Mweka hazina wa Umoja wa Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda
ya Afrika Mhe. Request Muntanga (Zambia) akiongoza kikao cha Bajeti cha
Umoja huo kilichokutana leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa
Bunge la Tanzania Dkt. Thomas Kashililah ambae pia ni Katibu wa Umoja
huo Afrika.
Mweka hazina wa Umoja wa Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Request Muntanga (Zambia) akipitia Jarida la Umoja huo wakati wa kikao cha Bajeti cha Umoja huo kilichokutana leo Jijini Dar es Salaam.
POLISI KUTUMIA “WHATSAPP” KUDHIBITI UHALIFU
Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha (ACP) Edward Balele akifungua kikao kati ya Jeshi hilo na Taasisi za ulinzi kujadili mustakabali wa usalama ndani ya mkoa huu. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Jijini hapa (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ulinzi ya KK kanda ya Kaskazini Claude Herssens akichangia mada katika kikao kilichoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa na kuziusisha taasisi mbalimbali za ulinzi (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Baadhi ya washiriki wa Taasisi za Ulinzi wakiwa wanasikiliza moja ya mada kwa umakini ili baadae waweze kutekeleza kwa vitendo. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Katibu wa TUPSE kanda ya Kaskazini Aisha Masoud akielezea umuhimu wa mikataba baina ya waajiri na waajiriwa wa Makampuni ya Ulinzi. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Mkuu wa Upelelezi ya Makosa Jinai Mkoa wa Arusha (SSP) Muliro Jumanne Muliro akielezea athari za kuwa na waajiriwa ambao hawana sifa kwenye kazi za ulinzi. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Mkoa wa Arusha (SSP) Mary Lugola akitoa elimu ya Huduma bora kwa mteja kwa Makampuni ya Ulinzi (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
……………………………………………………………………………………………………..
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi mkoani hapa
limeazimia kushirikiana na Makapuni binafsi ya Ulinzi na taasisi za
Ulinzi kutoka UN-ICTR, UNMICT, kitengo cha Ulinzi cha B.O.T pamoja na
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu katika kupeana baadhi ya
taarifa za uhalifu na wahalifu mara kwa mara kwa njia mtandao wa kijamii
wa “whatsApp”.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa
Operesheni wa Jeshi hilo mkoani hapa (ACP) Edward Balele wakati
akifungua kikao kilichofanyika katika Bwalo la Polisi mjini hapa
alipokuwa anazungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoani hapa
mwishoni mwa wiki kati ya Jeshi hilo na wawakilishi wa Makampuni 31 ya
Ulinzi, Benki Kuu Kanda ya Kaskazini, Mahakama ya Afrika ya Haki za
Kibinadamu,UN-ICTR na UNMICT.
Mkuu huyo wa Operesheni alisema
kwamba imefika wakati sasa kwa taasisi hizo kuzidi kuimarisha mahusiano
kwa ukaribu huku njia za kisasa za mawasiliano zikitumika katika kupeana
taarifa za uhalifu na pia kubadililishana uzoefu katika masuala ya
ulinzi na usalama.
Alisema awali taarifa juu ya
matukio mbalimbali sio kwamba zilikuwa hazipatikani bali zilikuwa
zinawafikia walengwa kwa mtindo wa ujumbe mfupi yaani SMS lakini kwa
kutumia mfumo wa kikundi cha “WhatsApp” ambacho kitapewa jina maalum,
taasisi hizo zitakuwa zinapata na kutoa taarifa kwa pamoja na kila
mhusika atakuwa anachangia mawazo yake huku wanachama wengine wa kikundi
hicho wakiwa wanaona ushauri wa kila mchangiaji.
Aidha mbali na uundaji wa kundi
hilo litakalotumia mtandao huo wa kijamii mbao umeshika kasi katika
mawasiliano pia aliyaomba Makampuni hayo kutoa ushirikiano zaidi hasa
kwa kutoa rasilimali vifaa pamoja na askari katika kuelekea mwisho wa
mwaka kwa nia ya kufanya doria ya pamoja hivyo kudhibiti vitendo vya
uhalifu ndani ya Mkoa wa Arusha.
Kwa upande wake Mkuu wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha (SSP) Muliro Jumanne Muliro
alisema kwamba Jeshi la Polisi na Makampuni hayo kila chombo kikiwa
kinawajibika ipasavyo katika nafasi yake mafanikio ya kudhibiti vitendo
vya uhalifu yatakuwa makubwa.
Alisema anathamini mchango
mkubwa unaotolewa na Makapuni hayo ya Ulinzi kwani matukio mengi ya
uvunjaji wa Maghala ya viwanda, Ofisi mbalimbali na Makampuni yamepungua
ukilinganisha na miaka ya nyuma kabla Makapuni hayo ya Ulinzi
kukubaliwa kisheria.
Mkuu huyo wa Upelelezi alisema
kwamba wakati wa uajiri wa askari hao wanatakiwa waangalie mambo
mablimbali ikiwemo akili ya kuweza kugundua kitu kinachoashiria uhalifu,
kuwa mwaminifu, kuwa mtulivu na kuwa mvumilivu na kusema kwamba huwa
anafadhaishwa sana pale anapopata shauri linalomhusisha askari yoyote
katika uhalifu hali ambayo inatia doa na aibu kwa taasisi zote za
Ulinzi.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Polisi
Jamii Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Mary
Lugola ambaye alizungumzia juu ya huduma bora kwa Mteja ambapo aliwataka
Wawakilishi wa Makampuni hayo kuwaelekeza askari wao kuwa, wawe na
lugha nzuri kwa wateja wao jambo ambalo pengine litakuwa linazidi
kuwavutia wengine na hatimaye kupata malindo mengi ambayo yatawaongezea
kipato, mbali na hilo pia aliwataka kutotumia nguvu kupita kiasi katika
ukamataji ili kupunguza madhara makubwa yanayoweza kutokea.
