwakilishi wa kombe la Dunia la mchezo huu, mashindano yaliyofanyika nchini Kenya katika jiji la Meru hapo Disemba, 2014.
Kwasasa kijana Innocent anaendelea na masomo yake ya ICT jijini Dar es Salaam na ametenga muda wake wa kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 13 :30 hadi saa 18:30 jioni kufika viwanjani Azania Sekondari kushiriki mazoezi ya timu ya Taifa ya baseball.
Katibu mkuu wa mchezo wa Baseball bwana Alpherio Nchimbi alipoulizwa juu ya ndoto ya kumuendeleza kijana huyo, bwana Nchimbi alisema kwa kifupi kuwa lengo kuu ni kuzalisha akina Innocent wengi lakini kwa Innocent anafanyiwa mipango mahususi ya kumpeleka nchini Japan kwa mafunzo zaidi.

WITO UMETOLEWA KWA WAMILIKI WA SILAHA KUHAKIKI SILAHA ZAO KWA WAKATI

Kamanda Liberatus Sabas, alipokuwa akifunga Kampeni za ABIRIA PAZA SAUTI, Jijini Arusha,
………………………………………………………………………….
Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limewataka watu wote wanaomiliki silaha kwa njia halali wafike kwenye kituo cha polisi kuhakiki silaha zao na kuzilipia kama inavyostahili na kwa kufuata utaratibu kama sheria inavyoagiza. 
 Hayo ya mesemwa Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, kwamba kila mwaka huwa kila mwenye silaha anafika polisi na silaha yake na vitabu vyake kwaajili ya kuihahiki na kuilipia kama inavyostahili ,na kama zipo tuhuma zozote kutokana na matumizi ya silaha, itasimamishwa kwaajili ya taratibu zingine na kunyang’anywa hadi hapo jeshi litakapojiridhisha kuwa silaha hiyo matumizi yake ni sahihi ama siyo sahihi
Kamanda amesema utaratibu huu huwa unaratibiwa na makao makuu ya jeshi la polisi kwaajili ya kuhakiki silaha ,ikiwa ni pamoja na kulipia mapato ya serikali ,amewataka watu wanaomiliki silaha wafuate masharti yake kama inavyotakiwa, nawakumbuke sheria inambana kila mtu mara anapotenda kosa ,na kama mtu akiitumia ndivyosivyo atanyang’anywa silaha kwa kutumia sheria iliyowekwa. 
Ameongeza kuwa wapo watu ambao wamewatishia silaha wenzao,na wengine kesi zao zipo tayari na zingine zimefutiwa umiliki kwa mujibu wa sheria, amesema kimsingi kabla mtu hajakabidhiwa silaha ili amiliki, yapo masharti yakufuata na yapo kwenye kitabu kile cha leseni anachopewa wakati wa umiliki, amesema kuwa ukitoka nje ya hayo masharti huna sifa ya kumiliki silaha. 
 Kamanda Sabas ametoa anagalizo kwa wamiliki wa silaha na kusema kuwu silaha ya moto siyo kama panga,silaha hiyo ukiifanyia kosa mara moja yaweza kuua mtu au watu hivyo amewataka kuwa makini sana katika ufuatiliaji wa umiliki, pamoja na namna zinavyotunzwa,amesema jeshi la polisi lipo makini kufuatilia kwa ukaribu wakithibitisha silaha haitunzwi kama inavyostahili utanyang’anywa.aidha amesema kwa wazee amabao umri wao umeenda nab ado wanamiliki silaha huwa wanaichukua na kuihifadhi . 
Amehitimisha kwa kusema kuwa kila , mtu amnayetaka kumiliki silaha, kamati za ulinzi na usalama kuanzia kwenye kata ,Wilaya, Mkoa wakamuidhinisha kuwa na silaha afuate masharti na kuitunza silaha isije ikaangukia kwenye mikono ya wahalifu wakaitumia isivyo halali sheria itafuata mkondo wake, Silaha huwa zinatakiwa kulipiwa kila mwaka kuanzia mwezi julai hadi septemba ukichelewa kulipia unapigwa penati kwa mujibu wa sheria.

MADEREVA DALADALA JIJINI MWANZA WATISHIA KUGOMA IKIWA MAJIPU YA TAX BUBU HAYATATUMBULIWA.

Ridhione Senga (wa pili kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Madereva wa Daladala wanaofanya shughuli zao katika barabara ya Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza, jana akilalamikia suala la uwepo wa tax bubu linalowasumbua katika shughuli zao.
 
Alisema licha ya madereva wa tax bubu wanaobeba abiria kama daladala katika eneo wanalofanyia kazi hususani kubeba abiria wanaoenda na kutoka katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kuzuiliwa, bado madereva hao wa tax bubu wameendelea na biashara hiyo kama kawaida.
 
Senga alibainisha kwamba hatua hiyo inawaweka katika wakati mgumu katika kutimiza majukumu yao kutokana na kupata hasara kila kukicha ambapo amesema ikiwa itaendelea wataitisha mgomo ili kushinikiza kilio chao kufanyiwa kazi.
 
“Sisi tunalipa mapato, lakini jambo la ajabu hawa madereva wa tax bubu ambao hawana leseni ya kubeba abiria wamekuwa ndio wanafanya kazi ya daladala licha ya kupigwa marufuku katika kikao tulichokaa ijumaa iliyopita baina ya Sumatra, halmashauri ya Jiji, Polisi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na wawakilishi wengine bila kuwasahau viongozi wa daladala na tax. Kama hali hii itaendelea tutafanya mgomo hapa na hakuna huduma yoyote ya kubeba abiria itakayotolewa”.Alisema Senga.
 
Ramadhan Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za Bugarika-Muzunguko Jijini Mwanza aliunga mkono hoja ya mwenyekiti huyo na kusema kuwa ikiwa mamlaka husika zitashindwa kutatua suala la tax bubu katika eneo hilo, wao watachukua hatua ya kusitisha huduma ya usafirishaji katika barabara hiyo ya Bugarika-Buzuruga.
 
“Hizi tax bubu tunasikia ni za wakubwa na ndiyo maana hawa madereva wanaoziendesha wana jeuri mno. Sisi tunasema haya ni majipu na tunawaomba viongozi wengine wakubwa akiwemo Mhe.Magufuli, waangalie huku Jijini Mwanza maana kuna majipu makubwa ya kutumbua”.Alisema Athuman Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza.
 
Kaptaini Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza, ameshauri suala hilo kutatuliwa na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuwa ndilo lenye jukumu la kukamata vyombo vya usafiri vinavyofanya kazi kwa kukiuka sheria na taratibu zilizoweka na mamlaka husika ikiwemo halmashauri ya Jiji Mwanza ambayo ndiyo inasimamia taratibu la utendaji kazi wa tax.
 
