Monday, December 7, 2015

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli avunja Bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa wafuatao:- 1. Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari – Prof. Joseph Msambichaka. 2. Mkurugenzi Mkuu wa Bandari – Bw. Awadhi Massawe.

TAARIFA YA WAZIRI MKUU KWA WATANZANIA ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE

1 
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa  akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo wakati alipotoa taarifa ya serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi wa TPA, TRA, Wizara ya Uchukuzi na TRL. kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni Sefue.
3 
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wa kwa utulivua wakati akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari , Kalia ni Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue.
4 
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa akiingia kwenye ukumbi wa mikutano tayari kwa kuzungumza na  waandishi wa habari.
…………………………………………………………………………………………………………….
Mnamo tarehe 27 Novemba, 2015 nilifanya ziara ya kushitukiza Bandari ya Dar es Salaam ambapo nilifichua mwanya wa ukwepaji kodi kwa makontena 329 yaliyopitishwa bandarini kinyume cha utaratibu.
Mtakumbuka pia tarehe 4 Desemba, 2015 nilirudi tena kufanya ufuatiliaji wa hatua ya udhibiti wa upitishaji wa bidhaa mbalimbali kinyume cha utaratibu.
Ziara yangu ilinipitisha hatua zote za upitishaji mizigo ambazo pia kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi wa Ndani wa tarehe 30 Julai 2015 Mamlaka ya Bandari uligundua kuwepo kwa mianya mingi ya ukwepaji kodi ikiwemo na makotena 2387 yaliyopitiahwa kati ya Machi – Septemba 2014 kinyume cha utaratibu, vitendo hivi vinaonyesha kuwa bandari yetu hupitisha makontena mengi bila ya kulipiwa kodi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.
Upotevu huo unaenda sambamba na mfumo usiokidhi wa kupokelea malipo (BILLING SYSTEM) ambao unatoa mwanya mkubwa wa kupoteza mapato ya Serikali. Bandari ni eneo muhimu ambako kama panasimamiwa vizuri panaweza kukusanya fedha nyingi na kuchangia Pato la Taifa.
Serikali haitavumilia kuona watu wachache au kikundi chochote kilichojipanga kuhujumu mifumo au kuiibia Serikali kwa namna yoyote ile kwa manufaa ya wachache.
Matokeo ya ziara hizo ni haya yafuatavyo:-
1. Nimeagiza mfumo wa kupokelea malipo ubadilishwe kutoka Billing System na uwekwe mfumo wa e-payment ambao tayari ulianza kuwekwa na uwe umekamilika kufikia tarehe 11 Disemba 2015.
2. Kwa kuwa ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji makontena hayo na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, kuanzia muda huu nawasimamisha kazi wale wote waliohusika kupitisha makontena kinyume na utaratibu.
1. Wasimamizi wa Bandari Kavu (ICD)
(i) Happygod Naftari
(ii) Juma Zaar
(iii) Steven Naftari Mtui
(iv) Titi Ligalwike
(v) Lydia Prosper Kimaro
(vi) Mkango Alli
(vii) John Elisante
(viii) James Kimwomwa – ambaye amehamishiwa Mwanza.
2. Wafuatao ni Viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya Bandari ambao hawamo kwenye ripoti ila ni wahusika wakuu.
1. Shaban Mngazija – Aliyekuwa Meneja Mapato ambaye kwa sassa amehamishiwa Makao Makuu kitengo cha Fedha.
2. Rajab Mdoe – Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu (ICD) – ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi Co-operate Services.
3. Ibin Masoud – Kaimu Mkurugenzi wa Fedha.
4. Apolonia Mosha – Meneja Bandari Msaidizi – Fedha.
5. James Kimwomwa.
Kutokana na utendaji mbovu wa Mamlaka ya Bandari kwa muda mrefu na kwa kitendo cha kutochukua hatua kwenye vyanzo.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amevunja Bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa wafuatao:-
1. Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari – Prof. Joseph Msambichaka.
2. Mkurugenzi Mkuu wa Bandari – Bw. Awadhi Massawe.
Ndugu Waandishi wa Habari mtakumbuka pia nilifanya ziara pia TRL ambako kwa awali nimegundua matumizi mabaya ya fedha Shilingi Bilioni 13 nje ya utaratibu ambako uchunguzi unakamilishwa.
Mheshimiwa Rais, pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia tarehe ya leo na atapangiwa kazi nyingine.

