Thursday, January 28, 2016

SERIKALI YAENDELEA KUREJESHA MALI ZILIZOPATIKANA NA UHUJUMU UCHUMI

DI1
Mkurugenzi wa upelelezi Jeshi la Polisi Kamishina Diwani Athumani akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano wa kuelezea mikakati na malengo ya Serikali katika kupamabana na kudhibiti wahalifu wa kuhujumu uchumi uliofanyika leo jijini Dar  es salaam.
DI2
Mkurugenzi wa Upelelezi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(TAKUKURU) Bw. Alex Mufungo akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano wa kuelezea mikakati na malengo ya Serikali katika kupamabana na kudhibiti wahalifu wa kuhujumu uchumi uliofanyika leo jijini Dar  es salaam pembeni yake ni Mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP Biswalo Mganga.
DI3
Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini maelezo ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Kamishina Diwani Athuman hayupo pichani wakati wa mkutano wa kuelezea mikakati na malengo ya Serikali katika kupamabana na kudhibiti wahalifu wa kuhujumu uchumi uliofanyika leo jijini Dar  es salaam.
Picha zote na Ally Daud -MAELEZO
………………………………………………………………………………………………………
NA MAGRETH KINABO NA ALLY DAUD – MAELEZO
Serikali inaendelea kusimamia urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kupitia mpango wa kupambana na uhalifu ulioanzishwa mwaka 2012 kwa kuwashtaki na kuwataifishia mali zao pindi upelelezi ukikamilika na kubainika mhalifu ana makosa hayo.
Baadhi ya watuhumiwa kadhaa wamepelewa mahakamani na kufungwa, ikiwemo mali zao kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Hayo yalisemwa na  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP) Biswalo Mganga wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ofiisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi   jijini Dar es salaam, ambapo  alisema kuwa hatua hizo zimechukuliwa mara baada ya  upelelezi wa makosa ya kuhujumu uchumi kukamilika na kumbaini mhusika.
Aidha Mganga aliongeza kwamba  mhusika  hushtakiwa na mali zake kutaifishwa kulingana na kosa lake, pia suala hili litamgusa kila mtu, wakiwemo  watumishi wa umma.
“Mhalifu wa kuhujumu uchumi wa nchi ikiwemo usafirishaji wa nyara za Serikali, uuzaji wa madawa ya kulevya na kujipatia mali kwa njia ya rushwa watatumikia adhabu ya kulipa faini, kufungwa jela na kutaifishiwa mali zake pindi atapobainika na makosa hayo” alisema  Mganga.
Alisema kufuatia mkakati huo, Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa kesi 23 ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ya hizo tatu (3) zimetolewa uamuzi na nyingine ishirini (20) ziko katika hatua ya maombi ya kupata amri ya mahakama ili ziweze kuziwa au kutaifishwa.
Alizitaja baadhi ya kesi za dawa za kulevya ambazo zimefikia ukomo na kutolewa uamuzi Januari 27, mwaka huu.
Mkoani Kilimanjaro kesi mojawapo ni Josephine Waizela, ambaye ni raia wa Kenya aliyetiwa hatiani  kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine  zenye uzito wa kilogram tatu zikiwa na thamani ya Sh. Milioni 162 na kufungwa kifungo cha maisha.
Kesi nyingine ni namba 46 ya mwaka 2014 kutoka pia mkoani Kilimanjaro ambayo ilihusisha watu watatu, mmoja kati yao ambaye ni Hamis Mbwana alitiwa hatiani kwa kukutwa na dawa za kulevya aina Heroine zenye uzito wa gram 3191.11 na thamani ya Sh. Milioni 143, watuhumiwa wengine wawili katika kesi hiyo waliachiwa huru.
Mganga alizitaja baadhi ya kesi nyingine za uhujumu uchumi ni namba 6 ya mwaka 2015, ilisikilizwa mkoani Mbeya ambayo iliwahusisha raia wanne kutoka nchini China waliotiwa hatiani kwa kosa la kukutwa meno ya vifaru 11. Raia hao ni  Song Lei , Xiao Shaodan, Chen Jianlin na HU Liang, ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 na kulipa faini ya Sh. Milioni 9,288 kwa kila mmoja.
Kesi nyingine  ya uhujumu uchumi namba 3 ya mwaka 2016 iliyomhusisha raia wa Tanzania Amani Rashid Ngaza aliyetiwa hatiani  kwa  kosa la kukutwa na meno ya tembo nane iliyosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Katavi, wilaya ya Mpanda. Mtuhumiwa huyo amefungwa kifungo cha miaka 30 na kullipa faini ya Sh. bilioni 1.2.
Katika mkutano huo, Mkurugenzi Maganga alibainisha baadhi ya mali zilizotaifishwa kutoka kwa wananchi kuwa ni magari matano aina ya Toyota Rv 4 mbili ,Suzuki, Toyota Surf , Hiace pamoja na nyumba  kutoka kwa washtakiwa mbalimbali wa makosa ya kuhujumu uchumi.
Aidha,  Mganga alitoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano bila uwoga katika kufichua mali za mafisadi ili sheria ichukue mkondo wake pamoja na kuwataka wananchi wasijihusishe kwa njia yoyote ile ili kuficha umiliki wa mali ya mtu mwingine aliyoipata kiharamu kwa nia ya kuficha uhalifu wake kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
“Kwa mujibu wa Sheria aliyeshirikikuficha mali ya mtu mwingine inayohusiana na uhalifukwa njia yoyote ile pia anaweza kushitakiwa kama aliyetenda kosa la ufisadi,” alisema.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Kamishna Diwani Athumani alisema kuwa atakayekamatwa na kosa la wizi au mali ya haramu atatumikia adhabu na mali zake kutaifishwa.
“Mhalifu akibainika na mshataka ya wizi au kujipatia mali kwa njia ya haramu atatumikia adhabu na kutaifishiwa mali zake kama vile magari, nyumba, boti, viwanja na fedha taslimu” alisema Kamishna Athumani.
Aidha, Kamishna Athumani aliongeza kuwa uzoefu wao unawaonyesha kwamba wahalifu wanatumia majina ya wake zao, waume zao, watoto wao na wakati mwingine kutumia majina ya watu ambao hawapo ili kuendelea kufaidika na mali walizozipata kwa niia za uhalifu.
“Hakuna mhalifu atakayepona katika mapambano haya pia uhalifu haulipi na hauna nafasi nchini” alisistiza Kamishina Athuman.
Mbali na hayo, Mkurugenzi wa upelelezi Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) Alex Mfungo pia alisema kuwa wameanzisha kitengo cha kutaifisha mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu ikiwemo rushwa.
Tangu mwaka 1990, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitambua utaifishaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kama kipaumbele katika mfumo wa haki jinai wa kupigana na uhalifu.  Haisadii sana katika jitihada za kupambana na uhalifu ikiwa mhalifu atapata adhabu ama ya kutozwa faini au kwenda jela ikiwa ataachiwa uhuru na kupewa fursa ya kutumia fedha au mali iliyopatikana kwa uhalifu huo.
Zaidi, fedha zilizoibwa na wanasiasa wala rushwa pamoja na wahalifu wengine, zinahitaji kutaifishwa na kuelekezwa katika maeneo muhimu yenye mahitaji.
Sheria ya Utaifishaji wa Mali Haramu ilipitishwa na Bunge mwaka 1991 ili kuendana na muelekeo wa Kimataifa pamoja na mikataba ya Kimataifa ambayo imeridhiwa na nchi yetu.

