Monday, January 25, 2016

Kanali Mstaafu, Issa Machibya ashiriki katika uchimbaji mtaro shule ya msingi Muungano mkoani Kigoma

7Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya Katikati akichimba mtaro kwa ajili ya kupitisha maji katika shule ya msingi Muungano iliyopo Mwanga mkoani Kigoma, anayechimba naye mtaro ni Diwani wa Mwanga Kusini (CCM), Mussa Maulid akishiriki katika uboreshaji huo wa miundombinu ya shule hiyo, hivi sasa mkoa wa Kigoma una mvua nyingi.
8Diwani wa Kata ya Mwanga Kusini, Mussa Maulid (mwenye suti ya michezo)akishiriki kuweka mazingira safi katika shule ya msingi Muungano iliyoko Mwanga mkoani Kigoma sambamba na wanafunzi wa shule hiyo.
(Picha na Mpigapicha Wetu)

Mtandaowa Tigo 4G LTE kupanuka hadi Moshi

New Picture (1)Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa 4G mjini moshi pia udhamini wa Tigo katika mbio za Kili NusuMarathon ambapo mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
………………………………………
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambayo inaongoza kwa kuendesha maisha ya kidijitali
imetangaza mpango wake wakupanua huduma ya intaneti ya 4G hadi Moshi ifikapo Februari
mwakahuu. Huduma hiyo ilizinduliwa kwanza jijiniDar es Salaam mwanzoni mwa mwaka
jana na baadaye ilisambazwa kwenye mikoa ya Arusha, Tanga, Dodoma na Morogoro,
kwa ufanisi na hivyo kuufanya mtandao wa 4G kuwa mpana na wakasi nchini Tanzania.
Ikichukuliwa kama teknolojia nzuri ya hivi karibuni kwenye sekta Ya mawasiliano duniani isiyo na dosari katika kuifikia huduma ya intaneti, teknolojiaya 4G LTE inakasi takribani maratan ikilinganishwa na teknolojiaya 3G Ambayo inatumiwa na watoaji wengine wahuduma hiyo kwenye soko la Tanzania.
Akizungumza kwenye mahoajiano maalum na vyombo vya habari kwenye ofisiza Tigo mjini Moshi pempezoni
mwa uzinduzi rasmi wa mbio za kila mwaka za masafa za Kilimanjaro Marathon, Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha alisema kusambazwa kwa mtandaowa 4G kuna fanyika ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo wa kuwapatia wateja wake huduma ya hali ya juu duniani ilikuwawezesha kuendesha maisha ya kidijitali.
“Mpango wa kupanua mtandao wa Tigo wa 4G hadi Moshi kwa mara nyingine umeonesha sio tu kwamba Tigo inaongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu pamoja na ubunifu kwenye soko, balipia kujikita kwake Kuongeza kufikiwa kwa intaneti kwaWatanzania wengi kadri iwezekanavyo,”alisema Wanyancha na kubainisha kuwa kuwalengo kubwa la kampuni hiyo ya simu ni kuhakikisha huduma hiyo inaenea nchi nzima ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2016.
Akizungumziambioza Kilimanjaro Marathon ambazo Tigo ni mdhamini mwenza,Wanyancha alisema kwamba kama
kampuni ya maisha ya kidijitali aTigo imeamua Kuwaunga mkono wanamichezo wa umekwa wake hapa nchini ilikuwasaidia kufikia malengo yao ya muda mrefu katika maisha.Wanyancha alihitimisha kuwa tangu mwaka jana Tigo ilishawekeza dolamilioni 120 kwa mwaka kwenye upanuzi wa mtandao wake pamoja na kuboresha maeneo ya mitandao
ya 4G na 3G na mkongo wa mawasiliano na hali kadhalika kuongeza idadi ya kufikiwa kwa huduma kwa wateja nchi nzima.

KUMEKUCHA DODOMA HAPA KAZI TU HALF MARATHON.