Kwa upande wake Mkuu wa kikosi
cha kutuliza ghasia (FFU) Mkoa wa Arusha (SSP) Ramadhani Giro yeye
aliyataka makampuni hayo kufanya mazoezi ya mara kwa mara na alisema
baadhi ya Makampuni ya Ulinzi huwa yanapata mafunzo mbalimbali kama
vile matumizi sahihi ya silaha, ukakamavu na mbinu mbalimbali za kuweza
kubaini uhalifu na wahalifu toka kwa askari waliopo katika kikosi hicho
na kutoa wito kwa askari wa makapuni mengine kujitokeza ili waweze
kupata mafunzo hayo na kupunguza madhara yanayoweza kutokea huko
mbeleni.
Wakichangia katika kikao hicho
baadhi ya wawakilishi wa Makampuni ya Ulinzi, Mwakilishi toka Kampuni ya
KK Security ambaye pia ni Meneja Mkuu wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini
Bw. Claude Herssens alilisifu Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa kuitikia
wito kwa haraka pindi wanapoomba msaada na kuongeza kwamba mtandao huo
utawasaidia sana na hivyo kuwafanya wajue tukio ambalo wanatakiwa kwenda
kutoa msaada nje ya mipaka yao ya kazi na tukio ambalo litakuwa
linawahusu Polisi pekee.
Naye Katibu wa Chama Cha
waajiriwa wa Makampuni Binafsi Kanda ya Kaskazini (TUPSE) Aisha Masoud
alizidi kusisitiza kwamba bado baadhi ya Kampuni hizo zinachangamoto
hasa katika suala zima la mishahara ya wafanyakazi wao japokuwa
serikali toka mwaka 2013 mwezi Agosti ilishatangaza mishahara mipya
lakini baadhi yao hawajatekeleza hilo na kuwataka wafanye hivyo pamoja
na kuwaingiza katika mifuko ya Jamii.
Mara kwa mara Jeshi la Polisi
Mkoani hapa limekuwa likifanya vikao na Makapuni ya Ulinzi lengo likiwa
ni kukumbushana majukumu ya utendaji wa kazi za kila siku hali ambayo
inasababisha kuimarika kwa hali ya usalama.
Serikali ya awamu ya tano yapongezwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa hatua ambazo Serikali
yake imeanza kuzichukua ikiwemo kubana matumizi.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
salaam na Mfanyabiashara maarufu nchini Bw. Mohamed Raza wakati wa
mkutano na waandishi wa habari uliolenga kuipongeza Serikali kwa hatua
inazochukua katika kuwaletea watanzania maendeleo.
Akifafanua Raza amesema sasa ni
wakati muafaka kwa watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu
ya tano kwa kuwa Mh. Rais John Pombe Magufuli ameonyesha dhamira ya
dhati ya kuwakomboa watanzania kwa kujenga Tanzania mpya.
“Tumeshuhudia kwa dhati kabisa Mh.
Rais akionyesha kwa vitendo dhamira yake ya kuwainua wanyonge kwa
kubana matumizi ya Serikali ili fedha zitakazopatikana zitumike
kuboresha huduma za jamaii na tayari ameshaanza kutekeleza hilo”
alisisitiza Raza.
Katika kuimarisha huduma za jamii
kama afya,elimu na miundo mbinu Raza amaesema kuwa tayari Serikali
imeanza kufanya kazi kwa juhudi kubwa ili kuimarisha huduma hizo kote
nchini.
Kwa kuzingatia umuhimu wa rasilimali za Taifa Raza amebainisha kuwa Serikali imeshaonyesha msimamo wake kuwa ni lazima zitumike kuwanufaisha watanzania wote na si vinginevyo .
Kwa kuzingatia umuhimu wa rasilimali za Taifa Raza amebainisha kuwa Serikali imeshaonyesha msimamo wake kuwa ni lazima zitumike kuwanufaisha watanzania wote na si vinginevyo .
Sambamba na juhudi za Serikali
Raza amebainisha kuwa chama cha mapinduzi (CCM) kina ilani inayojibu
changamoto za watanzania na itawanufaisha wote bila kujali itikadi za
vyama na ndio maana CCM imeendelea kuaminiwa na watanzania kwa kupewa
nafasi ya kuongoza nchi.
Pia Raza alitoa wito kwa
watanzania wote bila kujali itikadi zao,rangi, wala maeneo wanayotoka
kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili kujiletea maendeleo kwa Kuwa
Serikali ya awamu ya tano imeonyesha kwa vitendo dhamira hiyo na ni
jukumu la kila mwananchi kuiunga mkono.
Baadhi ya hatua zilizochukuliwa na
Serikali ya awamu ya tano ni kubana matumizi kwa kuondoa matumizi
yasiyo ya lazima,kufuta safari za nje zisizo na ulazima, kusimamia kwa
dhati ukusanyaji wa kodi na kusimamia kwa karibu utendaji Serikalini ili
kuongeza tija kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KWA MOTO
Na Mahmoud Ahmad Arusha
MTU moja amefariki dunia , na vyumba vinne vya madarasa na ofisi mbili za walimu zikiteketea wa moto usiku wa kuamkia leo.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Edward BaleLe, amesema matukio hayo yanatokana na yanzo tofauti .
Amesema mtu mmoja ambae ni
kijana amefariki kwa kuteketea kwa moto alipokuwa amelala kwenye nyumba
ya mzazi wake eneo la Njiro jijini Arusha.