 

Waogeaji wa Dar Swim Club watamba kutwaa medali, kwenda Dubai Jumatano

index
Wachezaji wa klabu ya Dar Swim Club wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka
……………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Kocha wa klabu ya kuogolea ya Dar Swim Club, Michael Livingstone ametamba kuwa waogelaji wake chipukizi watatwaa medali mbalimbali katika mashindano ya kuogelea ya kimataifa ya Dubai yanayojulikana kwa jina la “Hamilton Aquatics Dubai Long Course” yaliyopangwa kuanza Desemba 11.
Akizungumza jijini jana,  Livingstone alisema kuwa waogeleaji wote 13 wapo katika morali ya hali ya juu baada ya kupata maandalizi ya miezi miwili.
Livingstone alisema kuwa mashindano hayo ambayo yanashirikisha waogelaji kutoka nchi mbalimbali duniani, mbali ya kusaka medali, pia yatawapa uzoefu wachezaji wao ambao ni bado chipukizi.
Alisema kuwa mashindano hayo ni makubwa sana katika mchezo huo na hivyo watatumia fursa ili kuwapa uzoefu wa kimatafa waogelaji wao ambao ni hazina ya Tanzania katika mashindano ya kimataifa katika miaka ijayo.
“Timu yetu inaundwa na waogeleaji chipukizi sana, wengi wao chini ya miaka 15, mbali ya kushindana, pia watakuwa wanapata uzoefu wa kimataifa kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano mengine ya kimataifa kama, Mashindano ya Dunia, Jumuiya ya Madola namichezo ya Olimpiki,” alisema Livingstone.
Alisema kuwa waogeleaji wamesema kuwa hakuna cha kuogopa katika mashindano hayo ambayo yatamalizika Desemba 12, Livingstone, Kocha mwingine wa klabu hiyo,
Kocha mwingine wa timu hiyo, Ferick Kalengela alisema kuwa pamoja na kujiandaa katika katika bwawa la kuogelea la mita 25, wataweza kushindana katika Bwawa la Mita 50 kwani waliongeza muda na umbali wakati wa mashindano.
Kalengela alisema kuwa wamejifunza stamina, kasi ya kuogelea na mambo mengine mengi yanayohusu mashindano hayo na kupata majina ya waogeleaji bora 13.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro alisema kuwa maandalizi yote ya safari hiyo yamekamilika na wanatarajia kuondoka nchini kesho Jumatano kuelekea kwenye mashindano hayo.
Inviolata aliwataja waogeleaji hayo kuwa ni Lidia Janik, Deeptti Venugopal, Maia Tumiotto, Ursula Khimji, Anna-Clara Azzoni, Maya Somaiya and Niki Somaiya. Also in the list are Smriti Gokarn, Anjani Taylor, Kayla Temba, Celina Itatiro, Peter Itatiro na Marin de Villard.
Viongozi ni Michael Livingstone na Kanis Mabena ambao ni makocha na  Inviolata ambaye ni meneja na mkuu wa msafara.

WAPINGA COCO BEACH KUUZWA

index 
Mwenyekiti wa Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania (JUHWATA), Ally Hapi akizungumza na waandishi wa habari, katika ukumbi wa Hoteli ya Travertine Ubungo jijini Dar es Salaam, kupinga hatua ya Mfanyabiashara mmoja wa jijini Dar es Salaam kutaka kuuziwa na Jiji Ufukwe wa Coco Beach, uliopo Oysterbay. Kulia ni Katibu Mkuu wa JUHWATA, Mtela Mwampamba. (Picha na Bashir Nkoromo).


