Sunday, January 31, 2016

ONGEZEKO LA BAJETI KATIKA SEKTA YA UTALII

Katika mipango ya kukuza uchumi,  sekta ya utalii chini ya Prof Jumanne Maghembe ambaye ni Waziri mpya wa maliasili na utalii imeamua kuanza kuweka mikakati katika kuongeza bajeti ya kutosha kwa mwaka 2016,  ili kuongeza bidhaa na huduma zenye ubora kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi nchini.
Sekta ya utalii imekuwa na mpango wa kuongeza watalii wa kigeni zaidi ya Million 3 mpaka kufikia 2018, ambapo mkakati huu utaenda sambambana na ongezeko la pato la taifa kuongezeka mara mbili ya kinachopatikana kwa sasa.
kwa upande wake mdau wa masuala ya Utalii, Bw. Andrea Guzzoni, Meneja mkazi wa JovagoTanzania alifafanua kuwa sekta ya utalii imekuwa mstari wa mbele katika kukuza uchumi baada ya kilimo, hivyo kama suala hili litatiliwa mkazo basi tunasubiria Tanzania mpya katika uchumi.
Aliendelea kwa kufafanua kuwa, “Sekta hii inabidi ikabiliane na matatizo yanayoikabili katika ukusajji wa kodi, kwa namna moja au nyingine inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kama hatuta chukua hatua yeyote”.
“Hata hivyo,inabidi tuangalie maboresho katika nyanja tofauti tofauti, bado kuna wahudumu wasio na ujuzi wa kutosha, ukilinganisha na huduma ukiwa nje ya nchi na hapa ni tofauti, hivyo tujaribu kuweka mafunzo ya ziada kwa waajiriwa na waajiri ili kuongeza ufanisi katika kazi”.

MAJALIWA ATAKA WATANZANIA WAFUNGUE SPORTS ACADEMY

Kidongo-chekundu 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wafungue shule za michezo yaani Sports Academy ambazo zitalenga kukusanya wahitimu wa shule za msingi na sekondari na kuwafundisha sayansi ya michezo.
Ametoa wito huo jana mchana (Jumamosi, Januari 30, 2016) kwenye uwanja wa Jamhuri wakati akizungumza na mamia ya viongozi na wananchi mbalimbali walioshiriki mashindano ya mbio za nusu marathon (km. 21 na km. 5) zilizofanyika mjini Dodoma. Mashindano hayo yalijulikana kama “HAPA KAZI TU HALF MARATHON”.
“Michezo ni sayansi kwa hiyo tunahitaji kuwafundisha vijana wetu sayansi ya michezo na kuwapa mbinu tofauti za kufaulu kwenye mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema wapo Watanzania wachache ambao wamethubutu kufungua shule za michezo na kuwataja Filbert Bayi (shule ya Filbert bayi) na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu (shule ya Lord Baden). “Tumeona matunda ya sports academy hizo kwani zimeibua vijana ambao tayari wameshiriki michuano ya kimataifa,” alisema.
Alisema michezo ina nafasi kubwa ya kulitangaza Taifa la Tanzania na ndiyo maana Serikali imeamua kuimarisha sekta ya michezo, utamaduni, sanaa na habari.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimpongeza kijana Joseph Stanford ambaye ameamua kutembea kwa miguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kumuunga mkono Rais Dk. John Pombbe Magufuli kwa utendaji wake wa kazi.
Kijana Joseph (19) ambaye alikuwepo uwanja wa Jamhuri, alisema ametumia siku 13 tangu aanze safari hiyo ikiwa ni wastani wa km. 80 kwa siku. “Ninatembea kwa saa 12 kwa siku na ikifika jioni natafuta mahali penye mji na kupumzika,” alisema.
Joseph ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana katika shule ya sekondari ya Mtoni iliyoko Mwanza-Mabatini, amesema hivi sasa anasubiri matokeo ya mitihani yake lakini ameguswa na utendaji kazi wa Rais Magufuli ndipo akaamua kuanzisha matembezi hayo ili kumuunga mkono.
Alipoulizwa anafanyaje anapopita kwenye maeneo ya misitu mikubwa au mapori ya kutisha, Joseph alisema hajakutana na misitu mikubwa ya kutisha isipokuwa kwenye milima ya Sekenke na eneo moja kabla ya kuingia mkoa wa Dodoma.
Joseph amesema anatarajia kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam kesho kutwa (Jumanne, Februari 2, 2016) kwani anasubiri kukutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nape Nnauye hapo kesho.