Juhudi za kuwatafuta madereva wa tax hizo zinazodaiwa kufanya kazi kinyume cha sheria (tax bubu) bado zinaendelea ili kujua kuzungumzia malalamiko yanayowakabiri.
Ramadhan Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za Bugarika-Muzunguko akitoa malalamiko yake.
Athuman Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza.
Kulia ni Kaptaini Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi wake.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo

MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI WANUFAISHA KAYA MILIONI 1.1 NCHINI

Mpango wa Kijamii wa Uzalishaji Salama ili kusaidia kaya masikini kupambana na umasikini (PSSN) umefanikiwa kuwa na matokeo mazuri kwa kusaidia kaya Milioni 1.1 nchini na kusaidia juhudi za serikali kupambana na umasikini.
Hayo yamefahamika wakati washirika wa maendeleo ambao ni Umoja wa Mataifa, Benki Kuu ya Dunia, Serikali ya Uingereza kupitia kitengo cha Maendeleo ya Kimataifa, Irish Aid, USAID, Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Sweden (SIDA) walipotembelea miradi ya maendeleo katika wilaya za Unguja, Chamwino, Babati, Sumbawanga (Manispaa na Wilaya), Singida na Hanang kwa kipindi cha siku tatu kuanzia Januari, 19 hadi 22.
unnamed
Bi. Kazijya Kila ambaye ni mmoja wa wanufaikaji wa fedha akitoa ushuhuda kuhusu mradi wake wa chakula ulivyowezeshwa na TASAF ambapo hadi hivi sasa anatengeneza faida ya Shilingi 7000 kwa siku na kabla ya kuwezeshwa alikuwa akikaa nyumbani na mama yake bila kuingiza kipato chochote.
Katika Mpango huo ambao utekelezwaji wake unasimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) unafanyika Tanzania Bara na Tanzania visiwani ukiwa na lengo la kuzisaidia kaya masikini pesa za matumizi ili kukidhi mahitaji ya kupata chakula pamoja na kuwawezesha kusaidia watoto wao kupata elimu jambo ambalo linaonekana kuzaa matunda kwa maeneo mengi ikiwepo Tanzania visiwani.
Serikali ya Tanzania imekuwa ikisaidia na washirika wa maendeleo ili kupunguza umaskini uliokithiri kwa wananchi wake na mwaka 2013 iliweka mpango wa kusaidia kaya masikini 275,000 kwa kipindi cha miaka mitano na tangu ianzishe mpango huo ilifanikiwa kusaidia kaya 275,000 kwa mwaka 2013 pekee katika wilaya nane nchini.
unnamed (1)
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed (kushoto) na Msimamizi wa mpango wa PSSN, Bw. Ramadhani Madari wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu kwa wanufaikaji wa fedha hizo.
Na mpaka kufikia sasa mpango huo umeshatoa malipo mara 12 na jumla ya kaya masikini milioni 1.1 zimeshafaidika na mpango huo ikiwa ni kwa wilaya 161 na vijiji 9789 nchini.
Malengo ya serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa ni kuhakikisha kufikia mwaka 2030 kunakuwa hakuna masikini hivyo ni wajibu wa kila nchi kuhakikisha inawasaidia wananchi wake ili wajijengee uwezo wa kujitegemea na kuondoka katika janga la umasikini.
unnamed (2)
Asilimia kubwa ya wanufaikaji wa mpango huo ni wanawake, kama wanavyoonekana pichani.
unnamed (3)
Mkurugenzi wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus Kamagenge akizungumza na wanufaikaji wa mpango wa TASAF (hawapo pichani).
unnamed (4)
Mkurugenzi wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus Kamagenge (kushoto) akifurahi jambo na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed.
unnamed (5)
Timu ya TASAF na wadau wa maendeleo wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo.
unnamed (6)
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed na Aine Mushi wa UN/NRA.
unnamed (8)
Bi Jabo Omari Othman akiwa kwenye shamba lake alilonunua kutokana na fedha za TASAF visiwani Unguja.

SIMBA SPORT CLUB WAZINDUA DUKA LA VIFAA VYA MICHEZO

Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Akikata Utepe wakati wa Uzinduzi wa Duka la Vifaa vya Michezo akiwa Ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuuwa Eaggroup Ndugu Iman Kajula Pamoja na Wadau wengine wa Club Hiyo.
 Katika kukuza wigo wake wa mapato pamoja na upatikanaji wa vifaa, klabu ya Simba leo imezindua duka lake rasmi kwa ajili ya kuuza vifaa vya michezo vyenye chapa ya Simba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Rais wa Simba Evans Aveva alisema “kama  mtakumbuka moja ya malengo ambayo uongozi wangu huu uliopo madarakani ulijiwekea ni pamoja na kuongeza wigo wa mapato kupitia vyanzo vyake vilivyopo lakini pia kuja na mkakati kabambe kwa ajili ya kuongeza na leo wote tunakuwa mashuhuda katika kuzindua duka letu la vifaa vya michezo. Duka ambalo litakuwa likiuza kila bidhaa ambayo inachapa Simba hivyo wanachama na wapenzi wa Simba kuweza kujua ni wapi mahala pa kupata vitu halisi vya Simba na kwa bei nafuu zaidi”
 Duka hili si tu litasaidia katika kuongeza mapato kwa klabu lakini pia litaziba mianya yote ya wale watu wote wasio itakia mema klabu yetu na kuamua kutengeneza vitu feki vyenye chapa ya Simba, kwakuwa sasa mtu ukikutwa na bidhaa feki basi mkono wa sheria utakuwa juu yako. Nipende kuwa sisistiza wanachama, wapenzi na wadau wote wa Simba na soka la Tanzania kwa ujumla kuwa kwanza tupende vyetu vya nyumani lakini pia tupende kutumia vitu halisi na kuachana na utamaduni wa mazoea ya kutojali ni kipi halisi na kipi ni feki” aliongeza Rais Aveva
Akizungumza kwenye ufunguzi huo Mkurugenzi wa kampuni ya EAG Group Ltd ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya biashara na masko kwa klabu ya Simba Bw. Imani Kajula alisema “nadhani sasa wanasimba tunaweza kufurahia vya kwetu kwani kwa sasa tunajua ni wapi vinapatikana na ni wapi ukienda huwezi kukutana na kitu feki chenye chapa ya Simba na hapo si pengine bali ni Simba Sports Shop lililopo katika jingo la DarFree Market. Pamoja na kuwepo kwa duka hili lakini pia vifaa vyote vitakavyokuwa vikipatikana hapa ndani ya siku za hivi karibuni vitakuwa vikipatikana kwenye duka mtandao (Online Shops) na hivyo kuweza kuwafikia watu wote popote walipo nchini Tanzania”. 
 
Unapotaka vifaa vyenye ubora wa hali ya juu hakuna sehemu nyingine zaidi ya Simba Sports Shop. NUNUA HALISI ICHANGIE TIMU YAKO. Alimalizia Mkurugenzi wa EAG Group Ltd Imani Kajula
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa duka hilo msimamizi wa Duka la vifaa vya michezo venye chapa ya Simba mkurugenzi wa kampuni ya Insight Media Bw. Tahir Othman ambao ni waamiliki wa Dukakwa kuhamasisha wapenzi wote wa Soka Tanzania kuweza kuunga mkono juhudi zinazofanywa na klabu ya Simba ili kuweza kukuza mapato kwa klabu yetu lakini pia kuweza kupata bidhaa bora na halisi za chapa ya Simba. 