Amesema kulingana na maelezo ya
baba yake na marehemu, ambae ni mhadhiri mstaafu wa chuo ,mtoto wake
alirejea majira ya saa tisa usiku na kuingia ndani ya chumba chake na
baada ya muda mfupi moto ulizuka na kuteketeza nyumba hiyo .
Amesema bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na chanzo cha tukio hilo.
Amesema moto huo unasadikiwa
ulizuka majira ya saa kumi usiku wa kuamkia leo muda mfupi tu baada ya
marehemu kuingia ndani ya nyumba hiyo na kulala na ndipo moto ulipozuka
na kuteketeza nyumba hiyo.
Katika tukio lingine vyumba vinne vya madarasa vimeteketea kwa moto kwenye shule ya msingi ya Daraja mbili ya jijini Arusha.
Kamanda Balele, amesema chanzo
ni hitilafu ya umeme ambayo imesababisha pia ofisi mbili za walimu
kuteketea kwenye tukio hilo na hasara kamili bado haijajulikana.
Wakati huo huo kamanda
wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Aruha, Philemon
Mollel, ambae pia ni mgombea ubunge jimbo la Arusha, amefika kwenye
shule hiyo na kuahidi tofali 2000 za Saruji.
Zaidi ya wagonjwa 200 kutoka maeneo mbalimbali mkoa wa Arusha wapewa elimu kutambua vyanzo vya magonjwa
ZAIDI ya wagonjwa 200 kutoka
maeneo mbalimbali katika mkoa wa Arusha wamefanikiwa kupewa elimu ya
kutambua vyanzo vya magonjwa yao pamoja na kuepukana na mbinu mbalimbali
ambazo zinafanywa na wataaalamu wa afya kwa malengo ya kupata faida
Hataivyo Elimu hiyo imetolewa na
Hospitali ya Shree Hindu Union Charitable iliopo maeneo ya Faya jijini
Arusha ambapo elimu hiyo inatolewa bure kwa kila siku.
Akiongea na waandishi wa habari
kuhusiana na mpango huo wa utoaji wa elimu, mganga mkuu wa hospitali
hiyo Dkt Rajendra Patama alisema kuwa lengo halisi la kuanzisha mpango
huo ni kuweza kuwaokoa watanzania ambao mara nyingi wanadanganyika kuwa
wanaumwa na kumbe hawaumwi.
Rajendra alifafanua kuwa mpango
huo umeanza hivi karibuni kwani kwa sasa wapo baadhi ya wataalamu wa
afya ambao wanatumia mwanya wa wagonjwa kuumwa na kisha kuwabambikiza
magonjwa ambayo sio yao ili waweze kuapata viapato vyao vya kila siku
Dkt huyo alidai kuwa hali hiyo
inawafanya wagonjwa wengi kuishi kwa wasiwasi huku kwa upande wa wengine
nao wakijikuta wanatumia dawa ingawaje hawaumwi na chochote hali ambayo
nayo inasababisha miili kujaa sumu kubwa sana.
“Hapa kila siku lazima tutoe elimu
ya magonjwa mbalimbali lakini hata kiiini cha magonjwa yanayoambukiza
na yale ambayo hayaambukizi na ambao wameshapata elimu hii kwa kweli
hawawezi kutapeliwa bali wanachukua tahadhari tuu wao na jamii
zao”aliongeza.
Wakati huo huo alisema kuwa kwa
kutambua umuhimu wa tiba kwa watanzania wameshaweza kuwasafirisha
wagonjwa 6 nje ya nchi kwa ajili ya kuweza kufanyiwa vipimo na tiba
kubwa na mpaka sasa hali za wagonjwa hao zinaenedelea vema.
“Huu mkakati wetu wa kuepukana na
vifo visivyo vya lazima pamoja na kutoa elimu umeweza kuwasafirisha
wagojwa 6 na bado tupo kwenye mchakato wa kuwasidia walio wengi
zaidi”alisisitiza Dkt huyo.
Alimalizia kwa kuwataka watanzania
hususani wanawake kuhakikisha kuwa wanajiwekea utaratibu wa kupima afya
zao kila mara na pia kujitokeza kwa wingi kwani wanatarajia kutoa
wataalamu wa masuala mbalimbali ya afya kutoka Nchini India.
WAFADHILI KUTOKA MAREKANI WATOA MSAADA WA MADAWATI YA MILIONI 6
ASASI ya Joy Moja kutoka nchini
Marekani imefanikiwa kutoa msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya
milioni 6 katika shule ya msingi ya Kisongo kwa malengo ya kuboresha
elimu shuleni hapo
Akikabidhi msaada huo mapema jana
mkurugenzi wa asasi hiyo hapa nchini,Gidion fanuely alisema kuwa msaada
huo umetoka moja kwa moja marekani ambapo umelenga kuwasaidia watoto
katika changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo
Fanuely alisema kuwa asilimia
kubwa ya wanafunzi wa kitanzania wanashindwa kufikia malengo yao
kutokana na changamoto hususani za uhaba wa vifaa kama vile madawati
hali ambayo inasababisha madhara kwao
Alidai kuwa ili elimu iweze kuwa
nzuri kuna hitajika kuwepo na vifaa vya uhakika ambapo moja ya vifaa
hivyo ni kama vile madawati, lakini kama kukiwa hakuna madawati basi
hata miandiko ya watoto itakuwa mibaya sana
Mbali na hayo fanueli alisema kuwa
ufike wakati sasa wataalamu lakini wafadhili mbalimbali wan chi
mbalimbali waone changamoto ambazo zinaikabili sekta ya elimu hapa
Tanzania na kamwe mzigo huo usibaki kwa serikali pekee kwani bado kuna
changamoto lukuki.