MAJALIWA ATAKA WATANZANIA WAFUNGUE SPORTS ACADEMY

MAJALIWA 

IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JANUARI 31, 2016.

WAZIRI MBARAWA ATAKA MAKANDARASI KUTOA MIKATABA YA AJIRA

mba1
Mkandarasi wa SynoHydo Corporation Ltd akimkabidhi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa Km. 43.65 inaojengwa kwa kiwango cha lami
mba2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimuagiza Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International Corporation Group Ltd (hayupo pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo (wanaomsikiliza).
mba3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International Corporation Group Ltd (pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo.
mba4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiagiza kuwekwa lami juu ya Daraja la Kola Wilayani Kondoa mkoani Dodoma ili kuanza kupitika na kupunguza usumbufu wa magari wakati wa mvua. (kushoto) ni Meneja ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga (Km.88.8) Eng. Stone Cheng na (Kulia) ni Mhandisi Mshauri wa barabara hiyo.
mba5
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) kuhusu hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika barabara ya Mela-Bonga (Km. 88.8) inayojengwa kwa kiwango cha lami, (Wa pili kulia) ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Godfrey Kombe na (wa kwanza kushoto) ni Eng. Deusdedit Kakoko kutoka TANROADS makao makuu.
mba6
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya Km. 43.65 ambao ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 80.
mba7
Kazi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela yenye urefu wa Km. 99.35 ukiendelea.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
…………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewaagiza Makandarasi wa ujenzi wa barabara kutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kwa kuzingatia haki, usawa na taaluma ya mtu kama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya ajira hapa nchini ili kuwezesha kazi za ujenzi kukamilika kwa wakati.
Amesema hayo wilayani Chemba Mkoani Dodoma wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati ambao ujenzi wake umegawanywa katika sehemu tatu ambazo Dodoma-Mayamaya Km. 43.65, Mayamaya-Mela Km. 99.35 na Mela-Bonga Km. 88.8 ili kuharakisha kasi ya kukamilika kwake.
“Hakikisheni leo hii mnawapa mikataba halali kwa mujibu wa taaluma zao na inayozingatia sheria za Tanzania ili kujega uhusiano mwema wa kiutendaji na hivyo kazi zenu zitakuwa na tija na ubora unaokusudiwa”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amekagua madaraja makubwa manne katika barabara hiyo ambayo ni Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 200, Msui lenye urefu wa mita 45, Kingali lenye urefu wa mita 30, na Mela lenye urefu wa mita 30 na kuhimiza kasi ya ujenzi wa madaraja hayo kabla ya mvua za masika.
Barabara ya Dodoma-Babati ni sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini (The Great North Road) inayoanzia Cairo nchini Misri hadi Cape town Afrika Kusini.
“Barabara hii ni kiungo muhimu cha miundombinu ya barabara za Tanzania kwani inaunganisha mikoa maarufu ya kilimo ya nyanda za juu kusini, nyanda ya kati na nyanda ya kaskazini na pia ni kiungo kikuu cha kwenda nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Eng. Deusdedit Kakoko kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) makao makuu, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wamejipanga kuhakikisha barabara hiyo ujenzi wake unakamilika kwa wakati ili kufungua fursa za kiuchumi na kuunganisha kirahisi mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha.
“Mheshimiwa Waziri tutaendelea kusimamia mradi huu umalizike kwa wakati na muda uliopangwa na hatutaendelea kuvumilia wale wote wasioweza kumaliza mradi huu kwa wakati”, amesisitiza Eng. Kakoko.
Waziri Mbarawa amezungumzia umuhimu wa ubora wa barabara zinazojengwa na makandarasi wote nchini kudumu  kwa muda mrefu ili thamani ya fedha inayotumika kuwalipa iwiane na huduma inayotolewa.
Hadi sasa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya (Km. 43.65), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80 wakati barabara ya Mayamaya-Mela (Km. 99.35), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 52.2  na ujenzi wa barabara Mela-Bonga (Km. 88.8), umekamilika kwa asilimia 45.17 ambapo ujenzi wa barabara yote Dodoma-Babati unatarajiwa kukamilika baadaye mwakani.

