Friday, November 27, 2015

Wajibu wa waajiri kuwasilisha michango mifuko ya pensheni




Afisa wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Saluna Aziz Ally, (kushoto), akimeuelekezea mwanachama wa Mfuko huo jinsi ya kupata taarifa za michango yake iliyopelekwa na mwajiri wake  PPF kupitia simu ya mkononi, huduma ijulikanayo kama “PPF Taarifa’’.

Christian Gaya Mwananchi Alhamis26 Novemba 2015 
 
Wiki iliyopita tuliona ya kuwa mara nyingi waajiri wanatoa sababu zinazofanana zinazowafanya wasipeleke michango ya wafanyakazi wao

Lakini kutokana na utafiti uliofanywa unaonyesha ya kuwa waajiri wengi huchukulia michango kama gharama kubwa kwao ambapo wakati mwingine inasababisha hata kupandisha bei za bidhaa zao wanazopeleka sokoni na hivyo kufidiwa na mlaji ambapo unakuta ndiyo huyo huyo mwanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii.


Na mara nyingi hupunguza hata idadi ya wafanyakazi wake wanapotoa taarifa kwa wakaguzi wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Madharani ana wafanyakazi 100 lakini utakuta walioandikishwa kama wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii ni 50 tu.

Na wakati mwingine wanapunguza hata kuonyesha mishahara kamili ya wafanyakazi wao kwa wakaguzi wa mifuko hii ya pensheni kwa kukubaliana na baadhi ya wafanyakazi ya kwamba atakuwa anachukua tofauti ili kukwepa makato ya michango ya pensheni. 

Kwa kawaida mfanyakazi ambaye ni mwanachama wa mfuko wa pensheni hukatwa asilimia 10 ya jumla ya mapato yake yote kwa mwezi na mwajiri analazimika huchangia asilimia 10 ya mapato yote ya mshahara wa mfanyakazi hivyo na kufanya kuwa jumla ya asilimia 20 na yote kupelekwa kwenye akaunti ya mwanachama wa mfuko wa pensheni wa hifadhi.

Au mwajiri huweza kuchangia asilimia 15 na mwajiriwa asilimia 5 au asilimia yote 20 inaweza kutolewa na mwajiri kwa mfanyakazi wake kulingana na makubaliano.

Mfano jumla ya pato la mshahara wa mfanyakazi kwa mwezi ni shilingi 700,000.00 hiyo asilimia kumi ya mchango wa mfanyakazi utakuwa shilingi 70,000.00 na mwajiri naye lazima atachangia asilimia kumi ya shilingi 700,000.00 ambayo ni shilingi 70,000.00. kwa hiyo mchango wa pensheni wa kila mwezi wa mfanyakazi huyo itakuwa shilingi 140,000.00.

Hivyo basi kwa kujiunga na mfuko wowote wa pensheni wa hifadhi ya jamii unapata faida ya kuongezwa pato kutoka kwa mwajiri wako kwa kuchangiwa kwenye pensheni yako ya sasa na ya baadaye.

Na tambua ya kuwa makato yako ya pensheni hukatwa kabla ya makato yoyote ya kodi ili kutunisha pensheni yako wewe mwanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

Na nadharia nyingi na kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakisema ya kuwa baadhi ya wakaguzi wanashirikiana na waajiri wasio waaminifu kudidimiza michango ya pensheni kutokusanywa ipasavyo na hata kupunguza idadi ya wafanyakazi wanaotakiwa kuandikishwa na mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii ukiwemo na ujanja mwingine uliotajwa hapo juu ingawa hauna ushahidi wowote.

Na hata wakati mwingine kesi za jinai na madai ya michango ya pensheni ya hifadhi ya jamii kucheleweshwa kwa muda mrefu kusababishwa na ucheleweswaji wa uendeshwaji wa kesi ambapo huchukua muda mrefu  sana mpaka kupatikana kwa michango wa wanachama. 

Na hapa inaonyesha ya kuwa watu wengi wamekuwa wakilipwa michango ya pensheni pungufu kwa wakati wote huu wa kuondoa michango ya pensheni kabla ya wakati wake na kwa sababu wengi wamekuwa wakikimbilia kwenye akaunti zao za michango ya pensheni ya hifadhi ya jamii kwa kutatua shida zao za kijamii na za kiuchumi kwa kuwa na mitazamo tofauti juu ya jambo hili.

Lakini wakati mwingine imekuwa ni faida kwa upande wa mifuko kwa kuwalipa pungufu wateja wao na kubakiwa na idadi kubwa ya michango ambayo haitafuatiliwa na wadai.

Ikumbukwe ya kuwa utafiti unaonyesha michango mingi ya pensheni inayotolewa na wanachama ni ya uwongo au kudanganya kwa sababu idadi kubwa ya wanachama waliojitoa bado wako kazini aidha kwa kushirikiana na waajiri wenyewe. 

Jambo la kujiuliza hapa ni kwamba ni wajibu wa nani kukusanya michango. Na inaonyesha ya kuwa mpaka Machi 2015 mifuko ilikuwa inadai shilingi bilioni 18 zikiwa kama michango ya pensheni ambayo haijawasiliswa kwenye mifuko ya jamii ya NSSF na PPF.

Mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) na mfuko wa pensheni wa PPF wanasema mpaka kufikia mwezi Septemba 2013 zaidi ya waajiri wapatao 230 walikuwa hawajawasisha michango ya pensheni ya wafanyakazi wao ambayo kwa kweli ni makosa ya jinai kisheria

Kulingana na gazeti la The Guardian la tarehe 17 Novemba 2013 mkuu wa idara ya uhusiano na huduma kwa wateja wa NSSF Bi. Eunice Chiume alisema zaidi ya waajiri 200 walikuwa wameshidwa kuwasilisha  michango na kusababisha hasara ya bilioni 16.
Kati ya hizi zote,  bilioni 6 zilikuwa zimesabishwa na Mamlaka ya Reli ya Tazara. Wakati kwa upande wa mfuko wa pensheni wa PPF Bi Vupe Ligate ambaye ni mkurugenzi wa sheria alisema ya kuwa zaidi ya waajiri 30 nao walikuwa wameshidwa kuwasilisha makusanyo ya michango ya wafanyakazi wao ambayo ni kama jumla ya bilioni 6 kwenye mfuko wa pensheni wa PPF 
Ingawa mifuko imeweza kuwafunguliwa mashtaka ya jinai karibu waajiri wote wanalioshidwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao. Lakini pamoja na hayo baadhi ya waajiri walisha waachisha kazi wafanyakazi wao kwa sababu mbalimbali
Na ndio maana Bi. Chiume wa NSSF alisema NSSF wameanzisha mfuko unaitwa akaunti ya hasara ya kuwalipia baadhi ya wanachama wanaodai au wanaotaka kutoa michango yao ya pensheni aidha baada ya kuachishwa kazi, au kufikisha umri wa kustaafu au kumaliza mkataba wake.
Kwa vile wajibu wa kufuatilia michango ya pensheni ya  mwanachama ya kuwa inawasilishwa na waajiri ilikuwa ni NSSF na mkataba ulikuwa kati ya NSSF na mwanachama kwa kumpatia hata kadi ya uwanachama  imemlazimu NSSF kuwalipia wanachama  wake kama wateja wake kiasi cha bilioni 2.
Na mpaka wakati huo mzigo ulikuwa kwa mfuko wa pensheni wa NSSF kupambana na waajiri hao kuhakikisha ya kuwa wanawasilisha michango yote ya wanachama wao kisheria

No comments :

Post a Comment