Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumza na wanahabari ofisini
kwake kuhusu ugeni wa Waziri mkuu ,Majaliwa Kassim Majaliwa mkoani
Kilimanjaro.
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala ali-pozung4umza nao ofisini kwake.
……………………………………………………..
NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MRADI WA UMWAGILIAJI GEREZA LA KILIMO IDETE, MKOANI MOROGORO
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mhe. Balozi Simba Yahya
akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuwasili
gerezani hapo kwa ziara ya kikazi Januari 29, 2016 kujionea ujenzi wa
mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete lililopo Wilaya ya
Kilombero, Mkoani Morogoro(anayefuatia) ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba
Yahya(wa pili kulia) akiwa ameongozana na Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kushoto) kuelekea
katika Ukumbi wa Gereza hilo kwa ajili ya kupata taarifa kamili ya
utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kutoka kwa
Wakandarasi wa mradi na Mshauri Mwelekezi mradi(kulia) ni Katibu Tawala
wa Wilaya ya Kilombero, Bw. Yahya Sinaniya.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya
akiangalia sehemu ya banio la kutunzia maji ya mradi wa Gereza la Kilimo
Idete akiwa pamoja na msafara wa Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi(wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Kitengo cha
Manunuzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Manyama Mapesi(wa pili
kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa.
Muonekano
wa mfereji wa maji yatakayokuwa yakitumika katika mradi wa umwagiliaji
wa Gereza la Kilimo Idete, Mkoani Morogoro kama inavyoonekana katika
picha.
Mshauri
wa Mradi, Mhandisi Nzobonaliba Imani akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya(katikati)
alipotembelea mradi wa umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete lililopo
Mkoani Morogoro(kulia) ni Mkuu wa Gereza hilo, Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza, Nsajigwa Mwakenja wakiaangalia ujenzi wa mradi wa umwagiliaji
wa Gereza hilo
Wakandarasi
wa Kampuni ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa Gereza Kilimo Idete,
lililopo Mkoani Morogoro wakiendelea na ujenzi wa mifereji ya maji kama
inavyoonekana katika picha.
Wajumbe
wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakipata maelezo
ya Kitaalam kutoka kwa Mshauri Mwelekezi walipotembelea mradi huo
kujionea hatua mbalimbali za ujenzi. Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kilombero.
……………………………………………………………………….
Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Morogoro
……………………………………………………………………….
Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Morogoro
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba
Yahya amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya “Tanzania Building Works ya
Jijini, Dar es Salaam” inayojenga mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo
Idete kuukamilisha mradi huo katika muda walioongezewa ili kuwezesha
kuanza kwa shughuli za uzalishaji gerezani hapo.
Akizungumza na Wakandarasi wa Kampuni hiyo alipofanya ziara ya kikazi Gereza Idete, Balozi Yahya amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni mkombozi kwa Jeshi la Magereza kwani utawezesha uzalijashi wa chakula cha kutosha cha wafungwa waliopo magerezani pamoja na kuzalisha ziada itakayouzwa kwa Wananchi ili kuongeza Mapato Serikalini.
“Ni matarajio yangu kuwa Mkandarasi wa Mradi huu kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi na Wadau wa Jeshi la Magereza atakamilisha mradi huu kwa wakati kama alivyotuahidi hivyo kuanza mara moja shughuli za uzalishaji”. Alisisitiza Balozi Yahya.
Naye Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Lodia Mallion alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo tayari uchimbaji na ujenzi wa mifereji itakayokuwa ikipitisha maji kwenda mashambani imekwisha kukamilika.
“Mito inayotumika kama vyanzo vya maji ni mto Kilombero pamoja na mto Kiwiliwili ambapo banio linalotunza maji kwa shughuli za umwagiliaji tayari limekamilika”. Alisikika Mhandisi Mallion.
Awali Mkuu wa Gereza Idete, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja akiwasilisha taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Yahya amesema kuwa kazi ya kuandaa mradi huu ilianza rasmi mwaka 2013 ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka huu 2016 ambapo gharama za mradi huo zinakadiriwa kufikia kiasi cha Tsh. 2.5 Bilioni.
