Wednesday, January 27, 2016

KONGAMANO LA UNESCO NA WIZARA YA ELIMU LAMALIZIKA, VIPAUMBELE VYA ESDP VYAPATIKANA

????????????????????????????????????
Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zalmira Rodrigues akizungumza wakati wa kufunga kongamano la siku mbili Januari 27, 2016 jijini Dar es Salaam kongamano hilo lilikuwa linajadili vipaumbele kwa miaka mitano ijayo vinavyotakiwa katika kuandaa mpango ili kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua na ubora zaidi ambapo vipaumbele vimepitishwa ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa miaka mitano kuanzia 2017 – 2021.
(HABARI PICHA-NA PHILEMON SOLOMON FULLSHANGWEBLOG)
???????????????????????????????????? 
Wadau wa elimu pamoja na mashirika ya dini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kongamano hilo kumazika.
………………………………………………………………………………….
Kongamano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) likisaidiana na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi limemalizika leo jijini Dar es Salaam baada ya kupitisha vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa miaka mitano kuanzia 2017 – 2021.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha vipaumbele ambavyo vitatumika ili kuifanya elimu ya Tanzania kuwa bora na yenye manufaa kwa miaka ya mbeleni.
Alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha ili kuwapo na elimu bora nchini kunahitajika kuwa na walimu wenye sifa na ubora unaohitajika, mashuleni kutumika vitabu vya ziada na kiada, kuimarisha huduma ya ukaguzi mashuleni, watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapelekwe shuleni na kuwajengea uwezo wa stadi za kazi wahitimu ili hata wanapomaliza masomo waweze kujiajiri.
“Tumethibitisha yale maeneo muhimu ya sekta ya elimu ambayo tumegundua kwamba ili tuweze kusonga mbele lazima tuimarishe ubora wa elimu yetu kama ni walimu wasome vizuri wawe na ubora, tuwe na vitabu wanafunzi wapate maarifa kutoka kwenye vitabu, kudhibiti ubora wa elimu na watoto waende shule kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu,” alisema Tandari.
Aidha Tandari alieleza kuwa awali walikuwa wakishindwa kuwa na mipango ya aina hiyo kutokana na kutokuwepo kwa fedha lakini kwa sasa wataweza kugharamia mpango huo wa elimu kutokana na serikali kuwa tayari kusimamia mpango huo wa kuboresha elimu ya serikali.
Aliongeza kuwa wao kama Wizara ya Elimu wanaamini kuwa mfumo wa elimu kwa sasa utakwenda vizuri kutokana na kasi aliyonayo rais wa awamu ya tano, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi sekondari na kutokana na kasi yake ya utendaji kazi wanataraji utendaji utafanyika kama jinsi unavyopangwa.
Nae Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zalmira Rodrigues alisema kuwa kongamano hilo limekuwa zuri kutokana na makubaliano ambayo washiriki wameyafikia katika kusaidia elimu ya Tanzania kukua kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na hiyo ni hatua ya awali ambayo wameanza nayo na hadi kufikia mwezi Mei watakuwa wameshakamilisha hatua zote zikiwepo bajeti na jinsi utekelezaji huo utakavyofanyika.
Awali Zalmira alieleza kuwa UNESCO ndiyo shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linasimamia elimu na wao ndiyo wameandaa mpango huo wa ESDP na wataendelea kusaidia kukua kwa elimu nchini na hiyo ni moja kati ya kazi wanazozifanya katika kusaidia ukuaji wa elimu na kuifanya kuwa bora katika nchi mbalimbali ambazo shirika hilo wanafanya kazi.

SI KWELI KWAMBA RAIS MAGUFULI KUZURU KENYA KUHUDHURIA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU JARAMOGI ODINGA NA FIDEL ODINGA

Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi Odinda na Fidel Odinga Jumamosi hii. 
Inasikitisha kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwanhabari wa Rais wa Tanzania kwa kuwa na  ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko waTanzania wenyewe. 
Haijulikani ni nini has nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni batili na ya uongo uliotukuka. Hawa watani wetu wa jadi wana lao jambo! 
Wapuuzeni. Taarifa hiyo si ya kweli.

MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA KAZI CHA BARZA LA MAWAZIRI

MAJ1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza Kkao cha Kazi cha Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa Tamisemi mjini Dodoma hivi karibuni. . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments :

Post a Comment