Spika wa Bunge Job Ndugai
(kulia) akimwapisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mbarawa , bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu
Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia) akimwapisha Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango, bungeni mjini Dodoma Januari 26,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi
akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akijibu
swali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Wabunge wakisikiliza hoja mbalimbali bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Mawaziri wa wizara mbalimbali wakisikiliza maswali na majibu Bengeni leo.
Profesa Sospeter Muhongo Waziri
wa Nishati na Madini kulia na Dk Philip Mpango Waziri wa Fedha na
Mipango wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea bungeni
leo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde
akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akijibu maswali Bungeni mjini
Dodoma Januari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitoa hoja ya kutaka Bunge lijadili Hotuba ya Mheshimiwa Rais John
Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipofungua Bunge la Kumi na Moja
Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mbunge wa Mvomero, Murad Sadiq akichangia bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MWESIGWA AFUNGUA KOZI YA NGAZI YA JUU KWA WANAWAKE
Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine leo amefungua kozi ya
ngazi ya juu ya ukocha kwa wanawake (High Level Coaching Course)
iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na FIFA.
Akiongea na waandishi wa habari
wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo, Mwesigwa amewataka washiriki wa kozi
hiyo kuzingatia mafunzo hayo na kuitumia vyema fursa hiyo adimu
waliyoipata.
Mwesigwa amewataka washiriki
kuhakikisha kozi hiyo ya siku tano, inawasaidia na kwenda kuwa walimu wa
mpira wa miguu kwa wanawake, na kuongeza mwamko kwa wanawake wengi
kuupenda na kuucheza mpira wa miguu.
Aidha Mwesigwa, amewataka
washiriki wa kozi hiyo kuzingatia maelekezo ya mkufunzi, nidhamu ya
ndani na nje ya uwanja kwani imekua ni bahati nzuri kwao kupata nafasi
ya kushiriki kozi hiyo ya ngazi ya juu.
Naye mkufunzi wa kozi hiyo
anayetambulika na FIFA/CAF, Sunday Kayuni amesema atatumia uwezo wake
wote kuhakikisha washiriki wa kozi hiyo wanajifunza na kuelewa vizuri
mafunzo yake, ili waweze kuwa walimu wazuri watakapokwenda kuanza
kufundisha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la
Wanawake ya TFF, Amina Karuma ameishukuru TFF kwa kuendesha kozi hiyo
na kusema kupatikana waalimu wengi wa kike kutaongeza mwamko wa wanawake
kuucheza mpira wa miguu.
Jumla ya washiriki 25 wanashiriki
kozi hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao ni Fatuma Omary, Esther
Chabruma, AMina Mwinchum, Sweetie Charles, Pendo John, Berlina
Mwaipungu, Mariam Mchaina, Elizabeth Sokoni, Sophia Mkumba, Marry
Masatu, Aziza Mbwele, Fadhila Yusuph.
Wengine ni Veneranda Mbano,
Mariam Aziz, Hilda Masanche, Chichi Mwidege, Sophia Edward, Asha Rashid,
Fatuma Khatibu, Neema Sanga, Hindu Muharami, Tatu Malogo, Komba Alfred,
Veroinca Ngonyani, Judith nyatto na Ingfridy Kimaro.
AZAM, SIMBA, YANGA ZAFUZU 16
Timu za Azam FC, Simba SC, Yanga
zimeungana na timu zingine saba kufuzu kwa hatua ya 16 Bora ya michuano
ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa nne
utakaochezwa mwishoni mwa mwezi Februari, huku michezo mine ikichezwa
leo katika viwanja mbalimbali nchini.
Jumla ya michezo 10 mpaka sasa
imeshachezwa na timu kumi kujikatia tiketi ya kucheza mzunguko wa nne,
ambao utazikutanisha jumla ya timu 16 mwezi ujao kusaka timu nane
zitakazosonga mbele hatua ya nane bora (Robo Fainali).
Timu zilizofuzu hatua ya 16 bora
mpaka sasa ni Azam FC, JKT Mlale, Mwadui FC, Ndanda FC, Panone FC, Rhino
Rangers, Simba SC, Tanzania Prisons, Toto Africans na Young Africans.
Leo michezo minne itachezwa,
Mtibwa Sugar v Abajalo (Jamhuri – Morogoro), Geita Gold v Mgambo
Shooting (Nyankumbu – Geita), Lipuli FC v JKT Ruvu (Wambi – Mafinga), na
African Sports v Coastal Union (Mkwakwani – Tanga).