Uzinduzi wa wiki ya Mahakama mkoani Iringa

ri1
Mkuu wa wilaya ya Iringa leo amezindua wiki ya mahakama kwa maandamano mjini Iringa yaliyoongozwa na brass band ya Magereza. Akihutubia majaji pamoja na wananchi amesisitiza uharaka wa kutoa HAKI. kesi nyingi zinachelewa kuisha na wananchi wengi wamedhrumiwa haki yao na huu ni uvunjwaji katiba.
Pia amesisitiza wakimama wasimamiwe haki zao. Kasesela pia alisisitiza polisi na ofisi ya mwanasheria mkuu wakae pamoja kubaini kwa nini kesi nyingi ushahidi unakuwa haujakamilika? Wakamilishe ushahidi kabla ya kufungua kesi. Bila haki nchi haiwezi kuendelea hata kidogo.
Akitoa salamu zake Jaji Mfawidhi kanda ya Iringa Mh Mary Shangali aliahidi kuharakisha kesi pia kutembelea magereza yote ili kubaini waliocheleweshewa haki zao.
ri2 ri3 ri4 ri5

BONDIA VICENT MBILINYI APIGIA MKWALA MZITO MWINYI MZENGELA KUPIGANA PASAKA

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi anaenolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ amemchimbia mkwala mkali bondia Mwinyi Mzengela watakapokutana siku ya April 26 katika sikukuu ya Pasaka 
Mbilinyi amemtangazia kiama Mzengela baada ya kukubali kupambana nae katika uzito wa KG 63 amesema nitamsambalatisha mapema mno bondia huyo ambaye ni bingwa wa uzito wa KG 63 kupitia Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC)
 
Mbilinyi aliongeza kwa kusema namuheshimu Mzengela kwa kuwa ni bingwa wa Taifa hata hivyo nitahakikisha nausambaratisha utawala wake na mimi nakuwa juu yake kwa kuwa nia ninayo uwezo ninao na nitaonesha jinsi ngumi zinavyochezwa  
Najuwa katika ngumi za kulipwa sina muda mrefu sana na nimeshatambulika kwa kuwa najua nini nakifanya katika mchezo uhu wa masumbwi nchini
Nimeingia katika ngumi za kulipwa sio kupoteza mda kwa kuwa najua mchezo wa ngumi ila kwangu mimi ni ajira na ndio ninayo itegemea.

WATUMISHI 508 WA MAHAKAMA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU ASEMA JAJI MKUU MHE. MOHAMED OTHMAN CHANDE.

jaji
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Othman Chande akizungumza wa waandishi wa Habari kuhusu kuanza kwa Mwaka wa Sheria 2016, Wiki ya Sheria na Utendaji wa Mahakama ya Tanzania kwa mwaka 2016. Wengine Kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (Kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaaban Lila (kulia).
………………………………………………………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Othman Chande amesema kuwa Mahakama ya Tanzania itawachukulia hatua za kinidhamu na za kisheria Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo,Wilaya na wale wa Mahakama za Hakimu Mkazi wapato 508 kote nchini waliotekeleza majukumu yao chini ya kiwango na kushindwa kutimiza wajibu wa Mahakama wa Utoaji wa Huduma Bora kwa wananchi katika mwaka wa Sheria wa 2015/2016.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam alipokua akitoa ufafanuzi kuhusu  kuanza kwa mwaka mpya wa Sheria wa 2016 na Maadhimisho ya Wiki ya Sheria ambayo kilele chake kitakua Januari 4,2016 Jaji Mkuu amesema  kuwa kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa Mahakama na upimaji wa viwango vya utendaji kazi vilivyowekwa, Mahakimu hao wa Mahakama za wilaya na Hakimu Mkazi 121 na 387 wa Mahakama za Mwanzo watatakiwa  kutoa maelezo ndani ya siku 7 juu ya sababu zilizowafanya washindwe kutimiza lengo lililowekwa la kushughulikia mashauri 260 kila mmoja.
Amesema watakaothibitika  kamati za nidhamu na maadili za kila wilaya na Mikoa ambazo ni Kamati ndogo za Tume ya Utumishi wa Mahakama zitawafungulia kesi za kinidhamu ndani ya siku 21.
“Wale watakaobainika watakumbwa na adhabu ya kupewa Onyo, kushushwa vyeo na kufukuzwa kazi ili iwe fundisho kwa wengine, ninajua wapo baadhi ambao waliajiliwa katikati ya mwaka, wengine kwenda mafunzo ya vitendo vyuoni, wajawazito na baadhi vituo vyao kuwa na kesi chini ya 260 kwa mwaka” Amesisitiza.
Aidha, katika hatua hiyo amewapongeza Mahakimu waliofanya vizuri katika utendaji wao wakiwemo 14 walioshughulikia mashauri zaidi ya 700 kila mmoja, Mahakimu 50 walioamua kesi zaidi ya 500 kila mmoja baadhi wakitokea wilaya ya Mkuranga, Rufiji  na Bukoba mjini na wengine wawili kutoka Dar es salaam walioamua kesi zaidi ya 900 kila mmoja na  kuvuka lengo la utendaji lililowekwa la kushughulikia mashauri 260 kwa mwaka.
Akitoa tathmini ya utendaji wa Mahakama kwa mwaka wa sheria uliopita amesema kuwa Mahakama ya Tanzania ina Mahakama za Hakimu Mkazi kila Mkoa na Mahakama za Wilaya 111 katika wilaya za Kiserikali 133 pamoja na Mahakama za Mwanzo ambazo hupokea asilimia 93 ya mashauri yanayofunguliwa kote nchini.
 Amesema mwaka 2015 Mahakama zote nchini zilipokea jumla ya mashauri 206,115, kati ya hayo mashauri 220,815 yaliamuliwa kukiwa na ziada ya mashauri 14700 jambo linaloonyesha kuwa Mahakama zinapokea mashauri na kuyashughulikia kwa kasi inayoridhisha huku mashauri yanayosababisha mrundikano ni yale yaliyo nje ya idadi iliyopangwa.
Ameongeza kuwa katika katika kipindi cha mwaka huo wa 2015 Mahakama za Mwanzo zilipokea mashauri 141,025 ambapo kati ya hayo Mashauri 149,757 yalishughulikiwa huku idadi ya Mahakimu walioshughulikia mashauri hayo ni 1240.
“Ukiangalia mwenendo wa ufunguaji wa mashauri yote kote nchini hasa Tanzania Bara utagundua kuwa Mahakama za Mwanzo, Wilaya na zile za Hakimu Mkazi  zinapokea mashauri mengi kwa asilimia 93 ,katika kila mashauri 4 yanayofunguliwa nchini 3 yako mahakama za mwanzo ambako wananchi wengi wanatafuta ufumbuzi wa kesi zao lazima tuweke mkazo” Amesema Jaji Mkuu.
Kuhusu kuanza kwa mwaka mpya wa Sheria mwaka 2016 amesema Mahakama inauanza chini ya Kauli Mbiu Isemayo “Huduma Bora kwa Wananchi ni Wajibu wa Mahakama na Wadau wake”  ikiwa na kesi 20,431 ikilinganishwa na 34,126 ilizoanza nazo mwaka 2015 na kuongeza kuwa licha ya changamoto zinazoikabili Mahakama ya Tanzania mkakati uliopo ni kupunguza idadi hiyo hadi kufikia 0 kwa kila mwanzo wa mwaka wa sheria.
Akitoa ufafanuzi kuhusu upatikanaji wa Nakala za hukumu amesema Serikali inaendelea kuijengea uwezo wa kifedha Mahakama wa kuajiri wachapaji wa nakala wengi zaidi ili Nakala za Hukumu za Kesi ziweze kupatikana pindi tu kesi zinapomalizika katika mahakama zote nchini tofauti na ilivyo sasa ambapo hupatikana Mahakama Kuu na Mahakama za Rufani.
Aidha, amesema Mahakama inaendelea kuboresha miundombinu yake ikiwemo majengo na ujenzi wa mahakama mpya katika maeneo yasiyo na huduma hiyo katika mwaka 2016. “ Hivi sasa tuna wilaya 23 hazina Majengo ya Mahakama za wilaya, kwenye baadhi ya maeneo kesi zinasikiliziwa Ofisini kwa Hakimu wakati ilitakiwa ziwe kwenye jengo lenye ukumbi wa wazi,tumejiandaa kwa michoro ya majengo kwa mahakama zote ili tuanze kujenga kwa gharama nafuu”  
Mhe. Chande ametoa wito kwa wananchi kutosita kuitumia Mahakama ya Tanzania katika kupata ushauri wa kisheria kupitia wataalamu wake, kuhudhuria maonesho mbalimbali ya kisheria yanayofanyika nchini huku akitoa angalizo kwa baadhi ya watu wanaochangia kuwepo kwa mrundikano wa kesi kwa kufungua kesi za madai au kupeleka mashauri Mahakamani kama sehemu ya maegesho ya masuala yao.
“Baadhi ya watu wamekuwa wakipeleka kesi Mahakamani kama sehemu ya maegesho, huzifungua kisha hushindwa kujitokeza Mahakamani hizi ni tofauti na zile zenye vipengele vingi ndani ya kesi moja au zile ambazo mashahidi wake wamehama kutoka eneo moja kwenda linguine, hizi nawahakikishia tutazifuta ili kupunguza mrundikano wa kesi kwenye Mahakama zetu” Amesisitiza Mhe. Chande.

