Friday, January 29, 2016

SUMAYE AIANGUKIA SERIKALI WANANCHI KUVAMIA SHAMBA LAKE LA EKARI 33 MABWEPANDE

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye  Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya kuwasili eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kuangalia eneo la ekari 33 la Sumaye lililovamiwa na wananchi.
 WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (wa pili kulia), na mke wake mama Esther (kushoto), wakimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia) eneo la shamba lake la ekari 33 lililopo Mabwepande Manispaa ya Kinondoni lililovamiwa na wananchi walipotembea eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
 Hapa Sumaye na viongozi wengine wakitafakari jambo.
 DC Makonda akihutubia katika mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe.
 Mheshimiwa Sumaye (kushoto), akiongoza kuonesha mpaka wa shamba lake.
 Mhe. Sumaye akielezea uhalali wake wa kumiliki eneo hilo.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mpya,  Justine Chiganga (kulia), akizungumza katika mkutano huo 
 Moja ya kibanda kilichojengwa na wananchi waliovamia eneo la Mhe Sumaye.
 Baadhi ya vibanda vilivyojengwa na wananchi katika eneo la Sumaye.
 Askari Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa mchakato wa kutembelea eneo hilo lililovamiwa.
 Wananchi wa eneo la Mabwepande wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mkazi wa eneo hilo Athuman Mnubi akielezea jinsi walivyovamia eneo la Sumaye.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabwepande Abdalla Omari Kunja akizungumza katika mkutano huo.
 Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Ardhi Manispaa ya Kinondoni, Matinga Ernest akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Ardhi katika Manispaa hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Dotto Mwaibale
 
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, ameiangukia serikali na kuomba msaada baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia eneo lake la ekari 33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 
Serikali imemuahikikishia Sumaye kuwa haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge wala tajiri hivyo itahakikiha inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki mbili kwa kua imesikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo. 
 
Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wananchi wa kitongoji  cha Kimondo mtaa wa mji mpya Kata ya Mabwepande na Sumaye  Dar es Salaam leo asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro huo ambao Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali kuingilia kati ni lazima busara kutumika.
 
Alizitaka pande hizo mbili kuiachia serikali kwa wiki mbili ili kutafuta njia bora ya kumaliza tatizo hilo huku wananchi wakitakiwa kuache kuendelea na ujenzi na kugawiana maeneo katika shamba hilo.
 
“Serikali ya Rais Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa tayari kumsikiliza Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na kusikiliza wananchi ili kutenda haki tunatambua migogoro ya ardhi ilivyokuwa na athari kwa jamii hatuna mpango wa kumkandamiza tajiri wala mnyonge,”alisema.
 
Alisema katika eneo hilo anajua jinsi wananchi walivyotumia nguvu katika kuwekeza ujenzi na rasilimali zao lakini kwa sasa wasitishe shughuli hizo na kuendelea kugawana maeneo na Sumaye pia kuacha uwekezaji ili kutafuta suluhu.
 
Zipo njia nyingi tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa kuangalia iwapo mzee wetu alikiuka taratibu kweli za kumiliki ardhi kama ilivyodaiwa na wananchi hatua gani serikali tuchukue,”alisema.
 
Alisema pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali hasara kwa kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi  hao ambao hawana makazi au Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei nafuu.
 
Alizitaka pande hizo mbili kutambua umuhimu wa kulinda amani katika mgogoro huo kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia nguvu.
 
Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya utambuzi wa wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye.
 
Awali katika mkutano huo Sumaye alimueleza Makonda jinsi serikali ilivyo na kazi ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia busara zake kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.
 
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu sana hasa kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli eneo hili namiliki kihalali nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka na nilikuwa katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa kujenga Chuo Kikuu,”alisema.
 
Alisema  yeye na familia yake waliuziwa eneo hilo toka mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.
 
 Diwani wa kata hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo lilikuwa pori na Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha uhalifu ikiwemo wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu mbalimbali.
 
Alisema kutokana na hatua hiyo   walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na ushirikiano kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha maji alikataa kuwapa wananchi .
 
Suzan alisema kutokana na hasira za wananchi hao kwa kukosa huduma za kijamii kwa muda mrefu ikiwemo eneo hilo kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo cha polisi waliamua kuvamia na kujigaia maeneo. 
 
Mmoja wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri kweli hawana umiliki halali wa eneo hilo na katika hatua ya kutafuta makazi walivamia msitu huo uliotelekezwa na Sumaye.
Alisema wanaamini kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora maeneo yaliyotelekezwa  na wawekezaji watasaidiwa.
 
WAKATI huo huo Makonda alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na mchanga, wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India  Sules Waljan wanaochimba mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande.
 
Hatua hiyo imekuja baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na alipowahoji wafanyakazi na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema hawana.
 
Makonda amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill ili kutoa maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama kubwa kwa uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika vyanzo vya maji na matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni makubwa.

