Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Malawi hapa
nchini Mhe. Hawa Ndilowe Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba
8, 2015
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa
Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe Ikulu jijini Dar es salaam leo
Jumanne Desemba 8, 2015
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza na Balozi wa Malawi hapa
nchini Mhe. Hawa Ndilowe baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam
leo Jumanne Desemba 8, 2015
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea barua za salamu toka na Balozi
wa Sweden hapa nchini Mhe. Katarina Rangnitt alipomtembelea Ikulu jijini
Dar es salaam leo Jumanne Desemba 8, 2015.
PICHA NA IKULU
Muhimbili Yaendelea Kupokea Misaada
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa
Mseru akizungumza leo katika mkutano uliowajumuisha viongozi wa Jumuiya
ya Australia na Tanzania kabla ya hospitali hiyo kukabidhiwa vifaa vya
wagonjwa vikiwamo vitanda na baiskeli za magurudumu matatu.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akimsikiliza Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mseru leo wakati wa mkutano na
viongozi wa jumuiya hiyo na wataalamu wa hospitali hiyo. Kulia ni
Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario wa MNH.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha
akiwa katika mkutano huo uliofanyika leo kabla ya kukabidhiwa kwa vifaa
vinavyotumika kuwasaidia wagonjwa wakati wa kupatiwa matibabu.
Mkuu
wa Idara ya Uuguzi na Mazingira ya Ndani, Bi. Zuhura Mawona
akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier
Murcia kabla ya kupokewa kwa msaada huo leo katika hospitali hiyo.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akiwa katika picha
ya pamoja na wauguzi wa hospitali hiyo baada ya kukabidhiwa msaada huo
leo.
Mkurugenzi
wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Bi.
Agness Mtawa akipokea msaada wa vitanda na vifaa vingine leo kwenye
hospitali hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na
Tanzania, Didier Murcia akimkabidhi Sister Mtawa vifaa hivyo na kulia ni
Mkurugenzi wa jumuiya hiyo, Thierry Murcia.
……………………………………………………………………………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) leo imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vitakavyotumika
kuwahudumia wagonjwa katika hospitali hiyo.
Msaada wa vitanda kumi utatumika
katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na wodi nyingine.
Msaada huo umetolewa na Jumuiya ya Australia na Tanzania.
Vifaa vingine vilivyotolewa ni
pamoja na Stretcher’ nne zitakazotumika kusafirishia wagonjwa ambao
hawawezi kukaa, kifaa cha kufanyia mazoezi kwa wagonjwa na baiskeli
ya magurudumu matatu.
Akipokea msaada huo Mkurugenzi
wa Huduma za Uuguzi katika hiyo Agness Mtawa ameishukuru Jumuiya hiyo
na kutoa rai kwa wadau wengine kuendelea kutoa msaada katika hospitali
hiyo.
SERIKALI YA JPM KIBOKO, “UKIBEEP WANAPIGA”, DKT MPANGO ATINGA TRA SAMORA BAADA YA MWANANCHI KUTUPIA UJUMBE MTANDAONI
KUNA
ule msemo wa watu wa mjini, “Uki-beep, napiga” na kweli leo hii Desemba
8, 2015 pale Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, barabara ya Samora
katikati ya jiji la Dar es Salaam, mlipa kodi mmoja alitupia ujumbe
kwenye mtandao wa kijamii akiomba wataalamu wa IT wa TRA, wafike haraka
kwenye ofisi zao za TRA Barabara ya Samora kwani mitambo ya ku-print
Motor Vehicles License ime-collapse”, na watu wamekaa tu wasijue la
kufanya.
ilichukua
kama dakika 15 au 20 hivi, watu wawili waliovalia suti maridhawa na
dada mmoja “aliyeshiba”, walitinga kwenye ofisi hizo, na kukuta walipa
kodi wakiwa wamejazana kwenye mabenchi wakijipepea tu, kutokana na joto
kali.
Mmoja
wa watu hao waliovaia suti, alianza kuwauliza walipa kodi, “Jamani vipi
huduma za hapa mnaridhika nazo.”? Aliuliza mmoja wao.
Walipa
kodi hao kwanza walimtazama, na mmoja “akajilipua”, hapana haturidhiki
nazo, hapa unapotuona tumeshakaa sana, huduma hakuna tunaambiwa mtandao
haupo, tumeshindwa kuchapishiwa stika za malipo ya kodi ya barabarani.
Mwingine
akasema, hata hali ya hewa humu ndani kama unavyoiona joto kali, hakuna
viyoyozi, na tumekuja kulipa kodi hii ni sawa??, akahoji mlipa kodi
huyo.
Baada
ya majibu hayo, Mlipa kodi mmoja aliibuka na kuwaambia wenzake, jamani
semeni huyo ndiye bosi mpya wa TRA, “tiririkeni” yaani semeni, na hapo
malalamiko yakawa mengi, naye bosi huyo ambaye si mwingine bali ni Dkt.