‘asasi yetu ipo hapa Tanzania
lakini hata marekani na tuliona kuwa watoto wa shule hii wanakabiliwa na
changamoto kubwa sana hasa kwenye suala zima la madawati yaliyokuwepo
ni michache ukilinganisha na uhitaji halisi na tumehaidi kuendelea kutoa
msaada lengo tukimaanisha kuwa watoto wanatakiwa kuwa na ndoto na ndoto
hizo zinaanzia kuanza shule za msingi’aliongeza
Naye mkuu wa shule hiyo Cosmas
Lyimo alisema kuwa hapo awali madawati yalikuwa 171 na kwa sasa
wafadhili hao wameleta madawati 80 ila bado kuna uhitaji wa madawati
mengine 35
Lyimo alisema kuwa msaada huo wa
madawati utakuwa ni chachu kubwa sana shuleni hapo kwani hapo awali
watoto walikuwa wanaelekea kukaa chini kutokana na wingi wa watoto na
madawati yakiwa machache
Alisema kuwa mbali na upungufu huo
wa madawato lakini bado shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba
wa viti vya walimu hali ambayo nayo inawafanya walimu washindwe kufanya
kazi zao kwa raha hasa wanapokuwa madarasani.
“Kwa sasa tunaitaji viti 36
vilivyopo ni 16 pekee hivyo basi tunawaomba wafadhili wengine nao waje
kututatulia changamoto hiyo ili tufundishe wanafunzi kwa raha zaidi na
wapte elimu bora zaidi.
BALOZI WILSON MASILINGI AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VYAMA VYA SIASA DMV AHUDHURIA MKUTANO WA HALMASHAURI YA CCM DMV
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi leo Jumamosi Desemba 5,
2015 alihudhuria mkutano wa Halmashauri ya CCM tawi la DMV ikiwa ni moja
ya ziara zake anazotarajiwa kuzifanya kutembelea matawi ya vyama vya
siasa nchiMarekani yenye lengo la kudumisha mshikamano na ushirikiano wa
Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao.
Akiongea kwenye mkutano wa
Halmashauri ya CCM DMV Mhe. Wilson Masilingi amesema lengo kuu ni kuwa
karibu na vyama vya siasa kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano ndani
ya Jumuiya za Watanzania nchini Marekani na pia kuvitambua kama sehemu
na sura ya Diaspora na kutoa wito kwa Watanzania waishio Marekani
kuelekeza nguvu katika kuwekeza nyumbani bila kujali ufuasi wa chama
unachoamini au kushabikia, wote ni Watanzania.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi
aliiomba Halmashauri hiyo ya CCM DMV kusaidia katika maendeleo ya
Tanzania kwa kupanua wigo wao pamoja na kwamba lengo lao ni siasa na
siasa ni sehemu ya maisha ya jamii na maendeleo ya jamii yanategemea
siasa, kwa hiyo basi mnaposikia kuna muwekezaji yupo tayari kuwekeza
Tanzania msisite Ubalozi upo wazi na utafanya kila liwezekanalo
kuhakikisha muwekezaji huyo hapati vikwazo vyovyote.
Mwisho Balozi Wilson Masilingi
aliwashukuru Watanzania kwa kuwa mabalozi wazuri nchini Marekani na
kuwaasa kuishi kwa kufuata misingi na sheria za nchi ya Marekani.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi
akiongea jambo na mwenyekiti wa tawi CCM DMV Bwn. George Sebo kwenye
mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015
mkutano uliofanyika Hampton Inn, College Park, Maryland. Picha na Kwanza

Mkutano ulianza kwa sala na kuwakumbuka wote waliotangulia mbele ya haki.
Mwenyekiti tawi la CCM DMV Bwn.
George Sebo akifungua kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika
siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College
Park, Maryland.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea
machache kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika siku ya
Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College Park,
Maryland.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea machache kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM DMV
Picha ya pamoja.
Bwn. John Mbatta katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Given katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Tino Malinda katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Aunty Grace Sebo katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Grace Mlingi katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Mzee Joel katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Dr. Secelela Malecela katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Katibu wa CCM DMV Bi.Jesca Mushala katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Mwenyekiti wa CCM DMV Bwn. George Sebo katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
ABDALLAH LUWANJE NA SHEDRACK IGNAS WATAMBIANA KUPIGANA KATIKA MPAMBANO WA KUFUGUA MWAKA JANUAR 2 /2016
Mabondia Hassan Salumu kushoto na
Hassan Mgosi wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga
Januari 2 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es a salaam Picha
na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA mbalimbali wa ngumi za
kulipwa wamesaini mkataba wa mpambano wa kufungua mwaka kuzipika siku
ya januar 2 mwakani katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa
Akizungu wakati wa kusaini
mikataba hiyo mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema
kuwa mabondia walio wasainisha kuwa ni Shedrack Ignas atakaepambana na
Abdallah Luwanje na
Hassan Salumu atakabiliana na
Hassan Mgosi nae Shomari Mirundi atapambana na Husein Mbonde na Ramadhani Maonya atakumbana na Said Faraji wakati Kelvin Majiba atakumbana na Ibrahimu Hamis mabondia wengine walio saini ni Mohamed Muhunzi na Mohamed Kashinde
Abdallah Pazi ‘Dula Mbabe’ atakumbana na Zumba Kukwe
Hassan Salumu atakabiliana na
Hassan Mgosi nae Shomari Mirundi atapambana na Husein Mbonde na Ramadhani Maonya atakumbana na Said Faraji wakati Kelvin Majiba atakumbana na Ibrahimu Hamis mabondia wengine walio saini ni Mohamed Muhunzi na Mohamed Kashinde
Abdallah Pazi ‘Dula Mbabe’ atakumbana na Zumba Kukwe
Mpambano huo umeandaliwa na
kampuni ya Butamanya General Tredes and Boxing Promotion imeandaa
mpambano huo kwa ajili ya kukuza viwango vya mabondia chipukizi na
kuimarisha zaidi wale wenye uwezo kwa ajili ya kuwapatia mipambano
mbalimbali ya ndani na nje ya nchi
Super D aliongeza kwa kusema kuwa
siku hiyo kutakuwa na burudani za nguvu pamoja na ulinzi wa kutosha na
ngumi zitaanza mapema ili wapenzi wa mchezo wa masumbwi warudi majumbani
mapema wakiwa na furaha ya mchezo utakaochezwa siku hiyo.