TIMU ZA ,MAFUNZO NA JKU ZAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO

dk1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Vifaa vya Michezo Nahodha wa Timu ya Mafunzo Mpira wa Miguu (Football) Haji Ramadhan Mwambe katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja leo,timu hiyo itashiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika kwa kupambana na Timu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) kwenye Uwanja wa Amaan tarehe 13 Februari, 2016 (katikati) Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi.Sharifa Kahamis,[Picha na Ikulu.]
dk2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Vifaa vya Michezo Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu JKU Ponsiana Malik Joseph katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja leo,timu ya JKU ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho itapambana na timu ya Gaborone United ya Botswana katika uwanja huo huo  wa Amaan Studium tarehe 14 Februari,2016.[Picha na Ikulu.)

UMOJA WA WANAWAKE TUGHE TAWI LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAKUTANA, WAJADILI UMOJA NA USHIRIKIANO JIJINI DAR ES SALAAM

ni1
Mwenyekiti wa Mfuko wa Kusaidiana wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jackline Semu (kulia meza kuu) akizungumza na wajumbe wa Umoja huo walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano uliopo ndani ya umoja wao. Katikati meza kuu ni Katibu wa Mfuko huo, Joyce Ngonyani na kushoto meza kuu ni Mweka Hazina wa mfuko huo, Christina Kaale. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
ni2
Mwenyekiti wa Mfuko wa Kusaidiana wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jackline Semu (kulia meza kuu) akizungumza na wajumbe wa Umoja huo walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano uliopo ndani ya umoja wao. Katikati meza kuu ni Katibu wa Mfuko huo, Joyce Ngonyani na kushoto meza kuu ni Mweka Hazina wa mfuko huo, Christina Kaale. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


CCM yaridhishwa na Tume ya Uchaguzi ZEC kwa kutangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi Zanzibar

WARE
Na Ally Ndota, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  kimeelezea kuridhishwa kwake na maamamuzi ya Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani.
Kimesema  maamuzi  ya kufanyika uchaguzi huo Machi 20 mwaka huu, yanaenda sambamba na matakwa ya wananchi waliokuwa wengi katika kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa mujibu wa miongozo ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu alisema kwamba CCM inaungana na vyama vingine vya kisiasa nchini vilivyobaini kaso
ro za uchaguzi mkuu uliopita kuwa na kasoro na kuunga mkono maamuzi ya ZEC kuwa ni sahihi kwani yamefuata hatua muhimu za Kikatiba.
Waride alisema msimamo wa CCM katika Mkwamo wa kisiasa uliopo Zanzibar ni kurudi katika uchaguzi wa marudio ili kila chama cha kisiasa kinachoriki katika uchaguzi uliopita kipate haki ya kungia madarakani kwa njia halali na zinazokubalika kisheria.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo  Waride alieleza kwamba maamuzi hayo ndiyo kipimo sahihi cha kuweka uzani wa ukomavu wa kisiasa na demokrasia katika mfumo wa vyama vingi kwani lazima kila chama chenye haki ya kushiriki katika uchaguzi kiridhike na hatua zote zinazofanywa mpaka kupatikana kwa mshindi anayeongoza  kwa wingi wa kura halali.
“ Tunachukua fursa hii kuwaomba wananchi wote wenye haki ya kupiga kura hasa wafuasi wa CCM pamoja na wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura  Machi 20 mwaka huu.
Tukumbuke kwamba maamuzi hayo yamefanywa na Chombo chenye Mamlaka ya kusimamia masuala yote ya Uchaguzi nchini baada ya kujiridhisha kuwa kuna kasoro zilizotokea katika uchaguzi uliofutwa na kuona kuna haja ya kila mwananchi kupata haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa njia huru, wazi na zinazokubalika kisheria”. Alifafanua Waride na kuongeza kuwa uchaguzi huo ndiyo njia mwafaka ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar.
Katibu huyo aliongeza kwamba pia wanaunga mkono msimamo wa vyama vya vyote vya kisiasa vilivyokubali kushiriki uchaguzi wa marudio pamoja ushauri wa Msajili wa Vyama vya Sisasa nchini, Francis Mtungi kwa kuvitaka vyama vyenye usajili kushiriki katika mchakato huo ili kudumisha Demokrasia na malengo na malengo ya vyama kutumia uchaguzi kushika Dola.
Akizungumzia suala la CUF kususia Uchaguzi wa marudio alisema kwamba walichofanya ni mwendelezo wa migomo na kususa kwa mipango  ya maendeleo inayofanywa na mamlaka za serikali katika kufanya mipango mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi, hivyo hakuna jipya wala athari inayoweza kuathi hali ya kisiasa Zanzibar.
Alisema kwamba upinzani wa aina hiyo hauna nia njema ya kujenga maendeleo ya nchi bali una nia malengo ya kukwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi kwa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoweka mbele tamaa ya madaraka kuliko maisha ya wananchi.
“ Kila chama kina sera zake na misimamo yake sasa wao kama wameona kususia uchaguzi wa marudio ndiyo njia ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar hiyo ni juu yao,  lakini sisi tutashiriki kikamilifu ili chama chetu kipate ridhaa ya wananchi kurudi madarakani ya kidemokrasia.
Aidha alisema  chama hicho kinaamini kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka 2015 ulikuwa na kasoro nyingi zilizosababisha uchaguzi huo kukosa sifa ya kuwa uchaguzi huru na wa haki na hatimaye kufutwa.
Kupitia taarifa hiyo Waride wamewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa mikoa minne kichama ya Unguja katika uzinduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM itakayofanyika katika  Afisi kuu ya CCM Kisiwandui, January 31 mwaka huu.
Alisema Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.

MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE LEO MJINI DODOMA

NG1
Baadhi ya wabunge wakiwasili katika ukumbi wa bunge kuhudhuria kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG2
Naibu Spika Mhe Dkt Tulia Ackson akiongoza  kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG3
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Adrew Chenge akiwakiwasilia tayari kuongoza kikao cha Bunge katika Bunge la 11 linaloendelea mjini Dodoma
NG4
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt Philip Mpango akiwasilisha hoja ya Serikali ili Bunge lijadili na kuidhinisha Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano
NG5
Naibu Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Suleiman Jafo akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG6
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG7
Waziri wa Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya ufundi Mhe.Prof Joyce Ndalichako  akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG8
Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza Naibu wake
Mhe.Annastazia Wambura walipokuwa katika kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG9
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mbunge wa Kigoma  Mjini (ACT) Mhe. Zitto Kabwe  walipokuwa katika kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma

Tanzania kuadhimisha siku ya Ukoma Duniani

UM1
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akiongea an waandishi wa habari (Hawapo Pichani) leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya ukoma duniani Kushoto ni Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt Beatrice Mutayoba.
UM2
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akitoa tamko la Wizara hiyo leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya ukoma duniani
UM3
Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt Beatrice Mutayoba akitoa ufafanuzi juu ya Ugonjwa wa ukoma na kwa Tanzania Elimu zaidi itatolewa ili kupambana na ugonjwa huu.
UM4
Mratibu wa Ukoma toka  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Dkt Deus Kamara akiafanua jambo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani
UM5
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akiangalia picha zikionesha  wagonjwa wa Ukoma kulia ni Mratibu wa Ukoma toka  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Dkt Deus Kamara akiafanua jambo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO.
…………………………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Tanzania inaungana na nchi nyingine Duniani kuazimisha siku ya Ukoma Duniani itakayoadhimishwa tarehe 29 Januari 2016 kwa kutoa elimu juu ya kujikinga na kupambana na Ukoma Tanzania na kuifanya Tanzania iweze kuondokana na  m
aambukizi mapya ya ukoma.

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akitoa tamko la Wizara hiyo leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani ikiwa ni harakati za serikali kupambana na ugonjwa huu kwa kutoa elimu kwa umma wa watanzania.
Mhe.Ummy Mwalimu amesema siku hii itawapa fursa ya kutathimini mwelekeo wa jitihada za nchi na zile za kimataifa katika kupambana na ugonjwa huu ambao  umekuwa ukiogopwa sana katika jamii yetu toka enzi na enzi hasa kutokana na ukweli kwamba unasababisha ulemavu wa kuduma.
“Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014,jumla ya wagonjwa 2,134 wa Ukoma waligunduliwa ambapo wagonjwa 271 kati ya hao ambao ni sawa na asilimia 13walikuwa na ulemavu na pia bado kuna Wilaya 17 za Tanzania bara na 2 za Tanzania Visiwani zilizogunduliwa idadi  kubwa ya wagonjwa wa Ukoma”
“ Nizitaje wilaya hizi ambazo zimekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa Ukoma kwa Tanzania Bara ni Liwale,Ruangwa,Lindi Mjini,Lindi Vijini,Masasi Vijijini,Newala,Nanyumbu,Namtumbo,Tunduru,na Nkasi. Nyingine ni Mkinga,Muheza,Korogwe,Musoma,Korogwe,Musoma Vijijini ,Chato,Shinyanga Manispaa na Rufiji na kwa Tanzania Visiwani ni Mkoa wa Mjini Magharibi na katika wilaya za kati na kusini. Alisema Mhe Mwalimu.
Aidha amesema kuwa Tanzania katika kuadhimisha siku hii Serikali inayashukuru mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa michango yao katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukoma hapa Tanzania na hivyo kuhakikisha tunakuwa na Tanzania isiyo na maambukizi mapya ya Ukoma.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 17 Duniani ambazo bado zina viwango vya juu vya ugonjwa wa Ukoma na kwa zaidi ya miaka 62, siku ya ukoma Duniani imekuwa ikiadhimishwa ulimwenguni kote kila Jumapili ya mwisho wa mwezi wa Januari.

