Rais
Mstaafu wa awamu Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
kwa Mhe. Rais wa China Xi Jinping, wakati walipokutana kwenye Mkutano wa
Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China uliofanyika Jijini
Johannesburg. Mhe Rais Mstaafu amehudhuria Mkutano huo kama Rais
Mstaafu. Picha na OMR
Droo ya kwanza ya Jaza Mafuta na Ushinde kutoka Gapco yachezeshwa jijini Dar
Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya GAPCO Tanzania, Vijay Nair (katikati) akibonyeza
kitufe kwenye Kompyuta kuwatafuta washindi wa promosheni ya “Jaza Mafuta
na Ushinde” inayowawezesha wateja wa mafuta katika vituo mbali mbali
vya GAPCO jijini Dar es salaam kujipatia mafuta ya bure. Jumla ya Wateja
25 hupata bahati ya kuwekewa mafuta bure. Kushoto ni Mkaguzi wa Michezo
ya kubahatisha nchini, Abdallah Hemedy na kulia ni Mejena Mradi wa
GAPCO, Mohit Sharma.
Watumiaji wa simu na Krismasi ya aina yake
Kwa mara nyingine tena na kama ada ya kila mwaka katika
kipindi hiki, sikukuu ya Krismasi inakaribia. Kama yalivyo mazoea
mihemko na kelele za kadi za sikukuu yatakuwapo ila tofauti na zamani,
barua, kadi za sherehe za Krismasi n.k sio tena jambo la kujivunia.
Wakati jamii ikiwa inafikiria kuhusu hadhi yake kiuchumi na kijamii
kutokana na kukabiliwa na mabadiliko, hadhi ya mtu binafsi pia imekuwa
inaangaliwa. Hivyo ndivyo vipaumbele.
Kwa baadhi ya watanzania hivi sasa licha ya mahitaji
muhimu ya binadamu ambayo ni chakula, malazi, mavazi, huduma za afya
na elimu kipaumbele kinachofuata ni kuwa na simu ya mkononi. Hali hiyo
inatokana na sababu njia za mawasiliano zilizozoeleka kama barua simu
za kawaida za nyaya zimeanza kutoweka kwa kasi.
Hata hivyo baadhi ya vitu havitabadilika inawezekana
kusema hivyo angalau kwa muda mfupi ujao. ‘Makazi asilia’ kwa
kuzingatia mazingira ya kiafrika siku zote yatabakia kuwa hivyo na
ndio maana watanzania wengi wanaoishi mjini nyakati za sikukuu husafiri
kuelekea majumbani mwao kwa ajili ya kusherehekea tukio hili la mwaka na
wapendwa wao na marafiki wakiwa wamewachukulia zawadi.
Kwa hiyo kufanya manunuzi ya zawadi kwa ajili ya ndugu
kunaweza kuwa shughuli ngumu, lakini hilo halimaanishi kuwa kuibuka na
wazo la kufikiria zawadi ni jambo lililoepukikika kutoa zawadi kwa
kila mtu bila kujali jinsia zao au umri.
Watu wanatafuta mbali na kwa mapana, wakijaribu, wakionja
na kutafuta aina ya zawadi za Krismasi kwa ajili yao na wapendwa wao
ikiwa ni kuwapatia zawadi nzuri na ya kipekee.
Kwenye enzi hizi za kidijitali njia mbadala ni nyingi kwa
wale wanaotafuta zawadi itakayodumu kwa muda mrefu kwa wapendwa walio na
uelewa wa teknolojia itakuwa vipi kuwepo kwa ongezeko la mawasiliano
ya simu za mkononi hata kwenye maeneo ya ndani vijijini ambako
mwandishi wa makala haya ana bibi yake mzee wa miaka 90 na ana simu ya
mkononi!