WAZIRI MBARAWA ATAKA MAKANDARASI KUTOA MIKATABA YA AJIRA

1
Mkandarasi wa SynoHydo Corporation Ltd akimkabidhi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa Km. 43.65 inaojengwa kwa kiwango cha lami.
2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimuagiza Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International Corporation Group Ltd (hayupo pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo (wanaomsikiliza).
3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza kwa Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International Corporation Group Ltd (pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo.
4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiagiza kuwekwa lami juu ya Daraja la Kola Wilayani Kondoa mkoani Dodoma ili kuanza kupitika na kupunguza usumbufu wa magari wakati wa mvua. (kushoto) ni Meneja ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga (Km.88.8) Eng. Stone Cheng na (Kulia) ni Mhandisi Mshauri wa barabara hiyo.
5
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) kuhusu hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika barabara ya Mela-Bonga (Km. 88.8) inayojengwa kwa kiwango cha lami, (Wa pili kulia) ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Godfrey Kombe na (wa kwanza kushoto) ni Eng. Deusdedit Kakoko kutoka TANROADS makao makuu.
6
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya Km. 43.65 ambao ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 80.
7
Kazi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela yenye urefu wa Km. 99.35 ukiendelea.
……………………………………………………………….
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewaagiza Makandarasi wa ujenzi wa barabara kutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kwa kuzingatia haki, usawa na taaluma ya mtu kama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya ajira hapa nchini ili kuwezesha kazi za ujenzi kukamilika kwa wakati.
Amesema hayo wilayani Chemba Mkoani Dodoma wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati ambao ujenzi wake umegawanywa katika sehemu tatu ambazo Dodoma-Mayamaya Km. 43.65, Mayamaya-Mela Km. 99.35 na Mela-Bonga Km. 88.8 ili kuharakisha kasi ya kukamilika kwake.
“Hakikisheni leo hii mnawapa mikataba halali kwa mujibu wa taaluma zao na inayozingatia sheria za Tanzania ili kujega uhusiano mwema wa kiutendaji na hivyo kazi zenu zitakuwa na tija na ubora unaokusudiwa”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amekagua madaraja makubwa manne katika barabara hiyo ambayo ni Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 200, Msui lenye urefu wa mita 45, Kingali lenye urefu wa mita 30, na Mela lenye urefu wa mita 30 na kuhimiza kasi ya ujenzi wa madaraja hayo kabla ya mvua za masika.
Barabara ya Dodoma-Babati ni sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini (The Great North Road) inayoanzia Cairo nchini Misri hadi Cape town Afrika Kusini.
“Barabara hii ni kiungo muhimu cha miundombinu ya barabara za Tanzania kwani inaunganisha mikoa maarufu ya kilimo ya nyanda za juu kusini, nyanda ya kati na nyanda ya kaskazini na pia ni kiungo kikuu cha kwenda nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Eng. Deusdedit Kakoko kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) makao makuu, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wamejipanga kuhakikisha barabara hiyo ujenzi wake unakamilika kwa wakati ili kufungua fursa za kiuchumi na kuunganisha kirahisi mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha.
“Mheshimiwa Waziri tutaendelea kusimamia mradi huu umalizike kwa wakati na muda uliopangwa na hatutaendelea kuvumilia wale wote wasioweza kumaliza mradi huu kwa wakati”, amesisitiza Eng. Kakoko.
Waziri Mbarawa amezungumzia umuhimu wa ubora wa barabara zinazojengwa na makandarasi wote nchini kudumu kwa muda mrefu ili thamani ya fedha inayotumika kuwalipa iwiane na huduma inayotolewa.
Hadi sasa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya (Km. 43.65), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80 wakati barabara ya Mayamaya-Mela (Km. 99.35), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 52.2 na ujenzi wa barabara Mela-Bonga (Km. 88.8), umekamilika kwa asilimia 45.17 ambapo ujenzi wa barabara yote Dodoma-Babati unatarajiwa kukamilika baadaye mwakani.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO

Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu  Majaliwa.
Waziri Mkuu  akislimiana na Mstahiki meya wa  Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya .
Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali  ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara  ya  kushtukiza.
Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia  pcha za mionzi (X Ray) katika hosspitali  ya rufaa  ya Mawenzi.
Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo  wagonjwa wanahudumiwa.
Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga  mkuu wa mkoa  wa Kilimanjaro,Dkt Mtumwa  mwako.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri  mkuu  Kassim Majaliwa.
Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika mkutano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia walipokutana Ikulu ndogo mjini Moshi.
Baadhi ya Viongozi walifika Ikulu ndogo mjini Moshi kwa ajili ya kumsikiliza ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPILI YA MAWENZI

MAJALIWA
Akuta uhaba wa dawa, x-ray mbovu, theatre haifanyi kazi ipasavyo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili mkoani Kilimanjaro na kufanya ziara kushtukiza kwenye hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali ya mkoa huo.
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye mara baada ya kuwasili Ikulu ndogo ya Moshi mjini jana jioni (Jumamosi, Januari 30, 2016) alipangiwa kupokea taarifa ya mkoa huo, alimweleza Mkuu wa mkoa huo kwamba anataka kufanya ziara katika hospitali hiyo na kuwaomba radhi watendaji waliokuwa wanasubiri taarifa ya mkoa iwasilishwe.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu ameamua kufanya ziara katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali yetu ya mkoa na atakuja kupokea taarifa ya mkoa wetu tukishatoka huko,” alisema Mkuu wa mkoa huo, Bw. Amos Makalla.
Mara baada ya kuwasili hospitalini, Waziri Mkuu alielekeza apelekwe kwenye chumba cha upasuaji (theatre) huku akimuuliza maswali kadhaa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Bingileki Lwezaula.
Katika chumba cha upasuaji ilibainika kuwa kuna vyumba vitatu  vya kufanyia upasuaji lakini kinachotumika ni kimoja tu kwa sababu vingine havina dawa za kulaza wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji (anesthesia) licha ya kuwa jengo la upasuaji lina mwaka sasa tangu lilipozinduliwa Februari, 2015 na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Akiwa katika wodi ya utabibu ya wanawake, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa juu ya kukosekana kwa dawa hospitalini hapo. Afisa Muuguzi wa wodi hiyo, Bi. Anjela Mwakalile alisema wametuma maombi ya kupatiwa dawa kutoka MSD lakini bado hazijafika.
Hali hiyo ilijitokeza pia kwenye wodi ya watoto. Akizungumza na wazazi wa watoto aliowakuta wamelazwa, mama mmoja alimweleza Waziri Mkuu kwamba sera ya Taifa inasema watoto wachanga hadi walio na miaka mitano wanapaswa kupata matibabu bure, lakini wao hapo hospitalini wanalazimika kununua dawa.
Waziri Mkuu alimtaka Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako kubadili haraka mfumo wa uagizaji wa dawa baada ya kupokea maelezo ya Dk. Lwezaula kwamba wametuma maombi MSD tangu miezi miwili iliyopita lakini hadi sasa hawajaletewa dawa walizoomba.
“RMO ni kwa nini hamuwezi kuagiza dawa nyingi (bulk) kwa magonjwa ambayo mnajua yanajirudia mara kwa mara ili wagonjwa weu wasipate usumbufu? Hii ni hospitali ya mkoa na mgao wa dawa unaopaswa kuja hapa ni wa level ya mkoa? Haiwezekani mnafanya hivyo ili wagonjwa wajinunulie dawa kutoka kwenye maduka yenu?,” alihoji Waziri Mkuu.
“Hii hospitali ni kubwa kuliko idadi ya wagonjwa wanaofika kutibiwa hapa na hii ni kwa sababu wengi wao wanaishia kwenye hospitali za wilaya. Kwa hiyo mlipaswa kuwa na dawa za kutosha. Wodini nimekuta wagonjwa wachache katika wodi nilizopita, ina maana mna ahueni hapa… mnao madaktari wa kutosha, wataalamu 12, lakini ni kwa nini hakuna dawa za kutosha?” alihoji.
Wakati akitoka wodi ya watoto, kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Bakari Hussein ambaye anauguza mgonjwa wake hospitalini hapo alimweleza Waziri Mkuu kwamba dawa pekee wanayopatiwa kwenye hospitali hiyo ni paracetamol tu.
“Hapa dawa ya bure pekee unayopata ni paracetamol tu. Dawa nyingine zote unaandikiwa ukanunue maduka ya nje. Na ukizipata ni kati ya sh. 60,000/- hadi 70,000/- kwa mkupuo.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Severine Kahitwa apeleke maombi ya kupatiwa mafundi wa mashine za xray haraka iwezekanavyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kukuta mashine kubwa kwenye chumba cha mionzi cha hospitali haifanyi kazi na inayofanya kazi ni ndogo haiwezi kufanya baadhi ya vipimo.
Akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa kitengo cha Radiolojia, Dk. Ephraim Minja alisema: “Tuliambiwa spare parts zimekwama bandarini, na vifaa hivyo vikipatikana vitaweza kutatua tatizo lililopo.”
Alipoulizwa na Waziri Mkuu kabla ya mashine ya kuharibika alikuwa akihudumia wagonjwa wangapi, Dk. Minja alisema kwa wastani alikuwa akihudumia wagonjwa 60 hadi 70. “RAS fuatilia mafundi kwa Katibu Wizara ya Afya. Hii ni hospitali kubwa tena ya Serikali kwa hiyo haiwezekani wagonjwa waje hapa na kuambiwa waende kupata vipimo mtaani,” alisema.