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AWATEUA MAKAMISHNA PAUL CHAGONJA NA CLODWING MTWEVE KUWA MAKATIBU TAWALA MWANZA NA KATAVI


MTWEVE

PROFESA MBARAWA AKAGUA ATHARI ZA BARABARA MORO – DODOMA

B1
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Ntenga akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa namna maji yanavyopiga kingo za daraja la Dumila wakati Waziri huyo akikagua ujenzi wa kingo mpya zinazojengwa kudhibiti mafuriko hayo.
B2
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Leornad Chimagu (kulia),akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu athari za mafuriko katika kingo za barabara ya Gairo-Dodoma eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
B3
Muonekano wa Daraja la Dumila mkoani Morogoro lilivyo sasa kufuatia mvua zinazonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha mafuriko yanayoelekea katika Mto Mkondoa.
B4
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kingo za barabara zilizo athiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha uharibifu wa barabara katika eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
B5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akitoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma Eng. Leornad Chimagu kuhusu ujenzi wa kingo za barabara hiyo kabla hazija athiri huduma za usafirishaji.
B6
Gari likipita sehemu iliyoathirika zaidi katika eneo la Kibaigwa barabara kuu ya Gairo-Dodoma.
B7
Magari yaliyoegeshwa katika kingo za barabara yanavyochangia uharibifu wa barabara na kusababisha ajali, hili ni eneo la Kibaigwa mkoani Dododma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
………………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu kuhakikisha ukarabati wa barabara katika eneo la Kibaigwa unaanza jumapili.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo alipokuwa akikagua athari za uharibifu wa barabara zilizosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa – Dodoma na kusababisha mafuriko yanayoharibu kingo za barabara.
“Hakikisheni Jumapili kazi ya ujenzi hapa inaanza na ikamilike kwa muda mfupi ili kutoathiri huduma ya usafiri katika barabara hiyo kutokana na umuhimu wake”, alisema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amewataka TANROADS washirikiane na Kikosi cha Usalama Barabarani kudhibiti magari yanayoegeshwa katika maeneo yasiyo rasmi na hivyo kusababisha ajali na uharibifu wa barabara hususani katika maeneo ya Dumila mkoani Morogoro na Kibaigwa mkoani Dodoma.
Mapema Waziri Mbarawa alikagua ujenzi wa kingo za barabara unaoendelea katika eneo la Dumila mkoani Morogoro ambapo amemuagiza Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Ntenga kuhakikisha ujenzi huo wa kudhibiti barabara na daraja la Dumila unakamilika kabla ya Februari 15 ili kukabiliana na mafuriko wakati wa mvua za masika zinazokaribia kuanza.
“Chimbeni mchanga kwenye mto ili kuwezesha maji kupita kwa urahisi na kuondoa tishio la mafuriko yanayo athiri daraja hilo wakati wa mvua za masika”, alisisitiza Waziri Mbarawa.
Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Eng. Dorothy Ntenga amesema ili kudhibiti mafuriko katika eneo la Dumila juhudi zinaendelea kupunguza mchanga na hivyo kuwezesha kupita maji kwa urahisi.
Profesa Mbarawa alikuwa katika ziara ya kukagua athari za mafuriko katika barabara ya Morogoro-Dodoma ambapo maeneo ya Dumila na Kibaigwa yameathirika zaidi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

BAWATA waunga mkono tamko la Serikali

WMkurugenzi wa Baraza la Waganga Tanzania (BAWATA)David Wiketye akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili nchini, kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Shaka Mohamed Shaka.
Picha na Beatrice Lyimo
…………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho-Maelezo
 
Baraza la Waganga Tanzania (BAWATA) wameunga mkono tamko la Serikali la kukataza waganga wa tiba asili kujitangaza katika vyombo vya habari.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Waganga Tanzania Shaka Mohamed Shaka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili nchini.
‘’Sisi kama Baraza la Waganga Tanzania tukishirikiana na Serikali tunatoa wito kwa vyombo vya habari wasitoe matangazo ya waganga wa tiba asili kwakua jambo hili ni kosa kwa mujibu wa sheria”alisema Shaka
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza hilo David Witekye ameiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) Abdulraham Lutenga kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila kushirikiana na kamati yake tendaji wala vyama vinavyounda shirikisho hilo na kuwatetea wafanyabiashara wa tiba asili ambao wamejivika kilemba cha utabibu asili.
“kwa niaba ya BAWATA, tunaiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa SHIVYATIATA kupinga tamko la Serikali, tunaamini lile ni tamko lake binafsi na sio la shirikisho”. alisema Wiketye.
Ameongeza kuwa,wameafiki tamko la Serikali kuhusu upimaji na usajili wa dawa asili na  kupendekeza  zoezi hili kuangaliwa upya ili kuwezesha watabibu asilia kumudu gharama hizo.
Tamko hilo lilitolewa baada ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoa huduma wa tiba za  asili kutozingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali inayohusu afya ya jamii.

ZIARA YA WANAFUNZI WA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA MAKAO MAKUU YA POLISI

z1
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana .
Z2
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akimkabidhi zawadi Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana.DIGP ni mmoja wa Viongozi waliopitia katika chuo hicho.
Z3
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba na Brigedia Jenerali Minja.
Z4
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho katika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA – Januari 29, 2016.