MKURUGENZI MKUU NHC AZUNGUMZIA UMUHIMU WA MIKOPO YA NYUMBA KONGAMANO LA WAHANDISI
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza
kwenye kongamano la 28 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (Institution of
Engineers Tanzania – IET) juu ya mchango wa sekta ya fedha na mikopo ya
nyumba katika kuimarisha sekta ya ujenzi wa nyumba endelevu za gharama
nafuu nchini. Kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es
Salaam linafanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu
Julius Nyerere. IET ni Taasisi inayojitegemea iliyoundwa mwaka 1977,
ikiwa na lengo la kuimarisha fani ya Uhandisi hapa nchini. Taasisi hii
tayari ina jumla ya wanachama 3,000 kutoka katika sekta mbalimbali hapa
nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu
akizungumza kwenye kongamano la 28 la taasisi ya Wakandarasi Nchini
(IET) juu ya mchango wa sekta ya fedha katika kuimarisha sekta ya ujenzi
wa nyumba endelevu za gharama nafuu nchini. Kongamano hilo
linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam linafanyika kwenye
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere.

Washiriki
wa kongamano la 28 la Taasisi ya Wakandarasi Nchini (IET) juu ya
mchango wa Wahandisi katika kujenga Mazingira Endelevu kwenye ujenzi wa
nyumba za gharama nafuu nchini Kongamano hilo linalofanyika kwa siku
mbili jijini Dar es Salaam linafanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kwakiwa katika banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa NHC

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ALIPOWASILI AFRIKA YA KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA TANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan,
akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia
Msuya, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini
Johannesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu
wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan,
akisalimiana Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini
(Defence advisor) Brig. Gen Ibrahim A. Kimario, wakati alipowasili
kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johanesburg jana Desemba 3,
2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za
Afrika na China. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya
Kusini, Radhia Msuya. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na Rais wa China, Xi Jinping, wakati wa Mkutano Mkuu wa
Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum)
uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia
amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na
OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
(mwenye kitambaa cheupe) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa
Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015
jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe
Magufuli katika mkutano huo. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
(mwenye kitambaa cheupe katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano
huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa
Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia
amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na
OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan
(kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto
Nyusi, walipokutana kwenye ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa
Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo
Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John
Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na OMR
Baadhi
ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika
waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg. Picha na

TAMISEMI YAENDELEA KUHAMASISHA SUALA LA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi
ya viongozi wa mkoa wa Dar es salaam na Halmashauri ya Wilaya ya Ilala
wakiwasili eneo la soko la Feri jijini Dar es salaa kujionea hali ya
usafi wa soko hilo.
Baadhi
ya wahudumu wakiendelea na usafi eneo la soko la Feri jijini Dar es
salaa huku Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba na msafara wake
wakikagua na kujionea hali ya usafi wa soko hilo.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba (aliyevaa miwani) akishuhudia Majuto Alli
Majuto akiendelea na kazi yake ya kukaanga samaki aina ya pweza katika
soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam.
Vijana
wakiendelea kazi ya kukaanga samaki katika soko la Feri katika
mazingira ambayo hali ya usafi siyo ya kuridhisha kwa ajili ya kulinda
afya ya mlaji.
Kijana
Hamisi Misango akimnyanyua samaki aina ya taa ili amuandae tayari kwa
kumuuza kwa wateja wanafuata kitoweo katika soko la samaki la Feri
jijini Dar es salaam.
Msafara
wa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba wakishuhudia moja ya shimo la
maji mchafu ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa afya ya wananchi
wanaofika katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam au wale
watakaotumia samaki hao kama hawatakuwa wameandaliwa katika hali ya
usafi na salama. Lengo ni wananchi wengi wanaofika sokoni hapo ni
kununua samaki waweze kuwauzia watu wasoweza kufika sokoni hapo na
wengine kwa ajili ya matumizi yao ya nyumbani.