Philip Mpango, ambaye hivi karibuni,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, alimteua kukaimu nafasi ya Kamishna
Mkuu wa TRA, akiziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Kamishna Rished
Bade, akawajibu, nimeyapokea malalamiko yenu, na ndiyo maana mmeniona
niko hapa, nilipokea ujumbe kutoka kwa mlipa kodi akilalamika kuwa hapa
kwenye tawi letu huduma zimesimama, nikaona nfike kujua nini kimetokea.
Alisema Dkt. Mpango akiwaambia walipa kodi hao ambao walionekana
kufurahishwa na maneno hayo.
Wakati
akiwaeleza hayo, mitambo hiyo ghafla ikaanza kufanya kazi na waliokuwa
jirani na madirisha walianza kuitwa mmoja mmoja na kupatiwa huduma.
Hiyo ndiyo serikali mpya ya awamu ya tano yenye kauli mbiu “Hapa Kazi Tu”, hakuna kulala kila mtu anapiga kazi tu.
“figisu
figisu” ya kile wafanyakazi wa hapo waliwaambia wateja wao kuwa “system
iko down”, yaani kwa maana ambayo wao wamezoea kuwaambia wateja kuwa
mtandao wa computer haufanyi kazi kwa hivyo walipa kodi kibao
waliokuwepo kwenye ofisi hizo, walilazimika kukaa tu kwenye mabenchi
wakimuomba mungu mtandao huo upone ili waweze kupata “stika” za magari
yaani Motor Vehicles License.
Pichani Dkt. Mpango (kushoto), akizungumza na walipa kodi hao kwenye tawi la TRA, barabara ya Samora Desemba 8, 2015
Khalfan Said Photojournalist
K-VIS MEDIA P.Box 77807 Mobile; +255 646-453/+255-653-813-033
Blog:http//khalfansaid.blogspot.com Dar es Salaam, Tanzania
KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA YATEKELEZA AGIZO LA RAIS YAKABIDHI VIFAA VYA USAFI VYA MILIONI 5.5 MANISPAA YA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Mkurugenzi
Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (wa tatau kulia),
akimkabidhi vifaa mbalimbali vya usafi wa mazingira vyenye thamani ya
sh.milioni 5.5, Katibu Tawala (DAS), wa Wilaya ya Temeke, Laurence
Mlangwa Dar es Salaam leo mchana, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo,
Sophia Mjema kwa ajili ya kusaidia kufanyia usafi leo hii ikiwa ni
kuunga mkono agizo la Rais Dk. John Magufuli la kutumia Sikukuu ya Uhuru
kufanya usafi nchini kote. Kulia ni Ofisa Usalama na Mazingira wa Puma,
Jonathan Mmari na wengine ni maofisa kutoka Manispaa ya Temeke
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti, akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo.
Ofisa
Usalama na Mangira wa Puma, Amani Mmari (kulia) akizungumza katika
mkutano huo wa makabidhiano wa vifaa hivyo. Wa pili kulia ni Meneja
Rasimali Watu (HR) wa Puma, Loveness Hoyange.
Vifaa hivyo vikikaguliwa.
Mkurugenzi wa Puma akitoa maelekezo wakati wakikabidhi vifaa hivyo.
Vifaa hivyo vikipangwa katika toroli.
Mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo.
Baadhi ya vifaa hivyo.
Matoroli yaliyokabidhiwa na Puma kwa Manispaa ya Temeke.
Matoroli yakipakiwa katika gari la Manispaa ya Temeke baada ya kukabidhiwa.
…………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Mafuta ya Puma imetoa vifaa vya usafi wa mazingira vyenye thamani ya
sh.milioni 5.5 kwa manispaa ya Temeke ili kutekeleza agizo la Rais John
Magufuli alilotaka kila mmoja wetu kushiriki kufanya usafi katika
kilele cha Sikukuu ya Uhuru ambayo inafanyika nchini kote leo.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke,
Laurence Mlangwa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema Dar es
Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Philippe
Corsaletti alisema aliguswa mno na agizo la Rais na kuona ni vema Puma
nao wakamuunga mkono rais.
“Baada
ya kusikia katika vyombo vya habari kuwa rais ameagiza katika sikukuu
ya uhuru mwaka huu badala ya kufanya sherehe hufanyike usafi niliguswa
na kuamua kumuunga mkono” alisema Corsaletti.
Alisema
wameamua kutoa vifaa hivyo kwa manispaa ya Temeke ili kusaidia kazi ya
usafi katika maeneo mbalimbali ambao utafanyika leo nchini kote.
Alitaja
baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni matoroli 10, mipira ya kuvaa mikononi
wakati wa kufanya usafi, viatu vya mvua, vizibao na vinginevyo vyote
vikiwa na thamani ya sh.milioni 5.5
Kwa
upande wake Katibu Tawala wa Manispaa hiyo Laurence Mlangwa akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo, aliishukuru Kampuni hiyo kwa kutoa
vifaa hivyo ambapo alisema vifika wakati muafaka ambapo leo vitatumika
kufanyia usafi kama Rais Magufuli alivyo agiza.