01 Waziri  Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na wabunge wa Mkoa wa Simiyu, Ofisini kwake mjini Dodoma Januari 29, 2016.  Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa huo Erasto Mbwilo.
0302Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 29, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wanamauzo 4,760 wapewa elimu ya ujasiriamali na Tigo


Baadhi ya wanamauzo wa kanda ya pwani ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja siku ya mahafali yao ya kuhitimu mafunzo maalum ya ujasiriamali yaliyotolewa na Tigo ……………………………………………………………

TRA yasitisha upokeaji wa maombi ya nafasi za kazi.

indexISO 9001:2008 CERTIFIED
KUSITISHWA KWA MUDA UWASILISHWAJI WA MAOMBI YA KAZI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitoa tangazo la nafasi za kazi katika magazeti mbalimbali ambapo waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi kupitia tovuti ya TRA.
Kutokana na maombi ya nafasi za kazi kuingiliana na shughuli za kulipa kodi mwisho wa mwezi kupitia tovuti, TRA inasitisha kwa muda upokeaji wa maombi ya kazi kupitia tovuti hadi Jumanne tarehe mbili Februari 2016 ili kuruhusu ulipaji wa kodi uendelee bila usumbufu.
Pia TRA imeongeza muda wa kupokea maombi hadi tarehe 17 Februari 2016.
Waombaji wote wa nafasi za kazi zilizotangazwa wanaombwa kutuma maombi yao kuanzia Jumanne tarehe mbili Februari 2016.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
kituo cha huduma kwa wateja
08000780078, 0800750075, 0713800333
Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao Makuu

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MKOANI KIBAHA WAPO HATARINI KUPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA MIUNDOMBINU KUWA MIBOVU

NDIKINA VICTOR MASANGU, PWANI
…………………………………………..
SHULE ya msingi ya mkoani iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa madawati, madarasa  pamoja na miundombinu ya madarasa kuwa mibovu na vyoo kuwa na nyufa hali ambayo inatishia usalama wa maisha yao kutokana na mazingira wanayosemea ni   hatarishi na  sio rafika kwao.  
 Hali hiyo imebainika baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikio kufanya ziara ya kushitukiza katika shule  hiyo na kuweza kujionea ubovu  wa majengo hayo  wanayoyatumia katika shule hiyo kuwa ni chakavu kutokana na kutofanyiwa ukarabati kwa kipindi kirefu.
Mkuu wa shule hiyo Pregua  Mseja amekiri kuwepo kwa hali hiyo ambapo alisema   kwamba licha ya  shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya ubovu wa miundombini lakini bado inakabiliwa na uhaba wa madawati pamoja na nyumba sita vya madarasa vina vuja maji kutokana na mapaa yake kutoboka hivyo wanafunzi wananyeshewa  na mvua.
“Kwa sasa Mkuu wa Mkoa shule hii ina changamoto nyingi sana kwani licha ya ubovy wa majengo pamoja na vyoo bado mambo ya msingi yanahitajika kwa shule hii ili wanafunzi waweze kujisomea katika mazingira mazuri kwa mfano sasa kuna madasara sita ambayo yanavuja kweli wanafunzi wananyeshewa na mvua,” alisema Mseja.
Akizungumzia kuhusiana na fedha ambazo tayari wameshakwisha zipokea katika shule hiyo kutoka serikalini kwa ajili ya uendeshaji wa elimu bure alisema  kwamba  wameshapokea kiasi cha shilingi laki 437 ambazo zitatumika katika mahitaji mbali mbali ikiwemo suala la utawala michezo pamoja na mahitaji mengine ya msingi.
 Baada ya Mkuu wa Mkoa kumaliza kufanya ukaguzi katika maejengo ya utawala, madarasa ya wanafunzi pamoja na kutembelea vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi hao alitoa agizo kwa halmashauri ya mji wa Kibaha kuhakikisha wanatafuta fedha haraka  iwezekanavyo kwa ajili ya kukarabati miundombinu hiyo ili kuwatendea haki ya msingi watoto hao.
Ndikiro alisema kuwa majengo hayo yanatakiwa kufanyiwa ukarabati wa haraka na kwamba halmashauri ya mji wa Kibaha ihakikishe inatafuta fedha ambazo zitaweza kusaidia katika kukarabati miundombinu hiyo ya majengo ili watoto waweze kujisomea katika mazingira mazuri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kibaha Mauld Bundala aliunga mkono kauli ya Mkuu wa Mkoa ambapo alisema anaskitishwa sana na kuona wanafunzi wnasoma katika majengo amabyo yana nyufa kwani kunaweza kupelekea watoto hao kuangukiwa na majengo.
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kibaha Grory Diamunye ambao nao walikuwepo katika ziara hiyo alisema atalivalia njuga suala hilo na kuahidi kulishughulikia haraka sana ili wanafunzi hao waweze kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki kwao kwani kufanya hivyo kutaweza kuwafanya waongeze hata kiwango cha ufaulu.
Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 764 kwa sasa bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati, madarasa, matundu ya vyoo, uchakavu wa miundombinu ya majengo ahali mbayo inwapa wakati mgumu wanafunzi hao kusoma katika mazingira ambayo ni hatari kwa masiha yao.