Mama
lishe Zainabu Hamad anayefanya shughuli zake za kutoa huduma ya chakula
katika soko la Feri zoni 4 kizimba namba 12 akiongea na Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba alipotembelea sokoni hapo kwa lengo la
kuhamasisha suala la usafi kwa manufaa ya kulinda afya ya wananchi
wanatumia huduma hiyo wakiwa sokoni humo.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba na msafara wake wakiwa katika eneo la soko
la Kariakaoo kukagua suala la usafi unavyozingatiwa sokoni humo. Licha
ya uchafu uliopo katika soko la Kariakoo, wafanyabiashara wa matunda
hawachukui tahadhari yeyote ya kulinda afya za walaji wa matunda ambapo
wanauza matunda aina ya mananasi bila kuyafunika sa kusababisha inzi
kuyazonga zonga matunda hayo kitu ambacho ni hatari kwa suala la usalama
wa afya ya malaji.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba akijionea wafanyabiashara wadogo
walivyovamia miundombinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo kwa kasi katika
eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam huku mafundi wakiendelea na kazi
ya kupaka rangi.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba akitembelea maeneo mbalimbali ya soko la
Kariakoo jijini Dar esa salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TFF
Juma
lililopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liliaga timu ya
Taifa ya Vijana Chini ya umri wa miaka 15 (U15) ikianza ziara yake ya
Afrika Mashariki kuanzia kucheza na Burundi mjini Kigoma na baadaye
Kigali, Rwanda, Kampala, Uganda na mwisho Nairobi Kenya.
Bahati mbaya ziara hiyo itaishia
Mwanza na Kigoma kufuatia Mamlaka ya Kodi ya Mapato (TRA) mkoa wa Ilala
kuzuia fedha kwenye akaunti zote za Shirikisho kwa madai ya kulipwa
kiasi cha Shilingi 1,637,334,000 (bilioni 1.6 tshs) ikiwa ni kodi kwa
kipindi cha 2010 – 2013 sehemu kubwa ikiwa ni makato kwenye mishahara
(PAYE) ya walimu wa kigeni, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Jacob Michelsen
na vilevile kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mchezo wa Timu ya
Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Brazili uliofanyika mwaka 2010.
Walimu wa Timu za Taifa wamekuwa
wakilipiwa mishahara na Serikali na hivyo TFF haikuwajibika kuwakata
kodi. Aidha, mchezo kati ya Tanzania na Brazil ulisimamiwa na kamati
maalum ya Serikali na fedha zake hazikuingizwa katika akaunti za TFF.
Kutokana na hatua hii ya TRA shughuli nyingine za mpira zitakazohathirika nazo ni:
1. Kulipia madeni ya usafiri,
chakula na posho za Timu za Taifa zilizoshiriki mtoano wa kombe la Dunia
na mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Challenge Cup)
2. Program za mpira wa Wanawake na vijana zitalazimika kusimama.
3. Mashindano ya kombe la Shirikisho raundi ya pili iko kwenye hatihati kwani hakuna fedha za kugharimia michezo hiyo.
Serikali yayatahadahrisha makampuni ya simu.
(Picha na Hassan Silayo)
WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
TAARIFA
KWA UMMA KUHUSU KANUNI MPYA ZA HUDUMA ZA ZIADA ZA MWAKA 2015 ZA SHERIA YA
MAWASILIANO YA KIELEKTRONIKI NA POSTA YA MWAKA 2010

(THE
ELECTRONIC AND POSTAL COMMUNICATION ACT 2010 (VALUE ADDED SERVICES) REGULATIONS
2015)

Ndugu Waandishi wa Habari
1.
Awali ya yote namshukuru
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutupatia uhai na afya njema na kutuwezesha
kukutana leo kupeana taarifa kuhusu Kanuni Mpya za Huduma za Ziada za Mwaka
2015 ambazo zinatokana na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya
Mwaka 2010. Napenda pia kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa kukubali mwito kushiriki
nasi katika siku hii ya leo. Karibuni sana.

Ndugu waandishi wa Habari
2. Sekta
ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) imeendelea kukua kwa kasi
duniani na hapa nchini kwetu na imeleta mafanikio mengi katika nyanja
mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii kwenye ngazi ya kitaifa na kwa
mwananchi mmoja mmoja katika maisha ya kila siku kwa waishio mijini na vijijini.