REBECCA MALOPE KUTIKISA TAMASHA LA KUSHUKURU

MS1 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni jijjini Dar es salaam wakati akitambulisha ujio wa mwimbaji wa muziki wa injili Rebecca Malope kutoka Nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la Kushukuru linalotarajiwa kufanyika Desemba 25 kwenye uukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam , kulia ni Mratibu Tamasha la Kushukuru masuala ya usalama Bw. Hamisi Pembe.
MS2 
Mratibu Tamasja la Kushukuru masuala ya usalama Bw. Hamisi Pembe akifafanua jambo kuhusu usalama wa mashabiki wa muziki wa injili pamoja na mali zao wakati wa tamasha hilo, kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
……………………………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI nguli wa muziki  wa Injili barani Afrika, Rebecca Malope ambaye ni raia wa Afrika Kusini anatarajia kuongeza nguvu katika Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama muimbaji huyo atakuwa jukwaa moja na wenzake Sarah K wa Kenya  na Ephraim Sekeleti  wa Zambia ambao watafikisha shukrani za Watanzania baada ya kufanya uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu, uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Msama alisema Kamati yake inaendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo ambalo ni muendelezo wa Tamasha la Amani lililofanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Aidha Msama alisema Watanzania walichukilie tamasha hilo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kutupitisha katika kipindi kigumu cha uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika kwa amani na utulivu ingawa kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani.
Msama alisema waimbaji wa Tanzania watakaosindikiza tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua Mlelwa, Kwaya ya Wakorintho wapili huku kamati ikiendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo.
“Tumejipanga vilivyo na tamasha la Krismasi, hivyo tujiandae kupiga goti la kumrudishia Mungu Shukrani baada ya uchaguzi Mkuu ambao ulikuwa na mguso wa aina yake kutoka kwa vijana walioonesha kutaka maendeleo kutoka kwa serikali,” alisema Msama.
Naye mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo, Khamis Pembe aliwahakikishia Watanzania watakaohudhuria tamasha hilo ulinzi wa uhakika kupiia Jeshi la Polisi.

CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI (MoCU) CHAFANYA MAHAFALI YA KWANZA.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi  (MoCU) Pius Msekwa akitunuku Shahada ,Stashahada na Astashahada kwa wahitimu wa Chuo hicho wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho.
Wahitimu wa kozi mbalimbali waliohitimu katika Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi,(MoCU)
Miongoni mwa wageni waalikwa alikuwepo pia Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael.
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) Profesa Faustine Bee akizungumza wakati wa sherehe za mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Chuo hicho.

MKUU WA MAJESHI MSTAAFU,JENERALI GEORGE WAITARA AONGOZA TIMU YA MAAFISA 24 WA JESHI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akizungumza katia hafla fupi ya kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa maofisa 24 wa jeshi la wananchi Tanzania .kulia ni Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara na kushoto ni Mnadhimu mkuu wa Jeshi la wananchi ,Luteni Jenerali ,Samweli Ndomba.
Baadhi ya washiriki wa zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wapandaji.
Mhifadhi Mkuu ,Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,( KINAPA) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Washiriki.

Afisa Masoko wa KINAPA,Antypas Mgungusi akieleza jambo wakati wa hafala hiyo.


Mgeni rasmi katika hafla hiyo ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi,Fulgence Mponji akikabidhi bendera kwa Mkuu wa majeshi mstaafu ,Jenerali George Waitara ambaye ndiye kiongozi wa msafara huo.
Washiriki wakijiandaa kuanza safari.
Mhifadhi mkuu KINAPA,Erastus Lufunguro akiongozana na mgeni rasmi kwa ajili ya kukabidhi bendera kwa wapandaji mlima hao.
Safari ya kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro ikaanza kwa maafisa 24 wa JWTZ . Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kada ya Kaskazini (0755659929).