Bingwa wa michuano ya Kombe la
Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mwaka huu, ataiwakilisha
Tanzania mwaka 2017 kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika
(CAF-CC)
TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA KOCHA MINGANGE
Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa Kocha Mkuu wa klabu ya
Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Meja Mstaafu Abdul Mingange
kufuatia kifo cha mke wake Fatma Juma kilichotokea mwishoni mwa wiki
jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake kwenda kwa
familia ya marehemu, TFF imempa pole mme wa marehemu Meja Mingange,
ndugu jamaa, marafiki pamoja na klabu ya Mbeya City kufuatia kifo hicho.
Mazishi ya marehemu Fatma Juma yamefanyika Jumapili iliyopita katika makaburi ya Matombo mkoani Morogoro
VYAMA VYA SIASA VYAASWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA ZANZIBAR
Na mwandishi wetu
Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini Mhe.Jaji Francis Mutungi ameviasa Vyama vya Siasa kushiriki
chaguzi zinazotangazwa na tume za uchaguzi nchini ikiwemo uchaguzi wa
Machi 20, mwaka 2016 uliotangzwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Kwa mujibu wa barua
iliyotolewa kwa vyama hivyo leo na kusainiwa na Jaji Mutungi ilieleza
kwamba, kimsingi Sheria ya Vyama Vya Siasa Sura ya 258 inasisitiza
vyama vya siasa kushiriki katika chaguzi zote zinazotangazwa na tume za
uchaguzi ili kufikia malengo yake ya kushika dola.
“Katika nchi kidemokrasia na
kwa chama cha siasa kinachoamini misingi ya kidemorasia ya vyama vingi
vya siasa, hakuna njia mbadala kwa chama cha siasa kufikia malengo yake
zaidi ya kushiriki uchaguzi.
“Ni wajibu wa kila chama cha
siasa nchini kama wakala wa kukuza demokrasia, utawala wa sheria na
amani ya nchi, kuwa wa kwanza kutii matamko ya kisheria yanayotolewa na
mamlaka husika . Kama kuna chama cha siasa hakiridhiki au kimekwazwa kwa
njia moja au nyingine na suala lolote kuhusu masuala ya uchaguzi, njia
stahiki na inayonyesha ukomavu wa kisiasa si kuhamasisha kugomea
uchaguzi, bali ni vema kikafuata utaratibu uliowekwa katika sheria za
uchaguzi,” alisema Jaji Mutungi.
Aidha Msajili huyo amesema kwa
mujibu wa Sheria za Nchi bado ni suala la hiari kwa chama kushiriki
uchaguzi lakini utashi huo wa hiari unaenda sanjari na umuhimu wa kila
chama kushiriki kila uchaguzi unaotangazwa na tume ya uchaguzi.
“Hivyo ni muhimu basi kila
chama cha siasa kuelewa kuwa,uchaguzi ni kipimo cha uhai wa chama cha
siasa. Chama cha siasa kisiposhiriki uchaguzi kinaua uhai wake katika
mtazamo wa harakati za kisiasa,” alisisitiza.
Aliongeza kwamba hivi sasa,
mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na vyama vya siasa vimeimarika, hivyo
sio vyema kwa chama cha siasa kujirudisha nyuma au kujiua kisiasa kwa
kutoshiriki uchaguzi wakati kina uwezo wa kufanya hivyo.
MAJALIWA ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWANASHERIA WA BUNGE
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Masuala ya
Sheria wa Bunge, marehemu Oscar Mtenda nyumbani kwa marehemu mjini
Dodoma Januari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akiwapa pole wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa
Mshauri Mkuu wa Masuala ya Sheria wa Bunge, marehemu Oscar Mtenda
nyumbani kwa marehemu mjini Dodoma Januari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Baadhi ya waombolezaji
walioshiriki katika ibada ya kumwombea aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Masuala
ya Sheria wa Bunge, maerehemu Oscar Mtenda iliyofanyika nyumbani kwake
mjini Dodoma Januari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya waombolezaji
walioshiriki katika ibada ya kumwombea aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Masuala
ya Sheria wa Bunge, maerehemu Oscar Mtenda iliyofanyika nyumbani kwake
mjini Dodoma Januari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU ATANGAZA KIAMA KWA WALA RUSHWA HASA WATUMISHI WA UMMA
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini
(Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola akizungumza na wanahabari.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini
(Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola (kushoto), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari ofisini jijini Dar es Salaam leo asubuhi
kuhusu mikakati mbalimbali ya taasisi hiyo ya kupambana na rushwa nchini
hasa kwa watendaji wa Umma na kesi zinazochunguzwa ili watuhumiwa
wafikishwe mahakama wakati wowote baada ya kukamilika kwa uchunguzi
wake.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. Kulia ni John David wa Gazeti la Majira.