Alisema shughuli za usafi huo zitaanzia viwanja vya Mbagala Zakhem na kutawanyika kuelekea maeneo mengione mbalimbali.
KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KUPITIA RASIMU YA MPANGO WA WA JESHI LA MAGEREZA
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akifungua Kikao Maalum
cha Wadau kutoka nje ya Magereza(hawapo pichani) cha kujadili rasimu ya
Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa
waliopo Magerezani. Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 8, 2015 katika
Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Mshauri
Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Beatus
Kundy(aliyesimama) akiwasilisha rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa
kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani. Jeshi la
Magereza limeandaa rasimu hiyo ili kuipunguzia Serikali gharama za
kuwalisha wafungwa waliopo magerezani.
Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa
Andiko hilo(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji,
Eng. Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna wa
Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Hashim Kimmwe akitoa
mchango wake wakati wa kujadili rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa
kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani.
Wataalam
wa Jeshi la Magereza walioshiriki kikamilifu katika maandalizi ya
Andiko la Mpango wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula kwa
kushirikiana na Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wakifuatilia majadiliano ya rasimu hiyo(Picha zote na Lucas Mboje wa
Jeshi la Magereza).
Katibu mtendaji BAKITA amkabidhi kamusi kuu mpya ya kiswahili katibu mkuu wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo.
Mkuu
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel(kulia) akikabidhiwa kamusi kuu mpya ya Kiswahili kutoka kwa
Katibu Mtendaji kutoka baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA) Dkt Selemani
Sewangi.Kamusi hiyo mpya ina jumla ya maneno makuu Zaidi ya elfu
thelathini na sita(36000) na kurasa 1264.
Katibu
Mtendaji kutoka baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt Selemani
Sewangi(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel kwa
baadhi ya maneno ambayo yapo katika kamusi mpya iliyotolewa na Baraza
hilo leo jijini Dar es Salaam.
TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa
familia ya marehem Willie Chiwango aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki
na mazishi kufanyika eneo la Buguruni jijini Dar e salaam.
Katika salam zake, TFF inawapa
pole familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na kusema kwa niaba ya
familia ya mpira wa miguu nchini, wako pamoja katika kipindi hiki cha
maombolezo.
Marehemu Willie Chiwango ni
miongoni mwa waandishi wa habari wa michezo wakongwe kabisa, aliambatana
na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ iliyoshiriki michuano ya Mataifa Afrika
mwaka 1980 nchini Nigeria.
TFF ilimpa cheti cha heshima
marehemu Chiwango katika zoezi la kuwakumbuka na kutambua mchango wa
viongozi, wachezaji, waandishi wa habari za michezo waliojitoa katika
sekta ya mpira wa miguu nchini.
U15 YAREJEA DAR
Ziara
ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15)
iliyoanzia kanda ya ziwa na kanda ya Magharibi kisha kuendelea katika
nchi za Rwanda, Uganda na Kenya mwezi huu imesitishwa kutokana na
kufungwa akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na Mamlaka ya
Mapato nchini (TRA).
Timu hiyo ya vijana iliondoka wiki
iliyopita kuelekea jijin Mwanza, ambapo iliagwa na kukabidhiwa bendera
ya Taifa na katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki
na timu ya Alliance kabla ya kuelekea mkoani Kigoma.
Ikiwa Kigoma U-15 ilicheza michezo
miwili ya kirafiki na timu ya kombaini ya mkoa wa Kigoma U-15, jumapili
ikacheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Burundi U-17, na jana
asubuhi kuanza safari ya kurejea jijini Dar essalaam.
Awali ziara ya timu hiyo ya U-15
ilikua iendelee katika mji wa Kigali kwa kucheza na U17 ya Rwanda,
Kampala kucheza na Uganda U17, jijini Nairobi kwa kucheza na U17 ya
Kenya na kumaliza ziara hiyo kwa kuchez ana U15 kombaini ya mkoa wa
Arusha Disemba 23, na kurejea jijin Dar es salaam Disemba 24, 2015.
U-15 inajiandaa na michuano ya
Viajana U17 kuwania kufuzu kwa Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini
Madagascar itakayoanza kutimua vumbi Juni 2016.
Naibu Inspekta jenerali wa polisi aanzisha mpango wa kuboresha usalama wa jamii
Na. Tamimu Adam – Jeshi la Polisi.
Jeshi la polisi nchini, limeanzisha mpango wa kuboresha usalama
wa jamii nchi nzima ambao unalenga kuboresha utoaji wa huduma bora kwa
wananchi, kuboresha mawasiliano ya ndani na nje ya Jeshi la polisi kwa
kuwashirikisha wadau mbalimbali wa usalama ambapo mpango huo utaanza
kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi kinondoni ambapo lengo lake ni
kupunguza uhalifu kwa asilimia kumi ifikapo mwaka 2019.