Idadi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini imeendelea kuongezeka kutoka
line za simu za viganjani milioni 2.96 mwaka 2005 hadi kufikia milioni 32.1
mwezi Desemba 2014. Watumiaji wa mfumo wa intaneti nao wameongezeka kutoka
milioni 3.56 mwaka 2008 hadi kufikia milioni 11.34 mwaka 2014. Mafanikio haya yanathibitika nanyi mmekuwa ni
mashahidi kwa kuongezeka kwa huduma za mawasiliano na huduma za ziada za
matumizi ya mitandao ambapo imerahisisha kutoa na kupata huduma kwa haraka na
kwa wakati; na wananchi hawalazimiki
kusafiri; na kupunguza urasimu kama vile huduma za kutuma na kupokea pesa;
kulipia ankara za maji, umeme, ada; ukusanyaji wa mapato; kulipia leseni;
kusafirisha taarifa na data; huduma mtandao kama vile Serikali mtandao,
biashara mtandao, shule mtandao na tiba mtandao. Kwa mfano kuna ongezeko kubwa
la huduma za ziada kupitia mawasiliano ya simu za kiganjani. Huduma hizo ni
pamoja na miamala ya kifedha ambayo ina watumiaji wapatao 12,330,962 na ununuzi
wa huduma na bidhaa kwa kutumia miamala ya kibenki. Hivi sasa, wananchi
wanaweza kufanya malipo ya huduma mbalimbali wanazozitumia kupitia simu za
kiganjani ambapo katika kipindi cha Julai, mwaka 2013 hadi Aprili, mwaka 2014
jumla ya miamala 972,641,605 yenye thamani inayofikia shilingi Trilioni 28.3
imefanyika. Maendeleo haya yamesaidia kuokoa muda na kupunguza msongamano
sehemu za kulipia na kupata huduma hizi.

3.
Aidha, mafanikio hayo
yameleta changamoto mbalimbali kwenye Sekta na katika jamii yetu. Kwa leo
tunazungumzia uwepo wa changamoto ya utoaji wa huduma za ziada kwa watumiaji wa
huduma za ziada bila kuwa na utaratibu unaoeleweka kati ya mtoa huduma na mpokea
huduma au mlaji. Baada ya kujitokeza kwa
changamoto katika utoaji wa huduma za ziada, Serikali kupitia Wizara ya
Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ilitunga Kanuni Mpya za Huduma za Ziada za
Mwaka 2015 (Value Added Services – VAS Regulation 2015). Kanuni hizo
zimetangazwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 7 Mwezi Agosti mwaka huu 2015
na kupewa GN. Namba. 320. Kanuni hizo zimetokana na Sheria ya Mawasiliano ya
kielektroniki na Posta ya Mwaka 2010 (The Electronic and Postal Communication
Act 2010) iliyotungwa na kuridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
mnamo tarehe 29 Januari 2010 na badae kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 20
Machi 2010.

Serikali yaahidi kuendelea kuweka mazingara bora na wezeshi katika Tasnia ya Filamu
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.
Mwamini Juma Malemi (kushoto) akiwasili kuelekea kufungua kikao cha
wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu
katika tasnia ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na kulia ni Rais wa Shirikisho
la Filamu Nchini Bw. Simon Mwakifwamba
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.
Mwamini Juma Malemi (katikati) akizungumza na wasanii pamoja na wadau wa
filamu (hawapo pichani) wakati wa kufungua kikao cha wadau wa Filamu
kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya
filamu leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Bibi. Joyce Fisoo na kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini
Bw. Simon Mwakifwamba
Wasanii
na wadau wa filamu wakisikiliza kwa makini mada zilizokua zikiendelea
wakati wa kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na
kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.
Mwamini Juma Malemi (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na
wasanii na wadau wa filamu nchini leo jijini Dar es Salaam baada ya
kufungua kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na
kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu. Wapili kulia ni Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na wapili kushoto ni Rais wa
Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon Mwakifwamba
Picha na: Genofeva Matemu – MAELEZO
………………………………………………………………………………………………………………..

Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Serikali imeahidi kuendelea
kujenga mazingira bora na wezeshi katika tasnia ya filamu kwa kuimarisha
na kuboresha sekta ya Utamaduni nchini ili iweze kuchangia kikamilifu
katika kudumisha Utamaduni wa Mtanzania.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Mwamini Juma Malemi wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
“ Kama Ilani ya mwaka 2015 – 2020 ilivyodhihirisha serikali itaendelea kuimarisha uwezo wa Bodi ya Filamu nchini ili isimamie kwa ukamilifu utekelezaji wa sheria zinazohusu shughuli za filamu na ubunifu kwa lengo la kulinda haki na maslahi ya wanatasnia wa filamu” alisema Bibi Malemi.