WALIMU WA SKULI MBALI MBALI ZA WILAYA WAPATIWA MAFUNZO YA MICHEZO NA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA (TOC) MJINI ZANZIBAR
Mkufunzi wa Mafunzo ya Walimu wa Michezo wa Skuli yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Suleiman Mahmoudu Jabiri akitowa maelezo kwa washiriki katika siku ya mwisho ya mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 01 mwenzi huu.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu Fak akifunga mafunzo ya walimu wa michezo wa Skuli katika Skuli ya Elimu Mbadala Rahaaleo Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu Faki akiwakabidhi vyeti washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Kamati ya TOC katika Ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Zanzibar.
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar
Idara ya ya Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar imeshauriwa kuwaandalia michezo nje ya nchi walimu wa
michezo wa skuli kwa lengo la kujipatia taaluma zaidi na kukukuza
mechezo nchini ,
Hayo yameelezwa huko Rahaleo
katika Ukumbi wa Elimu Mbadala na Watu wazima na Mkurugenzi Idaraya hiyo
Zanzibar Mashavu Faki wakati akifunga mafunzo yalioandaliwa na Kamati
ya Olimpiki Tanzania (TOC) yaliyofunguliwa tarehe 1 mwezi huu.
Amesema iwapo walimu wa michezo
watapatiwa mafunzo zaidi nje ya nchi wataweza kuwasomesha wanafunzi wao
wa skuli na kuinua sekta ya michezo Zanzibar.
Mkurugenzi Mashavu amesema katika
mwaka 2013 kulifanywa utafiti wa kimchezo na kuonekana kuwa nchi
zinazoimarisha michezo maskulini ndizo zinazofanya vizuri zaidi katika
masomo yao.
Aidha amesema michezo huimarisha
afya, kujenga upendo, udugu na uzalendo katika jamii hivyo hakuna budi
kuendelezwa kwa manufaa ya wanamichezo wenyewe na Taifa kwa jumla.
Sambmba na hayo Mkurugenzi huyo
amewashauri waalimu waliopata mafunzo hayo kwa kushirikiana na Idara
husika kuandaa mafunzo kila baada ya miezi mitatu.
Nae mkufunzi wa mafunzo hayo
Suleiman Mahamoud Jabir amewataka washiriki wa mafunzo hayo kujenga moyo
wa kujitolea kwani katika kufundisha mara nyingi hujitokeza matatizo
mengi.
Kwa upande wao waalimu waliopata
mafuzo hayo Mussa Abdulrab na Arafa Talib Omar wamesema wamejifunza
mambo mengi wasioyajua na kuahidi kuwa watayafanyia kazi.
Mafunzo hayo ya siku tano ya walimu wa michezo wa skuli mbali mbali za Zanzibar yameandaliwa na Kamati Tanzania.
RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG AACHANA NA UKAPERA
Bibi
harusi Mary Michael Mbaya (kushoto), akimvisha pete ya ndoa mume wake
Richard Mwaikenda ambaye ni mpiga picha mkuu wa gazeti la Jambo Leo na
mmiliki wa Kamanda wa Matukio Blog, baada ya kubariki ndoa yao katika
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kivule Dar
es Salaam mchana huu.
Bwana harusi Richard Mwaikenda akiwa amepozi na mke wake Mary Michael Mbaya wakati wa ibada yao ya ndoa.
Mchungaji wa Kanisa hilo, Naory Chuma (kushoto), akiwabariki maharusi hao.
Baba wadogo wa bwana harusi Richard Mwaikenda wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wazazi wa bibi na bwana harusi wakiwa kwenye ibada hiyo.
Ndugu na jamaa wa maharusi hao wakiwa katika ibada hiyo.
Hapa ni furaha tupu kwa ndugu wa maharusi.
Baadhi
ya Waandishi wanaofanyakazi na bwana harusi wakijumuika katika ibada
hiyo. Kutoka kushoto ni Peter Mwenda (Majira), Anicetus Mwesa, Said
Mwishehe na Peter Ambilikile wote kutoka gazeti la Jambo Leo.
Maharusi na wapambe wao wakiwa mbele ya kanisa.
Wanandoa hao wakionesha shahada ya ndoa yao baada ya kukabidhiwa.
Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
Maharusi hao wakitoka kanisani na wanandoa wenzao baada ya kufunga ndoa. Ndoa 11 zilifungwa katika kanisa hilo.
Wanahabari wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi hao.
Hapa ni furaha tupu. Wa tatu kulia ni mwanahabari, Nyakasagani Masenza.
WATENDAJI WA TAMISEMI WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA KUHUSU USAFI, UJENZI HOLELA, WANAOFANYA BIASHARA MAENEO YA DART
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati akizungumza na watendaji mbalimbali wa ofisi hiyo leo katika mkutano wa kikazi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dares Salaam , ambapo lengo kuu lilikuwa ni kutoa maelekezo ya utendaji kazi kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Afya -TAMISEMI ,Dkt .Deo Mutasiwa .
Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) wakimsilikiza Katibu Mkuu wa ofisi ambaye hayupo pichani.
Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) wakimsilikiza Katibu Mkuu wa ofisi
ambaye hayupo pichani.
Picha namba Magreth Kinabo- MAELEZO.
………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo – maelezo
Serikali imewataka watendaji
wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha kwamba wanafanyakazi
kwa uadilifu weledi wa taaluma zao na kufuata sheria zilizopo katika
kusimimia suala la usafi wa mazingira, likiwemo la kudhibiti biashara
holela, gereji bubu,uegeshaji wa magari holela.
Pamoja na hayo wasimamie,
upigaji holela wa muziki katika vilabu, baa na kumbi zaidi ya saa
zilizopangwa na kuzuia bodaboda zinazosafirisha abiria hadi maeneo ya
miji katikati, pia kuzuia ujenzi holela.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati akizungumza na watendaji
mbalimbali wa ofisi hiyo katika mkutano wa kikazi uliofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa Karimjee, jijini Dar es Salaam ambapo lengo kuu
lilikuwa ni kutoa maelekezo ya utendaji kazi kama ilivyoagizwa na
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.
Akizungumzia kuhusu suala la
usafi wa mazingira kufuatia ziara iliyofanyika hivi karibuni imeonekana
kuwa na changamoto mbalimbali alisema;
“Kazi zetu haziendi vizuri kwa
sababu hatusimamii sheria zilizopo ndio kumekuwa na malalamiko katika
utendaji wa kazi zetu, mfano katika suala la gharama za usimamizi wa
usafi wa mazingira ni kubwa . Lakini kinachofanyika ni kweli
kinalinganishwa na gharama hizi?” alihoji Katibu Mkuu huyo.
Akitolea mifano gharama
zinazotumika katika suala hilo, kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa
2014/2015 alisema kwa upande wa manispaa ya Kindondoni wanatumia Sh.
bilioni 2.6, Ilala ni Sh. bilioni 2.6, wakati Temeke wanatumia Sh.
bilioni 1.2 .
“Kilichobainika ni kwamba
mikataba ya watu wanaojishughulisha na usimamizi wa usafi wa mazingira
ni ya mwaka mmoja na wanaopewa mikataba hiyo ni watu ambao hawana uwezo
wa kutosha wa kutekeleza jukumu hilo.
“ Ama watu wasio na uwezo ama
mnaofahamiana nao. Au kampuni zenye mahusiano na baadhi ya watumishi wa
mamlaka za serikali za mitaa au wenye uhusiano na viongozi wenu,
Jiepusheni na kuwapa watu hawa kwa sababu kutokana na hali hiyo
hamtaweza kukabiliana nao. Kama kuna kiongozi ambaye mmepatia nafasi
hii lazima athibitishe kuwa na uwezo. Na kama pia ni miongoni mwenu
hakikisheni kuwa ni mtu mwenye uwezo. Kazi zetu haziendi vizuri kwa
sababu ya nasaba au viongozi wenu,” alisisitiza Katibu Mkuu huyo, huku
akisema lazima wabadilike na kuangalia kama hawana uwezo wajitoe au
wafukuzwe.
Aliongeza kwamba katika suala
hilo kumekuwa na migongano ya watumishi wa halmashauri ambao
wanatakiwa kufanya kazi kama timu; mfano maafisa afya, mazingira na
usafishaji, lakini akasema wanaonana kama maadui.
“ Hawa wangepaswa kufanya kazi
kwa kushirikiana ,lakini ni maadui kwa sababu ya maslahi … hili ni lenu
wakurugenzi kwani hata watoto wako wakisambaratika ni lazima
huwaketishe chini ili mambo yaende, asiyekubali unamwajibisha,”
alisema.
Sagini alisema watendaji hao ,
wote ni wadau wa usafi, hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano,
hivyo aliwataka wapeane mikono katika kikao hicho, ambapo walifanya
hivyo ikiwa ni hatua ya kuonesha ushirikiano.
Pia alisema watu wanaosafirisha
bidhaa za vyakula kwa kutumia majani ya migomba au matenga
wasiruhusiwe kufanya hivyo wapewa muda wa wiki moja au mbili kutumia
utaratibu mwingine.
Aliwataka pia watendaji
mbalimbali wa TAMISEMI kuwa na ushirikishwaji katika ngazi za chini
kwenye halmashauri kwa kuwa haliko vizuri.
Sagini alisema ni vizuri
kukawekwa mfumo wa TAMISEMI wa kushirikisha ngazi za chini kama ilivyo
kwa mjumbe wa nyumba kumi kwenye masuala ya vyama .
“ Ni lazima tuingie katika mfumo
huu wa kuwa na watendaji wa kaya 30 ambao watakuwa chini ya
TAMISEMI . Suala hili lina faida ya ulinzi na usalama na kuwatambua
wageni… tunaangalia jinsi ya kulitekeleza,” alisema.
Aliwataka wakurugenzi wasikae
maofisini kwenye madawati bali watembelee maeneo mbalimbali ili kutatua
kero za wananchi na kuangalia mipangilio ya miji na majiji.
Katika suala hilo la usafi wa
mazingira alisema mtu mwenye uwezo wa kusafisha jiji liwe safi apewe
nafasi huku akisisitiza suala la kushirikisha sekta binafsi ni muhimu
katika mambo mbalimbali likiwemo la ujengaji wa maegesho ya magari,
ambapo sasa yanahitajika kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo
haraka(DART).
“ Kwenye eneo hili la DART
lazima mbadilike tunataka barabara za DART ziwe nyeupe yaani watu
wasifanye biashara,” alisisitiza huku akitaka kuanzia Jumatatu wiki
ijayo yatekelezwe.