Aidha amesema kuwa chakula kitakachopatikana katika mradi huo wa Gereza Idete kitatumika kulisha wafungwa waliopo magerezani na ziada itakayopatikana itauzwa kwa Wananchi hivyo kuongeza pato la Taifa.
Gereza la Kilimo Idete lipo Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro linajishughulisha na Kilimo cha mpunga wa chakula na pia mpunga kwa ajili ya mbegu bora za Kilimo hapa nchimi. Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1983 kwa ajili ya Kilimo cha mazao mbalimbali hususani Kilimo cha mpunga.
Akizungumza na Wakandarasi wa Kampuni hiyo alipofanya ziara ya kikazi Gereza Idete, Balozi Yahya amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni mkombozi kwa Jeshi la Magereza kwani utawezesha uzalijashi wa chakula cha kutosha cha wafungwa waliopo magerezani pamoja na kuzalisha ziada itakayouzwa kwa Wananchi ili kuongeza Mapato Serikalini.
“Ni matarajio yangu kuwa Mkandarasi wa Mradi huu kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi na Wadau wa Jeshi la Magereza atakamilisha mradi huu kwa wakati kama alivyotuahidi hivyo kuanza mara moja shughuli za uzalishaji”. Alisisitiza Balozi Yahya.
Naye Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Lodia Mallion alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo tayari uchimbaji na ujenzi wa mifereji itakayokuwa ikipitisha maji kwenda mashambani imekwisha kukamilika.
“Mito inayotumika kama vyanzo vya maji ni mto Kilombero pamoja na mto Kiwiliwili ambapo banio linalotunza maji kwa shughuli za umwagiliaji tayari limekamilika”. Alisikika Mhandisi Mallion.
Awali Mkuu wa Gereza Idete, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja akiwasilisha taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Yahya amesema kuwa kazi ya kuandaa mradi huu ilianza rasmi mwaka 2013 ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka huu 2016 ambapo gharama za mradi huo zinakadiriwa kufikia kiasi cha Tsh. 2.5 Bilioni.
Aidha amesema kuwa chakula kitakachopatikana katika mradi huo wa Gereza Idete kitatumika kulisha wafungwa waliopo magerezani na ziada itakayopatikana itauzwa kwa Wananchi hivyo kuongeza pato la Taifa.
Gereza la Kilimo Idete lipo Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro linajishughulisha na Kilimo cha mpunga wa chakula na pia mpunga kwa ajili ya mbegu bora za Kilimo hapa nchimi. Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1983 kwa ajili ya Kilimo cha mazao mbalimbali hususani Kilimo cha mpunga.
MWONEKANO WA KUUDHI KATIKA LANGO KUU LA KUINGILIA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA.
Mwonekano
katika lango Kuu la Kuingilia katika Uwanja wa mpira wa CCM Kirumba
Jijini Mwanza pindi mvua inaponyesha. Ni zaidi ya Usumbufu, kero na adha
kwa wanaoingia na kutoka Uwanjani hapo pindi mvua inaponyesha.
Ni
zaidi ya Usumbufumbu kwa mashabiki wa mpira pindi mvua inaponyesha
wanapokuwa wakiingia amba kutoka Uwanjani, katika Uwanja wa CM Kirumba
Jijini Mwanza kutokana na maji kutuama katika barabara inayoingia na
kutoka katika lango Kuu la kuingilia Uwanjani hapo.
Wahusika mlione hili kama changamoto inayopaswa kutafutiwa utatuzi.
Picha na George Binagi-GB Pazzo Wa BMG.
BONDIA OMARI KIMWERI KUPANDA TENA ULINGONI FEB. 26 MWAKA HUU AUSTRALIA
BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatarajia kucheza mpambano wake mwingine feb 26 akizipiga na Michael Camellion kutoka Philippines mpambano wa raundi kumi wa ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title .
………………………………………………………………………………………………….