LEO NI HEPI BESDEI YA BLOG YA VIJIMAMBO YATIMIZA MIAKA 6

 Vijimambo ilizaliwa Januari 31, 2010 na kuzinduliwa Oktoba 23, 2010 na aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar. Picha ni siku ya uzinduzi ukumbi wa Mirage  uliopo Hyattsville, Maryalnd.
Hapa Balozi Mwanaidi Maajar akiwa mgeni rasmi miaka 2 ya Vijimambo iliyofanyika Machi 31, 2012 ukumbi wa Mirage uliopo Hyattsville, Maryalnd.
 
Rais mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo iliyofanyia Julai 6, 2013 katika ukumbi wa Hampton Inn uliopo Capitol Heights. Maryland.
Mwenyekiti wa Vijimambo akiwapokea wasanii Shilole na Masanja waliokuja kunogesha sherehe ya miaka 3 ya vijimambo.
Mhe. Nyarandu (kulia) akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo iliyofanyika Septemba 13, 2016 Hotel ya Growne Plaza iliyopo Rockville, Maryland.
Wasanii Aunty Ezekiel na Cassim Mganga wakija kunogesha miaka 4 ya Vijimambo, kushoto ni NY Ebra akipata ukodak moment na wasanii hao walipotembelea New York City.
Cassim Mganga na Aunty Ezekiel wakitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York siku walipotembelea pande za New York City, kulia ni Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Tuvako Maniongi

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ASIFU MIRADI YA UFUGAJI GEREZA LA UZALISHAJI MIFUGO MTEGO WA SIMBA, KINGOLWIRA MKOANI MOROGORO

uf1
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la Mtego wa Simba, Constatus Magori akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) alipotembelea Gereza hilo Januari 30, 2016 kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa gerezani hapo mkoani Morogoro.
uf2
Kundi la ng’ombe wa maziwa wanaofugwa katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la Mtego wa Simba, Kingolwira mkoani Morogoro wakiwa malishoni kama wanavyoonekana katika picha.
uf3
Mtaalamu wa mifugo katika mradi wa ufugaji kuku wa mayai na nyama uliopo Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, lililopo Kingolwira mkoani Morogoro, Sajenti Sarah Kabunda (wapili kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) alipotembelea Gereza hilo Januari 30, 2016 kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji  zinazofanywa gerezani hapo.