RAIS MAGUFULI AMHAMISHA SUZAN MLAWI KUWA NAIBU KATIBU MKUU UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA.

IMG-20160201-WA0040

TUME IPO HURU HAIJAWAHI KUINGILIWA KIMAAMUZI NA RAIS WALA KIONGOZI YOYOTE- JAJI LUBUVA.

IMG-20160201-WA0039

UMOJA WA WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE YA HEGONGO,MUHEZA WAANGUSHA PARTY LA NGUVU

Wanafunzi waliowahi kusoma miaka ya 80 katika Shule ya Sekondari ya Hegongo, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, wakicheza muziki wakati wa hafla yao ya kukumbukana iliyofanyika kwenye Mgahawa wa City Sports Lounge, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Martine Jengo (kulia) na Mzee Hassan wakiserebuka
Mmiliki wa TSN Group, Farouq Baghoza (kulia), ambaye pia alisoma katika shule hiyo, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kumbukumbu.
Mmiliki TSN Group,  Farouq Baghoza (kulia) akiwa na wanafunzi aliosoma nao katika shule ya Hegongo,  Mkurugenzi wa Mgahawa wa City Sports Lounge, Benny Kisaka (kushoto) pamoja na Gerald Yambi ambaye ni mwanachama maarufu Kundi la  Friends of Simba. Baghoza aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Saidia Taifa Stars Ishinde.
Sasa ni wakati wa mlo
Mwanafunzi Edwin Pemba (kushoto) akiwa na Mwalimu John Sebo (katikati) aliyewahi fundisha katika Shule ye Sekondari ya Hegongo.
Aliyewahi kuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Hegongo, John Sebo akishukuru kualikwa na waliokuwa wanafunzi wake katika hafla hiyo muhimu.Kulia ni Mwanafunzi Benny Kisaka ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Mgahawa wa City Sports Lounge.
Hawa walimaliza Kidato cha Nne katika shule hiyo 1985.
Hawa walisoma katika shule hiyo na kumaliza Kidato cha Nne miaka ya tisini

JAJI MKUU OTHUMAN CHANDE ATOA SIKU SABA KWA MAHAKIMU 508 WATOE MAELEZO KWANINI WASIFUNGULIWE MASHITAKA KWA KUFANYA KAZI CHINI YA KIWANGO

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana , kuhusu utendaji wa mahakimu wa mahakama za hakimu mkazi, mahakama za wilaya na mahakama za mwanzo ambapo alitoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo kwani ni wasifunguliwe mashitaka ya nidhamu na kuwajibishwa kwa kufanya kazi chini ya kiwango. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omari Mallungu na kulia ni Jaji Kiongozi wa Tanzania, Shaban Omari Lila. Jaji Chande alitoa kauli hiyo kwenye maonyesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja. 
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akikaribishwa kutembea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo.
 Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na  Maadili Mahakama ya Tanzania, Warsha Ng’humbu (kushoto), akimuelekeza jambo Balbina Mrosso (kulia), kutoka Babati mkoani Manyara aliyetembelea banda la Idara ya Malalamiko kuomba msaada wa kisheria katika maonyesho hayo.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akisoma moja ya daftari katika banda la Idara ya Malalamiko kwenye maonyesho hayo. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Malalamiko Mahakama ya Tanzania, Happiness Ndesamburo.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (kulia), akielekezwa jambo katika banda la Divisheni ya Biashara katika maonesho hayo. 
…………………………………………
Na Dotto Mwaibale
 