Akihitimisha maabara ya mpango huo iliyofanya kazi kwa wiki sita, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Abdulrahmani Kaniki aliwahakikishia washiriki wa maabara ya kuboresha usalama wa jamii, kuwa Jeshi la polisi litatekeleza kwa vitendo mapendekezo yote yaliyotokana na maabara hiyo, kwani baadhi ya mapendekezo hayahitaji bajeti hivyo utekelezaji wake utaanza mara moja.
“Kazi iliyofanywa na maabara hiyo ni kubwa na umuhimu katika kuboresha usalama wa jamii katika nchi yetu hivyo mapendekezo yote ni lazima yafanyiwe kazi ili kuleta mafanikio chanya”. Alisema Kaniki.
Aliongeza kuwa mpango huo umeanzia katika mkoa wa kipolisi kinondoni na baadaye utaenea nchi nzima, ambapo alizitaja sababu zilizopelekea kuanza na kinondoni kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa makosa, kupanuka mji, idadi kubwa ya watu na uwepo na shughuli nyingi za kiuchumi ukilinganisha na maeneo mengine.
Naye, Mtendaji mkuu wa ofisi ya Rais ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi (PDB), Omari Issa alisema mpango huo wa uboreshaji wa usalama wa jamii ambao unaanza na mkoa wa Kinondoni uliandaliwa kwa kuwashirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali na kijamii ambao kwa pamoja walishirikiana kwa pamoja katika kuangalia namna ya kuboresha usalama wa jamii ili kuwezesha jamii kuwa salama.
Aliongeza kuwa mpango wa matokeo makubwa sasa unahitaji kuzingatia vitu vikuu vitatu katika utekelezaji wake ambavyo ni kujiwekea vipaumbele, nidhamu ya utekelezaji na uwajibikaji hivyo alisema hana wasiwasi na Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa mpango huo hapa nchini.
Mpango wa uboreshaji wa usalama wa jamii unalenga kuboresha na kurahisisha huduma mbalimbali zinazotolewa na Jeshi la polisi ikiwemo kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa askari, usimamizi wa rasirimali watu na vifaa na kuweka mikakati ya kuwashirikisha wadau wa kada mbalimbali ndani ya jamii katika kuboresha usalama wa jamii.
Maabara hiyo ya kuboresha usalama wa jamii ripoti yake inatarajiwa kukabidhiwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi hivi karibuni ili kuanza utekelezaji wake kwa kuanza na mkoa wa kipolisi wa Kinondoni.

PANAFRICAN ENERGY YATOA YAFADHILI UJENZI WA WODI YA ‘MAMA NGONJEA’ HOSPITALI YA WILAYA KINYONGA KILWA KIVINJE NA KUKARABATI WODI ZA UZAZI NA CHUMBA MAALUM CHA UANGALIZI WA AKINA MAMA
Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni
ya PanAfrican Energy Andrew
Kangashaki (kushoto ) na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa
Twalib Mbasha wakikabidhiana mkataba wa miradi ya ujenzi wa nyumba ya mama ngojea katika hospital ya Kinyonga na ukarabati wa wodi ya uzazi mara baada ya kumaliza kusaini mikataba hiyo katika hafla fupi iliyofanyika jana Kilwa Kivinje.

Kangashaki(wa tatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa
Twalib Mbasha (wa tatu kulia) wakisaini makubaliano ya miradi miwili ya ujenzi
wa mama ngojea ‘maternity waiting home’ yaani nyumba maalum kwa kina mama
wajawazito watakaokua wakisubiri kujifungua itakayojengwa katika hospitali ya
Kinyonga – Kilwa Kivinje na kukarabati wodi ya uzazi na chumba maalum cha
uangalizi wa akina mama mara tu baada ya kujifungua katika kituo cha afya cha
Kilwa Masoko. Huku wakishuhudiwa na Mwanasheria wa Wilaya Mh. Godfrey Makary
(wapili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Juma Abdalah Njwayo(wa pili
kushoto), Mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia chama cha CUF Mh. Vedasto
Edgar Ngombale(wakwanza kushoto) pamoja na Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama
cha CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wakwanza kulia).

Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha
CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wapili kulia) akitoa neno la shukrani kwa
Kampuni ya PanAfrican Energy kwa niaba ya wananchi wa Kilwa Kusini mara baada
ya makabidhiano ya mkataba wa miradi itakayowanufaisha wananchi wa kilwa.

Wafadhili wa mradi wa ujenzi wa wodi ya
wazazi Kampuni ya PanAfrican Energy pamoja wakiwaonesha wanahabari chumba cha
uzazi katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko ambacho kipo katika mradi uliosainiwa
kati ya wilaya ya Kilwa na kampuni hiyo. Hii ni katika kuunga jitihada za
serikali za kuboresha huduma za afya.