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro,( KAA) Liston Methacha wakati wa uzinduzi rasmi wa mbio za Dodoma Hapa Kazi tu Half Marathoni 2016 zinzotarajia kufanyika January 30 mwaka huu mjini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa Riadha wakifuatiia mkutano wa uzinduzi wa Mbio za Dodoma Hapa kazi tu Half Marathon 2016 uliofanyika katika Hotel ya Nyumbani mjini Moshi.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza na wanahabari (hawako pichani ) wakati wa uzinduzi rasmi wa Mbio hizo.
Kocha wa timu ya taifa ya Riadha ,Francis John akiwa na wanariadha ,Alphonce Felix na Said Makula waliofuzu viwango vya kushiriki mashindano ya Olyipiki ,walipotamburishwa mbele ya wanahabari .
Raisi wa RT ,Mtaka kifanya mahojiano na Mwandishi wa habari ,Enos Masanja wa Azam TV. …………………………………..
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania(RT) limeandaa mbio fupi kwa ajili ya kuhitimisha siku 100 za rais Dk.John Pombe Magufuli kuwa Ikulu zitakazotimua vumbi jumamosi hii januari 30 mwaka  huu mjini Dodoma.
Mbio hizo zimepewa jina maalumu la Dodoma ‘hapa kazi tu’ Half Marathon ambazo zitashirikisha washiriki mbali  mbali wakiwamo waheshimiwa wabunge,mawaziri,wanafunzi,walemavu na wanariadha wakongwe nchini.
Akizindua mbio hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki zinazodhaminiwa na Kampuni ya JSM,Rais wa shirikisho hilo,Anthony Mtaka alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa mbio hizo ambazo zimeandaliwa na kuendeshwa na shirikisho hilo ni kufufua michezo hapa nchini.
Pia alisema mbio hizo zitatumika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kutimiza siku 100 tangu aingie maradakani ambazo zitakuwa februari 14 mwaka huu.
Kwa mujibu wa rais huyo wa RT,mbio hizo zimegawanywa katika makundi matatu ambako mbio za kwanza ni za kilomita 2.5 ambazo zitashirikisha wabunge,mawaziri,walemavu,wanafunzi ,wazee na watu mbalimbali.
Mbio za kilomita 5 ambazo ni za kujifurahisha zitashirikisha wakimbiaji wote na mbio za nusu marathon ambazo zitakuwa ni mbio za ushindani washindi watapata zawadi .
Akitangaza zawadi  kwa washindi,Mtaka alisema mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaumme na 
wanawake atapata zawadi  ya piki piki yenye thamani ya sh,Milioni 2.8,mshindi wa pili akipata bati 100,wa tatu bati 40,mshindi wa nne akipata sh,200,000 huku mshindi wa tano akiondoka nash,100,000.
Mshindi wa sita hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha sh,50,000 kila mmoja huku waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa  ndiye atayakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mbio hizo na atashiriki  mbio za kilomita 2.5.
Wanafunzi waatakaopenda kushiriki mbio hizo watasajiliwa kwa sh,500,huku vwasio wanafunzi wakisajiliwa kwa sh,1,000 na wingine ambao hawakutajwa ni kundi gani wakisajiliwa kwa sh,5,000 na fedha hizo kwa mujibu wa Mtaka zitasaidia kambi ya wanariadha watakaoshiriki michuano ya Olimpiki.
Uzinduzi huo pia ulitumika kuwatambulisha wanariadha wawili ambao wamekidhi vigezo vya kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mapema mwezi Agosti mwaka huu  ambako nchi zaidi ya 216  kutoka kila kona ya dunia zitashiriki.
Wanariadha hao ni Alphonce Felix ambaye ana wastani wa muda wa kukimbia wa saa 2:12.01 na Said Makula ambaye muda wake wa kukimbia ni saa 2:13.27 na watatumia mbio hizo mjini Dodoma kama majaribio yao ya kitaifa kati ya majaribio sita ya kitaifa kabla ya kwenda Brazil.
Julai 6 mwaka jana,Felix alishiriki mbio za Gold Coast Marathon nchini Australia na kumaliza nafasi ya sita huku Makula akishiriki mbio za Casablanca Marathon oktoba 25 mwaka jana  na kumaliza katika nafasi ya nne.

TAARIFA KUHUSU KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA-NEMC

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
NEMBO YA TAIFA 
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Katika kikao kilichoitishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Mb), tarehe 24 Januari 2016, mjini Dodoma kuhusu kuimarisha utendaji ndani ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC maamuzi yaliyofikiwa ni kama ifuatavyo:
1. Kuhusu suala la kiwanda cha kusindika minofu ya punda Mkoani Dodoma, imegundulika kulikuwa na ukiukwaji mkubwa, wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa NEMC walioshughulika na kiwanda hicho. Hivyo, Mhe. Makamba ameagiza watumishi wa NEMC wafuatao wasimamishwe kazi mara moja:
a. Dkt. Eladius Makene -Afisa Mazingira Mwandamizi,
b. Wakili Heche Suguta Manchare – Mwanasheria Daraja la II
c. Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi, Afisa Mazingira
Hatua nyingine za kinidhamu na kisheria zitafuatia.
2. Vilevile, imebainika kwamba usimamizi wa watumishi wa NEMC siyo makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza. Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya apewe barua ya onyo kali la mwisho kwa udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa Baraza.
3. NEMC kama chombo muhimu nchini kilichopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira inatarajiwa kazi zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na majukumu yaliyoko kwa mujibu wa Sheria. Hivyo, kwa mapungufu yanayojitokeza Mhe. Makamba, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili kutathmini utendaji wa NEMC na changamoto mbali mbali katika usimamizi wa hifadhi ya mazingira na kuishauri Serikali ipasavyo.
4. Ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa NEMC, ndani ya wiki moja litatolewa Tangazo litakalokuwa na mambo yafuatayo: Anwani ya barua pepe (email), Nukushi (fax), Namba ya simu, Namba ya Whatsapp ili mtu yeyote mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa ama chochote na watumishi wa NEMC ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao atoe taarifa mara moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.
5. Kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja, NEMC ipitie upya orodha ya wataalamu na taasisi elekezi zilizosajiliwa na kufuta wataalamu na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao likiwemo suala la kuwasilisha taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha kazi za wateja wao na kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji wa maombi yao.
6. Ndani ya wiki tatu uitishwe mkutano wa dharura wa Bodi ya NEMC kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika Baraza.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
08.01.2016