JULIAN BANZI NAIBU GAVANA MPYA BENKI KUU

BANZI

VIJANA HAWA WATOKA NA WIMBO “SIKUACHI”

waleo - sikuachi
This is Brand new Audio from Tanzanian Artist Called WALEO, Song Called “SIKUACHI” Produced by Fraga Studio:: Uprise Music.Enjoy the Good Music

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUZUNGUMZA NA WABUNGE NJE YA UKUMBI WA BUNGE

majl1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge kwenye viwanja vya Bunge jini Dodoma Januari 28, 2016. Kutoka kushoto ni Jumanne Kishimba wa Kahama, Edwin Ngonyani wa Namtumbo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Hussein Amar wa Nyangwhale, Prosper Mbene wa Morogoro Kusini na Joseph Kalanda wa Sikonge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
majl2

Matukio Bungeni katika picha bungeni Dodoma leo

mh1
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
mh2
Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akielezea juu ya ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo ya kuzama kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro.
mh3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera,Uratibu na Bunge Mhe.Jenesta Mhagama akieleza juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali mara baada ya kupata taarifa za kuzama kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro watu 30 wameokolewa katiaka ajali hiyo.
mh4
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
mh5
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akijibu maswali yahusuyo Wizara yake katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
mh6
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi(kushoto) na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi (kulia) wakifatilia shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
mh7
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akifatilia shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
mh8
Mbunge wa Ilala (CCM) Mhe. Mussa Hassan Zungu akiuliza swali katika moja ya kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma.
mh9
Baadhi ya wabunge wakifatilia moja ya kikao katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
mh10
Wabunge wa upinzani wakitoka ndani ya Bunge mara baada ya kuanza kujadili hotuba ya Rais
picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Elimu ya sheria Dar kuanza Januari 31