Hali
halisi ya mazingira ya wodi ya wagonjwa katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko,
hii ni wodi ya wanaume. Kiyuo hichi cha afya
kilijengwa mwaka 1952 enzi za ukoloni mpaka sasa hakijawahi
kukarabatiwa.
halisi ya mazingira ya wodi ya wagonjwa katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko,
hii ni wodi ya wanaume. Kiyuo hichi cha afya
kilijengwa mwaka 1952 enzi za ukoloni mpaka sasa hakijawahi
kukarabatiwa.
Wakisaini makubaliano ya miradi ya ujenziwa mama ngojea na ukarabati wa chumba cha uzazi na wodi maalum ya uangalizi wakina mama mara tu baada ya kujifungua wilayani Kilwa ni Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni ya PanAfrican Energy Andrew Kangashaki (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Twalib Mbasha (wa pili kulia) wanaowashuhudiwa ni Mwanasheria wa Wilaya ya Kilwa Mh. Godfrey Makary ( kulia), Mkuu wa Wilaya ya hiyo Juma Abdalah Njwayo (kushoto) jana katika hafla fupi iliyofanyika jana katika hospitali ya Kinyonga Kilwa Kivinje.
WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO SHULE
Mkuu
wa Divishen ya Elimu ya msingi Zanzibar Ahmed Abdul Majid akifafanuwa
jambo kwa washirikiwa wa mafunzo hayo juu ya Umuhimu wa Elimu ya
Maandalizi yaliyofanyika Kituo cha Walimu Kiembesamaki (TC), (kuliya)
Mkuu wa Mohamed Othman Dau.
…………………………………………………………………………………………………….
Na Majda Kasid –Maelezo Zaznzibar
Wazazi na Walezi wametakiwa kuwa
mstari wa mbele katika kuwapeleka watoto wao waliyofikiwa umri wa miaka
minne katika skuli za maandalizi kwa lengo la kuwakuza kielimu.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa
Divishen ya Elimu ya Msingi Zanzibar Ahmed Abdul Majid wakati alipokuwa
akitowa mafunzo kwa wazazi katika Kituo cha Walimu (TC) Kiembe
Samaki juu ya umuhimu wa Elimu ya Maandalizi.
Amesema wazazi na walezi ndio
wanao hitajika kufanya bidii kwa kila hali kuhakikisha watoto
wanawapa kipaumbele ili kuhakikisha wanapatiwa elimu ya maandalizi
na kujiandaa na elimu ya msingi na sekondari.
Amewataka walimu wanaofundisha
Wanafunzi kuanzia Elimu ya Maandalizi hadi Elimu ya Sekondari
kutowatolesha ada wanafunzi kwani hilo ni agizo lililotolewa na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.
Alifahamisha kwamba mafunzo
hayo yaliyowashirikisha Walimu wa skuli za maandalizi , Walimu wa
madrasa , Masheha pamoja na Wazazi yanalengo la kutoa elimu kwa
jamii .
Nae Mkuu wa Kituo cha Maendeleo
ya awali ya Makuuzi ya watoto (ECD) Muhammed Othman Dau amesema
lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa wazazi wa watoto ili waweze
kuanzishwa skuli za maandalizi mapema kuwajengea mfumo mzuri wa
masomo ya baadae.
Amesema watoto wanapopatiwa
elimu ya maandalaizi huwajengea mustakabali mzuri wa maisha ikiwemo
upeo wa maadili mema pamoja na kuwa na uwezo wa kubuni mambo
ambayo yatawakuza kiakili na kielimu.
Mohammed Othman Dau amesema hadi
hivi sasa watoto waliofikia umri wa miaka mine wanaoandikiswa skuli za
maandalizi imefikia asilimia 50 na lengo ni kuhakikisha watoto wote
wanapelekwa skuli za maandalizi.
Mmoja ya wazazi walioshiriki
mafunzo hayo Othman Khamis amesema ni vyema wanafunzi wa
maandalizi kupatiwa walimu wa masomo ya dini.
KAMATI KUU CCM: RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KANYAGA TWENDE
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na waandishi wa habari leo
Desemba 8, 2015, katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,
Lumumba jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
CCM Taifa ilifanya kikao chake cha kawaida mjini Dar es salaam kwa siku
moja. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kamati Kuu pia ilipokea taarifa juu ya utendaji wa Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020. Kwa ujumla na kwa kauli moja Kamati Kuu ya CCM Taifa iliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu na Waziri Mkuu Mhe. Kassim M. Majaliwa kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika utekelezaji wa Ilani hiyo.
Kamati Kuu kwa niaba ya Chama imeunga mkono hatua kadhaa zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 inatekelezwa kwa ufanisi. Aidha, inapongeza na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika maeneo ya:-
(1) Kusimamia vyanzo vya mapato ya Serikali:
Kamati Kuu inapongeza na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) zinasimamia ukusanyaji wa kodi za Serikali ipasavyo. Juhudi hizi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa muda mfupi zimezaa matunda yanayoonekana wazi. Aidha, Kamati Kuu inawataka wahusika mbalimbali kwenye maeneo hayo ya udhibiti wa vyanzo vya mapato kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Serikali ili lengo liweze kutimia.