CHAMA CHA KARATE MKOANI KILIMANJARO WAMEIOMBA SERIKALI KUTUPIA JICHO MCHEZO HUO

…………………………………………………….
Vero Ignatus – Moshi Kilimanjaro.
Chama cha Karate Mkoa wa Kilimanjaro wanaiomba serikali kutupia macho kwenye mchezo huo kwani imekuwa ikiwasahau ukizingatia mchezo huo ni michezo kama ulivyo mingine na kwamba mchezo huo umekuwa ukifundishwa pia katika majeshi mbalimbali hapa nchini.
Hayo yamesemwa nakapteni wa timu na katibu msaidizi wa chama cha Katrate mkoa wa Kilimanjaro bwana Wembo Hamisi katika viwanja vya mazowezi mkoani hapo na amekusema kuwa wamekuwa wakikwama mara wanapohitajika kwenye mechi za kirafiki,ndani na nje ya nchi kwasababu hawana sapoti kutoka serikalini na wafadhili. 
 Aidha amesema kuwa Karate ni mchezo ambao mtu yeyote anaweza kuucheza na akatengeneza afya ya mwili,na mchezo huo ni wa kawaida kama ilivyo michezo mingine kama mpira wa miguu amewataka watu wote kujitokeza kwa wingi kujiunga katika mchezo huo wa Karate kwa sifa kuu ya karate ni nidhamu.
Sambamba na hayo bwana Wembo amesema kuwa katika mchezo huo wapo wanawake na ameiomba jamii waondokane na ile dhana potofu kwamba mwanamke akicheza mchezo huo wa Karate hawezi kupata mtoto na kufanya shughuli nyingine za kijamii amesema huo ni upotoshaji kwani mwanamke anao uwezo wa kupata mtoto kama walivyo wengine na anatengeneza afaya nzuri kabisa. 
Aidha amesesema kuwa mchezo huo wa Karate kwa historia umeanzishwa miaka mingi kwa mkoa wa Kilimanjaro chama cha karate kina takribani miaka saba sasa tangia kuanzishwa kwa chama hicho,na baadae wakaunda shirikisho la Karate nchini Tanzania ambapo inajumuisha michezo yote ya karate ,ambapo januari 30 watakuwa na tamasha la Karate la kuwatambulisha wachezaji wa timu litakalofanyika mkoani hapo katika ukumbi wa shule ya msingi Mwenge. 
Katibu huyo ameinisha ratiba yao ndani ya miezi sita ambapo watafanya matamasha mbalimbali ikwemo februari 13/2016 watafanya tamasha wilayani Same katika ukumbi wa kimweli same mjini, machi 24-26, mashindano ya mchezo wa GOJUKAI KARATE ya Afrika Mashariki, Kampala Uganda , aprili 30 mashindano ya GOJUKAI Karate ya wazi ya kuuenzi mlima Kilimanjaro ambapo watashiriki watoto wenye umri wa kati na watu wazima yatafanyika Moshi, Mwisho ni Tamasha la shukrani litakalofanyika mei 16 hapo hapo Moshi Kilimanjaro.
Kwa mkoa wa Kilimanjaro mchezo wa karate unaochezwa unajulikana kama Gojukai Stayle, ambayo ilianzishwa kutoka nchini Japan,na chama katika mkoa huo kinaundwa na vilabu mbalimbali ambavyo klabu mama ni Ralway club, Pasua Club, Mwenge Club, Ccp Club,Rau Club,na vilabu vingine vinaundwa na wanafunzi mbalimbali ambapo kila club ina zaidi ya wanafunzi 20-30.hivyo wanawaomba ,Taasisi mbalimbali ,wafanyabiashara,makampuni mbalimbali hata watu binafsi kujitokeza kuudhamini mchezo huo wa Karate.

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO AWATUNUKU VYETI WAHITIMU WA CHUO CHA BAHARI.