katanga
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa sheria wanatarajia kutoa elimu ya sheria katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga alipokuwa akisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo.
‘’Natoa wito kwa wananchi kuhudhuria maadhimisho ya siku ya sheria nchini yanayoashiria kuanza mwaka mpya wa shughuli za mahakama”Alisema Kattanga.
Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya mwaka huu ni “huduma za haki kumlenga mwananchi:wajibu wa mahakama na wadau”
Ameongeza kuwa,miongoni mwa wadau watakaoshiriki katika kutoa elimu ya sheria ni pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Taasisi ya Sheria kwa Vitendo Tanzania (Law School), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA),Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Takukuru pamoja na Polisi.
Aidha Kattanga amesema kwamba wadau hao watatoa huduma za kisheria na kimahakama kwahiyo wananchi wenye mashauri ya muda mrefu,malalamiko yoyote na mapendekezo ya uboreshaji wa utendaji kazi wa mahakama wafike na kuonana na waheshimiwa Majaji, Mahakimu,Wasajili na Watendaji wa Mahakama.
Maadhimisho hayo hufanyika nchini kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi wa pili ambapo kwa Jiji la Dar es salaam inatarajia kufanyika tarehe 31 Januari hadi Februari 3.

Serikali kuendelea kujenga barabara zaidi kwa kiwango cha lami

UJ1
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Mhe Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma. picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
……………………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali imeahidi kuendelea na ujenzi wa barabara katika maeneo tofauti nchini kwa kiwango cha
lami ili kutatua adha kubwa ya ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.
 
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge waliouliza kuhusu mpango wa serikali kuboresha barabara zilizopo na kujenga mpya ili kukabiliana na adha ya ubovu wa barabara nchini.
 
Akijibu swali la Mhe Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumve (CCM) lililohitaji  ufafanuzi wa serikali ni lini ujenzi wa barabara ya Magu-Bukwimba –Ngudu-Hungumalwa itajengwa kwa kiwango cha lami, Mhe Eng Godwin Ngonyani amesema katika  mwaka wa fedha 2014/15 na 2015/16 serikali ilitenga jumla ya shilling millioni 200 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 70 na taratibu za kumtafuta Mhandisi Mshauri zinaendelea na baada ya kukamilika kwa usanifu na kupata gharama za mradi huo, Serikali itatafuta fedha za kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
 
Aidha akijibu pia swali la Mhe Fredy Atupele Mwakibete  Mbunge wa Busokelo (CCM) aliyehitaji kujua ni lini barabara ya Katumba-Mbambo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 82 inayoanzia Katumba(RDC) kupitia Mpombo,Kandete,Isange,Lwanga, Mbambo (BDC) hadi Tukuyu (RDC) itajengwa kwa kiwango cha lami.
 
Akijibu swali hilo, Mhe. Eng Godwin Ngonyani amesema kuwa Serikali kupitia  Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, katika mwaka wa fedha 2009//10 Serikali ilianza maandalizi ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami na ambapo upembuzi yakinifu na sanifu wa kina ulikamilika na baadae Serikali iliamua kujenga kilometa 10 ambapo mwezi April,2014 Wakala wa Barabara na kampuni ya CICO ilijenga barabara hiyo kuanzia Lupaso hadi Buseji,Wilayani Busokelo.
 
Serikali kupiti Wakala wa Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika Kata, Wilaya na Mikoa mbalimbali nchini  ili kukabiliana na adha ya ubovu wa barabara ambao umesababisha watu kukosa mawasiliano baina ya maeneo.

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA BALOZI WA UTURUKI NCHINI

ak1Spika wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Yasemin Eralp aliyemtembelea ofisini kwake leo tarehe 28 Januari, 2016, Mjini Dodoma.
ak2
Spika wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai akisitiza jambo wakati akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Yasemin Eralp  aliyemtembelea ofisini kwake. Katikati ni Katibu wa Balozi huyo.
ak3
ak4
Spika wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini Yasemin Eralp aliyemtembelea ofisini kwake Mjini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Bunge)

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA BARABARA YA MPANDA – KOGA – TABORA