Simba yaitandika timu ya African Sports ya Tanga uwanja wa Taifa

(Kwa hisani ya Saleh Jembe Blog)
MPIRA UMEKWISHAAA 
Dk 90+2, Simba sasa wanatoa shoo tu, ni pasi fupifupi

DAKIKA 3 ZA NYONGEZADk 89, Mgosi anafunga bao zuri kabisa, lakini mwamuzi anasema aliotea. Inaonekana mwamuzi wa akiba hakuwa makini

DK 87, Mgosi aliyeingia punde, anakanyagwa na beki Gereza wa African Sports, lakini mwamuzi anashindwa kutoa adhabu katika tukio hilo

Dk 84, Majegwa na Kessy wanagongeana vizuri lakini shuti la ajib linapanguliwa na kipa wa Sports
KADI Dk 80 Ally Ramadhani wa Sports analambwa kadi ya njano kutokana kucheza kindava

SUB Dk 77 Simba inamtoa Ugando na nafasi yake anachukua Said Ndemla
GOOOOOO Dk 75 Ugando anaifungia Simba bao safi kabisa baada ya Simba kufanya shambulizi la kushitukiza

Dk 73, Ally Ramadhani anapiga shuti, mpira taratibu unagonga mwamba lakini unaokolewa
Dk 70, Uganda anajaribu kuwatoka mabeki wawili wa Sports lakini mpira unashindwa kufika alivyotarajia

Dk 63, Simba wanafanya shambulizi tena lakini Sports wanakuwa makini na kuokoa
Dk 57, krosi nzuri ya Ramadhani inaokolewa na Isihaka na Simba wanaondosha hatari.
Dk 56, Bado Simba wanaonekana kuwa vizuri zaidi wakitawala mchezo katika kiungo
Dk 51, Ajibu anamlamba chenga beki mmoja ana kuachia shuti kali, kipa Zacharia Maarufu anadaka, anautema lakini anauwahi

Dk 46, Simba wanaanza kwa kasi utafikiri wanatakiwa kusawazisha lakini Sports wanaonekana pia bado wako vizuri
MAPUMZIKO
Inaonekana Simba wametawala mpira kwa 58% dhidi ya 42% ya Sports. Hivyo ni kipindi bora zaidi kwa upande wa Simba

Dk 44 hadi 45, Simba ndiyo wanaonekana kumiliki mpira zaidi na presha kubwa kwa African Sports
GOOOOOO Dk 43, Kiiza anawachambua mabeki wa African Sports na kufunga bao safi kabisa 
Dk 35 hadi 40, Simba wanendelea kumiliki mpira kwa kupiga pasi fupifupi
Dk 34, Ajib anawatoka mabeki wa Sports lakini anachelewa na mpira wake unaishia mikononi mwa kipa wa Sports
GOOOOOOO Dk 31, Kessy anafanya kazi nzuri na kufunga bao zuri kabisa la pili kwa mchezo wa leo

Dk 28 hadi 30, Simba wanaendelea kuumiliki mpira kwa pasi fupifupi huku wakipiga krosi ndefu na fupi na African Sports wanaendelea kucheza pasi ndefu
Dk 27, Simba wanagongena vizuri, Ajib anatoa pasi nzuri ya Kisigino kwa Kiiza, lakini shuti lake linapita nje ya lango

Dk 24, Kessy anawachambua walinzi wawili wa African Sports, hata hivyo mwamuzi anasema Kiiza alikuwa ameishaotea
Dk 16  hadi 19, Simba wanaonekana kuongeza mashambulizi na kuwapa presha kubwa Sports huku Kazimoto anaonekana kuwa mwiba zaidi kwa viungo wa Sports
GOOOO Dk 14, krosi nzuri kabisa ya Kessy inatua kwa Kiiza anamalizia vizuri na kuandika bao kwa Simba
Dk Dk 5 hadi 8, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja na hakuna timu iliyofanya shambulizi kali
Dk 2 hadi 4, Simba wanaendelea kutawala katika, KAzimoto, Mkude wakiendelea kugongeana vizuri na kuwapa wapinzani wao wakati mgumu

Dk 1, mpira unaanza taratibu, Simba wanaonekana kupiga pasi nyingi katikati, lakini African Sports pia wanaonyesha utulivu

No comments :

Post a Comment