Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini
Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Januari
2, 2015 (Picha na Ikulu).
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu
Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar
es Salaam leo Januari 2, 2016. Semina hiyo ya kwanza katika utawala wa
serikaliya awamu ya tano kwa viongozi wakuu wa serikali, imefanyika sikumoja tu
baada ya makatibuna manaibu wao kuapishwa na rais Dkt. John Pombe Magufuli
Ikulu jijini Dar es Salaam, Ijumaa Januari 1, 2016. (Picha na Ikulu)
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu
wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini
Dar es Salaam
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu
wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini
Dar es Salaam
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu
wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini
Dar es Salaam
SAFARI ZA TRNENI YA KWENDA MIKOA YA KIGOMANA MWANZA ZAFUTWA BAADA YA MAFURIKO
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL
umetangaza kusitisha kwa muda kuanzia jana Januari 01, 2016, kutoa huduma zake za usafiri baada ya eneo la reli kati
ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma tuta la reli kukumbwa na
Mafuriko.
Taarifa fupi iliyotolwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana
leo Jumamosi Januari 2, 2015 imesema, taarifa za kifundi eneo lililoathiriwa na
mafuriko ni kubwa hivyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako eneo la mafuriko
kutathmini ukubwa wa kazi yenyewe.
Kutokana na uamuzi huo treni ya abiria kutoka bara ilibidi safari yake ikatizwe ilipofika Dodoma na tayari utaratibu unaandaliwa wa kupata mabasi 17 kuwasafirisaha hadi Dar es Salaam abiria 1,119 . wa treni hiyo.
Hali kadhalika kwa vile tarahe ya kuanza tena huduma bado haijaujulikana, safari zote kuanzia jana Januari 01, 2016, kwenda bara zimefutwa na abiria husika wametakiwa kufika katika vituo vya reli walikokata tiketi ili warejeshewe fedha zao na kupata fursa ya kutafuta usafiri mbadala.
Aidha imesisitizwa kuwa Uongozi kwa wakati muafaka itatoa taarifa kamili kuhusu lini huduma za TRL kwenda bara zitaanza tena.
Wito unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.
No comments :
Post a Comment