JUMUIYA YA KIMATAIFA YAOMBWA KUSAIDIA HUDUMA KAMBI YA NYARUGUSU

IMG_6503 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu walipita ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita kumsalimia pamoja na kusaini kitabu cha wageni. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
JUMUIYA ya Kimataifa imekumbushwa kuisaidia Tanzania katika kuhudumia wakimbizi kutoka Burundi na Kongo ambao wanaishi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Kigoma.
Alisema kwamba serikali ya Tanzania kwa miaka mingi imekuwa na moyo wa huruma wa kusaidia majirani zake kwa kuhifadhi wakimbizi na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuona hilo na kusaidia Tanzania kufanikisha hifadhi ya wakimbizi.
Alisema Umoja wa Mataifa umekuwa ukishuhudia namna ambavyo serikali ya Tanzania inahudumia wakimbizi na kuridhika na hata pale ilipowapatia haki za kuwa Watanzania kwa kuwapa uraia na pia kusaidia kuwarejesha makwao wakati hali ilipokuwa njema.
Hata hivyo amesema kwa sasa hali ya Burundi na Kongo si njema na hivyo Watanzania kupata tena kazi yakuhifadhi wakimbizi.
Alisema Tanzania kwa huruma yake imetoa ardhi zaidi ili kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kusaidia kukamilisha makazi hayo mapema kabla ya mvua za masika ili wananchi hao waweze kuishi kwa amani.
IMG_6505 
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akimsikiliza kwa makini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.
Alisema kambi ya Nyarugusu ni ya tatu kwa ukubwa duniani na inahifadhi zaidi ya wakimbizi 150,000 wakiwemo watoto na wanawake na wanahitaji huduma za shule, afya, maji na mengine.
Aidha wanahitaji nishati na hali hiyo haiwezi kuwezeshwa na serikali ya Tanzania pekee kwani watakuwa wakielemewa na huruma yake na moyo wa upendo kwa majirani zake.
“Dunia ikumbuke wema wa watanzania kwa miaka yote hii, na isaidie kuweka sawa hali ya kambi hiyo ili huduma zote muhimu za wananchi zipatikane” alisema mratibu huyo.
Akizungumza kuhusu wajibu wa Umoja wa Mataifa, alisema mashirika yake yamekuwa yakishirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba wanatoa huduma kwa wakimbizi hao na kutaka wadau duniani kusaidia mashirika hayo na serikali ya Tanzania kufanikisha mahitaji muhimu kwa wakimbizi hao hadi hali itakapokuwa shwari katika nchi zao na kurejea kuishi makwao.
Tanzania imetoa maeneo matatu zaidi ya kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na maeneo hayo yanahitaji huduma za msingi kama barabara, maji, vituo vya afya na shule.
Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na kukagua maendeleo ya kambi ya Nyarugusu pia walikagua miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani ILO na ile ya Shirika la Mpango wa idadi watu duniani UNFPA.
ILO Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
IMG_6515
Katika msafara huo walikuwepo maafisa kutoka Shirika la linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu mkoani Kigoma (walioipa mgongo kamera).
Alisema kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya familia zao.
“Naona uwezekano wa vijana hawa kujiajiri na kuziwezesha familia zao kuondokana na tatizo la kipato.. elimu hii inaweza kutanzua mambo mengi na kuondoa changamoto nyingine zinazoambatana na kukosa kipato” alisema mratibu huyo.
Mkoa wa Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi mbalimbali za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.
Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Afya Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Uzazi (UNFPA), Shirika la Kazi la Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia Watoto ( UNICEF), Shirika la Kuhudumia Wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la maendeleo (UNDP).
Akizungumza Afisa anayeshughulikia Ustawi na Usalama UNHCR, Kasulu, Bi. Zenobia Mushi, alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na ya mkoa wa Kigoma katika kuhudumia wakimbizi kwa kuhakikisha kwamba mahitaji yao ya msingi yanapatikana.
Naye Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya alishukuru Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa tayari kusaidia mkoa wake.
“ Tunashukuru kwa mambo yanayofanywa na Umoja wa Mataifa katika dhima nzima ya ushirikiano katika kuhakikisha kwamba pengo la maskini na matajiri linazibwa na umaskini unaondolewa katika mkoa wa Kigoma.”
IMG_6520 
Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipiga picha kwenye bango linaloonyesha Serikali zinazofadhili misaada kwa Wakimbizi nchini Tanzania lililopo katika ofisi za UNHCR Kasulu.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akizungumza kuhusu hali ya kambi ya Nyarugusu alisema kwamba hali ya kambi si nzuri na wakati msimu wa masika ukikaribia ni vyema Jumuiya ya Kimataifa ikaharakisha kukamilisha miundombinu ili kupunguza msongamano Nyarugusu.