(2) Kudhibiti matumizi ya Serikali:
Kama ilivyoagizwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, Serikali ya Awamu ya Tano imeanza vizuri na kwa kasi kusimamia udhibiti wa matumizi yasiyo ya lazima katika Serikali, ili kutumia fedha hizo kwenye utoaji wa huduma kwa wananchi. Kamati Kuu inaunga mkono juhudi hizi na kuwataka wote wanaohusika kwa namna moja ama nyingine na udhibiti wa matumizi hayo wamuunge mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika jitihada hizi.
(3) Uhimizaji wa wananchi katika kufanya kazi kwa bidii:
Kamati Kuu inawataka wanaCCM na wananchi wote kwa ujumla nchini kumuunga mkono Rais na Serikali yake kwa kuitikia wito wa kufanya kazi kwa bidii, kwa maarifa na uzalendo. Kamati Kuu inawahimiza watu wote kwenye maeneo yao ya kazi kujituma na kuchapa kazi ili kujenga nchi yetu na kumuunga mkono Rais Magufuli.
(4) Kusimamia na kuhimiza uwajibikaji katika Serikali, Taasisi na Mashirika yake:
Kamati Kuu pia inapongeza na kuunga mkono juhudi zinazoendelea za kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji mkubwa Serikalini ili kuongeza kasi na ubora wa utoaji huduma. Katika kipindi cha muda mfupi matunda yake yameanza kuonekana na hivyo kuweka msingi mzuri wa kuboresha huduma kwa umma kwa njia endelevu.
(5) Juhudi na jitihada hizi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Magufuli zimeleta matumaini mapya kwa sehemu kubwa ya wananchi na kukuza imani kwa Serikali yao. Hivyo, kila Mtanzania ana wajibu wa kuunga mkono jitihada hizi.
Pamoja na kuunga mkono na kupongeza kasi waliyoanza nayo Rais Magufuli, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, Kamati Kuu inawataka Viongozi wengine wote kuiga mfano huu mzuri na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo ili kutekeleza kwa haraka zaidi Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuleta maendeleo nchini.
Aidha, Kamati Kuu inawatakia Watanzania wote kheri ya Krismas na mwaka mpya wa 2016, na inaamini mwaka ujao utakuwa wa kuchapa kazi na wenye mafanikio zaidi.
Imetolewa na:-
Abdulrahman O. Kinana,
KATIBU MKUU WA CCM 08/12/2015
Tume ya Haki za Binadamu yaandaa Mpango Endelevu kufikia malengo ya Millenia
Mgeni
Rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu Bi. Rehema
Ntimizi akiongea na wadau hawapo pichani walioshiriki katika kongamano
la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es
salaam leo.
Mkurugenzi
wa Tume ya Haki za Binadamu Bw. Francis Nzuki akiongea na waandishi wa
habari katika kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya
Milenia jijini Dar es salaam leo.
Wadau
kutoka sehemu mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja waliposhiriki
kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini
Dar es salaam leo.
Wadau
kutoka sehemu mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja waliposhiriki
kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini
Dar es salaam leo.
………………………………………………………………………………………..
Na Shamimu Nyaki¬¬-Maelezo
Dar es salaam
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu duniani ambayo ni tarehe10 Disemba mwaka huu,Tume ya haki za binadamu na Utawala bora leo imeandaa kongamano la siku moja kujadili Mpango wa Maendeleo Endelevu unaotarajia kuanza rasmi januari mwaka2016.
Mgeni Rasmi katika kongamano hilo Bi Rehema Ntimizi kutoka Tume ya haki za binaadamu ameiomba jamii kushiriki kwa ukamilifu katika kuleta maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla kwa kuwa maendeleo yanaanza na watu wenyewe kwa kuhakikisha wanaondokana na umasikini,kuwa na afya bora ,pamoja na elimu na kutambua kuwa ni haki yao kuwa na uwelewa wa suala hilo.
“Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa hivyo wote tuwajibike katika maendeleo”Alisema bi Ntimizi.
Bi Rehema ameongeza kuwa dunia nzima kwa sasa inashirikisha makundi yote katika jamii katika kutoa maamuzi hasa yale yaliyosahaulika kama wanawake,wazee na watoto waishio vijijni hivyo wakati umefika sasa kwa kila mtu katika jamii kushiriki hatua zote za maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili mpango huo leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Tume ya haki za Binaadamu bw Francis Nzuki ameeleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kujadili mpango huo wa maendeleo endelevu jinsi gani utaleta matokeo chanya katika kufikia malengo ya millenia ifikapo mwaka 2030.