13
Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa, Barabara ya Mpanda – Koga – Tabora imefungwa kwa muda kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini zilizosababisha kufurika kwa mto Koga na kufanya daraja la Koga, lililopo mpakani mwa Mikoa ya Katavi na Tabora kutopitika na hivyo kukata mawasiliano ya barabara katika mikoa hiyo
Kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara kupitia daraja hilo, tunaomba wananchi kusitisha safari kwa kutumia barabara hiyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hadi hapo barabara hiyo itakapofunguliwa mara tu baada ya maji kupungua katika eneo hilo.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha 41 (1) cha Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni ya 8 (1) ya Kanuni za Usimamizi za Barabara za Mwaka 2009.
Wizara, inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote.
Imetolewa na:
Eng. Joseph Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI) 
28/01/2016

KONGAMANO LA UNESCO NA WIZARA YA ELIMU LAMALIZIKA, VIPAUMBELE VYA ESDP VYAPATIKANA

????????????????????????????????????
Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akisisitiza jambo wakati wa kongamano la kujadili vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) lililofanyika katika ukumbi wa NACTE, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Philemon Solomon wa Fullshwangweblog)
……………………………………………………………
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Kongamano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi limemalizika jana jijini Dar es Salaam baada ya kupitisha vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa miaka mitano kuanzia 2017 – 2021.
Akizungumza na Mo Dewji Blog, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha vipaumbele ambavyo vitatumika ili kuifanya elimu ya Tanzania kuwa bora na yenye manufaa kwa miaka ya mbeleni.
Alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha ili kuwapo na elimu bora nchini kunahitajika kuwa na walimu wenye sifa na ubora unaohitajika, mashuleni kutumika vitabu vya ziada na kiada, kuimarisha huduma ya ukaguzi mashuleni, watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapelekwe shuleni na kuwajengea uwezo wa stadi za kazi wahitimu ili hata wanapomaliza masomo waweze kujiajiri.
“Tumethibitisha yale maeneo muhimu ya sekta ya elimu ambayo tumegundua kwamba ili tuweze kusonga mbele lazima tuimarishe ubora wa elimu yetu kama ni walimu wasome vizuri wawe na ubora, tuwe na vitabu wanafunzi wapate maarifa kutoka kwenye vitabu, kudhibiti ubora wa elimu na watoto waende shule kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu,” alisema Tandari.
Aidha Tandari alieleza kuwa awali walikuwa wakishindwa kuwa na mipango ya aina hiyo kutokana na kutokuwepo kwa fedha lakini kwa sasa wataweza kugharamia mpango huo wa elimu kutokana na serikali kuwa tayari kusimamia mpango huo wa kuboresha elimu ya serikali.
Aliongeza kuwa wao kama Wizara ya Elimu wanaamini kuwa mfumo wa elimu kwa sasa utakwenda vizuri kutokana na kasi aliyonayo rais wa awamu ya tano, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi sekondari na kutokana na kasi yake ya utendaji kazi wanataraji utafanyika kama jinsi unavyopangwa.
2Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari akiwaelezea washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani) kuhusu Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) ambao utafanyiwa kazi kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2017 – 2021.
Naye Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema kuwa kongamano hilo limekuwa zuri kutokana na makubaliano ambayo washiriki wameyafikia katika kusaidia elimu ya Tanzania kukua kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na hiyo ni hatua ya awali ambayo wameanza nayo na hadi kufikia mwezi Mei watakuwa wameshakamilisha hatua zote zikiwepo bajeti na jinsi utekelezaji huo utakavyofanyika.
Awali Zulmira alieleza kuwa UNESCO ndiyo shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linasimamia elimu na wao ndiyo wameandaa mpango huo wa ESDP na wataendelea kusaidia kukua kwa elimu nchini na hiyo ni moja kati ya kazi wanazozifanya katika kusaidia ukuaji wa elimu na kuifanya kuwa bora katika nchi mbalimbali ambazo shirika hilo wanafanya kazi.
3Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akielezea jambo katika kongamano la kujadili vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
4Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo akizugumza kuhusu Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), Katikati ni Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari.
5Mmoja wa wanakikundi akiwaelezea wanakikundi wenzake kuhusu kipaumbele ambacho walikuwa wamechaguliwa kukijadili na baadae kuwasilisha mbele ya washiriki wote jinsi kipaumbele hicho kitakavyotumika pamoja na faida zake.
7Mkuu wa kitengo cha Ushirikiano wa Kiufundi kutoka Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kutoka Ufaransa, Anton De Grauwe akimuelekeza jambo mwana kikundi mwenzake wakati wa kongamano la kujadili vipaumbele vitakavyotumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
8Baadhi ya wanakikundi wakiwa makini kufuatilia kila jambo ambalo linaendelea katika kongamano hilo la siku mbili ili kupata vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
9
10
11 

No comments :

Post a Comment