JAJI Mkuu wa Tanzania Othuman Chande ametoa siku saba kwa mahakimu 508  watoe maelezo ni kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa, baada ya kufanya kazi chini ya kiwango.
Jaji Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Sheria.
Alisema kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama hizo wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.
Alibainisha kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo mahakimu Wakazi na Mahakimu  wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.
“Ukiondoa wale ambao wameajiriwa karibuni, wanaofanya kazi kwenye mahakama za mwanzo zisizokua na mashauri mengi au waliyokwenda masomoni kati kati ya mwaka  au likizo za ujauzito hawatahusika katika sakata la kujieleza.
“Majaji Wafawidhi nimewaagiza wachambue na kuanisha mahakimu wote walioshindwa kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua kesi 250 na kesi 260 kwa mwaka jana na kuwataka watoe maelezo ndani ya siku saba kwa nini wasichukuliwe hatua,” alisema Jaji Chande
Jaji Chande alitoa muda wa kukamilika kwa mchakato huo, ambapo walizitaka idara husika ndani ya siku 21 kila kitu kiwe kimekamilika ili ijulikane ni hatua gani wanachukuliwe.
“Mahakama haikubali hakimu ambaye anabembeleza kesi. Hakimu hatakiwi kufanya hivyo anatakiwa asikilize kesi hizo naazimalize. Haiwezekani katika mahakama moja hakimu mmoja anamaliza kesi 800 mwingine anamalizia chini ya 100  hilo halitakubalika kutokana na kasi ambayo tunayo,” alisema
Jaji Chande alisema mahakimu hao watapelekwa katika kamati zao kwa hatua ya kujieleza. Kazi kuu ya kamati hizo ni kupeleleza, kuchunguza na kushughulikia mashtaka yote ya nidhamu ya mahakimu.
“Mahakimu wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na kushindwa kutoan sababu za kuridhisha kwa nini wameamua idadi ndogo ya kesi kuliko walivyopaswa, ambapo itashughulikiwa haraka na Kamati za Maadili za Mahyakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki,” alisema
Hata hivyo, Jaji Chande alitoa pongezi kwa mahakimu ambao wamevuka kiwango, ambapo mahakimu 14 wameamua zaidi ya kesi 700 kwa mwaka jana na mahakimu wengine wamesikiliza kesi 915,789 na 778.
Alisema mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza, kwa sababu kuna baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa zikimaliza kesi na kuanza mwaka upya.
Jaji Chande alisema Januari 1, 2015 mahakama za mwanzo zilianza na kesi 34,126 na mwaka huu Januari 1 zilianza na kesi 20,431. Kiwango cha kumaliza kesi ukilinganisha na idadi ya kesi zilizosajiliwa 2015 nni zaidi ya asilimia 100. Mahakama ya Mkuranga asilimia 141, Rufiji asilimia 121 na Bukoba Mjini asilimia 224.

BALOZI WA SWEDEN AMTEMBELEA SPIKA OFISINI KWAKE

1 
Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt akisaini kitabu cha Wageni alipomtembelea leo ofisini kwake tarehe 01 Febuari, 2016 Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Afisa wa Ubalozi wa Sweden Bw. Ludvig Bontell.
3Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnittaliyemtembelea leo Ofisni kwake Mjini Dodoma
4Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifanunua jambo wakati akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt. Wengine katika picha ni maafisa wa Ubalozi wa Sweden na Wabunge.
5Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pmoja na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt na Maafisa wengine wa Ubalozi wa Sweden na wa Bunge
6Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiaagana na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt mara baada ya kuzungumza anye ofisini kwake. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Sweden Bw. Ludvig Bontell.
9Katibu wa Jukwaa la Wahariri Bw Neville Meena akifafanua jambo kwa Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah wakati alipomtembele Ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo. Kuli kwa Spika ni Naibu Katibu wa Bunge-Shughuli za Bunge Bw. John Joel.Wengine katika picha ni Viongozi wa Jukwaa la Wahiri na Maafisa wa Bunge.
(Picha na Ofisi ya Bunge)

WANANCHI WAMESHAURIWA KUACHA TABIA YA KULA KATIKA MAZINGIRA SI SALAMA

images 
Na Magreth Kinabo –MAELEZO
……………………………………………
Wananchi wameshauriwa kuacha tabia ya kununua matunda yaliyomenywa barabarani au kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira ambayo si safi na salama ili kuweza kuepuka ugonjwa kipindupindu na kulinda afya zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto,Michael John wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dares Salaam kuhusu taarifa za ugonjwa huo kwa nchi nzima.
“Suala la kuepukana na ugonjwa wa kipindupindu linahitaji ushirikiano wa watu wote.Usiponunua matunda yaliyomenywa na watu wanaouza barabarabani, hata wale wanaouza wataacha kuuza. Pia Serikali itatumia nguvu kidogo kwa ajili ya kuwadhibiti,” alisema John.
Akizungumzia kuhusu juhudi zinazofanyika za kukabialiana na ugonjwa huo, alisema hivi sasa kuna timu ya wataalamu ambayo imekwenda Morogoro ikiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Mpoki Ulisubisya na nyingine mkoani Dodoma ambayo itakuwa na Waziri wa wizara hiyo,Ummy Mwalimu ili kuweza kushirikiana na mamlaka, watendaji na baadhi ya wadau kuudhibiti ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa ripoti ya ugonjwa huo kwa kipindi cha wiki jumla ya wagonjwa 459 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo katika mikoa 15 na vifo vitano.
Alisema mkoa wa Simiyu ndio unaongoza kuwa na idadi ya wagonjwa wengi, ukifuatiwa na Mwanza, Mara na Morogoro. Pia mikoa ya Njombe , Ruvuma na Mtwara haijawahi kuripotiwa na ugonjwa huo.

MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA

1Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza Bungeni Mjini Dodoma Februari 1, 2016.
6Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu akizungumza Bungeni Mjini Dodoma Januari 1, 2016.
7 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akisoma Mapendekezo ya Mpango wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha, 2016/2017, bungeni mjini Dodoma Februari 1, 2016.
4 
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangallah akijibu Maswali Bungeni Mjini Dodoma Februari 1, 2016.
5 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akijibu Maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari 1, 2016.
2Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki (katikati) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Februari 1, 2016.
3Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete Bungeni Mjini Dodoma Februari 1, 2016.   8Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 1, 2016.
9Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Jukwaa la Wahariri nchini kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Februari 1, 2016. Kutoka kushoto ni Mjumbe , Jesse Kwayu, Makamu Mwenyekiti, Deodatus Balile na Katibu Mkuu Neville Meena.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YAPANGA KUFANYA MATUMIZI YENYE TIJA

indexWaziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango akiwasilisha mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 imejipanga kufanya matumizi yeneye tija kwa kuelekeza bajeti kubwa kwenye mambo muhimu hasa sekta zenye za kutoa huduma na zile zenye kuleta maendeleo ya nchi moja kwa moja.
Akiwasilisha mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango amesema mwongozo wa mpango na bajeti umezingatia mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/2017 pamoja na kuzingatia sera za uchumi na hadi sasa sera za bajeti kwa mwaka 2016/2017 zinaonesha jumla ya shilling trillion 22.9 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika kipindi hiki.
“ Kati ya mapato hayo,serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya shillingi trillion 14.1 sawa na ongezeko la asilimia 14.1 ikilinganishwa na makadirio ya mwaka 20015/2016, na kwa mapato yasisiyo ya kodi na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri ni shilling trillion 1.1.
“ katika mwaka wa fedha 2016/2017,Serikali tunatarajia kukusanya jumla ya shilling trilllioni 14.1 kutoka kwenye vyanzo vya kodi ,sawa na asilimia 13.2 ya pato la taifa hii ni sawa na ongezeko la asilimia 14 ukilinganisha na matarajio ya kukusanya jumla ya shilling trillion 12.3 kwa mwaka wa fedha 2015/2016” Alisema Mhe. Mpango.
Mhe Philip Mpango amesema mapato yote yatakusanywa na Wizara ya Fedha na Mipango, hivyo basi maafisa,Masuuli,wa Wizara,idara za serikali,Wakala,Taasisi,Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa watatakiwa kuwasilisha mapato yote yatakayokusanywa na kuwasilisha kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na yatagawiwa kulingana na bajeti iliyoidhinishwa.
\
Aidha amesema Serikali itahakikisha Mashirika ya Umma yaliyoundwa kwa lengo la kujiendesha kibiashara yanajiendesha kwa faida bila ya kutegemea ruzuku ya Serikali, na ameyataja baadhi ya mashirika hayo kuwa ni Shirika la Umeme(TANESCO),Shirika la Reli ya Tanzania Zambia (TAZARA), Shirika la Reli ya Kati (TRL), Shirika la Ndege (ATCL),Wakala wa Vipimo (WMA), Bodi ya Mazao, na mashirika mengine.
Serikali itahakikisha kuwa inahimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuelekeza matumizi kwenye maeneo yenye tija kwa manufaa ya watanzania wote.

SERIKALI IMEWATAKA WANANCHI KUYATUNZA MAENEO YENYE ARDHI OEVU.

1
Afisa Wanyamapori kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw.Sadick Lotha akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya ardhi oevu Duniani inayotarajiwa kufanyika februari 2,2016 ambapo siku hiyo itatumika kutoa elimu kwa kuwakumbusha watu kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za ardhi oevu. Kulia ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw. Lusungu Helela, kushoto ni Afisa Wanyamapori Mkuu na Mratibu Kitaifa wa Uhifadhi Ardhi Oevu Bw. Pellage Kauzeni.
2
Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw. Pellage Kauzeni akitoa wito kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya ardhi oevu kushirikiana na Serikali katika kuyatunza maeneo hayo kushoto ni Afisa Wanyamapori kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw.Sadick Lotha na kulia ni Afisa Habari wa wizara hiyo Bw. Lusungu Helela.
3
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatlia mkutano wa Wizara ya Mali Asili na Utalii uliolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu maadhimisho ya siku ya ardhioevu ambayo huzuia mmomonyoko wa udongo kwenye fukwe unaoweza kusababishwa na mawimbi ya bahari.
( Picha zote na Frank Mvungi )
………………………………………………………………………………..
Na Fatma Salum-Maelezo
Serikali imewataka wananchi wanaoishi katika maeneo yenye ardhi oevu kushiriki katika kuyatunza maeneo hayo ili waweze kunufaika na rasilimali zinazotokana na uwepo wa maeneo hayo.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar Es Salaam na Afisa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Sadiki Lotha wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Ardhi oevu husaidia upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu, mimea na wanyama hivyo vyanzo vyake havina budi kulindwa kwa kuepuka shughuli zinazopelekea kuathiri vyanzo hivyo.” Alisema Bw. Lotha.
Akizitaja baadhi ya shughuli zinazoathiri ardh ioevu Bw. Lotha alisema ni ufugaji holela, ujenzi kwenye vyanzo vya maji, kilimo na ukataji wa miti ovyo.
Naye Mratibu wa Kitaifa wa Uhifadhi wa ardhi oevu Bw. Pellage Kauzeni alisema kuwa uharibifu wa ardhi oevu hupelekea athari katika sekta ya uvuvi, utalii, kilimo cha umwagiliaji na ufugaji hivyo kuharibu bioanwai, uchumi, shughuli za kijamii na kiikolojia.
Aidha Bw. Kauzeni alisema Tanzania imeridhia makubaliano ya kimataifa ya mkataba wa Ramsar kuwa ndio msingi wa usimamizi na matumizi endelevu ya ardhi oevu duniani uliosainiwa na nchi wanachama mjini Ramsar nchini Iran mwaka 1971.
Siku ya Ardhi Oevu duniani itafanyika kesho tarehe 2 Februari, 2016 ikiwa na kaulimbiu “MAISHA YA KIPATO ENDELEVU”.

MKUU WA WILAYA YA WETE RASHID HADID AMEWATAKA WALIMU WAKUU KUSIMAMIA UPATIKANAJI WA HATI MILIKI YA MAENEO YA SKULI ZAO .

weteNa Masanja Mabula –Pemba
…………………………………………
MKUU wa Wilaya ya Wete  Rashid Hadid Rashid amewataka walimu wakuu katika wilaya hiyo , kusimamia upatikanaji wa hati miliki ya maeneo ya skuli zao .
Amesema kuwa maeneo mengi ya Skuli  ndani ya Wilaya ya Wete yanakabiliwa na migogoro ya ardhi inayosababishwa na kutokuwepo na hati miliki .
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na walimu Wakuu wa Wilaya hiyo kwenye ukumbi wa mikutano wa zamani wa Chuo cha uwalimu Benjamini Mkapa kwenye mkutano wa kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo  .
 ‘Kila mwalimu analojukumu la kusimamia upimaji wa maeneo ya Skuli na kisha kupatiwa hati miliki , hii itaondoa migogoro inayojitokeza kwa sasa ”alisisitiza
Amesema kwamba Serikali ya Wilaya iko tayari kushirikiana na Uongozi wa Skuli katika Wilaya hiyo kuhakikisha maeneo hayo yanapimwa na kupatiwa  hati miliki .
“Serikali ya Wilaya iko tayari wakati wowote kutoa msaada wa uoatikanaji wa hati miliki ya maeneo ya Skuli , tunashirikiana kufuatilia katika ngazi zinazohusika ”aliafahamisha.
Mapema Afisa Elimu na Mafunz ya Amali Wilaya hiyo Khamis Said Hamad amesema kwamba yapo baadhi ya maeneo ya Skuli yamepimwa lakini imekuwa ni vigumu kupatikana kwa hati miliki .
Hivyo ameiomba Serikali ya Wilaya kusaidia kupatiokana hati miliki katika Skuli hizo ambazo tayari maeneo yake yamepimwa ikiwa skuli ya Sekondari ya Pandani .
“Zipo skuli tayari maeneo yake yamepimwa lakini bado hati miliki hazijapatikana , ikiwemo Skuli ya Sekondari ya Pandani ambayo eneo lake limeshapimwa ”alifahamisha.
Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mchangamdogo Juma Said Hamad ameiomba Serikali ya Wilaya kulipa kipaumbele suala la kuyapima maeneo ya skuli .
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba asilimi 60 ya maeneo ya Skuli za Wilaya ya Wete hayana hati miliki jambo ambalo linasababisha maeneo hayo kuvamiwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na makaazi