Mwendeshaji wa Mtandao wa Fullshangwe, John Bukuku (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
Broad Based InterSect Organisation yatangaza tuzo mpya za AMAN
Katibu
Mtendaji wa Broad Based Intersect Organization (BBIO) Amani Joram
Mgullo (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu
ya utambulisho wa Tuzo mpya za AMAN AWARD katika tasnia ya Muziki,
Filamu na Habari. Kushoto ni Afisa Mahusiano Balozi Gepard na kulia ni
Afisa Habari Salesi Malusa.
Afisa
Habari wa Broad Based Intersect Organization (BBIO) Salesi Malusa
(Kulia) akitoa ufanunuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna
ambavyo wananchi watashiriki kuchagua washindi wa tuzo hizo kwa
kuwapigia kura. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa (BBIO) Amani Joram.
Picha na Beatrice Lyimo
Picha na Beatrice Lyimo
…………………………………………………………….
Na Lilian Lundo-Maelezo Dar es Salaam
Taasisi isiyo ya kiserikali “Broad Based Intersect Organization” (BBIO) ambayo inaratibu uhamasishaji na uimarishaji wa mikakati ya maendeleo, yenye makao makuu mjini Dodoma imetambulisha tuzo mpya ziitwazo AMAN Awards katika tasnia za muziki, filamu na habari.
Tuzo hizo zimetambulishwa leo, jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Aman Joram Mgullo.
Mgullo alisema kuwa, tuzo hizo zimetokana na mradi uitwao “Advocacy Mission Awards Network” (AMAN) unaohusika na uhamasisha na uimarishaji wa juhudi za utekelezaji wa mikakati ya maendeleo
“Wazo la utoaji wa tuzo za AMAN limekuja baada ya Tanzania pamoja na mataifa mengine ulimwenguni kuzindua mkakati mpya wa maendeleo (the Agenda 2030 of Sustainable Development Goals) ikiwa na adhima ya kutengeneza Maisha bora na Dunia bora kwa kila mwanadamu ulimwenguni,” alisema Mgullo.
Mgullo aliongeza kwa kusema kuwa, kutokana na mikakati mingi iliyotangulia kutofanikiwa kufikia malengo yake na kufanya jamii nyingi kuendelea kuishi katika hali duni ndicho kilichopelekea taasisi ya BBIO kufanya juhudi za ushawishi na uwezeshaji kupitia wasanii na wanahabari ili mradi huo wa maendeleo ufikie malengo yake kupitia tuzo za AMAN.
Kutokana na tafiti nyingi kuthibitisha kuwa tasnia za muziki na filamu, kupitia vyombo vya habari zinauwezo mkubwa wa ushawishi na uwezeshaji kwa jamii. Hivyo kwa kuwashilikisha wasanii kutoa ujumbe wa maendeleo kwa jamii kupitia tuzo za AMAN kutaleta mabadiliko kwa jamii ya Tanzania.
Mgulla alizitaja tuzo zitakazowaniwa kuwa ni Aman Music Awards, Aman Film Awards na Aman Media Awards ndani ya kila Tuzo kutakuwa na vipengele tofauti tofauti, na wananchi watashiriki kwa kupigia kura na kuchagua msanii au mwanahabari ambaye amefikisha ujumbe wa maendeleo katika jamii.
Lengo la tuzo za AMAN ni kuhakikisha dhima ya maisha bora na dunia kwa kila mwanadamu kwa kuchochea umahiri katika kutoa, kueneza na kufikisha ujumbe wa maendeleo endelevu kupitia tasnia za muziki, filamu na habari.
Taasisi isiyo ya kiserikali “Broad Based Intersect Organization” (BBIO) ambayo inaratibu uhamasishaji na uimarishaji wa mikakati ya maendeleo, yenye makao makuu mjini Dodoma imetambulisha tuzo mpya ziitwazo AMAN Awards katika tasnia za muziki, filamu na habari.
Tuzo hizo zimetambulishwa leo, jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Aman Joram Mgullo.