Serikali imetoa maeneo mengine ya Nduta yaliyoko Kibondo na na Ntendeli, Kakonko kwa ajili ya kupunguza uwingi wa watu katika kambi hiyo.
DC huyo pia alisema kwamba kuna uharibifu mkubwa wa mazingira na lazima wadau wote washirikiane kuhakikisha kwamba mazingira yanaboreshwa pamoja na kupokea wakimbizi na kuwapa makazi.
Alisema kambi hiyo ilipangwa kuwa na watu elfu 50 kwa miaka ya 1996 lakini sasa inaweka wakimbizi wengi zaidi.
Aidha alisema kwamba pamoja na kupokea wakimbizi hao, inaonekana baadhi yao wameingia kufanya uhalifu na kuomba wakimbizi kushirikiana na polisi kuwataja wahalifu hao ili wadhibitiwe.
IMG_6551 
Kuwepo kwa kundi kubwa la wakimbizi kunasababisha uharibifu wa mazingira kama inavyoonekana pichani wakimbizi wakitoka kukata kuni kwenye misitu iliyopo karibu na kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Aidha katika mazungumzo ya shukurani kwa namna serikali ya Kigoma inavyotoa ushirikiano kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika miradi ya maendeleo na misaada kwa wananchi na kwa wakimbizi, Mwakilishi wa Shirika la mpango wa idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem alisema kwamba kumekuwepo na mafanikio mengi kutokana na ushirikiano huo.
Alisema anachokiona yeye anaona hali ya baadae ya taifa la Tanzania kuwa bora zaidi kutokana na kuwapo kwa ushirikiano mzuri kati ya serikali, mashirika ya umma na kundi kubwa la vijana ambalo kwa sasa linapokea elimu mbalimbali kwa manufaa yao na ya baadae.
“Taifa la Tanzania nusu yake ni vijana na sehemu kubwa ni chini yake, taifa hili lina hali njema kabisa ya siku za usoni kutokana na ushirikiano wenye lengo la kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na wengi” alisema Kanem.
Anasema kwa kuangalia program zilizopo zinazotekelezwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali anaona mafanikio ya mafunzo ya ujasiriamali na pia elimu inayotolewa kwa watu kwa malengo ya kufanikisha maendeleo.
IMG_7365 
Alisema UNFPA imefurahishwa sana namna mafunzo yanavyoendeshwa kwa vijana mafunzo ambayo yanaleta mshikamano wa pekee katika kufanikisha ustawi wa jamii na taifa kwa jumla.
Aidha alifurahi kuona kwamba wanawake wanashiriki katika kutoa elimu hivyo kuingiza sauti katika mafanikio ya jamii na uongezaji wa uelewa miongoni mwa jamii.
Mratibu huyo Mkazi wa UN Tanzania, Alvaro Rodriguez na timu yake wamerejea Dar es Salaam baada ya ziara ndefu kuangalia miradi ya Umoja wa Mataifa inavyoleta tija na ufanisi wa maisha katika jamii.
Mratibu huyo alitembelea mikoa ya Manyara, Singida, Tabora na Kigoma.
Katika ziara yake alioneshwa kufurahishwa na miradi hiyo inavyobadili jamii husika na kusema kwamba umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya maendeleo nchini Tanzania.
IMG_6558
IMG_6601 
Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (kulia) akielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili kambini hapo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kutembelea makazi ya wakimbizi hao.
IMG_6608 
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakirekodi mambo muhimu wakati wa kupokea taarifa ya maendeleo ya kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu kutoka kwa Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (hayupo pichani).
IMG_6632 
Kutoka kushoto ni Afisa mahusiano wa UNHCR, Ofisi ya Kasulu, Agnes Mwangoka, Mshauri na Mtaalum wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce Temu, Mwandishi wa Habari, Prosper Kwigize pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakielekea kwenye kambi za Wakimbizi baada ya kupokea taarifa.
IMG_6664 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakikagua ndani ya mahema wanakoishi Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_6661 
Mmoja wa Wakimbizi akiwa na mwanae nje ya chumba chake na mwanae katika kambi ya Nyarugusu.
IMG_6682 
Kuni zikitumika kupikia chungu cha Maharage kambini hapo.
IMG_6703 
Mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akikoleza moto ulioonekana kufifia wakati akijiandalia chakula chake cha mchana kama alivyonaswa na kamera yetu.
IMG_6710 
Moja ya familia ya Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu wakiangalia msafara wa Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini uliotembelea kambini hapo mwishoni mwa juma.
IMG_6725 
Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipozi na moja ya familia katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu.
IMG_6732 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Rais wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Bi. Abilola Angelique wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.Kwa matukio zaidi ya picha bofya link hii