Walemavu: Msama anajitambua

indexNa Mwandishi Wetu
………………………………………….
BAADHI ya walemavu hapa nchini  wametoa wito kwa Watanzania wengine kujitambua kuhusu Mungu na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii ikiwa ni kuelekea Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 27 jijini Mwanza.
Akizungumza jana kwa niaba ya Esperance Wetewabo ambaye ni mlemavu wa mikono na mguu, mchungaji wa Godfrey Rubanzibwa ‘Punda  wa Yesu’ alisema jamii inatakiwa kujitambua kuhusu Mungu kama alivyo Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama anavyotekeleza majukumu yake katika muziki huo.
Punda wa Yesu alisema Msama amejitambua ndio maana anashirikisha kada mbalimbali katika jamii kuelekea Tamasha la Pasaka ambalo lina mafunzo mengi kwa jamii.
Punda wa Yesu alisema katika tamasha lake Msama anashirikisha waimbaji chipukizi, walemavu na wengineo ambao wanabeba dhana ya tamasha hilo ambalo dhamira yake ni kumuimbia na kumtukuza Mungu.
“Msama anajitambua waimbaji chipukizi na viongozi wa dini mbalimbali wanaohudhuria tamasha hilo, ivyo wengine nao waige mfano huo,” alisema Punda wa Yesu.
Naye Honoratha Michael alitoa wito kwa Watanzania kujiandaa vilivyo na tamasha la Pasaka ambako pia alitoa wito kwa jamii kujitokeza kuwasaidia walemavu kama anavyofanya Msama.
Honoratha aliumia fursa hiyo kuwapa usia Watanzania wote wakiwemo walemavu kuiga mfano wa Msama ambaye anatekeleza majukumu hayo.

MALINZI AMPONGEZA MAKUNGA

makungaRais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Theophil Makunga kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) mwishoni mwa wiki.
Katika salamu hizo, Malinzi amempongeza Makunga kwa nafasi hiyo aliochaguliwa na kusema imani waliyonayo wahariri wenzake juu ya utendaji wake wa kazi ndio kumepelekea wao kumchagua kuongoza jukwa hilo.
Aidha Malinzi amewapongeza Deodatus Balile aliyechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na Neville Meena aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa jukwaa hilo na kuahidi kuwa TFF itaendelea kushirikiana nao.

TFF YAIPONGEZA RUVU SHOOTING

malinziArstShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake, Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Ruvu Shooting kwa kufanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.
Malinzi ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Ruvu Shooting, Col. Charles Mbuge, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji na kuwataka kujipanga kwa maandalizi ya nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Ruvu Shooting imekua timu ya kwanza kupanda ligi kuu msimu huu baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa na kufikisha alama 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka katika hilo la B.
Washindi wawili kutoka maundi ya A, na B wataungana na Ruvu Shooting kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao huku timu zote zikiwa zimebakiza michezo miwili miwili kabla ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza msimu huu.

TFF HAINA VITA NA ZFA

mwesiShirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limesema hakuna vita kati ya Shirikisho na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) bali mawasiliano yanaendelea kati ya TFF na vyombo husika kuhakikisha ZFA ambaye ni mwanachama mshiriki wa CAF anaendesha shughuli zake kwa mujibu wa taratibu.
Kanuni na taratibu za CAF ziko wazi kuhusu nani aongoze Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na anapatikana kwa utaratibu upi.
Kikubwa ni kuzuia ZFA isipate madhara ya kufungiwa na Chama Cha Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).

BALOZI SIMBA AWAPONGEZA WAOKOAJI AJALI YA MV KILOMBERO

1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati) pamoja na ujumbe wake, wakiingia katika lango kuu la kuingilia abiria wakati alipotembelea eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II na kushuhudia shughuli za uokoaji wa magari, utafutaji miili ya watu na uokoaji wa kivuko hicho ukiendelea. Balozi Simba alifanya ziara ya kikazi mkoani Morogoro kwa kutembelea miradi ya maendeleo ya Jeshi la Magereza mkoani humo.
2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akisalimiana na Askari wa Kikosi cha Wanamaji wa Uokoaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao wanashiriki katika shughuli za uokoaji miili ya watu waliozama baada ya kivuko cha MV Kilombero II kuzama Januari 27.
3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akiongozana na ujumbe wake kuelekea eneo la tukio ambapo kivuko cha MV Kilombero II kilizama wiki iliyopita. Kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, SACP Dkt. Kato Lugainunura.
4
Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero, Yahya Naniya (kulia), akitoa maelezo juu ya shughuli za uokoaji zinavyoendelea kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wa tatu kushoto) na ujumbe aliofuatana nao mara baada ya kufika eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II wiki iliyopita. Naibu Katibu Mkuu alikuwa mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki kwa ziara ya kikazi.
5
Wasamaria wema waliojitolea kushiriki zoezi la uokoaji katika ajali ya kivuko cha MV Kilombero II kilichotokea wiki iliyopita mkoani Morogoro, wakimuelekeza dereva wa gari la kunyanyua vitu vizito (halipo pichani), wakati wa uokoaji wa moja ya magari yaliyozama wakati wa ajali hiyo.
6
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) na ujumbe aliofuatana nao wakiangalia shughuli za uokoaji zinavyoendelea mara baada ya kivuko cha MV Kilombero kuzama huku baadhi ya vitu vikiokolewa.
7
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akiondoka eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero mara baada ya kushuhudia shughuli za uokoaji zikiendelea vizuri.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA

1
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwasili Bungeni katika kuanza kikoa cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
3
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza sala ya kuliombea Bunge kabala ya kuanza kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
4
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji akiwasilisha hoja ya Serikali kuhusu Mpango wa Maendeleo mwa mwaka mmoja katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Yussuf Massauni akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
6
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
7
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
8
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbalawa wakati kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
9
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelline Mabula akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
10
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na Waziri wa NChi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakati kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
11 12
Baadhi ya wabunge wakifatila kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION YAWAKOMBOA WANAWAKE WA ZANZIBAR KIUCHUMI

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser .
Taaasisi ya Manjano Foundation inaendesha mafunzo ya siku 5 kwa Wanawake wa mjini Zanzibar. Taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kumkomboa mwanamke aweze kujiongezea kipato na kukua kiuchumi.Katika mafunzo hayo yanayoendelea kwenye Hotel ya Mtoni Marine Zanzibar wanawake  hao watapatiwa elimu namna ya kuanzisha na kuendesha biashara. Pia watajifunza  namna ya kujiwekea akiba na kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao.
Washiri wa mafunzo hayo..
Mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza  washiriki watapewa mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendesha biashara, pia kuwapa uwezo wa kutambua nafasi yao kwenye jamii wakiwa kama wanawake na kuondoa woga wa kujihusisha na kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika biashara zao ambapo Mkufunzi wa masomo hayo ya maswala ya Biashara ni Mama Salma Salim Omar wa Zanzibar Chamber of Commarce.
  