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
Kimweri mpaka sasa amepanda
ulingoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa
ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3
Bondia huyo mtanzania
anayefanya shughuli zake Australia amewaomba watanzania kumuombea dua
kwa ajili ya mchezo wake huo ili afanye vizuri na kushinda mchezo huo
ambapo baada ya hapo atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA.
Kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana
akishinda mchezo
huo itabadilisha maisha ya mchezaji huyo wa masumbwi na kuwa na kipato
kikubwa wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani
akianzia na mkanda wa WBA ambao ameahidiwa kucheza baada ya kushinda
mechi yake hii ya Feb. 26
Kimweri alitoa shukrani kwa
wadau wanaomsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi
ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa kwake katika
mchezo wa masumbwi, makocha hao ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka
yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila ‘Super D’
Kocha wa Tanzania Prison Remmy
Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa
pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge
Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga
Ambao wamekuwa chachu kwake
katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na
hata kama anaishi nje ya Tanzania amesema hawezi kusahau asili yake kwa
kuwa kitovu Tanzania ndipo kitovu chake kilipozikiwa.
Mwanzilishi
na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation (kushoto) na Meneja
Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi wakionekana
wenye nyuso za furaha baada ya kufunua kitambaa kwenye jiwe la msingi.
Meneja
Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi akikata utepe
kuzindua rasmi choo cha kisasa katika shule ya Msingi Msinune
kilichojengwa na Mo Dewji Foundation. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule
ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Msami Mgoto pamoja na wanafunzi wa
shule hiyo wakishuhudia tukio hilo.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.
Taasisi
ya Flaviana Matata, imekabidhi choo katika Shule ya Msingi Msinune ya
Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani kitakachosaidia wanafunzi wa shule
hiyo.
Tukio
la kukabidhi choo hicho limefanyika katika shule hiyo mapema leo na
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Bi. Flaviana
Matata ambapo ameelezea kuwa, wamekua wakiwapatia wanafunzi wa Msinune
vifaa vya shuleni tangu mwaka 2014 na mwanzoni mwa mwaka jana aliombwa
kuwa mlezi wa Shule na kuweza kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili
shule hiyo ikiwemo suala hilo la vyoo vya waalimu na wanafunzi,
madarasa pamoja na nyumba za walimu.
Flaviana
amesema baada ya kuguswa aliweza kumshirikisha Mkurugenzi Mtendaji na
Rais wa Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji, alikubali
kutoa msaada huo kupitia taasisi yake hiyo ya Mo Dewji Foundation na
kuweza kujenga choo hicho chenye matundu nane.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Shule hiyo ya Msinune, Bw. Msami Mgoto ameshukuru
taasisi ya Mo Dewji kwa msaada wa kufadhili ujenzi wa choo hicho huku
akielezea kuwa itasaidia wanafunzi zaidi ya 300 wanaosoma hapo licha ya
kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya majengo.
Naye
Mwenyekiti wa Kijiji cha Msinune, Ramadhani Mtokeni aliishukuru Taasisi
ya Mo Dewji kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Msinune huku akiomba
iendelea kuwasaidia pindi wanapokuwa na matatizo.
Kwa
upande wa mwakilishi kutoka Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi
amepongeza juhudi za Flaviana Matata za kusaidia jamii ikiwemo kukua
kwa elimu hapa nchini hivyo wataendelea kushirikiana naye bega kwa bega.
Francesca
ameongeza kuwa, Mo Dewji kupitia msaada huo, wanafunzi watakuwa katika
mazingira mazuri na safi kwa afya zao ikiwemo kusoma bila kuwa na tatizo
la awali la choo, kwa sasa na miaka ijayo choo hicho kitakuwa mkombozi
na msaada mkubwa.