Ameongeza kuwa mpango huo umejikita katika malengo kumi na saba ambayo miongoni mwao ni kuondoa umaskini,kutoa Elimu bora, afya bora pamoja na maji safi kwa kila kundi lililopo katika jamii ambao ni vijana,wazee, wanawake, pamoja na watoto katika jamii ya Watanzania ili kuweza kufikia malengo ya millenia.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa Tume itaanzisha utaratibu wa kutembelea hospitali za umma kuanzia ngazi ya mkoa hadi kijiji ili kuweza kubaini malalamiko na changamoto wanazopata wananchi ,lakini pia kutoa elimu jinsi watakavyoweza kusaidiwa na tume pale wanakutana na changamoto katika suala linalohusu haki na utu wao.
Kauli mbiu katika kongamano hilo ni “Haki zetu uhuru wetu daima”.
Aidha mshiriki kutoka shirika linalowahudumia wazee linaloitwa Helpage Intanational Fund Bw Joseph Mbasha amesema kuwa wazee wanapaswa kushirikishwa katika masuala yote ya maendeleo kwa kuwa nao ni binaadamu na wana uhuru wa kutoa mawazo na kupewa afya bora, kuondokana na umaskini lakini pia kumiliki ardhi.
“Kila mmoja ashiriki katika maendeleo yake na Taifa kwa ujumla”Alieleza Mbasha.
Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za binaadamu wakiwemo Haki Elimu,YUNA,Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Chuo cha Uhasibu.

MASHINDANO YA BASEBALL KUANZA KUTIMUA VUMBI IJUMAA WIKI HII JIJINI DAR ES SALAAM
Nahodha
wa Timu ya Baseball ya Kibasila Pius Peter (kulia) akiwaonyesha
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam jinsi ya mchezo huo
unavyochezwa. Kushoto ni Nahodha wa Timu ya Baseball ya Tigers Mussa
Mbugi.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Baseball nchini Alpherio Nchimbi(kushoto)
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
kuhusu Mashindano ya Kitaifa ya Awamu ya Tatu ya Mchezo wa Baseball
yanayotarajia kuanza Ijumaa ya wiki hii jijini Dar es salaam. Wengine ni
Nahodha wa Timu ya Baseball ya Kibasila Pius Peter (wa pili kulia)
,Nahodha wa Timu ya Baseball ya Tigers Mussa Mbugi( wa pili kushoto) na
Nahodha wa Timu ya Baseball ya Giants Douglas Stanslaus(kulia).
Nahodha
wa Timu ya Baseball ya Kibasila Pius Peter (wa pili kulia ) akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Mashindano ya
Kitaifa ya Awamu ya Tatu ya Mchezo wa Baseball yanayotarajia kuanza
Ijumaa ya wiki hii jijini Dar es salaam . Wengine Katibu Mkuu wa Chama
cha Mchezo wa Baseball nchini Alpherio Nchimbi(kushoto) ,Nahodha wa Timu
ya Baseball ya Tigers Mussa Mbugi( wa pili kushoto) na Nahodha wa Timu
ya Baseball ya Giants Douglas Stanslaus( kulia).
……………………………………………………………………………………………
Na Nyakongo Manyama-MAELEZO-Dar es salaam.
Mashindano ya Kitaifa ya Awamu ya Tatu ya Mchezo wa Baseball yanatarajiwa kuanza Ijumaa ya wiki hii jijini Dar es salaam.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu
Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Baseball nchini Alpherio Nchimbi leo jijini
Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Amesema kuwa mashindano
yatashirikisha timu tisa kutoka Tanzania bara na Visiwani na
yanatarajiwa kufunguliwa na Balozi wa Japani nchini Tanzania Mhe.
Masaharu Yoshida.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo ,
mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika katika shule ya Sekondari ya
Azania iliyopo jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa mashindano hayo yanayojulikana kama 3rd Koshien Tanzania National Championship yatafanyika kwa muda wa siku tatu kuanza tarehe 11 hadi 13 mwezi huu.
Nchimbi amezitaja timu
zitakazoshiriki kuwa ni Shule za Sekondari ya Azania, Kibasila ,
Iyunga, Sanya Juu, Londoni , na Mwanza Baseball Club, Mwanakwerekwe “C” ,
Tigers na Giants.
Amesema kuwa mshindano ya mwaka
huu yanatarajiwa kusimamiwa na wataalamu kutoka nchini Japan
wakishirikiana na wataalam kutoka nchini katika kutoa uamuzi na masuala
mengine ya kiufundi.
Nchimbi amesema lengo la
mashindano hayo ni kupata timu ya Taifa ya umri wa chini ya miaka 21 kwa
ajili ya kuanza maandalizi ya kushiriki mashindano yatakayofanyika
Afrika kusini hapo mwezi wa pili(February ) mwakani (2016).
Kwa upande wa Nahodha wa Timu ya
Giants Douglas Stanslaus ametoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi
kwa ajili kuona mashindano hayo na kuwatia moyo ili waweze kukuza mchezo
huo nchini.