1
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, akisaini kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), wakati wa Mahafali ya Chuo hicho. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Yasini Songoro.
2
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, akipata maelezo kutoka kwa Mhandishi wa Meli Stephen Mziray kuhusu utendaji kazi wa mashine mbalimbali za kuongozea Meli.
3
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, akionyeshwa Mitambo mipya katika chumba maalum cha kuongozea Meli kutoka kwa Eng. Deizm Mley.
4
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, (wa nne kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo hicho pamoja na baadhi ya wahitimu.
5
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, akizungumza na wahitimu (hawapo pichani) katika mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
6
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, akimtunuku cheti mmoja kati ya wanafunzi bora waliofanya vizuri katika masomo yao Chuoni hapo.
…………………………………………………………………………………….
Wahitimu wa kozi mbalimbali wa Chuo cha Bahari, Dar es Salaam (DMI), wametakiwa kufuata weredi na kufanya kazi kwa bidii ili kukuza uchumi wa nchi ili kufikia lengo la kustawisha pato la kati ifikapo mwaka 2025.
Pia wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za kazi kitaifa na kimataifa sanjari na kuwa waadilifu ili wasiwe majibu na waendane na kasi ya Rais wa awamu ya tano Dk. John Mafuguli katika utendaji kazi na kuwa na uzalendo kwa taifa kwa kutanguliza maslahi ya nchi mbele.
Wahitimu hao pia wametakiwa kujiendeleza kitaaluma ili kuendana na kasi ya mahitaji ya dunia ya sasa kwa lengo la kupambana na soko la ajira kulingana na vigezo vinavyohitajika kitaifa na kimataifa.
Hayo yalizungumzwa juzi jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Joseph Nyamhanga wakati wa mahafali ya 11 ya chuo hicho.
Eng. Nyamhanga alichukua fursa hiyo akimwalisha Waziri wa wizara hiyo Makame Mbarawa ambaye alikuwa katika majukumu mengine ya kiserikali.
Katika mahafali hayo, Eng. Nyamhanga hakusita kuutaka uongozi wa chuo hicho kuhakikisha wanatunza vema vifaa vya kufundishia ili vidumu kwa kipindi kirefu ili ziendelee kutoa huduma ya mafunzo kwa wanafunzi wengine waliopo na watakaojiunga na chuo hicho kwa fani mbalimbali za ubaharia.
Aliongeza kuwa kwa sasa Wizara hiyo inajipanga kwa ajili ya utanuzi wa majengo ya chuo hicho kwa ajili ya kutoa fursa kupunguza changamoto ya ufinyu wa madarasa kutokana na ongezeko la wanafunzi.
Aliongeza kuwa licha ya kuwa katika mchakato huo, eneo la chuo lililoko Mkuranga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam tayari wakazi husika waliokuwa wakimiliki eneo hilo wameshalipwa kwa asilimia 98 hali inayotoa fursa kwa chuo hiyo kujipanga zaidi kuboresha mahitaji ya chuo hicho.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho, Meja Jenerali mstaafu Ligata Sande alisema kuwa chuo kinajipanga kuweka mifumo makini kwa ajili ya maendeleo yanayohitajika sanjari na kutoa wahitimu wenye sifa stahiki watakaoweza kupambana na soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Pia msoma risala kwa upande wahitimu Amani Mshana, alisema wanafunzi wa DMI wanakabiliwa na changamoto ya kutoshirikishwa kwa katika vikao vya bodi kutokana na kukosekana kwa mwakilishi hali ambayo inasababisha wanafunzi kushindwa kuwasilisha matatizo yao kwenye bodi ya usimamizi wa chuo na kushindikana kutotekelezwa kwa mahitaji yao.
Aliongeza kuwa chuo hicho kina upungufu wa walimu ambapo kwa sasa mwalimu mmoja anafundisha masomo zaidi ya manne na baadhi yao hawana sifa stahiki hususan katika shahada ya kwanza ya uhandisi wa meli na unahodha.
Kutokana na changamoto hizo injinia Nyamuhanga aliwahakikishia wahitimu hao, changamoto hizo kuzifikisha kwa Waziri kwa ajili ya utatuzi.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

JOCKTAN MALULI, DANIEL MSIRIKALE WAIBUKA WASHINDI KATIKA SHINDANO LA BONGO STYLE

 

Mshindi wa Ubunifu mitindo Jocktan Cosmas Maluli A.k.a Makeke(aliyeshika cheti)
akiwa katika picha ya pamoja na  waratibu wa shindano hilo kuanzia
kushoto ni  Zamda George, Comfort Badaru, Martin Kadinda, Reuben Nabora na
Stanley Kamana.
Mshindi wa kipengele cha The Best Photographer, Daniel Msirikale (mwenye miwani) akipokea tuzo yake.
Mlezi wa FASDO, Reuben Nabora akitoa salamu kutoka kwa mwasisi wa FASDO, Lilian Nabora aliyeko Ubelgiji.
Mratibu wa FASDO nchini, Joyce Msigwa  akitoa muhtasari wa shindano la Bongo Style.
Mshereheshaji, Mario Mpingirwa akifafanua jambo.
Mtumbuizaji wa ngoma za asili akionesha uwezo wake wa kuchezea nyoka.
 Baadhi ya viongozi wa wa FASDO wakifuatilia shindano hilo.
Majaji wa ubunifu mitindo wakitathmini kazi za washiriki wao.
Majaji wa upande wa wapiga picha wakitazama kazi za washiriki wao.  
 Mshindi wa ubunifu mitindo, Jocktan Maluli 
  akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo wanaoonesha mavazi yake.
 Wanamitindo wakionesha mavazi yaliyobuniwa na washiriki.
 Washiriki wa ubunifu wa mitindo wakitambulishwa mbele za watazamaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Entango, Emma Kawawa akitoa salamu zake na kuendesha harambee kwa ajili ya FASDO.
Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Chande akizungumza jambo.
Mwenyekiti wa FASDO, Stanley Kamana akiongea jambo.
 Mshindi wa kipengele cha Best Personality of The Year, Shahbaaz S. Yusuf akipokea tuzo kutoka kwa mlezi wa FASDO, Reuben Nabora.
 Mshindi wa Peoples Choice Awards for Fashion Designer, Winfrida Touwa akipokea tuzo yake.
Mshindi wa Peoples Choice Awards for Photograph, Rasheed Hamis akipokea tuzo.
 Msanii Alvin Dullah ‘DY’ akitumbuiza baadhi ya nyimbo zake.
 Baadhi ya washiriki wakichukua vyeti vya ushiriki wa shindano hilo.
 Baadhi ya watu wakijifotoa.
 Baadhi ya wadau wakiongozwa na Mzee Nabora wakizitazama picha za washiriki.
Umati wa watu waliohudhuria fainali hizo wakifutatilia shindano hilo kwa umakini.
(Picha na Fredy Njeje)
………………………………………………………………………………………………
WASHIRIKI
wa shindano la Bongo Style linaloratibiwa na asasi isiyo ya kiserikali
ya FASDO, Jocktan Cosmas Maluli  (25) na Daniel Msirikale (24) wameibuka kidedea
kwa kujinyakulia tuzo za shindano hilo katika fainali iliyofanyika
katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar.
 
Shindano hilo lililoanzishwa mtandaoni mwezi Septemba
mwaka 2015, lilijumuisha washiriki wapatao mia tatu wenye vipaji vya
upigaji picha na ubunifu wa mitindo huku washiriki kumi pekee wakiingia
kwenye fainali baada ya michujo mbalimbali kabla ya washiriki hao wawili wakishinda tuzo hizo.
 