WADAU WAHAMASISHWA KUWEKEZA TASNIA YA UONGEZAJI THAMANI MADINI
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe
akiangalia madini mbalimbali kupitia kifaa kinachotumika kukuza mawe ya
madini ili yaweze kuonekana vizuri ikiwemo kubaini kasoro . Kabla ya
kutunuku vyeti Wahitimu 14 wa Mafunzo ya kunga’risha na kukata madini ya
Vito, Prof. Msofe amepata fursa ya kuangalia bidhaa mbalimbali za
mapambo zilizotengenezwa na wahitimu hao ikiwemo vifaa vinavyotumika
wakati wa mafunzo. Anayemwonesha kushoto ni Mtumishi katika cha
Jimolojia Tanzania, Salome Tilumanywa (kushoto). Wengine wa kwanza kulia
ni Kaimu Mratibu wa Kituo hicho John Mushi, anayefuata ni Kamishna
Msaidizi wa Madini anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Biashara ya
Madini, Salim Salim.
Mmoja wa Walimu katika Kituo cha
Jemolojia Tanzania (TGC), Ramadhan Haizer (kushoto) akimwonesha mfano wa
mapambo ya vito ambayo Wahitimu wamepata mafunzo ya kutengeneza katika
mikato mbalimbali katika fani za Unga’rishaji na uchongaji madini ya
vito Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia
Sekta ya Madini, Profesa James (wa pili kushoto). Katikati ni Kaimu
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Ally Samaje.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James
akiangalia madini ya vito yaliyokatwa katika maumbo mbalimbali kutoka
kwa Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Unga’rishaji na Ukataji wa Madini
ya Vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).
Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya
Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito wakitumia mashine mbalimbali za
Kuchonga katika maumbo mbalimbali na kungarisha madini ya Vito.
Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya
Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito wakitumia mashine mbalimbali za
Kuchonga katika maumbo mbalimbali na kungarisha madini ya Vito.
Wahitimu wa Mafunzo ya Ukataji na
Unga’rishaji Madini ya Vito wakiwa wameshika mchoro wa umbo la Ramani
ya Tanzania ambalo lililowekwa Madini ya aina katika maumbo mbalimbali
kulingana aina za madini hayo yanavyopatikana katika maeneo mbalimbali
nchini, ambapo wamemkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Profesa James Mdoe ikiwa ni njia ya kuonesha ubunifu wao baada
ya kuhitimu mafunzo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe
(katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya
Nishati na Madini kutoka Makao Makuu na walio katika ofisi za Madini za
ARusha na Moshi na Kituo cha Jemolojia Tanzania, wakati wa Mahafali ya
Pili ya Mafunzo ya Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito.
……………………………………………………………………………………………………….
Na Asteria Muhozya, Arusha
Serikali kupitia Wizara ya
Nishati na Madini imetoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje katika
Sekta ya Madini kuwekeza katika kuanzisha Vituo vya Uongezaji Thamani
Madini ili kuendeleza fani hiyo kwa manufaa ya uchumi wa taifa.
Wito huo umetolewa leo jijini
Arusha na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe wakati wa Mahafali
ya Pili katika fani za Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito katika
Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGDC).
Profesa Mdoe amesema kuwa,
uongezaji thamani madini unalenga kuongeza fursa za ajira, kwa
Watanzania watakaofanya kazi katika vituo hivyo, ikiwemo pia kutoa fursa
za wataalamu wa sekta hiyo kujiajiri na hivyo kuongeza mapato kwa
Serikali jambo ambalo pia litasaidia kuongeza mchango wa sekta hiyo
katika Pato la Taifa.
Ameongeza kuwa, Kituo hicho kina
historia ya ya pekee katika historia ya sekta ya Madini kwa kuwa
kimekuwa kituo cha kwanza na pekee kuanzishwa hapa nchini, na kuongeza
kuwa, uwepo wake ni kielelezo sahihi cha kazi za ubunifu na uongezaji
thamani madini ya vito.
Pia amesema kuwa, kuanzishwa kwa
kituo hicho ni moja ya hatua za Serikali za kutimiza malengo yaliyomo
katika Sera ya Madini ya Mwaka 2009 yenye lengo la kuongeza mchango wa
Sekta ya Madini katika Pato la taifa na ajira kwa watanzania kupitia
uongezaji thamani madini, ikiwa pamoja na mafunzo ua Jemomojia, ukataji
na unga’rishaji wa madini ya vito , utengenezaji wa bidhaa za mapambo na
uchongaji wa vinyago vya mawe.