Aidha Bibi. Malemi amewakumbusha wasanii kutekeleza sheria, kanuni na taratibu kwani ni wajibu wa kila mtu kutii bila shuruti na kuwataka kutambua ya kuwa utekelezaji wa sheria hauna mbadala na siyo wa hiari.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo amesema kuwa kikao kazi cha wadau filamu kinatoa fursa kwa wadau wote wa tasnia ya filamu kujifunza kutoka kwa wataalamu mbinu mbadala za kimaendeleo pamoja na kutoa fursa ya kujitathmini wao wenyewe ili kuweza kufikia azma yao na azma ya kuinua tasnia ya filamu nchini.
Naye msanii wa filamu nchini Bibi. Coletha Raymond amesema kuwa kikao cha wadau wa filamu kimefanyika wakati muafaka na kuviomba vyombo husika pamoja na wasanii kushirikiana kuunganisha nguvu kutekeleza yale watakayoyaainisha katika kikao hicho kinacholenga kuboresha tasnia ya filamu nchini.
Bibi Coletha amewataka wasanii wasiwe wabishi na kung’ang’ania kufanya kitu cha aina moja bali wawe wabunifu kwani mchango wa wasanii umekua ukionekana katika matukio mbalimbali ya kitaifa na yasiyo ya kitaifa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yafanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni tano kwa wakwepa kodi
Kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Philip Mpango
(Kulia)akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
alipokuwa akitoa taarifa ya upatikanaji wa makontena 43 pamoja na malipo
ya kodi ya Zaidi ya shilingi bilioni tano kutoka kwa wakwepa
kodi,kushoto kwake ni kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Bw.Lusekelo Mwaseba.
Naibu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Bw.Lusekelo
Mwaseba(Kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Kaimu Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Philip Mpango.
Mkurugenzi
wa Huduma na elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA),Bw. Richard Kayombo akieleza jambo wakati wa mkutano na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Kaimu Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Philip Mpango
…………………………………………………………………………………………………….
Na Lorietha Laurence
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya kodi ya zaidi ya shilingi bilioni tano kutoka kwa wafanyabiashara waliokuwa wamekwepa kulipa kodi.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Philip Mpango amesema hatua hiyo imekuja kufuatia agizo kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Kassim alipofanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam Novemba 27 mwaka huu .
Katika Maagizo hayo ya Mhe.Kassim aliitaka TRA kubaini wamiliki wa makontena 329 yaliyoondolewa kwenye bandari kavu kinyume na taratibu pamoja na kutaja bidhaa zilikuwemo ndani ya kontena hizo ikiwemo wakwepaji wa kodi na kuwachukulia hatua watumishi wa TRA walihusika katika mchakao huo.
Aidha Dkt. Mpango aliongeza kwa kusema mpaka sasa wamefanikiwa kubaini jumla ya kampuni 43 zilizohusika katika uigizaji wa makontena ambayo yaliondolewa katika bandari kavu kinyume na taratibu.
“Katika kontena tulizozikamata hizo tumekuta bidhaa za matairi ya magari,samani mbalimbali,betri za magari,vifaa vya ujenzi,nguo na bidhaa mchanganyiko” alisema Kamishna Mpango.
Kwa upande wa watumishi wa TRA mpaka sasa watumishi 35 wa ngazi mbalimbali wamesimamishwa kazi wakiwemo 27 waliokamatwa wiki hii katika geti namba 5 ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Pia aliendelea kufafanua kuwa Uongozi wa TRA unawataka watumishi wote kuorodhesha mali zao ili kuhakiki uhalali wa mali hizo na endapo watabainika kuwa wamezipata mali hizo kinyume na sheria hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.
Naye Naibu Kamishna Mkuu Lusekelo Mwaseba ameeleza kuwa kwa sasa TRA inapitia kwa upya taratibu za utoaji wa leseni ili kuondoa mianya pamoja na kuweka udhibiti katika uondoshaji wa mizigo katika bandari zote,ICDs na bohari za forodha.
“Sambamba na kufuatilia taratibu hizo,TRA pia itahakikisha inawafuatalia mawakala wote wa forodha walioshiliki katika upotevu wa makontena na kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafungia leseni na adhabu nyingine kulingana na sheria zilizowekwa” alisema Mwaseba.