Washiriki
hao walishinda kutokana na kura za majaji waliobobea katika fani hizo
ambapo kwa upande wa picha majaji hao walikuwa ni: Sameer Kermalli,
Hanif Abdulrasul, Idd John na Angela Kilusungu huku kwenye ubunifu wa
mavazi majaji hao wakiwa ni: Martin Kadinda, Rio Paul, Zamda George na
Comfort Badaru.
 
Jocktan Maluli ambaye ameshinda katika kipengele cha Best Fashion Designer 2015
na Daniel Msirikale aliyeshinda katika kipengele cha Best Photographer
2015, wote pamoja wamepokea kitita cha dola 500 kila mmoja huku wakipata
nafasi ya kwenda nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuonesha ubunifu wao
katika maonesho ya Africa Firm Festival Belgium kuonesha kazi zao pamoja
na washiriki 18 walioshiriki shindano hilo, yatakayofanyika hivi
karibuni nchini humo.
 
Aidha washindi wa vipengele vingine
ni: Shahbaaz  Yusuf aliyeshinda kipengele cha Best Personality of the
Year 2015, Winfrida Touwa aliyeshinda katika kipengele cha Peoples
Choice Award for Fashion Designers na Rasheed Rasheed aliyeshinda
kipengele cha Peoples Choice Awards for Photograph.
 
Fainali
hizo zilizohudhuriwa na wageni waalikwa na wadau mbalimbali wa kazi za
sanaa na kupambwa na burudani mbalimbali kama vile nyimbo za asili,
muziki na maonesho
ya mavazi na kazi za sanaa kutoka kwa washiriki hao.
 
 

SHINDANO LENYE FURSA YA KUKUZA MITAJI KWA VIJANA LA MO MJASIRIAMALI LAZINDULIWA

DSC07284-2
Mwenyekiti wa Taasisi wa MO Dewji, Mohammed Dewji
Na Modewjiblog team
Mwenyekiti wa Taasisi wa MO Dewji, Mohammed Dewji kwa kushirikiana na kampuni ya Darecha Limited leo (jumatatu) wamezindua shindano la Mo Mjasiriamali lenye lengo la kusaidia kukuza ujasiriamali miongoni mwa vijana.
Shindano ya Mo Mjasiriamali litatoa fursa ya ukuzaji wa mitaji, ulezi wa wajasiriamali na mitandao ya biashara kuongeza mwanga, ujasiri na kuzalisha wajasiriamali Tanzania.
“Mimi kama Mjasiriamali kijana na mzaliwa wa Singida vijijini, sikufikiria hata mara moja kama leo ningekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa moja ya makampuni yaliyofanikiwa sana katika nchi yetu na hata barani Afrika.” Inasema taarifa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa MeTL kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki.
Aidha alisema Afrika ni moja ya bara linalokua kwa haraka na lenye ukuaji imara wa uchumi na amini vijana wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kutumia fursa hizo ili kujiletea uchumi endelevu.
Lakini pamoja na ukweli huo changamoto kama za ukosefu wa mitaji, ukuzaji ujasiriamali na mitandao ya biashara zimekatisha tamaa vijana wengi kukuza kwa mafanikio makampuni yao hapa Tanzania na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa watu wa kipato cha kati.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), watu wenye kipato cha kati katika bara la Afrika wataongezeka na kufikia watu bilioni 1.1 ifikapo mwaka 2060.
Watu wa kipato cha kati ndio wanaochagiza ukuaji wa uchumi kutokana na mahitaji yao na pia ari ya ujasirimali.
Pamoja na ukweli huo kunachangamoto nyingi zinawakabili watu hao wa kipato cha kati. Mathalani nchini Tanzania changamoto kubwa kwa vijana wajasirimali ni gharama za kutafuta mtaji kwa kazi hizo.
“Kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba vijana hawa wanaondolewa tatizo la ujasirimali ili waweze kusukuma mbele uchumi wa Tanzania.” inafafanua taarifa hiyo.
Aidha kwa kuwa Tanzania inaelezwa kuwa ni nchi ya 19 katika bara la Afrika kuhusiana na fursa na ujasirimali ipo haja ya kusaidia ili kuiondoa katika nafasi hiyo. Taarifa ya nafasi ya Tanzania imo katika ripoti yake ya mwaka 2014 ya Africa Prosperity Report.
Taarifa ilifafanua zaidi kwamba kutokana na haja hiyo Taasisi ya Mo Dewji na Darecha Limited wameungana pamoja na kuanzisha shindano la Mo Entrepreneurs ili kutambua na kuuenzi mchango wa wajasirimali chipukizi na kufanikisha ndoto zao.
Ili kufanikisha nia ya kuwa na wajasiriamali wengi, shindano hilo linatarajiwa kuwa daraja kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji, Mohammed Dewji (MeTL Group na Mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation) ambapo vijana ambao wanaonekana wana kitu cha kufanya, lakini hawana msaada watashiriki kwa lengo la kupata msaada katika mfumo wa mtaji, mtandao na usimamizi wa ukuaji wa shughuli wanayofanya au kutaka kuifanya ili kuianzisha na kuikuza.
Mambo hayo yatatekelezwa katika mfumo wa shindano litakalogusa wajasiriamali ambao wana ari na nia ya dhati ya kuendeleza shughuli walizofikiria na kuzianzisha kwa lengo la kuinua uchumi wao binafsi na wa taifa.
Washindi watatu watakaotangazwa Aprili mwaka huu watapatiwa mtaji wa kuanzia au kuendeleza, pia watapatiwa maarifa ya kuendeleza shughuli zao na kuanzishwa mtandao wa kibiashara na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa MeTL Group na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Mohammed Dewji.
Wakati akipewa tuzo ya Forbes ya mwaka 2015, Mohammed Dewji aliitoa kwa heshima ya vijana akiwatakia kila la heri waking’aa, kuvunja nira ya woga, kukabili changamoto na kuendelea katika ujasiriamali kwa lengo la kufanya dunia yetu mahali bora pa kuishi.
Kwa habari zaidi tembelea:

BONDIA VICENT MBILINYI AENDELEA KUJIFUA NA KUTAFUTA WAPINZANI

 New Picture
VICENT MBILINYI KG 63 TANZANIA 2016
New Picture (1)1
Bondia Vicent Mbilinyi akielekezwa jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi yake yakawaida .
Picha na SUPER D BOXING NEWS
……………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea kujifua baada ya kumchakaza bondia mkongwe wa siku nyingi Deo Njiku sasa anaendelea na mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kuwasambalatisha mabondia wengine watakaopita mbele yake
bondia huyo mpaka sasa ameshacheza michezo tisa na kushinda 7 kupoteza na droo 1 ambapo imemuweka katika rekodi nzuri ya mchezo uho kwa mwaka jana
Akizungumza na mwandishi wa habari hizo Mbilinyi amesema kwa sasa yupo fiti kucheza na mtu yoyote kwa keshaiva kikamilifu baada ya kupata mazoezi ya aina mbalimbali yanayo mjengea kujiamini katika mchezo wa masumbwi akiwa chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila ‘Super D’
aliendelea kwa kusema kuwa nilingia katika ngumi za kulipwa kama najitolea lakini siku zinavyozidi kwenda ndio najijengea mashabiki na kujulikana zaidi katika mchezo niupendao hivyo na ahidi sito waangusha na wala sito lewa sifa wanazonipa nitaendelea kujifua ili niendelee kupambana zaidi katika mchezo
nae kocha anaemnowa bondia huyo Super D amesema kuwa Mbilinyi ana moyo wa kufika mbali hivyo ameonesha nia ya kucheza mchezo uhu katika mazingila magumu hivyo kwa mwaka 2016 ni wake wa kutoka katika mchezo wa ngumi
na naisi katika uzito wake kwa sasa akuna wa kumsumbua kwa sababu amekutana na mabondia wa lika zote ambao wanatamba na waliotamba
Kocha Rajabu Mhamila ‘Super D’ kwa sasa anawasimamia mabondia wake akiwemo Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ Shabani Kaoneka, Shomari Milundi, Vicent Mbilinyi Mwenyewe na mwanadada Lulu Kayage ambao wote wapo chini ya Super D Boxing Promotio ambayo kazi yake kubwa ni kuwafundisha na kuwajengea uwezo na kuwatafutia mipambano mbalimbali ya nje na ndani

NAPE ASIMIKWA UCHIFU MKOANI MWANZA

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (katikati)
akizungumza na Machifu wa kisukuma kwenye kituo cha Utamaduni Bujora,
kulia pichani ni Jaji Mstaafu Mark Bomani na kushoto ni Chifu Charles
Kafipa wa Bukumbi mkoani Mwanza
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesimikwa uchifu wa kisukuma mara baada ya kutembelea kituo cha utamaduni wa kisukuma cha Bujora.
Katika tuzo hiyo ya watemi wa kisukuma ambayo risala yake imeandikwa na kusainiwa na Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma Mtemi CM. Dotto Itale, wamemtakia heri na kumuomba mwenyezi mungu amsaidie kufanya kazi zake vizuri na kumtunukia cheo cha Manju Mkuu kiongozi wa ngoma kubwa mwenye kughani umati wote ukaitikia, na kumpa jina la Sangija ambalo linaunganisha Mamanju wote.
BOFYA HAPA UTAZAME VIDEO YA KUSIMIKWA KWA MHE.NAPE

DK.REGNALD MENGI ASHIRIKI CHAKULA CHA MCHANA NA WATU WENYE ULEMAVU DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk. Regnald Mengi (kushoto), akizungumza na Cosmas Anthony ambaye ni mlemavu wa miguu kwenye tafrija ya chakula cha mchana aliyoiandaa maalumu kwa watu wenye ulemavu iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo mchana.
 Mwanamuziki wa kizazi kipya, Beny Paul (kulia), akipagawasha kwenye tafrija ya chakula cha mchana maalumu kwa watu wenye ulemavu iliyoandaliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk. Regnald Mengi Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk. Regnald Mengi akitoa hutuba fupi kwenye tafrija hiyo.
 Wafanyakazi wa IPP waliokuwa wakitoa huduma mbalimbali katika tafrija hiyo.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk. Regnald Mengi, akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (Shivawata), Ummy Hamisi kwenye tafrija hiyo.
 Dk.Mengi akimpa chakula mmoja wa walemavu aliyehudhuria hafla hiyo.
 Dk.Mengi akimpa chakula mmoja wa walemavu aliyehudhuria hafla hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye tafrija hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye tafrija hiyo.
 Tafrija ikiendelea.
 NI furaha tu katika tafrija hiyo watu wamekula na kunywa.
 Dk.Mengi akiteta jambo na mtoto mwenye ulemavu Roida Undule.
 Dk.Mengi akisalimiana akina mama waliohudhuria hafla hiyo.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mchungaji Alphonce Temba akiomba kabla ya kuanza kwa tafrija hiyo.