Mgullo alisema kuwa, tuzo hizo zimetokana na mradi uitwao “Advocacy Mission Awards Network” (AMAN) unaohusika na uhamasisha na uimarishaji wa juhudi za utekelezaji wa mikakati ya maendeleo
“Wazo la utoaji wa tuzo za AMAN limekuja baada ya Tanzania pamoja na mataifa mengine ulimwenguni kuzindua mkakati mpya wa maendeleo (the Agenda 2030 of Sustainable Development Goals) ikiwa na adhima ya kutengeneza Maisha bora na Dunia bora kwa kila mwanadamu ulimwenguni,” alisema Mgullo.
Mgullo aliongeza kwa kusema kuwa, kutokana na mikakati mingi iliyotangulia kutofanikiwa kufikia malengo yake na kufanya jamii nyingi kuendelea kuishi katika hali duni ndicho kilichopelekea taasisi ya BBIO kufanya juhudi za ushawishi na uwezeshaji kupitia wasanii na wanahabari ili mradi huo wa maendeleo ufikie malengo yake kupitia tuzo za AMAN.
Kutokana na tafiti nyingi kuthibitisha kuwa tasnia za muziki na filamu, kupitia vyombo vya habari zinauwezo mkubwa wa ushawishi na uwezeshaji kwa jamii. Hivyo kwa kuwashilikisha wasanii kutoa ujumbe wa maendeleo kwa jamii kupitia tuzo za AMAN kutaleta mabadiliko kwa jamii ya Tanzania.
Mgulla alizitaja tuzo zitakazowaniwa kuwa ni Aman Music Awards, Aman Film Awards na Aman Media Awards ndani ya kila Tuzo kutakuwa na vipengele tofauti tofauti, na wananchi watashiriki kwa kupigia kura na kuchagua msanii au mwanahabari ambaye amefikisha ujumbe wa maendeleo katika jamii.
Lengo la tuzo za AMAN ni kuhakikisha dhima ya maisha bora na dunia kwa kila mwanadamu kwa kuchochea umahiri katika kutoa, kueneza na kufikisha ujumbe wa maendeleo endelevu kupitia tasnia za muziki, filamu na habari.
TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU MALIPO YA UMEME KWA ASKARI POLISI
Katika
gazeti la Tanzania Daima ukurasa wa 5, toleo namba 4070 la tarehe 25
Januari, 2016, lilichapisha habari yenye kichwa cha habari Polisi
“waisoma” namba. Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa askari Polisi hivi
sasa wanatakiwa kujilipia gharama za umeme.
Jeshi la Polisi nchini,
linakanusha vikali taarifa hiyo kwamba siyo sahihi. Ukweli ni kwamba
askari polisi wote makambini wanalipiwa umeme na serikali, ikiwemo wale
ambao nyumba zao zimefungiwa luku kama njia ya kuboresha huduma na
matumizi sahihi ya umeme. Baada ya askari kununua umeme hutakiwa
kuwasilisha stakabadhi ya malipo ya umeme kwa ajili ya kurudishiwa kiasi
cha fedha walichonunulia umeme kila mwisho wa mwezi.
Aidha, habari iliyochapishwa na
Tanzania Daima ililenga kupotosha umma na mwandishi wa habari hiyo
hakutafuta ufafanuzi kutoka kwenye mamlaka husika.
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la
Polisi nchini, linamtaka mhariri wa gazeti la Tanzania Daima na
waandishi wake wa habari kuwa makini na habari wanazoziandika hasusani
taarifa zinazohusu vyombo vya ulinzi na usalama ili kuepuka madhara ya
kiusalama yanayoweza kutokea kutokana na habari wanazozitoa zisizo na
usahihi.
Imetolewa na:-
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu.
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu.
Basata: Tamasha la Pasaka liwe njia ya jamii
……………………………….
BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza Kampuni ya Msama Promotions kwa utekelezaji wake wa majukumu yake kwa jamii.
Basata walieleza hayo baada ya kufanikisha kibali cha Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza kufanyika Machi 26-28 hapa nchini.
Kwa Mujibu wa Katibu Mtendaji
Godfrey Mungereza, Msama ameliandaa tamasha hilo kufanikisha waimbaji
wa injili kupanda jukwaa moja bila kuchagua imani kwa kuamrishana mema.
Mungereza alisema, waimbaji wa
muziki wa injili wanabadilishana uzoefu hasa na waimbaji kutoka nje ya
Tanzania ambako muziki huo unapiga hatua kimataifa.
Mungereza alisema kupitia tamasha
hilo kutambulika zaidi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania hiyo ni
ishara ya kuendelea kufahamiana zaidi.