Kaimu Kamishna Mkuu Mpango alitoa wito kwa wote wanaohusika na uondoshwaji wa makontena kutoka bandari kavu kinyume na taratibu kujitokeza na kulipa kiasi cha kodi yote wanayodaiwa kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli aliaagiza kwamba wadaiwa wote walipe madeni yao ndani ya siku saba baada ya hapo watachukuliwa hatua kufuatana na mujibu wa sheria.

KASI YA RAIS DK. JOHN MAGUFULI YAWAFIKISHA KORTINI MAOFISA NANE WA TRA KWA KUHUJUMU UCHUMI
Mshitakiwa
namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, Tiagi Masamaki (katikati) na
washitakiwa wenzake wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam leo mchana baada ya kusomewa mashitaka yao.
Watuhumiwa hao wakisindikizwa na maofisa wa polisi kuingia chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea.
Watuhumiwa wa kesi hiyo wakiingia ndani ya gari.
Mmoja wa watuhumiwa hao akiwa ndani ya gari la Polisi.
Watuhumiwa hao waliokaa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Gari la polisi lililowabeba watuhumiwa hao likiondoka mahakamani hapo.
…………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale KASI ya utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa imeanza kuwagusa baadhi ya watendaji wa Serikali baada ya maofisa wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7 za kitanzania.
Ukimuondoa Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya (51)
Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa mawili.
Alidai makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya Serikali na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya uhujumu uchumi.
Ilidaiwa katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya Juni 1 na Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali kuwa sh. bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya Azam, baada ya kodi zote kutolewa.
Katika shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na Novemba 17 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya sh. bilioni 12.7.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo hawatakiwi kujibu chochote kama kweli au si kweli.
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo kama wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika mahakama hiyo.
“Kama mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi kutoa dhamana,” alisema Hakimu Shahidi
Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa mahakamani hapo bila kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto mchanga kwa hiyo wanaiomba mahakama imfikirie.
Wakili Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com simu namba 0712-727062)

Benki ya ADB yatoa mkopo wa bilioni 750 kwa Tanzania kwa ajili miradi miwili ya maendeleo
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akisaini
mkataba kutoka Benki ya Maendeleo Afrika kwa ajili ya Mradi wa Ujenzi
,kulia ni mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero akitia saini
wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akikabidhiana
hati ya makubaliano ya msaada wa fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi na
mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero wakati wa makabidhiano hayo
leo jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akiongea na
waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa makabidhiano ya fedha kwa
ajili ya mradi wa ujenzi kulia akiwa na mwakilishi wa benki hyo Dkt.
Tonia Kandiero wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
Mtendaji
Mkuu wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale
akiongea na waandishi wa habari baada ya makabidhiano ya fedha kwa
ajili ya mradi wa ujenzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA ALLY DAUD- MAELEZO
……………………………………………………………………………………….
Na jacquline Mrisho-maelezo
Dsm
Dsm
Wizara ya Fedha na Benki ya
Maendeleo Afrika(ADB) zimesaini mikataba yakuikopesha Tanzania shilingi
bilioni 750 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi sekta mbili za maendeleo
ya ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege nchini.
Mikataba hiyo imesainiwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt Servacius Likwelile kwa upande wa Tanzania na Mwakilishi wa Benki hiyo Dkt Tonia Kandiero.
Akizungumza mara baada ya kusaini mikataba hiyo Dkt . Likwelile alisema kuwa katika mkopo wa kwanza utasaidia katika kuinua uchumi nchini kwa kuimarisha miundo mbinu ya barabara ya Tanzania bara na visiwani.
Dkt Servacius Likwelile aliongeza kuwa,mradi huu utapunguza gharama za matengenezo ya barabara pamoja na muda usafirishaji na ukarabati wa vyombo vya usafirishaji.
Naye Mwakilishi wa Benki Maendeleo ya Afrika Dkt Tonia Kandiero alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara kwa ajili ya kuimarisha kilimo hasa katika mikoa ya Tabora, Katavi na Ruvuma ambapo asilimia 90 ya watu wake ni wakulima.