WAZIRI MKUU LESOTHO ATAKIWA KUTANGAZA MATOKEO YA TUME YA SADC

KAMA
KIKAO maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika) kimeiagiza Serikali ya Lesotho iwe imetangaza matokeo ya Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya kisiasa nchini humo ifikapo Februari Mosi, mwaka huu.
Agizo hilo lililotolewa kwa Waziri Mkuu wa Lesotho, Dk. Pakalitha Mosisili katika kikao cha SADC Double Troika kilichofanyika mapema wiki hii Gaberone, Botswana, chini ya Mwenyekiti wake, Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama ambaye pia ni Rais wa nchi hiyo.
SADC Double Troika ni kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation) kilichofanyika kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa (GICC), jijini Gaborone, Botswana.
Pamoja na kutaka Lesotho itangaze matokeo ya tume hiyo, SADC Double Troika iliitaka nchi hiyo iandae mchakato wa kueleza njia za utekelezaji wa mageuzi kama yalivyopendekezwa kwenye ripoti ya tume hiyo ifikapo Agosti, mwaka huu.
“Vilevile, nchi ya Lesotho inatakiwa kuandaa mazingira wezeshi yatakayotoa nafasi kwa viongozi wa upinzani na baadhi ya maofisa wa kijeshi wanaoishi uhamishoni ambao walikimbia machafuko, waweze kurejea nyumbani,” ilisema sehemu ya taarifa iliyotolewa na sekretariati ya SADC siku moja baada ya kikao hicho kumalizika.
Mkutano huo wa Botswana ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli; Rais wa Botswana, Luteni Jenerali Khama; Rais wa Afrika Kusini, Bw. Jacob Zuma; Rais wa Msumbiji, Bw. Filipe Jacinto Nyusi; Waziri Mkuu wa Swaziland, Dk. Barnabas Dlamini na Waziri wa Mambo wa Nje wa Zimbabwe, Bw. Simbarashe Mumbengegwi ambaye alimwakilisha Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo.  
SADC Double Troika ni mkutano unaohusisha viongozi wakuu watatu wanaoongoza chombo cha ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama na wengine watatu kutoka kwenye Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC. Hawa wanawakilisha mwenyekiti aliyepo madarakani, mwenyekiti aliyemaliza muda wake na mwenyekiti ajaye ambaye huwa ni makamu mwenyekiti.
Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Balozi Radhia Msuya, chini ya muundo wa SADC, kuna mambo makuu mawili; la kwanza likiwa ni utangamano wa kikanda ambao unasimamiwa na mkutano wa wakuu wa nchi (SADC Summit) na la pili ni la siasa, ulinzi na usalama ambalo linasimamiwa na chombo maalum (SADC Organ).
Akifafanua zaidi, Balozi Msuya alisema wajumbe wa mkutano wa SADC Organ ni Msumbiji (Mwenyekiti); Afrika Kusini (Mwenyekiti aliyemaliza muda wake) na Tanzania inayotarajia kuchukua uenyekiti wa chombo hiki ifikapo Agosti, 2016. Botswana, Zimbabwe na Swaziland ndizo zinaunda SADC Summit.
Mapema, kikao hicho, kilipokea taarifa ya msuluhishi wa SADC kwenye mgogoro wa Lesotho ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Dk. Cyril Ramaphosa ambayo iliainisha mambo kadhaa yakiwemo ya kikatiba na kiusalama ndani ya nchi hiyo.

Dk. Ramaphosa alitakiwa kuhakikisha kuwa mgogoro huo uliovihusisha vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi ya Lesotho, unatatuliwa kwa njia ya mazungumzo kati ya wadau husika ili kuhakikisha kuwa nchi hiyo inarudi kwenye hali ya amani – kisiasa na kiusalama.

Mgogoro wa Lesotho umehusisha kuuawa kwa aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Lesotho, Luteni. Jenerali Maaparankoe Mahao, mnamo Juni 25, 2015. Pia baadhi ya wananchi wanadaiwa kutiwa vizuizini na wengine kuwekwa ndani.

NAIBU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

VIT1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Mwaimu (kulia), wakati alipotembelea kituo cha kumbukumbu cha Mamlaka hiyo, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam. Kushotoni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho (NIDA), Paul Bwathondi.
VIT2
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Mwaimu (kushoto),akimuongoza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya NdaniyaNchi, Balozi Simba Yahya (kulia),kutembelea ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, mwishonimwa wiki ,jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kuona jinsi shughuli zaUchapaji na Uzalishaji wa Vitambulisho vya Utaifa zinavyofanyika.
VIT3
Msimamizi wa Mifumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ami Mohamed (kulia), akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), jinsi taswira ya muombaji kitambulisho inavyohifadhiwa kwenye mfumo ili kuwezesha kuiweka kwenye kitambulisho. Naibu Katibu Mkuu  alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
VIT4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia),akiuliza swali baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Noel Chikwindo (kushoto), Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
VIT5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (aliyenyooshamkono), akifuatilia kwaumakini uhakiki wa taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Utaifa, wakati alipotembelea kitengo cha Uhakiki waTaarifa cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi .Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
VIT6
Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Paul Bwathondi (kulia), akitoa ufafanuzi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (watatu kutoka kulia waliosimama), Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
VIT7
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akielezea jambo wakati alipotembelea Kitengo cha kudhibiti ubora wa Vitambulisho vya Taifa, kilichopo kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Katikati ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi na kushoto ni Afisa Usajili anayeshughulikia ubora, Jemima Mulokozi. Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
VIT8
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), anayeshughulikia ubora, Jemima Mulokozi (kushoto), akimuelezea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), jinsi wanavyothibiti ubora wa Kitambulisho cha Utaifa kabla akijachapishwa.Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.( (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MABONDIA ABDALLAH PAZI NA GORGER DIMOSO WASAINI KUZIPIGA MACHI 5 BAGAMOYO MKOA WA PWANI