Aidha, Profesa Msofe ametoa wito
kwa Kampuni zinazofanya biashara ya madini ya vito na wadau wengine
kuchangia maendeleo ya Kituo hicho ili kiwe kitovu cha kutoa Wataalamu
wanaokidhi mahitaji ya tasnia ya madini ya vito nchini.
Akizungumzia zuio la mwaka 2010 la kusafirisha Tanzanite ghafi
inayozidi gramu moja nje ya nchi, amesema lengo la zuio hilo ilikuwa ni
kuhamasiaha ujenzi wa vituo , vyuo, taasisi na viwanda vya kuongeza
thamani ya madini hayo nchini na kuongeza kuwa, jambo hilo pia ndilo
lililopelekea Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kuanzisha
kituo hicho.
Awali, akisoma risala kwa niaba
ya wahitimu wa mafunzo hayo, Monica Laiton, amesema kuwa, mafunzo hayo
yamewapa ujuzi wa kukata madini ya aina tofauti ikiwemo Tanzanite
katika mikato mbalimbali na kuongeza kuwa, ujuzi huo utawawezesha
kuajiliwa au kujiajiri na kuongeza kuwa, mafunzo hayo yamedhihirisha
wazi kuwa, wanawake wanaweza kufanya kazi katika sekta hiyo tofauti na
dhana iliyokuwepo awali kwamba shughuli za sekta hiyo zinafanywa na
wanawake pekee.
Jumla ya Wahitimu 14 wamehitimu
mafunzo hayo kwa muda wa miezi sita, ambapo walipata ufadhili kupitia
Kamati inayoandaa Maonesho ya Vito ya Arusha (Arusha Gem Fair) chini
ya Mfuko wa kuendeleza Wanawake katika tasnia ya madini. Maonesho ya
Arusha huandaliwa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA)
kwa ushirikiano na Wizara ya Nashati na Madini. Mwaka huu maonesho hayo
yatafanyika jijini Arusha katika Hotel ya Mount Meru kuanzia tarehe 19-
21, Aprili, 2016.
MBWANA SAMATA ASAINI MKATABA WA MIAKA MINNE KUCHEZEA TIMU YA GENK YA LIGI KUU UBELGIJI
Mbwana Samata amewasili nchini
Ubelgiji na kusaini mkataba wa miaka minne na Club mpya ya FC Genk ili
kucheza katika ligi kuu ya nchi hiyo, Ubelgiji imekuwa moja ya nchi
zinazotoa wachezaji wakubwa ulaya na kikosi cha timu ya Taifa ya nchi
hiyo ni moja kati ya timu kali duniani.
Mbwana amesema katika ukurasa
wake wa Instagram kuwa anamshukuru Mungu kwa fursa hii na ataitumia
vyema ili kujiletea mafanikio na kuleta mafanikio kwa taifa lake pia.
Meneja wa mshambuliaji huyo, Jamal Kisongo, alisema amewasiliana na Samatta na kumweleza kwamba amefika salama na ameanza kufuata taratibu zote ili aweze kufanya kazi nchini humo.
Samatta ambaye alitwaa tuzo ya kuwa Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, alikubali kujiunga na timu ya KRC Genk na kugomea ofa zilizotolewa na klabu za Nantes na Olympique Marseille za Ufaransa
Meneja wa mshambuliaji huyo, Jamal Kisongo, alisema amewasiliana na Samatta na kumweleza kwamba amefika salama na ameanza kufuata taratibu zote ili aweze kufanya kazi nchini humo.
Samatta ambaye alitwaa tuzo ya kuwa Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, alikubali kujiunga na timu ya KRC Genk na kugomea ofa zilizotolewa na klabu za Nantes na Olympique Marseille za Ufaransa
No comments :
Post a Comment