Maeneo ambayo mradi huu yatakayoshughulika ni barabara ya kutoka Tabora (Pangale) hadi Mpanda na nyingine kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay kwa Tanzania Bara na kwa Zanzibar barabara itatoka Bububu hadi Mkokotoni na nyingine kutoka vijijini hadi Bitumen standadi.
Mkopo mwingine unaelekezwa katika ujenzi wa viwanja vya ndege vya Msalato kwa Tanzania Bara na Pemba kwa Zanzibar.

MAGEREZA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI KATIKA MIAKA 54 YA UHURU WA TANGANYIKA
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza John Minja akiwasilia katiki viwanja vya
Magereza Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya hafla ya kukabishi bendera kwa
watumishi 39 wa Jehi hilo wanaotarajia kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa
Tanganyika kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza John Minja akikabidhi bendera ya Magereza kwa
kiongozi wa Msafara Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy leo
tarehe 04/12/2015 wakiwa wanajiandaa kupanda Mlima tarehe 06/12/2015 ili
ifikapo tarehe 09 siku ya Uhuru wa Tanganyika wawe kileleni
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Minja akitoa nasaha kwa wapanda mlima wa Jeshi la Magereza (Hawapo pichani)
Baadhi
ya wadau wa Magereza Utalii Klabu walio tayari kupanda Mlima
Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini nasaha za Kamishna Jenerali wa
Magereza John Minja katika hafla ya kukabidhiwa bendera ya Jeshi hilo
kuipeleka katika Kilele cha Mlima huo.
Baadhi
ya wadau wa Magereza Utalii Klabu walio tayari kupanda Mlima
Kilimanjaro wakiimba nyimbo za hamasa baada ya kupokea bendera kutoka
kwa Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja katika hafla ya kukabidhiwa
bendera ya Jeshi hilo kuipeleka katika Kilele cha Mlima huo.
Wapanda
Mlima Kilimanjaro wa Jeshi la Magereza wakiwa katika picha ya pamoja na
Mkuu wa Jeshi la Magereza John Minja (Katikati),wa tatu kulia ni Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Arusha SACP Hamis Nkubasi, na Mkuu wa Magereza Mkoa
wa Kilimanjaro SACP Venant Kayombo, wa tatu kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa
Magereza Mkoa
Wadau
wa Magereza Utalii Klabu wakiwa katika mazoezi mbalimbali ya kukimbia
na kutembea katika viunga vya mji wa Moshi ikiwa ni maandalizi ya
kuelekea katika kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika sambamba na kuamasisha
utalii wa ndani.
Picha zote na Mrakibu Msaidizi wa Magereza Deodatus Kazinja na Koplo Mfaume Abdalah wa Jeshi la Magereza
……………………………………………………………………………………………..
Na Deodatus Kazinja
Katika kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba watumishi wapatao 39 Jeshi la Magereza wakiwa katika uwiano wa wanaume 30 na wanawake 9 wataadhimisha siku hiyo kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
Washiriki hawa wanatoka katika vituo vya Makao Makuu ya Magereza, Chuo cha Taaluma ya urekebishaji Ukonga Dar es salaam, Kikosi Maalum cha Kutuliza Gasia Magereza (KMKGM), Pwani, Dar es salaam, Iringa, Mbeya, Mara, Tabora, Tanga, Kilimanjaro na Arusha ambao kwa gharama zao wameamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa kufanya utalii wa ndani.
Akiongea na waandishi wa habari Kamishna Jenerali wa Magereza nchini John Casmir Minja katika hafula fupi ya kuwakabidhi bendera watumishi hao katika viwanja vya Magereza Mkoa wa Kilimanjaro amesema amefurahishwa mno na uamuzi wa askari hao kwa vile unalitangaza Jeshi la Magereza nje ya mipaka yake.
Kamishna Minja alisema pia mbali na kulitangaza Jeshi la Magereza unawaweka timamu watumishi hao katika kufanya kazi zao vizuri ikiwa ni kuunga kauli mbiu ya serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi tu.