Bondia Geoger Dimoso akisaini mkataba wa kuzipiga na Abdallah Pazi wa pili kushoto kulia ni mlatibu wa mpambano huo Pembe Ndava na kushoto ni kocha Mbaruku Heri
Mabondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani katikati ni mratibu wa mpambano uho Pembe Ndava Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Abdallah Pazzi na Gerger Dimoso wamesaini mkataba wa kuzipiga Bagamoyo mkoa wa Pwani March 5 katika uzito wa Kg 74
Akizungumza wakati wa kutiliana saini Promota wa mpambano huo Muhusin Sharif amesema kuwa wameamua kupeleka mpambano huo Bagamoyo kwa ajili ya wakazi wa mkoa wa Pwani wapate burudani ya masumbwi siku hiyo
Aliongeza kwa kusema kuwa anaomba makampuni mbalimbali kutoa sapoti kwa ajili ya udhamini wa mapambano hayo kwa kuwa Bagamoyo mchezo huo unapendwa na ndio unachipukia hivyo anaomba sapoti kwa makampuni na taasisi mbalimbali kusaidia mchezo uho ili uendelee kukua hapa nchini
Ambapo kwa Bagamoyo atuna jukwaa ‘ring’ la ngumi hata moja mpaka tukodishe kutoka Dar es salaam ili yaje hapa kwa ajili ya  vijana  kucheza  mchezo hivyo naomba wadau mbalimbali wajitokeze kuchangia upatikanaji wa jukwaa hilo kwa ajili ya mchezo wa ngumi ili mchezo huu uweze kusonga mbele
Siku hiyo mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia Sadiq Momba atakumbana na Baina Mazola katika uzito wa Kg 59 na Adam Yahaya atakumbana na Selemani Bagaiza katika uzito wa Kg 49 na Juma Khan atapambana na Bruno Vivuaviwili na Abdallah Zamba atakumbana na Twalibu Tuwa

KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE YAKUTANA CHINI YA UENYEKITI WA SPIKA WA BUNGE

kam1Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Y. Ndugai (MB) akiongoza kikaoo cha Kamati ya Uongozi ya Bunge-Ofisi za Bunge Mjini Dodoma leo tarehe 24 Januari 2016. Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ni Wenyeviti wote wa Kamati za Kudumu za Bunge.
kam2Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (MB) akiwasalimia wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge kabla ya kuanza kwa kikaoo.
kam3Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mheshimiwa George Masaju akimsalimia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe (MB) kabla ya kuanza kwa kikaoo cha Kamati ya Uongozi. Kushoto ni Mwwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji Dkt Mary Nagu (MB)
kam5Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mheshimiwa Jenista Mhagama (MB) (aliyesimama katikati) akizungumza na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe (MB) (kushoto) pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mheshimiwa George Masaju (kulia).
kam6Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mheshimiwa George Masaju (kulia) akizungumza na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe (MB) (kushoto) kabla ya kuanza kwa kikaoo cha Kamati ya Uongozi.
kam7Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge ambao ni Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge wakisubiri kuanza kwa kikaoo cha kwanza cha Kamati hiyo.
(Picha na Ofisi ya Bunge)

Mashindano ya Michezo ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu yafunguliwa Rasmi jijini Dar es Salaam.

leo1
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Leonard Tadeo akikabidhi Jezi kwa moja ya timu zinazoshiriki katika mashindano ya michezo yanayohusisha wanafunzi  wa vyuo vikuu  leo jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia kwake ni mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam Bw.Imani Matabula.
leo2
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Leonard Tadeo akikagua timu ya chuo kikuu cha Dar es salaam wanaokaa  Chuoni wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo ya  vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya michezo vya chuo kikuu cha Dar es Salaam.
leo3
Mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam Bw.Imani Matabula(aliyesimama) akimkaribisha Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Leonard Tadeo(kushoto) wakati wa ufunguzi  wa mashindano ya michezo ya  vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya michezo vya chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Pich na Daudi Manongi-WHUSM

SHUGHULI MBALIMBALIZA WAZIRI MKUU MAJLIWA BUNGENI

jal1
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunhe kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma Januari 24, 2016. Kutoka kushoto  ni  Dkt. Raphael Chegeni wa Busega, Adadi Rajabu wa Mhuheza  na Jason Rweikiza wa Bukoba Vijijini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jal3
 Waziri Mkuu, Kassim Majlaliwa akizungumza na wenyeviti wa Kamati za Bunge Ofisini kwake mjini Dodoma Januari 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jal4 jal5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mbunge wa Busega, Dkt.Raphael Chegeni kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma Januari 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments :

Post a Comment