Naye Nahodha kwa timu ya
Kibasila Pius Peter amewaomba vijana wengi kujitokeza kuona na kujifunza
jinsi mchezo huo unavyochezwa ili hatimaye mchezo huo umeweze kuenea
sehemu mbalimbali nchini kama fursa ya vijana kushirikiana na kujenga
umoja.
Aidha Katibu Mkuu wa Katibu wa
Chama cha Mchezo wa Baseball nchini Nchimbi amewaomba wadau mbalimbali
kuthamini mchezo wa Baseball kama ilivyo michezo mingine na kujitokeza
kuufadhili ili uweze kukua na kutengeneza ajira kwa vijana.
Viingilio Tamasha la Krismasi 50,000/-
KAMPUNI ya Msama Promotions ambayo ni waandaaji wa Matamasha
ya Pasaka na Krismasi, imetangaza viingilio vya juu kwenye Tamasha la
Krismasi kuwa ni Shilingi 50,000 kwa viti maalum, Tamasha ambalo
litafanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam.
Tamasha hilo linalokwenda na shukrani kwa Mungu baada ya
uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 ambako kabla, Msama waliandaa
tamasha la Kuombea Amani uchaguzi Mkuu lililofanyika Oktoba 4 kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama VIP watachangia shilingi 10,000 na viti vya kawaida watachangia shilingi 5000.
Msama alisema maandalizi ya
kuelekea tamasha hilo yanakwenda vizuri, huku waimbaji kama Rose
Muhando, Upendo Nkone, Ephraim Sekeleti, Rebecca Malope, Kwaya ya
Wakorintho Wapili, Joshua Mlelwa na Christina Shusho wamethibitisha
kushiriki tamasha hilo.
TGDC NA MKAKATI WA UZALISHAJI WA UMEME KUPITIA JOTOARDHI
Meneja
Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC),
Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu toka Kampuni
ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakikabidhiana Mkataba wa Maelewano
(MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya
upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini
Dar es Salaam.
……………………………………………………………….
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Kutokana na ongezeko la mahitaji ya nishati ya umeme nchini, nishati itokanayo na jotoardhi (Geothermal Energy) imetajwa
kuwa ni muhimu katika kuepukana na hasara kubwa na isiyo ya lazima
inayotokana na matumizi ya mitambo ya mafuta katika kuzalisha umeme na
kuifanya Tanzania kuondokana na tatizo la umeme usiokuwa na uhakika
pamoja na kuleta maendeleo nchini.
Ili kuleta Maendeleo haya katika
sekta ya nishati, Tanzania hainabudi kugeukia katika vyanzo vingine vya
uzalishaji umeme ikiwemo nishati hiyo ambayo kwa kutumia mvuke wa maji
yaliyochemshwa na joto la asili lililopo chini ya ardhi, nishati ya
umeme inaweza kuzalishwa na kukidhi mahitaji ya nishati ambayo yatasaidia kuwa kiunganishi cha ukuaji wa uchumi nchini.
Tanzania iko
katika ukanda wa Bonde la Ufa (Rift Valley), hivyo kuna uwezekano mkubwa
wa uwepo wa hifadhi kubwa ya nishati itokanayo na jotoardhi ambayo
inaweza kutumika katika uzalishaji wa umeme na kuinua uchumi wan chi
yetu.
Nishati hii
itakuwa mkombozi kwa taifa letu hususani kwa mwananchi wa kipato cha
chini kwani tunaamini kuwa matumizi ya nishati hiyo yatapelekea kupungua
kwa gharama za manunuzi ya umeme na kutokana na ukweli kwamba nishati
hiyo pindi ipatakinapo haitarajiwi kuisha.
Unafuu wa
umeme utakaozalishwa na jotoardhi unatokana na ukweli kwamba mitambo
inayotumika kuzalisha umeme huo kuendeshwa kwa mvuke ambao unatokana na
majimoto toka ardhini tofauti na uzalishaji wa umeme uliokuwa unatumika
kwa kutumia mitambo yenye kutumia mafuta ambayo gharama yake ilikuwa
juu kwa Serikali.
Hapa nchini,
kuna viashiria vingi vinaonyesha uwepo wa jotoardhi hasa kwa maeneo ya
vijijini ambako umeme sehemu nyingi haujafika, kutokana na hilo sasa
Serikali yetu hainabudi kutupia macho katika nishati hii kwa kuhakikisha
kwamba wananchi ambao wnaaishi maeneo ambayo nishati hiyo inapatikana
wananufaika na umeme huo.
Jotoardhi ina
matumizi mengi kwa jamii yetu, mfano majimoto yatokayo ardhini yanaweza
kutumika katika kukaushia mazao mfano matumizi ya Vitalu shamba (Green Houses)
badala ya kutegemea jua. Mwananchi wa kipato wa chini anaweza kutumia
majimoto kukausha mazao yake kwa mfano mpunga, maharage, mahindi,
karanga katika ubora ule ule kama wa jua.

No comments :
Post a Comment