Makamu wa Rais ahudhuria Hafla ya kuwapongeza Vijana wa kuhifadhi Qur’an

5
Dkt Abdallah Ghaylaan Mwakilishi wa taasisi ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-an wa Saudia akimkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mh Samia Suluhu Hassan Tunzo ya kutambua mchango wake katika Malezi wakati wa Hafla ya kuwapongeza Vijana wa jumuia ya Kuhifadhi Qur-an Tanzania waliohitimu katika  Vyuo Vikuu mbali mbali  jana tarehe 28/01/2016 kwenye hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.
3
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Cheti mwanafunzi Aziza Juma  wakati wa hafla ya  kuwapongeza Vijana wa Jumuia ya kuhifadhi Qur an yalifonyika katika Hotel ya Hyatt Regency, jijini Da es Salaam.
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan  akimkabidhi cheti Hamza Lusanga wakati wa hafla ya kuwapongeza Vijana wa  jumuia ya Kuhifadhi  Qur –an yaliyofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam jana tarehe 28/01/2016
2
   Baadhi ya Mabalozi nchini Tanzania wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania alipokuwa anahutubia kwenye Hafla ya kuwapongeza vijana wa jumuia kuhifadhi Qur an jana tarehe 28/01/2016
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mshereheshaji Sheikh Saleh wakati alipowasili kwenye Hafla ya Kuwapongeza Vijana wajumuia ya kuhifadhi Qur an jana kwenye Hotel ya Hyatt Regency

Msama aishukuru Basata

indexNa Mwandishi Wetu
…………………………….
MWENYEKITI wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka  Alex Msama amelishukuru Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa mchango wake wa kufanikisha maendeleo ya tamasa hilo na sanaa kwa ujumla.
“Tunaishukuru  Basata na tunazingatia maelekezo ya Serikali ambayo ndio muongozo wa kufanikisha maendeleo ya sanaa na wasanii pia,” alisema Msama.
Msama alisema yeye na kamati yake wanashukuru kwa kupata kibali kutoka Basata na wanazingatia maelekezo ya baraza hilo kama ilivyo sheria na taratibu zinazvyoeleza.
Msama alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo lenye mlengo wa kusaidia jamii yenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane ambao wanahitaji msaada.
Aidha Msama alisema mbali ya kuhusika na maendeleo ya jamii pia linafanikisha kuibua vipaji vya waimbaji wa muziki wa Injili ambao unafikisha ujumbe was neno la Mungu  kwa jamii.
“Tamasha la Pasaka malengo yake ni kusaidia jamii yenye uhitaji maalum pia linaibua vipaji vya waimbaji wa nyimbo za Injili ambavyo vinatakiwa kutekelezwa kupitia tamasha letu,” alisema Msama.  
Msama alimalizia kwa kueleza kauli mbiu ya Tamasha la Tamasa la Pasaka mwaka huu ni Umoja na Upendo, hudumisha amani katika taifa letu.

MGODI WA BULYANHULU WATOA ZAIDI YA MILIONI 300 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG’WALE KAMA USHURU WA HUDUMA.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akiwa na wafanyakazi wengine wa Bulyanhulu Gold Mine wakikabidhi mfano wa hundi kwa kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Nyang’wale Venance Ngeleuya ,Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Ibrahim Marwa .
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akiteta jambo na mkuu wa idara ya Mahusiano ya Jamii wa Mgodi  huo Sara Terri wakati wa hafla ya kukabidhi hundi.
Madiwani wa halmashauri ya Nyang’wale wakishuhudia makabidhiano ya hundi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyangwale Venance Ngeleuya akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza na baadhi ya viongozi na madiwani wa halmashauri ya Nyang’wale (hawapo pichani)wakati wa kukabidhi hundi kwa halmashauri hiyo.
Viongozi wa Mgodi wa Bulyanhulu  wakiwa kaika picha ya pamoja na Viongozi wa seriali pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale. …………………………………………..
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Tatu Thelathini na Nne, Laki Sita na Elfu Themanini na Sita kwa Halamashauri ya Wilaya ya Nyang’wale.
Fedha hizo ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi ya mgodi huo kwa halmashauri ambapo Bulyanhulu inalipa kwa halamashauri ya Nyang’wale kutokana na makubaliano ya mwaka jana kwamba asilimia 35 ya malipo hayo yaende kwa wilaya hiyo na asimia nyingine kwa Halamashauri ya Msalala ambayo ndiyo mwenyeji wa Mgodi wa Bulyanhulu kwa asilimia kubwa.
Akipokea hundi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mheshimiwa Ibrahim Marwa amesema, “Leo wenzetu wa Mgodi wa Bulyanhulu wamefunga safari kuja kutuletea hundi ya ushuru wa huduma kwa ajili ya halmashauri ya Nyangw’ale huo ni mwanzo mzuri, sasa tumepata chanzo kizuri cha mapato kutoka mgodi wa Bulyanhulu.”
“Lakini hiyo haitoshi tukijenga mahusiano vizuri watatusaidia zaidi, kuna eneo lao ambalo kuna wachimbaji wadogo wamevamia eneo hilo na baadhi ya viongozi wanawatetea, sasa ni lazima tuwe wa kweli kwenye mambo haya ya msingi, tunataka huku ushuru halafu huku tunataka kutetea wavamizi wa eneo lao ambalo wanalimiliki kwa leseni halali ya uchimbaji, hivi mtu akija nyumbani kwako akavamia akasingizia kwamba ana njaa ivi hiyo ni sababu.”
“Tutachukua hatua za juu ili tuwaondoe wale wachimbaji waliovamia katika kijiji cha mwasabuka wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita”
Akizungumza baada ya kukabidhi hundi, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew amesema, “Ninashukuru sana kwa ushirikiano kutoka jamii na wilaya zinazozunguka mgodi wa Bulyanhulu, nashukuru pia kuona serikali ya awamu ya nne inahamasisha hapa kazi nafikiri hilo ni jambo zuri tuendelee kushirikiana ili kwa pamoja tulete maendeleo kwa taifa zima. Ijapokuwa bei ya dhahabu imeshuka lakini mgodi wetu wa Bulyanhulu bado umejidhatiti kuhakikisha kuchangia juhudi za maendeleo ya huduma za maendeleo ya jamii kadiri itakavyowekzekana.
Malipo ya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi ya mgodi yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement – MDA) baina ya Serikali na Migodi ikiwemo wa Bulyanhulu, kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali.

MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA YAFUTA KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA TARIME VIJIJINI.

5Mahakamani kabla ya mashauri kutolewa.
6Mahakamani kabla ya mashauri kutolewa.
1Mrimi Zabloni (Katikati) ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini akiongea na wanahabari
2Wakili wa mjibu maombi Paul Kipeja akihojiwa na wanahabari.
3Wakili wa mleta maombi Costantine Mutalemwa akihojiwa na wanahabari
7Kulia ni Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara akiongea na wanahabari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
…………………………………………………………………………………
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza jana imeitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana, katika Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, iliyofunguliwa na
aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
Christopher Ryoba Kangoye.
Katika kesi hiyo, wajibu maombi walikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe.John Heche
(Chadema), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ambapo mtoa maombi alikuwa akiiomba Mahakama kutengua matokeo
ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo hilo kwa kuwa haukuwa huru na haki.
Baada ya Mahakama hiyo kupitia kwa Jaji Lameck Mlacha kusikiliza utetezi wa pande zote, iliamua
kuifuta kesi hiyo ambayo ilikuwa ni nambari nne ya mwaka 2015 kutokana na hoja
za mleta maombi kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo kutoainisha majina ya
waliokuwa wakilalamikiwa kuvuruga uchaguzi Jimboni humo.
Wakili wa mleta maombi Costantine Mutalemwa pamoja na Wakili wa mjibu maombi Paul Kipeja
aliekuwa akisaidiana na Wakili Tundu Lisu katika kesi hiyo, wameelezea kuridhika na maamuzi ya Mahakama hiyo.
Nae Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara, ameelezea kuwa na imani na
Mahakama kutokana na maamuzi iliyoyatoa katika kesi hiyo pamoja na kesi
nyingine zilizowahi kuamuliwa Mahakamani hapo na kuongeza kuwa sasa kazi imebaki moja kwa Mhe.Heche ambayo ni kuwatumikia wakazi wa Jimbo la Tarime Vijijini.
Kwa upande wake Mrimi Zabloni ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, ameelezea furaha
kwa wananchi wa jimbo hilo huku akiwasihi kuweka imani na Mahakama hapa nchini
katika kutoa maamuzi ya kesi mbalimbali.
Wananchi wengi Mahakamani hapo kutoka Jimboni Tarime Vijijini walikuwa ni wafuasi wa Chadema
na wameonyesha kuyapokea maamuzi ya mahakama hiyo kwa furaha kubwa na kwamba wao waliamua ushindi wa Heche tangu Novemba 25 mwaka jana kwenye daftari la kupigia kura.
Kesi hiyo ilisikilizwa January 19,2016 mwaka huu na kuahirishwa hadi juzi January 27,2015 kwa ajili
ya kutolewa maamuzi, lakini pia iliahirishwa hadi jana January 28,2016 ambapo maamuzi
yameweza kutolewa.