KESI RUFAA YA TALAKA DHIDI YA MTEMBEI YAAHIRISHWA

wooden gavel and books on wooden table,on brown background 
Na Mwandishi wetu
KESI ya rufaa ya madai ya talaka dhidi ya mfanyabiashara na Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya St Mathew, Thadei Mtembei imeahirishwa baada ya wakili wa Mtembei, Mussa Kyoboya kudai mrufaniwa yuko India kwa matibabu.
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Tarimo.
Katika kesi hiyo, mpeleka rufaa, Magreth Mwangu anawakilishwa na wakili Chacha Mrungu. Kesi hiyo ilikuja mahakamani juzi ambapo mrufaniwa alitakiwa kupeleka majibu ya rufaa.
Hata hivyo, wakili wake alisema majibu hayako tayari kwani kuna vipengele ambavyo alitakiwa kusaini, lakini ilishindikana kutokana na kuwa nchini India kwa matibabu. Kesi hiyo imepangwa kuendelea Desemba 16 mwaka huu.
Awali, kesi hiyo ilisikilizwa katika Mahakama ya Mwanzo Kizuiani mbele ya hakimu Rajab Tamaambele, ambapo Mwangu na watoto wake walionekana hawana haki, kwa madai sio mke halali na watoto hao ni wa zinaa kutokana na kuzaliwa nje ya ndoa.
Katika madai ya msingi, Mwangu anataka talaka, mgawanyo wa mali na matunzo ya watoto.
Katika sababu za rufaa, mrufani alieleza kusikitishwa na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Mwanzo Kizuiani Septemba Mosi mwaka huu, kwa hakimu kukosea kisheria kwa kutosaini nakala ya hukumu ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa saini za wazee wa baraza.
Sababu nyingine ni Mahakama kukosea kisheria kwa kunyang’anya haki ya watoto kwa kutotoa matunzo ya watoto kwa mama, ambaye anaishi na mrufaniwa kwa miaka 20 na kuvunja Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009. Maamuzi ya Mahakama ya Kizuiani yalishindwa kufuata sheria kwa wazee wa baraza kushindwa kutoa maoni yao.

No comments :

Post a Comment