Aliwataka watu wanaohusika na vyombo vya usafiri na usafirishaji kutovunja sheria, akatolea mfano boda boda.
Michango ya wasamaria wema yafanikisha Dada Joyce wa Mbeya kuwasili Muhimbili kwa matibabu
Dada Joyce akiwa ameketi kwa utulivu kwenye siti yake ndani ya ndege
…………………………………………………………………………………………………………
Mpiganaji Deo Kakuru akiwa na dada Joyce ndani ya FastJet wakitoka Mbeya keuelekea Dar es salaam
Mpiganaji Deo Kkuru akiwa na dada Joyce mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam
Msamaria
mwema Mama Rozi akimhudumia dada Joyce akiwa kitandani kwake Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI katika wodi ijulikanayo
kama Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu
Dada Joyce akiwa wodini Moi
MATUKIO YA PICHA ZA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU SEMINA YA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE
Mwezeshaji wa Semina hiyo Andreas Nshala ambaye ni Afisa Mipango akitoa elimu juu ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele jana wakati semina kwa waandishi wa habari kuhusu magonjwa yasiyopewa kiupaumbele iliyofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dare Salaam.(Picha zote na Magreth Kinabo – maelezo)
TGDC NA KAMPUNI YA TOSHIBA WATILIANA SAINI MKATABA WA MAELEWANO (MOU) WA UTAFUTAJI WA NISHATI YA JOTOARDHI
Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakiweka saini Mkataba wa wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) akikabidhi zawadi ya kinyago cha Twiga kwa Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara mara baada ya kusaini Mkataba wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kulia) akikabidhi zawadi ya kinyago cha Kimasai kwa Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara mara baada ya kusaini Mkataba wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Shirika la
Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na Kampuni ya
TOSHIBA ya nchini Japan zimetiliana saini Mkataba wa Maelewano wa
kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji
wa nishati ya jotoardhi.
Utiaji saini
wa mkataba huo umefanyika Desemba 4, 2015 Jijini Dar es Salaam katika
Ofisi za TGDC ambapo hatua hiyo itaiwezesha TGDC kuweza kupata msaada wa
kitaalam ambao utaliwezesha shirika hilo kuweza kuchimba ardhini kwa
lengo la kupata mvuke utakaoweza kuzalisha umeme.
Akiongea
ofisini kwake, Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe amesema
kuwa kupitia Serikali ya Japan hususani Shirika la Maendeleo Japan
(JICA), Kampuni ya TOSHIBA watasaidia kuomba ufadhili wa Serikali yao
ili kuweza kuendeleza ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme pamoja na
matumizi mengine yanayoendana na nishati hiyo.
“Katika
utafiti wa nishati ya jotoardhi tunahitaji watu wenye elimu na uzoefu na
ujuzi wa kutosha, miongoni mwa makubaliano ndani ya mkataba huu
tuliosaini leo ni wafanyakazi wetu kadhaa kuwapeleka nchini Japan kwenye
vyuo vyao ili kuweza kupata mafunzo ya darasani na kutembelea maeneo
ambayo Japan wana vituo vya jotoardhi ili wapate ujuzi wa kufanya kazi
na Wajapan na kutuletea ujuzi huo hapa nchini”, alisema Njombe.
Aidha,
ameeleza kuwa kupitia ushirikiano huo na Serikali ya Awamu ya Tano, nchi
ya Japan itaendelea kuisadia Tanzania katika kuendeleza nishati ya
jotoardhi kwakuwa ni nishati yenye tija katika kutimiza ndoto za
Tanzania kwa kuifanya kuwa nchi yenye kipato cha kati kufikia mwaka
2020.
Mhandisi
Njombe aliongeza kuwa kwa niaba ya Serikali TGDC iko tayari kushirikiana
na TOSHIBA ambapo Januari mwakani wataanza kuaninisha maeneo ya
ushirikiano huo na kuyawekea muda wa utekelezaji na mwezi Machi Wataalam
toka TGDC wataweza kwenda nchini Japan kwa ajili ya kwenda kupata elimu
zaidi ya nishati hiyo.
Kwa upande
wake Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara
ameeleza kuwa kampuni yao iko tayari kuisaidia Tanzania katika masuala
yanayohusu jotoardhi na iko tayari kuomba ufadhili kupitia Serikali ya
Japan ikiwemo kuwapa Wataalam wa TGDC elimu ya kutosha inayohusu nishati
hiyo ili waweze kuhkikisha kuwa nishati hiyo inapatikana na kuleta
maendeleo kwa Tanzania.
“Tunafuraha
ya kushirikiana na TGDC katika kufanya tafiti zinazohusu jotoardhi kama
mkataba wetu tuliousaini unavyosema, kupitia Serikali ya Japan na
Shirika la JICA tutaomba ufadhili kwa ajili ya TGDC ili muweze kuleta
wataalam wenu kuja kujifunza Japan pamoja kuwasaidia katika masuala
mengine yanayohusu shughuli ya utafutaji wa nishati hii”, alisema
Kurahara.
TGDC ni
Shirika Tanzu lililopo chini ya Kampuni ya Ugavi wa Umeme Tanzania
(TANESCO) ambapo limepewa lengo na Serikali la kuharakisha upatikanaji
wa nishati ya jotoardhi kufikia Megawati 200 mwaka 2020.