MTEJA AILALAMIKIA TANESCO CHARAMBE KWA KUCHELEWA KUMUWEKEA UMEME

Mteja Ambwene Kyoga
Dotto Mwaibale
……………………………..
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Charambe Temeke jijini Dar es Salaam limelalamikiwa na mteja wake mmoja kwa kushindwa kumfungia umeme kwa wakati licha ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo kuagiza wateja wapya kufungiwa umeme katika kipindi kifupi.
Malalamiko hayo yametolewa na mteja wa shirika hilo Ambwene Kyoga ambaye amelipa sh. 320,960 kwa ajili ya kuwekewa umeme na kupatiwa lisiti namba TDB 16841 kwa ajili ya nyumba yake iliyopo Mbagala Kuu Bucha.
Ambwene alisema sasa anaingia mwaka wa pili bado haja fungiwa umeme kwani mwaka jana mwanzoni alipeleka maombi yake ofisi za shirika hilo za Kurasini lakini alipofuatilia aliambiwa faili lake limepotea hivyo aende ofisi za Charambe ambapo alilipa fedha hizo Desemba 28 mwaka jana tangu hapo licha ya kupelekewa nyaya amekuwa akizungushwa kwa kuambiwa nguzo inayotakiwa achukulie umeme imeoza ingawa inaendelea kutumika.
“Watu wa dharura wamekwisha toa taarifa kuhusu nguzo hiyo lakini bado haijabadilishwa jambo linaloweza kuleta maafa iwapo ikianguka na kibaya zaidi wamekuwa na maneno mengi badala ya kazi sijui wanataka kujenga mazingira ya rushwa” alilalamika Kyoga.
Kyoga alisema waziri wao Mhongo anafanya kazi kwa kujituma na alimsikia katika vyombo vya habari akiagiza kuwa ndani ya wiki moja mwombaji wa umeme awe amefungiwa lakini anashangaa Tanesco Charambe jinsi wanavyofanya kazi kwa kusuasua.
Msemaji wa Tanesco ofisi za  Charambe ambaye alifahamika kwa jina moja la Mugaya alipopigiwa simu jana ili kuzungumzia suala hilo simu yake ilikuwa ikiita kwa muda mrefu bila ya kupokewa hata hivyo gazeti ili linaendelea kumtafuta.

KAMANDA WA MATUKIO BLOG YAPONGEZWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KWA COVERAGE NZURI YA UCHAGUZI MKUU 2015

 Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, ambaye pia ni Mmiliki wa Blogu ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda (kushoto) akikabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Habari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Clarence Nanyaro cheti maalumu cha kutambua mchango wa blogu hiyo namna ilivyoshiriki katika kurusha matangazo, mijadala, habari na michezo iliyoelimisha na kuhamasisha wananchi kujitokeza katika shughuli mbalimbali za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hafla hiyo ya kukabidhi vyeti kwa vyombo vya habari vilivyofanya vizuri kazi hiyo, ilifanyika Makao Makuu ya NEC Dar es Salaam leo.
Mwaikenda, alishiriki kikamilifu katika coverage ya kampeni za miezi miwili za Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli katika mikoa mbalimbali nchini.Kazi zake zilikuwa zinatumika kwenye gazeti la Jambo Leo  analofanyia kazi na kusambazwa pia kwenye blogu mbalimbali nchini.
Pia alikuwa miongoni mwa wapigapicha waliofanya coverage wakati wa kutangazwa kwa matokeo,mshindi wa urais na kuapishwa Rais Dk John Magufuli Novemba 5, 2015, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
(PICHA NA MARGARET CHAMBIRI-NEC)
 Mwaikenda akifurahia kupata cheti hicho

ATHARI ZA MVUA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Vijana wakiwa wamekaa nje baada ya nyumba wanazoishi kujaa maji maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam kufuatia mvua zilizonyesha leo.
 Kituo cha daladala za kwenda Gongolamboto cha Suwata Kariakoo kikiwa kimejaa maji hivyo  kuleta adha kwa watumiaji kufuatia mvuo hizo.
 Dimbwi la maji likiwa mbele ya jengo la Yanga.
 Daraja la Jangwani na Kituo cha mabasi ya mwendokasi kikiwa kizingirwa na maji.
 Magari yakipita kwenye dimbwi la maji barabara ya mtaa wa Lindi Ilala.
 Moja ya vibanda wanavyoishi wananchi waliobomolewa eneo la Kinondoni Mkwajuni maji yakipita katikati yake jambo ambalo ni hatari kwa watu wanaoishi ndani humo.
 Nyumba ikiwa imezingirwa na maji eneo la Mchikichini Ilala kufuatia mvua hiyo iliyonyesha leo
Vijana wakiuangalia Uwanja wa Klabu ya Yanga ulivyojaa maji.

MCHEKESHAJI KUTOKA KENYA, ERIC OMONDI AWASIJI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

MWIGIZAJI na mchekeshaji wa nchini Kenya, Eric Omondi amewasili mchana huu jijini Dar leo akiwa na kikosi kazi chake wakiwa tayari kwa ‘LIVE SHOW’ kesho katika ukumbi wa mikutano wa Marqee uliopo hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na kikosi kazi chake wakiwasili katika jengo la Alosco Tower lililopo Lumumba jijini Dar es Salaam leo.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa katika pozi na bango la GSM Media leo alipo wasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya ‘LIVE SHOW’ itakayofanyika kesho katika hoteli ya Hyatt katika ukumbi wa Marqee jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji (katikati) na Dj wa mchekeshaji huo, wakiwa katika ofisi cha GSM Media leo mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiteta jambo na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji leo jijini Dar es Salaam.
Kikosi kazi cha Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi.
Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji akiwakaribisha wanakikosi kazi wa Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi leo mara baada ya kuwasili katika ofisi za GSM Media zilizopo jengo la Alosco Tower Lumumba jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji na Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi wakiwa katika picha na kikosi kazi cha mchekeshaji huyo ambapo ‘LIVE SHOW’ itakayofanyika kesho jijini Dar es Salaam.(Picha na michuziblog)

No comments :

Post a Comment