Baadaye mtaalamu wa maswala ya urembo na matumizi ya sahihi ya vipodozi Mama Shekha Nasser atatoa ujuzi wa matumizi ya vipodozi pendwa vya LuvTouch Manjano, mfano kupamba maharusi na utunzaji wa ngozi.
Picha ya Pamoja ya Wanawake wa Zanzibar waliojitokeza kwenye Mafunzo ya Ujasiriamlai .
Mwisho wa mafunzo haya washiriki wote watakopeshwa mitaji kwa ajili ya kuanzisha na  kuendesha biashara zao. Katika hatua nyingine washiriki wa mafunzo hayo waliojitokeza kwa wingi wameishukuru Taasisi ya Manjano Foundation kwa kuwakomboa na mafunzo ya kiuchumi na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.

DAWATI LA MSAADA (HELP DESK)

TANGAZO-20001

WATUMISHI WA AFYA NCHINI WATAKIWA KUACHA KUHUJUMU DAWA ZINAZOPELEKWA KWA AJILI YA WANANCHI

Naibu Waziri maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dkt.hamisi kigwangwala akizungmza na watumishi wa Afya.
D1
Baadhi ya wafanyakazi wa bohari ya dawa(msd)kanda ya kaskazini  wakimsikiliza naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto(hayupo pichani)
D2 
Watumishi wa hospitali ya mkoa ya mount meru wakimsikiliza kwa makini dkt.hamis kigwangwala.
D4
watumishi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya naibu waziri.
(Habari na picha toka wizara ya afya)
…………………………………………………………………………………….
Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuacha kuhujumu dawa zinazopelekwa kwa ajili ya wananchi na si za biashara kama wanavyofanya
Onyo hilo yamesemwa mwishoni mwa wiki na naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,dkt.hamisi kigwangwalla wakati akiongea na wafanyakazi wa bohari ya dawa(msd)pamoja na wale wa hospitali ya mkoa ya mount meru.
Dkt. Kigwangwalla alisema serikali ya awamu ya tano yenye kaulimbiu ya “hapa kazi tu”haitawavumilia watumishi wa aina hiyo na kama wapo basi waanze kujipima kabla rungu la dola halijawafikia
Aidha,alisema suala la upatikanaji wa.dawa kwa wananchi na kwa bei nafuu ni moja ya mambo yaliyopewa kipaumbele katika serikali ya awamu ya tano
“Wananchi wanatakiwa kupata dawa sahihi,kwa bei nafuu na kwa wakati,ndo maana serikali imeamua kufungua maduka ya dawa ya ndani ya hospitali,Hii ni moja ya malengo yaliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha Malibu”
Hatahivyo aliongeza kuwa katika kudhibiti upotevu wa draws nchini,serikali imeanza kutekeleza uwekaji nembo ya GoT katika vidonge vyote”na mimi nawapa changamoto ya kuweka mkakati wa kuweka rangi Maalum ‘colour code’
Kwa dawa zote zinazokuwa.zimenunuliwa na serikali,sambamba na huo mkakati wenu wa nemo
Licha ya hivyo aliwataka wakuu wa hospitali,vituo vya afya pamoja na zahanati wasipokee dawa bila kuwepo kwa kamati ya afya ambayo ndio wawakilishi wa wananchi wa mahali husika ili kusiwepo na udanganyifu na kwenda kwenye mfumo usio rasmi pamoja na kuzibandika dawa.zilizopokelewa kwenye mbao.za matangazo
Aliitaka bohari ya dawa(msd)kukamilisha uwekaji nembo dawa zilizosalia na wawe na utaratibu wa kusimamia na kukagua kama dawa Za.serikali zimefika.hadi sasa vidonge vipatavyo 65 vimekwishawekewa nembo ya GoT.

Rais Mstaafu JK akutana na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma mara tu baada ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Afrika katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa  Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (kulia) kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika  katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
Kufuatia uteuzi huo uliotangazwa rasmi na AU jana katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika, Rais Mstaafu Kikwete leo asubuhi amekutana na Dkt. Zuma makao makuu ya AU leo na kufanya nae mazungumzo kuhusu jukumu alilokabidhiwa.
Mheshimiwa Dkt. Kikwete amemshukuru Dkt. Zuma na Wakuu wa Nchi za AU kwa imani kubwa waliyoonyesha kwake kwa kukabidhiwa jukumu hilo zito.  Amewashukuru pia wadau wa siasa nchini Libya kwa kuridhia uteuzi wake.
Naye Dkt. Zuma amemshukuru Dkt. Kikwete kwa kukubali uteuzi huo na  kuwa tayari kubeba jukumu hilo. Amemueleza kuwa Umoja wa Afrika na Afrika nzima inayo matarajio makubwa juu yake na iko nyuma yake. Amemuhakikishia kumpa kila aina ya ushirikiano atakaouhitaji kukamilisha katika kutekeleza majukumu yake.

Serikali kujenga Vyuo Vya VETA kila Wilaya

VETANaibu Waziri Elimu Wazira wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akijibu maswali kutoka kwa wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Picha na raymond Mushumbusi MAELEZO.
……………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi inatarajia kujenga Vyuo vya Ufundi (VETA) kwa kila wilaya ili kutoa fursa kwa wananchi wengi hususani vijana kupata mafunzo mbalimbali ya ufundi yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kujenga taifa.
Akijibu swali la Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Kilasike Mwambalaswa (CCM) kuhusu ujenzi wa vyuo vya VETA kwa kila Wilaya ambapo Wilaya ya Chunya ni moja kati ya Wilaya kumi za mwanzo zilizo katika mpango wa ujenzi wa vyuo hivyo wakati wa maswali na majibu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Chuo Cha VETA sio kwa wilaya ya Chunya tu bali kwa Wilaya zote nchini, tayari maandalizi ya awali ya ujenzi wa chuo cha VETA ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa stadi zinazohitajika katika vyuo hivyo.
“ Natoa wito kwa wabunge katika majimbo yao kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya zote watafute ardhi kwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivi ili hata mipango ya ujenzi ikikamilka ikute eneo lipo tayari kwa kuanza utekelezaji wake”Alisema Mhe.Manyanya.
Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshateua wataalamu elekezi watakaoshindanishwa kutayarisha andiko la jinsi ya kuifanya kazi ya kubuni majengo na kupata gharama ya kazi hiyo ili kuanza ujenzi mara moja.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipanga kutoa elimu bora ya ufundi yenye kuleta ufanisi katika maendeleo ya ufundi stadi nchini ili kuwawezesha wahitimu kupata ujuzi ulio bora kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFANYA MAZUNGMZO NA RAIS UHURU KENYATA WA KENYA AU ADDIS ABABA

MAKAMU WA RAISMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya walipokutana kwenye ukumbi wa mikutano katika Ofisi ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia, Viongozi hao wanahudhuria mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili masuala ya Usalama Barani Afrika ambapo Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.
(Picha na OMR)

No comments :

Post a Comment