Aidha Kamishna huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikijitolea kulisaidia Jeshi la Magereza ambapo alitoa taarifa kuwa tayari mikataba ya kununuliwa magari yapatayo 905 na ujenzi wa nyumba za watumishi zipatazo 9500 imesainiwa na magari yataanza kuingia mapema Januari 2016.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Magereza Utalii Klabu ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Ndugu Estomih Hamis mbali na kumshuruku Kamishna Minja akwa namna ambavyo amejitolea katika kufanikisha uanzishwaji wa Klabu hiyo kuelezea dhima nzima ya utalii huo.
“ Tumeamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa mfumo huu kwa sababu kadhaa. Mosi , ni kuunga mkono jitihada za serikali za muda mrefu za kuhamasisha utalii wa ndani ambacho ni chanzo kimojawapo cha kuongeza mapato ya ndani ya serikali”
“Pili, ni kuleta mwamko kwa watumishi wa umma na watanzania kwa ujumla katika kutembelea vivutio vya utalii vya ndani kuliko ilivyo sasa ambapo sehemu kubwa ya watalii ni wageni kutoka nje ya Tanzania”
Aidha, ndugu Hamis aliongeza kuwa zoezi la upandaji mlima Kilimanjaro ni zuri kwa kuimarisha afya za watumishi hivyo kujiepusha na magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu na utimamu wa mwili na hasa kwa askari wanaotakiwa kuwa hivyo muda wote.
Tukio la watumishi wa Magereza kupanda mlima Kilimanjaro litakuwa ni la pili kwa mwaka huu ambapo mara ya mwisho walipanda mlima tarehe 6 March, 2015 wakiwa ni jumla ya watumishi 20 ambapo 16 walifanikiwa kufika kileleni na wanne kurudia njiani kwa sababu mbalimbali.
Zoezi la upandaji mlima lililopita lilifanyika kwa mafanikio makubwa kiasi cha kuibua hoja y wa unndwaji wa chombo cha pamoja kinachoweza kuratibu shughuli za utalii ndani ya Jeshi la Magereza kwa kuwaunganisha watumishi wote.
Hoja hiyo ilifanikiwa kwa kuundwa kwa Klabu ya Utalii ya Magereza, klabu ambayo iko katika hatua za mwisho za usajili. Tayari Klabu hiyo inao viongozi wakiongozwa na Mwenyikiti ndugu Hamis, katibu wake akiwa ni Mkaguzi wa Magereza Dominick Mshana na Mweka Hazina ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Erasto Kipingu.
Nani analipa gharama za utalii huo?
Akijibu swali hilo katibu wa Klabu hiyo Mkaguzi Mshana alisema kwa hivi sasa watumishi hao wanapanda kwa gharama zao wenyewe kutoka katika mishahara yao ambapo karibu kila mshiriki amechanga wastani wa shilingi 300,000.
Mshana amesema ni matumaini yake kuwa katika siku za mbeleni kama watapatikana wadhamini gharama hizo zinaweza kupungua sana kutoka mifukoni mwa washiri.
Aidha amesema gharama za kupanda mlima na kutembelea vivutio vingine kwa ujumla ni kubwa kwa mtu mmoja mmoja lakini kunakuwa na unafuu mkubwa watu wakipanda kama kikundi.

MAADHIMISHO YA SIKU YA KUJITOLEA DUNIANI YAFANYIKA JIJINI DAR
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni Prof. Elisante Ole Gabriel wa
pili kutoka kulia akiongea na wanahabari katika maadhimisho ya siku ya
kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo,wa kwanza kulia
ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Volountary
Overseas (VSO) Dkt. Philip Goodwin.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akiongea na vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za
kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya
kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Bi
Ritha Mushi (VSO Volunteer) akiongea na Vijana wenzake juu ya umuhimu
wa kujitolea katika kongamano la siku ya kujitolea duniani lililofanyika
jijini Dar es Salaam leo.
Bw. Ian Tarimo anaejitolea katika Shirika lisilo la Kiserikali la Youth
For Change akiongea na Vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali
za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya
kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Dr
Ven kutoka DFID akiwaasa vijana wanaojishughulisha na shughuli
mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho
ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Kijana
akipata maelezo juu ya utendaji kazi wa shirika lisilo la Kiserikali la
JICA wakati wa kongamano la siku ya kujitolea lililofanyika jijini Dar
es Salaam leo.

No comments :
Post a Comment