Aidha Mungereza alisema Tamasha la
Pasaka linaiweka Tanzania katika sura ya kimataifa zaid i jambo ambalo
ni la msingi kwa serikali.
Aliongeza kuwa jamii inapata mafunzo mbalimbali kwani jamii kwani waimbaji na jamii wanaunganisha uelewa kupitia tamasha hilo.
Sambamba na hayo Mungereza alisema
Tamasha la Pasaka ni sehemu ya jamii hasa katika uwakilishaji wa pato
linalotokana na viingilio vya tamasha hilo.
TRA yawaomba wananchi kutoa ushirikiano
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
……………………………………..
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yawaomba
wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za Maafisa wanaofanya kazi
kinyume na maadili.
Akiongea na mwandishi wa habari hii leo
Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi
Richard Kayombo amesema kuwa TRA ina Idara Maalumu ijulikanayo kama
Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo inashughulika na kufuatilia
maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.
“Tunawaomba wananchi kushirikiana na Idara
ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa kuwapa taarifa juu ya maafisa wa TRA
wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi wa Umma,”alisema Kayombo.
Mkurugenzi Kayombo ameongeza kuwa wananchi wanaweza kutoa taarifa kwa kupiga simu kwa namba 0689122515 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwa simu namba 0689122516 na kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakua zimefika sehemu husika na zitafanyiwa kazi.
Aidha Kayombo amependa kuwatoa wasiwasi
wananchi kuwa namba hizo ni za siri na hakuna mwananchi atakayepata
tatizo lolote kwa kutoa taarifa za maafisa wasio na maadili.
TRA kupitia Idara yake ya Mambo ya Ndani
imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya watumishi wa TRA
wanaoenda kinyume na maadili, wameyafanyia uchunguzi na baadhi ya
watumishi wamefukuzwa na wengine kupewa adhabu kali.
MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHINA WAKISHIRIKIANA NA MADAKTARI WA ZANZIBAR WATOA HUDUMA ZA MATIBABU KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA MATEMWE UNGUJA
Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar
UBALOZI MDOGO WA INDIA ZANZIBAR WAADHIMISHA MIAKA 67 YA UHURU WA JAMHURI YA INDIA
Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
Dk Shein Ashiriki Mazishi ya Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki dua ya kuuombea
Mwili wa Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakati alipofika nyumbani kwa
marehemu fuoni michezani Unguja kutoa mkono wa pole kwa wanafamilia leo
asubuhi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimfariji Mjane wa Marehemu
Ramadhani Nyonje Panda alipofika nyumbani kwao fuoni michezani kutowa
mkono wa pole kwa wana familia, kulia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh
Khamis Haji Khamis.
WANANCHI wakiwa katika msiba wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu aliyewahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Zanzibar.
WANANCHI wakiwa katika msiba wa
marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakiwa nyumbani kwa marehemu fuoni
michezani Unguja wakisubiri taratibu za mazishi ya marehemu Ramadhani
Nyonje Pandu yaliyofanyika Kijiji kwao Jambiani Wilaya ya Kusini
Unguja..
WANANCHI wakisoma hitma ya marehe
katika msiki wa fuoni kabla ya kusaliwa kwa ajili ya marehemu
Ramadhani Nyonje Pandu yaliyofanyika Kijiji kwao Jambiani Wilaya ya
Kusini Unguja…
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi katika
kisomo cha hitma ya Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu, iliosomwa katika
msikiti wa fuoni.
WANANCHI wakiitikia dua baada ya kusomwa kwa hitma ya marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakati ikisomwa na Shekh Soraga.
WANANCHI wakiwa na jeneza likiwa na mwili wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu kwa ajili ya kusaliwa katika msikiti wa fuoni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki katika kubeba
jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu aliyewahi
kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Zanzibar na Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya CCM.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na Viongozi na Wananchi
wakishiriki katika Sala ya kumsalia marehemu Ramadhani Nyonje Pandu
iliofanyika katika msikiti wa fuoni marehemu Ramadhani Nyonje Pandu amezikwa Kijiji kwao Jambiani Wilaya ya Kusini Unguja..
(Picha na Ikulu)
DTB YAAGA MWAKA KWA STYLE YA KIPEKEE

Wafanyakazi wa Tawi la Benki ya DTB Makao Makuu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya tawi lao kupata tuzo ya Tawi Bora Tanzania 2015 kati ya matawi 24 ya benki hiyo ambapo 10 yapo Dar es Salaam na 14 mikoani. Meneja wa Tawi hilo, Shahista Karim (katikati) akiwa ameshikilia tuzo hiyo aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu (hayupo pichani) katika sherehe za kufunga mwaka zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Ledger Plaza ulioko Bahari Beach.