KONGAMANO LA MSAFARA LILILOFANYIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM LAWAJENGA VIJANA WENGI
Msanii
wa sanaa za Maonesho Vanensia Shule, ambaye pia ni Mkufunzi wa Chuo
kikuu cha Dar es salaam upande wa sanaa na Filamu akielezea jinsi Sanaa
inavyoweza kumkomboa kijana,na kutoa mifano ya baadhi ya wasanii
walioanzia chini na sasa wanamafanikio makubwa.
wa sanaa za Maonesho Vanensia Shule, ambaye pia ni Mkufunzi wa Chuo
kikuu cha Dar es salaam upande wa sanaa na Filamu akielezea jinsi Sanaa
inavyoweza kumkomboa kijana,na kutoa mifano ya baadhi ya wasanii
walioanzia chini na sasa wanamafanikio makubwa.
Matata ambaye anajihusisha na kilimo pia Mjasiliamali kupitia ufugaji
wa nyuki akielezea safari yake ya mafanikio ,na kuwashauri vijana
wasingoje kuajiliwa bali wawe wabunifu na kujiunga katika ujasiliamali, jana tarehe 4.12.2015
wa nyuki akielezea safari yake ya mafanikio ,na kuwashauri vijana
wasingoje kuajiliwa bali wawe wabunifu na kujiunga katika ujasiliamali, jana tarehe 4.12.2015
Rais
wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam Kitaponda Ahadi,
akielezea kuhusu elimu na changamoto alizo zipata wakati wa akiwa Shule
mpaka ndoto yake ilivyotimia ya kuja kusoma chuo kikuu na kuwa kiongozi,
amewasihi vijana wenzake wasikate tamaa wafanye bidii katika masomo
watafikia malengo.
wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam Kitaponda Ahadi,
akielezea kuhusu elimu na changamoto alizo zipata wakati wa akiwa Shule
mpaka ndoto yake ilivyotimia ya kuja kusoma chuo kikuu na kuwa kiongozi,
amewasihi vijana wenzake wasikate tamaa wafanye bidii katika masomo
watafikia malengo.
……………………………………………………………….
Vijana
mbalimbali wamejitokeza katika kongamano la msafara kusikiliza baadhi
ya vijana wenzao ambao wametoa historia zao kuhusu walipotokea mpaka
wamefanikiwa kufika hapo walipofikia na kuwatia moyo vijana wengine
wasikate tamaa kwa sababu mafanikio yapo.
mbalimbali wamejitokeza katika kongamano la msafara kusikiliza baadhi
ya vijana wenzao ambao wametoa historia zao kuhusu walipotokea mpaka
wamefanikiwa kufika hapo walipofikia na kuwatia moyo vijana wengine
wasikate tamaa kwa sababu mafanikio yapo.
Msafara
ambao unalenga kuibua na kurudisha ndoto za vijana katika sekta zote
kwa kutambua kuwa kila eneo lina mchango mkubwa katika mafanikio na
maendeleo ya vijana. Wazungumzaji tofauti tofauti walijikita katika
maeneo makuu yafuatayo Sayansi na Teknolojia,Kilimo, Biashara, Sanaa na
usanii, Elimu, Uongozi, Michezo, utunzaji Mazingira, haki sawa za
kijinsia pamoja na harakati.
ambao unalenga kuibua na kurudisha ndoto za vijana katika sekta zote
kwa kutambua kuwa kila eneo lina mchango mkubwa katika mafanikio na
maendeleo ya vijana. Wazungumzaji tofauti tofauti walijikita katika
maeneo makuu yafuatayo Sayansi na Teknolojia,Kilimo, Biashara, Sanaa na
usanii, Elimu, Uongozi, Michezo, utunzaji Mazingira, haki sawa za
kijinsia pamoja na harakati.
Maeneo
hayo yalikuwa ni nguzo kuu ya kufanya vijana kuwa na fursa ya
kukabiliana na changamoto za kimaisha katika kufikia mafanikio na
malengo yao. Katika safari hii ya Msafara matukio mbalimbali yatafanyika
ikiwemo kuwaleta vijana wa rika moja wenye umri wa miaka 15-24 ili
kuwaleta kwa pamoja wapate kujifunza kutoka kwa wengine waliofanikiwa,
wenye fani mbalimbali/Taaruma zao, hii itawajengea ujasili wengine
katika kufikia mafanikio yao.
hayo yalikuwa ni nguzo kuu ya kufanya vijana kuwa na fursa ya
kukabiliana na changamoto za kimaisha katika kufikia mafanikio na
malengo yao. Katika safari hii ya Msafara matukio mbalimbali yatafanyika
ikiwemo kuwaleta vijana wa rika moja wenye umri wa miaka 15-24 ili
kuwaleta kwa pamoja wapate kujifunza kutoka kwa wengine waliofanikiwa,
wenye fani mbalimbali/Taaruma zao, hii itawajengea ujasili wengine
katika kufikia mafanikio yao.
Progamu
hii inaendeshwa na muungano wa Mashirika na Makundi Matano yaliyopo
hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na DARUSO, YouthCAN, NGAO YOUTH na Young
Feminist Forum na inaratibiwa na Oxfam Tanzania, msafara itakuwa ni moja
ya fursa kwa vijana kutangaza na kuonesha ubunifu wao na mafanikio
waliyofikia kimaisha ingawa kuna changamoto na vikwazo mbalimbali. Safari ya
hii inaendeshwa na muungano wa Mashirika na Makundi Matano yaliyopo
hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na DARUSO, YouthCAN, NGAO YOUTH na Young
Feminist Forum na inaratibiwa na Oxfam Tanzania, msafara itakuwa ni moja
ya fursa kwa vijana kutangaza na kuonesha ubunifu wao na mafanikio
waliyofikia kimaisha ingawa kuna changamoto na vikwazo mbalimbali. Safari ya
msafara itaendelea Ifakara mkoani Morogoro tarehe 12.12.2015

No comments :
Post a Comment