PITON CHINI: Wanawake wa benki ya DTB wakicheza muziki wa asili katikasherehe za kuaga mwaka katika usiku uliokuwa na kauli mbiu ya ‘Usiku wa Afrika’. Sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Ledger Plaza ulioko katika Hoteli ya BahariBeach jijini Dar es Salaam. Kati ya mambo ambayo sherehe hiyo ilisherehekea ni pamoja na kutambua mafanikio benki hiyo ilipata katika mwaka 2015. Kati ya matawi yote 24 nchini, Tawi la Masaki na lile la Makao makuu yaliibuka washindina kujizotea tuzo. DTB ina matawi 10 Jijini Dar es Salaam na 14 mikoani.



Dance ilisakatwa chapati maelezo, JUU na CHINI baadhi ya wafanyakazi wa DTB kutoka katika matawi mbalimbali ya Benki hiyo wakiwajibika ipasavyo

KWA HISANI YA IMMA MATUKIO
Watumishi wa Umma wahimizwa kuvaa beji zianazoonesha majina yao.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
………………………………………………………
………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ameagiza na kusisitiza
ofisi zote Umma kusimamia na kuhakikisha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa
mwezi Machi mwaka huu kila watumishi awe na kitambulisho (beji)
kinachoonesha jina lake.
Akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es salaam Balozi Sefue alisema hatua hiyo ya watumishi wa
umma kuvaa beji zenye majina kila wakati wanapotekeleza majukumu yao
itasaidia wananchi kuwatambua kwa majina watumishi wanaowahudumia na
kuwasaidia kulingana na mahitaji yao kwenye ofisi hizo.
Ili kutekeleza azma ya kuwahudumia
wananchi, Balozi Sefue alisema kuwa kuanzia sasa watumishi wote wa umma
wavae beji zenye majina yao iwe rahisi kwa mwananchi kumtambua
anayemhudumia na hivyo kumsifu mtumishi wa umma anayewahudumia kwa
weledi, uaminifu na kwa wakati na kumtolea taarifa yule anayefanya mambo
ya hovyo.
Zaidi ya hayo, Balozi Sefue
amewahimiza viongozi na watumishi wote katika Utumishi wa Umma
kubadilika kwa dhati kwenye utendaji na uadilifu wao na kuwahudumia
wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima.
“Rais na sisi wote tunaomsaidia
hatuoni raha kuchukua hatua dhidi ya viongozi na watumishi wengine,
tungependa kila mtu mwenyewe ajirekebishe na kutomfikisha Rais mahali
ambapo inabidi amchukulie hatua” alisema Sefue.
Mambo muhimu yanayopaswa
kuzingatiwa ni pamoja na kila kiongozi na mamlaka ya nidhamu isipate
kigugumizi kusimamia utendaji na maadili ya kazi ili kuchukua hatua za
nidhamu, lakini afanye hivyo kwa kuzingatia kwa ukamilifu sheria, kanuni
na taratibu katika Utumishi wa Umma.
Balozi Sefue amewahimza viongozi
na watumishi wa umma kuwahudumia wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na
heshima ambapo kila ofisi ya Serikali inapaswa kuwa na dawati la
kusikiliza shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kwa upande wa Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wote nchini wametakiwa kujenga uwezo wa
kushughulikia shida za wananchi kwa ukamilifu na kwa wakati.
“Kwa muundo wa Serikali yetu
hakuna sababu kwa mwananchi kufunga safari mpaka Ikulu Dar es Salaam kwa
kuamini kuwa ni Rais tu ndiye anayeweza kumaliza matatizo yake, maana
wawakilishi wa Rais wako kila pembe ya nchi yetu, ikibidi wananchi
wafike Ikulu inamaana hao wawakilishi wa Rais hawakutimiza wajibu wao”
aliongeza Balozi Sefue.
Aidha, Balozi Sefue alisema kuwa
ofisi zote za Serikali zinatakiwa kuwa na dawati la kupokea maoni ya
wananchi kuhusu huduma inayotolewa kwenye ofisi hizo na kushughulikia
haraka maeneo yote ambayo wananchi wataonesha kutoridhika na huduma
inayotolewa.








No comments :
Post a Comment